Quantcast
Channel: VIJIMAMBO
Viewing all 45933 articles
Browse latest View live

WAJAWAZITO,WATOTO KILOMBERO WAKOSA CHANJO KUTOKANA UMBALI WA VITUO VYA AFYA.

$
0
0

Wajawazito na watoto katika maeneo mengi ya wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro wamekosa huduma za msingi za chanjo na ushauri mwingine wa kiafya, huku kina mama wajawazito wakijifungua njiani na kupata matatizo mbalimbali ya uzazi, kutokana na umbali mrefu wa kuvifikia vituo vya afya na zahanati zinazotoa huduma hiyo.
Maria Mayanda ni mkazi wa kitongoji cha Mikochini Namawala B, kata ya Namawala wilayani Kilombero, ambaye ni miongoni mwa kina mama waliojifungulia njiani, kutokana na umbali wa zaidi ya kilometa 40 kufikia zahanati au kituo cha afya, ambaye anadai kupata tatizo hilo baada ya mito ya maeneo yao kufurika maji  nyakati za mvua na njia kushindwa kupitika kirahisi, hali iliyofanya viongozi wa maeneo hayo wakiongozwa na mwenyekiti wao matia nyambo,kuhamasishana na kujenga banda maalum kwaajili ya kupatiwa huduma za mkoba yaani mobile cliniki.
Shirika la Plan International Tanzania kwa msaada wa kampuni ya Dalichi Sankyo kutoka Japan, wameona changamoto hizo na kuanzisha mradi wa miaka mitatu wa huduma za mkoba, ili kuisaidia serikali kutokomeza maradhi yanayozuilika na kupunguza vifo vya watoto na akina mama wilayani Kilombero, kwa kuwezesha huduma za chanjo katika maeneo magumu kufikika na yaliyo mbali na vituo vya afya, nia hasa ikiwa kutokomeza magonjwa kama surua, polio, kifua kikuu, dondakoo, kifaduro, homa ya ini, homa ya uti wa mgongo, kichomi, nimonia na pepopunda kwa watoto wa hadi miaka mitano kwa kutumia chanjo,
Mpango huo utakaofanywa bure, ukiwa unagharimu milioni 660 hadi kukamilika, umekwenda sambamba na halmashauri hiyo kukabidhiwa gari kwaajili ya huduma za mkoba zitakazotolewa kwa kata 18, ambapo Mkurugenzi wa halmashauri ya Kilombero Denis Londo, aliyeomba msaada zaidi wa pikipiki tano kurahisisha upelekaji huduma, amekiri mwaka jana wameshindwa kufikia lengo la kutoa chanjo kwa asilimi 95 kama wizara ya afya ilivyogiza badala yake wakatoa asilimia 85 tu lakini wanaimani hali hiyo itapungua kupitia mradi huo, huku mkuu wa wilaya ya kilombero  james ihunyo,akibainisha dhamira ya serikali ya awamu ya tano kutokomeza vikwazo vinavyosababisha vifo kwa mama na mtoto kwa kukosa huduma.
Katika mwaka 2013, wilaya ya Kilombero ilikuwa na vifo 144 vitokanavyo na uzazi kwa kila vizazi hai 1,000 huku vifo vya watoto wa umri chini ya miaka mitano vikiwa vinne kati ya vizazi hai 1,000, na hadi sasa wilaya hiyo ina vituo vichache vinavyotoa huduma ya chanjo, ambapo kati ya vituo vya afya 63, ni vituo 40 tu vinavyotoa huduma za mkoba na kupitia mradi huo Kilombero wameainisha vituo 66 vilivyo umbali wa zaidi ya kilometa 35 kutoka vituo vya afya ambavyo ni vigumu kufikika kirahisi lakini mradi huo utafikia vituo 49 tu.

CHANZO : ITV TANZANIA

WABUNGE WANAWAKE WAJUMUIKA KUFANYA MAZOEZI YA PAMOJA UWANJA WA JAMHURI MJINI DODOMA

$
0
0

Naibu Spika wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiongea na Wabunge (hawapo pichani) pamoja na Waandishi wa Habari kuhusu umuhimu wa kufanya mazoezi kwa ajili ya kulinda afya leo katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.
Naibu Waziri, Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazia Wambura (Mb) akiongea na Wabunge wenzake (hawapo pichani) kuhusu umuhimu wa kufanya mazoezi kwa ajili ya kulinda afya ya miili pamoja na matarajio ya Uzinduzi wa Mazoezi yanayotarajiwa kuzinduliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo yatatangazwa hivi karibuni.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Mhe. Ritta Kabati akiongea na Wabunge wenzake pamoja na Waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa kufanya mazoezi kwa ajili ya kulinda afya ya miili wakati wa mazoezi ya pamoja kwa Wabunge hao wanawake yaliyofanyika leo 03/02/2017 Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma. 
Mbunge wa Jimbo la Ilemela Jijini Mwanza (CCM), Mhe. Angeline Mabula akiongea na Wabunge wenzake pamoja na Waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa kufanya mazoezi kwa ajili ya kulinda afya ya miili wakati wa mazoezi ya pamoja kwa Wabunge hao wanawake yaliyofanyika leo 03/02/2017 Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma. 
Baadhi ya Wabunge wanawake wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa wameongozana na Spika wa Bunge (wa pili kushoto) wakifanya mazoezi (Jogging) ikiwa ni sehemu ya kufanya mazoezi ya pamoja kwa ajili ya kuweka sawa miili, mazoezi hayo yamefanyika leo 03/02/2017 katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma. 



Baadhi ya Wabunge wanawake wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa wakifanya mazoezi ikiwa ni sehemu ya kufanya mazoezi ya pamoja kwa ajili ya kuweka sawa miili, mazoezi hayo yamefanyika leo 03/02/2017 katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma. 
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (wa pili kushoto) akifanya mazoezi ya mwili ikiwa ni sehemu ya ya kuweka sawa mwili, mazoezi hayo yamefanyika leo 03/02/2017 katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma. 

(Picha zote na Benedict Liwenga)

Ripotini vyuo vikuu vinavyotoza kwa dola – Serikali

$
0
0
Serikali imetoa wito kwa Watanzania kutoa taarifa wizara ya Elimu ikiwa kuna chuo chochote kinachotoza ada kwa Watanzania fedha za Kigeni ili hatua stahiki za kisheria zichukuliwe dhidi ya wahusika.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhandisi Stella Manyanya, mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali lililohusu kwamba kumekuwa na malalamiko ya wanafunzi wa Elimu ya Juu Tanzania ambao ni wazawa kulipishwa ada ya masomo yao kwa fedha za kigeni badala ya fedha za Kitanzania.
Mhandisi Manyanya alijibu, “Sarafu inayotakiwa kutumika Tanzania ni shilingi ya Kitanzania kwa mujibu wa kifungu cha 25 na 26 cha Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT) ya mwaka 2006. Aidha, kwa Tanzania malipo ya kitu au
huduma yoyote inapaswa kulipwa kwa shilingi ya Kitanzania kama ilivyoainishwa kwenye kifungu cha 28 cha Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania, 2006,” alifafanua.
Aliongeza “Japo Wizara haijapokea malalamiko yoyote ya kutozwa fedha za kigeni kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu tangu itoe agizo kama hilo kwa wamiliki wa vyuo Septemba 07, 2016. Vyuo ambavyo bado vinatoza wanafunzi watanzania fedha za kigeni kuacha mara moja kwani vyuo hivyo vimeelekezwa kutoza wananchi wa Kitanzania kwa pesa ya Kitanzania. Natoa wito kwa Watanzania kutoa taarifa wizara ya Elimu ikiwa kuna Chuo chochote kinachotoza ada kwa Watanzania fedha za Kigeni ili hatua stahiki za kisheria zichukuliwe dhidi ya wahusika.”
Mkutano wa Bunge uliopita swali kama hili liliwahi kuulizwa, na bado serikali imeweka mkazo kukataa wanafunzi wa kitanzania kulipa ada kwa fedha hizo.

SERIKALI YAZINDUA MWONGOZO WA UJENZI WA BARABARA ZINAZOPITISHA MAGARI MACHACHE

$
0
0
 Mkurugenzi wa Barabara, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng.  Ven Ndyamukama, akitoa hotuba ya utangulizi katika uzinduzi wa Mwongozo wa ujenzi wa Barabara zinazotumiwa  na magari machache, uliozinduliwa leo jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamuhanga, akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa Mwongozo wa ujenzi wa Barabara zinazotumiwa na magari machache, uliozinduliwa leo jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamuhanga (kushoto), akikata utepe kwenye kitabu cha Mwongozo wa ujenzi wa Barabara zinazotumiwa na magari machache, mara baada ya kuuzindua leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Meneja wa AFCAP Kanda ya Mashariki na Kati mwa Afrika, Eng. Nkulule Kaleta.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamuhanga (kushoto), akimkabidhi nakala ya kitabu cha Mwongozo wa Ujenzi wa Barabara zinazotumiwa na magari machache, mmoja wa wadau waliohudhuria uzinduzi huo, leo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamuhanga (wa nne kutoka kulia waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe  waliohudhuria uzinduzi wa Mwongozo wa ujenzi wa Barabara zinazotumiwa na magari machache hapa nchini.

 Serikali imezindua mwongozo wa mpango na usanifu wa ujenzi wa barabara zinazopitisha magari machache kwa lengo la kutoa maelekezo na kuwawezesha wahandisi wanaofanya usanifu wa barabara hizo kutumia gharama nafuu za ujenzi.
Akizungumza katika uzinduzi huo leo jijini Dar es salaam Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga amesema kuwa mwongozo huu utakuwa tiba na kuwezesha Serikali kujenga barabara nyingi na gharama nafuu.
“Ujenzi na ukarabati ya barabara zinazopitisha magari chini ya 300 kwa siku utakuwa wa gharama nafuu, kama tutatumia mwongozo huu kwani utasaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazokabili barabara nyingi hususan za vijijini”, amesema Katibu Mkuu.
Amewataka wahandisi na Mafundi ujenzi kutumia mwongozo huo katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuweza kusaidia kazi na miradi mbalimbali ya barabara kuweza kufanyika kwa viwango vilivyo bora na gharama nafuu.
“Hakikisheni wahandisi na Mafundi ujenzi mnafuata mwongozo huu ipasavyo na kuanzia sasa uwe dira kwenu katika kazi zenu za kila siku”,  amesisitiza Eng. Nyamhanga.
Ameongeza kuwa kutokana na tafiti mbalimbali zilizofanywa Serikali imegundua uhitaji mkubwa katika mtandao wa barabara nchini ili kusaidia maendeleo ya kila mwananchi mijini na vijijini.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Barabara katika Wizara hiyo Eng. Ven Ndyamukama amesema kuwa mwongozo huo  unafananua namna ujenzi wa barabara hizo unavyokuwa ikiwemo kujenga kulingana na idadi ya magari yanayopita.
Ameongeza kuwa Mwongozo huo unaelekeza kutumia rasilimali chache zilizopo na kuhakikisha masuala ya mazingira  katika maeneo yanayojengwa barabara hizo yatazingatiwa.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

HALMASHAURI YA WILAYA YA KISARAWE YATENGA KATA 10 KWA AJILI YA KILIMO CHA MKATABA

$
0
0
Mgeni rasmi katika uzinduzi wa mradi wa kilimo cha mkataba kupitia Taasisi ya Winamwanga Cultural Heritage Association kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, ambaye ni Ofisa Maendeleo ya Jamii, Wanchoke Chinchibera akihutubia wadau wa kilimo wa wilaya hiyo wakati wa semina ya siku moja iliyohusu kilimo cha mkataba iliyofanyika juzi wilayani humo. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa mradi huo, Mwajuma Motto, Ofisa Kilimo na Umwagiliaji wa wilaya hiyo, Elliot Mwasabwite na Mwenyekiti wa Bodi wa Taasisi hiyo, Esabela Luoga.

Mmoja wa maofisa wa Taasisi hiyo, Wilson Kibugu akitoa maelezo kwa wadau wa kilimo wa wilaya hiyo wakati wa semina hiyo ya siku moja iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa Wilaya hiyo.
Semina ikiendelea.
Meza kuu.

Ofisa Utawala wa Taasisi hiyo, Fatma Shaib (kushoto), akisoma lisala.
Mgeni rasmi Wanchoke Chinchibera akipokea lisala kutoka kwa Ofisa Utawala wa Taasisi hiyo, Fatma Shaib.
Mratibu Mradi wa Kilimo wa Taasisi ya  Winamwnga Cultural Heritage Association, Saidi Simkonda (katikati), akitoa mada katika uzinduzi  wa mafunzo ya kilimo hai na mafunzo ya ufugaji wa kuku chotara na mafunzo ya utunzaji wa mazingira yaliyofanyika wilayani Kisarawe mkoani Pwani juzi. 
Ofisa Mauzo wa Kampuni ya Syngeta Tanzania Limited, John Ngoma akielezea ubora wa mbegu aina ya Sy 514 inayosambazwa na kampuni hiyo kupitia miradi ya kilimo ya taasisi hiyo.
Mkurugenzi wa Mradi wa kilimo wa Taasisi ya  Winamwnga Cultural Heritage Association, Mwajuma Motto (katikati), akizungumza katika uzinduzi wa mafunzo ya kilimo hai na mafunzo ya ufugaji wa kuku chotara na mafunzo ya utunzaji wa mazingira kwa kutumia vikundi vya ufugaji wa nyuki yaliyofanyika wilayani Kisarawe mkoani Pwani jana. Kulia ni Mwezeshaji, Filbert Luoga na kushoto ni mratibu wa miradi wa taasisi hiyo, Saidi Simkonda. 
Ofisa Kilimo na Umwagiliaji wa wilaya hiyo, Elliot Mwasabwite akichangia jambo kwenye semina hiyo.

 Dotto Mwaibale, Kisarawe
HALMASHAURI ya Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani imetenga Kata 10 kwa ajili ya kilimo cha mkataba kitakachoendeshwa na Taasisi ya  Winamwanga Cultural Heritage Association.

Mratibu wa mradi huo kutoka taasisi hiyo, Saidi Simkonda akizungumza juzi katika uzinduzi wa mafunzo ya kilimo hai na mafunzo ya ufugaji wa kuku chotara na mafunzo ya utunzaji wa mazingira kwa kutumia vikundi vya ufugaji wa nyuki yaliyofanyika wilayani humo juzi alisema mradi huo umelenga kuwainua kiuchumi wananchi wa Kisarawe na Mkoa wa Pwani kiujumla.


Alisema taasisi hiyo imepanga kuanzisha vikundi vya kuweka na kukopa ili kuinua uchumi wa wananchi kupitia vikundi vya ujasiriamali wa kilimo hai na ufugaji wa kuku chotara pamoja na kuwawezesha kupata fursa za mikopo katika asasi za kifedha zilizopo wilayani humo.

"Taasisi yetu imejipanga kuanzisha kilimo cha mkataba ambapo mazao yatakayopatikana itayanunua na tayari serikali ya Kijiji cha Kuluwi imetoa ghala la kuhifadhia mazao hayo.

Mgeni rasmi katika uzinduzi wa mradi huo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmshauri hiyo ambaye ni Ofisa Maendeleo ya Jamii, Wanchoke Chinchibera alisema mradi huo utawasaidia wananchi na kuwa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe imetenga kata kadhaa kwa ajili ya mradi huo ambazo ni Maluwi, Vikumburu, Kuluwi na Mafizi.

Alisema kwa sababu mradi huo ni mpya katika wilaya yao na utafanya shughuli zake kwa kilimo cha mkataba aliishauri taasisi hiyo kujenga ushirikiano mkubwa na wananchi kupitia vikundi ambavyo tayari vimesajili na majina yake kuwepo katika daftari ofisini kwa mkurugenzi wa halmshauri hiyo.

UHAMIAJI KUTOA PASIPOTI KWA SIKU TANO KUANZIA SASA, NAIBU KATIBU MKUU SIMBA AZINDUA MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA, JIJINI DAR

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa Idara ya Uhamiaji. Mkataba huo ambao unalenga kuimarisha huduma mbalimbali za Idara hiyo pia umeelekeza kuanzia sasa Hati za Kusafiria (Pasipoti) zitatolewa kwa siku tano za kazi kwa watakaoomba Makao Makuu Dar es Salaam na Zanzibar, pia Wateja wa mikoani watapata Pasipoti hizo kwa siku zisizozidi kumi. Wapili kushoto ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Idara hiyo, Victoria Lembeli. Uzinduzi huo umefanyika Makao Makuu ya Idara hiyo, Kurasini jijini Dar es Salaam. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya akizungumza na wananchi (wateja) waliofika Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji kabla ya Balozi huyo hajazindua Mkataba wa Huduma kwa Mteja ulioandaliwa na Idara hiyo. Simba alisema Mkataba huo unalenga kuimarisha huduma za Uhamiaji ambapo kuanzia sasa Pasipoti zitapatikana kwa siku tano za kazi mara baada ya mteja kuiomba Makao Makuu Dar es Salaam na Zanzibar, pia Wateja wa mikoani watapata Pasipoti hizo kwa siku zisizozidi kumi. Uzinduzi huo umefanyika Makao Makuu ya Idara hiyo, Kurasini jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (aliyevaa tai) akimsikiliza mteja aliyefika kupata huduma ya Pasipoti Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, Kurasini jijini Dar es Salaam mara baada ya Balozi huyo kuwauliza maswali wateja waliofika ofisini hapo. Hata hivyo, wateja hao walisema wanapewa huduma nzuri na maafisa wa Idara hiyo. Balozi Simba alizindua Mkataba wa Huduma kwa Mteja ambao unalenga kuimarisha utoaji wa huduma bora katika Idara hiyo. Katikati ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Idara hiyo, Victoria Lembeli.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya akizungumza na Watendaji Wakuu wa Idara ya Uhamiaji nchini kabla ya Balozi huyo kuzindua Mkataba wa Huduma kwa Mteja ulioandaliwa na Idara hiyo ambao unalenga kuboresha zaidi huduma zitolewazo na Uhamiaji ambapo kuanzia sasa Pasipoti zitapatikana kwa siku tano za kazi mara baada ya mteja kuiomba Makao Makuu Dar es Salaam na Zanzibar, pia Wateja wa mikoani watapata Pasipoti hizo kwa siku zisizozidi kumi. Uzinduzi huo umefanyika Makao Makuu ya Idara hiyo, Kurasini jijini Dar es Salaam. Watatu kushoto (upande wa pili) ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Idara hiyo, Victoria Lembeli.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (katikati), akimsikiliza Kaimu Kamishna Jenerali wa Idara hiyo, Victoria Lembeli alipokuwa anatoa maelezo mafupi jinsi Watendaji wa Idara yake walivyouandaa Mkataba wa Huduma kwa Mteja ambao Balozi huyo aliuzindua Makao Makuu ya Idara hiyo, Kurasini, jijini Dar es Salaam. Mkataba huo unalenga kuboresha zaidi huduma zitolewazo na Uhamiaji ambapo kuanzia sasa Pasipoti zitapatikana kwa siku tano za kazi mara baada ya mteja kuiomba Makao Makuu Dar es Salaam na Zanzibar, pia Wateja wa mikoani watapata Pasipoti hizo kwa siku zisizozidi kumi.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kulia), akimkabidhi Vitabu vya Mkataba wa Huduma kwa Mteja Kaimu Kamishna Jenerali wa Idara Uhamiaji, Victoria Lembeli mara baada ya Naibu Katibu Mkuu huyo kuzindua Mkataba huo katika Ofisi za Makao Makuu ya Idara hiyo, Kurasini, jijini Dar es Salaam leo. Mkataba huyo unaelekeza kuanzia sasa Pasipoti zitapatikana kwa siku tano za kazi mara baada ya mteja kuiomba Makao Makuu Dar es Salaam na Zanzibar, pia Wateja wa mikoani watapata Pasipoti hizo kwa siku zisizozidi kumi.

Musician Recaptures Tanzanians Lost Glory

$
0
0
Tanzania has regained its lost glory in world of music fame that has dwindled since the eighties.

When the name of Tanzania is currently mentioned in international music circles the name of Ebrahim Makunja popularly known as Ras Makunja of FFU and his “The Ngoma Africa Band” aka FFU based in Germany cannot be slighted. FFU has earnestly strived to place Tanzania in the international music charts.

It is the only Tanzanian band that is based overseas. Its contribution in the music industry both in Tanzania, East Africa and abroad is superb. The band has often been able to bring its records to radio stations back at home.

Many of their hits touch the souls of their fans. Two of their hits, which are very popular in local radio stations and contained in “50 Uhuru Anniversary” CD are “Shangwe”, and “Miaka 50 ya Uhuru”. The rumba style songs are composed by band leader Ras Makunja.

He pairs in singing with the comical solo guitarist Chris-B. Apart from the well composed lyrics and the highly perfected musical beat the songs carry very strong and emotional messages to the community. Their messages are acclaimed not only in Tanzania but world all over.

Ras Makunja of FU, is not only a seasoned tactful and artistic composed. He too has visionary messages to the society. To call him Kamanda (Commander) Ras Makunja is not demeaning him.

He ensured that two of his CDs including “Jakaya Kikwete 2010″ which claimed global fame reached more than 310 radio stations in the world. This CD earned him the mark of being a hard headed musician from some quarters.

His band now dubbed FFU (Fanya Fujo Uone) literally means creates chaos and see, immediately came up with a CD “Anti Corruption Squad” which has the song “Rushwa ni Adui wa Haki”. The fans see this song as the Al-Albadir of the corrupt.

The song was a smash hit within Tanzanians. It placed Ras Makunja and his band ‘Ngoma Africa’ not only as ordinary musicians in the musical arena. They had something else to offer the society apart from the usual entertainment. Visionary eye opening and soul searching messages.

Yet despite all this no one seems to realize the onerous task that this musicians does. They have never been ordained with a single medal here at home. As a popular Swahili goes “Asiyekuwepo na lake halipo” (He who is not there (present) so is his/her share). Ras Makunja and Ngoma Africa may not be with us, but his works and messages are!

The official web of the band is www.ngoma-africa.com One can become a fan member of the band by signing up. The good work the band is doing in promoting Tanzania in the field of music deserves local support both in cash and form.

Tamasha la Sauti za Busara linakuza utamaduni wa utalii

$
0
0
2 FEBRUARY 2017 – NGOME KONGWE, ZANZIBAR: Alhamis ya wiki ijayo tarehe 9 Februari tamasha la Sauti za Busara litaanza na sekta ya utalii ndani ya Zanzibar itachukua sura mpya. Baada ya mwaka mmoja wa kutofanyika kwa tamasha hilo, sasa tamasha limerudi kuutangaza utamaduni, kujenga uwezo na kukuza uchumi wa ndani pamoja na kutoa ajira na mafunzo kwa watu wa Afrika Mashariki.

Tamasha la Sauti za Busara limetengeneza zaidi ya dola 70 za kimarekani kwenye pato la Zanzibar tangu limeanza mwaka 2004. Kila mwaka, timu ya watu 10 huongezeka kufikia watu 150 ambao huajiriwa kufanya kazi kwa ajili ya tamasha na kipaumbele hutolewa kwa wazawa kwenye upande wa kusimamia mambo ya wasanii, utawala, mahusiano ya habari, tiketi, vibanda vya mauzo na ulinzi.

Lengo la Busara kutoa mafunzo na ujuzi ni kukuza uchumi wa jamii ya ndani. Mwaka 2016 Busara Promotions ilitoa mafunzo juu ya usimamizi wa jukwaa, ufundi wa sauti, usimamizi wa mwanga jukwaani, mambo ya habari na ujuzi wa masoko. Kwa ushirikiana na matamasha kama Bushfire huko Swaziland na Oya huko Norway, timu ya Busara imefaidika na kubadilishana ujuzi na maswasiliano na timu za matamasha mengine.

Sauti za Busara imeseadia kuiweka Zanzibar kwenye ramani ya utalii. Trish Dhanak, mmiliki wa Upendo hotel anafafanua, “Kama muwekezaji, ni wajibu wetu kuwaonesha wasafiri uzuri wa Zanzibar, na kujifunza kwa kina uhalisia wa kisiwa hiki. Sauti za Busara ni kiunganisho kwa wasafiri kutoka sehemu mbalimbali duniani na Afrika ni muziki Zanzibar na ni matarajio yetu kuwa wakati wa uwepo wao wata[ata sababu ya kuwafanya warudi.”

Kwa sasa Februari ni mwezi ulio juu kwa kuwasili wageni zaidi ya elfu 40,000. Mpaka sasa huduma za usafiri nyingi zimejaa. Hoteli na migahawa yote ishakuwa tayari kuelekeza nguvu kuhudumia wageni wa tamasha,

Kadri tamsha linavyokua na kuvutia wageni wengi wa kimataifa kila mwaka tunafanya tamasha kuwa kipaumbele kwa wazawa. Mwaka huu, kwa watanzania tu kwa siku zote nne ni Sh 20,000 au Sh6,000 kwa siku, Wenye asi za kusafiria za Afrika watalipa Sh120,000 au Sh50,000 kwa siku. Tiketi zitapatikana Ngome Kongwe kuanzia Jumanne tarehe 7 February, kuanzia saa 4:00 kamili asubuhi.

Tamasha la Sauti za Busara 2017 limedhaminiwa na: Ubalozi wa Norway, Hirika la Uswis la Ushirikiana na Maendeleo (SDC), ZANTEL, Africalia, Ubalozi wa Ujerumani, Zanlink, Memories of Zanzibar, Ethiopian Airlines, Mozeti, Coastal Aviation, Ikala Zanzibar Stone Town Lodge, Music in Africa, Chuchu FM Radio, Tifu TV na Zanzibar Media Corporation.

Kwa mawasiliano zaidi: busaramusic.org

<<<<<<<<<< [MWISHO]

WAZEE KATAVI WAFURAHIA FEDHA ZA TASAF

$
0
0
Na Mussa Mbeho Katavi

WAZEE wanaonufaika na fedha zinazotolewa na serikali katika mpango
wake wa kunusuru kaya maskini kupitia mradi wa TASAF III Mkoani Katavi wameanza kufunguka juu ya manufaa wanayopata
kupitia mpango huo.

Wakizungumza na mwandishi wa gazeti hili hivi karibuni wakati wa zoezi la kugawiwa fedha hizo ikiwa ni mgao wa 15 tangu kuanza kwa mradi huo, wazee hao walisema wazi kuwa mpango huo umeanza kuboresha maisha yao sambamba na afya zao.

Walisema fedha hizo zimewawezesha kuwa na uhakika wa maisha sambamba na kupata milo 3 ya chakula na sasa wana afya
njema sana.

Mzee Paschal Daniel (75) mkazi wa kijiji cha misunkumilo
katika kata ya misunkumilo alisema mwanzoni alipewa sh 30,000 akazitumia kwa chakula tu lakini mgao uliofuata alinunua kuku 2 baadae 3.

Aliongeza kuwa fedha hizo japo ni kidogo lakini zinawasaidia sana kimaisha kwani zamani alikuwa anaishi maisha ya taabu sana ikiwemo kuomba omba lakini sasa haombi tena kwa watu.

‘Sasa siombi tena chakula kwa watu, naomba serikali
iache mradi huu uendelee, wasiuondoe,' aliongeza.

Mzee Magubika Andrea (80) mkazi wa kijiji cha Mitwigu anaeleza kuwa
tangu aanze kupata hela za TASAF III maisha yake yamebadilika sana
kwani ana uhakika wa kupata chakula kila siku na tayari amefuga kuku
10 na amepanga kununua bati moja moja ili kuezeka nyumba yake, anataka
kuondoa nyasi.

Mzee VITARIS PETRO (74) wa kijiji cha Ilembo alieleza bayana kuwa
alikuwa anaumwa sana na chakula kilikuwa hamna, lakini baada ya kupata
hela hizo akanunua dawa na chakula, sasa ameshapona na afya yake
imerudi vizuri hana wasiwasi tena ameanza kunawili.

‘Kama sio hizi hela za serikali ningekufa mapema, nilikuwa
naumwa sana, ndani chakula hamna, watoto hawaendi shule hata nguo
walikuwa hawana, baada ya kupewa hela sasa watoto wanasoma, na mimi
nimepona kabisa na nina kuku 6’, aliongeza.

Bi.Mery Paulo (74) mkazi wa kitongoji cha kawajense anasema hali yake ilikuwa duni sana lakini baada ya kuwezeshwa 40,000 za awali watoto wake 3 na wajukuu 2 waliokuwa wameacha shule sasa wanaenda wote na mmoja amekuwa wa kwanza darasani kati ya watoto 60.

‘Nyumba yangu ilikuwa ya nyasi sasa nimebadilisha nimeweka bati upande
mmoja nitamalizia upande mwingine kidogo kidogo nikipata hela
nyingine’, alisema Salome.

Kwa upande wake Mratibu wa Mradi wa TASAF Mkoa wa katavi Iginas Kikwala alisema kuwa mradi huu umewasaidia sana wananchi wengi kwani wengi wao walikuwa wanakula mlo mmoja tu kwa siku kutokana na kuishi maisha ya umaskini.

Alisema kuwa changamoto kubwa anayokumbana nayo kuwa ni baadhi ya
wananchi kuomba kuongezewa hela kwa msingi kwamba hela wanayopewa ni kidogo na kwamba wanashindwa kuigawa kwa chakula na kuanzisha miradi.

KUSAFIRI KUSIKUNYIME FURSA YA KUFANYA MAZOEZI

$
0
0

Na Jumia Travel Tanzania

Je, unapenda mazoezi? Umeshawahi kujikuta ukiwa njia panda ukijiuliza aidha usafiri au la, kwa kuhofia kutopata fursa ya kufanya mazoezi? Basi ondoa shaka kwani Jumia Travel inakujulisha kuwa hoteli zifuatazo zina sehemu na vifaa vya kisasa kwa ajili ya kufanyia mazoezi.    

Ledger Plaza Bahari Beach Hotel
Hii ni hoteli ya kisasa inayopatikana katika fukwe safi za mwambao wa bahari ya Hindi, Kunduchi jijini Dar es Salaam. Licha ya kuwa na huduma mbalimbali ambazo mteja atazihitaji akiwa pale, hoteli imezingatia uwepo wa sehemu ya kufanyia mazoezi iliyosheheni vifaa vya kisasa kabisa. Lengo ni kukidhi haja ya baadhi ya wateja ambao kwao mazoezi ni sehemu ya maisha yao. Hoteli ipo karibu na mji wa Bagamoyo ambapo ni mwendo wa takribani dakika 30 na pia itakuchukua dakika 10 kusafiri kwa kutumia boti kufika kisiwa cha Mbudya.   
Jangwani Sea Breeze Resort
Hoteli hii inapatikana Tanzania bara na inajivunia kuwa na mazingira rafiki kwa watoto. Hii ni kwa sababu wanaweza kwenda na wazazi wao huku wakipatiwa chumba chenye michezo mbalimbali kwa ajili yao. Ukiwa pale itakuchukua mwendo wa dakika 10 kwa boti kufika katika visiwa vya Mbudya na Bongoyo wakati kufika mji wa kihistoria wa Bagamoyo ni takribani dakika 40 tu. Hoteli hii nayo ina sehemu na vifaa vya kufanyia mazoezi, hivyo kuwatoa hofu wapenda mazoezi pindi wakiwa pale.
  

Harbour View Suites
Kama unapenda kufurahia mandhari nzuri ya katikati ya jiji la Dar es Salaam, Harbour View Suites itakuwa ni chaguo sahihi kwako. Hoteli hii ya kifahari yenye nyota nne ina sehemu yenye vifaa vya kutosha kwa ajili ya mazoezi, sehemu ya kuogelea pamoja na ‘kasino.’ Ni sehemu nzuri kufikia na kupumzika kama una shughuli za kibiashara katikati ya mji kwa sababu ipo karibu na ofisi muhimu pamoja na kumbi za mikutano.

Mermaids Cove Beach Resort & Spa
Mbali na huduma nzuri utakazozikuta pale, hoteli hii inayopatikana katika fukwe safi za Pwani ya Mashariki mwa visiwa vya Zanzibar, inazo shughuli mbalimbali za kukufanya uburudike. Ikiwa na chumba kilichotengenezwa maalumu kwa michezo mbalimbali pia ina sehemu ya kufanyia mazoezi. Kwa kuongezea ina ukumbi wa mikutano, sehemu ya kupumzika pamoja na duka kwa ajili ya manunuzi madogo madogo ukiwa hotelini. 
Hii inaweza kuwa changamoto kwa wamiliki wa hoteli kutakiwa kuzingatia kutengeneza sehemu ya mazoezi pamoja na kuweka vifaa vya kisasa. Kutokuwa na huduma hii licha ya kuwa na nyinginezo inaweza ikawa ni sababu ya wateja kutochagua kufikia kwenye hoteli yako.
Tembelea dream deals ili kujionea ofa kabambe za namna ya kwenda kufurahia huduma kwenye hoteli zilizoorodheshwa hapo juu pamoja na zifuatazo: Hotel White Sands: The Beach Resort, Golden Tulip Hotel na Ramada Resort za Dar es Salaam; Paradise Beach Resort na Golden Tulip Zanzibar Boutique Hotel za Visiwani Zanzibar; Nashera Hotel (Morogoro), Kwetu Hotel (Tanga); na Ngare Sero Mountain Lodge (Arusha)  


SELF LOVE AND GROWTH : AN OPEN LETTER

$
0
0
By Helena Nyerere

The one lesson that 2016 taught me was to appreciate the beauty of growth. It was Sunday morning, in Dar es Salaam, and it was the first Christmas I was spending alone.

I sat in my room and evaluated on the person that I had became during the past year. I didn’t like this person I was becoming, and neither did the people around me.

I was holding on to broken relationships, I constantly kept pointing out my failures, and I procrastinated on the simplest things. Believing in myself was something that started to become unfamiliar. That was the person I was before I accepted growth.

I was stuck in this world where I thought I had to settle, and where I thought being average was ok. But deep down I knew that person wasn’t me. I knew it was more to life than just being basic, and I wanted to be great! It was that very moment, when I realized that the lack of self love was keeping me from greatness.


And in order for me to be great, I needed to grow. I knew I had to love myself more so I can blossom and become who I was destined to be.

So I promised myself, I will no longer continue to be this person that I’m not. I promised myself I’ll go back to being the charismatic, social, smart, and witty Helena I once was. I promised myself that I’ll love me, even if no one would.

I promised myself that I’ll have faith in myself, just like the way God has faith in me. I promised myself I will leave anger, fear, insecurities, negativity, broken relationships, failures, and doubts all in 2016.

I promised myself that I would accept my flaws, be passionate about what I love, inspire others through my creativity, and break my people pleaser habits. I promised myself that I would only become greater with time, and I would never allow myself to go down that path again. And I did just THAT.

If you are reading this, then I challenge you to participate in the #SelfLove challenge and make promises to yourself, and live up to them. Try new things. DO whatever that makes YOU happy but do it without losing yourself.

Let go of negative relationships. Embrace your flaws. Break the people pleaser habits. Live for yourself. Inspire others. Love yourself the best way you know how!

Always remember that you are a gem, and you were put on this earth to be nothing but great! If anyone is getting in the way of your greatness, then push them out of your way and keep going.

Don’t let anyone tell you what you can and cannot do. No one knows you better than you know yourself. Accept growth, and gain self love. It will change your life forever.

SERIKALI ITAOKOA SH.BILIONI 900 KWA MWAKA ENDAPO IKIFANIKIWA KUTEKELEZA MKAKATI WA UWAZI KATIKA UJENZI NCHINI.

$
0
0
Kaimu Mtendaji Mkuu Baraza la Taifa la Ujenzi,Elias Kissamo akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa mchakato wa utoaji wa taarifa za miradi ya ujenzi wa miundombinu ya umma katika ukumbi wa Holiday Inn jijini Dar es Salaam jana.
Katibu Mkuu kutoka Ofisi ya Rais Ikulu,Peter Ilomo,akifungua mkutano wa mchakato wa utoaji wa taarifa za miradi ya ujenzi wa miundombinu ya umma katika ukumbi wa Holiday Inn jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Mwenyekiti wa Sekta ya Uwazi na Uwajibikaji katika Ujenzi (Cost Tanzania),Mhandisi Kazungu Magili na Kaimu Mtendaji Mkuu Baraza la Taifa la Ujenzi,Elias Kissamo. (PICHA NA ELISA SHUNDA)
Wadau wa masuala ya ujenzi wakifuatilia kwa umakini wakati mkutano huo ukiendelea.
Mwenyekiti wa Baraza la Ujenzi la Taifa (Cost Tanzania),Mhandisi Kazungu Magili,akizungumza katika mkutano huo. 
Katibu Mkuu kutoka Ofisi ya Rais Ikulu,Peter Ilomo akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Baraza la Taifa la Ujenzi Tanzania na wadau wa masuala ya ujenzi nchini.

NA MWANDISHI WETU

SERIKALI itaokoa angalau Sh.bilioni 900 kwa mwaka endapo itafanikiwa katika utekelezaji wa Mkakati Uwazi katika Ujenzi (CoST).

Aidha kupitia mkakati huo, miradi mbalimbali ya mashirika ya umma 10 inatarajiwa kufanyiwa tathmini itakayokamilika ifikapo Julai mwaka huu.

Akizungumza katika mkutano wa mashauriano ya utoaji wa taarifa za miradi ya ujenzi wa miundombinu ya umma wa baraza la wajenzi, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu, Peter Ilomo alisema kuwa mkakati huo utapunguza rushwa na upotevu wa fedha za Serikali.

Ilomo alisema CoST itaisaidia Serikali na umma kujua fedha zinavyotumika katika ujenzi wa miundombinu, kuokoa fedha za umma kwa kupunguza rushwa na kuboresha usimamiaji wa utekelezaji wa miundombinu.

Mwenyekiti wa CoST, Kazungu Magili alitaja mashirika yatakayofanyiwa tathmini na kuweka wazi miradi yake kuwa ni, Wakala wa Majengo (TBA), Wakala wa Barabara (Tanroads) na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)/.

Mashirika mengine ni mifuko wa Taifa wa hifadhi ya jamii ya NSSF, GEPF, LAPF, Wizara ya Elimu na Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii jinsia Wazee na Watoto na kutoa taarifa kwa umma ambapo utaweza kuitumia kufuatilia utekelezaji wa miradi husika.

Alisema kupitia tathmini hiyo, CoST itapata fursa ya kutambua majengo yaliyojengwa kwa mujibu wa vigezo ama chini ya kiwango halisi cha fedha zilizotolewa na thamani ya jengo husika.

Magili alisema ikitokea kuna baadhi ya miradi imejengwa chini ya kiwango itafikishwa katika mamlaka mbalimbali ikiwemo Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Mamlaka ya Manunuzi ya Umma (PPRA) na Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) ili hatua mbalimbali zichukuliwe.

Aidha alisema kuwa awali kabla ya kuanzishwa mkakati huo mambo mengi yalikuwa hayawekwi wazi hali ambayo imekuwa ikisababisha upotevu wa fedha.

Imeandaliwa na Mtandao wa www.elisashunda.blogspot.com mawasilianoelisashunda@gmail.com namba ya simu 0719976633.

HALMASHAURI YA WILAYA YA KISARAWE YATENGA KATA 10 KWA AJILI YA KILIMO CHA MKATABA

$
0
0
Mgeni rasmi katika uzinduzi wa mradi wa kilimo cha mkataba kupitia Taasisi ya Winamwanga Cultural Heritage Association kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, ambaye ni Ofisa Maendeleo ya Jamii, Wanchoke Chinchibera akihutubia wadau wa kilimo wa wilaya hiyo wakati wa semina ya siku moja iliyohusu kilimo cha mkataba iliyofanyika juzi wilayani humo. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa mradi huo, Mwajuma Motto, Ofisa Kilimo na Umwagiliaji wa wilaya hiyo, Elliot Mwasabwite na Mwenyekiti wa Bodi wa Taasisi hiyo, Esabela Luoga. 
Semina ikiendelea.
Meza kuu.
Mmoja wa maofisa wa Taasisi hiyo, Wilson Kibugu akitoa maelezo kwa wadau wa kilimo wa wilaya hiyo wakati wa semina hiyo ya siku moja iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa Wilaya hiyo.
Ofisa Utawala wa Taasisi hiyo, Fatma Shaib (kushoto), 
akisoma lisala.
Mgeni rasmi Wanchoke Chinchibera akipokea lisala kutoka kwa Ofisa Utawala wa Taasisi hiyo, Fatma Shaib.
Mratibu Mradi wa Kilimo wa Taasisi ya Winamwnga Cultural Heritage Association, Saidi Simkonda (katikati), akitoa mada katika uzinduzi wa mafunzo ya kilimo hai na mafunzo ya ufugaji wa kuku chotara na mafunzo ya utunzaji wa mazingira yaliyofanyika wilayani Kisarawe mkoani Pwani juzi. 
Ofisa Mauzo wa Kampuni ya Syngeta Tanzania Limited, John Ngoma akielezea ubora wa mbegu aina ya Sy 514 inayosambazwa na kampuni hiyo kupitia miradi ya kilimo ya taasisi hiyo.
Mkurugenzi wa Mradi wa kilimo wa Taasisi ya Winamwnga Cultural Heritage Association, Mwajuma Motto (katikati), akizungumza katika uzinduzi wa mafunzo ya kilimo hai na mafunzo ya ufugaji wa kuku chotara na mafunzo ya utunzaji wa mazingira kwa kutumia vikundi vya ufugaji wa nyuki yaliyofanyika wilayani Kisarawe mkoani Pwani jana. Kulia ni Mwezeshaji, Filbert Luoga na kushoto ni mratibu wa miradi wa taasisi hiyo, Saidi Simkonda. 
Ofisa Kilimo na Umwagiliaji wa wilaya hiyo, Elliot Mwasabwite akichangia jambo kwenye semina hiyo.

Dotto Mwaibale, Kisarawe

HALMASHAURI ya Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani imetenga Kata 10 kwa ajili ya kilimo cha mkataba kitakachoendeshwa na Taasisi ya Winamwanga Cultural Heritage Association.

Mratibu wa mradi huo kutoka taasisi hiyo, Saidi Simkonda akizungumza juzi katika uzinduzi wa mafunzo ya kilimo hai na mafunzo ya ufugaji wa kuku chotara na mafunzo ya utunzaji wa mazingira kwa kutumia vikundi vya ufugaji wa nyuki yaliyofanyika wilayani humo juzi alisema mradi huo umelenga kuwainua kiuchumi wananchi wa Kisarawe na Mkoa wa Pwani kiujumla.

Alisema taasisi hiyo imepanga kuanzisha vikundi vya kuweka na kukopa ili kuinua uchumi wa wananchi kupitia vikundi vya ujasiriamali wa kilimo hai na ufugaji wa kuku chotara pamoja na kuwawezesha kupata fursa za mikopo katika asasi za kifedha zilizopo wilayani humo.

"Taasisi yetu imejipanga kuanzisha kilimo cha mkataba ambapo mazao yatakayopatikana itayanunua na tayari serikali ya Kijiji cha Kuluwi imetoa ghala la kuhifadhia mazao hayo.

Mgeni rasmi katika uzinduzi wa mradi huo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmshauri hiyo ambaye ni Ofisa Maendeleo ya Jamii, Wanchoke Chinchibera alisema mradi huo utawasaidia wananchi na kuwa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe imetenga kata kadhaa kwa ajili ya mradi huo ambazo ni Maluwi, Vikumburu, Kuluwi na Mafizi.

Alisema kwa sababu mradi huo ni mpya katika wilaya yao na utafanya shughuli zake kwa kilimo cha mkataba aliishauri taasisi hiyo kujenga ushirikiano mkubwa na wananchi kupitia vikundi ambavyo tayari vimesajili na majina yake kuwepo katika daftari ofisini kwa mkurugenzi wa halmshauri hiyo.

(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

MADARASA YA KISWAHILI DMV YANAENDELEA KILA SIKU YA JUMAMOSI

$
0
0
Kwa watu wote kuanzia umri wa miaka 5 Na kuendelea.

Anuani: 4600 Powder mill Rd,
Suite 450Q,
Beltsville, MD 20705

Muda: Saa 8 mchana - 10 Jioni
Siku: Kila Jumamosi

Mwalimu Aunty Jasmine Lubama akiwafundisha watoto wa darasa la Kiswahili DMV siku ya Jumamosi Silver Spring kwenye darasa hilo abalo limeanzishwa tena mapema mwaka huu.
Kushoto ni Mwalimu wa darasa la Kiswahili dada Asha Nyang;anyi akiwapa somo watoto wa darasa hilo sikuya Jumamosi Silver Spring, Maryland.
Wanafunzi wa darasa la Kiswahili wakijielezea kwa lugha hiyo.
Wanafunzi wakiendelea na kujieleza kwa Kiswahili
Wanafunzi wa darasa la Kiswahili DMV wakimsikiliza mwenzao (hayupo pichani)
Wanafunzi wa darasa la Kiswahili DMV wakiwa darasani.

WABONGO NIGHT FREE NO COVER CHARGE LEO IJUMAA

$
0
0
kiota kipya Crystal under new management mama safari is back msosi kama safari, njoo uvunje mifupa kungali meno iko.Fika utikise kichwa, urushe mikono na kujiachia huku ukipata muziki kutoka kwa madj wako wakaree DMV Dj Moe na Dj Dave leo Ijumaa Feb 3 na kila siku ya Ijumaa CRYSTAL LOUNGE club inayolingana na hadhi yako anuani ni 1401 University Blvd, Hyattsville, MD 20783 KaRiBu

Kichupa cha leo BEAZI - LIAR LIAR REMIX | [Official Music Video] | MoStack - Liar Liar |...

TANZANIAN SOCIAL EVENING. AN EVENING FULL OF ADVENTURE AND CULTURE.

$
0
0

Justa found wa Curious on Tanzania na ndiyo mwandaaji wa shughuri hii na kuwakaribisha watu mbali mbali kuwatangazia mazuri juu ya  utalii wa nchi yetu Tanzania. Justa ni Mtanzania mwenye makazi yake New York ndiyo C.E.O na found wa Curious on Tanzania kampuni inayojishughurisha na mambo ya utalii na utamaduni unaopatikana ndani ya Tanzania.

Wageni waalikwa wakisikiliza hotuba fupi kutoka kwa Justa Found wa Curious on Tanzania hapa akiwambia historia ya Tanzania na vivutio vya utalii pale watakavyotumia pata nafasi ya kutumia kampuni yake kwa safari.


KokuGonza akitumbuiza wageni waalikwa ukumbuni hapo


Kulikuwa na vitafunwa vya Kitanzania vilivyoandaliwa na mpishi mkuu James Lupembe, kwa picha zaidi nenda read more.

MAGARI MANNE YAGONGANA BARABARA YA NYERERE ENEO LA MTAVA JIJINI DAR ES SALAAM NA KUMJERUHI DEREVA TEKSI

$
0
0
 Wananchi wakimuangalia dereva wa teksi aliyejeruhiwa baada ya gari lake lenye namba za usajili T 625 AWS kugongana na gari dogo lenye namba usajili T 214 CFX wakati likiingia barabara ya Nyerere likitokea Jengo la Kibiashara la Quality Centre Dar es Salaam leo asubuhi.
 Mwonekano wa Teksi hiyo namba T 625 baada ya kugongana.
 Wananchi wakiangalia ajali hiyo.
 Wananchi wakiangalia gari dogo aina ya Toyota Corolla lenye namba T 214 CFX baada ya kuyagonga magari namba T 741 DEK na T 596 BCG katika eneo hilo la Mtava.
 Askari wa Usalama Barabarani akipima ajali hiyo.
 Gari dogo aina ya Toyota Corolla lenye namba T 214 CFX likiwa eneo la ajali kabla ya kuondolewa.

Na Dotto Mwaibale
DEREVA wa gari dogo teksi yenye namba za usajili T 625 AWS amenusurika kufa baada ya gari lake alilokuwa akiliendesha kutoka mjini akielekea Uwanja wa Ndege kugongana na gari dogo lenye namba T 214 CFX aina ya Corolla lililokuwa likiingia Barabara ya Nyerere likitokea Jengo la Biashara la Quality Centre eneo la Mtava jijini Dar es Salaam leo asubuhi.

Mashuhuda wa ajali hiyo wakizungumza na waandishi wa habari eneo la ajali walisema ajali hiyo ilisababishwa na gari hilo dogo aina ya Corolla lililokuwa likiingia barabara ya Nyerere bila kuchukua tahadhari.

"Chanzo cha ajali hii ni gari hilo dogo aina ya corolla ambalo liliingia barabara ya Nyerere bila ya dereva wake kuchukua tahadhari na kama dereva wa gari namba T 625 AWS angekuwa katika mwendo wa kawaida madhara yake yasingekuwa makubwa kiasi hicho" alisema shuhuda aliyejitambulisha kwa jina la Mlugulu.

Mlugulu alisema baada ya magari hayo kugongana gari hilo aina ya Corolla liligeuka na kwenda kuyagonga magari mengine namba T 596 BCG na T 741 DEK yaliyokuwa yamesimama yakisubiri kuingia upande ambao lipo Jengo la Kibiashara la Quality Centre.

Katika ajali hiyo gari namba T 625 AWS liliacha njia na kuhamia upande wa pili wa barabara ya kutoka Tazara kwenda mjini.

Baada ya ajali askari wa usalama barabarani walifika na kupima ajali hiyo na kuchukua maelezo ya madereva wote wanne ambapo magari mawili T 214 CFX na T 625 AWS yakiondolewa na  magari ya kukokota magari mabovu (Breck Down) na kupelekwa kituo cha Polisi cha Chang'ombe Temeke jijini Dar es Salaam kwa hatua zingine za kisheria.

MISA TANZANIA YAWAKUTANISHA WABUNGE NA WANAHABARI KUJADILI NAMNA NZURI YA KUSHIRIKIANA

$
0
0

Mhariri Mtendaji wa The Guardian Ltd, Jesse Kwayu akiwasilisha mada kuhusu namna ya kufanya mahusiano ya kikazi kati ya bunge na wanahabari kwa baadhi ya wabunge, wahariri na waandishi wa habari katika ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma. Picha na Geofrey Adroph

 Afisa Habari na Utafiti wa MISA-Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa akizungumza jambo mbele ya baadhi ya  wabunge pamoja na baadhi ya wahariri na waandishi wa habari waliofika katika semina ili kujadili jinsi ya kutengeneza mahusiano ya kikazi kati ya Bunge na wanahabari yatakayoleta ukaribu kwa pande zote.




Baadhi ya wabunge wakichangia mada kuhusu kutengeneza mahusiano ya kikazi kati ya Bunge(wabunge) na wanahabari pamoja na kutoa maoni yao ili kuboresha utoaji wa habari kwa wananchi boila kujali itikadiza kivyama.

Mhariri Mtendaji wa The Guardian Ltd, Jesse Kwayu akijibu maswali kutoka kwa wabunge katika mkutano uliowakutanisha wabunge, wahariri na waabdishi wa habari katika ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma leo.
 Mhariri mtendaji wa Jamhuri Media, Deodatus Balile akitolea ufafanuzi baadhi ya maswali yaliyoulizwa na waandishi pamoja na wabunge walioudhuria mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Hazina ndogo mjini Dodoma. 
 Mmoja wa waandishi wa habari akitoa changamoto anazozipata kwenye kazi zake za kila siku za kuripoti habari mbalimbali

Baadhi ya wabunge, wahariri na waandishi wa habari wakiwakwenye mkutano 


Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania kwa kushirikiana na Wakfu wa Taasisi Huru za Uwazi Afrika (OSIEA) wamewakutanisha  wabunge pamoja na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma. Mkutano huu ulikuwa na lengo la kuwajengea Wabunge na Wanahabari uhusiano mzuri katika utendaji wao wa kazi. Bunge na Vyombo vya Habari ni Mihimili miwili ya dola (Mmoja ukiwa Rasmi na mwingine usio Rasmi) inayotegemeana sana katika utendaji wake wa kazi.

Kutokana na kazi kubwa ya Bunge ambayo ni kutunga sheria na kuwakilisha Umma katika mijadala mbalimbali ya maendeleo katika ngazi za Taifa na Jimbo lazima kutumia vyombo vya Habari kwenye kazi ya kutafsiri mipango na mikakati mbalimbali inayofanywa na Bunge katika lugha ambayo mpiga kura/mwananchi wa kawaida anaweza kuelewa. Lengo kuu likiwa ni kuharakisha maendeleo ya mtu mmoja mmoja na jamii nzima.

Katika siku za karibuni kumetokea changamoto mbalimbali katika utendaji kazi wa muhimili huu rasmi na muhimili huu usiokuwa rasmi, na hasa kutoaminiana na kushutumiana kwa namna moja ama nyingine. Kutokana na changamoto hizo hakuna budi kwawaandishi wa habari paamoja ili kujadili changamoto na kuja na suluhisho la changamoto hizo.



Semina hiyo imeshirikisha watu 55 ikiwa ni pamoja na wabunge mbalimbali toka vyama vyote, Wahariri wa vyombo Habari vilivyoko Dodoma na Bureau Chiefs wa vyombo vya Umma na Binafsi vilivyopo Dodoma.

HALMASHAURI YA NSIMBO YAJIPANGA KUKOMESHA MIMBA ZA UTOTONI

$
0
0
Na Mussa Mbeho, Katavi

HALMASHAURI ya wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi imeanza kuweka mikakati thabiti itayosaidia kukomesha na kutokomeza mimba za utotoni kwa wanafunzi  wa shule za msingi na sekondari  ili kuweza kuwasaidia kusoma na kufikia malengo yao.

Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili ofisini kwake Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo  Mairwa Pangani alisema Kuwa kwa sasa  wamedhamiria kukomesha vitendo vya mimba mashuleni   kwa kuweka mikakati mikali  kwa walimu,wazazi na wanafunzi wenyewe.

Alisema kuanzia sasa wale wote watakaobainika kuwapa ujauzito  wanafunzi watakamatwa mara moja na kukabidhiwa kwa vyombo vya dola kwa ajili ya kufikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.

Alibainisha mikakati iliyowekwa na halmashauri  hiyo kuwa ni kuhakikisha zoezi la upimaji ujauzito linafanyika mara kwa mara  kwa mabinti wa shule za msingi na sekondari huku akiwataka  walimu wa shule zote kutoa ushirikiano wakati wa zoezi hilo.


Pangani  alisema  wataendelea  kushirikianas na  wadau wa elimu wilayani humo wakiwemo wazazi na walezi wa watoto hao ili kuweka mikakati ya pamoja itakayosaidia kudhibiti vitendo hivyo hata wakiwa nyumbani ili kuwasaidia waweze kusoma na kufikia malengo yao.

Aidha Pangani alibainisha kuwa walimu wote watatakiwa kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwa wammafumzi wanaoishi katika shule zenye  mabweni ili kuhakikisha hakuna mwanafunzi anaeweza kulala nje kwa lengo la kudhibiti tatizo la mimba katika halmashuri hiyo

Pangani Alifafanua mkakati mwingine kuwa ni kuhakikisha walimu wanawajengea hali ya ujasiri na kujiamini wanafunzi wao ili kuondokana na woga wa kukubali udanganyifu wa wanaume huku akikisitiza vipindi vya dini kutiliwa mkazo katika shule zote ili kuwajengea imani sambamba na kuwa na hofu ya Mungu.

Aidha aliwataka walimu wakuu  na wakuu wa shule za msingi na sekondari  kuhakikisha wanawabana  walimu wa madarasa katika kufuatilia mienendo ya wanafunzi wao na kubainisha taarifa za kila mwanafunzi kwa kila muhula huku mkuu wa shule akitakiwa kuwa na njia mbadala ya kupata taarifa za wanafunzi kutoka kwa wazazi moja kwa moja.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Rafael Kalinga aliwataka Madiwani, Watendaji na Watumishi wote wa halmashauri hiyo kutoa ushirikiano wa  hali ya juu utakaosaidia kutiwa mbaroni wanaume wote wanaorubuni wanafunzi ikiwemo wazazi watakaoozesha watoto wao wa kike walio chini ya miaka 18.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya  ya Mpanda Bi Lilian Matinga ambae anasimia halmshauri hiyo  ametoa onyo kali kwa walimu wote watakaobainika kujihusisha na vitendo vya kurubuni wanafunzi wao wa kike ili wafanye nao mapenzi huku akisema kuwa  hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Viewing all 45933 articles
Browse latest View live