Quantcast
Channel: VIJIMAMBO
Viewing all 45934 articles
Browse latest View live

MFUKO wa LSF watoa msaada wa Laptop kwa wasaidizi wa kisheria kwa jamii

$
0
0
Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Einar H. Jensen (kulia) akimkabidhi mmoja wa wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria laptop kwa niaba ya taasisi yake. Msaada huo ulitolewa na Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) unaofadhiliwa na Shirika la DANIDA la nchini Denmark na Shirika la DFID kutoka Uingereza. Kushoto ni Mkurugenzi wa LSF, Kees Groenendijk akishuhudia. Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Einar H. Jensen (kulia) akimkabidhi mmoja wa wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria laptop kwa niaba ya taasisi yake. Msaada huo ulitolewa na Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) unaofadhiliwa na Shirika la DANIDA la nchini Denmark na Shirika la DFID kutoka Uingereza. Kushoto ni Mkurugenzi wa LSF, Kees Groenendijk akishuhudia.Mshauri Kiongozi wa DFID Tanzania, Helen Barnes (kulia) akimkabidhi mmoja wa wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria laptop kwa niaba ya taasisi yake. Msaada huo ulitolewa na Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) unaofadhiliwa na Shirika la DANIDA la nchini Denmark na Shirika la DFID kutoka Uingereza. Mshauri Kiongozi wa DFID Tanzania, Helen Barnes (kulia) akimkabidhi mmoja wa wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria laptop kwa niaba ya taasisi yake. Msaada huo ulitolewa na Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) unaofadhiliwa na Shirika la DANIDA la nchini Denmark na Shirika la DFID kutoka Uingereza.
Mjumbe wa Bodi ya LSF, Dk. Benson Bana (kulia) akimkabidhi mmoja wa wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria laptop kwa niaba ya taasisi yake. Msaada huo ulitolewa na Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) unaofadhiliwa na Shirika la DANIDA la nchini Denmark na Shirika la DFID kutoka Uingereza. Katikati akishuhudia ni, Mkurugenzi wa LSF, Kees Groenendijk. Mjumbe wa Bodi ya LSF, Dk. Benson Bana (kulia) akimkabidhi mmoja wa wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria laptop kwa niaba ya taasisi yake. Msaada huo ulitolewa na Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) unaofadhiliwa na Shirika la DANIDA la nchini Denmark na Shirika la DFID kutoka Uingereza. Katikati akishuhudia ni, Mkurugenzi wa LSF, Kees Groenendijk.Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Einar H. Jensen akizungumza katika hafla ya Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) kuwakabidhi wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria laptop kwa niaba ya taasisi zao zinazotoa msaada wa kisheria kwa jamii. Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Einar H. Jensen akizungumza katika hafla ya Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) kuwakabidhi wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria laptop kwa niaba ya taasisi zao zinazotoa msaada wa kisheria kwa jamii.Mshauri Kiongozi wa DFID Tanzania, Helen Barnes akizungumza katika hafla ya Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) kuwakabidhi wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria laptop kwa niaba ya taasisi zao zinazotoa msaada wa kisheria kwa jamii. Mshauri Kiongozi wa DFID Tanzania, Helen Barnes akizungumza katika hafla ya Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) kuwakabidhi wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria laptop kwa niaba ya taasisi zao zinazotoa msaada wa kisheria kwa jamii.Mjumbe wa Bodi ya LSF, Dk. Benson Bana akizungumza katika hafla ya Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) kuwakabidhi wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria laptop kwa niaba ya taasisi zao zinazotoa msaada wa kisheria kwa jamii. Mjumbe wa Bodi ya LSF, Dk. Benson Bana akizungumza katika hafla ya Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) kuwakabidhi wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria laptop kwa niaba ya taasisi zao zinazotoa msaada wa kisheria kwa jamii.Baadhi ya laptop zilizotolewa kwa wasaidizi hao wa kisheria kwa jamii. Baadhi ya laptop zilizotolewa kwa wasaidizi hao wa kisheria kwa jamii.Viongozi hao wakiwa katika hafla hiyo leo jijini Dar es Salaam. Viongozi hao wakiwa katika hafla hiyo leo jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi wa LSF, Kees Groenendijk (kulia) akimkabidhi mmoja wa wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria laptop kwa niaba ya taasisi yake. Msaada huo ulitolewa na Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) unaofadhiliwa na Shirika la DANIDA la nchini Denmark na Shirika la DFID kutoka Uingereza. Mkurugenzi wa LSF, Kees Groenendijk (kulia) akimkabidhi mmoja wa wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria laptop kwa niaba ya taasisi yake. Msaada huo ulitolewa na Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) unaofadhiliwa na Shirika la DANIDA la nchini Denmark na Shirika la DFID kutoka Uingereza.[/caption] MFUKO wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) umekabidhi laptop 170 kwa asasi mbalimbali zinazotoa msaada wa kisheria kwa wananchi wahitaji katika mikoa anuai nchini Tanzania. Akizungumza kabla ya kukabidhi vitendea kazi hivyo kwa wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa wa kisheria, Mjumbe wa Bodi ya LSF, Dk. Benson Bana aliwataka sema shirika hilo linaamini zitatumika katika kutatua changamoto anuai kwa asasi husika ikiwa ni chachu ya kuongeza ufanisi kwa kazi zao. Laptop hizo 170 zimekabidhiwa leo jijini Dar es Salaam na Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Einar H. Jensen huku akizitaka asasi hizo muhimu kuendelea kuisaidia jamii inayoitaji msaada wa kisheria popote walipo kwani zipo familia hasa wajane wanaitaji na wanashindwa namna ya kupata. LSF ni mfuko huru wa msaada wa kisheria unaotoa msaada kwa mashirika watoa msaada wa kisheria, kitaasisi na kiufundi ili kuongeza uwazi na uwajibikaji katika sekta ya sheria chini ya ufadhili wa Shirika la DANIDA la nchini Denmark na Shirika la DFID la Uingereza. Afisa Ufuatiliaji na Matokeo wa Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF), Saada Mkangwa (kushoto mbele) akiwasilisha mada ya kuwajengea uwezo wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria leo jijini Dar es Salaam. Afisa Ufuatiliaji na Matokeo wa Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF), Saada Mkangwa (kushoto mbele) akiwasilisha mada ya kuwajengea uwezo wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria leo jijini Dar es Salaam.Meneja Ufuatiliaji na Matokeo wa Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF), Said Chitong (kulia) akiwasilisha mada ya kuwajengea uwezo wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria leo jijini Dar es Salaam. Meneja Ufuatiliaji na Matokeo wa Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF), Said Chitong (kulia) akiwasilisha mada ya kuwajengea uwezo wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria leo jijini Dar es Salaam.Sehemu ya wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria wakiwa katika semina ya kuwajengea uwezo. Sehemu ya wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria wakiwa katika semina ya kuwajengea uwezo

ALL GOALS: Yanga vs Stand United February 3 2017, Full Time 4-0

WAKUU WA SHULE NA WAKURUGENZI DAR WATAKIWA KUTOA SABABU ZA SHULE ZAO KUFELI

$
0
0
Kufuatia Dar es Salaam kufanya vibaya katika mtihani wa kidato cha nne kwa mwaka 2016 kwa kuingiza shule 6 kati ya kumi zilizofanya vibaya, ofisi ya Elimu Mkoa imewaagiza wakuu wa shule na wakurugenzi kutoa taarifa za kina juu ya sababu zilizopelekea kufanya vibaya.

Akiongea na TBC, kaimu Afisa elimu mkoa, Janeth Nsunza, alisema bado wanaendelea na kikao kujadili tathmini ya matokeo hayo na wamesema watatoa taarifa kamili watakapomaliza majadiliano.
Alisema, “Kati ya shule 10 ambazo hazikufanya vizuri shule hizo ni Kitonga, Nyeburu, Mbopo, Mbondole, Somangila day na Kidete kufuatia shule hizo sita kutofanya vizuri mkoa wa Dar es Salaam, mkoa umepokea taarifa hizo kwa masikitiko makubwa kwani imekuwa ni kinyume cha matarajio yetu na serikali yetu kwa ujumla.”
“Kwakuwa matokeo yametanganzwA, hatua za kufahamu nini hali hiyo imejitokeza zimechukuliwa mara baada ya matokeo hayo kutangazwa ambapo wahusika wanaendelea kutoa maelezo yao, licha kwa kuwepo kwa viashiria katika mtihani wa Mock na wakurugenzi waliwaelekeza wakuu wa shule hizo kuondoa hali hizo mapema,” aliongeza Nsunza.

SERENGETI BOYS YAFUZU AFCON U-17

$
0
0
Tanzania imefuzu kwa mara ya kwanza kucheza fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana U-17 zitakazofanyika Gabon mwaka huu.
Serengeti Boys ilifuzu baada ya kushinda rufaa yake dhidi ya Congo iliyomchezesha mchezaji aliyezidi umri.
Tanzania itaingia Kundi B ikichukua nafasi ya Congo kundi hilo lina timu za Niger, mabingwa watetezi Mali na Angola.
Timu nne zinazofanikiwa kuingia katika nusu fainali zitafuzu moja kwa moja Kombe la Dunia la Fifa U17 litalofanyika India baadaye mwaka huu.
Waziri wa Michezo, Nape Nnauye aliandika kwenye akaunti yake ya twiter kuipongeza Serengeti Boys kwa kufikia hatua hiyo.
“Mungu Mkubwa! Tumefuzu kwenye fainali za Afrika chini ya umri wa miaka 17. Nia, uwezo na sababu za kuchukua kombe hili tunazo. Hongera TZ” aliandika Nape.

HOSPITALI YA KAIRUKI YATOA HUDUMA ZA AFYA YA MACHO BURE

$
0
0
 Daktari Bingwa wa magonjwa ya macho Dk. Mustafa Yusufali akimpima macho, Alphonce Joseph mmoja wa wagonjwa waliofika katika Hospitali ya Kairuki Mikocheni jijini Dar es Salaam, ikiwa sehemu ya maadhimisho ya 18 ya Kumbukizi  ya  Hayati Prof. Hubert Kairuki, ambapo upimaji wa awali wa afya ya macho umefanyika kuanzia Februari 3-4 kwa gharama za hospitali hiyo pamoja na utoaji wa miwani ya kusomea na upasuaji mdogo bure.

 Daktari Bingwa wa magonjwa ya macho Dk. Mustafa Yusufali akimpima macho, Alphonce Joseph mmoja wa wagonjwa waliofika katika Hospitali ya Kairuki Mikocheni jijini Dar es Salaam, ikiwa sehemu ya maadhimisho ya 18 ya Kumbukizi  ya  Hayati Prof. Hubert Kairuki. 
Muuguzi wa Hospitali ya Kairuki Mikochezni jijini Dar es Salaam, Athuma Makolela akichukua maelezo ya mmoja wa wagonjwa wa macho waliofika hospitalini hapo kupata huduma zilizokuwa zikitolewa kwa gharama za hospitali hiyo. 
 Dk. Kenneth Munanu akimpima macho mgonjwa aliyefika katika hospitali ya Kairuki Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Wananchi wakipata hudumza za matibabu ya Afya ya Macho katika hospitali ya Kiruki Mikocheni. Huduma hizo zimegharamiwa na hosptali hiyo.   
 Wagonjwa wakisubiri kupata huduma.
 Mgonjwa akipima macho.
 Regina Shadrack akipimwa macho.
 Huduma zikiendelea.
wananchi wakisubiri kupata huduma.

WAFANYA BIASHARA WAFANYA KONGAMANO KUJADILI FURSA ZA UWEKEZAJI MKOANI SHINYANGA

$
0
0
Kushoto ni mgeni rasmi katika kongamano la wafanyabiashara ,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Kilimo mkoa wa Shinyanga,(TCCIA) Mchungaji Dr. Kulwa Ezekiel Meshack wakiwa katika ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga leo Ijumaa Februari 3 2017

Hapa ni katika ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga ambako leo Ijumaa Februari 03,2017 kumefanyika Kongamano la wafanyabiashara kutoka wilaya ya Shinyanga lililoandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Kilimo(TCCIA) kwa kushirikiana na mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro.

Kongamano hilo lililokutanisha wafanyabishara kutoka Shinyanga Mjini na Vijijini na nje ya mkoa wa Shinyanga  lililenga la kuibua na kujadili fursa za uwekezaji zilizopo mkoani Shinyanga na kujadili changamoto zinazowakabili wafanyabiashara wenye viwanda na kilimo.
Mgeni rasmi katika Kongamano hilo ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro.Wafanyabiashara wakiwa ukumbini
Wafanyabiashara wakiwa ukumbini
Wafanyabiashara wakiwa ukumbini
Tunafuatilia kinachoendelea
Sekretariati wakiwa ukumbini
Afisa Tawala wilaya ya Shinyanga Charles Maugira aliyemwakilisha katibu tawala wa wilaya hiyo akitambulisha viongozi wa serikali waliohudhuria kongamano hilo
Wafanyabiashara wakiwa ukumbini
Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Geofrey Ramadhan Mwangulumbi akiwasalimia wafanyabiashara
Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Geofrey Ramadhan Mwangulumbi akiwasalimia wafanyabiashara,kulia ni naibu meya wa manispaa ya Shinyanga Agnes Machiya
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo mkoa wa Shinyanga Mchungaji Dr. Kulwa Ezekiel Meshack akizungumza wa kufungua kongamano hilo ambapo alisema wameamua kukutana ili kujadili fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo mkoani Shinyanga.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo mkoa wa Shinyanga Mchungaji Dr. Kulwa Ezekiel Meshack alitumia fursa hiyo kumpongeza rais John Pombe Magufuli kwa kuhimiza uchumi wa viwanda na kuahidi kuwa wafanyabiashara mkoa wa Shinyanga wapo tayari kumuunga mkono
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo mkoa wa Shinyanga Mchungaji Dr. Kulwa Ezekiel Meshack pia aliiomba serikali kupunguza rundo la kodi kwawafanyabiashara kwani kodi hioz zinawakatisha tamaa kuendelea kufanya biashara
Meneja wa Benki ya Maendeleo -TIB Kanda ya ziwa Zacharia Kicharo akitoa mada wakati wa kongamano hilo
Meneja Miradi kutoka Tanzania Local Enterprise Development (TLED) Stanley Magese akitoa mada wakati wa kongamano hilo
Wafanyabiashara wakiwa ukumbini
Kongamano linaendelea
Mwalimu wa walipa kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Shinyanga Anthony Faustine akitoa mada kuhusu ulipaji kodi
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwahutubia wafanyabiashara wilaya ya Shinyanga waliohudhuria kongamano hilo ambapo aliwaasa kujitokeza kuwekeza katika sekta mbalimbali ikiwemo viwanda kwani serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na rais John Pombe Magufuli inataka watanzania kuwekeza katika viwanda
Mkuu huyo wa wilaya Josephine Matiro alisema serikali ya wilaya ya Shinyanga ipo tayari kushirikiana na wafanyabishara katika kukuza uchumi wa mkoa wa Shinyanga
Matiro aliwapongeza wafanyabiashara waliojitokeza kwa wingi katika kongamano hilo na kuwaomba kuendelea kuwekeza
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga akizungumza
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisisitiza jambo
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza ukumbini
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro(kushoto) akiteta jambo na mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Shinyanga Mchungaji Dr. Kulwa Ezekiel Meshack na katibu wa Katibu wa TCCIA mkoa wa Shinyanga Marcelina Saulo
Mc Mama Sabuni anayeongoza Kongamano hilo akiwa ukumbini
Wafanyabiashara wakiwa ukumbini
Wafanyabiashara wakifuatilia kinachoendelea ukumbini
Wafanyabisahara wakiwa ukumbini.Kulia ni mkurugenzi wa Vigimark Hotel bi Victoria Majige
Tunafuatilia kinachoendelea
Kulia ni Katibu wa TCCIA mkoa wa Shinyanga Marcelina Saulo,kushoto ni Afisa tawala wilaya ya Shinyanga Charles Maugira wakifuatilia kinachoendelea ukumbini
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga Said Pamui akitoa mada wakati wa kongamano hilo ambapo aliwasisitiza wafanyabiashara kujenga mazingira ya kukopesheka,kuwa waaminifu na kulipa madeni yao kwa wakati kama wanavyokubaliana na benki 
Pamui alitumia fursa hiyo kuwapongeza wafanyabiashara wilaya ya Shinyanga kujitokeza kwa wingi katika kongamano hilo na kuwataka kujenga utamaduni wa kujitokeza katika vikao na mikutano mbalimbali ili kubadilishana uzoefu na kupeana mbinu mpya za kufanya biashara.
Wafanyabiashara wakifuatilia yanaliyokuwa yanajiri ukumbini
Mkurugenzi wa Vigimark Hotel iliyopo mjini Shinyanga Victoria Majige akizungumzia changamoto ya ubovu wa barabara inayoelekea katika hoteli hiyo ambapo aliiomba serikali kutengeneza barabara hiyo walau kwa kiwango cha moramu 
Mfanyabshara wa Uyoga wilayani Shinyanga Hamisa Nuhu akichangia hoja wakati wa kongamano hilo
Meneja wa shule ya Msingi Little Treasures Mwita Nchagwa akichangia hoja ukumbini
Wafanyabiashara wakiwa ukumbini
Tunafuatilia kinachoendelea
Katibu wa Wachimbaji wadogo wa madini mkoa wa Shinyanga Gregory Kigusi akichangia hoja ukumbini
 Katibu wa TCCIA Marcelina Saulo akielezea kuhusu namna wafanyabishara wanavyokerwa na bei kubwa ya mabango ya matangazo na kuiomba serikali kuangalia namna ya kupunguza gharama za matangazo kwani inawakatisha tamaa wafanyabishara na kuamua kuondoa matangazo

Afisa Biashara wa manispaa ya Shinyanga Sunday akieleza namna serikali inavyofanya kuhakikisha kuwa gharama za matangazo inapungua

Mkuu wa Polisi wilaya ya Shinyanga Dotto Mdoe akijitambulisha kwa wafanyabishara ambapo alisema serikali itaendelea kuwalinda wafanyabiashara katika kuuweka mji wa Shinyanga salama
MC Mama Sabuni akifanya yake ukumbini
Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Shinyanga Gasto Mkono akizungumza wakati kufunga kongamano hilo ambapo aliwaomba wafanyabiashara kujitokeza kutoa taarifa za watumishi ama idara yoyote inayowaomba rushwa katika biashara zao.

Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog

SERIKALI YATOLEA UFAFANUZI MADAI YA WALIMU NA RIBA KUBWA KATIKA MABENKI

$
0
0
Serikali imetolea ufafanuzi kuhusu kero mbalimbali za Wabunge ikiwemo kuhusu maslahi ya walimu nchini na kadhia ya riba kubwa katika mabenki. Ufafanuzi huo umetolewa leo wakati wa vikao vya Bunge vinavyoendelea mjini hapa.

Stahili za Walimu
Serikali imesema kuwa ni kweli inadaiwa na walimu madeni yasiyo ya mishahara yanayofikia  shilingi 26,042,581,697 hadi kufikia Desemba,2016. Naibu Waziri, Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo amesema deni hilo litaanza kulipwa hivi karibuni kwa kuwa deni hilo lote limeshahakikiwa.

Kuhusu madeni ya mishahara, Naibu Waziri Jafo ameliambia Bunge kuwa uhakiki wa deni la shilingi 10,034,495,540 umekamilika na kinachosubiriwa ni kulipwa kupitia akaunti ya mtumishi anayedai. Ameongeza kuwa, deni linalobaki ni shilingi 8,067,922,773 ambalo linaendelea kuhakikiwa ili nalo liweze kulipwa.

Upungufu wa Vyumba vya Madarasa na Maabara
Akijibu hoja kuhusu mkakati wa Serikali wa kupunguza tatizo la vyumba vya madarasa na maabara, Naibu Waziri Jafo amesema kuwa, Serikali katika bajeti ya mwaka 2016/17 imetenga jumla shilingi bilioni 29.3 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 3,306 kwa shule za msingi na shilingi bilioni 16.3 zimetengwa kujenga vyumba vya madarasa 1,047 kwa shule za sekondari.

Ameliambia Bunge kuwa utekelezaji wa malengo hayo pia utafanywa kupitia Mpango wa Maendeleo wa Elimu ya Sekondari (MMES II) ambako pia zimetengwa shilingi bilioni 23.6 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa vyumba 1,642. Upande wa maabara Serikali imetenga shilingi bilioni 18.9 kwa ajili ya ukamilishaji wa vyumba 2,135.

Kumuinua Mwanamke Kiuchumi
Serikali imesema kuwa hadi kufikia Desemba, 2016 Benki ya Wanawake imeshafungua matawi katika mikoa saba (7) ya Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza, Iringa, Njombe, Mbeya na Ruvuma ambapo huduma mbalimbali za kuwainua akina mama kiuchumi zimetolewa. Katika huduma hizo, dirisha la kuhudumia maeneo ya Iringa na Makambako pekee hadi kufikia Desemba, 2016 jumla ya Wajasiliamali 6,850, wanawake 5,350 na wanaume 1,500 walipatiwa.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Hamis Kigwangalla ambapo aliongeza kuwa Benki hiyo imefungua vituo vya kutolea mikopo 252 kufikia Desemba 2016.

Riba Kubwa katika Mabenki
Serikali imesema kuwa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) haiwezi kuweka ukomo wa riba za mabenki kwani si tu inapingana na jukumu lake la msingi la kusimamia mabenki, bali pia hilo liinapingana na mfumo wa uchumi wa soko huria. Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.Dkt. Ashatu Kijaji ametoa kauli hiyo wakati akijibu hoja inayohusu uwepo wa riba kubwa katika mabenki.

Dkt.Kijaji ameeleza kuwa, suala la Benki Kuu kutoa maelekezo kwa mabenki kutumia viwango fulani vya riba katika biashara zao, kutaifanya Benki Kuu kukosa nguvu na mamlaka ya kuyachukulia mabenki hatua endapo yatapata hasara kwa kutumia riba ambayo Benki Kuu imeelekeza. “Benki Kuu haina mamlaka kisheria ya kuweka ukomo wa riba au riba elekezi itakayotumiwa na mabenki katika kutoa mikopo,” alisema.

Hali ya Kituo cha Biashara cha Taifa Nchini Uingereza
Serikali imesema kuwa imekifunga rasmi Kituo cha Biashara cha Taifa kilichopo mjini London, Uingereza kutokana na changamoto mbalimbali za kituo hicho ikiwemo ufinyu wa bajeti pamoja na upungufu wa rasilimali watu.

Akijibu hoja hiyo Bungeni leo kwa niaba ya Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji amesema, badala yake, shughuli zote za kituo hicho zimehamishiwa Ubalozi wa Tanzania uliopo mjini London.

Imetolewa na:
Idara ya Habari-MAELEZO.

WAKUU WA MIKOA NA WILAYA WAPEWA RUNGU LA KUTUMBUA WATUMISHI

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  George Simbachawene amesema kuwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya wanafanya kazi kwa mujibu wa sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Simbachawene ameyasema hayo leo Bungeni, Mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la  nyongeza la Mbunge wa Jimbo la Chemba Juma Nkamia kuhusu Wakuu wa Wilaya na Mikoa kuwa wababe katika maeneo yao ya kazi.

“Wakuu wa Mikoa na Wilaya wanasimamia maeneo yao kwa mujibu wa sheria na wana haki ya kuwachukulia hatua watumishi ambao hawatekelezi majukumu waliyopewa,” alifafanua Simbachawene.

Aliendelea kwa kusema kuwa, hata kama kuna Wakuu wa Mikoa na Wilaya ambao ni wababe katika maeneo yao ya kazi hauwezi kusema kila Mkuu wa Mkoa au Wilaya aliyechukua hatua dhidi ya mtumishi ambaye hawajibiki katika kazi yake ni mbabe au muonevu.

Aidha, Simbachawene amesema kuwa ni wakati sasa wa watumishi wa Umma kutekeleza wajibu wao na kuacha kufanya kazi kwa mazoea. Kwani hakuna kiongozi ambaye ataweza kumchulia hatua mtumishi ambaye anawajibika na kazi zake kama alivyopangiwa.

Vile vile amesema kuwa, wakuu hao wa Mikoa na Wilaya wamekuwa wakifanya kazi nzuri katika maeneo wanayoyasimamia, kutokana na watumishi wengi wa Serikali walikuwa wamejisahau kutekeleza wajibu wao na kufanya kazi kimazoea.

WAZIRI MAHIGA APOKEA NAKALA ZA HATI ZA UTAMBULISHO KUTOKA KWA BALOZI WA IRAN

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Balozi Mteule wa Iran Nchini Tanzania Mhe.Mousa Ahmed Farhang aliwasili Wizarani kuwasilisha nakala za hati za utambulisho 
Waziri Mhe. Balozi Dkt. Mahiga akizungumza mara baada ya nakala za hati za utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Iran nchini Tanzania Mhe.Farhang. Kushoto ni Maafisa kutoka Ofisi za Ubalozi wa Iran nchini na Maafisa Kutoka Wizarani (kulia) wakifuatilia mazungumzo. Katika mazungumzo hayo Waziri alimkaribisha Balozi na kumhaidi kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kutoa ushirikiano wa dhati katika utekelezazi wa majukumu yake na kwa nchi ya Iran kwa ujumla, ili kuendeleza na kudumisha uhusiano wa Kidiplomasia uliodumu kwa muda mrefu kati ya Tanzania na Iran. 
Waziri Mhe. Balozi Dk. Mahiga akizungumza na mgeni wake Mhe.Balozi Farhang 
Balozi Mteule wa Iran Mhe. Farhang akizunguza mara baada ya kuwasilisha nakala za hati za utambulisho
Waziri Mhe.Balozi Dkt. Mahiga akipokea nakala za hati za utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Iran nchini Tanzania Mhe. Farhang 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Balozi Mteule wa Oman nchini Mhe. Ali A. Al Mahruqi alipowasili Wizarani kuwasilisha nakala za hati za utambulisho
Waziri Mhe. Balozi Dkt. Mahiga na Balozi Mteule wa Oman nchini Tanzania Mhe. Mahruqi wakionesha nakala ya hati ya utambulisho
Waziri Mhe.Balozi Dkt. Mahiga akimsikiliza Balozi Mteule wa Oman nchini
Mazungumzo yakiendelea, Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Balozi Abdallah Abasi Kilima akifuatila mazungumzo
Picha ya pamoja

Waziri Mahiga apokea nakala za hati za utambulisho wa Balozi Mteule wa Oman

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Balozi Mteule wa Oman nchini Mhe.Ali A. Al Mahruqi alipowasili Wizarani kuwasilisha nakala za hati za utambulisho 
Waziri Mhe. Balozi Dkt. Mahiga na Balozi Mteule wa Oman nchini Tanzania Mhe. Mahruqi wakionesha nakala ya hati ya utambulisho 
Waziri Mhe.Balozi Dkt. Mahiga akimsikiliza Balozi Mteule wa Oman nchini 
Mazungumzo yakiendelea, Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Balozi Abdallah Abasi Kilima akifuatila mazungumzo 
Picha ya pamoja 

Waziri Mahiga afanya mazungumzo na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Balozi wa Kuwait nchini Mhe.Jasem Ibrahim Al Najem walipokutana kwa mazungumzo Wizarani Jijini Dar es Salaam. Mazungumzo hayo yalijikita katika kujadili namna ya kutekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo nchini itakayo fadhiliwa na serikali ya Kuwait ikiwemo uchimbaji visima vya maji, miradi ya kuendeleza elimu na kuboresha sekta ya afya. 
Waziri Mhe. Mahiga akimsikiliza Balozi wa Kuwait nchini Mhe.Najem 
Waziri Mahiga na Balozi wa Kuwait nchini wakifurahia jambo

WAFANYA BIASHARA WAFANYA KONGAMANO KUJADILI FURSA ZA UWEKEZAJI MKOANI SHINYANGA

$
0
0
Hapa ni katika ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga ambako leo Ijumaa Februari 03,2017 kumefanyika Kongamano la wafanyabiashara kutoka wilaya ya Shinyanga lililoandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Kilimo(TCCIA) kwa kushirikiana na mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro.
Kongamano hilo lililokutanisha wafanyabishara kutoka Shinyanga Mjini na Vijijini na nje ya mkoa wa Shinyanga  lililenga la kuibua na kujadili fursa za uwekezaji zilizopo mkoani Shinyanga na kujadili changamoto zinazowakabili wafanyabiashara wenye viwanda na kilimo.
Mgeni rasmi katika Kongamano hilo ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro.
Mwandishi wetu Kadama Malunde, ametuletea picha za matukio yaliyojiri katika kongamano hilo lililoanza majira ya saa 11:25 jioni na kumalizika saa 4:06 usiku…Tazama hapa chini
Kushoto ni mgeni rasmi katika kongamano la wafanyabiashara ,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Kilimo mkoa wa Shinyanga,(TCCIA) Mchungaji Dr. Kulwa Ezekiel Meshack wakiwa katika ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga leo Ijumaa Februari 3 2017
Wafanyabiashara wakiwa ukumbini
Wafanyabiashara wakiwa ukumbini
Wafanyabiashara wakiwa ukumbini
Tunafuatilia kinachoendelea
Sekretariati wakiwa ukumbini
Afisa Tawala wilaya ya Shinyanga Charles Maugira aliyemwakilisha katibu tawala wa wilaya hiyo akitambulisha viongozi wa serikali waliohudhuria kongamano hilo
Wafanyabiashara wakiwa ukumbini
Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Geofrey Ramadhan Mwangulumbi akiwasalimia wafanyabiashara
Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Geofrey Ramadhan Mwangulumbi akiwasalimia wafanyabiashara,kulia ni naibu meya wa manispaa ya Shinyanga Agnes Machiya
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo mkoa wa Shinyanga Mchungaji Dr. Kulwa Ezekiel Meshack akizungumza wa kufungua kongamano hilo ambapo alisema wameamua kukutana ili kujadili fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo mkoani Shinyanga.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo mkoa wa Shinyanga Mchungaji Dr. Kulwa Ezekiel Meshack alitumia fursa hiyo kumpongeza rais John Pombe Magufuli kwa kuhimiza uchumi wa viwanda na kuahidi kuwa wafanyabiashara mkoa wa Shinyanga wapo tayari kumuunga mkono
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo mkoa wa Shinyanga Mchungaji Dr. Kulwa Ezekiel Meshack pia aliiomba serikali kupunguza rundo la kodi kwawafanyabiashara kwani kodi hioz zinawakatisha tamaa kuendelea kufanya biashara
Meneja wa Benki ya Maendeleo -TIB Kanda ya ziwa Zacharia Kicharo akitoa mada wakati wa kongamano hilo
Meneja Miradi kutoka Tanzania Local Enterprise Development (TLED) Stanley Magese akitoa mada wakati wa kongamano hilo
Wafanyabiashara wakiwa ukumbini
Kongamano linaendelea
Mwalimu wa walipa kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Shinyanga Anthony Faustine akitoa mada kuhusu ulipaji kodi
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwahutubia wafanyabiashara wilaya ya Shinyanga waliohudhuria kongamano hilo ambapo aliwaasa kujitokeza kuwekeza katika sekta mbalimbali ikiwemo viwanda kwani serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na rais John Pombe Magufuli inataka watanzania kuwekeza katika viwanda
Mkuu huyo wa wilaya Josephine Matiro alisema serikali ya wilaya ya Shinyanga ipo tayari kushirikiana na wafanyabishara katika kukuza uchumi wa mkoa wa Shinyanga
Matiro aliwapongeza wafanyabiashara waliojitokeza kwa wingi katika kongamano hilo na kuwaomba kuendelea kuwekeza
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga akizungumza
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisisitiza jambo
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza ukumbini
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro(kushoto) akiteta jambo na mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Shinyanga Mchungaji Dr. Kulwa Ezekiel Meshack na katibu wa Katibu wa TCCIA mkoa wa Shinyanga Marcelina Saulo
Mc Mama Sabuni anayeongoza Kongamano hilo akiwa ukumbini
Wafanyabiashara wakiwa ukumbini
Wafanyabiashara wakifuatilia kinachoendelea ukumbini
Wafanyabisahara wakiwa ukumbini.Kulia ni mkurugenzi wa Vigimark Hotel bi Victoria Majige
Tunafuatilia kinachoendelea
Kulia ni Katibu wa TCCIA mkoa wa Shinyanga Marcelina Saulo,kushoto ni Afisa tawala wilaya ya Shinyanga Charles Maugira wakifuatilia kinachoendelea ukumbini
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga Said Pamui akitoa mada wakati wa kongamano hilo ambapo aliwasisitiza wafanyabiashara kujenga mazingira ya kukopesheka,kuwa waaminifu na kulipa madeni yao kwa wakati kama wanavyokubaliana na benki 
Pamui alitumia fursa hiyo kuwapongeza wafanyabiashara wilaya ya Shinyanga kujitokeza kwa wingi katika kongamano hilo na kuwataka kujenga utamaduni wa kujitokeza katika vikao na mikutano mbalimbali ili kubadilishana uzoefu na kupeana mbinu mpya za kufanya biashara.
Wafanyabiashara wakifuatilia yanaliyokuwa yanajiri ukumbini
Mkurugenzi wa Vigimark Hotel iliyopo mjini Shinyanga Victoria Majige akizungumzia changamoto ya ubovu wa barabara inayoelekea katika hoteli hiyo ambapo aliiomba serikali kutengeneza barabara hiyo walau kwa kiwango cha moramu 
Mfanyabshara wa Uyoga wilayani Shinyanga Hamisa Nuhu akichangia hoja wakati wa kongamano hilo
Meneja wa shule ya Msingi Little Treasures Mwita Nchagwa akichangia hoja ukumbini
Wafanyabiashara wakiwa ukumbini
Tunafuatilia kinachoendelea
Katibu wa Wachimbaji wadogo wa madini mkoa wa Shinyanga Gregory Kigusi akichangia hoja ukumbini
 Katibu wa TCCIA Marcelina Saulo akielezea kuhusu namna wafanyabishara wanavyokerwa na bei kubwa ya mabango ya matangazo na kuiomba serikali kuangalia namna ya kupunguza gharama za matangazo kwani inawakatisha tamaa wafanyabishara na kuamua kuondoa matangazo
Afisa Biashara wa manispaa ya Shinyanga Sunday akieleza namna serikali inavyofanya kuhakikisha kuwa gharama za matangazo inapungua

Mkuu wa Polisi wilaya ya Shinyanga Dotto Mdoe akijitambulisha kwa wafanyabishara ambapo alisema serikali itaendelea kuwalinda wafanyabiashara katika kuuweka mji wa Shinyanga salama
MC Mama Sabuni akifanya yake ukumbini
Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Shinyanga Gasto Mkono akizungumza wakati kufunga kongamano hilo ambapo aliwaomba wafanyabiashara kujitokeza kutoa taarifa za watumishi ama idara yoyote inayowaomba rushwa katika biashara zao.

Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog

IBADA YA KISWAHILI FEB 5, 2017

JPCC KATI YA TANZANIA NA MALAWI NI CHACHU YA KUIMARISHA MAHUSIANO

$
0
0

JPCC kati ya Tanzania na Malawi ni chachu ya kuimarisha mahusiano
Wajumbe wanaoshiriki katika Kikao cha 4 cha Tume ya Pamoja ya Kudumu yaUshirikiano (JPCC) kati ya Tanzania na Malawi kilichofunguliwa leo jijini Lilongwe, Malawi wamehimizwa katika majadiliano yao yasiku tatukubuni mkakati utakaowezesha kutatua changamoto zinazojitokeza kutokana na muingiliano mkubwa wa ngazi mbalimbali za ushirikiano baina ya wananchiwamataifa hayo mawili.
Kauli hiyo imetolewa na Kiongozi wa ujumbe wa Tanzania katika ngazi ya Wataalam, Balozi Ramadhan Mwinyi ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alipokuwa anasoma hotuba ya ufunguzi.
"Kama mnavyofahamu kunapokuwa na maingiliano makubwa ya wananchi wa nchi mbili kama zilivyo nchi zetu, changamoto haziwezi kukosa kujitokeza. Hivyo ni jukumu letu sisi wataalamu kubuni mkakati wa kuhakikisha kuwa changamoto hizo zinashughulikiwa haraka iwezekanavyo".
Balozi Mwinyi alieleza kuwa kikao hicho ni fursa nzuri kwa Serikali za Tanzania na Malawi kujadili masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya nchi zao katika maeneo tofauti ikiwemo uchumi, uwekezaji, biashara, kutunza mazingira, elimu, Tehama, kilimo, uhamiaji, uchukuzi na masuala ya ulinzi na usalama, Hivyo alihimiza wajumbe wa pande zote mbili kuwa wabunifu katika majadiliano yao ili watoke na mipango inayotekelezeka kwa kuwa wananchi wanachohitaji ni maendeleo na sio mikakati inayoishia katika makabrasha.
Aidha, Balozi Mwinyi aliekeza kuwa watu wengi walistaajabu kusikia ujumbe wa Tanzania unakuja Malawi kushiriki kikao hiki kama walivyostaajabu kuona Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli alipofanya mazungumzo hivi karibuni na Rais wa Malawi, Mhe. Prof. Peter Mutharika pembezoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Umoja wa Afrika jijini Addis Ababa, Ethiopia. Alisema hakuna cha kustaajabisha hapo, isipokuwa ifahamike lengo kuu la pande zote mbili ni kuona uhusiano kati ya Tanzania na Malawi unaimarishwa na kwamba mkutano huo ni ushahidi kuwa nchi hizi mbili zipo karibu zaidi kuliko hapo awali.
Naibu Katibu Mkuu aliihakikishia Serikali ya Malawi kuwa Serikali ya Tanzania imedhamiria kushirikiana na nchi hiyo katika kuboresha mahusiano ya kidiplomasia, uchumi na kijamii, hivyo alisisitiza umuhimu wa yale yote yatakayoafikiwa katika mkutano huo yanatekelezwa katika muda uliopangwa.
Alishauri iundwe timu ya ngazi ya Makatibu Wakuu ambayo itakuwa inakutana kila baada ya miezi sita kutathmini utekelezaji wa maazimio ya kikao hicho.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Malawi, Dkt. Dalitso Kabambe alisisitiza umuhimu wa nchi hizi mbili kuweka mikakati itakayorahisisha wananchi kufanya biashara bila vikwazo. "Bisahara ni jambo muhimu lazima tuhakikishe kuwa Serikali zetu zinaweka mazingira mazuri ili wananchi wafanye biashara kwa wepesi".
Kikao hicho kinatarajiwa kufungwa rasmi na Mawaziri wa Mambo ya Nje siku ya Jumapili tarehe 05 Februari 2017 ambapo Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anatarajiwa kuwasili Malawi tarehe 04 Februari 2017. Mawaziri hao pia wataweka saini Mikataba mitatu ya ushirikiano katika mashauriano ya kisiasa na kidiplomasia, usafiri wa anga na utalii.
Wajumbe wa Tanzania katika kikao hicho wanatoka katika sekta mbalimbali wakiwemo wajumbe kutoka mikoa miwili ya Mbeya na Ruvuma inayopakana na Malawi ambao wanaongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Amos Makalla.
Imetolewa na: Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Tarehe 03 Februari 2017

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Malawi na Mwenyekiti Mwenza wa Kikao cha JPCC kati ya Tanzania na Malawi, Dkt. Kalitso Kabambe akisoma hotuba ya iufunguzi na ukaribisho.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan Mwinyi akisoma houtuba ya ufunguzi wa kikao cha Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (JPCC) kati ya Tanzania na Malawi. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Malawi, Dkt. Dalitso Kabambe. Kikao hicho kinafanyika Lilongwe, Malawi kwa muda wa siku tatu kuanzia tarehe 03 Februari 2017.

Wajumbe wa Tanzania wakisikiliza hotuba za Makatibu Wakuu. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Amos Makalla, Mkurugenzi Msaidizi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, Bw. Suleiman Salehe na Kaimu Mkurugenzi kutoka Mamlka ya Viwanja vya Ndege.
<!--[if gte mso 9]>

JESHI LA POLISI LAWASIMAMISHA KAZI ASKARI 12 WANAODHANIWA KUJIHUSISHA NA BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA

NAPE AIPONGEZA SERENGETI BOYS KWA KUFUZU FAINALI ZA AFCON GABON 2017

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye

Mahakama yasitisha amri ya Trump dhidi ya Wahamiaji-BBC

$
0
0
Raia waandamani wakipinga amri ya donald Trump ya kuwazuia Waislamu kutoka mataifa saba kuingia Marekani
Jaji mmoja wa Marekani amesimamisha kwa muda utekelezaji wa amri ya Rais Donald Trump ya kuwazuia raia kutoka mataifa saba, yaliyo na raia wengi wa imani ya Kiislamu kuingia nchini Marekani.

Jaji wa Seattle alipuuzilia mbali sababu zilizotolewa na mawakili wa Serikali na kusema kuwa amri hiyo inaweza kusimamishwa mara moja huku kesi hiyo ikiendelea kusikilizwa mahakamani.

Serikali inatarajiwa kukata rufaa ya dharura dhidi ya uamuzi huo wa mahakama, ambao ni changa moto kubwa kwa utawala wa Trump.

Serikali ya Marekani inasema kuwa makumi ya maelfu ya visa zimefutiliwa mbali tangu rais Trump kutia sahihi amri ya kupunguza idadi ya watu wanaopaswa kuingia nchini Marekani juma lililopita.

Wakati huohuo waziri Mkuu wa zamani wa Norway, Kjell Magne Bondovik, alisema kuwa alizuiwa katika uwanja mmoja wa ndege mapema juma hili, katika tukio alilosema ni la uchokozi, kwa sababu eti alikuwa na visa ya Iran katika paspoti yake.

Wengi Wanaachika kwa Kutikisa Kiberiti, Jifunze!

$
0
0
Na ERICK EVARIST |RISASI JUMAMOSI| LOVE STORY
“MWANAMKE wangu ukimuambia naomba uwe unazima friji kwa kipindi ambacho halina ulazima, huwa anajaribu kuliacha ili aone nitamfanya nini. “Anatikisa kiberiti. Anapuuza makusudi, nikiliona friji linaunguruma na wakati huo hakuna ulazima wa kuliwasha, nikimuuliza kwa nini umeliacha, ananiambia nilisahau. “Mimi nalizima. Namueleza kwamba anapaswa kuwa makini sababu ya kubana matumizi. Kesho tena unakuta ameacha hivyohivyo, ukimueleza anakwambia ‘kwani si ulizime wewe kama umeliona, hadi nizime mimi?’
“Namueleza kwamba asifanye hivyo, hali ya uchumi ni ngumu na mlipaji ni mimi, siku nyingine asifanye hivyo halafu nalizima. Unakaa siku mbili tatu, tatizo lile tena linajirudia. “Unakwenda kwenye shughuli zako, ukirudi unakuta friji linaunguruma tena kutwa nzima kukiwa hakuna kitu chochote kilichowekwa ndani yake. “Jambo hili sio kwenye friji tu. Hata KWA KUTIKISA Wengi wanaachika KIBERITI, JIFUNZE!
kwenye vitu vidogovidogo. Wakati mwingine, namuambia ajitahidi akichana nywele zake kwa kitana ambacho natumia, ahakikishe anatoa nywele zinazobaki kwenye kitana, anaziacha tu makusudi. “Anafanya hayo yote kama kutikisa kiberiti.

Anajaribu kunitunishia msuli. Akiona nimemaindi, anashuka. Anakuwa mpole. “Yaani kuna ukorofi huwa nauona kama vile huwa anaamua tu kuufanya.
Unamuachia nguo na kumwambia azifue mwenyewe, asimuachie dada wa kazi kwani amekuwa akikosea kufua vile ambavyo unataka. Anakusikiliza leo, kesho ukirudi unamkuta dada wa kazi anafua. Nakasirika kwelikweli. “Sasa kuna wakati niliamua kumuonesha sura ya kukasirika na kumkemea kwa hasira katika kila jambo, aliliacha mara moja. Nikamwonesha kwamba nimekasirika, kwa kila jambo nilimwambia kama ataendelea nalo, nitamfanyia kitu ambacho hatakisahau maishani,” huo ni mfano kutoka kwa msomaji wangu. Karibu tujifunze sasa;
SOMO KWA WANAWAKE Kuna wanawake wana kasumba ya namna hiyo. Wanapenda kuwajaribu wenzi wao katika mambo fulani ili kuona watafanya nini. Akiambiwa usifanye hivi, yeye anafanya. Akiona umenyamaza, hujaonesha kumkaripia, kesho anarudia. Yaani anafanya ilimradi tu. Anataka kuona utakasirika kiasi gani. Unamwambia naomba uniwekee maji ya kuoga, anakwambia nenda kaweke mwenyewe.
Au anakupa yale majibu ya ‘mimi mwenzako nimechoka’. Anaambiwa na mumewe, nipigie pasi majibu yake ni ‘kapige mwenyewe. Na mimi huwa nachoka’ HILI NI TATIZO!
Mwanamke anapofanya hivyo, anasababi sha ugomvi wa mara kwa mara na kuamua kumuacha mwanamke wa aina hiyo bila hata ya kumuambia nini tatizo lake. Wanaume wengi wanakutana changamoto hiyo.
Wapo wanaoweza kutenda kwa kumchimba mkwara mwenzi wake na kufanikiwa kunyoosha mambo lakini wengine wanaamua kufanya maamuzi yao moyoni. Anabwanga manyanga chini, anaendelea mbele. Wanaume wanapofanyiwa mambo hayo huwa wanaamini wamedharauliwa.
Unapomfanyia jambo ambalo anaona unaweza kulifanya anaudhika mno. Anajenga ile dhana ya yeye ni kichwa cha familia. Anakasirika kuona kwenye eneo hilo anashindwa kuheshimika hata kama ni jambo dogo kiasi gani lakini linaweza kuleta madhara makubwa ambayo yanaweza kugharimu kabisa uhusiano wenu. Kwenye akili yake anafikiri, usipomheshimu yeye utamheshimu nani? Amekueleza usifanye hivi kwa sababu unamkera, unafanya halafu unasikilizia.
Mungu asaidie aamue kukuchimba mkwara na wewe ufanye. Au akuseme halafu mgombane, muachane.
INAKUGHARIMU NINI KUTII?
Nimeshawahi kusema kwenye makala zangu huko nyuma, kuna gharama gani mke akimtii mumewe katika mambo ambayo hayana gharama yoyote kwake? Utapungukiwa nini? Ukimtii mumeo unayemfahamu kwamba ndiye kichwa cha familia?
JIFUNZE KWA MAANDIKO HAYA!
“Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu. Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili. Lakini kama vile kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo,” Waefeso 5: 21-23. Sasa

NASHONA NC KUFUNGUA DUKA LAKE MWENYEWE LEO JUMAMOSI

OLD SCHOOL REUNION, COLUMBUS, OH KUWAKA MOTO LABOR DAY NICO NA RENATUS NJOHOLE KUINGOZA SIMBA UGHAIBUNI, WACHEZAJI WALIOTAMBA PAZI, VIJANA, DON BOSCO KUONYESHANA MAUJUZI

$
0
0
Kikosi cha Simba kikiongozwa na Nico na Renatus Njohole Dallas, Texas.
Kikosi cha Yanga
Kikosi cha Simba kikiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Balozi Wilson Masingingi na mkewe siku walipotwaa ubingwa Dallas, Texas wakati wa kongamano la DICOTA
Kulia ni mkuu wa Wilaya Mhe. Kasesela akiwa Hoston katika picha ya pamoja na wachezaji wa Pazi enzi hizo Vitalis Gunda na Atiki Matata aliyekuja toka Uingereza kuiwakilisha Pazi.
Timu ya Tanzania iliyoundwa na wachezaji waliotamba enzi hizo katika timu za Pazi, Vijana, Don Bosco na kwengineko wakinyanyua juu kikombe walicho kipata baada ya kuifunga timu ya Gabon
Viewing all 45934 articles
Browse latest View live

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>