Quantcast
Channel: VIJIMAMBO
Viewing all 45984 articles
Browse latest View live

Picha ya kwanza ya Ibra da hustler kwenye kituo cha kusaidia walioumizwa na dawa za kulevya.

$
0
0
Rehema Chalamila ‘Ray C’ baada ya mchakato wakutafuta logo kwa ajili ya foundation yake ya kupambana na kusaidia vijana wasiingie kwenye matumizi ya dawa za kulevya hatimaye ameanza kazi.

Ray C ametembelea kituo cha vijana walioamua kuachana na matumizi ya dawa za kulevya na tabia hatarishi huko Kigamboni ambapo kwenye kituo hicho Ray C alikutana na msanii aliyekua wa Nako II Nako Ibra Da Hustler.

Ibra yupo kwenye kituo hicho na vijana wengine walioachana matumizi ya dawa za kulevya ambapo Ray C amemuhoji hivyo hiyo interview itaonekana kwenye program inayoandaliwa na foundation yake.
CREDIT:MILLARD AYO

Ibra akiwa na Ray C.


BURUDANI ZATAWALA KANUMBA DAY DAR LIVE

DUDU BAYA, Amkata Mama Yake Sikio kwa Madai ya USHIRIKINA.

$
0
0
Msanii mkongwe wa miondoko ya Hip Hop nchini Tanzania ajulikanae kama DUDU BAYA, anatafutwa na POLISI kwa mashtaka ya kumkata MAMA yake MKUBWA sikio kwa madai ya kishirikina. Kwa mujibu wa kituo cha redio cha mjini Dar Es Salaam CLOUDS FM mtandaoni wamesema…….. ”Kwa mujibu wa mdogo wake aitwaye Muweta alisema kuwa siku ya tukio msanii huyo alimfuata mama yake huyo nyumbani kwake na kumlaza kwenye makochi na kuanza kumkata sikio kwa kisu huku akimwambia kwanini anamroga baada ya kufanya tukio hilo alitokomea kusikojulikana”
DUDU BAYA ni msanii ambae katika fani yake ya muziki hapa nchini hiyo ni moja ya tabia zake kama anavyojulikana kwa UGOMVI, UONEVU na mambo ya ukorofi baina ya Wasanii wenzake mpaka kwa mashabiki. Kutokana na mila na desturi za kitanzania, binadamu kama hawa hawatakiwi kuwepo kwenye jamii tulivu sababu wao ndio wanahatarisha amani kwa wananchi. Kitendo tu cha kukatwa sikio kwa kisu, tena ukizingatia anaemsababishia maumivu hayo ni MWANAMKE, hiki ni kitendo cha kinyama kiasi gani?….. kuweza kufikia kufanya kitendo cha kinyama kama yeye sio bianadamu. Serikali iangalie na itilie mkazo utafutwaji na aweze kuikabiri vyombo vya sheria, sababu itakuja story nyingine kuwa kamkata sikio mwananchi mwingine.
Credit:Ngongamix

MHE. BERNARD MEMBE, NAIBU SPIKA JOB NDUNGAI WAONGELEA SWALA LA RAIA PACHA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI MAREKANI

$
0
0

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa Mhe. Beranard Membe akiongoza mazungumuzo ya Raia Pacha alipokua akiongea na Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV Bwn. Idd Sandaly na Katibu wake Amos Cherehani (hawapo pichani) wakiwemo maafisa wa Ubalozi na baadhi ya WanaDMV kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani siku ya Jumanne April 8, 2014 alipokaribishwa chakula cha jioni Ubalozini hapo huku Naibu spika Mhe. Job Ndungai akiongezea mawili matatu. Chini ni Audio ya mazungumuzo hayo.
Mhe. Bernard Membe akiongelea swala la Raia pacha kulia ni naibu spika Job Ndungai akifuatilia mazangumuzo hayo.

Kushoto ni Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV Rasi Idd Sandaly na Mhe. Balozi Liberata Mulamula wakifuatilia mazaungumuzo
 Kikao kikiendelea kwa picha zaidi bofya soma zaidi na picha zaidi baadae


HALIMA KIMWANA AFUNGUKA KUHUSU MASTAA KUMTONGOZA DIAMOND

$
0
0
Aliyejipachika kuwa dada wa hiyari wa Mbongo-Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye ni zao la Shindano la Kimwana Manywele, Halima Haruna ‘Kimwana’ amefungukia ishu ya mastaa kibao kujitongozesha wenyewe kwa jamaa huyo
Halima Kimwana alielezea sakata hilo wikiendi iliyopita baada ya kuulizwa undani wa skendo inayomkabili ya kumkuwadia au kumtongozea Diamond kwa mastaa na kuwabadilisha kama nguo.
Kwa mujibu wa Halima Kimwana, huwa Diamond hajisumbui kumtongoza mwanamke zaidi ya hao mastaa kujitongozesha wenyewe kwake.

Halima Kimwana alidai kwamba yeye kama dada wa mwanamuziki huyo (hakutaka kufafanua dada kivipi), amefikia hatua ya kusumbuliwa na wasichana wa kila aina hasa mastaa wakimuomba awatongozee kwa Diamond tena kwa ahadi kemkemu.
“Kwani unafikiri Diamond anajihangaisha kuwatongoza hao mastaa? Wao ndiyo kila kukicha wanamsumbua na kutuhangaisha sisi wakitaka tuwatongozee kwa kaka yetu.

Tena wengine wanatoa ahadi nyingi tu kama tukiwafanikishia,” alisema Halima Kimwana na kuongeza kuwa katika listi hiyo ya mastaa wanaojitongozesha kwa Diamond, wapo mastaa wakubwa ambao anawahifadhi ili asiwavunjie heshima.

GPL

SHANGAZI YA RAIS OBAMA AFARIKI DUNIA

$
0
0
Shangazi wa rais Barack Obama Zeituni Onyango wakati wa uhai wake huko Boston.
Shangazi wa rais Obama Zeituni Onyango ambaye kwa wakati fulani alinyimwa hifadhi hapa Marekani lakini akaendelea kuishi kinyume cha sheria kwa miaka kadhaa katika jimbo la Masachussets amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 61.
Wakili wa masuala ya Uhamiaji wa Onyango amesema amefariki katika hospitali moja baada ya kuugua ugonjwa saratani na matatizo ya kupumua . Aliugua tangu mwezi January.
Onyango alihamia Marekani kutoka Kenya mwaka 2000 na alinyimwa hifadhi ya kisiasa na jaji wa Uhamiaji mwaka 2004. Hakuondoka nchini na aliendelea kuishi kwenye nyumba za umma huko Boston. Hali yake ya ukaazi wa Marekani ilitangazwa hadharani siku chache kabla ya Bw.Obama kuchaguliwa rais Novemba 2008.

Wema Sepetu ''IN MY SHOES'' Episode 19

NYAMA CHOMA....MBUZI...CHIPS YAI...MANDAZI..VITUMBUA...MAMBO SASA KUANZIA IJUMAA HII MGAHAWA KUFUNGULIWA WASHINGTON DC!


YANGA YAIBUKA NA POINTI TATU KWA MABAO 2-1 DHIDI YA KAGERA, AZAM v/s RUVU MCHEZO UMEAHIRISHWA

$
0
0

Wachezaji wa Yanga, wakishangilia bao la pili lililofungwa na Didier Kavumbagu (pichani wa pili kushoto) katika dakika ya 34 ya kipindi cha kwanza, huku bao la kwanza likifungwa na Hamis Kiiza katika dakika ya 3, mabao yaliyodumu hadi mwisho wa mcheo huo. 
Bao la kufutia machozi la Kagera Sugar, lilifungwa na Daud Jumanne, katika dakika ya 63 baada ya beki wa Yanga Oscar Joshua, kujaribu kumrudishia kipa wake mpira wa kichwa uliokuwa mfupi na kunaswa na mshambuliaji huyo aliyemchambua kipa wa Yanga, Deogratias Minishi. 
Hadi mwisho wa mchezo huo Yanga ya Jijini Dar es Salaam, 2 na Kagera Sugar ya Mjini Bukoba 1. Na katika habari kutoka Mlandizi zinasema kuwa mchezo kati ya Azam Fc na Ruvu Shooting, umeahirishwa kutokana na Uwanja wa Mlandizi Mabatini kujaa maji kutokana na mvua iliyonyesha leo, na mchezo huo sasa unatarajiwa kuchezwa kesho.
Mabeki wa Kagera Sugar, akimdhibiti Simon Msuva.
Didier Kavumbagu, akitunishiana msuli na wachezaji wa Kagera Sugar.
Hii si Sarakasi bali ni moja kati ya staili ya kuokoa hatari....
Hapa si kwamba wanacheza Bruzi, bali ni beki wa Kagera Sugar akijaribu kumdhibiti mshambuliaji wa Yanga, Didier Kavumbagu.
Sio kwamba ni staili ya kwenda mpaka chini, bali hapa beki wa Kagera Sugar, akiendelea kumdhibiti Kavumbagu.
Simon Msuva, akijiandaa kupiga Krosi.
Didier Kavumbagu (kulia) akimfinya beki wa Kagera Sugar.
Sehemu ya mashabiki wa Yanga.
Hussein Javu, akimburuza beki wa Kagera Sugar.

ZIARA YA KINANA KASULU YALETA NEEMA KWA CCM

$
0
0

  •  Zaidi ya watu 700 wajiunga na CCM akiwemo aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF Kata ya Rungwe mpya.
  • Asema mtaji wa vyama vya Upinzani ni matatizo ya wananchi na hawasaidii katika kuyatatua badala yake wanataka wananchi waendelee kuumia ili wao wajijenge kisiasa .
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Nyenge  kata ya Kurugongo wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma ikiwa sehemu ya ziara yake mkoani humo.
 Mbunge wa Viti Maalum Ndugu Josephine Gezabuke akihutubia wakazi wa kijiji cha Nyenge kata ya Kurugongo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo na mgeni wa heshima alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa ofisi ya Tawi CCM kata ya Kurugongo wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akila karanga za kuchemsha pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye baada ya kumaliza mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya michezo shule ya Msingi Nyenge kata ya Kurugongo wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma.
 
 Balozi Ali Abeid Karume akicheza ngoma ya asili ya Kasulu wakati wa mapokezi kwenye viwanja vya Stendi ya taxi Kasulu mjini.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Ndugu Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Kasulu mjini kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kituo cha stendi ya Taxi na kuwaambia wananchi hao CCM imedhihirisha kuwa komavu kwenye demokrasia ya kweli na hali inavyoendelea hivi sasa wapinzani wameanza kupotea kabisa kwenye siasa kwani kwenye uchaguzi wa madiwani kati ya kata 27 walipata tatu, ubunge Kalenga na Chalinze wameanguka vibaya sana .
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa Kasulu mjini na kuwaambia kuwa CCM itaendelea kuhakikisha maendeleo yaliopangwa yanazidi kutekelezwa licha ya kuwa na changamoto mbali mbali hasa wapinzani kutaka wananchi wateseke ili wao wajijenge kisiasa alisema sivyema vyama pinzani kutafuta  sifa kwenye matatizo ya wananchi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwainua juu wanachama wapya waliojiunga leo kutokea vyama vya upinzani kulia ni Ndugu Nahasoni Kigamba alikuwa Mwenyekiti wa CUF kata ya Rungwe mpya na Adolf Yanda aliyekuwa Katibu wa Chadema kwa wanafunzi wa chuo cha SUA,katika mikutano miwili mikubwa ya leo zaidi ya wanachama 700 walijiunga na CCM .

Samba Boys ruksa ngono Scolari awaruhusu Brazil kuwa na wapenzi wao

$
0
0
Kocha wa Timu ya Taifa ya Brazil, Luiz Felipe Scolari amewaruhusu wachezaji wake kuendelea kufanya ngono wakati wa mechi za Kombe la Dunia linaloanza Juni mwaka huu nchini Brazil.

Scolari alisema kwamba hakuna marufuku yoyote ya wachezaji kuwa na wapenzi au wake zao wakati wa mashindano hayo na kwamba watatakiwa kuendelea na mfumo wao wa kawaida wa mapenzi na si vinginevyo.

Imekuwa kawaida baadhi ya timu kuweka marufuku ya wachezaji kuwa na wake au wapenzi wao nyakati za mashindano makubwa kwa ajili ya kutaka kuwaweka wachezaji kuwa katika mazingira ya kimchezo na kukita akili kwenye mechi inayofuata.

England ni moja ya timu inayolaumiwa kwamba imekuwa ikifanya vibaya kwenye michuano ya kimataifa kutokana na athari za kuwapo wake au wapenzi wao kwenye kambi ya timu na kubadili maana nzima ya timu ilichokwenda kufanya.
Samba Boys, hata hivyo, watakuwa huru kujirusha wakati wote wa mashindano lakini lazima wahakikishe wanakuwa fiti kimchezo wakati wote, ameonya kocha huyo maarufu aliyepata pia kuwafundisha Chelsea.

“Mapenzi kikawaida yanaruhusiwa kwa wachezaji wetu, kwa njia mbayo itawapa uwiano mzuri na kwa mfumo usio mbaya maana kuna wengine wanafanya mithili ya kuruka sarakasi, sasa hiyo haifai wala kuruhusiwa,” akasema Big Phil ambaye pia ni Mbrazili.

Katika michuano ya Kombe la Dunia 2002 Scolari alikuwa mkali sana kwenye masuala hayo, ambapo aliwapiga marufuku wachezaji wake kujiingiza kwa namna yoyote ile kwenye vitendo vya ngono wakati wote wa mashindano hayo, ili kuhakikisha wanatwaa kombe, na kweli wakalitwaa.

Ronaldo alikasirikia hatua ya kuzuiwa kufanya ngono, akasema pamoja na kufurahia kutwaa kulinyanyua kombe hilo kwa furaha, kitu kingine ambacho hatakisahau ni walivyozuiwa kufanya ngono na kocha huyo mkali hivyo kumfanya awe na wakati mgumu kipindi chote cha mashindano hayo.

WADAU HII IMEKAAJE ?

$
0
0
KATUUNI HII IMELETWA KWENU KWA IDHINI YA MDAU WETU MARCO TIBASIMA

Korason by Jay fire ( Video Official 2013)

MH:MWIGULU NCHEMBA ATIMIZA AHADI YA KUSAMBAZA MAJI JIMBONI KWAKE

$
0
0
Mh: Waziri wa Maji Prof.Maghembe akiwa ameambatana na Mbunge wa Iramba Mh:Mwigulu Nchemba wakitoka kwenye Tanki Kubwa la Kutunzia maji ndani ya Kijiji cha Nang'uli.
Waziri wa Maji Mh:Maghembe akizindua Mradi Mkubwa wa Maji Kijiji cha Nang'uli Jimbo la Iramba hii leo,Kulia ni Mh:Mwigulu Nchemba akishuhudia tendo kubwa la Maendeleo ndani ya Jimbo lake.
 Hatimaye Wananchi wa Kijiji cha Nang'uli na Vijiji Vya Jilani wamepata Mkombozi wa Maji,Mh:Mwigulu Nchemba akimtwisha Ndoo Mama wa
Kijijini hapo kuashiria Wamepata Mkombozi wa Maji.
Wananchi wakiwa na Furaha mara baada ya Kukabidhiwa Mradi wa Maji Kijiji cha Nang'uli hii leo.Wananchi wameunda Uongozi wao unaosimamia Uuzaji wa Maji kwenye Chanzo hiki,Ndoo Moja inauzwa Sh.25 tu.Mh:Mwigulu Nchemba akipokelewa na Wananchi wa Kata ya Kinapanda hii leo.Wananchi wa Kinapanda wakifuatilia Mkutano kuhusu Maji yatakavyoanza kupatikana Mapema kabla ya Mwaka huu Kuisha.
 Mh:Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa Kata ya Kinapanda kuwaeleza namna anavyoanza kutimiza ahadi yake ya Maji kwenye Kata hiyo,Mh:Mwigulu Nchemba amemleta Mh:Waziri wa Maji kwaajili ya Kutoa kauli yake kuhusu hatma ya Maji ndani ya Kata ya Kinampanda.Waziri Maghembe ameahidi kuwa Kufikia Mwezi wa 12 Mwaka huu,Makao makuu ya Kata ya Kinampanda yatakuwa na Maji ya Kutosha na Wataanza Kusambaza Maji vijiji vya Jilani.Mh:Maghembe akisalimiana na Wananchi wa Ulemo-Iramba wakati akiwasili kwenye Mkutano wa Kuzungumza nao kuhusiana na Upatikanaji wa Maji ndani ya Kata yao na namna Serikali Ilivyojipanga kusambaza Maji Vijijini.
Viongozi wakibadilishana Mawazo,Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mh:Yahya Nawanda,Katikati ni Waziri wa Maji Mh:Maghembe na Mwisho Kulia ni Mh:Mwigulu Nchemba Naibu Waziri wa Fedha na Mbunge wa Jimbo la Iramba.
 Mh:Mwigulu Nchemba akimshukuru sana Waziri wa Maji kwa Kufanikisha Miradi ya Maji katika Jimbo lake hasa Kata ya Ulemo,Kinampanda,Kiomboi,Ndago na Kijiji cha Nang'uli.
Waziri wa Maji Prof,Maghembe akizungumza na Wananchi wa Ulemo kuhusiana na Utekelezaji wa Mradi wa Maji ndani ya Kata yao.Waziri ameahidi kuwa Serikali imetenga zaidi ya Sh.800 Milioni kwaajili ya Kusambaza Maji kata ya Ulemo.Zoezi hilo limekabidhiwa kwa Mhandisi wa Mkoa/Wilaya na Ofisi ya Mkurugenzi tayari kwaajili ya Kuanza kutimizwa."Maji safiiiiiiiiiiiiiiii"
 Wananchi wa Kijiji cha Nang'uli wakishangilia Kupata Maji ndani ya Kijiji Chao.
Waziri wa Maji Mh:Maghembe hii leo amefanya ziara ya Kukagua Maendeleo ya Utekelezaji wa Miradi ya Maji Jimbo la Iramba,Katika hatua hiyo Mh:Maghembe amefungua Rasmi Mradi wa Maji wa Kijiji cha Nang'uli na Kuukabidhi kwa Wananchi Waanze kuutumia.

Mbali na Kufungua Mradi huo,Akiwa ameambatana na Mbunge wa Iramba Mh:Mwigulu Nchemba,Prof Maghembe amezungumza na Wananchi wa Kata ya Kinampanda na Ulemo kuhusu Mpango wa Kusambaza Maji ndani ya Vijiji vya Kata hizo pia Kuchimba Visima Vikubwa vya Maji ilikuwezesha Upatikanaji wa Maji ya Uhakika kwa Wananchi.
Maghembe amesema "Serikali imetenga Fedha zaidi ya Milioni 80 kwa Kijiji cha Uleo kwaajili ya Kusambaza Maji,Pia Imetenga fedha kwaajili ya Kuchimba Kisima Kikubwa kata ya Kinampanda kwaajili ya Kupata Maji mengi na hatimaye yasambazwe Vijiji mbalimbali ndnai ya Kata hiyo,Mh:Maghembe amewasihi Wananchi kuunga mkono Juhudi hizo zinazofanywa na serikali ya CCM,Pia amempigia Chepuo Mh:Mwigulu Nchemba kuwa amekuwa Moja ya Wabunge wanaofuatilia sana Mahitaji ya Wananchi wake hasa Maji.
Mbali na Mh:Maghembe,Mbunge wa Iramba N/Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa Kinampanda amesema atahakikisha anatimiza kile alichokiahidi kabla hajakwenda kuomba ridhaa ya kuwaongoza tena wananchi wa Iramba,"Niliwaahidi maji hapa,nitahakikisha Maji yanapatikana Kabla ya Mwaka 2014 kumalizika,Nashukuru Waziri ametoa kauli kuwa Fedha zipo kilichobaki ni utekelezaji tu,Mkataba wangu na Nyie Wananchi ni Maendeleo tu,Nikishindwa Kuwaletea Maendeleo ni Kutowatendea haki".Mwigulu.
Wakizungumza kwa Nyakati tofauti Wananchi wa Nang'uli na Ulemo wametoa Pongezi zao za dhati kwa Mbunge wao Mwigulu Nchemba kwa Kuwapelekea Maji,Wamesema Wanaona Kazi anayoifanya kwenye Umeme,Elimu,Afya na sasa amewapelekea Maji,Hivyo hawahitaji Kumpoteza kiongozi huyo kwakuwa ni Mchapakazi sana.
Habari/Maelezo na Sanga Festo

MABASI MAPYA YA SHABIBY NDIYO HABARI YA MJINI JE VYOO HIVI VITATUMIWA KWA USTAARABU AU ITAKUWA KAMA YALE YALE YA VYOO VYA TAIFA?

$
0
0
VYOO VILIVYOMO NDANI YA MABASI HAYO YA MWENDO KASI NCHINI
HAPA MOJA YA BASI HILO LIKIWA KWENYE KITUO CHA MAFUTA CHA SHABIBY MKOANI DODOMA WIKI ILIYOPITA KABLA YA KUANZA SAFARI
HAPA BASI HIZO KWA NDANI KAMA ZINAVYOONEKANA
MABASI HAYO YAKIWA YAMEJIPANGA KWENYE YADI YA SHABIBY DODOMA MJINI KWA HATUA ZA MWISHO KABLA YA KUANZA SAFARI ZAKE.
MWANDISHI WA BLOG YA XDEEJAYZ TANZANIA 
BW. LIVINGSTONE MKOI AKIKAGUA KAGUA MABASI HAYO BAADA YA KUPEWA MWALIKO WAHESHIMA NA MH SHABIBY KWENYE UZINDUZI WA MABASI HAYO.
MWANDISHI HUYO AKIPIGA PICHA KAMA KUMBUKUMBU NDANI YA MABASI HAYO YA KISASA.
Na Sakina Shabani -Dodoma
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mabasi mapya yaendayo kasi ya ajabu yliyoshushwa na kampuni ya Shabiby Line yamezidi kuwa gumzo kutokana na wananchi wengi kuyakimbilia huku wakiponda mabasi mengine.
Habari toka Mkoani Dodoma ndiko makao makuu ya kampuni hiyo ukiacha Gairo zinasema kuwa wananchi wengi kwa sasa wamekuwa wakitaka kupanda mabasi hayo kwa ajili ya kujihakikishia usalama wao na kila siku ya mungu mabasi hayo hujaa siti zake mapema.
Akiongea na Xdeejayz meneja wa Kampuni hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Saidi alisema" Dada unajua haya mabasi ni mapya hivyo wananchi wengi wanahitaji kusafiri salama na haraka hivyo kwa siku mabasi yote hujaa hali inayowafanya abiria kubuku safari siku mbili kabla kwa kuhofu kukosa nafasi ndani mabasi hayo" Alisema
Hata hivyo pongezi za dhati zimfikie Mbgunge wa Jimbo la Gairo Mh' Ahmed Shabiby kwa kuonesha upendo kwa watanzania kwa kuwaondolea adha za usafiri kwani mabasi hayo mapya 26 yameanza safari wiki iliyopita na lengo lake ni kabla ya mwaka huu kumalizika atashusha mengine kama haya kwa ajili kukidhi haja ya usafiri mikoa yote Tanzania. CREDIT:XDEEJAYZ

WATUHMIWA SUGU WA KUCHAKACHUA VIROBA VYA KONYAGI WASHINDWA DHAMANA NA KURUDISHWA RUMANDE.

$
0
0
Watuhumiwa wa Kuchakakachua bidhaa za kampuni mbalimbali wakisindikiwa mahakamani kujibu tuhuma zao leo mida hii katika mahakama ya mjini Moshi Tanzania.(Picha kwa hisani ya Mtandao wa prhabari.blogspot.com)



WAELEZEWA NI WATU HATARI SANA WAIOFAA KUACHILIWA KWA DHAMAN

WANATUHUMA KILA PEMBE YA NCHI IKIWEMO DAR ES SALAAM

YAELEZWA, KONYAGI FEKI WANAZOTENGENEZA ZIMEATHIRI WATANZANIA WENGI 

BAADHI YA WAMILIKI WA MABAA WALIOHUDHURIA MAHAKAMANI HAPO WAMETOA RAI KWA WANANCHI KUACHA KUNUNUA KONYAGI VICHOCHORONI NA BADALA YAKE KWENYE MABAA HALALI AU MADUKANI


MAHAKAMA ya hakimu mkazi Moshi, leo imefurika mamia ya wananchi waliokwenda kushuhudia watuhumiwa sugu wa utengenezaji wa konyagi feki na bidhaa nyingine mbalimbali na kuzibandika nembo za TRA ambayo inadiwa kudhuru maelfu ya watanzania.

Hata hivyo mahakama ya mkazi moshi imewaachia kwa dhamana watuhumiwa hao nane ambao wanakabiliwa na tuhuma za kutumia alama za biashara za makampuni mengine kwa nia ya kutapeli.nakujipatia pesa kinyume cha utaratibu.

Watuhumiwa hao ni Yusuph George, Richard Leonard, Preygod Urassa, Mohamed Rashid, Greyson Jonathan, George Kisivani, Hagai Nelson na Jackson Shayo, ambao wanatuhumiwa kwa pamoja kwa
kutumia kwa nia ya kutapeli alama ya biashara ya Konyagi kinyume cha sheria huku wakijua wazi ya kuwa alama hiyo ni ya kibiashara ya halali ya kampuni ya Tanzania Distilleries Limited.

Watuhumiwa hawa wana kesi mbalimbali ikiwemo ile ya kutumia nyaraka za mamlaka ya mapato nchini TRA ikiwemo mihuri yenye namba za kodi ya mapato jambo ambalo linadaiwa kuikosesha serikali mapato mengi.

Wakili wa serikali Julius Semali ameiambia mahakama ya mkazi Moshi kuwa watuhumiwa hao ni hatari na kwamba wanakabiliwa na kesi za namna hiyo maeneo mbalimbali hapa nchini.

Singida wana kesi ya namna hii na ambayo itaendelea tena Aprili   30, 2014, Ilala wanatafutwa na polisi kwa kukutwa na nyaraka za TRA wakati Arusha wanatafutwa kwa kukiuka dhamana na kutoroka mwaka 2012.

Pamoja na kupewa dhamana kwenye kesi hiyo huko Moshi, bado hakimu aliamuru warudishwe rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Kesi hii imevutia wammia ya wakazi ambapo miongoni mwao ambao ni wafanyabiashara za mabaa wametoa wito kwa wananchi kuepuka kunywa konyagi vichochoroni kutokana na madhara ambayo wameshapata watu wengi.

KANALI MASSAWE AISHUKURU VODACOM KUIKOMBOA GOZIBA.

$
0
0

 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Fabian Massawe (wa tatu kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Muleba Lembris Kipuyo (wa pili kushoto) wakiwa pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom ambao baadhi yao walifundishwa na Kanali Massawe wakati alipokuwa Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Jitegemee jijini Dar es salaam.Kanali Massawe alifika Makao Makuu ya Vodacom kwa shughuli za kikazi ambapo alivuta hisia za wafanyakazi waliowahi na hata ambao hawakuwahi kupitia mikononi mwake enzi za ualimu na hivyo kuleta hali ya furaha ikitawaliwa na utani na ukumbusho wa matuko ya Shule.
 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Fabian Massawe akifurahia jambo na Mfanyakazi wa Vodacom Shomary Shomary mara baada ya kukumbushana enzi za Kanali Massawe alipokuwa Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Jitegemee wakati huo Shomary nae akiwa ni mwanafunzi shuleni hapo. Wawili hao walikutana wakati Mkuu huyo wa Mkoa alipofika Makao Makuu ya Vodacom kwa shughuli za Kikazi.Kanali Massawe ni mmoja wa waliowahi kuwa Walimu wakuu na kupata heshima na sifa kubwa hapa nchini.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Fabian Massawe akihojiwa na Mhina Shemweta wa kampuni ya Gin Din inayotoa huduma za ushauri wa masuala ya Mawasiliano kwa kampuni ya Vodacom Tanzania. Katikati ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim. Kanali Massawe alifika Makao Makuu ya Vodacom jijini Dar es salaam kwa shughuli za kikazi.

Ni ya kwanza kufikisha huduma za mawasiliano, Afya

Dar es Salaam, April 9, 2014 … Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe, amezungumzia jinsi ambavyo uboreshawaji wa huduma za mawasiliano zinavyochochea kubadili maisha ya watu kupitia kuboreka kwa shughuli za kiuchumi na kijamii huku akipongeza maamuzi ya kampuni ya Vodacom ya kupelekea mawasiliano kwenye kisiwa cha Goziba kilichopo Ziwa Viktoria eneo la mkoa wa Kagera.

Kanali Masawe, ameyasema hayo wakati alipotembelea Makao Makuu ya Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom jijini Dar es salaam na kukutana na Ofisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wake Georgia Mutagahywa ikiwa ni sehemu ya kutoa Shukurani kwa kufanikisha kuweka mnara wa simu katika kisiwa cha Goziba pamoja na kusaidia ujenzi wa kituo cha afya kisiwani humo kupitia Vodacom Foundation.

Amesema tangu Goziba ilipounganishwa kwenye mtandao wa simu za mkononi kumekuwepo na mabadiliko makubwa katika maisha ya wakazi wa  kisiwa hicho huku ikisaidiwa kwa kiwango kikubwa suala la ulinzi na usalama na kuifungua Goziba.

“Tunawashukuru sana Vodacom, mmekuwa wa kwanza kufikisha huduma za mawasiliano ya simu kisiwani Goziba na hivyo kuwafanya wakazi wake kuendelea kuwakumbuka kwa namna mlivyowakomboa. “Alisema Massawe.

“Hali ya ulinzi na usalama kwenye kisiwa cha Goziba haikuwa nzuri hata kidogo, kisiwa kilikuwa kikibaliwa na wimbi kubwa la uvamizi wa majambazi waliokuwa wakiwavamia wavuvi na kuwapora fedha na mali zao ikiwemo nyavu na mashine za boti huku wakikosa msaaada wowote kwani kisiwa hakina kituo cha Polisi na hawkauwa na namna ya kuomba msaada kutoka Bukoba kutokana na kukosa huduma za mawasiliano.”

Pamoja na kuipongeza kampuni hiyo, Kanali Masawe amesema kuwa, huduma hizo za Mawasiliano pia zimefungua fursa za kiuchumi kwa wakazi wa kisiwa hicho ambacho sasa wanawasiliana moja kwa moja na watu walioko katika maeneo mengine ya nchi na hata nje ya Nchi hususa Nchi jirani ya Kongo ambayo wanafanya nayo biashara ya kuuza dagaa.

“Hali hii imeimarisha shughuli za uvuvi ambao ndio msingi wa maisha ya wanaGoziba kwani pia kwa sasa wanawasiliana na wachuuzi wa bara na hata nje ya nchi hususan Congo DRC ambao ni wanunuzi wakubwa wa samaki na dagaa wa kutoka Goziba na hivyo kuw ana uhakika na soko na hivyo kupunguza usmbufu na gharama za biashara, hili ni jambo litakaloendela kukumbukwa na kuheshimiwa na wana Goziba na mkoa kwa ujumla.”

Akizungumzia ujenzi wa kituo cha afya, Mkuu huyo wa Mkoa amesema kama ilivyo kwa huduma za mawasiliano, kisiwa cha Goziba hakikuwa na huduma za afya na hivyo kuwafanya wakazi wake kuishi katika mazingira magumu.

Kisiwa cha Goziba kilichomo nfdanmi ya eneo la kiutawala la Wilaya ya Muleba kipo umbali wa zaidi ya Maili 20 kutoka Bukoba ikiwachukua wakazi wake safari isiyopungua ya saa kati ya 9 hadi 10 kufika huduma za kijamii ikwemo afya.

“Tunawashukuru pia Vodacom kupitia mfuko wake wa kusaidia Jamii kwa kutusaidia kwenye ujenzi wa zahanati likiwa ni ombi la wananchi hao wakati w ahafla ya uzinduzi wa mnara. Mngeweza kusema huduma za mawasiliano zimetosha lakini mlikubali pia kusaidia ujenzi wa Zahanati ya kwanza ksiwani humo ambayo inasbiriwa kwa hamu na wananachi.”

“Serikali ya Mkoa ina mpango wa kuipandisha hadhi Zahanati hiyo hiyo kuwa kituo cha afya pindi tu ujenzi wake utakapokamilika ili kiwe na uwezo wa kutoa huduma nyingi na bora zaidi kwa wananchi.”Aliongeza  Massawe.

Mkuu huyo wa Mkoa amesema kilichofanywa na Vodacom kwa watu wa Goziba cha kuwafikishia mawasiliano na huduma za afya ni jambo lililoacha alama kwa wakazi wa Goziba na Kagera kwa ujumla. Ni upendo wa hali ya juu wa kampuni kwa wananchi wanaowzunguka ni vema wengine wakaona kazi hii kubwa na nzuri ya Vodacom ili nao wajitoe kwa jamii ikiwemo za pembezoni ambazo zinakabiliwa na changamoto mbalimbali za kijamii.”
Kisiwa cha Goziba bado hakina shule na kituo cha polisi.

TUKIO KATIKA PICHA: HUU NI UBUNIFU MK UBWA NA WA KIPEKEE KUTOKA MKOANI IRINGA! TAZAMA HAPA

$
0
0

Kenny Mwangoka akiendesha gari hilo ambalo bodi lake limetengenezwa kwa mbao


Kenny Mwangoka akifungua mlango wa nyuma wa gari hilo akionesha umadhubuti wa bori lake

Mwanahabari huyu Oliva Motto wa Star TV hakuamini kama kilichounda bodi ya gari hilo ni mbao mpaka alipogusa na kujiridhisha

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Peter Tweve akimpongeza Mwangoka kwa ubinifu huo

Na Francis Godwin, Iringa

Amini usiamin. Bodi la gari hili aina ya Hiace lenye namba za usajili T921 BME limetengenezwa kwa mbao aina ya mlingoti na pine. Linamilikiwa na mvunaji na mfanyabishara wa mbao wa Nyololo, Mafinga, mkoani Iringa Bw.Kenny Mwangoka.

Mwangoka alilinunua gari hilo lililokuwa linamilikiwa na mission ya kanisa katoliki Mafinga baada ya kupata ajali na kuharibika vibaya. Jitihada zake za kulifufua gari hilo kwa kuvisha bodi mpya hazikuzaa matunda na ndipo alipotumia ubunifu huu.
"Mimi mwenyewe ni fundi wa magari, kwahiyo kazi ya kuunda na kuvisha bodi hili la mbao nilifanya mwenyewe," anasema, na kuongeza kuwa baada ya matengenezo hayo gari hilo limekuwa kivutio kikubwa sehemu mbalimbali anazopita nalo.
"Sasa nalitumia kuhamasisha utalii, hasa utalii wa mazingira nikiwa na maana kwamba tukiyatunza mazingira yatatufaa kwa mambo mengi ikiwa ni pamoja na matengenezo ya magari kama hili langu," anasema, na kuongeza kuwa  atalipeleka kwenye maonesho ya nanenane mwaka huu kama moja ya njia za kuhamasisha upandaji wa miti

Matokeo ya UEFA,Wafungaji na Dakika Walizofunga,MAN UNITED,BARCELONA OUT

WEMA KUMSINDIKIZA DIAMOND MAREKANI TAYARI MICHAKATO YA KUTAFUTA VIZA IMEANZA KWA WEMA UNAJUA KWA NINI?

$
0
0
Na Sakina Shabani
Katika hali isiyokuwa ya kawaida na kushtua Mrs Diamond Wema Sepetu amedaiwa kujiandaa na safari ya kuelekea Maarekani akimsindikiza mumewe Diamond.
Nyeti hizo moto moto toka kwa mtu wa karibu na Wema zikisema" Wivu mbaya sana Wema anaondoka na Diamond Marekani hiyo inatokana na kumlinda Diamond anaesubiriwa kwa hamu na maelfu ya watanzania waishio nchini huko" Alisema mtu huyo
wa karibu wa Wema, Wema alitafutwa kupitia simu yake ya mkononi kwa ajili ya kupata ukweli wa mambo lakini kwa bahati mbaya hakuweza kupatikana na kutanabaisha juu ya nyeti hizo.
CREDIT:XDEEJAYZ TANZANIA
Viewing all 45984 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>