Akikabidhi seti moja ya jezi, katikati ni mdhamini wa kombe hilo Jackson Kiwaga |
Hapa alikabidhi zawadi ya seti moja ya jezi kwa mshindi wa pili Nyabula FC, mwenye kofia nyeupe ni mdhamini wa ligo hiyo Jackson Kiswaga |
zawadi ya pili kwa mshindi wa pili ulikuwa mpira |
waamuzi wakifurahi baada ya kumaliza mpambano huo salama |
moja ya tukio katika mchezo huo, hapa golikipa wa Nyabula akiutazama mpira uliozama katika lango lake huku akionesha kukata tamaa |
Kikosi cha Ugwachanya kikifurahi |
Golikipa wa Nyabula kala pozi lililoashiria mchezo huo umekwisha |
sehemu ya mshabiki waliojitokeza |
PAZIA la ligi daraja la tatu wilaya ya Iringa Vijijini lililoshirikisha timu 12 limefungwa wakati wa maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika juzi kwa timu ya Ugwachanya FC kuibamiza bila huruma mabao 3-0 klabu ya Nyabula FC.
Mchezo huo uliohudhuriwa na mamia ya wakazi wa kata ya Tanangozi na vitongoji vyake uliokuwa na shamrashamra za aina yake kutoka kwa mashabiki wa timu zote mbili.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Simu za Mkoani ya TIGO Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Jackson Kiswaga ambaye pia ni mdhamini wa ligi hiyo ameahidi kuongeza dau la udhamini msimu ujao wa ligi hiyo ili kuiongezea hadhi.
Kwa ushindi huo, Ugwachanya FC ilipata kikombe na seti moja ya jezi huku Nyabula FC ikijipatia seti moja ya jezi na mpira.
Dalili za Ugwachanya FC kuwa bingwa wa ligi hiyo ilidhihiri katika dakika zote 90 za fainali hiyo baada ya wachezaji wake kuutawala vyema mchezo huo.
Goli la kwanza la timu hiyo liliwekwa kimiani katika dakika ya 14 baada ya mshambualiji wake Oscar Mhelela aliyepokea pasi ndefu kutoka Baraka Cheyo kuwahadaa walinzi wa Nyabula FC na kupiga shuti kali lililomshinda golikipa wa timu hiyo FC Fred Chilala.
Katika dakika 30 ya mchezo Ugwachanya FC iliongeza bao la pili kupitia kiungo wake mshambuliaji Nasibu Ndauka aliyehitimisha karamu ya mabao ya timu hiyo katika dakika ya 34 kwa kufunga bao la tatu.
Hasira za timu ya Nyabula kuchabangwa ilitaka kuiharibu fainali hiyo baada ya kujitokeza baadhi ya mashabiki wa timu hiyo kuvamia meza kuu na kumtuhumu Katibu wa Chama cha Soka cha Wilaya hiyo, Juma Lalika kuhusika kuihujumu timu yao kwa kuruhusu wachezaji ambao hakuwasajiliwa na Ugwachanya kuichezea timu hiyo.
Hasira zilizidi zaidi katika daakika 55 ya mchezo huo baada ya mshambualiji wake Fadhil Nganga kukosa penati waliyotunikiwa ikiwa ni matokeo ya mchezaji wake Octavian Balama kuchezewa rafu katika eneo la hatari.
Mratibu wa kombe la Muungano, Daudi Yasin alikuwa mgeni rasmi wa fainali hiyo na baada ya kukabidhi zawadi kwa washindi alisema mashindano hayo yatasaidia kukuza sekta ya mpira wa miguu mkoani Iringa.
Ugwachanya FC; Good Kibiki, Paulo Malekela, Method Mkonnda, Oscar Mhelela, Salum Mapunda, Steven Mhelela, Veda Kiwele, Baraka Cheyo, Nasibu Ndauka, Kingunge Ndenga na Austin Mlwale.
Nyabula FC; Fredy Chilala, Pascal Luluzile, Yohel Mashaka, Benson Mlawa, Fadhil Ngaga, Joseph Mlawa, Said Kigomba, Amazon Lundimba, Exaud Kaduma, Octavian Balama na Gerald Nganga.