Quantcast
Channel: VIJIMAMBO
Viewing all 45933 articles
Browse latest View live

Burkina Faso vs Egypt 1:1 (3-4) 2017 - All Penalty Shotoout RESUME ( CAN...


Mtazame Mhe Ridhiwani Kikwete akipinga kitendo cha Diamond kukabidhiwa b...

Kiongozi wa upinzani Kongo afariki

$
0
0
  File Photo
Mwananchi
Brussels.Kiongozi mkongwe wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Etienne Tshisekedi amefariki dunia usiku huu nchini Ubelgiji.

Tshisekedi amefariki akiwa na umri wa miaka 84 aliekea nchini humo kwa matibabu ya kiafya kwa mujibu wa chombo cha habari cha AFP.

Chombo hicho cha habari kiliongezea kuwa hatua hiyo inajiri wakati ambapo chama chake kinaendelea na mazungumzo ya kugawana mamlaka kufuatia hatua ya Rais Laurent Kabila kukataa kujiuzulu baada ya muda wake wa kumalizika kukamilika mwezi uliopita.

Harakati za Tshisekedi kama mwanasiasa wa upinzani zilianza tangu nchi hiyo kujinyakulia uhuru kwani ndiye mmoja wa wachache tu waliothubutu kumkosoa hata Rais Mobutu Sese Seko wakati wa utawala wake uliokuwa umepiga marufuku vyama vya kisiasa vya upinzani.

MAGAZETI YA LEO FEBRUARY 02, 2017

VIDEO: RIDHIWANI KIKWETE AFAFANUA KWANINI ILIKUWA NI AIBU KWA TFF NA WAZIRI, DIAMOND KUKABIDHIWA BENDERA KWENDA GABON

$
0
0
Ridhiwani Kikwete aliingia kwenye headlines mwanzoni mwa mwezi uliopita pale alipoandika post Instagram akisikitishwa na kitendo cha Diamond kukabidhiwa bendera na Waziri wa michezo, Nape Nnauye kwenda kutumbuiza kwenye ufunguzi wa kombe la mataifa ya Afrika, nchini Gabon.

Mbunge huyo wa Chalinze, amedai kuwa, post yake haikumlenga Diamond, bali aliwapa ujumbe shirikisho la soka Tanzania, TFF na Waziri Nape.

“Kilichonifanya niandike ile meseji ni baada ya kuona kwamba mashindano yanayoenda kufanyika ni ya mpira wa miguu, sisi tunayo timu ya taifa ya mpira wa miguu, lakini to our surprise, badala ya kutoa bendera kwa timu ya mpira wa miguu, tunawapa waburudishaji kwa maana ya wanamuziki kama Diamond,”
Ridhiwani alisema kwenye mahojiano na The Beauty TV.

“Matarajio yetu sisi ni kumuona kapteni wa taifa ndiye anayepokea bendera na sio wanamuziki,” ameongeza. “Pia watu wa TFF, kwamba nao wanashangilia yale anayoyafanya waziri?” Hivi vitu lazima tuwe serious.”
“Diamond yeye nampongeza sana, kwa hatua aliyofika, anafanya kazi nzuri, na ndio maana watu wamemuona, wamempa nafasi ya kwenda kutumbuiza ambayo sisi kama watanzania we feel proud. Lakini the bottom line ni kwamba, nini agenda kubwa inayomfanya Diamond aende Gabon? Ni mpira wa miguu, Diamond si mchezaji wa mpira wa miguu, hata kama labda anashabikia mpira wa miguu, lakini yeye ni mshabiki tu, wanaoenda kushiriki pale ni wachezaji.”
Ridhiwani amekiri kuwa kitendo hicho kilimsikitisha na ndio maana hakupenda kukaa kimya.
“Si kwamba sikupenda kwasababu amepewa Diamond, hapana, sikupenda kwa sababu, matarajio ya mimi mpenzi wa mpira ni kumuona kapteni wangu wa timu ya taifa anapokea bendera kwa niaba ya watanzania wote, anakwenda kutuwakilisha kule, hata kama tutashindwa, hata kama tutafanikiwa lakini anayetakiwa kwenda kule ni kapteni wa timu ya mpira wa miguu kwenda kutuwakilisha kama taifa na si vingine.”

Kiongozi wa upinzani Kongo afariki

$
0
0
Kiongozi mkongwe wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Etienne Tshisekedi amefariki dunia usiku huu nchini Ubelgiji.
Tshisekedi amefariki akiwa na umri wa miaka 84 aliekea nchini humo kwa matibabu ya kiafya kwa mujibu wa chombo cha habari cha AFP.
Chombo hicho cha habari kiliongezea kuwa hatua hiyo inajiri wakati ambapo chama chake kinaendelea na mazungumzo ya kugawana mamlaka kufuatia hatua ya Rais Laurent Kabila kukataa kujiuzulu baada ya muda wake wa kumalizika kukamilika mwezi uliopita.
Harakati za Tshisekedi kama mwanasiasa wa upinzani zilianza tangu nchi hiyo kujinyakulia uhuru kwani ndiye mmoja wa wachache tu waliothubutu kumkosoa hata Rais Mobutu Sese Seko wakati wa utawala wake uliokuwa umepiga marufuku vyama vya kisiasa vya upinzani.

MKUU WA MKOA AMGOMEA WAZIRI MAGHEMBE

$
0
0
Uamuzi uliofanywa wiki iliyopita na Waziri wa Maliasili na Utalii, Professa Jumanne Maghembe wa kuagiza kuendelea mchakato wa kulitenga eneo la pori tengefu la Loliondo umepingwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.

Badala yake, RC Gambo ameagiza Kamati ya wataalamu iliyoundwa kwa maelekezo ya Waziri Mkuu, Khasimu Majaliwa inayochunguza chanzo cha mgogoro wa Loliondo iendelee na kazi iliyopewa na hatimaye itoe mapendekezo yake ya namna ya kumaliza mgogoro huo uliodumu kwa miongo miwili.

Gumbo alikuwa akizungumza jana katika mkutano wa wadau wa vyombo vya habari   katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC).

Alisema hakuna kiongozi yeyote mwenye mamlaka ya kukosoa au kusimamisha maagizo ya Waziri Mkuu isipokuwa Makamu wa Rais na Rais. 


RC Gumbo alionekana dhahiri kuwa amekerwa na kukasirishwa na uamuzi wa Waziri Maghembe wa kufanya ziara ya kushtukiza katika eneo la Loliondo na   kutoa maagizo ya kugawa eneo la kilometa za mraba 1500  kuokoa Hifadhi ya Serengeti.

Alisema uamuzi uliotolewa na waziri  huyo ni ushauri kwa kamati yake na jambo linalozusha sintofahamu juu ya mwenye mamlaka zaidi kati ya Waziri na Mkuu wa Mkoa . 

“Hakuna kiongozi mwingine yeyote mwenye kukosoa maagizo au maelekezo ya Waziri Mkuu isipokuwa Makamu wa Rais na Rais.

“Sisi kauli ya waziri tunaichukulia kama ushauri ambao unaweza kutolewa na mwananchi yeyote, ” alisema.

Alisema ni lazima kamati ya wataalamu aliyoundwa ikamilishe kazi yake ikiwa ni pamoja na kujiridhisha kuhusu mipaka, vyanzo vya maji, maeneo ya ufugaji, uhifadhi, mipaka ya vijiji na hatimaye  kuwasilisha mapendekezo yake serikalini   yafanyiwe kazi na si vinginevyo.

Mkuu huyo wa Mkoa alishangazwa na uelewa na umakini wa Wizara ya Maliasili na Utalii katika kulitambua na kufuatilia eneo la pori tengefu.

RC Gumbo alisema inaelekea  wataalamu wa wizara hawana uelewa wowote kuhusu kinachoendelea Loliondo.

“Wizara inazungumzia pori tengefu lakini tayari kuna mji pale, hata eneo la kilometa za mraba 1500 wanazosema tumewauliza inaanzia wapi na kuishia wapi hawajui.

"Hata aliyechora ramani naye hajui mipaka ndiyo maana nasema tuache kamati imalize kazi yake," alisema.

WAZIRI MKUU AJIBU MASWALI YA PAPO KWA PAPO BUNGENI MJINI DODOMA

$
0
0

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijibu maswali ya papo kwa papo, bungeni mjini Dodoma Februari 2, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe wakati alipouliza swali katika kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu, Bungeni mjini Dodoma Februari 2, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Wema atajwa kuhusika na dawa za kulevya

$
0
0

 Msanii wa filamu nchini Wema Sepetu ametajwa kuwa ni kati ya wasanii ambao wanatumia dawa za kulevya hivyo anapaswa kesho kukutana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda katika kituo cha polisi.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaama amewataja wasanii wengine akiwepo TID, Chid Benz, pamoja na Recho na kusema anahitaji kesho wafike makao makuu ya kituo cha polisi.

"Naomba tukutane kesho pale polisi Central akiwepo TID, akiwemo Wema Sepetu, wakiwepo wakina Junior Sniper, wakina Ditto, Titoo, kuna Ally Denya, kuna wakina Chacha, kuna kina Mecky wengine hawa wakina Petit Man tayari nishawatia mikononi mwa sheria, kuna watu kama kina Recho, Chid Benz wote hawa nawahitaji ni vijana wenzangu nafikiri tutaelewana vizuri" alisema Paul Makonda

VIDEO: MAKONDA AWAANIKA WANAOTUMIA NA KUFANYA BIASHARA HIYO, WAKO WASANII NA ASKARI 9

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewataja askari 9 wanaotuhumiwa kushirikiana na wafanya biashara ya madawa ya kulevya.
Aidha amewataja wasanii wanaojihusisha na matumizi na uuzaji wa Madawa ya kulevya na kuwataka kuripoti kituo cha polisi kesho.
Akiongea na waandishi wa habari akiwa ofisini kwake Alhamisi hii, RC Makonda amewataka wauzaji wote kufika makao makuu ya polisi kwajili ya kujieleza.

“Nimeamua kuingia kwenye hii vita kwa sababu najua siku moja Mungu ataniuliza, nilikupa mkoa wa Dar es salaam kupitia Rais John Pombe Magufuli watoto waliangamia kwa Madawa ya kulevya, sitaki kufika mbungini nisiwe na jibu, nipo tayari kupoteza ukuu wangu wa mkoa, nipo tayari kutangulia kwa aliyeniumba lakini niwe na jibu kwa mungu wangu aliyeniumba kwamba Madawa ya kulevya hayakubaliki ndani ya Dar es salaam,” alisema Makonda.
Aliongeza,’Wapo tuliowakamata pamoja na dawa zao tumeshawafikisha Central Polisi na wanaendelea na mambo yanayotakiwa. Lakini wapo ambao bado, majina ni mengi sana mtayapitia wenyewe, kuna Mchafu, Director Joan, Mirror, Rommy na wengine wengi, wapo wauzaji wadogo na wengine wakubwa. Lakini wapo wengine wanasemekana wanatumia lakini hakuna ushahidi kwamba wanatumia ingiwa wenzao wanasema wanatumia, ni bora nikakutana nao kesho pale Central, akiwemo TID, Wema Sepetu,”


List ya watuhumiwa

RC Makonda amewataja wanaotuhumiwa kutumiwa dawa za kulevya wakiwemo TID, Wema Sepetu, Chid Benz, Recho, amewataka kesho wakutane polisi

Kuna maeneo watu wanatuambia madawa ya kulevya wanayapata sehemu hizo, wamiliki wake kesho niwakute polisi, wasipokuja nitawafuata - RC Makonda

Kama unajua una eneo unafanya biashara za dawa za kulevya DSM natoa siku 7 biashara hii iishe, operesheni hii naiongoza mwenyewe - RC Makonda

Kama Kamishna Sirro na timu yake watashindwa kutokomeza dawa za kulevya DSM maana yake wamekosa sifa za kuendelea kuwa askari - RC Makonda

Watano tayari nimeshawakamata na wengine nimewakamata wakiwa na dawa za kulevya - RC Makonda


RAIS MAGUFULI AZINDUA MWAKA MPYA WA KIMAHAKAMA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea  na Kaimu Jaji Mkuu wa  Tanzania Profesa Ibrahim Hamisi Juma  wakati wa uzinduzi wa Mwaka Mpya wa Kimahakama katika viwanja vya Mahakama vya Mtaaa wa Chimala Ocean Road jijini Dar es salaam leo February 2, 2017
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamisi Juma  akihutubia wakati wa uzinduzi wa Mwaka Mpya wa Kimahakama katika viwanja vya Mahakama vya Mtaaa wa Chimala Ocean Road jijini Dar es salaam leo February 2, 2017 wakati wa uzinduzi wa Mwaka Mpya wa Kimahakama katika viwanja vya Mahakama vya Mtaaa wa Chimala Ocean Road jijini Dar es salaam leo February 2, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akihutubia wakati  wa uzinduzi wa Mwaka Mpya wa Kimahakama katika viwanja vya Mahakama vya Mtaaa wa Chimala Ocean Road jijini Dar es salaam leo February 2, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli  akipokea ripoti ya mahakama kuhusu kesi za uchaguzi kutoka kwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamisi Juma  wakati wa uzinduzi wa Mwaka Mpya wa Kimahakama katika viwanja vya Mahakama vya Mtaaa wa Chimala Ocean Road jijini Dar es salaam leo February 2, 2017. Kulia ni Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli  akikabidhi kwa Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai  ripoti ya mahakama kuhusu kesi za  uchaguzi wakati wa uzinduzi wa Mwaka Mpya wa Kimahakama katika viwanja vya Mahakama vya Mtaaa wa Chimala Ocean Road jijini Dar es salaam leo February 2, 2017. Kulia ni Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai

RAIS DKT MAGUFULI ATEUA MKUU WA MAJESHI NA MNADHIMU MKUU

$
0
0
Luteni Jenerali Venance Mabeyo ambaye ameteuliwa na Rais Dkt Magufuli kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania

WANA USALAMA WA CUF YA PROFESA LIPUMBA WATOA ONYO KALI KWA WANAOTAKA KUKIHUJUMU CHAMA HICHO

$
0
0
 Mkurugenzi wa Usalama wa Chama cha Wananchi (CUF), Masoud Mhina, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana, kuhusu madai ya hujuma zinazopangwa kufanywa dhidi ya chama hicho. Kushoto ni Ofisa  Dawati wa CUF, Awadhi Mdoe.
 Ofisa  Dawati wa CUF, Awadhi Mdoe, akizungumza katika mkutano huo. Kutoka kulia ni Naibu Kamanda wa Blue Gurd, Wilaya ya Kinondoni,  Mohamed Kiotola, Mkurugenzi wa Haki za Binadamu, Zainabu Mdolwa, Mkurugenzi wa Usalama wa Chama cha Wananchi (CUF), Masoud Mhina na Mkurugenzi wa Blue Gurd wa Wilaya ya Temeke, Saidi Mtumbwe.
Wafuasi wa chama hicho wakiwa kwenye mkutano huo.

Wahe,Waandishi wa Habari,nimewaiteni hapa leo kwa ajili ya kuwapa Taarifa za hujuma zinazopangwa kufanywa dhidi ya chama chetu.

Kama mnavyofahamu kwamba,Chama chetu kiko katika sintofahamu ya Mgogoro wa Kiuongozi.


Hata hivyo pampja na hali hiyo kuwepo,tunaimani kwamba,sintofahamu hii ya Kiuongozi tutaumaliza wana CUF wenyewe.


Mara nyingi huwa siyo kawaida yangu kusimama hadharani kuzungumzia hali ya chama kupitia Vyombo vyenu vya habari,lakini kwa hali ilivyo nimewajibika kutokeza hadharani kuzungumza nanyi.


Kwa mujibu wa Katiba ya CUF Ibara ya 88 (2)   Nanukuu.Katibu wa Kamati ya Ulinzi na Usalama atakuwa na wajibu Ufuatao,Mwisho wa kunukuu.


Ibara ya  88 (2) (a) Atakuwa Mtendaji Mkuu wa Kamati ya Ulinzi na      Usalama ya Chama Ibara ya 87 (1)Wajibu wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Taifa ni kuhakikisha Usalama wa Chama Nchini kote


Nimeona ninukuu vifungu hivi vya Katiba ya CUF ili kuweka sawa uhalali wangu katika kutoa Taarifa hii kwenu ninyi Waandishi wa Habari.


Tunazo Taarifa kwamba,Katibu Mkuu wetu anafanya Vikao mbalimbali na Viongozi wa Chadema vyenye muelekeo wa kuhujumu harakati za chama chetu  pamoja na baadhi ya Viongozi wa CUF upande wa Tanzania Bara.


Napenda kuchukua fursa hii kumsihi Katibu Mkuu wa Chama changu,Mhe,Maalim Seif,kwamba aache kufanya hivyo kwani vikao hivyo havina tija kwake ziadi ya kujenga Uhasama dhidi ya Wanachama na Viongozi wa CUF wa Bara na Zanzibar.


Nimshauri Katibu Mkuu wangu kwamba,Viongozi wa Chadema anaowatumainia kama ndiyo wataweza kumsaidia katika dhamira zake,atakuwa anapoteza muda wake bure.


Tunazo Taarifa kwamba kuna Vijana wanaandaliwa kuja kuvamia Ofisi Kuu za CUF Buguruni  kwa ajili ya kufanya Uharibifu wa Mali za Chama.


Nichukue fursa hii pia kutoa ONYO KALI kwamba Vijana hao wasithubutu wala kujaribu kufanya kitu kama hicho kwani Ulinzi wa Chama umejipanga vyema kukabiliana vikali na Kikundi chochote ambacho kina dhamira ya kufanya hujuma yeyote dhidi ya chama chetu cha CUF.


Kuhusu kuwafanyia hujuma baadhi ya Viongozi wa Chama chetu,tunawaambia kwamba,wote wanaotaka kufanya Vitendo hivyo tunawajua mmoja mmoja na anapoishi,ila kwa sababu maalum,sitoweza kuwataja kwa sasa,lakini kwa kuwa,chama chetu kinafanya kazi kwa mujibu wa sheria za Nchi,Tayari tumevitaarifu Vyombo vya Ulinzi na Usalama vya Serikali juu ya Vitisho ya vitendo dhalimu vinavyokusudiwa kufanywa na Wasaliti wa Chama chetu dhidi ya Viongozi wetu wa Chama upande wa Tanzania Bara.


Lakini pia napenda kuchukua fursa hii kutoa Onyo pia kwa wale wanaojiita ni Viongozi wa CUF halafu wanazungumzia Uchochoroni na kuwatukana Viongozi halali wa Chama cha CUF,kwamba waache mara moja,tumewavumilia sana kiasi cha kutosha sasa dawa yao iko jikoni mmoja mmoja baada ya mwingine tutawajibika nao.


Waheshimiwa Wanahabari nawashukuru,asanteni sana kwa kunisikiliza.


HAKI SAWA KWA WOTE

Masoud Omar Mhina
MKURUGENZI WA ULINZI NA USALAMA CUF TAIFA.

VIDEO: MWANAMKE AZUA TAFRANI MBELE YA RAIS DKT MAGUFULI

$
0
0
Leo katika uzinduzi wa mwaka mpya wa kimahakama jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Rais Dkt John Pombe Magufuli. Rais Magufuli alizungumza mambo mengi ambapo alipongeza Mahakama kwa kufanya kazi nzuri ya kutatua kesi mbalimbali kwa mwaka mmoja uliopita. 

Aidha, Rais Dkt Magufuli alielezea baadhi ya changamoto zinazokabili muhimili wa mahakama ambapo alisema kuwa tatizo la rushwa limekuwa likisababisha kukosekana kwa haki kwa atu wanyonge huku kesi nyingine zikicheleweshwa kwa makusudi. Rais Dkt Magufuli amewataka watumishi wa mahakama kuhakikisha wanatoa huduma bila upendeleo.

Baada ya kuzungumza huko, tafrani kubwa ilizuka baada ya mama mmoja kunyanyuka akiwa na kitambaa kilichoandikwa jumbe mbalimbali kuelekea kwa Rais akionyesha kudhulumiwa haki yake huku mahakama na polisi wakihusika.

Hapa chini ni video ya tukio hilo;

HAPPY BIRTHDAY

$
0
0
OLIVIA ANDREW WA NEW JERSEY!
Timu ya Vijimamboblog na wadu wake wanakutakia kheri ya siku yako ya kuzaliwa.


Mama mjane aliyeliza watu mbele ya Rais Magufuli afunguka mengine

MAGAZETI YA LEO FEBRUARY 03, 2017

TIMU YA WANAHABARI IRINGA YAPIGWA JEKI NA MBUNGE RITTA KABATI

$
0
0
Mbunge  wa  viti  maalum  mkoa  wa  Iringa Ritta Kabati (CCM) akimkabidhi mwenyekiti wa waandishi wa habari mkoani Iringa moja ya jezi alizotoa kwa waandishi wa habari kwa ajili ya mechi mbalimbali za timu hiyo
 Mbunge  wa  viti  maalum  mkoa  wa  Iringa Ritta Kabati (CCM) ameipiga jeki timu ya wandishi wa habari mkoa wa Iringa kwa kuwapatia   jezi  seti  moja ,mpira na pesa taslim kiasi cha Tsh  50O,000 ili viwasaidie katika malengo yao ya kukipiga ligi daraja la kwanza .
na fredy mgunda,Iringa

Mbunge  wa  viti  maalum  mkoa  wa  Iringa Ritta Kabati (CCM) ameipiga jeki timu ya wandishi wa habari mkoa wa Iringa kwa kuwapatia   jezi  seti  moja ,mpira na pesa taslim kiasi cha Tsh  50O,000 ili viwasaidie katika malengo yao ya kukipiga ligi daraja la kwanza .

 Akikabidhi  msaada  huo kwa mwenyekiti wa chama cha wandishi wa habari mkoa wa Iringa Frank Leonard juzi    mbunge huyo alisema kuwa  yeye kama mlezi  wa timu hiyo ameamu kujingiza kwa miguu yote kuisaidi timu hiyo ambayo inaonekana kufanya vema kwenye mchezo wa soka mkoani hapo .

Kabati alisema kuwa licha ya kuwa mpira ni ajira pia unamsaidia mtu kuwa na afya njema itakayomsaidia kujiepusha na magonjwa yanayoepukika ikiwemo presha .
“Niwatie moyo hichi mulichokianzisha ni kizuri na timu yenu ina fanya vizuri na juzi tu mumenyakua kombe la Spanest  kwa kuwanyuka kitisi huu ni ushahidi tosha mukiendelea hivi hivi mutakuja kuingia ligi daraja la kwanza na baadaye ligi kuu .

Kabati  aliwataka   wadau  wengine mkoa  Iringa na nje ya  Iringa  kuendelea  kujitolea  kuisaidia   timu   hiyo    ya wanahabari ili iendele kufanya vema ndani na nje ya mkoa wa Iringa 

Akipokea vifaa hivyo mwenyekiti wa wanahabari mkoa wa Iringa Frank Leonard alimshukuru mbunge huyo kwa vifaa na fedha alizotoa huku akimuahidi mbunge huyo kuwa timu hiyo itakipiga na timu mbalimbali ikiwemo timu ya bunge la jamuhuri wa muungano wa Tanzania

Frank alisema kuwa timu hiyo imekuwa ikifanya vema kutokana na kuwa na wandishi wazuri vijana waliona ari ya kusakata kambumbi hivyo ni vema timu ya bunge kujipanga kisawasa kwani hawata toka salama pindi watakapokipiga nao mjini Dodoma

Wafanyabiashara wa Tanzania tupo tayari kwa ubia- Dkt Mengi

$
0
0
 Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Dkt. Reginald Mengi (katikati) akifurahi jambo na Mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye Viwanda Nchini (CTI) Dr. Samwel Nyantahe (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Bw. Godfrey Simbeye (kushoto) mara baada ya kuwasili kwenye hafla ya chakula cha mchana na kuwapongeza mabalozi wapya wa Tanzania nje ya nchi iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Bw. Godfrey Simbeye akiwasilisha 'presentation' iliyoainisha maeneo muhimu ya fursa za kibiashara kwenye masoko ya kimataifa kwa mabalozi wapya wa Tanzania nje ya nchi walioapishwa hivi karibuni wakati wa hafla ya chakula cha mchana kwa mabalozi hao iliyoandaliwa na TPSF jijini Dar es Salaam
  Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Dkt. Reginald Mengi akizungumza na mabalozi wapa wa Tanzania nje ya nchi kwenye hafla ya chakula cha mchana na kuwapongeza mabalozi hao watakaoiwakilisha Tanzania katika nchi za Uturuki, Italy, China, UN Geneva na Brazil iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Dkt. Reginald Mengi akisisitiza jambo kwa mabalozi wapya watakaoiwakilisha Tanzania kwenye nchi za Uturuki, Italy, China, Brazil na UN Geneva (hawapo pichani) katika hafla ya chakula cha mchana na kuwapongeza mabalozi hao iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye Viwanda nchini–CTI Dr. Samwel Nyantahe akisisitiza umuhimu wa ushirikiano katika uwekezaji, kutafuta masoko mapya, kubadilishana bidhaa na utafutaji fursa za biashara kwenye masoko ya kimataifa kwa wafanyabiashara katika hafla ya chakula cha mchana na kuwapongeza mabalozi wapya watakaoiwakilisha Tanzania kwenye nchi za Uturuki, Italy, China, Brazil na UN Geneva iliyoandaliwa na TPSF katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam
 Mwenyekiti wa Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs (TASWE - SACCOSS), Anna Matinde akizungumzia umuhimu wa kumshirikisha mwanamke katika ukuzaji wa biashara kubwa na ndogo ndogo, ambapo amesema wanawake ni nguzo muhimu katika ukuaji wa sekta binafsi nchini kutokana na uchapaji kazi wao katika sekta mbalimbali.
 Balozi mpya wa Tanzania nchini Uturuki, Prof Elizabeth Kiondo  akitoa shukrani kwa TPSF kwa kuandaa hafla fupi kama hiyo ya kubadilishana mawazo kwa jinsi gani wanaweza kukuza diplomasia ya kiuchumi katika vituo vyao vya kazi walipopangiwa.
 Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki, akizungumza kwenye hafla hiyo  ambapo amesisitiza wafanyabiashara kutoka Tanzania watumie fursa adimu ambayo ipo kati ya Tanzania na China ambapo mahusiano na ushirikiano ulianza tangu enzi za Mao na Mwalimu Nyerere.
 Balozi wa Tanzania, Geneva, Dkt. James Msekela akisisitiza jambo kwa bodi ya TPSF kwenye hafla ya chakula cha mchana kwa mabalozi hao wapya iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Wafanyabiashara wa Tanzania wamesema wapo tayari kwa kufanya ushirikiano wa kibiashara wa ubia na wafanyabiashara kutoka nje ili kukuza diplomasia ya kiuchumi na mataifa mengine.

Akizungumza katika hafla ya chakula cha mchana na mabalozi wa Tanzania nje ya nchi kilichoandaliwa na Taasisi ya sekta binafsi (TPSF) nchini, Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Dkt. Reginald Mengi amesema wafanyabiashara watanzania si omba omba na wapo tayari kwa kufanya biashara ya ubia na wenzao.

“Napenda kusisitiza kwamba sisi watanzania si omba omba kwa wafanyabishara wa nje, tuna nia uwezo, ujuzi na tunajiamini kwa kufanya biashara za kimataifa kwa ubia ili kukuza uchumi wa nchini zetu,” amesema Dkt. Mengi.

Amesema kwamba fursa za uwekezaji zipo nchini kwenye sekta za kilimo, mafuta, gesi, usindikaji na mawasiliano ila ni muhimu kuunganisha nguvu za wafanyabiashara ili kuweza kupata matokeo chanya.

Dkt. Mengi alilisisitiza kwamba sekta binafsi nchini ina imani kubwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli katika adhma yake ya kukuza sekta ya viwanda ili kutatua tatizo la ajira na kuongeza mapato ya nchini.

“Ni muhimu kuimarisha sekta binafsi ili iweze kutoa mchango mkubwa katika uanzishwaji wa viwanda hapa nchini, kwa vyovyote vile sekta hii binafsi ndio itakayojenga viwanda hapa Tanzania,” aliongeza

Kwa Upande wa Mabalozi, Dkt. Emmanuel Nchimbi ambaye anakwenda kuiwakilisha nchi huko Brazil, amesema kwamba mabalozi ni kiungo muhimu kati ya wananchi wa mataifa husika katika kukuza mahusiano na ushirikiano wa kimataifa.

“Sisi ni wawakilishi wenu huko kwenye mataifa ya nje na zaidi na kukuza mahusiano au diplomasia ya kiuchumi kwa maslahi ya wananchi wetu,” amesema Dkt. Nchimbi

Naye Balozi wa Tanzania, Geneva, Dkt. James Msekela amesema kwamba ni muhimu kuanzisha mawasiliano ya mara kwa mara kati ya wafanyabishara na mabalozi ili kusaidia upatikanaji wa taarifa za fursa mbalimbali za uwekezaji au masoko kutoka kwenye bidhaa za nyumbani.
“fursa zipo kwenye kila sekta ni muhimu wafanyabishara wa ndani wakajenga uaminifu na kujiamini ili kuweza kuingia katika ushindani wa kibiashara katika soko la kimataifa,” amesema Dkt. Msekela.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi, Geofrey Simbeye amesema wataanzisha mawasiliano ya kudumu na mabalozi wa Tanzania nje ya nchi ili kuweza kubadilishana mawazo na taarifa juu ya fursa za kibiashara katika nchi wanazokwenda kuwakilisha.

Alifafanua kwamba serikali imefungua milango kwa sekta binafsi kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kukuza uchumi wa Tanzania na kuondoa tatizo la umaskini.
Kikao hicho kati ya sekta binafsi na mabalozi wa Tanzania wanaokwenda kuwakilisha nchi katika mataifa matano ambapo mabalozi hao ni Dkt Emmanuel Nchimbi-Brazil, Dkt. James Msekela-Geneva, Profesa Elizabeth Kinyondo-Uturuki, Mbelwa Kairuki-China na Balozi George Madafa- Italy

Fainali ya AFCON 2017 ni Misri na Cameroon

$
0
0
Timu ya taifa ya Cameroon watakutana na timu ya taifa ya Misri katika fainali ya kombe la mataifa ya Afrika 2017 baada ya magoli mawili ya kipindi cha pili kuiondosha Ghana katika mashindano hayo.

Timu zote zilicheza mchezo wa kuvutia huku ikishuhudiwa kipindi cha kwanza kikimalizika kwa sare ya bila kufungana.
Magoli ya Cameroon yalifungwa na Michael Ngadeu dakika ya 72 kabla ya Christian Bassogog kuzima ndoto za Ghana kucheza fainali dakika za nyongeza, ushindi huo unaifanya Cameroon kutinga fainali ya AFCON 2017 na watacheza na fainali dhidi ya Misri, fainali ambayo itakuwa inajirudia ya mwaka 2008 ambapo Misri alimfunga Cameroon na kutwaa taji lake la sita.
Viewing all 45933 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>