Quantcast
Channel: VIJIMAMBO
Viewing all 45921 articles
Browse latest View live

MGODI WA BUZWAGI WALIPA KODI ZAIDI YA MIL 700 KWA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA

$
0
0
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo(wa pili kutoka kulia) na Meneja Uendelevu wa Mgodi wa Buzwagi ,George Mkanza wakikabidhi hundi ya kodi ya huduma ya zaidi ya Sh Mil 740 kwa Mkuu wa wilaya ya Kahama ,Fadhili Nkurlu(wa pili toka kushoto) tukio lililofanyika juzi mjini Kahama ,Wa kwanza kushoto ni makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Kahama Bi Marry Manyambo. 
Mkuu wa Wilaya Kahama,Fadhili Nkurlu na akimkabidhi hundi iliyotolewa na Mgodi wa Buzwagi kama Kodi ya Huduma yenye thamani ya zaidi ya Sh Mil 740 , Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Anderson Msumba kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa hospitali kubwa ya wilaya ya Kahama, mradi ambao ujenzi wake utategemea fedha zinazotokana na kodi za ushuru wa huduma unaolipwa na Mgodi huo. 
Baadhi ya waheshimiwa madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Kahama wakifuatilia hafla ya kukabidhi hundi kwa halmashauri ya mji wa Kahama.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo akiwahutubia waheshimiwa madiwani wa halmashauri ya Kahama pamoja na wadau mbalimbali waliohudhuria hafla ya kukabidhi hundi kwa halmashauri ya Mji wa Kahama
Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu (aliyesimama) akihutubia wageni waalikwa wakati wa hafla ya kupokea hundi ya ushuru wa huduma kutoka Mgodi wa dhahabu wa Buzwagi. Kutokea kushoto waliokaa ni Katibu tawala wa wilaya Kahama Timothy Ndanya na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo.
Mkuu wa wilaya Kahama na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi wakiteta jambo.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.

HALMASHAURI ya mji wa Kahama mkoani Shinyanga imepokea kiasi cha Sh Mil 700,040,000 kutoka kwa kampuni ya Acacia inayomiliki mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi ikiwa ni sehemu ya kodi ya huduma (service levy) ya kipindi cha mwezi Julai na Desemba 2016.

Kiasi hiki ni zaidi ya kilichotolewa kipindi cha Julai na Desemba mwaka 2015 ambapo mgodi huo uliikabidhi halmashauri ya mji wa Kahama hundi yenye thamani ya kiasi cha sh Mil 500,088,000 kama kodi ya huduma ikiwa ni utekelezaji wa sheria kwa kulipa kodi zilizopo kwa mujibu wa sheria.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya Hundi ,Meneja mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Mhandisi Asa Mwaipopo alisema Buzwagi inamatumaini makubwa kuwa katika siku za karibuni halmashauri itaanza kutekeleza mradi huo na hivyo kutoa matumaini kwa wananchi wa Kahama kupata huduma nzuri za afya ndani ya wilaya.

“Mpaka sasa kama Kampuni tumekwisha kabidhi kwenu takribani kiasi cha bilioni 1.4 hii ikiwa na maana ya kodi yote ya ushuru wa huduma katika kipindi cha mwaka 2016, wananchi wangetamani kuona mradi huu unaanza maana kiasi hicho kilichopo kama kitatumika kinaweza kutekeleza sehemu kubwa ya mradi huu kwa kuanzia wakati tukisubiri awamu zingine” alisema Mwaipopo.

Katika hafla hiyo ya makabidhiano iliyofanyika katika viwanja vya makazi ya viongozi katika wilaya hiyo,Mwaipopo alisema licha ya Kampuni yake kulipa kodi mbalimbali bado imekuwa ikijishughulisha katika kuhakikisha inakuwa mdau muhimu wa maendeleo kwa kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo katika maeneo yanayozunguka Mgodi.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kahama ,Fadhili Nkurlu aliyepokea hundi hiyo kutoka kwa uongozi wa Buzwagi na baadae kuikabidhi kwa mwenyekiti wa halmashauri ya Kahama ameupongeza uongozi wa Mgodi wa Buzwagi kwa jitihada ambazo wamekuwa wakizifanya katika kuhakikisha wanalipa kodi mbalimbali pamoja na jushirikiana na Jamii katika kutekeleza miradi mbalimbali.

Alisema Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi umeekua mstari wa mbele katika kulipa kodi mbalimbali ambako mpaka kufikia sasa zimefikia zaidi ya shilingi bilioni 197 ambazo zimetolewa katika vipindi tofauti.

Akizungumzia matumizi ya pesa hizo katika kutekeleza mradi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Kahama Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Kahama Anderson Msumba alisema halmashauri iko katika hatua za mwisho za utekelezwaji wa ujenzi huo.

Miloni 700,040,000 zilizotolewa zinafanya juma ya pesa zote zilizotolewa katika vipindi vya miaka miwili kufikia Bil 1.2 fedha ambazo zitasaidia katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ukiwemo wa Afya.

Mwisho.

MHANDISI MTIGUMWE AWAONDOA HOFU WATUMISHI KUHAMIA DODOMA

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhandisi Mathew John Mtigumwe akisisitiza jambo wakati wa kikao cha pamoja na wafanyakazi wa wizara hiyo
Watumishi wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi wakimsikiliza kwa makini Katibu mkuu wa wizara hiyo Mhe Mhandisi Methew Mtigumwe



Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhandisi Mathew John Mtigumwe hii leo amewaondoa hofu watumishi wa wizara yake kuhusu zoezi la serikali kuhamia Dodoma kuwa litafuata misingi na stahili za watumishi kwa mujibu wa kanuni za utumishi wa Umma.

Mhandisi Mtigumwe ametoa kauli hiyo wakati wa kikao maalumu cha kuhusiana na uamuzi wa serikali kuhamia Makao Makuu ya Nchi mkoani Dodoma kilichokuwa na lengo la kujadili kwa pamoja namna ya utendaji kazi katika wizara hiyo sambamba na kutoa utaratibu utakavyokuwa kuelekea mjini Dodoma.

Mtigumwe amebainisha kuwa Awamu ya Kwanza ya uhamisho utawahusisha watumishi 88 kutoka Idara Kuu ya Mazao, ambapo katika mchakato huo watumishi 41 watahamia Dodoma kuanzia tarehe 14 – 15/2/2017 na wengine 47 waliobaki watahamia muda wowote katika kipindi cha kuanzia mwezi Februari hadi kufikia mwezi Juni.

Mtigumwe amewaeleza watumishi hao kuwa maandalizi ya ofisi za Wizara ya kilimo zilizopo mjini Dodoma zinaendelea vizuri na tayari baadhi ya maeneo yamekamilika huku mengine yakiendelea kukamilishwa ili kukidhi matakwa kwa ajili ya watumishi wote watakapohamia mjini Dodoma.

Uamuzi wa Watumishi wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi kuhamia mjini Dodoma ni kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli la kuitaka Serikali yote kuhamia Dodoma ili kutekeleza uamuzi uliofikiwa tangia miaka ya 70 na Serikali ya Awamu ya Kwanza chini ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kutambua na kutangaza kuwa Dodoma ndio Makao Makuu ya Nchi.

Mhandisi Mtigumwe amebainisha hayo hii leo katika kikao cha pamoja na watumishi wa wizara ya kilimo katika Mkutano huo ulifanyika Makao Makuu ya Wizara hiyo Manispaa ya Temeke Jijini Dar es Salaam.

Fay Destiny - Hold On / "Subiri" (Official HD Music Video)

Acha Papara, Usikubali Wakuachie Majuto

$
0
0
NINA hasira kama nini hapa mnaponiona, yaani nimevurugwa kabisa. Mwenyewe nilijua timu yangu ndiyo tunachukua ubingwa msimu huu, mara eti katimu hakana hata historia na huu mchezo kamekuja kutuvurugia. Tangu siku ile sijatoka ndani, maana jirani yangu alikuwa ameweka madebe barazani anapiga ananisubiri! Kama siyo shoga yangu Ma Muhaji kuja nidokeza kisa cha mke wa rafiki wa mwanaye wa kiume, basi nilitaka leo niahirishe hili somo, nikae zangu ndani niendelee kusikilizia maumivu, yanaumajeee!!
Basi, Mama Muhaji kaniambia, eti mke wa rafiki wa mwanaye kaondoka nyumbani kwa ngoma, yaani kajaza watu akimtukana mumewe, matusi makubwamakubwa na watu wanashangilia. Kijana wa watu, nasikia kakaa kimya ndani, kavumilia mvua ya matusi na dharau, mwisho wa siku huyo dada kachukua begi lake, akaondoka kwa mbwembwe, eti wataonana kuzimu! Sasa alichonishangaza shosti, eti huyo bi dada kakaa huko alikokaa wiki tatu tu, karudi anataka waendelee na maisha na kijana wa watu.

Kilichonifurahisha, mvulana kamwambia mkewe, yupo tayari kuendelea kuishi naye ili mradi tu, ajaze watu kama alivyofanya siku ile anaondoka, halafu awaambie kwa nyodo zilezile kwamba anataka kurudi! Fyuutu, unadhani aliweza, akaishia kulialia na hadi jana anaondoka hapa kwangu Ma Muhaji, hata hatujui nini kinaendelea, maana mjumbe kakataa kwenda kusuluhisha, majirani wote hawataki na marafiki ndiyo kabisaa, wenyewe kwanza wanaona aibu wakikumbuka shoga yao alivyokuwa akitamba kwa pozi siku ile! Sasa kwa sababu hiyo ndo nimeona acha niwape kidogo uzoefu, maana nyie wengine mnadhani kubadilisha wanaume, au kuwa wajeuri ndiyo mnaonekana wajanja.
Kwanza shurti mjue, siku zote, pamoja na uzuri walionao, shepu zao na hata majukumu yao, heshima ya mwanamke inatokana na mwanaume. Asikudanganye mtu, achilia mbali kuolewa, ile tu kuishi na mwanaume ndani, ni heshima tosha kwa mwanamke.
Ile inakuonyesha ni kwa kiasi gani wewe una baraka za Mwenyezi Mungu, kwa sababu kuna wanawake na uzuri wao, hakuna mwanaume anafikiria kuishi nao. Na wasikudanganye ukisikia wanasema hawana shida na mwanaume, ni waongo. Mwanamke na hata awe na hela vipi, anaweza kutoka kwenye jumba lake la kifahari, akamfuata mwanaume anayeishi mbavu za mbwa.
Ukimpata mwanaume, shikamana naye. Usije kufanya jambo kwa sababu ya kutaka sifa kutoka kwa mashoga. Kwanza katika hao mashoga wanaoshangilia unapomkosea adabu mwanaume wako, wangapi wanaishi na wanaume? Mwanamke anayeishi na mume, hawezi kukuunga mkono kwenye ujinga huo, labda na yeye awe hamnazo! Kitu kingine ambacho sisi wanawake tunakuwa hatujui ni kwamba wenzetu wanaume, hata waache wanawake mara ngapi, hata hawaonekani kuwa na dosari, lakini sisi sasa, eti umeachika mara tatu tu, nakuambia hata kosa si lako utaonekana wewe ndiyo tatizo! Ninachotaka mjue, kile kitendo tu cha mwanaume kukubali kukuweka ndani, ni heshima kubwa sana.
Kuna maelfu ya mashoga huko mitaani wameshindwa kuwapata, tena wadada wazuri, wanajiremba, wanavaa, lakini ndiyo wanaishia maisha ya klabu, kila mwanaume anaguna ukimuambia amuweke ndani! Cha msingi, ukimpata, kaa naye chini mrekebishane makosa, lakini jivunie kuwa naye! Kwa leo ni hayo tu mashosti, tukutane wiki ijayo ni mimi Anti Nasra, Shangingi Mstaafu!
GPL

Matokeo ya Kidato cha Nne Mwaka 2016 Yametoka, Bofya Hapa Kuyaona

$
0
0

Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2016 ambapo umefaulu wa jumla umeongezeka kwa 2.56% kutoka 67.53% mwaka 2015 hadi 70.09% mwaka 2016.
Katibu Mtendaji wa barza hilo, Dkt Charles Msonde amesema kati ya wanafunzi 408,372 waliofanya mtihani, jumla ya wanafunzi 277,283 wamefaulu, wakiwemo wasichana 135,859 sawa na asilimia 67.06 na wavulana 141,424 sawa na asilimia 73.26.
Kwa upande wa watahiniwa wa shule, Dkt Msonde amesema kuwa 244,762 sawa na asilimia 70.35 ya waliofanya matihani wamefaulu ikilinganishwa na wanafunzi 240,996 sawa na asilimia 67.91 waliofaulu mwaka 2015.
Kwa upande wa ubora wa ufaulu, amesema watahiniwa wa shule wenye ufaulu mzuri wa Daraja la kwanza hadi la tatu ni 96,018 sawa na asilimia 27.60.

Kwa upande wa masomo, amesema ufaulu katika masomo ya History, Geography, Kiswahili, English Language, Basic Mathematics, Physics, Biology, Commerce na Book keeping umepanda kwa kati ya asilimia 0.12 na 8.08 ikilinganishwa na mwaka 2015.
Somo lililoongoza kwa ufaulu ni Kiswahili ambapo asilimia 77.75 wamefaulu na somo la mwisho ni Basic Maths ambalo asilimia 18.12 ya watahiniwa wa shule wamefaulu.
Kati ya wanafunzi 10 bora kitaifa, wanafunzi 5 ni wasichana na 5 ni wavulana wakiongozwa na Alfred Shauri kutoka Feza Boys ya Dar es Salaam
Kati ya shule 10 zilizofanya vibaya kitaifa, shule 6 zinatoka katika mkoa wa Dar es Salaam wakati shule iliyoongoza ikiwa ni Feza Boys ya Dar es Salaam. Pia katika shule kumi bora kitaifa, hakuna shule ya serikali
Mkoa wa Njombe umeongoza katika mikoa 10 iliyofanya vizuri zaidi kitaifa ukifuatiwa na Iringa, Kagera, Kigoma na Kilimanjaro huku halmashauri za Bukoba Mjini, Njombe, Kakonko, Kahama na Wang’ing’ombe pia zikiibuka vinara.

BOFYA HAPA KUYAONA===> MATOKEO KIDATO CHA NNE 2016

BOFYA HAPA KUYAONA===> MATOKEO MTIHANI WA MAARIFA (QT) 2016

HABARI ZA MATOKEOA KWA HISANI YA GPL

EU: Donald Trump ni tishio kwa Ulaya-BBC

$
0
0
Rais wa muungano wa Ulaya Donald Tusk
Rais wa Baraza la muungano wa Ulaya Donald Tusk ameonya kwamba maamuzi ya kutia wasiwasi yanayofanywa na Donad Trump ni miongoni mwa chanagmoto zinazokumba muungano huo.

Amesema kuwa mabadiliko yaliofanyika nchini Marekani ni miongoni mwa vitisho kutoka nje vinavyojumuisha China, Urusi na Waislamu wenye itikadi kali kwa muungano huo.

Katika barua kwa viongozi 27 wa bara Ulaya bw Tusk pia amesema kuwa anaamini kwamba wote wanakubaliana naye.

Taarifa kadhaa kutoka Washington zimesababisha maandamano dhidi ya Trump katika miji mikuu ya Ulaya.

Katika barua iliotolewa kabla ya kikao cha muungano huo huko Malta wiki hii, Bw Tusk alisema kuwa utawala mpya wa Donald Trump umeiweka EU katika hali ngumu kwa kuwa unahoji sera ya kigeni ya Marekani ya miaka 70 iliopita.

Alimalizia kwa kusema: Hatuwezi kusalimu amri kwa wale wanaotaka kudhoofisha ushirikiano wetu ambao bila amani hauwezi kufanikiwa.

Tunawakumbusha marafiki zetu wa Marekani kwamba Umoja ndio nguvu.

Uganda yakana kutomuunga mkono mgombea wa Kenya

$
0
0
Rais Yoweri Museveni wa Uganda
Taifa la Uganda limekana madai kwamba halikumuunga mkono waziri wa maswala ya kigeni kutoka Kenya Amina Mohammed kugombea wadhfa wa mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika

Bi Mohammed ambaye alikuwa anapigiwa upatu kushinda wadhfa huo aliyalaumu mataifa ya Afrika mashariki kwa kuihadaa Kenya na kutaka uchunguzi ufanywe.

Vyombo vya habari nchini Kenya vimesema kuwa mataifa ya Uganda, Burundi na Djibout hayakumpigia kura Amina Mohammed katika raundi ya mwisho na hivyobasi kumsaidia mgombea wa Chad Moussa Faki Mahamat kushindwa kiti hicho.

Bw Mahamat alipata thuluthi mbili ,ama kura 36 na kutangazwa mshindi.

Serikali ya Kenya ilidaiwa kutumia dola milioni 3 katika kampeni zake kumpigia debe bi Mohammed.

Kwa kawaida wadhfa huo huzunguka kati ya mataifa yanayozungumza kiingereza Anglophone na yale yanayozungumza kifaransa Francophone.

Mwenyekiti anayeondoka Nkosazana Dlamini Zuma kutoka taifa linalozungumza kiingereza Afrika Kusini alimrithi kiongozi aliyekuwa akizungumza Kifaransa Jean Ping 2012.

Uganda ilisema katika taarifa kwamba ilimuunga mkono Amina Mohammed kabla na hata baada ya uchaguzi huo.

Kenya: Majirani zetu walitusaliti AU

$
0
0
Mgombea wa wadhfa wa mwenyekiti kutoka Kenya katika tume ya Umoja wa Afrika AU Amina Mohammed ametaja usaliti miongoni mwa mataifa jirani ya Afrika Mashariki kuwa sababu ya yeye kutoshinda wadhfa huo.

Balozi Amina ambaye alipoteza wadhfa huo kwa mpinzani wake kutoka Chad Moussa Faki Mahamat alilaumu kushindwa kwake kulitokana na uwongo wa majirani za Kenya na siasa zinazoendelea kati ya mataifa yanayozungumza Kifaransa Francophone na wale wanaozungumza kizungu Anglophone.

Akiongea na vyombo vya habari vya kimataifa mjini Addis Ababa Amina alisema kuwa alipoteza wadhfa huo kutokana na usaliti wa majirani za Kenya ambao walikuwa wameunga mkono harakati zake.

''Baadhi ya majirani zetu hawakutuunga mkono, walisikika wakizungumzia swala hilo'', Amina alisema bila ya kutaja majina.Nadhani hofu kwamba pengine Kenya ingeshinda ndio iliowafanya kutotuunga

mkono''.

''Nadhani sisi Wakenya ni watu waaminifu sana kwa hivyo ni vigumu kushirikiana na watu wanaohadaa.kwa hivyo nadhani walijiondoa''.

Tukisonga mbele ni funzo zuri kwetu sisi. Katika raundi ya tano ya kura hizo Amina alikuwa anaongoza kwa kura 27 dhidi ya za Mahmat 25'',aliongezea Amina.

Taifa moja halikupiga kura.

Ni wakati huo ambapo mataifa mawili kutoka shirika la IGAD yaliamua kumpigia kura mpinzani wa Amina na hivyobasi kumpatia kura 28 zaidi ya 26 zilizohitajika ili mgombea kuibuka mshindi.

BBC

TaGLA YAWEZESHA MAFUNZO YA KUTOA HUDUMA KWA MAJERUHI WA AJALI KWA NJIA YA VIDEO

$
0
0
Mratibu wa Mafunzo ya Mabingwa wa Tiba ya Mifupa nchini (SICOT , Société Internationale de Chirurgie Orthopédique et de Traumatologie) Dk. Robert Mhina (kulia) kutoka Taasisi ya Mifupa Tanzania (MOI) , akishiriki mafunzo ya utoaji huduma kwa majeruhiwa wa ajali kwa njia ya video yaliyoratibiwa na kufanyika kwa njia ya video kwenye kumbi za Wakala ya Mafunzoa kwa Njia ya Mtandao, yakijumuisha nchi. Kushoto ni Dk.Lukwinyo na Dk.Mbaruku Mlinga.
 Madaktari mbalimbali wakifuatilia mafunzo hayo kwa makini.

Madaktari wa Tiba ya Mifupa wakishiriki mafunzo hayo. Kutoka kushoto ni Dk.Hamid Masoud, Dk.Valentine Restus na Dk. Joseph Msemwa.


Na Dotto Mwaibale

UMOJA wa Madaktari Bingwa wa Mifupa Duniani (SICOT) ikishirikiana na Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA), umetoa elimu ya  kutoa huduma kwa majeruhi wa ajali kwa njia ya mtandao wa mafunzo kwa njia ya video.

Umoja huo ulitoa elimu hiyo kwa kushirikiana na Madaktari Bingwa na wataalamu wa Mifupa kutoka nchi za Tanzania, Marekani, Pakistani na Brazil.

Akizungumza mara baada ya mafunzo hayo akiwa TaGLA, Dar es Salaam, Mratibu wa Umoja huo hapa nchini, Dk. Robert Mhina alisema kupitia mafunzo haya wameweza kujadili mambo mbalimbali yahusuyo ajali za barabarani.

“Huwa tunajadili mada mbalimbali kama ajali za barabarani kwa kubadilishana uzoefu na Madaktari wa nchi nyingine kwa kutumia mtandao wa mafunzo kwa njia ya video, na wakati wote huwa tunazungumza na nchi kutoka mabara mengine ili kubadilishana uzoefu,”alisema.

Alisema madaktari hao huwa wanakubaliana katika kujadili mada na kujadili kuhusu mambo muhimu yanayohusu tiba ya mifupa huku wakipeana majukumu.

“Kupitia vikao hivi hutusaidia sana hata kwa wale wanafunzi wanaojifunza Ubingwa kuona kitu gani kinaendelea duniani, bila gharama za kusafiri nje ya nchi” alisema Dk Mhina.

Alisema tayari Umoja huu inaangalia uwezekano wa kutoa nafasi kwa wanafunzi kutembela vituo kingine katika nchi hizo ili kuona na kuongeza uzoefu zaidi.

“Mwaka huu kuna vikao kama sita hivi, kikao hiki ni mwazo tu,”alisema na kuongeza kuwa kupitia mkutano huo itawasaidia wananchi kwa kuboreshewa ufanyaji wa tiba sahihi za mifupa hivyo kupata huduma za matibabu zilizoboreshwa kutokana na ajali za barabarani.

Watoa mada katika mkutano huo uliofanyika kwa njia ya video walikuwa ni pamoja na Dk. Syed M. Avais wa King Edward Medical University, Dk. Robert D. Zura wa Louisiana State University Health Science Center na Dk. Robert I. Mhina, wa  Taasisi ya Mifupa Tanzania (MOI) kutoka nchini Tanzania.


Uhakiki TIN wapasua kichwa

$
0
0
Mkurugenzi wa Elimu na Huduma kwa Mlipakodi wa
By Kalunde Jamal, Mwananchi kjamal@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Ikiwa jana ndiyo ilikuwa siku ya mwisho wa uhakiki wa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) mkoani Dar es Salaam, vituo vingi vilikuwa na misururu ya watu huku Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ikisisitiza haitaongeza muda.

TRA ilipanga kuhakiki na kuboresha taarifa za TIN kwa siku 60, kuanzia Agosti hadi Oktoba 2016 lakini kutokana na wingi wa watu iliongeza hadi Novemba 30, hata hivyo iliongeza kwa mara ya tatu hadi jana, Januari 31.

Mkurugenzi wa Elimu na Huduma kwa Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo alisema jana kwamba hawataongeza muda na jana ilikuwa ni siku ya mwisho.

“Lazima hatua nyingine zifuate, hatutaongeza muda kwa Dar es Salaam tutakuwa tumemaliza na tusonga mbele,” alisema.

Hata hivyo, watu waliojitokeza kuhakiki TIN zao walikuwa na maoni tofauti kuhusu suala hilo, Hamisi Kidanto aliyekuwa katika Kituo cha Millenium Tower kilichopo Kijitonyama Wilaya ya Kinondoni, aliuita utaratibu huo kama kumkomoa na kumsumbua mlipakodi anayelipa kwa hiari.

Alisema haamini kama kufanya hivyo ndiyo njia pekee ya kuhakiki taarifa za mlipakodi.

“Wanatukomoa, asubuhi nimekwenda Kituo cha Uwanja wa Taifa ambako niliambiwa hakuna foleni, nilichokuta anajua Mungu, nikaja hapa nusura nipoteze mwelekeo na kurudi nyumbani.

“Nina saa ya nne sielewi naelekea wapi na kufanya zaidi ya kununua fomu Sh500 hapo kwenye duka linalouza vifaa vya ofisini na kujaza,” alisema Kidanto.

Katika kituo cha Ilala, hali ilikuwa tofauti kidogo baada ya kuwapo utaratibu wa kukusanya fomu zilizojazwa kisha kuita mtu mmoja mmoja na kwa ajili ya hatua inayofuata.

Janeth Mathias aliyekutwa kwenye kituo hicho, alisema utaratibu huo ni mzuri lakini watu ni wengi, hivyo kuna kila dalili itafika saa kumi na moja jioni ya jana wakiwa bado wapo kituoni hapo.

MKUTANO MKUBWA WA MAOMBI DALLAS, SAVE THE DATE

DMV MANA CONFERENCE FEB 3 - 5 2017 MWL. CHRISTOPHER & DIANA MWAKASEGE

Kichupa cha leo IYO - Loving You Ft. Diamond Platnumz [Official Video]

HATUA ZILIZOCHUKULIWA NA SERIKALI DHIDI YA GAZETI LA MWANAHALISI BAADA YA KUMUOMBA RADHI RAIS

JE UNAWAJUA MABINGWA WA KUSAFIRISHA BIDHA TOKA USA HADI TANZANIA NA KENYA??

$
0
0


Please share with others. AllAfrika Travel & Logistics, we will Pick,Ship & Clear 4 You! CALL or WhatsApp @ +1-240-552-4870

RAIS DKT MAGUFULI AREJEA KUTOKA ADDIS ABABA, ETHIOPIA, ALIKOHUDHURIA MKUTANO WA UMOJA WA AFRIKA (AU)

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan va viongozi wengine mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Addis Ababa, Ethiopia, alikohudhuria Mkutano wa Kilele wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika leo February 1, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akishuka kwenye ndege katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Addis Ababa, Ethiopia, alikohudhuria Mkutano wa Kilele wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika leo February 1, 2017. Mbele yake ni Mkuu wa Itifaki Balozi Grace Martin.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilsalimiana na baadhi ya wafayanyazi katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam alipowasili akitokea Addis Ababa, Ethiopia, alikohudhuria Mkutano wa Kilele wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika leo February 1, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipungia wananchi mikono alipowasili katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Addis Ababa, Ethiopia, alikohudhuria Mkutano wa Kilele wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika leo February 1, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na Inspecta Jenerali wa Polisi IGP Ernest Mangu baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Addis Ababa, Ethiopia, alikohudhuria Mkutano wa Kilele wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika leo February 1, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt Juma Malewa baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Addis Ababa, Ethiopia, alikohudhuria Mkutano wa Kilele wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika leo February 1, 2017. PICHA NA IKULU.

RATIBA YA MSIBA WA EVA EKSI MWINGIZI

$
0
0


RATIBA YA MSIBA WA EVA EKSI MWINGIZI
( Eva Halifa Marealle)
Msiba upo nyumbani kwao Mbezi Beach eneo la kwa Zena Kawawa njia ya Kawe chini barabara opposite Shoppers Plaza , mtaa wa pili toka barabara ya Lami.Misa ya kumwombea itakuwa kanisa Katoliki Mt Gaspar Buffalo Mbezi Beach karibu na Shoppers Plaza Mbezi saa 07:00 mchana Jumamosi 4/2/2017 na MAZIKO yatakuwa makaburi ya KONDO BAHARI BEACH NA SIO KINONDONI
Kwa rambirambi tuma kwa :
1) Riwa H. Marealle +255 762 438 372
2) Dan H. Marealle +255 713 281 526
Tafadhali mjulishe mwingine.
Kwa wakazi wa DMV: Aunty Martha ameondoka leo kwenda nyumbani Tanzania kwa mazishi, utaratibu mwingine utafuata atakaporudi.

Immigration Legal Fee Fundraising!

$
0
0
Immigration Legal Fee Fundraising!

My brother John Kaiza is being detained by Immigration and Customs Enforcement (ICE) and is currently in removal proceedings. We have retaining a lawyer to represent him on this matter and we are asking for your assistance in raising funds towards his legal fees. His bond is currently set at $30,000 and we are unable to pay it since immigration bonds require 100% of the amount not the usual 5%. He will have to remain under custody unless the bond is paid. In the meantime, we are concentrating on securing funds for his legal fees.
We appreciate your support and thank you for your help!
Help spread the word!

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA RAIS WA GHANA MH. NANA ADDO AKUFO MJINI ADDIS ABABA, ETHIOPIA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Ghana Mhe. Nana Addo Dankwa Akufo katika Uwanja wa Kimataifa wa Bole Mjini Addis Ababa Ethiopia muda mfupi kabla ya kuondoka nchini humo alikokuwa akihudhuri Mkutano wa 28 wa wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) uliomalizika jana. Mhe. Rais Nana Addo ameahidi kuendeleza na kuimarisha zaidi ushirikiano na uhusiano kati ya nchi yake na Tanzania na amekubali mwaliko wa Mhe. Rais Magufuli wa kuitembelea Tanzania.

FAIDA ZA KUWAHI KAZINI MAPEMA

$
0
0
Na Jumia Travel Tanzania

Kuamka asubuhi ni mtihani mgumu ambao umewashinda watu wengi, si wafanyakazi, wanafunzi, wafanyabiashara au watu wa kawaida. Watu wengi hulazimika kuamka asubuhi kwa sababu inawalazimu kufanya hivyo vinginevyo wasingefanya hivyo.

Wataalamu mbalimbali wa afya, watu mashuhuri na waliofanikiwa katika shughuli zao, wametoa ushuhuda kuwa ukitaka kufanikiwa ni lazima ujijengee mazoea ya kuamka asubuhi na mapema. Jumia Travel inapenda kukushirikisha faida zifuatazo za kuwahi mapema kuelekea kwenye shughuli zako.

Inakuwezesha kuwahi usafiri
Hakuna asiyefahamu kwamba usafiri ni changamoto kubwa katika maeneo mengi duniani, sio barani Afrika peke yake. Iwe unatumia usafiri binafsi au wa umma, lazima utakumbana na aidha foleni au upatikanaji wa haraka wa usafiri. Jambo zuri ni kuwa wataalamu na washauri mbalimbali walikwishaliona hilo mapema na kupendekeza namna ya kulikabili. Ukiwahi asubuhi utajiepusha na foleni na kupata usafiri wa uhakika utakaokufikisha ofisini mapema tofauti na ukichelewa ambapo kila mtu amekwishaamka. 

Ni vizuri kwa kuanza siku
Kuwahi kazini mapema ni jambo ambalo linaleta amani kubwa sana moyoni kwa sababu unakuwa huna hofu ya jambo lolote. Ukiwahi itakuwezesha kujiandaa mapema tofauti na ukichelewa ambapo utakuwa unawaza mambo mengi kama vile, kazi ambazo hukuzimaliza jana au kumkuta bosi wako akiwa ameshafika tayari.

Kujibu barua pepe na simu zilizoingia wakati wewe haupo
Ulimwengu wa biashara hauna mipaka ya kwamba simu au barua pepe ziingie muda gani. Hivyo unaweza kujikuta unazipokea wakati muda wa kazi umekwisha na ukahitajika kuzijibu. Muda pekee wa kufanya hivyo ni pale unapowahi ofisini mapema, kwa kufanya hivyo utajikuta pindi muda wa kawaida wa kuanza kazi unawadia, wewe umekwishazijibu na kuanza upya na makujukumu yaliyoko mbele yako. 

Kuwavutia wakuu wako wa kazi
Wakati mwingine huna budi kuwaonyesha wakuu wako wa kazi kwamba unafaa na unastahili kwa majukumu uliyopewa. Kuchelewa kunaweza kutafsiriwa kwamba hauwezi kumudu majukumu mengi kama ukipewa ikiwa suala la kuwahi tu linakushinda. Hivyo kama ulianza tabia ya kuwahi basi endelea kufanya hivyo kwani jitihada zako zinaonekana kwa wakuu wako wa kazi.

Kujitengenezea mazingira mazuri ya utulivu
Asilimia kubwa ya ofisi nyingi huwa hazina utulivu pindi muda wa kazi unapofika kutokana na kuwa na wafanyakazi wengi huku kila mtu akiwa na majukumu yake ya kuyatimiza. Lakini kama ukiwahi asubuhi na mapema utaikuta ofisi katika hali ya utulivu kwa sababu wafanyakazi wengi wanakuwa hawajafika. Hii itakupa fursa ya kufanya kazi zako zile zinazohitajika kwa umakini wa hali ya juu na ustadi zaidi.

Unapata muda wa kupata kifungua kinywa na kufanya mazoezi
Sio ofisi zote mabosi ni waelewa ambao watakuwa wanakuruhusu kupata kifungua kinywa muda wa kazi. Katika ulimwengu huu wa biashara wafanyakazi wengi hulipwa kulingana na muda wanaoutumia ofisini. Kwa hiyo, kula wakati muda wa kazi umekwishafika ni upotezaji wa muda na huweza kutafsiriwa kwamba hauzingatii taaluma yako. Lakini ukiwahi kuamka mapema, unaweza kupata muda mfupi wa kupata kifungua kinywa na kufanya mazoezi na kuuweka mwili wako thabiti kwani sio wote wanaopata muda baada ya kutoka kazini.

Inakupa fursa ya kupangilia siku yako
Unapowahi ofisini asubuhi na mapema unapata muda wa kutosha wa kutafakari na kupangilia majukumu yanayokukabili siku uliyonayo. Mfanyakazi makini ni lazima azingatie muda wa kila kazi anayopewa kwani mwisho wa siku unalipwa mshahara kutokana na majukumu uliyoyatekeleza na sio kuhudhuria kazini.

Zipo faida nyingi ambazo zimekuwa zikishirikishwa na watu mbalimbali lakini hazitokwisha kama tukiamua kuzielezea zote hapa.  Wapo wanaodai pia kuwahi mapema husaidia kujenga hali ya kufanikiwa pamoja kuwa na utayari wa majukumu yako. Kwa faida hizo chache Jumia Travel inaamini kama ulikuwa umeshaanza kujenga mazoea ya kufanya hivyo utaendelea na kama hujaanza basi huu ndio muda muafaka ikiwa ndio mwaka bado mchanga.
Viewing all 45921 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>