Quantcast
Channel: VIJIMAMBO
Viewing all 45921 articles
Browse latest View live

NAIBU WAZIRI MPINA APOKEA RIPOTI YA ZIARA YA KAMATI YA YA ARDHI NA MAWASILIANO YA BARAZA LA WAWAKILISHI KUTOKA ZANZIBAR.

$
0
0
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa reais Profesa Faustin Kamuzora akimkaribisha Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Luhaga Mpina (katikati) wakati wa kikao cha kupokea ripoti ya ziara ya Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi kutoka Zanzibar katika ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Makamu wa Rais- Dar Es Salaam.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Luhaga Mpina akiteta jambo na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Profes Faustin Kamuzora wakati wa kupokea ripoti ya ziara ya Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi kutoka Zanzibar katika ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Makamu wa Rais- Dar Es Salaam.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Luhaga Mpina akiongea na Wajumbe wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi kutoka Zanzibarwalipofika Ofisini kwake kuwasilisha ripoti ya ziara yao Tanzania Bara.
Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi kutoka Zanzibar wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Luhaga Mpina (hayupo pichani) walipofika Ofisini kwake kuwasilisha ripoti ya ziara yao pamoja na kushukuru.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi kutoka Zanzibar akitoa shukrani kwa Niaba ya Kamati kwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Luhaga Mpina wakati walipofika Ofisini kwake kwa ajaili ya kumshukuru na kuwasilisha ripoti ya ziara yao.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Luhaga Mpina akipokea ripoti ya ziara ya Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi kutoka Zanzibar waliyoifanya Tanzania Bara.


MISS KIGOMA ANAKUKARIBISHA COLUMBUS, OHIO KWENYE MNUSO MKONGWE KULIKO YOTE SEPT 1-3

LISSU AWAONGOZA MAWAKILI KUGOMA KUINGIA MAHAKAMANI

$
0
0

RAIS wa Chama cha Mawakili Tanzania (TLS), Tundu Lissu amewaongoza mawakili nchini kugoma kuingia mahakamani kwa muda siku mbili leo Agosti 29 na 30, 2017 wakilaani tukio la kushambuliwa kwa ofisi za IMMMA Advocates iliyolipuliwa kwa bomu usiku wa kumakia Jumamosi iliyopita.

Akizungumza na wanahabari kuhusu uamzi wa Baraza la TLS, Lissu amesema ni haki ya kisheria ya mtu yeyote kutoa maoni yake, kupinga maamuzi ya TLS, sio dhambi na hatochukuliwa hatua.

“Mengi wamefanyiwa mawakili lakini hili la juzi tumesema hatukubali kukaa kimya wakati mawakili wetu wanashambuliwa. Kwa busara za TLS tuliona tufanye maamuzi ya kusimamisha kazi kwa siku mbili ili kupeleka ujumbe kuwa jambo hilo si jema,” alisema Lissu.

Kuhusu endapo mawakili wote wamegoma Lissu alisema hawezi kulizungumzia kwa sasa, hadi jioni ambapo ripoti kamili itakuwa imepatikana kwa kuwa kuna mawakili wengine walikuwa na kesi asubuhi, wegine mchana, hivyo haikuwa rahisi kufahamu ni mawakili wangapi wamegoma. GPL

OLD SCHOOL REUNION COLUMBUS OHIO THE HEART OF TANZANIAN'S ENTERTAINMENT IN THE USA ANDAA KIBUBU ZIMEBAKI ZIMEBAKI SIKU 3 TU

$
0
0
COLUMBUS, OHIO KIMATAIFA ZAIDI

HOTELS IN COLUMBUS

Hampton Inn Columbus I-70 E/Hamilton Road
2093 S Hamilton Rd, Columbus, OH 43232
hamptoninn3.hilton.com
(614) 552-2400

Holiday Inn Express & Suites Columbus Southeast
4041 Hamilton Square, Groveport, OH 43125
ihg.com
(614) 920-2400

Hawthorn Suites by Wyndham Airport Columbus East
2084 S Hamilton Rd, Columbus, OH 43232
wyndhamhotels.com
(614) 864-8844

La Quinta Inn Columbus Airport Area
2447 Brice Rd, Reynoldsburg, OH 43068
laquintacolumbusairport.com
(614) 866-6456

Comfort Suites Columbus
5944 Scarborough Blvd, Columbus, OH 43232
choicehotels.com
(614) 552-2525

Days Inn & Suites Columbus East Airport
2100 Brice Rd, Reynoldsburg, OH 43068
wyndhamhotels.com
(614) 864-1280

Courtyard by Marriott Columbus Airport
2901 Airport Dr, Columbus, OH 43219
marriott.com
(614) 475-8530

RATIBA KAMILI NI KAMA IFUATAVYO
Ijumaa Sept 1, 2017

Kuanzia saa 3 usiku ni Africa Night chini ya DJ Burundi na kutakua na onyesho la mavazi kutoka kwa Missy T na Asya Idarous Khamsin anuani ni


4257 Eastland Square Dr,
Columbus, OH 43243

Jumamosi Sept 2, 2017
Kuanzia saa 8 mchana ni BONANZA la mpira wa kikapu kutoka kwa vijana wa Pazi, Vijana, Don Bosco na kwengineko anuani ni
6615 Dublin center Dr,
Dublin, OH 43017

Jumamosi Sept 2, 2017
kuanzia saa 12 jioni ni mechi ya Simba na Yanga itakayokua na wachezaji waliocheza ligi kuu Tanzania anuani ni
Columbus Global Academy Stadium
4077 Karl Rd
Columbus, OH 43224

Na baadae kuanzia saa 3 usiku ni Old School Reunion chini na Ma DJ bora North America DJ Dennis (Funky House) na The Mix Master DJ Luke Joe anuani ni 4257 Eastland Square Dr
Columbus, OH 43243

Jumapili Sept 3, 2017 
kuanzia saa 12 jioni
NYAMA CHOMA anuani
Avery Park,
7501 Avery Rd,
Dublin, OH
43017

Na baadae kuanzia saa 3 usiku ni usiku wa Reggae anuani ni 
4257 Eastland Square Dr,
Columbus, OH 43243

MISOSI NA VINYWAJI VYAKUMWAGA

JUMAMOSI NAJUMAPILI KUANZIA SAA 4 ASUBUHI MPAKA SAA 8 MCHANA
Kutapatikana chakula kitamu cha Kitanzania 
6170 Busch Blvd
Columbus, OH 43229

Wakazi wa Shinyanga na Geita kunufaika na uwekezaji mradi wa umeme

$
0
0
Kampuni ya Acacia, kwa ushirikiano na TANESCO, imejenga kituo cha kupozea umeme kilichopo katika mgodi wake wa dhahabu wa Bulyanhulu ambacho kimeweza kuongeza uhakika wa upatikanaji wa umeme katika maeneo ya mgodi huo.

Acacia imewekeza shilingi bilioni 5.5 katika mradi huo ambao utanufaisha maeneo yanayozunguka migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu na maeneo mengine ikiwa ni pamoja na Kahama, Shinyanga, Msalala, na sehemu nyingine za Geita.

Ujenzi wa Kituo hicho ulianza Desemba 2016 na unatarajiwa kukamilika hivi karibuni.
Haya ni maendeleo makubwa kwa viwanda na biashara zinazozunguka eneo hilo ambazo zitafaidika na uwepo wa umeme wa uhakika jambo litakalosaidia kuboresha ufanisi na kuongeza uzalishaji.

Mkuu wa kitengo cha miradi ya maendeleo wa mgodi wa Bulyanhulu, Jiten Divecha ameeleza kuwa tatizo la mabadiliko ya nguvu ya umeme limekuwepo kwa muda mrefu na limekua likisababisha uharibifu mkubwa wa mashine.“Ujenzi wa kituo hiki utasaidia kupunguza athari zinazotokana na kuongezeka au kupungua kwa nguvu ya umeme katika migodi yetu hivyo kuboresha shughuli za uzalishaji. Wakazi na viwanda vinavyotumia umeme katika wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga na wilaya zingine za mkoa wa Geita zitafaidika na uwekezaji huu pia,” alisema Jiten.

Aliongeza: "Acacia inajitahidi kuleta manufaa ya kiuchumi ya pamoja kwa jamii zinazotuzunguka na wadau wake kupitia miradi endelevu."
Wakati wa ujenzi wa kituo hicho, ajira mbalimbali zilitolewa kwa jamii zinazozunguka mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu.

Akizungumzia fursa hiyo, David Nyanda alisema: “tunathamini sana ujenzi wa mradi huu kwa sababu tumepata fursa za ajira. Japokuwa fursa hizi ni za muda, tunaweza kupata mapato ili kuendesha familia zetu hasa katika kipindi hiki cha ukame.”

ANDREW HANGO'S RECOVERY FUND

$
0
0
As you all know, our brother Andrew Hango (Wash) suffered a stroke on Tuesday morning August 7th.

In the meantime, we are asking for your support and contributions to help Andrew with his expenses. Although we do not know for certain how long it will take for his recovery, we will update you with his progress as information becomes available.

Thank you for all your help and continued support.

TO DONATE PLEASE TAP HERE

THANK YOU

KAMISHNA WA MADINI AANZA ZIARA KANDA YA ZIWA

$
0
0
Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka (kulia), akifafanua jambo kwa Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Juma Samwel Sweda (wa pili kutoka kushoto), alipofika ofisini kwake akiwa katika ziara ya kazi wilayani humo. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Eliud Mwaiteleke. Wengine ni Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Viktoria-Magharibi, Mhandisi Yahya Samamba (kushoto kwa Mkuu wa Wilaya) na Mhandisi Rayson Nkya (wa kwanza kulia).
Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka (katikati), akisikiliza maelezo kutoka kwa mmoja wa viongozi wa Mradi wa Uchimbaji wa Kati wa Madini ya Dhahabu uliopo Ishokelahela wilayani Misungwi, Mkoa wa Mwanza, Mrisho Masebu, kuhusu utendaji kazi wa Mradi huo.

Mmoja wa Viongozi wa Mradi wa Uchimbaji wa Kati wa Madini ya Dhahabu uliopo Ishokelahela wilayani Misungwi, Mkoa wa Mwanza, Baraka Ezekiel (wa pili kutoka kulia), akifafanua jambo kwa Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka (katikati) na Ujumbe wake. Kamishna Mchwampaka alitembelea Mradi huo Agosti 28 mwaka huu akiwa katika ziara ya kazi Kanda ya Ziwa.
Viongozi wa Mradi wa Uchimbaji wa Kati wa Madini ya Dhahabu uliopo Ishokelahela wilayani Misungwi, Mkoa wa Mwanza, wakimwongoza Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka (katikati), kukagua shughuli mbalimbali zinazofanyika katika mgodi huo. 
Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka (katikati), akiwa ameambatana na baadhi ya maafisa wa Wizara ya Nishati na Madini na wafanyakazi wa Mradi wa Uchimbaji wa Kati wa Madini ya Dhahabu uliopo Ishokelahela wilayani Misungwi, Mkoa wa Mwanza, wakikagua sehemu mbalimbali za Mgodi huo.
Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka (mwenye koti), akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Mradi wa Uchimbaji wa Kati wa Madini ya Dhahabu uliopo Ishokelahela wilayani Misungwi, Mkoa wa Mwanza na Maafisa wa Wizara ya Nishati na Madini, mara baada ya kukagua Mgodi huo.
Shughuli za uchimbaji madini zikiendelea katika Mradi wa Uchimbaji wa Kati wa Madini ya Dhahabu uliopo Ishokelahela wilayani Misungwi, Mkoa wa Mwanza.

Na Veronica Simba – Mwanza
Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka, ameanza ziara ya kazi ya takriban juma moja katika mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa lengo la kukagua utekelezaji wa shughuli mbalimbali za sekta hiyo.
Katika siku ya kwanza ya ziara hiyo, Agosti 28 mwaka huu, Kamishna Mchwampaka alikutana na kuzungumza na wafanyakazi wa Ofisi ya Madini, Kanda ya Ziwa Viktoria-Magharibi pamoja na wafanyakazi wa Ofisi Ndogo ya Ukaguzi wa Madini Kanda ya Mwanza, iliyokuwa ikijulikana kama Wakala wa Ukaguzi Madini Tanzania (TMAA).
Akizungumza mara baada ya kupokea taarifa ya utendaji kazi wa Ofisi hizo mbili, Kamishna Mchwampaka aliwataka wafanyakazi hao kufanya kazi kwa bidii na kwa ushirikiano ili kufanikisha malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuwaletea wananchi wake maendeleo ya dhati.
Katika hatua nyingine, akizuru Mradi wa Uchimbaji wa Kati wa Madini ya Dhahabu uliopo Ishokelahela wilayani Misungwi, Mkoa wa Mwanza, Kamishna Mchwampaka, alipongeza jitihada za watendaji wa Mradi huo unaomilikiwa na wazawa wazalendo kwa asilimia mia moja, kwa ubia kati ya Isinka Federation 2014 Mining Cooperative Society Limited na Kampuni ya kitanzania ya Busolwa Mining Limited.
Alisema kuwa, jitihada zinazooneshwa na wajasiriamali hao wazalendo zinapaswa kuigwa na watanzania wengine kote nchini kwani Mradi huo una maendeleo ya kuridhisha na kujivunia japokuwa bado haujaanza uzalishaji.
“Sisi kama Serikali tunafarijika sana tunaposhuhudia wananchi wazalendo wakiweka jitihada na kufanikiwa katika biashara za madini kama hivi mnavyofanya ninyi. Tunaahidi kuendelea kuwasaidia kadri iwezekanavyo ili muweze kufikia malengo yenu na kuchangia katika kuinua uchumi wa nchi.”
Kwa upande wao, baadhi ya viongozi wa Mradi huo, Baraka Ezekiel na Mrisho Masebu, waliahidi kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kwa ubunifu ili mafanikio yao yaweze kuwahamasisha watanzania wengine.
Aidha, waliahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali kadri ipasavyo ikiwa ni pamoja na kulipa kodi zote stahiki pamoja na kufuata kanuni na sheria za madini zilizowekwa kwa mujibu wa sheria.
Kamishna Mchwampaka pia alipata fursa ya kuwatembelea na kuzungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Juma Samwel Sweda ambapo walikubaliana kushirikiana katika majukumu mbalimbali yanayohusu sekta ya madini kwa manufaa ya wananchi.
Hii ni ziara ya kwanza rasmi ya kikazi kwa Kamishna wa Madini, Mhandisi Mchwampaka tangu alipoteuliwa na Rais John Pombe Magufuli, kushika wadhifa huo, takribani miezi minne iliyopita.
Kamishna Mchwampaka anaendelea na ziara yake, ambapo katika siku ya pili atazuru Mkoa wa Geita.

Mtu anayefanya biashara ya dawa za kulevya anahusika na rushwa – Rais Magufuli

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amesema kuwa mtu anayefanya biashara ya dawa za kulevya kwa vyovyote vile anahusika na rushwa.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo alipotembelea na kuzungumza na wafanyakazi wa TAKUKURU katika ofisi za makao makuu ya taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam.
“Nataka chombo hichi cha TAKUKURU cha Tanzania nataka kifanye kama wanavyofanya wengine, msiwe na kigugumizi kwa kitu mlichokuwa na ushahidi na nyinyi msije mkawa party ya kudivert masuala ambayo yako wazi, chombo hichi kila mahali unapotaka kuplay party una play hata kama ni biashara ya madawa ya kulevya mtu anaefanya biashara ya madawa ya kulevya kwa vyovyote anahusika na rushwa,” alisema Rais Magufuli.

“Nilazima amewahonga watu, amedanganya watu kwa kumeza madawa hayo, ndugu Mkurugenzi nasema haya sitaki kuwa mnafki nataka niwaeleze ukweli changamoto zipo, je? changamoto zilizo katika kazi zenu je mnazishughulikia vizuri ,je mnajipangaje katika masuala mabyo ni muhimu investigation na mahali pengine, je anaefanya investigation qualification zake ni nzuri zinafaa kwa investigations.”
Hata hivyo Rais Magufuli amewataka viongozi wa Taasisi hiyo kutokuwa na kigugumizi cha kuchukua hatua pale wanapokuwa na ushahidi dhidi ya watu wanaojihusisha na vitendo vya rushwa.

RC TABORA ATAKA MAELEZO ALIYECHOMA MOTO KATIKA CHUO CHA ARDHI

$
0
0
Na Tiganya Vincent
SERIKALI Mkoa wa Tabora imeagiza kutafutwa na kuchukiwa hatua kali na kupata maelezo ya watu waliohusika na uchomaji moto katika maeneo ya Chuo cha Ardhi Tabora na kusababisha uharibifu mkubwa wa mistu asili na miti iliyokuwa imepandwa katika eneo hilo kama hatua za uhifadhi wa mazingira.
Kauli hiyo imetolewa jana mjini hapa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri baada ya kukuta eneo la Chuo hicho likiwa limeungua na moto wakati wa ziara ya ya kukagua vitalu vya kuoteshea miti ikiwa ni maandilizi ya zoezi la upandaji wa miti.
Alisema kuwa haiwezekani wananchi wanajitoa kwa moyo kupanda miti katika kampeni inayoendelea kisha watu wachache wanaamua kuua miti na kuharibu mazingira.
Mwanri aliongeza kuwa inasikitisha kuona hata sehemu za Taasisi za umma kama hiyo zinaacha moto unaunguza miti na wakufunzi wapo, wanachuo wapo bila kuchukua hatua ya kuuzima na kuwasaka waliohusika.
Alisema kitendo kinaonyesha jinsi wao nao wanahusika kwa namna moja au nyingine katika kuchangia uharibifu ulifanyika katika Chuo chako.
Kufuatia kitecho hicho Mkuu wa Mkoa alimwagiza Afisa Mazingira wa Manispaa ya Tabora kwenda kwa Mkuu wa Chuo kupata maelezo nini kilitokea na hatua zilizochukuliwa kwa wahusika na kama hawachukua hatua kwa wahusika basi Sheria za Mazingira zichukue mkondo wake.
Aliongeza kuwa pamoja na hatua hiyo zitakazochuliwa aliagiza uongozi wa Chuo hicho kuhakikisha wanarudishia miti yote iliungua mapema iwezekanavyo.
“Nimesikitishwa na kitengo nilichokiona katika eneo la Chuo cha kuchoma moto na kuunguza miti ….ikiwa kwa watu wasomi ambao wanatakiwa wawe mfano wa utunzaji wa mazingira wao ndio wanakuwa wa kwanza kuharibu mazingira kwa kuchoma moto…nimesikitishw
a sana” alisema Mkuu huyo wa Mkoa.
Naye Afisa Mazingira wa Manispaa ya Tabora William Mpangala alisema hadi hivi sasa Ofisi yake imekwishakamata watu 27 kwa makosa ya uchomaji moto ovyo na kuwapiga faini ya kuanzia 50,000/-
Alisema kuwa viongozi wa Taasisi wafahamu kuwa kunapotokea moto katika maeneo yao wakishindwa kuwakamata wahalifu wao watawajibika kulipa faini ya uharibifu wa mazingira ya kuanzia shilingi 500,000/-.
Utamaduni wa uchomaji moto ovyo katika Mkoa wa Tabora unaoenekana kama kama jambo la kawaida wengine wakitaka malisho mapya ya mifugo na mengine wakati wa kuandaa mashamba na wakati wa kulina asali.
Jambo hilo limekuwa likimuumiza kichwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora wakati mwingine kulizamika kuamuka usiku kuwavizia watu wanaowasha moto ovyo.
Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa wa Tabora ameziagiza Halmashauri zote mkoani kuhakikisha vitalu vya miti waliyotayarisha kwa ajili awamu ya pili ya upandaji mkoani hapa inayomiti ya kutosha kwa kadri walivyokubaliana.
Alisema kuwa Manispaa ya Tabora inapaswa kuhakikisha imeotosha miche 500,000, Nzega Mji na Wilaya miche 500,000 na nyingine zilizobaki 250,000 kila moja.
Mwanri idadi hiyo ni nje ya ile ambapo kila mkazi wa Tabora atakiwa kupanda au kupandiwa na mzazi wake kama ni mtoto miti miwili kila mmoja.

DIAMOND PLATNUMZ, HARMONIZE, RICH MAVOKO, RAYVANNY - ZILIPENDWA (OFFICIAL VIDEO)

HOTEL 92 ILIYOPO SINZA SHEKILANGO ROAD NA MADUKA YABOMOLEWA KWA AMRI YA MAHAKAMA

$
0
0
Jengo  la iliyokuwa hotel 92 Sinza Shekilango jijini Dar es salaam ambalo linatumika kama kanisa na maduka  plot namba 11 limevunjwa na kampuni ya CEMINA AUCTIONAL MART ikiwa ni utekelezaji wa hukumu ya Mahakama kuu kitengo cha Ardhi baada ya aliyekuwa mmiliki wa eneo hilo  NKUMILO ENTERPRESES kushindwa kesi mahakamani.

ITV imefika katika eneo hilo na kukuta shughuli za uvunjaji zikiendelea katika ploti hiyo iliyokuwa na maduka pamoja ukumbi ambao ulikuwa ukitumiwa na waumini wa kanisa la SHALOM TABERNACLE INTERNATIONAL CHURCH ambapo waumini walionekana wakihaha kutoa mali za kanisa hilo.

Akizungumza na radio one mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya CEMINA AUCTIONAL BI ROSE JOSEPH amesema wamepewa jukumu hiyo na mahakahama baada ya kesi ya ploti hiyo iliyodumu kwa miaka minne kumalizika na kumpa ushindi aliyenunua eneo hilo Bw. Yusuph Ismail


Wafanyabiashara waliokuwa na maduka katika ploti hiyo wamesema kwa sasa hawana cha kufanya kwani awali hawakaumbiwa kama eneo hilo linamgogoro .

Chanzo: ITV Tanzania

TAMCO EID EL A’DHA (HAJJ) – DMV

$
0
0

Assalamu Alaykum Wa Rahmatullaahi wa Barakaatuhu
Uongozi wa Tanzanian Muslims Community of Washington DC Metro (TAMCO) una Furaha Kuwakaribisha  WaTanzania Wote katika Sherehe za Eid El Adha (Eid el Hajj)  kuadhimisha Mahujjajj kufikia kilele cha Hajj yao huko Makkah, Saudi Arabia.
Friday, September 1, 2017
Chai ya Asubuhi ya Pamoja, Baada ya Salat El Eid pamoja na Dua kuwaombea Waliotangulia na Sisi  wenyewe

Kuanzia Saa Nne Asubuhi – Saa Sita Mchana 10AM-12PM
&
Sherehe za Eid za Jioni, Baraza la Eid pamoja na Nyama Choma

Kuanzia Saa Kumi Jioni Mpaka Saa Tatu Usiku 4PM-9PM
Meadowbrook Local Park
7901 Meadowbrook Lane
Chevy Chase, MD 20815

Kwa Taarifa Zaidi Wasiliana na

Ali Mohamed 301 500 9792
                                                         Jasmine Rubama 410 371 9966                                                                                                              Ally Mikidadi 201 628 2133                                                               Asha Nyanganyi 301 793 2833
                                                       Iddy Sandaly 301 613 5165                                                        Asha Hariz 703 624 2409


Labbaik Allah humma labbaik - Here I am O My Lord!

MSAADA WA HARAKA UNAHITAJIKA BADO KIDOGO TUTAFIKIA LENGO

$
0
0
Ndugu zetu Watanzania tunasikitika kuwafahamisha kuwa ndugu yetu na kaka yetu Meya Mlima (pichani juu)anashikiliwa na ICE (Immigration) tokea mwisho mwa wiki iliyopita huko New Hampshire.

Mpaka muda huu marafiki na wanafamilia ya Meya wanafuatilia kesi yake ili kujua jinsi gani tunaweza kumsaidia pamoja na kujua gharama za mwanasheria pia kujua mchakato mzima wa kesi itakavyosikilizwa.

Kamati inapenda kuwafahamisha marafiki, ndugu, na jamaa wa Meya kuwa kutahitajika msaada wa Pesa ili ndugu yetu aweze kutoka na kuendelea kuwalea vijana wake na kushiriki nasi katika gurudumu la maisha ya huku ughaibuni.

Kwa sasa Familia na kamati wako katika mchakano wa kupata mwanasheria mwenye uzoefu katika maswala ya uhamiaji (immigration) . Kamati na Familia itaendelea kuwafahamisha kila hatua itakayo piga katika kumsaidia ndugu yetu Meya Mlima

Kwa ushauri na maelezo zaidi wasiliana na wafuatao:

Babie Mgaza 2022005031
Raju Tambwe 4433177440
Jasmine Rubama 4103719966
Mganga Muhombolage 2023740988
Iddi sandaly 3016135165
Kessy Metro tires 2024135933
Jabir Jongo 2406040574

UNAWEZA KUTOA MSAADA WAKO HAPA TAFADHALI FAMILIA NA KAMATI INATANGULIZA SHUKURANI

KWA KUCHANGIA BOFYA HAPA

SHUKURANI KUTOKA KWA MAMA MZAZI WA MAYOR

SIDO DODOMA NA TSFR YA UINGEREZA ZATOA MSAADA WA ZANA ZA UFUNDI KWA WAJASILIAMALI WA WILAYA YA BAHI

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Bahi Elizabert Kitundu akimkabidhi Cheti Jafetty Maganigani baada ya kushiriki mafunzo ya ujasiliamali na kutumia Zana za ufundi zilizotolewa msaada na Shirika la kusaidia viwanda vidovidogo SIDO Mkoa wa Dodoma na TSFR ya Uingereza.
Mkuu wa Wilaya ya Bahi Elizabert Kitundu akizungumza kwenye mafunzo ya ujasiriamali na kutumia Zana za ufundi zilizotolewa msaada na Shirika la kusaidia viwanda vidovidogo SIDO Mkoa wa Dodoma na TSFR ya Uingereza.
 
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashari ya Wilaya ya Bahi Davis Komba akifafanua Jambo wakati alipokuwa akizungumza na vikundi vya wajasiriamali kabla ya SIDO kuwapa misaada ya nyezo za ufundi, wengine ni Mkuu wa Wilaya hiyo Elizabart Kitundu, Kaimu Meneja SIDO Mkoa wa Dodoma na Afsa Ufundi wa Shirika hilo Nyangusi Meitalami.
Mkuu wa Wilaya ya Bahi akikabidhi msaada wa Cherehani ya Kudalizia kwa wajasiriamali wa moja ya vikundi Vilivyoshiriki Mafunzo yaliyotolewa na SIDO Mkoa wa Dodoma ambapo Zana hizo za ufundi zimefadhiliwa na TSFR ya Uingereza.
Afsa Ufundi wa Shirika la kusaidia Viwanda Vidogo Vidogo (SIDO) Mkoa wa Dodoma Nyangusi Meitalami akiwaonyesha Baadhi ya Viongozi wa Wilaya ya Bahi na Wajasiriamali Zana ya kitobolea matundu kwenye uchongaji, Zana Hizo zenye Thamani ya Milion 20 zimetolewa na TSFR ya Uingereza kwa Vikundi 20 vya wajasiriamali wa Wilaya ya Bahi.
Picha ya Pamoja

WAZIRI MKUU AKUTANA NA MAKAMU WA RAISI WA KAMPUNI YA UTENGENEZAJI MELI NCHINI UFARANSA

$
0
0
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Makamu wa Rais wa Kampuni (Uendelezaji Bibiashara) wa Kampuni ya PIRIOU ya  utengenezaji na ukarabati wa  meli nchini Ufaransa, Bwana Michel Perrin kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Samweli Shelukindo.Waziri Mkuu amekuana naye leo Agosti 29, 2017 Paris nchini Ufaransa. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka watu wote wenye nia ya kutaka kuwekeza katika miradi mbalimbali nchini Tanzania kuhakikisha wanafuata sheria, kanuni na taratibu.


Ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Agosti 29, 2017) wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais (Uendelezaji Bishara) wa kampuni ya PIRIOU, Bw. Michel Perrin.

Waziri Mkuu amekutana na Bw. Perrin jijini Paris nchini Ufaransa kupitia ofisi ya ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa. Kampuni ya PIRIOU inataka kuja nchini kuwekeza katika utengenezaji na ukarabati wa meli.

Akizungumza na muwekezaji huyo Waziri Mkuu alimshukuru kwa nia yake ya kutaka kuwekeza nchini, ambapo alimtaka afuate sheria, kanuni na taratibu za uwekezaji nchini.

“Tanzania ni sehemu nzuri ya uwekezaji kwa sababu kuna fursa nyingi. Pia ni nchi yenye amani na utulivu wa kisiasa pamoja na mazingira mazuri ya uwekezaji hivyo nakukaribisha sana.”

Kwa upande wake Bw. Perrin amesema ameamua kuja kuwekeza nchini kwa kuwa Tanzania ni nchi salama na kwamba anauhakika wa kupata soko ndani ya nchi pamoja na mataifa jiraji.

Amesema anaamini uwekezaji wake nchini Tanzania utakuwa na tija, hivyo ameahidi kufanya kazi kwa ushirikiano wa karibu na Serikali na pia atahakikisha anafuata sheria zote za nchi.

Pia Bw. Perrin alitumia fursa hiyo kumshukuru Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Balozi Samwel Shelukindo kutokana na ushirikiano anaompa kuhusu masuala ya uwekezaji nchini.

Naye Balozi Shelukindo amesema atahakikisha anaendelea kutafuta wafanyabiashara mbalimbali na kuwashawishi waje kuwekeza katika sekta mbalimbali nchini

TFF YATOA NGAO MPYA YA JAMII

$
0
0

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetoa Ngao ya Jamii mpya kwa ajili ya kuipa Simba ambayo ilifanikiwa kuishinda Young Africans katika mchezo kuwania taji hilo uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Agosti 23, mwka huu. 

Siku hiyo mara baada ya mchezo ambao Simba ilishinda kwa mikwaju ya penalti 5-4, TFF ilitoa Ngao ya Jamii ambayo ilikuwa na makosa ya maandishi yaliyoonekana kwenye hivyo kuzua taharuki kwa wanafamilia wa mpira wa miguu.


TFF iliomba radhi na kuahidi kutoa Ngao ya Jamii nyingine ambayo sasa imetolewa leo Jumanne Agosti 29, mwaka huu na itakabidhiwa kwa Simba kabla ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya Azam FC jijini Dar es Salaam.

TAIFA STARS YAANZA MAZOEZI JIJINI DAR

$
0
0
Timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, imeanza kujifua leo asubuhi kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. 

Wachezaji wote kutoka klabu za Tanzania wamefika kadhalika baadhi kutoka nje ya mipaka ya Tanzania kama vile Nahodha Mbwana Samatta na Elias Maguli. Mazoezi hayo yataendelea kila siku hadi Ijumaa wiki hii.

Kikosi hicho kinachofanya mazoezi chini ya Kocha Mkuu, Salum Shabani Mayanga kinajindaa kucheza na Botswana katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa chini ya utaratibu wa kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA). 
Wiki ya FIFA kwa mechi za kimataifa inatarajiwa kuanza Jumatatu Agosti 28 hadi Septemba 5, mwaka huu ambako Tanzania imekubaliana kucheza Botswana kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam Jumamosi ya Septemba 2, 2017.


Katika kikosi hicho cha wachezaji 21, Kocha Mayanga amemwita upya Mlinzi wa Young Africans, Kelvin Yondani huku nyota kutoka nje ya mipaka ya Tanzania wakiwa ni saba.

Kikosi hicho kinachopiga kambi hoteli ya Sea Scape iliyoko Kunduchi, Dar es Salaam kina makipa Aishi Manula (Simba SC), Mwadini Ally (Azam FC) na Ramadhani Kabwili (Young Africans). 
Walinzi ni Gadiel Michael (Young Africans), Boniphas Maganga (Mbao FC), Abdi Banda (Baroka FC/Afrika Kusini), Kelvin Yondani (Young Africans), Salim Mbonde (Simba SC) na Erasto Nyoni (Simba SC). 

Viungo ni Himid Mao - Nahodha Msaidizi (Azam FC), Hamis Abdallah (Sony Sugar/Kenya), Mzamiru Yassin (Simba SC), Said Ndemla (Simba SC), Saimon Msuva (Difaa El Jadidah/Morocco), Shiza Kichuya (Simba SC), Farid Mussa (CD Tenerif/Hispania) na Orgenes Mollel (FC Famalicao/Ureno).


Washambuliaji ni Raphael Daud (Young Africans), Kelvin Sabato (Azam FC), Mbwana Samatta (KRC Genk/Ubelgiji) na Elias Maguli (Dhofar FC/Oman). Benchi la Ufundi la Mayanga linaundwa na yeye mwenyewe ambaye ni Kocha Mkuu, Fulgence Novatus (Kocha Msaidizi), Patrick Mwangata (Kocha wa Makipa), Danny Msangi (Meneja), Dkt. Richard Yomba (Daktari wa timu), Dkt. Gilbert Kigadye (Daktari wa Viungo) na Ally Ruvu (Mtunza Vifaa).

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na Katibu Mkuu Kiongozi pamoja na mawaziri wakisimama kwa heshima kumkumbuka aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri Marehemu Hassan Rashid shebuge aliyefariki mwezi Julai mwaka huu, kabla ya kuanza kwa kikao hicho kilichofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 29, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha baraza la Mawziri kulu jijini Dar es salaam leo Agosti 29, 2017.

WATU SITA WAFARIKI KWA AJALI YA LORI KIJIJI CHA KATIKA KIJIJI CHA KIJOTA, SINGIDA.

$
0
0

 Mmoja wa majeruhi akipatiwa matibabu ya mkono katika hospitali ya Mkoa wa Singida mara baada ya kupata ajali ya lori iliyoua watu 6 katika kijiji cha Kijota Singida.
 Mmoja wa majeruhi akiwa amelazwa huku akiendelea kupatiwa matibabu ya mkono katika hospitali ya Mkoa wa Singida mara baada ya kupata ajali ya lori iliyoua watu 6 katika kijiji cha Kijota Singida.
Baadhi ya ndugu na jamaa wa majeruhi wa ajali ya lori iliyoua watu sita wakiwa nje ya wodi za wagonjwa katika hospitali ya Mkoa wa Singida.

Watu sita wamefariki dunia huku wengine 42 wakijeruhiwa baada ya lori lenye namba za usajili T.806 AEL aina ya scania mali ya Abdalla Mussa (39) mfanyabiashara mkazi wa Mwenge mjini Singida, kuacha njia na kupinduka katika Kijiji cha Kijota, Singida.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida ACP Debora Magiligimba amesema ajali hiyo imetokea Agosti 27 mwaka huu saa 1.30 usiku katika kijiji cha Kijota wakati likitokea mnadani katika kijiji cha Mtinko Singida vijijini, likielekea Singida mjini.

ACP Magiligimba ametaja chanzo cha ajali kuwa ni uzembe wa dereva wa lori hilo Jumanne Kidanka (32) Kamanda huyo amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva ambaye hakuwa makini akiwa anaendesha lori hilo lililosheheni abira na mizingo mingi.

Amewataja waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni Haji Jumanne (35), Mikidadi Mohammed (40) wote wawili wakazi wa kijiji cha Mrama na Musa Salimu (30) mkazi wa kijiji cha Mwakiti.

ACP Magiligimba amewataja wengine kuwa ni Allen Mwangu (38) mkazi wa wilaya ya Ikungi, Lucas Stephano (40) mkazi wa kijiji cha Mrama na Sharifa Omari (19) mkazi wa kijiji cha Ilongero.

Ameongeza kuwa majeruhi 20 wamelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Singida, kumi wamelazwa hospitali ya misheni ya Mtinko na wanne ambao hali zao ni mbaya, wamelazwa katika hospitali ya misheni ya Hydom mkoani Manyara.

Ameeleza kuwa baadhi ya majeruhi walipatiwa matibabu na kurejea makwao huku wengine waliolazwa wamevunjika mikono, miguu na sehemu mbalimbali ya miili yao.

“Hawa wenye hali mbaya ni Fadhili Jumanne (33) mkazi wa Kibaoni mjini Singida, Mikidadi Hamisi, Jafari Hamisi na Idrisa Ibrahimu, wote wamevunjika miguu. Miili ya marehemu imehifadhiwa kwenye hospitali misheni Mtinko”, amesema.

NAIBU WAZIRI ANGELINA MABULA AFANYA ZIARA MKOANI GEITA, ASISITIZA UKUSANYAJI WA MAPATO YA ARDHI NA MAJENGO

$
0
0
 
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabula akiwasili kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Geita na akisalimiana na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa huo Nyuma yake ni mwenyeji wake ambaye ni Mkuu wa Mkoa, Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga
 Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabula,akisaini kwenye kitabu cha wageni ofisi ya mkuu wa Wilaya ya Mbongwe.
 Mkuu wa Wilaya ya Mbongwe Mathar Mkupasi akisoma taarifa ya ardhi na maendeleo ya ukusanyaji wa mapato ambayo yanatokana na ardhi pamoja majengo yaliyopo kwenye Halmashauri ya Wilaya Hiyo. Watumishi wa halmashauri ya Mboongwe pamoja na kamati ya Ulinzi na usalama wakifuatilia kikao cha Naibu waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbongwe Elias Kayandabila akionesha mchoro na ramani ya nyumba ambazo zinatarajia kujengwa na shirika la Nyumba la Taifa. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbongwe Elias Kayandabila akikabidhi ramani kwa meneja wa shirika la Nyumba Mwanza, Simiyu na Geita Mhandisi Benedict Kilimba . Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabula,akikagua mafaili kwenye ofisi za Ardhi za Wilaya hiyo. Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabula,akiangalia ramani ya Kijiji cha Bukandwe ambacho kipo kwenye Wilaya ya Mbongwe Mkoani Geita. Mkuu wa Wilaya ya Mbongwe Mathar Mkupasi akiagana na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabula wakati alipotembelea kijiji cha Bukandwe. Mkuu wa Wilaya ya Bukombe ,Josephat Maganga akisoma taarifa fupi ya Wilaya ya Bukombe kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula akikagua na kupatiwa maelezo na afisa ardhi mteule Joseph Kimondo . Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula ,akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Bukombe.PICHA ZOTE NA JOEL MADUKA .
Viewing all 45921 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>