Quantcast
Channel: VIJIMAMBO
Viewing all 45988 articles
Browse latest View live

Facebook Live with DICOTA & myAfyapal - Saturday October 14, 2017 @ 10:30 am

$
0
0

Pre Health Forum -Facebook Live  Event

myAfyapal

Leo | Jana | Kesho



On Saturday October 14, 2017 DICOTA, in partnership with myAfyapal, will host a Pre Health Forum -Facebook Live  Event.

Come learn about myAfyapal which was created mainly to offer a much needed  telehealth service to the majority of Tanzanians connected by telecom services. Join the Facebook Live Event to learn where they came from, where they are and where they’re heading.
TIME:
10:30 AM EST (USA)\
5:30 PM   EAT (Tanzania)

LOCATION

https://www.facebook.com/dicotausa

Visit DICOTA website for more information: http://www.dicotaus.org/events/




AGGREY & CLIFFORD WINS GOLD AWARD THROUGH VODACOM CAMPAIGN

$
0
0
Managing Director of Vodacom Tanzania PCL, Ian Ferrao (C) displays a gold award handed over by Aggrey & Clifford Founder and CEO, Rashid Tenga (R) during a press conference held in Dar es Salaam. Looking on is Vodacom’s Chief Officer of Communication, Rosayly Mworia. 
]Aggrey & Clifford Founder and Chief Executive Officer, Rashid Tenga, (R) speaks during a press conference to hand over a gold award to Vodacom Tanzania. Aggrey & Clifford had won the award for a TV commercial it had created for Vodacom Tanzania. The awards were issued recently in Singapore. Looking on is Vodacom Tanzania Plc Managing Director, Ian Ferrao (C) and Vodacom’s Head of Corporate Communications, Rosalyn Mworia. --- Aggrey & Clifford, an independent advertising agency headquartered in Dar es Salaam has scooped a prestigious international gold award from Spike Asia Festival of Creativity 2017, through Vodacom Tanzania’s Initial Purchasing Offers (IPO) campaign. Founded by a Tanzanian, Aggrey & Clifford was the only advertising agency from Africa to receive the gold award in one of industry’s global prestigious awards, held in Suntec, Singapore recently. The gold award marks Aggrey & Clifford’s second global recognition received this year. Earlier this year, the agency was recognized in London’s Campaign magazine as one of the World’s Leading Independent Agencies. Aggrey & Clifford won the gold award in the Film Craft category through a TV commercial it had created earlier this year for Vodacom Tanzania’s IPO campaign. In Spike Asia Festival of Creativity 2017 awards, Aggrey & Clifford was up against other agencies from Australia, New Zealand, China, Malaysia and Singapore. Aggrey & Clifford Founder and Chief Executive Officer, Rashid Tenga said receiving global recognition within the industry is proof that Aggrey & Clifford is executing world-class creative work for its clients. He thanked Vodacom Tanzania for trusting Aggrey & Clifford to provide them with marketing communication solutions especially in the creative department. “Vodacom has entrusted us with their most important marketing campaigns, for four years now Aggrey & Clifford has been Vodacom’s creative agency, I believe this is mainly because we have demonstrated that we have the knack for delivering world-class, outstanding creative work, and we couldn’t be prouder to get the opportunity to work with one of the most respectable brands in the telecom industry,” said Tenga. Vodacom Tanzania Managing Director, Ian Ferrao said, “I would like to thank everybody at Aggrey & Clifford and all of their team as well as Vodacom’s team for working together on this campaign which turned out to be a great success. This is a testimony of our the partnership we have with Aggrey & Clifford, it is one of the best agencies not just in Tanzania but across the entire continent.” Founded in 2009, Aggrey & Clifford has established branches in other East African countries, namely Uganda (Kampala), Rwanda (Kigali), Kenya (Nairobi). The agency offers a wide range of marketing communication services including public relations, media planning and media buying, social media and activations, to mention a few.

TAMKO LA MHE.WAZIRI MKUU - SIKU YA KIMATAIFA YA KUPUNGUZA ATHARI ZA MAAFA

$
0
0
Image result for majaliwa
 Ndugu Wananchi,
Oktoba13yakilamwakaniSikuyaKimataifayaKupunguzaMaafa. Maadhimishohayani utekelezaji waAzimio Na.64/200lililopitishwana BarazalaUmojawaMataifatarehe21Desemba,2009.Sikuhiiinalenga kukuzautamaduniwausimamiziwamaafakimataifa,ikiwanipamoja nakuzuia,kupunguzamadhara,kujiandaa,kukabilinakurejeshahali katika ubora zaidi pale maafa yanapotokea.


]
Ndugu Wananchi,
Katikakuadhimishasikuhii,SekretarietiyaUpunguzajiwaMadharaya MaafayaUmojawaMataifa(UnitedNationStrategyforDisaster Reduction-UNISDR)hutoaKaulimbiuyamwakahusika.Kaulimbiu ya mwaka huu inasema:
“MAKAZISALAMA:Punguza Makazi katika Maeneo Hatarishi,
Punguza Kuhama kutokana na Maafa
(HOME SAFE HOME: Reducing Exposure, Reducing Displacement).
Sikuhiinifursayakutambuamaendeleomakubwayanayofanywa katikakuletamatokeoyakupunguzahatarinamadharayamaafa katikamaisha,mifumoyamaishanaafya,kiuchumi,kijamii, kiutamaduninarasilimalizamazingira.Matokeohayonilengola Mkakati wa Sendai wa Kupunguza Madhara ya Maafawa 2015 2030.
1

MwakajanaKatibuMkuuwaUmojawaMataifaalifanyauzinduziwa "Kampeni ya Malengo Saba ya Sendai" ambayo inahamasishautekelezaji wamalengosabayaMkakatiwaSendaikatikakipindichamiakasaba. LengolamwakahuulinazingatiaKuzuia,KulindanaKupunguzaidadi yawatuwanaoathirikanamajanga,ambaloniLengolapili.Lengohili linahusuusalamawawatuwotelakinihasawalewaliokatikahatari zaidiyakifo,kuumia,kuathirikakiafya,madharayamfumowamaisha, kuhamamakaziyaonaukosefuwaupatikanajiwahudumazamsingi kutokananamatukioyamaafahasakwawanawake,watoto,watu wenyeulemavunawazee.Ikumbukwekatikanchiyetutunaidadi kubwayawananchiwaliokatikamakundihaya.Takwimuzetu zinaoneshaidadiyawazeeniasilimia5.5,watotochiniyamiakamitano niasilimia15.2nawatuwenyeulemavuwaainambalimbaliniasilimia
6.Makundihayanimuhimunahivyoyanahitajikuzingatiwakipekee katika mipango ya usimamizi wamadhara ya maafa.

Ndugu Wananchi,
Maadhimishohayayanasisitizaumuhimuwanyumbayafamiliakama mahalirasminasalamawakatiwamaafa.Nyumbayafamiliamara nyingindipomahalipakazizakujipatiakipatokwajamiizakipatocha chinihapanchini.Serikaliimekuwaikichukuahatuambalimbali kuhakikishawananchiwanaishikatikamaeneosalama,kwakuandaana kutekelezaSerayaTaifayaArdhiyamwaka1995naSerayaTaifaya MaendeleoyaMakaziyamwaka2000nakutunganakusimamia
2

utekelezajiwaSheriayaMipangoMijiyamwaka2007.Vilevile,Serikali imeendeleakuyapanganakuyapimamaeneoyamakaziilikuhakikisha wananchiwanaishikatikamakaziboranasalamakuepukamadharaya maafa.HadikufikiaSeptemba2017jumlayaviwanjatakriban3,500,000 vilikuwavimepangwanakatiyahivyotakribanviwanja1,500,000 vimepimwakatikaHalmashaurimbalimbalinchini.Vilevile,ili kupunguzaujenziholelanakatikamaeneohatarishi,Serikali imeendeleakuandaaMipangokabambeitakayoongozauendelezajina ukuajiwamiji.HadiSeptemba2017jumlayaHalmashauri13zilikuwa katika hatua mbalimbali za uandaaji wa mipango kabambe.

Ndugu Wananchi,
Kwakuelewaumuhimuwanyumbayafamilia,Serikaliimeendelea kuwalindawananchikutokananamadharayamaafakwakuimarisha mazingirayaonakuwahamishiakatikamaeneoyamakazibora. MiongonimwahatuahiziniukarabatiwatutalamtoMkondoa WilayaniKilosabaadayakuharibiwanamafurikoyaliyotokeamwezi Desemba,2009naJanuari,2010ambapokaya5,981zilikosamakazi. Vilevile,Serikaliiliwapatiawananchiviwanjakatikaeneola MabwepandebaadayakuathiriwanamafurikokatikaeneolaBondela JangwanimweziDesemba,2011iliwaishikatikaeneosalama.Nasisitiza SerikalizaMitaaziongezekasiyakupimaviwanjailiwananchi wakihitajikujengawapatemaeneosalama.Aidha,SerikaliyaAwamu yaTanoimendeleakuhakikishakwambamaeneoyaliyojengwakiholela yanarasimishwakwakupangwa,kupimwanakuwekewa miundombinu pamojana kutengewa maeneoyahuduma zajamiikatika
3

Halmashauri mbalimbali. Nyumba zilizojengwa katikamaeneohatarishi kamavilemabondeninakwenyemiteremkomikalihayafanyiwi urasimishaji.Vilevile,shughulizaujenzizifanyikekwakutumia wataalamwaliosajiliwanaBodiyaUsajiliwaWabunifuwaMjaengona WakadiriajiMajanzi,ambaohadimweziJuni2017Bodiimesajili wataalam 1,315 na makampuni 354.

Ndugu Wananchi,
Maafayanayotokananamatukioyanayohusiananahaliyahewa yanaongezekanakusababishaidadikubwayavifo.Vilevile,takwimu zinaoneshazaidiyanusuyavifovyamaafadunianihusababishwana matukiomakubwayamaafayakijiolojia,hasatetemekolaardhi.Hapa nchini,jumlayawananchiwapatao117,721waliathirikakutokanana tetemekolaardhiMkoaniKageratarehe10Septemba,2016na kusababishauharibifuwanyumbazamakazi,vifonamajeruhi.Serikali yaAwamuyaTanoinaendeleanajuhudizakuhakikishainarejeshahali kwauborazaidinahudumamuhimukwawananchiwalioathirika. Aidha,SerikalikupitiaWakalawaJiolojiaTanzaniainakusudia kusimikavituovyakuratibumatetemekoyaardhikatikamaeneoya mkoawaKageraambaokwasasaunakumbwanamatetemekoyaardhi yamarakwamara.MpakasasaSerikalikupitiaWakalaimesimikajumla yavituotisa(9)vyakudumuvyakuratibumatetemekoyaardhi ambavyovikokatikamaeneoyaDodomamjini,Kondoamjini,Kibaya mjini,Singidamjini,Mtwaramjini,Geitamjini,Arushamjini,Mbeya (eneo la gereza la Songwe) naBabatimjini.




MafanikioyautekelezajiwaMkakatiwaSendainimuhimukatika kufikiaAgendaya2030yaMaendeleoEndelevu,hasaMalengoya MaendeleoEndelevunaMkatabawaPariskuhusuMabadilikoya Tabianchi.Serikaliitaendeleakuzingatiamasualahayanaupunguzaji wamadharayamaafakatikautekelezajiwaMpangowaPiliwa MaendeleoyaTaifawaMiakaMitano2016/17-2020/21naDiraya MaendeleoyaTaifa2025.PamojanajuhudizaSerikali,nitoewito,Sisi sotetunawajibika,namafanikioyaMalengoyaMaendeleoEndelevu yanatutegemea.

Ndugu Wananchi,
Nidhahirikwambakuchukuahatuakatikasualahilikutaonesha kwambakunamikakatikatikangaziyataifanaserikalizamitaa inayolengausimamiziwamaafahapanchini.Sualahilinichangamoto kubwaambayoinawezakufanikiwaendapokutakuwanaushirikiano nauratibumzuribainayawadaumbalimbali.Serikaliinafanyamarejeo yaSerayaTaifayaUsimamiziwaMaafayamwaka2004nakufanya tathmininakuandaaramanikuoneshamaeneohatarishikwamajanga ili kusaidia katika kuhakikisha wananchi wanaishi maeneo salama.
HivyonitoeraikwaJamii,Wizara,IdaranaTaasisizaUmma,Sekta BinafsinaWadauwaMaendeleokuungamkonojitihadazaSerikaliya AwamuyaTanokatikakuhakikishawananchiwanaishikatika mazingirasalamadhidiyamadharayamajangambalimbali.Kwa ushirikianowapamoja,tutakuwatumefanikishakuwanaMakazi
5

Salama nakujengamwamkokwajamiikuhusukuchukuahatuastahiki kwa kutambua kuwa maafa hutokea wakati wowote.
“Punguza Makazi katika Maeneo Hatarishi, Punguza Kuhama
kutokana na Maafa
AHSANTENI SANA
KASSIM MAJALIWA MAJALIWA
WAZIRI MKUU





ALI KIBA MIMI SIO MTU WA KUSHOW OFF KAMA DAIMOND

BATULI MOHAMED AWAKILISHA TANZANIA KWENYE MASHINDANO YA UREMBO YA MISS GRAND INTERNATIONAL 2017 VIETNAM MSHINDI KUJULIKANA OCT 25

HUONI HAFIFU HUCHANGIA MATOKEO MABAYA KWA WANAFUNZI DARASANI

$
0
0

Mwalimu wa shule ya Msingi Nguvumali Jijini Tanga akichukua maelezo ya wanafunzi kabla ya kuanza zoezi la upimaji wa huduma ya macho wakati wa siku ya afya ya macho duniani ambapo siku hiyo iliendana na sambamba na upimaji macho ulioendeshwa na Duka la Miwani la Noor Optics kwa kushirikiana na halmashauri ya Jiji hilo kwa wanafunzi wa shule za msingi za mabokweni,kwanjeka na nguvumali,
Mratibu wa Huduma za Macho Mkoa wa Tanga,Dkt Frida Kassiane akiwapima macho mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi Nguvumali Jijini Tanga wakati wa siku ya afya ya macho duniani ambapo siku hiyo iliendana na sambamba na upimaji macho ulioendeshwa na Duka la Miwani la Noor Optics kwa kushirikiana na halmashauri ya Jiji hilo kwa wanafunzi wa shule za msingi za mabokweni,kwanjeka na nguvumali,
Amina Nasoro ambaye Mratibu wa Huduma ya Afya ya Macho katika kampuni ya kampuni ya Noor Optics inayojishughulisha na matibabu ya macho na utoaji wa miwani Jijini Tanga akichukua maeleza ya wanafunzi kabla ya kuwapima
Amina Nasoro ambaye Mratibu wa Huduma ya Afya ya Macho katika kampuni ya kampuni ya Noor Optics inayojishughulisha na matibabu ya macho na utoaji wa miwani Jijini Tanga akichukua maeleza ya wanafunzi kabla ya kuwapima
Zoezi la Uandikishaji wa majina wanafunzi wa shule ya Msingi Nguvumali kwa ajili ya upimaji wa macho likiendelea 
Zoezi la kuwapima wanafunzi likiendelea 

SABABU kubwa za wanafunzi wa shule za msingi kutokufanya vizuri darasani imeelezwa inatokana na uoni hafifi kwa baadhi yao na sio kwamba hawana akili .

Lakini pia imebainishwa pia kati ya watu 100 kati ya 15 wana kabi liwa na tatizo la macho ambalo limekuwa likiwaathiri kwa asilimia na kushindwa kufikia malengo yao.

Hayo yalibainishwa juzi na Mratibu wa Huduma za Macho Mkoani Tanga Dkt Frida Kassiane wakati wa siku ya afya ya macho duniani ambapo yalienda sambamba na upimaji wa macho uliokuwa ukiendeshwa na kampuni ya Noor Optics inayojishughulisha na matibabu ya macho na utoaji wa miwani Jijini Tanga.

Alisema hatua hiyo inatokana na baadhi ya wanafunzi kuumwa macho huku wakiwa hawajitambui kutokana na kutokuwepo kwa utaratibu za utoaji wa huduma za upimaji machi kwao hususani mashuleni.

“Ukiangalia leo hii baadhi ya wanafunzi utakuwa walikuwa wakifanya vizuri katika mitihani yao lakini ghafla wanaanza kushuka kiwango na hili unaweza kukuta linasababishwea na tatizo la macho kama lilivyogundulika kwa wanafunzi wachache kwenye shule tulizopita “Alisema.

Alisema suala hilo linasababishwa pia na lishe dunia kwa asilimia kubwa ya watoto wengi ikiwemo kukosa kupata vyakula vilivyokuwa na virutubisho vinavyoweza kuongeza nguvu na kinga ya macho.

Alisema zoezi hilo ambalo limeanza siku nne zilizopita limewafikia zaidi ya wanafunzi 1500 katika shule za Msingi,Kwanjeka,Mabokweni na Nguvumali ambapo baadhi yao walibainika kuna matatizo hayo na kusaidia matitabu zaidi na kampuni hiyo.

Naye kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Noor Optics, Raouf Nasser alisema lengo kubwa ni kutoa huduma hiyo katika shule zote za msingi ili kusaidia kubaini changamoto za macho zinazowakabili na namna ya kupatiwa ufumbuzi.

Alisema alisema kampuni hiyo kwa kushirikiana na halmashauri ya Jiji la Tanga wameamua kuendesha zoezi hilo kila mwaka ili kuweza kuwasaidia watoto ambao watabainika wanakabiliwa na matatizo hayo ili waweze kufikishwa kwa wataalamu kwa matibabu zaidi.

“Asilimia kubwa ya wazazi hawana uwezo wa kuwapeleka watoto wao katika hospitali kufanyiwa vipimo vya matatizo hayo hivyo sisi tumeamua kwa nia moja kusaidia jamii ikiwa ni kurudisha faida kwao kutokana na huduma tunazotoa “Alisema.

Aidha alisema msingi mzuri wa kuyatunza macho ni lazima kuwepo utaratibu wa kuyafanyia vipimo mara kwa mara hasa wanapokuwa kwenye hatua ya ukuaji kabla ya kufikia umri mkubwa ambapo tatizo hilo linaweza kuwa kubwa zaidi.

Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

MAGAZETI YA LEO OCTOBER 13, 2017

POLISI WAUA WATUHUMIWA WALIOMJERUHI MEJA JENERALI MSTAAFU

$
0
0
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dsm mnamo tarehe 11.10.2017 majira ya saa nne kamili usiku huko maeneo ya Mbezi Mshikamano kwa Mgalula, askari walipata taarifa kutoka kwaFRANCIS MINDE miaka 30, mfanyabiashara ambaye anamiliki duka la vitu mchanganyiko kwamba walifika watu wawili katika duka lake wakitumia pikipiki aina ya Boxer nyeusi ambayo haikusomeka namba na kumuuliza kama kuna huduma ya M-PESA na TIGO-PESA na kuwajibu kuwa hakuna huduma hiyo, aliwatilia mashaka huenda sio watu wazuri hatimaye alitoa taarifa Polisi.

Mara baada ya kupata taarifa hizo askari walikwenda eneo hilo na kuiona pikipiki ikiwa imeegeshwa gizani ikiwa na watu watatu, askari waliwaita watu hao ili kuwahoji lakini watu hao walianza kukimbia huku wakifyatua risasi upande waliopo askari, kuona hivyo askari nao walijibu mashambulizi na kufanikiwa kuwajeruhi majambazi wawili, mmoja kati yao alifanikiwa kukimbia na pikipiki waliyokuwa nayo.

Aidha eneo la tukio ilikutwa Silaha aina ya SMG yenye namba UC59821998 ikiwa na magazine mbili, magazine moja ikiwa na risasi kumi na tisa (19) na nyingine ikiwa tupu na maganda kumi na tatu (13) ya risasi aina ya SMG.

Katika ufuatiliaji wa tukio hilo ilibainika kuwa mmoja wa majambazi hao waliouwawa ni miongoni mwa watuhumiwa walioshiriki tukio la kuvamiwa kwa Meja Generali mstaafu wa Jeshi la Wananchi VICENT KARIONGO lililotokea mnamo tarehe 11/09/2017 majira ya saa kumi na moja jioni.

Majeruhi wote wawili walifariki dunia wakiwa njiani kupelekwa Hospitali ya Mwananyamala. Hakuna askari aliyeumia au kujeruhiwa, miili ya marehemu imehifadhiwa Hospitali ya Mwananyamala. Jitihada za kumtafuta jambazi aliyekimbia zinaendelea.

Wakati huo huo, Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dsm mnamo tarehe 12.10.2017 majira ya saa nane na nusu usiku huko maeneo ya Mbezi Luis, Tegeta “A” askari walipata taarifa kuwa katika Bar iitwayo TUMAINI, kuna majambazi ambao idadi yao haijajulikana wakiwa na gari no. T 563 TAH aina ya Toyota Noah rangi ya Blue ikiwa imetolewa viti vyote vya nyuma na kubaki siti ya dereva na abiria, lengo lao lilikiwa ni kupakia vitu ambavyo wangeiba kwenye Bar hiyo.

Wakati wakiendelea na uvunjaji askari walifika eneo la tukio na baada ya kugundua askari wamefika majambazi hao walifanikiwa kukimbia na kutelekeza gari hilo, majambazi hao hawakufanikiwa kuchukua mali yeyote na gari lipo kituo cha Polisi. Ufuatiliaji unaendelea wa kujua mmiliki wa gari lililotumika katika tukio hilo.

POLISI KANDA MAALUM DSM KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI KUANZIA TAREHE 06.10.2017 HADI TAREHE 11.10.2017 KIMEFANIKIWA KUKUSANYA TSH 466,350,000/= KWA TOZO ZA MAKOSA YA USALAMA BARABARANI

Jeshi la Polisi kanda maalum Dar es salaam kupitia Kikosi chake cha Usalama barabarani kinaendelea na oparesheni ya ukamataji wa makosa ya Usalama Barabarani kwa kipindi cha kuanzia tarehe 06.10.2017 hadi tarehe 11.10.2017 kama ifuatavyo:-

Idadi ya magari yaliyokamatwa – 14,340
Idadi ya Pikipiki zilizokamatwa – 413
Daladala zilizokamatwa -5,024
Magari mengine (binafsi na malori) -1,205
Bodaboda waliofikishwa Mahakamani
kwa makosa ya kutovaa helmet na kupakia mishikaki -15
Jumla ya Makosa yaliyokamatwa – 15,545
Fedha za Tozo zilizopatikana – 466,350,000 /=

Magari yaliyokamatwa kutokana na
Kuchelewa kulipa faini kwa wakati – 2,832
(zaidi ya siku 7)

Kiasi kilicholipwa – 264, 673,4000/=

L .B.MAMBOSASA – SACP
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM

STEPHEN WASIRA NDANI YA WASHINGTON, DC

$
0
0
Mh Stephen Wasira in Washington DC this week , meetings with U.S Chambers of Commerce, Hon Balozi of Tanzania HE Wilson Masilingi and finally Chief of Staff at American University , he's Alumni talking about Tanzania and our great nation, ahsante

MRADI WA UMEME MAKAMBAKO-SONGEA KUPUNGUZA GHARAMA ZA UENDESHAJI SHAMBA LA KAHAWA AVIV MKOANI RUVUMA KWA ASILIMIA 70

$
0
0

Meneja wa Shamba la Kahawa, Aviv linalomilikiwa na kampuni ya Olam Tanzania Limited lililoko kijiji cha Lipokela kilomita 45 kutoka Songea mjini Bw.Hamza Kassim, (katikati) akizungumzia mradi wa umeme wa Makambako-Songea ambao utaunganishwa kwenye kiwanda chake, mbele ya wahariri wa vyombo vya habari waliofika kiwandani hapo ili kujionea manufaa yatokanayo na mradi huo katika uwekezaji mkubwa, Oktoba 12, 2017.



NA K-VIS BLOG/KHALFANS SAID, SONGEA

UONGZI wa Shamba la Kahawa la Aviv, lililoko kijiji cha Lipokela, kilomita 45 kutoka Songea mjini, umesema Mradi wa umeme wa Makambako-Songea utaleta nafuu kubwa ya kupunguza gharama za kuendesha majenereta ya kufua umeme kwenye shamba hilo kwa asilimia 70,  Meneja wa shamba Bw.Hamza Kassim amesema.

Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari waliotembelea shamba hilo ili kupata maoni ya wamiliki kuhusiana na mradi mkubwa wa umeme wa 220kV, Makambako- Songea  Oktoba 12, 2017, Bw. Kassim alisemamahitaji ya umeme kwenye shamba hilo ni  Megawati 2.25 hadi 2.5 na zote hizo zinazalishwa na umeme wa kutumia mafuta (Jenereta). 


shamba hilo linalo ilikiwa na kampuni ya Olam Tanzania Limited yenye makao yake makuu nchini Songapo, lina ukubwa wa Hekta 1,012 kati ya hizo, Hekta 1,000,000 zimepandwa mazao.


“Mimea ya Kahawa ambayo imefikia hatua ya kupevuka (matured), ni Hekta 800, huku Hekta 200 bado ni Kahawa changa, tunatumia nishati ya umeme kwa shughuli za umwagiliaji na ubanguaji wa Kahawa ambapo kwa siku tunatumia lita 4,000 za dizeli kuendesha jenereta hizo.” Alifafanua Bw. Kassim.



Ujio wa mradi huu ni faraja kubwa kwetu na tunashukuru mradi huu utakapokamilika utatupunguzia gharama za uendeshaji kwa asilimia 70 na hivyo kutupa fursa ya kufanya upanuzi zaidi wa kilimo cha kahawa, Alibainisha Meneja huyo.



Kwa upande wake Meneja wa Shirika la Umeme Nchini, (TANESCO), Mkoa wa Ruvuma, Mhandisi Patrick Lwesya alisema, Shamba la Aviv, ni moja kati ya wateja wake elfu kumi, (10,000),  ambao wataunganishiwa umeme, Desemba mwaka huu 2017 baada ya kukamilika kwa ujenzi wa mfumo wa usambazaji umeme wa kilovolti 33 pamoja na kuunganisha wateja 22,700, katika mikoa ya Songea na Njombe.

“Shamba hili ndio wateja wetu wakubwa kabisa, na tunamuhakikishia muwekezaji huyu kumpatia umeme zaidi endapo atauhitaji kwani kwa sasa tunazalisha umeme kwa asilimia 99.75, lakini mradi ukikamilika tutazalisha kwa asilimia 100 na umeme utakuwa bora na wa uhakika.” Alisema Mhandisi Lwesya.

Alisema, pamoja na mteja huyo wa shamba la Kahawa la Aviv, pia wateja wengine watakaofikishiwa umeme chini ya mradi huo ni pamoja na wale wa Mji wa Songea, vijiji vilivyo katika wilaya za Mbinga, Namtumbo na Halmashauri ya Madaba.

“Nitoe wito kwa wawekezaji kuja kuwekeza mkoani kwetu kwani tunao umeme wa kutosha kutokana na uzalishaji wake ambapo tunazalisha jumla ya Megawati 6.3 huku mahitaji halisi ya Mkoa ni Megawati 5.3.” Alisema.

Hata hivyo kumekuwepo vitendo vya uharibifu wa miundombinu hiyo mipya iliyojengwa chini ya mradi huu vinavyofanywa na baadhi ya wananchi wanaochoma misitu kwa ajili hya kuandaa mashamba.

Wahariri walishuhudia nguzo mbili moja ikiwa imeungua vibaya huku nyingine ikiwa imeungua kabisa na kubaki nyaya zikining’inia kandokando ya barara ya Songea-Mbinga kwenye kijiji cha Lipokela.

“Vitendo hivi vinasikitisha sana, niwaombe wananchi waache tabia hiyo kwani mradi huu unakwenda kubadilisha maisha yao na kwa kufanya uharibifu huu ni kuhujumu jitihada za Shirika la Umeme TANESCO kwa niaba ya Serikali, kutatua changamoto ya upatikanaji umeme wa uhakika kwa wananchi.” Alisema Meneja wa Mradi wa umeme wa Makambako-Songea Mhandisi Didas Lyamuya.

Maneno ya Meneja huyo yaliungwa mkono na Meneja wa Shamba la Aviv ambalo liko jirani na eneo ambako nguzo hizo zilichomwa moto na kutaka utamaduni wa wananchi wa mkoa wa Ruvuma wa kuchoma moto nyasi na misitu kwa nia ya kutayarisha maeneo ya kilimo waache.

“Nilifurahi ni hivi majuzi tu Mkuu wa Mkoa alizunguzia vitendo hivi na kuwaagiza viongozi wa serikali kwenye kata na vijiji kuwaelimisha wananchi kuhusu madhara ya vitendo hivyo, na kwa uoande etu sisi tumejenga mifumo ya kuzima moto kuzunguka eneo letu la shamba.” Alibainisha.
Meneja wa Shirika la Umeme (TANESCO) Mkoa wa Ruvuma, Mhandisi Patrick Lwesya, (w akwanza kulia), akizungumza kwenye eneo la Shamba la Aviv, kuhusu hatua iliyofikiwa na TANESCO kupeleka umeme wa kutosha kwenye shamba hilo ifikapo Desemba mwaka huu wa 2017. Wengine pichani kutoka kushoto mstari wa mbele, ni pamoja na Meneja Mradi wa umeme Makambako-Songea, Mhandisi Didas Lyamuya, na Meneja wa Shamba hilo, Bw. Hamza Kassim, (katikati).

Kamimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji, akiwaonyesha Wahariri kibao cha alama ya hatari, kilichowekwa kwenye moja ya nguzo za umeme zilizoteketea kabisa kwa moto. Nguzo hizo mpya zimesimikwa hivi karibuni ikiwa ni utekelezaji wa ujenzi wa mfumo wa usambazaji umeme wa kilovolti 33 kwenye maeneo ya vijijini chini ya mradi huo wa Makambako-Songea. Uharibifu huo ulifanywa kwenye kijiji cha Lipokela kandokando ya barabara ya Songea-Mbinga, mkoani Ruvuma.
 Bi. Leila Muhaji na Bw. Fredrik Lewerstrom kutoka kampuni ya Sweco, wakionyesha kuhuzunika kufuatia uharibifu mkubwa wa kuchoma nguzo ya umeme kijiji cha Lipokela.
 Huu ndio uharibifu uliofanywa na wananchi wanaochoma moto nyasi na misitu mkoani Ruvuma na hivyo kuunguza miundombinu ya TANESCO


 Wahariri na wahandisi wa TNESCO wakiwepo wakandarasi wa Mradi wa umeme wa Makambako-Songea wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutembelea kituo cha sasa cha kufua umeme eneo la Lizaboni mjini Songea Oktoba 12, 2017.
  Wahariri na wahandisi wa TNESCO wakiwemo wakandarasi wa Mradi wa umeme wa Makambako-Songea wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutembelea eneo la ujenzi wa kituo kipya cha kupoza umeme mjini Songea Oktoba 12, 2017
 Meneja wa Mradi wa umeme wa 220kV, Makambako-Songea Mhandisi Didas Lyamuya, akifafanua baadhi ya mambo kwenye eneo la ujenzi wa kituo kipya cha kupoza umeme cha Songea ambacho kiko katika hatua ya ujenzi wa msingi wa kufungia mitambo. Chini ya mradi huo jumla ya vituo vipya viwili vya kupoza umeme vinajengwa huko Madaba na kimoja kinafanyiwa upanuzi huko Makambako
Taswira ya ujenzi wa msingi wa kufungia mitambo kituo kipya cha kupoza umeme cha Songea.

Viongozi wa makundi ya What's App waonywa

$
0
0
Image result for whatsapp
By Elizabeth Edward, Mwananchi

Dar es Salaam. Jeshi la polisi kitengo cha makosa cha makosa ya mtandaoni limewatahadharisha viongozi wa makundi ya What's App na kuwataka kutoa taarifa pindi uhalifu unapofanyika kwenye makundi yao.

Kufanya hivyo kutasaidia polisi kuchukua hatua dhidi ya mhusika aliyefanya uhalifu huo ili kukabiliana na ongezeko la vitendo vya uhalifu mtandaoni.

Hayo yameelezwa leo Ijumaa na naibu mkuu wa kitendo hicho, Joshua Mwangasa wakati wa semina iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano(TCRA) na kuwakutanisha viongozi wa dini wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Amesema makosa ya kimtandao yameendelea kuongezeka kwa kasi kubwa huku makundi ya What's App yakionekana kuwa kichocheo kikubwa.

Mwangasa amesema viongozi wa makundi hayo hawatakiwi kuvumilia makosa hayo hivyo wanatakiwa watoe taarifa polisi.

"Usikubali umeanzisha kundi kwa nia nyingine halafu mtu au watu wanaweka mambo yasiyofaa, toa taarifa hatua zichukuliwe kinyume na hapo hata wewe utahusika,"

Amesema kwa kiasi kikubwa makundi hayo yamekuwa yakitumika kusambaza taarifa za uongo na uchochezi.

Mwangasa ametumia fursa hiyo kuwaomba viongozi wa dini kuwahubiria waumini wao juu ya matumizi sahihi ya mitandao ili kujiweka mbali na uhalifu.

"Ukosefu wa maadili ndio unachangia haya yote haya, ndiyo sababu narudi kwenu viongozi wa dini wasisitizeni waumini wenu watumie mitandao kwa maendeleo," amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa TCRA, Mhandisi James Kilaba amesema mamlaka hiyo inaendelea kuchukua hatua kuimarisha ulinzi wa mawasiliano mtandaoni.

Amesema simu za mkononi kwa sasa zimekuwa kama silaha hivyo matumizi yake yanapaswa kuangaliwa kwa umakini zaidi.

JAFO AZIAGIZA HALMASHAURI ZINAZODAIWA NA BODI YA MIKOPO YA SERIKALI ZA MITAA KUREJESHA MIKOPO YAO.

$
0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo  akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo mjini Dodoma kuhusu hali ya urejeshaji mikopo kutoka  kwenye Mamlaka ya  Serikali za Mitaa zinazodaiwa na Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa.
 Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Mkopo ya Serikali za mitaa Bw. Richard Mfugale akizungumza na waandishi wa habari, leo Mjini Dodoma kuhusu jitihada zinazoendelea kuchukuliwa na Bodi hiyo katika kuhakikisha halmashauri zinazodaiwa zinalipa madeni yao kwa wakati.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo akiongea na waandishi wa habari kuhusu hali ya urejeshaji mikopo kutoka  kwenye Mamlaka ya  Serikali za Mitaa, wakati alipokutana na Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Mkopo ya Serikali za mitaa Bw. Richard Mfugale leo mjini Dodoma. 
(Picha na Beatrice Lyimo-MAELEZO, DODOMA)

Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo amezitaka Halmashauri zote zinazodaiwa na Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa kurejesha madeni yao kabla ya Desemba 30 mwaka huu.
Jafo ametoa agizo hilo leo Mjini Dodoma alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu marejesho ya mikopo katika bodi hiyo kutoka kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa.
“Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa imefanikiwa kutoa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 9.7 hadi Septemba 30, 2017 kwa Halmashauri 54. Hadi Septemba 30, 2017 jumla ya shilingi 6.57 zilirejeshwa,” alisema Jafo.
Aliendelea kwa kusema kuwa halmashauri nyingi zimejitahidi katika kurejesha mikopo waliyochukua lakini kuna Halmashauri 9 zimeonyesha usugu uliopitiliza katika kurejesha mikopo hiyo, ambapo zaidi ya shilingi bilioni 2 hazijarejeshwa kutoka katika Halmashauri hizo.
Jafo amezitaja Halmashauri zilizoonyesha usugu kuwa ni Halmashauri ya Jiji la Mwanza na Mbeya, Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, Singida na Morogoro, Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma, Karatu, Pangani, Igunga, Mbinga, Mji Mbinga na Kongwa.
Aidha amesema kuwa , kitendo cha usugu katika urejeshaji wa mikopo kinanyima fursa kwa Halmashauri nyingine kupata mikopo kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
Hivyo basi, Waziri Jafo amemtaka Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Mikopo kufanya ufuatiliaji ili wadaiwa wote waweze kurejesha mikopo yao na wadaiwa sugu kurejesha mikopo kabla ya Desemba 30, mwaka huu.
Hata hivyo Jafo ameitaka Bodi hiyo kuangalia utaratibu wa kupitisha mikopo inayolenga ujenzi wa viwanda na uwekezaji katika Halmashauri ili kukuza ajira na uchumi wa viwanda.
Kwa upande wake,  Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa Richard Mfugale amesema kuwa bodi itatekeleza agizo la Waziri na tayari imeshafanya mawasiliano na halmashauri zinazodaiwa kuona vyanzo vya mapato watakavyoviachia kwa ajili ya kulipa madeni yao.
Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa ilianzishwa kwa lengo la kuziwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa kupata mikopo ili kutekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo na utoaji huduma za jamii katika maeneo yao.

WASHIRIKI WA SHINDANO LA MISS SHINYANGA 2017 WAUNGA MKONO KAMPENI YA UPANDAJI MITI SHINYANGA

$
0
0

Washiriki wa shindano la kutafuta mrembo wa mkoa wa Shinyanga“Miss Shinyanga 2017”,wameunga mkono kampeni ya upandaji miti iliyoanzishwa katika wilaya ya Shinyanga na Mkuu wa wilaya hiyo Josephine Matiro hivi karibuni ili kupambana na hali ya ukame/jangwa mkoani humo.



Mapema leo Ijumaa Oktoba 13,washiriki hao wa shindano hilo la mrembo wa mkoa wa Shinyanga linalotarajiwa kufanyika Oktoba 15 mwaka huu,walimwagilia maji miti mbalimbali iliyopandwa mjini Shinyanga.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo,Mwandaaji wa shindano la Miss Shinyanga mwaka 2017,Grace Shija alisema pamoja na kufanya maandalizi ya shindano hilo pia wanashiriki katika shughuli za kijamii.
“Sisi kama sehemu ya jamii tumeamua kushiriki katika kampeni ya upandaji miti kwa kumwagilia maji miti iliyopandwa katika maeneo mbalimbali mjini Shinyanga kwa kujaza maji kwenye chupa zilizowekwa kutiririsha matone ya maji kwenye miti hiyo”,alieleza Shija.
Akizungumzia kuhusu shindano la Miss Shinyanga mwaka huu alisema jumla ya warembo 12 kutoka wilaya zote za mkoa wa Shinyanga watachuana siku ya Jumapili Oktoba 15,2017 katika ukumbi wa NSSF ya Zamani mjini Shinyanga kuanzia saa mbili usiku ili kupata mrembo wa mkoa mwaka huu.
Washiriki wa shindano la Miss Shinyanga 2017 wakitoka Diamond Fields Hotel walipoweka kambi mjini Shinyanga wakielekea kwenye maeneo ambayo yamepandwa kwa ajili ya kuweka maji kwenye miti hiyo.Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Washiriki wa shindano la kutafuta mrembo wa mkoa wa Shinyanga “Miss Shinyanga 2017” wakiwa wamebeba madumu ya maji kwa ajili ya kuweka kwenye miti ambayo inamwagiliwa maji kwa njia ya makopo ya maji yaliyotobolewa kwa ajili ya kutoa matone kidogo kidogo
Mshiriki wa shindano la Miss Shinyanga 2017 akimwaga maji kwenye kopo jingine
Mrembo akimwagia maji mti kwa kuweka maji kwenye kopo lililowekwa kwenye mti 
Zoezi la kumwagilia maji miti likiendelea
Warembo wakielekea katika eneo jingine kwa ajili ya kumwagili maji miti iliyopandwa hivi karibuni
Mrembo akimwagilia mti
Zoezi la kumwagilia miti likiendelea
Mrembo anamwagilia maji mti
Zoezi la kumwagilia maji likiendelea
Warembo wakimwagilia maji mti
Washiriki wa shindano la Miss Shinyanga wakimwagilia maji mti
Washiriki wa Shindano la Miss Shinyanga 2017 wakijaza maji kwenye makopo ili waendelee kuweka kwenye makopo yaliyowekwa kwenye miti
Zoezi la kujaza maji kwenye makopo likiendelea
Zoezi la kumwagilia maji likiendelea
Warembo wakimwagili maji kwenye miti
Washiriki wa shindano la Miss Shinyanga 2017 wakirudi kambini baada ya kumaliza kumwagilia maji kwenye miti iliyopandwa mjini Shinyanga.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Viongozi wa makundi ya WhatsApp waonywa

$
0
0
Jeshi la polisi kitengo cha makosa cha makosa ya mtandaoni limewatahadharisha viongozi wa makundi ya What's App na kuwataka kutoa taarifa pindi uhalifu unapofanyika kwenye makundi yao.
Kufanya hivyo kutasaidia polisi kuchukua hatua dhidi ya mhusika aliyefanya uhalifu huo ili kukabiliana na ongezeko la vitendo vya uhalifu mtandaoni.
Hayo yameelezwa leo Ijumaa na naibu mkuu wa kitendo hicho, Joshua Mwangasa wakati wa semina iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano(TCRA) na kuwakutanisha viongozi wa dini wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Amesema makosa ya kimtandao yameendelea kuongezeka kwa kasi kubwa huku makundi ya What's App yakionekana kuwa kichocheo kikubwa.
Mwangasa amesema viongozi wa makundi hayo hawatakiwi kuvumilia makosa hayo hivyo wanatakiwa watoe taarifa polisi.
"Usikubali umeanzisha kundi kwa nia nyingine halafu mtu au watu wanaweka mambo yasiyofaa, toa taarifa hatua zichukuliwe kinyume na hapo hata wewe utahusika,"
Amesema kwa kiasi kikubwa makundi hayo yamekuwa yakitumika kusambaza taarifa za uongo na uchochezi.
Mwangasa ametumia fursa hiyo kuwaomba viongozi wa dini kuwahubiria waumini wao juu ya matumizi sahihi ya mitandao ili kujiweka mbali na uhalifu.
"Ukosefu wa maadili ndio unachangia haya yote haya, ndiyo sababu narudi kwenu viongozi wa dini wasisitizeni waumini wenu watumie mitandao kwa maendeleo," amesema.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa TCRA, Mhandisi James Kilaba amesema mamlaka hiyo inaendelea kuchukua hatua kuimarisha ulinzi wa mawasiliano mtandaoni.
Amesema simu za mkononi kwa sasa zimekuwa kama silaha hivyo matumizi yake yanapaswa kuangaliwa kwa umakini zaidi.

Chanzo: Mwananchi

DHAHABU YA MAMILIONI YA PESA YAKAMATWA BANDARINI IKITOROSHWA

$
0
0
Mamlaka ya Bandari Tanzania, TPA, kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi imekamata madini ya dhahabu yenye uzito wa kilogramu 6.2 yenye thamani ya Shilingi milioni 500 katika bandari ya Dar es salaam ndani ya gari aina ya Toyota Noah iliyokuwa na watu wawili.

Noah hiyo ilikuwa imewapeleka watu hao wawili bandarini na walipotaka kushuka, walishtukiwa na askari, lakini dereva alikimbia huku akiliacha gari eneo la tukio.

Watu hao walikuwa wakipeleka mzigo huo unaokisiwa kuwa na thamani ya Sh500.3 milioni visiwani Zanzibar.

Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko alisema dhahabu hiyo iliyokamatwa katika eneo ambalo hutumiwa na wasafiri wanaokwenda Zanzibar ilikuwa katika miche mitano ambayo ilihifadhiwa kwenye begi.

Aliwataja watu hao kuwa ni Akifa Mohamed na Jaffer Hussein.

Kakoko alisema walipohojiwa, mmoja wao alidai kuwa nyaraka za dhahabu hiyo ziko Zanzibar, lakini uchunguzi wao umebaini hakuna nyaraka zozote.


Alisema mtuhumiwa mwingine alidai kuwa alikabidhiwa dhahabu hiyo ili aipeleke Zanzibar.

Kakoko alisema watuhumiwa wote wawili wako kituo cha Polisi cha Bandari ya Dar es Salaam na watafunguliwa shtaka la kupatikana na madini isivyo halali.

Akizungumzia walivyokamatwa, Kakoko alisema tukio hilo lilitokea Oktoba 10, saa 5:20 usiku eneo la Azam Sea Link/DMI, wakati askari wa TPA na wa vyombo vya ulinzi na usalama, walipokuwa katika ukaguzi wa abiria, mizigo na magari yaliyokuwa yakiingia katika meli ya MV Azam Sea Link – I.

Alisema watu hao wawili walikuwa wa mwisho kufika eneo hilo wakiwa na gari hiyo aina ya Toyota Noah.

Alisema begi lililokuwa na dhahabu hiyo lilifichwa kwenye viti vya nyuma vya gari.

Alisema mwanzoni watuhumiwa hao walikataa kukaguliwa, lakini walipobanwa walikubali na ndipo walipoufuma mzigo huo.

Alisema gari hilo linashikiliwa na dereva anaendelea kusakwa.

“Tunaendelea kuimarisha ulinzi na usalama ili kudhibiti uhalifu kwa kufanya ukaguzi wa mizigo yote kabla ya kupakiwa melini,” alisema Kakoko.

Katika siku za karibuni Serikali katika vita yake ya kiuchumi imekuwa ikikamata watu tofauti wanaokutwa na madini na rasilimali nyingine za nchi.


MVIWATA MANYARA WALIA NA MBEGU FEKI KWA WAKULIMA

$
0
0
Tatizo la  mbegu feki nchini bado ni changamoto kubwa kwa wakulima, kwani wakulima wa mkoa wa Manyara wamekuwa wakinunua mbegu ambazo wakizipanda zinakaa ardhini kwa muda mrefu bila mazao kuota hali inayolalamikiwa na wakulima wengi.

Mratibu wa Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) mkoani Manyara, Martin Pius aliyasema hayo kwenye mkutano mkuu wa 10 wa mkoa huo uliofanyika kwenye ukumbi wa White Rose mjini Babati.

Alisema pamoja na nia nzuri ya Serikali ya kutaka kukuza kipato cha mkulima kwa kuongeza bei ya chakula  anaiomba serikali upatikanaji wa bembejeo ya urahisi na gharama nafuu kwani kumekuwa na utolewaji wa pembejeo feki na kwa bei ya juu kutoka kwa wakala wanaopewa kazi hizo na serikali.

“Kutokana kubadilika kwa tabia ya nchi mbegu zilizobadilishwa vinasaba siyo njia ya kutatua changamoto hiyo, hivyo wataalamu wa kilimo wanapaswa kutafuta njia nyingine zitakazoleta tija kwa mkulima na siyo zitakazo ongeza changamoto,” alisema Pius.


Alisema mkutano wa mwaka huu umebeba kauli mbiu inayosema ‘uhakika wa mbegu kwa uhakika wa chakula' lakini kauli mbiu hiyo anaeleza bado ni changamoto kwani mbegu zinazosambazwa sio halisi.

Alisema baadhi ya wakulima wa mkoa huo  wamekuwa wakiuziwa mbegu feki za kilimo hali inayowarudisha nyuma katika shughuli za kilimo na pia kuwasababishia njaa.

Mgeni rasmi wa mkutano huo, mkuu wa mkoa wa Manyara,  Dk Joel Bendera aliwataka wakulima kutokata tamaa ya kulima zao la mbaazi kutokana na zao hilo kutokuwa na bei nzuri kwa mwaka huu .

Alisema anajua fika kuporomoka kwa bei ya zao hilo kumewaathiri wakulima wengi kwani ndilo zao kubwa la biashara ambapo mwaka jana walipambania bei ya zao hilo na kufikia kuuzwa sh 1,600 kwa kilo na mwaka huu zao hilo kufikia kuuzwa kwa sh 250 kwa kilo kutokana na wanunuzi wakubwa wa zao hilo ambao wapo India kudai kuwa wametosheka na mbaazi.

"Wakulima wanalima kulingana na soko, kwa bei hii ya mbaazi nani utamshawishi alime mbaazi mwakani, ndio maana tunasisitiza pamoja na kilimo tuwe na viwanda ili tuongeze thamani mazao yetu wenyewe," alisema Dk Bendera.

Alisema baada ya zao la pamba kushuka bei  wakulima walihamia kwenye mbaazi na mbaazi imeshuka bei wakulima watakosa la kufanya ila wasikate tamaa waendelee kulima, kwani kutatengenezwa kiwanda cha kubangulia mbaazi ili ifungashwe kwenye mifuko kisha ikauzwe nje ya nchi siyo lazima India pekee.

Aliwataka maafisa ugani wa halmashauri kuacha kukaa maofisini na badala yake kushirikiana na Mvitawa ili kuboresha teknolojia ya kilimo katika mkoa wa Manyara na kuwafundisha wakulima namna ya kulima kisasa, kuacha nafasi, kutumia mbolea na mbegu bora za kutumia.

"Hatuna maofisa ugani wa kutosha, angalau kila kata wawepo watatu, lakini hata hao waliopo kazi yao si kukaa maofisini watoke nje watu bado wanalima kienyeji  kazi zao zote wamewaachia Mviwata, kupitia halmashauri tutoe wataalamu wa kilimo kishirikiana na Mviwata," alisema Dk Bendera.

INTERNATIONAL NIGHT SAFARI DC

DKT ANGELINA MABULA AAHIDI WATAALAMU WA KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI MKOANI SINGIDA

$
0
0
  Naibu Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angelina Mabula akizungumza na wataalamu wa ardhi, viongozi na watendaji wa halmashauri ya Wilaya na Manispaa ya Singida (hawapo pichani), Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi. 
 Naibu Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angelina Mabula akizungumza na wananchi wa kijiji cha Singa tarafa ya Kinampundu Wilayani Mkalama, Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhandisi Jaksoni Massaka.
 Naibu Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angelina Mabula akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Ardhi wa Wilaya ya Iramba Lugano Sanga kuhusu utuzanji wa nyaraka za idara hiyo.
Naibu Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angelina Mabula akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi hati ya kumiliki kiwanja chake kilichopo Mjini Dodoma.

Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeahidi kutoa timu ya wataalamu watakao suluhisha mgogoro wa mpaka kati ya Wilaya ya Mkalama Mkoani Singida na Wilaya ya Hanang’ Mkoani Manyara.

Naibu Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angelina Mabula ametoa ahadi hiyo wakati wa ziara yake Mkoani Singida katika kijiji cha Singa tarafa ya Kinampundu Wilayani Mkalama ambapo amesema Wizara yake itatoa wataalamu watakaoweza kutatua mgogoro huo uliodumu kwa zaidi ya miaka 30.

“Kwakuwa pande zote mbili za Mkalama na Hanang’ zimekutana mara kadhaa bila mafanikio, nitaleta wataalamu wafike eneo la mpaka ili wataalam hao wawasomee alama moja baada ya nyingine, kila mmoja wenu afahamu eneo lake mwisho ni wapi, nadhani hapo tutakuwa tumewasaidia wananchi wetu”, amesema Dkt Mabula.

Amesema wananchi wa Kijiji hicho cha Singa wasiwe na wasiwasi endapo baada ya kuonyesha mpaka wao mashamba yao yakionekana yapo wilaya ya Hanang’ wataruhusiwa kuendelea kuyamiliki ila watatakiwa kwenda kujitambulisha katika Uongozi wa Wilaya hiyo.

Aidha Dkt Mabula amesema timu hiyo ya wataalamu itahakikisha inasuluhisha migogoro yote ya mipaka ya wilaya hiyo ambayo ngazi ya wilaya imeshindikana kutatuliwa.

Amewashauri wananchi hao kutouza au kugawa ardhi yao ovyo ovyo kwakuwa ardhi ni mali na mtaji popote pale hata kama ni vijijini hivyo watunze ardhi yao na kuiongezea thamani kwa kuipima na kuwa na hati ya umiliki.

Baadhi ya wananchi wa kijiji hicho walitoa malalamiko kwa Naibu Waziri huyo huku wakimueleza kuwa mgogoro huo uliodumu kwa muda mrefu umesababisha baadhi yao kupelekwa mahakamani kwa madai ya kuvamia mashamba.

Mzee Anaftali Amosi Majii amemueleza Naibu waziri kuwa taarifa za mgogoro huo zilitolewa muda mrefu na kuongeza kuwa wananchi wamechoka kushitakiwa kwa makosa ya uvamizi wa mashamba wakati wao wanaamini wanayamiliki kwa uhalali jambo ambalo linawachelewesha kimaendeleo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkalama Mhandisi Geofrey Sanga amesema Wilaya ya Mkalama ina migogoro ya mipaka kwa wilaya tano zinazowazunguka.

Mhandisi Sanga ameeleza kuwa Mkalama ina migogoro ya mipaka kati yake na Wilaya za Mbulu, Iramba, Hanang’ na Wilaya ya Singida jambo ambalo linawafanya baadhi ya wananchi kukwepa kuchangia shughuli za maendeleo wakidai wao sio wa Wilaya hiyo.

Wakati huo huo Naibu Waziri Dkt Angelina Mabula amefanya ziara Wilaya ya Iramba na kufanya ukaguzi wa kushtukiza katika masijala ya Ardhi ya Wilaya hiyo ambapo hakuridhishwa na utunzaji wa nyaraka pamoja na utendaji usioridhisha unaosababisha wananchi kuchelewa kupata hati za viwanja.

Dkt Mabula pia hakuridhishwa na kasi ndogo ya upimaji viwanja na utoaji wa hati wilayani humo huku akiwataka kuacha kukusanya kodi mbalimbali za ardhi kwa utendaji wa kimazoea bali wafanye kazi bidii.

FATAH NA HAMAS ZASAINI RASMI MAKUBALIANO YA UPATANISHO NA USHIRIKIANO

$
0
0
 Vyama vya Fatah na Hamas vya Palestina jana Alhamisi vimesaini rasmi makubaliano ya upatanisho na ushirikiano,yaliyofikiwa mjini Cairo nchini Misri kupitia mkutano wao na waandishi wa habari.
Katika hali hii, Mkuu wa ujumbe wa Chama cha Fatah katika makubaliano hayo “Azzam al-Ahmad” amesema kuwa, yamefikiwa makubaliano kamili ya kuwezesha dhana ya kurudi kwa serikali ya Palestina na uhalali wake, katika kufanya kazi za kawaida na kusimamia Ukanda wa Gaza.
 Aidha “Al Ahmad” katika mkutano huo uliohudhuriwa pia na mkuu wa ujumbe wa Chama cha Hamas “Saleh Al-Arouri” ameongeza kusema kuwa, yamefikiwa makubaliano ya kuiwezesha serikali hilo, kwa mujibu wa sheria na kanuni zinazotumika katika taasisi,wizara na jumuiya zote mjini Gaza bila kubagua, huku serikali ikisimamia kikamilifu vivuko vyote.
Ameweka wazi kwamba, wamekubaliana na idara ya vivuko ikiwa ni pamoja na upande wa Israel au ihusuyo kivuko cha Rafah,ambacho suala lake ni maalumu kwani kinahitaji taratibu fulani zinazohusisha uboreshaji wa majengo yake upande wa Misri,kwa kiwango ambacho kitaendana na hadhi ya Misri na pia taifa la Palestina ili kifanya kazi vizuri, huku mipango ya usalama ikisimamiwa na Mamlaka halali ya Palestina.
Vilevile ametangaza kuwa ulinzi wa Rais uttakuwepo pia upande wa mpaka wa Misri,huenda hatua hiyo isiwe kwa uharaka sana isipokuwa kwa vivuko vingine itakuwa ya haraka katika muda usiozidi Novemba Mosi ijayo, huku kila kitu kikipangiwa tarehe maalumu kwa ratiba.
Kwa upande wake, Rais wa Mamlaka ya Palestina “Mahmoud Abbas”, amepongeza mafanikio hayo yaliyopatikana katika mazungumzo kati ya Fatah na Hamas, yaliyofanyika mjini Cairo nchini Misri ambayo ndio iliyofadhili. Amesema hatua hiyo itaimarisha na kuharakisha hatua za kukomesha mgawanyiko na hatimae kurudisha umoja wa Wapalestina, ardhi na taasisi zake.
Aidha,Rais pia ameielekeza serikali yake,mashirika na taasisi zote, kufanyia kazi kwa bidii yale yote yaliyokubaliwa,huku akitoa wito kwa makundi na wadau mbalimbali kufanya juhudi katika kufikia kile kinacholengwa na Wapalestina ambacho ni kurejesha umoja wao. Rais amemshukuru Rais wa Misri “Abdel-Fattah Al-Sisiy”, kwa jukumu kubwa lililobebwa na nchi yake katika kufikia mafanikio haya muhimu.
Kwa upande mwingine, Rais Abbas amepokea pongezi kwa njia ya simu kutoka kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa “Antonio Guterres”, kwa hatua hiyo nzuri inayolenga kumaliza mgawanyiko na hatimae kurudisha umoja wa kitaifa wa Palestina, iliyofikiwa mjini Cairo. Huku akisisitiza utayari wa Umoja wa Mataifa katika kufanya kazi na Rais Abbas na Mamlaka yote ya Taifa ya Palestina, kuunga mkono jitihada za kuunganisha safu ya Wapalestina na kupunguza mateso ya watu wa Ukanda wa Gaza.
Kwa upande wake, Jumuiya ya Kiarabu imepongeza hatua hiyo iliyofikiwa na Palestina kati ya Hamas na Fatah chini ya ufadhili wa Misri, hatua ambayo itarudisha suala la Palestina katika mazingira ya kimataifa,huku Jumuiya hiyo ya Kiarabu pia ikiipongeza serikali ya Palestina inayoongozwa na Rais “Mahmuud Abbas” na wote waliohusika katika kufikia hatua hiyo nzuri, inayoimarisha msimamo wa Palestina dhidi ya changamoto zinazokabili suala la nchi hiyo.
Taarifa hiyo imesema kuwa, makubaliano hayo yanahesabiwa kuwa ni dhamana ya msingi ya kufikia malengo ya taifa la Palestina, ikiwemo kupata uhuru wake kamili, kumaliza uvamizi wa Israel katika ardhi ya Palestina na hatimae kusimamisha dola huru yenye mji mkuu wake Jerusalem ya Mashariki, kwa mujibu wa mipaka ya Juni 4 mwaka 1967.

MISA YA NDUGU YETU JOSEPH NDYAMUKAMA, KUFANYKA BALTIMORE

$
0
0


Ndugu zangu wana DMV, tunapenda kuwataarifu kuwa misa ya kumwombea marehemu Joseph Ndyamukama

itayofanyika Jumapili Oct, 15, 2017 saa nane mchana (2pm) katika kanisa la Mt.Edward address ni 901 Poplar Grove St, 
Baltimore, MD 21216


.tunaomba tujumuike pamoja kumuaga mwenzetu
Viewing all 45988 articles
Browse latest View live
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>