Quantcast
Channel: VIJIMAMBO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 45981

YANGA NA MBEYA CITY NI AJABU KWELI

$
0
0
Yanga ikiteleza Mbeya City anayeshiriki Ligi Kuu Bara kwa mara ya kwanza anaweza kupata tiketi ya kushiriki Kombe la Shirikisho.
NI ajabu lakini kwenye mambo ya mpira inaweza kutokea kweli ndani ya sekunde moja. Na ndicho kinachohofiwa na mashabiki kwamba kinaweza kutokea baina ya Yanga na Mbeya City kwenye mbio za mshindi wa pili.
Yanga ikiteleza Mbeya City anayeshiriki Ligi Kuu Bara kwa mara ya kwanza anaweza kupata tiketi ya kushiriki Kombe la Shirikisho. Iko hivi, Azam FC ndiyo wanaoongoza ligi sasa wakiwa na pointi 53 baada ya kucheza mechi 23, wakifuatiwa na Yanga ambao ni mabingwa watetezi wakiwa na pointi 46 katika mechi 22 mmoja pungufu dhidi ya waliopo juu yao lakini Mbeya City wapo katika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 45 wamecheza michezo 23.
Utamu au ugumu wa msimamo huo unakuja kufuatia timu zote tatu za juu zinaweza kushika nafasi mbili za juu endapo watashinda mechi walizobakiza au kupoteza jambo ambalo litatoa nafasi kwa timu nyingine kujihakikishia nafasi nzuri katika msimamo huo.
Azam imebakiza mechi tatu kumaliza ligi ambapo kwanza itacheza dhidi ya Ruvu Shooting ugenini Aprili 9 katika Uwanja wa Mabatini, baada ya hapo watasafiri kuwafuata Mbeya City Aprili 13 ambao mchezo wa mzunguko wa kwanza waligawana nao pointi baada ya kutoka sare ya mabao 3-3 na mchezo wa mwisho watamaliza na JKT Ruvu Aprili 19 mwaka huu.
Timu hiyo inahitaji kushinda mechi zote ilizozibakisha ili kujihakikishia ubingwa endapo watapoteza mmoja na kupata sare moja huku Yanga wakishinda mechi zao walizobakiza ni wazi wataambulia patupu. Ingawa ni ajabu na kweli.
Kocha wa Azam, Joseph Omog alisema; “Ukiangalia mechi tatu tulizobakisha ni ngumu sana, ni dhidi ya Mbeya City na Ruvu Shooting, hakuna aliyetarajia Yanga wangepoteza mechi dhidi ya Mgambo, hilo ni jibu tosha kwamba ligi ni ngumu.”
Tishio kubwa kwa Azam ambao hawajapoteza mechi yoyote tangu ligi ianze msimu huu ni mechi mbili ambazo watawafuata Ruvu Shooting na ule dhidi ya Mbeya City.
John Bocco ambaye ni nahodha wa Azam alisema; “Tunaona ugumu uliopo sasa, lakini tumejipangia mambo mawili, kwanza kuhakikisha tunajituma na kushinda mechi zote lakini pili tunasema kwamba kwa sasa kwetu hakuna mechi ya ugenini wala nyumbani.”
Yanga wamebakiza mechi nne dhidi ya JKT Ruvu Aprili 6, Kagera Sugar Aprili 9, watakwenda Arusha kwa JKT Oljoro na kumaliza na Simba Aprili 19.
Hans Pluijm ambaye ni Mholanzi Kocha wa Yanga alisema; “Mpira ni mchezo wa makosa, hatujatoka katika mbio za ubingwa tutalazimika kushinda mechi zilizosalia lakini wasiwasi wangu ni wachezaji wangu ambao wanashindwa kufikia malengo tuliyoyapanga kutokana na kufanya makosa yanayoepukika, tunaweza kuchukua ubingwa lakini shida ni wachezaji ambao tunapokubaliana na kuelekezana mambo ya kufanya wao wanafanya tofauti.”
Yanga vs Mbeya City
Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ambaye ni nahodha wa Yanga alisema; “Hatujakata tamaa ya ubingwa, tuna nguvu ya kushinda mechi zote zilizosalia lakini maombi yetu yatakuwa ni katika mechi mbili za Azam kuwa wapoteze au wapate suluhu dhidi ya Ruvu Shooting au Mbeya City.”Mbeya City wana uwezo mkubwa wa kuwashusha Yanga katika nafasi ya pili endapo watashinda mechi zao tatu walizobakiza dhidi ya Ashanti United Aprili 5 jijini Dar es Salaam na kurudi kwao kuwasubiri Azam FC ambapo watamaliza na wababe wa Yanga na Simba Mgambo JKT nyumbani Aprili 19,mwaka huu nafasi hiyo kwa vijana hao wa Kocha Juma Mwambusi inakuja tu endapo Yanga itapoteza mechi moja na kutoka sare ambapo nao wataweka historia kubwa msimu huu.
Kuhusu hali hiyo ya ushindani, Mwambusi alisisitiza kwamba wanaelewa kinachoendelea watatuliza mpira uwanjani mpaka dakika ya mwisho na uwezo wanao.
Tishio kubwa kwa Mbeya City katika mechi walizobakiza ni kwamba wanacheza na Ashanti na Mgambo ambazo zote zinapigana kutoshuka daraja jambo ambalo litaamsha upinzani mkubwa mara watakapokutana, pia wataumana na Azam ambao wanahitaji ushindi ili kujihakikishia ubingwa.
Mbeya City kupitia Mwenyekiti wao, Mussa Mapunda alisema; “Ili tufikie malengo yetu kwenye msimu huu wa ligi, basi lazima tuwafunge Azam mara tutakapovaana nao na hilo linawezekana, kutokana na morali ya wachezaji wetu, hao ndiyo wapinzani wetu wakubwa, tuliwakosa kwao na sasa tunataka kuwafunga hapa kwetu, hilo halina shida.”

Viewing all articles
Browse latest Browse all 45981

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>