Hii ni kwa wale tuliokulia mazingira ya ujamaa na kujitegemea tulianza kujitegemea toka umri huu. Je unakumbuka nini ukiona picha hii na hapo ulipo sasa?. Jitiririshe na mawazo yangu hapa chini labda utayapenda au na kuchangia na wewe mawazo yako. Comment nairusha hewani mimi mwenyewe kama utaandika jina lako.
Wanadiaspora tunaweza kubadirisha kule tuliko toka kwakufanya kitu chochote ambacho tunaweza kujivunia na kuwa kwetu Diaspora. Kwa kidogo tulichonacho twaweza kuleta furaha kwa kizazi cha eneo husika. Tusiwalaumu viongozi, Wakulaumiwa ni wananchi wa eneo husika kwa kuwapa dhamana viongozi walafi wanajali matumbo yao na familia zao tu. Serikali kwa kutokuwa na mtaala maalumu pia sera mbovu walizoziweka.