Ndege ya shirika la ndege la American iliyokua ikisafiri kutoka DallasTexas (DFW)kuelekea Baltimore (BWI) siku ya Jumatatu Sept 29, 2014 mida ya jioni na iliyokua imebeba abiria 140 akiwemo Mtanzania Baraka Daudi ilibidi itue kwa dharura kwenye uwanja huo wa Dalls baada ya rubani wa ndege hiyo kugundua gurudumu la mbele (norse gear) kutokua na upepo. Baada ya rubani kugundua hitilafu hiyo aliwasiliana na mnara wa kuongozea ndege wa uwanja huo wa Dallas (DFW) wajaribu kuingalia ndege hiyo kwa ukaribu zaidi kwamba ile taarifa aliyoipata kwenye computa yake ya ndege ilikua sahihi kwamba gurudumu la mbele halikua na upepo na kwamba kama anaweza kuendelea na safari kuelekea Baltimore. Maryland.
Waongozaji ndege waliona gurudumu lile na kumshauri rubani asiendelee na safari yake kwani asingeweza kutua ndege na kutumia breki kwani kungeweza kutokea ajali ya ndege hiyo pia ndege ilikua imejaza mafuta, walishauri azunguke angani kupunguza mafuta na baadae atue huku wakijaribu kuondoa ndege zote njiani kwa kwa tahadhali ya ndege kuwaka moto.
Vijimambo ilivyoongea na Baraka Daudi alisema kusema kwenye ndege kulikua na taharuki kubwa kutoka kwa abiria baada ya kupata taarifa hiyo toka kwa rubani lakini aliendelea kwa kusema anawasifu rubanii na wahudumu wa ndege hiyo kwa jinsi walivyoweza kuwatuliza abiria na kuwaonyesha kwamba tatizo hilo halikua kubwa na ndege ilipokua inatua ilibidi pia ifungue kama parachuti la kuwezesha kusaidia kupunguza kasi ya ndege na hatimae walitua salama na kutafutiwa ndege nyingine ya kuwasafirisha Baltimore na baadhi ya abiria walikataa kuendelea na safari lakini Baraka Daudi yeye aliendelea na safari na amefika salama salimini.