Quantcast
Channel: VIJIMAMBO
Viewing all 45984 articles
Browse latest View live

NINI HATMA YA WATOTO HAWA WAKIRUDI TANZANIA BAADA YA USHINDI HUU ULIOITANGAZA NCHI YETU CHAMA CHA SOKA TFF NA SERIKALI

$
0
0
WATOTO HAO BAADA YA KUSHINDA WAKIWA NA BOSI WAO MUTANI YANGWE..


Hatimaye Tanzania imegusa anga za mafanikio kidogo, baada ya kuondoka kwa siku chache kwenye anga za kichwa cha mwendawazimu kwa timu yake kutwaa ubingwa wa juu kabisa wa soka.
Timu ya Taifa ya Watoto wa Mitaani ya Tanzania imetwaa ubingwa wa Dunia wa Watoto wa Mitaani baada ya jana (Aprili 6 mwaka huu) kuilaza Burundi mabao 3-1 katika mchezo wa fainali uliochezwa jijini Rio de Janeiro, Brazil.
Mshambuliaji Frank William alifunga mabao matatu katika mechi hiyo iliyochezwa uwanja mkongwe na maarufu wa klabu ya Fluminense huku mgeni rasmi akiwa Waziri wa Fedha wa Uingereza, George Osborne.
Tanzania ilipata tiketi ya kucheza fainali baada ya kuitandika Marekani mabao 6-1 ambapo hadi mapumziko ilikuwa mbele kwa mabao 4-0.
Burundi ilipata tiketi ya kucheza fainali baada ya kuifunga Pakistan mabao 4-3 katika mechi ya nusu fainali ya pili.
Timu ya Tanzania inarejea nchini Alhamisi (Aprili 10 mwaka huu) ambapo itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 10 jioni kwa ndege ya Emirates.
CREDIT:SALEHJEMBE

NGASSA APELEKA MPIRA WA HAT TRICK ALIOPEWA TAIFA KWA WEMA SEPETU

$
0
0
WEMA
“Diamond ni rafiki yangu, lakini mpira huu nitampelekea Wema kwa kuwa ni shemeji yangu na tunaheshimiana sana,” alisema Ngassa na kuongeza:
Mrisho Ngassa wa Yanga, jana alifanikiwa kufunga mabao matatu ‘hat trick’ katika mechi dhidi ya JKT Ruvu, lakini ametoa kali kwa kusema kuwa mpira aliokabidhiwa kwa kufunga mabao hayo, anaupeleka kwa shemeji yake, Wema Sepetu.
Akizungumza baada ya mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara iliyomalizika kwa timu yake kupata ushindi wa mabao 5-1, Ngassa huku akionyesha kuwa na furaha, alisema kuwa mpira huo umeongeza hamasa kwa timu yake, lakini moja kwa moja atampelekea Wema ambaye ni mpenzi wa mwanamuziki Diamond.
“Mashabiki hawatakiwi kukata tamaa na timu yetu, sisi tutapigana mpaka dakika ya mwisho ili kuhakikisha tunashinda mechi zote. Wakati mwingine tunashindwa kucheza vizuri mikoani kwa kuwa viwanja vinakuwa havina ubora mzuri.” 
Yanga imepata ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya JKT Ruvu na hivyo kuamsha mbio za ubingwa dhidi ya Azam ambao ndiyo vinara wa Ligi Kuu Bara, lakini kipa Juma Kaseja na mshambuliaji raia wa Uganda, Emmanuel Okwi hawakuwepo kwenye kikosi kilichoanza wala kwenye benchi.

RED CARPET NDANI YA KANUMBA DAY DAR LIVE USIKU HUU

Don't Try Too Hard... Go With ATL To Experience The Difference!

TULIA SPA, BEAUTY AND HOTEL ARUSHA TANZANIA NI SEHEMU ITAKAYO KUFANYA UJISIKIA KAMA NA WEWE MMOJA WA FAMILIA

$
0
0
Tulia Spa, Beauty And Hotel Arusha ni sehemu usiyotakiwa kukosa kufika ukiwa ndani ya jiji la wajanja Arusha, Kuna huduma ya hotel na spa kwa wageni na wenyeji. Tulia spa wanatoa huduma  mzuri itakayokufanya ujisikie kurudi tena siku za usoni. Maadhari ya hotel ni mazurivitanda na vyumba vyenye nafasi vitakavyo kufana ujisikia nyumbani ukiwa ndani hotel hii.
Chumba ndani ya hotel 
 Ukiwa sehem hii ya hotel kunapatika boutique pia itakayokufanya upate nafasi ya kujipatia nguo na viatu kama ukitaka kuonekana fresh kwa out.
C.E.O wa Tulia Spa, Beuaty and Hotel anawakaribisha wote na mjisikia kama mko nyumbani kwa huduma za sehemu hii.
Verandah ya Tulia kabla ujaingia ndani ya Hotel
Swim poor ukitaka kujigeuza samaki hapa ndiyo penyewe
Tulia Garden kwa nje ukitaka kupata upepo unaovuma toka milima ya Meru Arusha...
Dining room kwa ajili ya chakula ukiwa Tulia hotel.
Vitanda imara na vya mbao vitakavyokufanya ujisikia very comfortably.
Double bed ndani ya Tulia 
Spa ndani ya Tulia hotel
Spa kwa watu wawili kila mtu na kitanda chake, mambo haya yote ni Tulia Spa, Beauty And Hotel inayopatikana Arusha Tanzania.

Tulia Hotel and Spa Beauty
Sakina,white rose road., Arusha, Tanzania
+255 272 545 761 , 
+255755700001, 
+255754700001
 or +255785586411
Always open

2014 SUSAN G. KOMEN GLOBAL RACE FOR THE CURE

$
0
0
This year Team Tanzania is participating again in the Susan G. Komen Global Race for the Cure in Washington D.C.
The race will take place on Saturday, May 10, 2014 at 7:00am.
Please support Team Tanzania by registering for the race or by making a donation. Each donation made to the team will make a big difference in someone’s life.Your donation funds life-saving local programs and cutting-edge breast cancer research. Susan G. Komen funded programs reach low-income, minority and uninsured women who fall through the healthcare gaps.
To register for the race or donate to the team please click the link below or copy and paste it to your web browser.
If there are questions or concerns feel free to email the team captain and co-captains:
Nelleta Kassembe – nelleta.kassembe@yahoo.com
Rehema Barksdale – rbarks54@yahoo.com
Joyce Kassembe – jkapea@gmail.com

KINANA NA NAPE WATUA KIGOMA

$
0
0

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipita katikati ya Chipukizi wa CCM Baada ya kuvishwa skafu alipowasili kwenye uwanja wa Kigoma ambapo atakuwa na ziara ya siku sita ndani ya mkoa wa Kigoma.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye mara alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kigoma, pia Katibu Mkuu alimpongeza Nape kwa ushindi mkubwa wa uchaguzi wa ubunge jimbo la Chalinze.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisaliminana na baadhi ya viongozi wa CCM Mkoa wa Kigoma waliofika kumlaki leo katika uwanja wa ndege wa Kigoma.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua miradi ya kiuchumi iliyojengwa kwenye ofisi za CCM Mkoa wa Kigoma.

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na vijana waliokuwa wanarekebisha mifereji kando kando ya uwanja wa Ndege wa Kigoma mara alipowasili mkoani hapo na kuwapongeza kwa kazi nzuri na kuwasihi kuwa wafanyakazi wenye kufikiria maendeleo ya kwao na ya kujenga nchi kwa jumla kwani nchi bado inawahitaji vijana wachapakazi kama wao.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akiwa kwenye picha ya pamoja na Kamanda wa Matukio Ndugu Richard Mwaikenda na Bakari Kimwanga mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kigoma.

MWIGULU NCHEMBA APELEKA UMEME VIJIJI 43 JIMBONI KWAKE,ROBO TATU YA JIMBO KUWAKA UMEME

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Singida(Kushoto) akibadilishana Mawazo na Waziri wa Nishati na Madini Mh:Sospeter Mhongo na Naibu Waziri wa Fedha Mh:Mwigulu Nchemba(kulia) hii leo baada ya Kuwasili Singida kikazi,Kubwa kutembelea Utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini ndani ya Wilaya ya Iramba Jimbo la Mh:Mwigulu Nchemba.
 Waziri wa Nishati na Madini Mh:Mhongo akiwa na Mbunge wa Iramba Magharibi Mh:Mwigulu Nchemba mara baada ya Kufika Iramba Kijiji Cha Kaselya kwaajili ya Kuzungumza na Wananchi wa Kaselya kuhusu Utekelezaji wa Mradi wa Umeme Kijijini Kwao Unavyoendelea na Wanavyopaswa Kujiandaa na Matumizi ya Umeme huo.
 Waziri wa Nishati na Madini akiwa na Mwenyeji wake Mh:Mwigulu Nchemba wakisalimiana na Wananchi wa Kijiji cha Kaselya.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mh:Yahya Nawanda(kulia) akibadilishana Mawazo na Mbunge wa Iramba Mh:Mwigulu Nchemba hii leo kwenye Mkutano na Wananchi wa Kaselya kuwaelezea Fursa waliyonayo kwenye Umeme walioingiziwa Kijijini Kwao.Mh:Mwigulu Nchemba akifurahia na Wananchi Wake wa Kijiji cha Kaselya mara baada ya Kupokea Umeme na Kuwaelimisha Wananchi faida za Umeme huo.
Mh:Mhongo Waziri wa Nishati na Madini na Mh:Mwigulu Nchemba(Mb) wakishikana Mikono na
Wakandarasi waliokabidhiwa Mradi huo wa Kusambaza Umeme Vijiji 43 ndani ya Jimbo la Iramba na Kukamilisha Mwezi wa Sita 2015 kwa Mkoa wote wa Singida.
 Mh:Mhongo akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Kaselya hii leo Jimboni Iramba kuwaelimisha Mradi wa Umeme unaeondelea Kutekelezwa Kijijini Kwao.
Wananchi wa Kijiji Cha Mgongo Wakimlaki Mbunge wao baada ya Kuwaletea Umeme.
Mh:Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wake wa Kijiji cha Mgongo walionufaika na Umeme unaoendelea Kusambazwa Jimbo la Iramba takribani Vijiji 43.
"Mkataba wangu na Nyie ni Maendeleo tu,Haina Maana kuniona Mara kwa Mara Jimboni hapa bila Kuleta Maendeleo,Furahieni kuona Kazi Inatendekea na Maendeleo yanaonekana"Mwigulu Nchemba.Furaha ya Kutimiza Mahitaji ya Wananchi Wako,Mwigulu Nchemba akishangiliwa na Wananchi mara baada ya Kuwapa taarifa ya Utekelezaji wa Mradi wa Umeme na Miradi Mingine ya Maendeleo Kijiji Cha Mgongo.
 Sehemu tu ya Nguzo Nyingi Zilizosambwa kwenye Vijiji 43 Jimboni Iramba,Hizi zipo Kijiji Cha Mbelekesye.
Sehemu ya Mamia ya Wananchi waliofika Kwenye Mkutano Kijiji Cha Mgongo kwaajili ya Kupatiwa Elimu ya Kupata Umeme na Kuutumia.Mh:Mhongo akimtambulisha Mkandarasi kwa Wananchi na Kuwaomba Kutoa Ushirikiano wakati wote wa Utekelezaji wa Mradi wa Umeme.
Wanafunzi wakiwa ni Wanufaikaji Wakubwa wa Umeme wakisikiliza Kwa Makini namna ya Kutumia Umeme huo.
 Mkoa Wa Singida husuasani Wilaya ya Iramba ni Watengenezaji wakubwa wa Mafuta ya Alizeti,Hapa Wanananchi wakitoa Zawadi zao za Mafuta kwa Mh:Mhongo na Mh:Mwigulu Nchemba.

Waziri wa Nishati na Madini Mh:Sospeter Mhongo hii leo akiwa na Mwenyeji wake Mbunge wa Iramba Magharibi Mh:Mwigulu Nchemba Wametembelea Utekelezaji wa Mradi wa Umeme Mkoani Singida kwa Wilaya ya Iramba.
Wilaya ya Iramba (JImbo la Mh:Mwigulu Nchemba) Mradi wa Umeme Vijijini Umevifikia Vijiji 43 katika Jimbo lote la Iramba,Mh:Mhongo amesema,Serikali imetenga Bilioni 31.9 kwa Mkoa wa Singida kuhakikisha Umeme unasambazwa sehemu Kubwa ya Vijiji ilikufungua Milango ya Kukua Uchumi na hatimaye Kuondokana na Umaskini.
Kwa Wananchi Watanufaika Zaidi na Mradi huo kwasababu Uunganishaji wa Umeme kwenye Makazi ni kwa Bei Nafuu sana,Mwananchi atatakiwa Kuchangia Tsh;27000(Elfu Ishirini na Saba tu) Kuunganishiwa Umeme Nyumbani Kwake tofauti na Kipindi cha Nyuma Umeme ulikuwa Unaunganishwa kwa Shilingi Laki nne na baadae Laki moja na Sabini.Hiyo 27000/= itakubalika tu endapo Mwananchi ataunganisha Umeme wakati Mkandarasi bado anaendelea na Ukamilishaji wa Mradi.
Akizungumza na Wananchi wa Mgongo,Mh:Mhongo amesema"Serikali ya CCM imedhamiria kufikisha Umeme kila Kona ya Nchi hii,Gesi tunayo ya Kutufanya tufikishe Umeme popote pale,Wananchi manaombwa Kuonesha Umoja wenu katika hatua hii ya MATOKEO MAKUBWA SASA ili Uchumi wa Nchi yetu ufikie pale tunapotakiwa Kufika.
Vilevile Mbunge wa Iramba Mh:Mwigulu Nchemba ametoa rai kwa Wananchi Wake kuchangamkia Fursa hiyo ya Kuunganishiwa Umeme kwa bei nafuu,Umeme wa bei nafuu Ulikuwa ni Historia kwa Nchi hii lakini sasa Umepatikana.Hivyo amewaomba Wananchi wa Vijiji Vyote 43 vinavyopitiwa na Mradi wa Umeme huo kujipanga Kutumia Umeme kwaajili ya Kuinua Uchumi wao.
"Mimi kazi Mkataba wangu na Nyie Wananchi nia Kuwaletea Maendeleo tu,Hivyo nitaendelea kuwaletea Maendeleo kadri ya Uwezo Wangu,Tuungane Mkono tufute Umaskini Kwa Wananchi wa Iramba" Mwigulu.
Kusoma Vijiji Ingia hapa>>>MWIGULU NCHEMBA
Picha/Maelezo na Sanga Festo

CHEGE AKINUKISHA INSTAGRAM KWA ANAETAKA KUMTIBULIA PENZI LAKE KWA MADAM NYASHI.

$
0
0

Hehehe watu wamevurugwa vibaya sana huko Instagram kila kukicha movie zinaanza mpya na zingine zinaendelea. Sasa leo hadi Chege kaamua kufungua ujue huko hakuna usalama. Kusema ukweli Insta ina raha na karaha zake omba tu yasikukute. Story ni hivi mchumba aka mke mtarajiwa wa msanii Chege alipost picha yake kama kawaida watu wote tunavyo fanya huko Instagram mara katika comment akatokea mtu na comment yake akidai yeye nae ni mwanamke wa Chege basi baada ya hapo Chege akaona isiwe tabu na kuamua kumtolea uvivu huyo MARIABYGIR asiyekuwa na picha wala followers kwa kuweka huo ujumbe na ujumbe wake kwa chini. Haya nakuanchia uendelee na movie kama ifuatavyo.....
Lol jamani watu ni wachokozi balaaa. Wacha movie iendeleee.

AOTA MAGAMBA YA MTI MGUUNI! TAZAMA PICHA HAPO CHINI KWA MAELEZO ZAIDI

$
0
0

Kijana, Andrea John (26) akiwa na mguu ulioota magamba mithili ya mti mkavu.AMA KWELI HUJAFA HUJAUMBIKA! Kijana, Andrea John, 26, amejikuta katika wakati mgumu mara baada ya kupatwa na ugonjwa wa ajabu uliosababisha mguu wake kuwa na magamba mithili ya mti mkavu. 
Andrea anayeishi kwa mateso makali maeneo ya Argentina, Manzese jijini Dar, anasema mwaka 2005 akiwa anafanya kazi katika mashine ya kusaga na kukoboa, alijikuta akianza kuumwa na vidole vya mguu wa kulia na baadaye maumivu hayo kuhamia kiunoni, kitu kilichomfanya kukosa raha.
Anaendelea kusimulia: “Mara baada ya kusikia maumivu ya vidole na kiuno, nilikwenda katika Hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Sehemu ya mguu wa Andrea Paul kwa karibu zaidi.
“Nilipofika huko, wakaamua kuchukua vipimo vya damu kwa ajili ya uchunguzi lakini hawakutaka kunipa majibu, nilishangaza sana kwa sababu sijawahi kuona kitu kama hicho.
KUFIWA NA MKE
“Mwaka 2006 nilifiwa na mke wangu, Nuru Kassim ambaye ameniachia mtoto mdogo, Agness mwenye umri wa miaka 7. Hilo lilikuwa pigo kubwa kwangu.
“Kutokana na matatizo ya kuugua nilishindwa kumlea mtoto wangu hasa ikizingatiwa kuwa sikuwa nafanya kazi, bahati nzuri mwanamke mmoja wa Kiarabu alijitokeza na kuamua kumchukua Agness na kuishi naye,” alisema Andrea kwa masikitiko.
Aliongeza kuwa aliendelea kupata matibabu japokuwa hayakubadilisha kitu chochote zaidi ya mguu wake kuanza kuota magamba ambayo yaliufanya kubadilika na kufanana na mti uliokauka. Baada ya kuona hali imekuwa hivyo na maumivu yakimzidia kila siku, aliamua kurudi Hospitali ya Mwananyamala ambapo walimwambia achukuliwe vipimo kwa mara nyingine.
KUHAMISHIWA MUHIMBILI
“Kilichofanyika ni kuchukuliwa vipimo kwa kutumia kipimo cha kupimia saratani ya ngozi ambacho hujulikana kitaalamu kama Biopsy na hivyo kukutwa na ugonjwa wa kansa ya ngozi uitwao Kaposis Sarcoma,” alisema.
Alisema hakuweza kupatiwa matibabu zaidi ya kuandikiwa karatasi ya kuhamishiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, jijini Dar.
Alipokuwa Muhimbili, Andrea alilazwa kwa muda wa miezi miwili bure kutokana na kutokuwa na uwezo kifedha, madaktari waliliangalia tatizo lake kiundani na wakashauri asikatwe mguu hivyo wakamuandikia dozi ya dawa za vidonge na kumruhusu kurudi nyumbani.
Mpaka sasa Andrea anaendelea na vidonge hivyo na hana msaada wowote zaidi ya kutembea mtaani na kuomba chochote japo apate chakula cha siku na anashindwa kurudi hospitali kwa kuwa hana hata senti tano.
Andrea anaomba msaada kwa yeyote aliyeguswa na habari hii ili aweze kupata fedha za kuendeleza matibabu yake na kujikimu. Kutoa ni moyo na ukimsaidia utapata baraka za Mungu. Unaweza kuwasiliana naye kupitia namba ya dada yake. Zainabu John Kimweri – 0656 037075.
-GPL

CHADEMA BADO MSALA WAMSIMAMISHA MWENYEKITI WA CHAMA HICHO MKOA WA KATAVI

$
0
0


WAJUMBE wa Mkutano Mkuu wa Chadema mkoani Katavi wameridhia kwa kauli moja na kubariki uamuzi wa kumsimamisha uongozi Mwenyekiti wa Mkoa wa Chama hicho, John Malack na viongozi wengine watatu waandamizi wa chama hicho, Jimbo la Mpanda Mjini.
 
Viongozi hao watatu ni pamoja na Mwenyekiti wa chama hicho Jimbo la Mpanda Mjini, Seif Sipia, Katibu wa jimbo hilo, Joseph Mona ambaye pia ni Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini kwa tiketi ya chama hicho, Said Alfi.
 
Katika orodha hiyo yupo pia Katibu Mwenezi wa chama hicho, Godfrey Maufi ambaye ameshavuliwa uanachama wa chama hicho akidaiwa kuiba nyaraka za siri za chama hicho na kuzisoma katika mkutano wa hadhara.
 
Pia mkutano huo umependekeza kuvuliwa uanachama wa chama hicho watu kadhaa akiwemo Iddi Nziguye ambaye ni Diwani kwa tiketi ya chama hicho Kata ya Makanyagio na Diwani wa Kata ya Kashaulili, John Matongo.
 
Uamuzi huo ulifikiwa juzi na wajumbe wa mkutano huo mkuu wa chama hicho uliofanyika mjini hapa ukiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Chadema wa Kanda ya Magharibi, Masanja Mussa Katambi.
 
Februari 22 mwaka huu kikao cha mashauriano cha chama hicho ngazi ya mkoa kiliwasimamisha viongozi hao, akiwemo mwenyekiti wa chama hicho mkoani hapa, Malack akituhumiwa kufungua na kuhutubia mkutano wa hadhara uliofanyika Februari 2, mwaka huu ambao unadaiwa uliwakashifu viongozi wa chama hicho ngazi ya Taifa

TAZAMA PICHA 10 ZA SHABIKI HUYU ALIYEANGUA KILIO KIKUBWA ILI APATE NAFASI YA KUPIGA PICHA NA DIAMOND

$
0
0

  HIKI NDO ALICHOKISEMA DIAMOND KUHUSANA NA TUKIO HILO
 Usiku uliopita umekuwa ni usiku wa furaha kwangu,baada
 ya dada angu kuzindua video yake ya WANATETEMEKA
 kwa,mafanikio makubwa..lakin tukio la huyu kijana 
aliyeangua kilio  akishinikiza anione
 na kupiga picha,ni tukio ambalo limenionesha ni kiasi gani nina
 watu out there walio upande wangu,watu
 wanaonipenda kwa dhat kabisa.
nikiwa backstage
 kulikokuwa kumejaa kidogo,alijitokeza kijana huyu
ambae
bahat mbaya sikuweza kumwona mapema..
mpaka niliposkia akilia,alikuwa akishinikiza
 apewe nafasi ya kuniona na kupiga picha,but kulingana
 na utaratibu wa kiusalama mlinzi alimzuia na ndipo 
alipoanza kulia mfululizo..na hata alipopata 
nafasi tukaonana na kupiga picha ni kama nilimwongeza spiidi ya kuendelea kulia
 mpka mda wangu wa kupanda stejini ulipofika..
nilipomaliza show na kurudi garini tayari kwa
 kuondoka alinifata akiwa na ombi lile lile,kupiga
 picha nilishuka nikazungumza nae kisha tukapiga picha na kuagana ....!!
NAWAPENDA SANA MASHABIKI WANGU
 Backstage.furaha iliporudi, baada ya kuonana nae na kupiga picha wote
 Nikijaribu kumbembeleza 
  akimpa mkono,lakini hii haikuwa shida yake,alitaka wapige picha tena 

Ilibidi Diamond ashuke kabisa kwenye gari ,akazungumza
 nae nakupiga picha ndipo akatulia

Akielezea furaha yake na sababu ya kufan

WAIGIZAJI WATANO WA KIKE BONGO MOVIES WANAO ONGOZA KWA KUSAKWA KWENYE Google HAWA HAPA

$
0
0

Kwa mujibu wa Technical research ya mtandao huu....kupitia Google, Kwakuangalia Most Keywords ni Tanzania...Haya ndio majina ya waigizaji wa kike ambao watu wengi huandika majina yao kwenye Google Search....

(1) Wema Sepetu


( 2) Elizabeth Michael aka Lulu

(3) Irene Uwoya


(4 ) Jackline Wolper

CreditDOMO ZEGE

TAZAMA PICHA ZA WASANII WA BONGO MOVIE WALIVYOZUA KIZAAZAA JANA KANUMBA DAY NDANI YA DAR LIVE

Mwakilishi wa Jimbo la kiembe Samaki atimiza ahadi kwa timu za jimbo lake

$
0
0



 Mwakilishi wa Jimbo la Kiembe samaki Mhe. Mahmoud Thabit Kombo (wakatikati) wakiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM Jimbo la Kiembe samaki Ramadhan Mrisho wa kushoto, kulia  Mwenyekiti wa Kamati ya michezo ya Jimbo hilo Juma Abdul-rabi kabla ya kukabidhi pesa taslim na vifaa vya michezo kwa tim za Jimbo hilo ikiwa ni ahadi aliyoitoa wakati wa kampeni zake hafla hiyo imefanyika katika Hoteli ya Ocean View Mjini Zanzibar.
 Diwani wa Jimbo la Kiembe samaki Bw. Gharib Mohamed Addy akizungumza na wanamichezo wa Jimbo hilo (hawapo pichani)kabla yakukabidhiwa vifaa vya michezo na Mwakilishi wa Jimbo la Kiembe samaki Mhe. Mahmoud Thabit Kombo
 
 Baadhi ya wanamichezo na viongozi mbalimbali wa Jimbo la Kiembe samaki wakimsikiliza Mwakilishi wa Jimbo hilo Mhe. Mahmoud Thabit Kombo (hayupo pichani) kabla ya kukabidhi pesa na vifaa vya michezo kwa timu za Jimbo lake. 
 
 Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akimkabidhi pesa sh/= laki nne kiongozi wa tim ya Smoll Zico ya Kiembe samaki ikiwa ni ahadi aliyoito wakati wa kampeni zake. 
 
Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akimkabidhi Katibu wa Tim ya Mbweni Kids Khalifa Khamis vifaa mbalimbali vya michezo, Jumla ya tim nane za Jimbo hilo zimepata pesa na vifaa mbalimbali vya michezo vyenye thamani ya shiling milioni saba na nusu.  
(PICHA NA MAKAME MSHENGA WA MAELEZO ZANZIBAR)

DULLY SYKES" DIAMOND HAENDI KWA WAGAGA ..HII NDIO SIRI YA MAFANIKIO YAKE"

$
0
0

Jina la Diamond Platinumz mtoto wa Tandale mwenye historia ya kuishi maisha ya ukata, sasa hivi ni moja kati ya majina makubwa kimuziki barani Afrika huku akishiriki kwenye project kubwa kama One Campaign iliyoongozwa na D’Banj huku akipewa mashavu na wasanii wakubwa wa Afrika Magharibi.

Dully Sykes ameuambia mtandao wa Times Fm moja kati ya sababu ambazo zinambeba mwimbaji huyo na kumpeleka kwenye level ya juu ya mafanikio kuwa ni kiu kubwa aliyonayo inayomfanya afanye kazi usiku na mchana huku akiwasumbua maproducer bila kusubiri wamuite studio.

“Wasimuone Diamond anafanya vizuri, Diamond anafika mbali wakafikiria Diamond anafanya kazi kwa kumsubiria hadi producer amuite studio, no sio kweli. Diamond anashinda usiku kila siku studio.” Amesema Dully Sykes.

Dully ameeleza kuwa hata yeye pia hukesha studio akifanya kazi na ndio sababu inayomfanya aendelee kufanya vizuri tangu alipoanza muziki bila kupotea na kwamba wasanii wengi wasiofanya hivyo huishia kuporomoka na kudai kuwa walioko juu wanafanya uchawi.

Mwimbaji huyo ambaye ni mmiliki wa studio ya 4.12 ameongeza kuwa akili ya kuwekeza kwenye vitega uchumi pindi uwapo juu ni moja kati ya sababu zinazomsaidia msanii kuendelea kuwa juu kwa muda mrefu.

“Kama wangekuwa wajanja sasa hivi wangekuwa na vitega uchumi…kitu kama studio ni kama jiko. Unakula kwa kutumia studio. Hata kama mtu haji lakini unaweza kutengeneza muziki kwa kutumia akili yako ukasema ‘leo bwana nimeamka saa kumi ya usiku nina idea yangu hebu ngoja niingie studio nidumbukize hii sauti pengine kesho itanifaa. Na kweli unakaa unapata idea nzuri na unatengeneza kitu kizuri.”

MAHAKAMA KUU KANDA YA MOSHI YAAWACHIA HURU WASHTAKIWA 9 NA KUWATIA HATIANI 3 KATIKA KESI YA MAUAJI YA NMB MWANGA.

$
0
0

Mshtakiwa namba 3, Kalisti Joseph Kanje ( aliyebeba mafaili),  Mshtakiwa namba moja, Samwel Gitau Saitoti (alifunika uso) na mwenzake  Mshtakiwa namba 2, Michael Kimani wakitoka nje ya mahakama kuu baada  ya mahakama hiyo kuwatia hatiani kwa kosa la kuua Askari polisi katika  tukio la uporaji wa benki ya NMB Mwanga
Washtakiwa namba 4 hadi 12, wakisaidiwa kupanda kwenye gari la Polisi baada ya mahakama kuu  kanda ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, kuwaachia huru leo mchana katika kesi ya mauaji ya askari polisi yaliyotokea Julai 11 mwaka 2007.
Mshtakiwa namba 3, Kalisti Joseph Kanje ( aliyebeba mafaili),  Mshtakiwa namba moja, Samwel Gitau Saitoti (alifunika uso) na mwenzake  Mshtakiwa namba 2, Michael Kimani wakitoka nje ya mahakama kuu baada  ya mahakama hiyo kuwatia hatiani kwa kosa la kuua Askari polisi katika  tukio la uporaji wa benki ya NMB Mwanga.
Mshtakiwa namba 12, Salome Materu aliyekuwa Mhasibu wa Benki ya NMB  Mwanga akisaidiwa kupanda katika gari la polisi baada ya mahakama kuu  kanda ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, kumuachia huru pamoja na wengine 8 katika kesi ya mauaji ya askari polisi yaliyotokea Julai 11 mwaka 2007.
Mshtakiwa namba 12, Salome Materu aliyekuwa Mhasibu wa Benki ya NMB  Mwanga akisaidiwa kupanda katika gari la polisi baada ya mahakama kuu  kanda ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, kumuachia huru pamoja na wengine 8 katika kesi ya mauaji ya askari polisi yaliyotokea Julai 11 mwaka 2007..(picha zote  na Fadhili Athumani)

Mwandishi Wetu, Kilimanjaro
MAHAKAMA kuu kanda ya Moshi, imewaachia huru washtakiwa 9 na kuwatia  hatiani wengine 3 wakiwemo Wakenya wawili na Mtanzania mmoja kwa kosa  la kumuua askari Polisi E6829 Michael Milanzi, aliyeuawa katika tukio  la Ujambazi lilitokea Julai 11mwaka 2007 kwenye Benki ya NMB tawi laMwanga.

Akisoma uamuzi mdogo wa mahakama hiyo, Jaji mfawidhi Kasusulo Sambo alisema kwa mujibu wa sheria wa sheria 293 ya muendelezo wa ushahidi  wa makosa ya jinai, kifungu kidogo cha 1, sura ya 20 kamailivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002, mahakama imeridhia kuwa Jamhuri  ilishindwa kabisa kujenga kesi dhidi ya watuhumiwa 9, Raia wa Tanzania, na hivyo inawaachia huru.

Jaji Sambo alisema katika uamuzi huo Mahakama vilevile ikiongozwa na sheria hiyo kifungu kidogo cha 2, sura ya 20 kama ilivyorekebishwa mwaka 2002, imeona kwamba upande wa Jamhuri ilifanikiwa kujenga Kesi dhidi ya mshtakiwa namba 1, Samwel Gitau, Mshtakiwa namba mbili Michael Kimani, wote raia wa Kenya na mshtakiwa namba 3, Kalisti Joseph Kanje, Raia wa Tanzania.

 "Mahakama ilitafakari ushahidi wote wa Jamhuri, na kufikia maamuzi kwamba mashahidi wote 18 waliofika mbele ya mahakama hii, walionesha ni jinsi gani Jamhuri ilivyoshindwa kujenga kesi dhidi ya washtakiwanamba 4,5,6,7,8,9,10,11, na 12,

"Aidha Mahakama hii tukufu imeridhishwa kwamba Jamhuri kwa kuzingatia sheria ya muendelezo wa makosa ya jinai, kifungu kidogo cha pili, sura ya 20 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002, ilifanikiwa kujenga kesi kwa kiwango kisicho mashaka dhidi ya washtakiwa namba 1,2 na 3,"alisema Jaji Sambo.

Katika uamuzi huo, Jaji Sambo aliongeza kuwa Mahakama inaamuru washtakiwa wote 4 hadi 12 walionekana kutokuwa na kesi ya kujibu dhidi ya tuhuma hiyo ya mauaji waachiwe huru maramoja isipokuwa kama wana kesi nyingine inayowakabili ambapo mtuhumiwa namba 10, ElizabethMsanze "Bella" ambaye anatuhuma za ujambazi alilazimika kuendelea kutumikia kifungo chake.

Washtakiwa walioachiwa huru ni mshtakiwa namba 4, Deodat Temu, mshtakiwa namba 5, Afande Nathaniel Wanyama, mshtakiwa namba 6, Emmanuel Mziray, mshtakiwa namba 7, Florian Kimati "Babylon", mshtakiwa namba 8 Devotha Msanze.

Wengine ni mshtakiwa namba 9, Juliana Msanze, Mshtakiwa namba 10 Elizabeth Msanze, mshtakiwa namba 11, Ntibasalila Msanze na mshtakiwa namba 12, Salome Materu ambaye alikuwa ni Mhasibu wa Benki hiyo wakati wa uvamizi.

Wakati huo huo upande wa utetezi unaomtetea mshtakiwa namba 3, Kalisti Joseph, unaowakilishwa na wakili wa kujitegemea, Prof. Jonas Itemba, umetoa ombi la kuwasilisha mashahidi wawili mahakamani hapo kwa ajili ya kutoa ushahidi wa utetezi kwa mteja wake.

Mashahidi hao ni Josephine Kalisti, ambaye ni mke wa Mshtakiwa huyo, raia wa Tanzania anayetuhumiwa kushiriki na kufadhili tukio la ujambazi lililopelekea mauaji, na mwengine ni Dafrosa Joseph.

Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa tena Aprili 10 mwaka huu, baada ya Mahakama kuridhia ombi la Washtakiwa namba 1 na 2 ambao hawana mashahidi, ya kutaka kuruhusiwa kuwasilisha mahakamani, maelezo ya Shahidi namba moja aliyoandika kwa mkono wake ambaye ni meneja wa Benki hiyo wakati huo, Robert Marandu.

VIJANA MAARUFU BONGO AMBAO WAPENZI WAO HAWAJULIKANI

$
0
0

Dullah Sykes
1. Martin Kadinda

Ni mwanamitindo maarufu apa bongo, na anayefanya vizuri kwenye tasnia hiyo, pia ni manager wa wema sepetu. Huyu amekuwa akipiga picha na warembo tofauti tofauti , ila haijawahi kuripotiwa popote mrembo anayetoka nae ata kwa kupakaziwa.

2. Salama Jabir
Huyu ni mtangazaji wa mkasi TV show, mbali na muonekano wake wa kuvutia ila hadi Leo haijawahi kuripotiwa mtu anayemmliki hata kwa kusingiziwa. 

3.Ben Pol

mwanamuziki classic wa bongo fleva, achilia mbali muonekano wake wa kuvutia , naye mpaka Leo mpenzi wake hajulikani, na wala haijawahi kuripotiwa popote kama ana mpenzi au la.

4. DJ Fettty

Huyu ni mtangazaji wa clouds FM, ana sura na umbo la kuvutia , ila hadi Leo haijulikani mtu anayekula mzigo nani, japo kwa kusingiziwa

5.Millard Ayyo

Mtangazaji machachari kutoka clouds FM, pamoja na utanashati wake ila haijawahi kuripotiwa popote kama yupo kwenye mahusiano na haijulikani mpenzi wake ni nani

6. B 12

Huyu kama ilivyo kwa Millard, hajawahi kuhusishwa na scandal yeyote ya kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi, haijulikani kama yupo au la.

7. Adam Mchonvu

huyu pia hajawahi kusikika au kuhusishwa na mahusiano ya aina yeyote.

8.Ally Rehmtulah

Mbunifu wa mavazi, naye huyu hajawahi kuhusishwa na wala haijuilikani kama ana mpenzi au la.

THE RISE OF QUEEN VICTORIA - EPISODE 1

MR NICE AELEZA SABABU ZA KUFIRISIKA , ASEMA ALIWAHI KUWA NA ZAIDI YA MILIONI 600 LAKINI KWA SASA NI MAJALALA.

$
0
0
Hivi karibuni baada ya kuchezea kichapo kisa kikidaiwa kuwa mke wa mtu na hapo alipigwa chupa ya bia iliyomchana chana uso mzima na kumuacha na kilema cha makovu.

Hapa Mr Nice Shavu dodo msafara wake ulikuwa zaidi ya gari nane hadi kumi huku zikiwa zimejaa wapambe na wachumba wa ukweli.
Mmoja wa wacheza shoo wa Mr Nice aliyekuwa kivutia kwa mashabiki alifahamika kwa jina la Wabog
Hapa Mr Nice kipindi akiwa safi pesa karatasi watoto wazuri full kumshobokea kama ilivyo kwa Diamond kwa sasa. 
Hapa Mr Nice akiwa hoi chini baada ya kupigwa ngumi zaidi ya 20 za chembe na Dudu Baya kwenye ukumbi wa Diamond miaka kadhaa iliyopita 
Hapa Dudu Baya akipambana na Mabaunsa kwa kumzuia asiendelee kumsurubu Mr Nice siku alipompa kipigo cha mbwa mwizi. Kulia mwenye shati jeupe ni Mkurugrnzi wa Clouds Media Lugemalila Mutahaba Na Livingstone Mkoi Katika hali isiiyokuwa ya kawaida mwanamuziki Lucas Mkenda maarufu kwa jina la Mr Nice ameibuka na kueleza sababu zilizomfanya kufirisika licha ya kuwahi kumiliki zaidi ya bilioni moja na nusu kwenye akaunti zake tofauti. Akiongea na Xdeejayz Tanzania mwanamuziki huyo ambae kwa sasa yupo nchini kwa muda mfupi kabla ya kurudi tena nchini Kenya alikohamishia makazi na kufanyia shughuri zake za kimuziki huko. Akizungumza na mwandishi wetu kwenye ukumbi wa mpya wa burudani wa Full Stop uliopo Mwanamboka Kwa Manyanya Kinondoni Jijini Dar ambapo alisema kuwa dunia imemfanyia kitu kibaya na hafahamu nini kimetoka katika maisha yake. Mr Nice alisema kuwa anashindwa kuelewa kwa nini maisha yamempiga kiasi hicho kwani pesa yote aliyokuwa anaipata alikuwa anaipata kwa jasho lake" Kaka naweza kusema hii ni mipango ya Mungu tu kwani sikuwahi kumdhurumu mtu wala kuiba cha mtu pesa yote nilikuwa naipata kwa hali naweza kusema hii ni mipango ya Mungu tu wala si mkono wa mtu" Alisema mwanamuziki huyo Aidha mwanamuziki huyo anasema" Niliwahi kumiliki zaidi ya milioni elfu moja na mia tano kwenye bank tofauti hapa nchini pesa hizo zilitokana kufanya shoo nyingi za nje ya nchi kama Marekani, Uingereza, Ujerumani, Sweden, Holand, Dubai, Afrika Kusini na kwingineko na kila shoo nilikuwa napata pesa ndefu sana" Alisema Hata hivyo Mr Nice nasema kuwa hizo ni nchi za mbali lakini bado shoo za alizokuwa anazifanya nchi za Kongo, Zambia, Uganda, Rwanda, Kenya na moja ya shoo ambayo akiikumbuka huwa inamtoa machozi ni ile ya nchini Rwanda ambayo siku anashuka Airport alikuta kitu cha kushangaza sana. Anasema alikuta umati mkubwa wa watu ukimsubiri pamoja na Waziri wa Michezo wa nchi hiyo pamoja maofisa wa ngazi za juu wa Polisi na Jeshi huku kukiwa na Red Capet kisha akapigiwa saluti huku akisindikizwa na mizinga ishirini na moja.Hata hivyo mwanamuziki huyo anasema alifikia uamuzi wa kujiita the milonea Mr Nice baada ya kuingia mkataba na kampuni ya TBL kupitia bia yake ya Safari alifanya shoo mikoa yote ishirini n tano kwa pesa ndefu na kufanya kuwa mwanamuziki mwenye pesa nyingi Afrika Masharki kuliko mwanamuziki yeyote. Mambo mengine ya kushangaza aliyokuwa nayo mwanamuziki huyo kipindi akiwa na pesa ni juu ya msafara wake uliokuwa umejaa wapambe wengi na kulazimika kutumia magari zaid ya nane kwenye mizunguko yake huku yakiwa hayazimwi Ac masaa ishirini na nne hata kama hayana watu ndani. Aidha Mr Nice alimaliza kusema kuwa anawashauri wanamuziki wa sasa kujifunza kwa waliopita ili nao yasijekuwakuta kama yaliyowakuta wao. 
CREDIT: XDEEJAYZ TANZANIA
Viewing all 45984 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>