Quantcast
Channel: VIJIMAMBO
Viewing all 45918 articles
Browse latest View live

Mwamuziki Mafumu Bilal Afariki Dunia

$
0
0
Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi nchini, Mafumu Bilal Bombenga maarufu ‘Super Sax’ amefariki Dunia Mei 11, 2020.

Mke wa Mafumu amethibitishia kuwa mumewe amefariki, baada ya hali yake kubadilika ghafla.

Mafumu aliyejifinza kupiga Saxophone mwaka 1972 akiwa JKT Makutupora kwenye Brass Band yao, alikuwa akisumbuliwa na Kisukari kwa muda mrefu hali iliyopelekea kukatwa kwa mguu wake mmoja

Mkongwe huyo ameimba kwenye bendi ya African Stars ambayo hata jina lake alilibuni yeye na kutamba na vibao kama Sakatu Sakatu, Mayanga, Maya, Afrika na Dance Dance

Aidha, alitamba pia na bendi kadhaa zikiwemo Maquis, MK Group, Bicco Stars, Bima Lee, African Stars na African Beats 
GPL

Asakwa kwa kumiliki kadi 21 za kupigia kura

$
0
0
amanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani, ACP Wankyo Nyigesa, akiwaonyesha waandishi wa habari kadi bandia za kupigia kura zilizokutwa katika nyumba anayoishi mtuhumiwa Yusuph Makarani wakati wa msako uliofanyika juzi huko Kerege Bagamoyo.

Na GUSTAPHU HAULE -PWANI, Mtanzania

JESHI la Polisi Mkoa wa Pwani linamsaka Yusuph Makarani (50) mkazi wa maeneo ya Kitonga, Kerege wilayani Bagamoyo kutokana na tuhuma za kukutwa na kadi feki za kupigia kura ndani ya nyumba aliyokuwa akiishi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa aliwaambia waandishi wa habari ofisini kwake jana kuwa tukio la kukamata nyara za Serikali lilitokea Mei 7, mwaka huu huko Kerege.

Nyigesa alisema polisi walipata taarifa kutoka kwa wasamaria wema, kuna mtu tapeli ambaye amekuwa akitapeli wananchi mashamba eneo la Mapinga kwa kutumia nyaraka mbalimbali za Serikali.

Alisema baada ya taarifa hizo, askari wake walikwenda haraka katika nyumba ambayo mtuhumiwa alikuwa anaishi na kufanya upekuzi ambao ulisaidia kukamata kadi feki za kupigia kura 21.

Nyigesa alisema kadi hizo zilikuwa hazijajazwa taarifa yoyote, lakini zimewekwa nembo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), huku nyaraka nyingine zikiwa ni mihuri 10 ya viongozi wa vitongoji mbalimbali, fomu za mauziano ya ardhi na vitabu saba vya stakabadhi ya malipo.

“Tulipofanya upekuzi wetu katika nyumba ya mtuhumiwa, tumekamata kadi feki 21 za kupigia kura zikiwa mpya hazijajazwa kitu pamoja na nyaraka mbalimbali za Serikali,” alisema Kamanda Nyigesa.

Alisema mtuhumiwa alifanikiwa kukimbia kabla ya kukamatwa na polisi wanaendelea kumtafuta ili achukuliwe hatua za kisheria.

Kamanda Nyigesa aliwatahadharisha wananchi kuwa wawe makini wanapotaka kununua ardhi kwa kuwashirikisha viongozi wa Serikali wa eneo husika, wakiwemo wenyeviti wa vijiji na maofisa kata, kwa kufanya hivyo kutasaidia kupunguza utapeli.

Katika hatua nyingine, jeshi hilo linamshikilia Hassan Malubara (30) mkazi wa Dunda kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya (mirungi) kilo 17.

Kamanda Nyigesa alisema tukio hilo lilitokea Mei 9, mwaka huu, saa 11 jioni huko Zinga wilayani Bagamoyo.

Alisema wakati polisi wakiwa katika msako wa kudhibiti biashara haramu, walimkamata mtuhumiwa akiwa amepakia mirungi kwenye pikipiki yenye namba za usajili MC 216 BBP aina ya Boxer rangi nyeusi.

Chadema yawafukuza uanachama wabunge wanne

$
0
0

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam, Mtanzania

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimewafukuza uanachama wabunge wake wanne, Joseph Selasini (Rombo) na Anthony Komu (Moshi Vijijini), David Silinde (Momba) na Wilfred Lwakatare (Bukoba Mjini) kwa kukiuka maagizo ya chama na kutoa maneno ya kejeli na kashfa dhidi ya viongozi na maagizo ya chama kwenye vyombo vya habari.

Aidha, kimemvua nafasi zake zote za uongozi ndani ya chama Mbunge wa Viti Maalumu, Mariam Msabaha kwa kushiriki kukiuka maagizo ya chama.

Uamuzi huo umetolewa na Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika leo Jumatatu Mei 11, ambapo amesema wabunge hao wamekuwa wakijitokeza kwenye vyombo vya habari na kutoa maneno ya kashfa na kejeli dhidi ya maagizo ya chama na viongozi.

“Selasini na Komu wamejipotezea sifa ya kuwa wanachama wao wenyewe kwa kutangaza kwenye vyombo vya habari kuwa hawakubaliani na falsafa ya Chadema wanakubaliana na falsafa ya chama kingine.

“Lakini bado wameendelea kutoa maneno ya kejeli na kashfa na kwa mazingira hayo, chama kimeazimia kuwafukuza uanachama na Kamati Kuu imemuelekeza Katibu Mkuu kumwandikia Spika juu ya uamuzi huu.

“Kuhusu Silinde na Lwakatare, si tu wamekiuka maagizo ya chama bali pia wamekuwa wakijitokeza kwenye vyombo vya hanbati na namna nyingine ya mawasiliano na kutoa maneno ya kashfa na kejeli dhidi ya maagizo ya chama na viongozi. Kamati Kuu ya chama imewafutia uanachama kwa kwenda kinyume na katiba, kanuni na maadili na miongozo ya chama.

“Aidha, Kamati Kuu imemjadili Mariam Msabaha, ambaye ameshiriki kukiuka maagizo ya chama wakati yeye ni Mjumbe wa Halmashauri ya chama alitakiwa kuwa mstari wa mbele kufuata maelekezo, hivyo amevuliwa nafasi zake zote ndani ya chama na atatakiwa ajieleze kuhusu ukiukaji huo alioufanya,” amesema Mnyika.

Wanamuziki wa Kiafrika waombwa kushiriki kwenye Mkutano wa ACCES Tanzania, Mwezi Novemba, 2020

$
0
0
Mkutano wa Music In Africa wenye lengo la kudumisha ushirikiano, kubadilishana uzoefu na kutumbuiza yaani (ACCES) unawaalika wanamuziki wa Kiafrika kutuma maombi yao kwaajili ya kushiriki kwenye mkutano huo wa ACCES 2020, utakaofanyika jijini Dar es salaam, kuanzia tarehe 26 hadi 28 Novemba mwaka huu. 

Mkurugenzi wa Music In Africa, Eddie Hatitye, anasema nafasi za upendeleo zitatolewa zaidi kwa bendi na wanamuziki wa Kitanzania kama washiriki wenyeji ili kuonesha ubora wa muziki wa Kitanzania na kubainisha kuwa mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 20/05/2020.

Mkutano huo wa ACCES, ambao umeandaliwa na Music In Africa Foundation (MIAF), hufanyika kila mwaka kwenye miji mbalimbali ndani ya Afrika, na kutoa fursa kwa wanamuziki kukuza na kujenge uwezo wao na kutumbuiza mbele ya hadhira iliyosheheni wageni wa kitaifa na kimataifa, ikiwemo waandaaji wa matamasha, mapromota, mawakala wa muziki, lebo za kurekodi muziki na hadhira yenye ushawishi mkubwa.

Mkutano huo pia unahusisha warsha mbalimbali za mafunzo, mazungumzo ya kitasnia, maelezo muhimu kupitia risala, maonesho ya moja kwa moja (mubashara), vikao vya kukuza umoja na mwasiliano, kurekodi nyimbo kwa pamoja na matembezi mbalimbali kwenye vituo muhimu vya tasnia ya muziki kwenye mji unapofanyika mkutano huo.

“ACCES inatoa nafasi za kushiriki kwa wanamuziki wanaoibuka wenye uwezo wa kutumbuiza moja kwa moja katika majukwaa na wenye utayari wa kutumbuiza katika majukwaa ya kimataifa. ACCES inahitaji washiriki walio tayari kunufaika kupitia mkutano huo kwa kukuza kazi zao kufikia hadhi za kimataifa” anasema Hatitye

Akizungumzia mlipuko wa unginjwa wa COVID 19, Hatitye anasema kuwa, wanafuatilia kwa ukaribu taarifa na kukagua maendeleo ya ugonjwa kwa nia ya kufanya uamuzi unaozingatia taarifa sahihi. 

“Kipaumbele cha kwanza cha Music In Africa Foundation ni usalama na ulinzi wa jamii yetu pana ya muziki na kila mtu anayehusika kutangaza tukio hili muhimu. Tunatumai kuwa ugonjwa wa COVID 19 utaisha mapema na mkutano wetu utaendelea kama ulivypangwa. Hivyo tunakuhimiza kuendelea kujisajili kwaajili ya mkutano na kutuma maombi ya kushiriki kwenye maonesho” anasema Hatitye.

Bonyeza hapa ili kupata Maelekezo ya namna ya kutuma maombi. Pia bonyeza hapa kupata Fomu ya maombi.

Msekwa azungumzia Spika Ndugai kuwalinda wabunge wa Chadema

$
0
0

MWANDISHI WETU -DAR ES SALAAM, Mtanzania

SIKU moja baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuwafukuza wabunge wake wanne na Spika wa Bunge kusema atawalinda, Spika mstaafu, Pius Msekwa na baadhi ya wachambuzi, wamezungumzia hali hiyo.

Wabunge waliofukuzwa ni Anthony Komu (Moshi Vijijini), Joseph Selasini (Rombo), David Silinde (Momba) na Wilfred Lwakatare (Bukoba Mjini) ambao wamefukuzwa kwa tuhuma za utovu wa nidhamu na kauli za kashfa na kejeli dhidi ya chama na uongozi wake na kukiuka makubaliano.

Hata hivyo wakati akihitimisha bunge juzi, Spika wa Bunge, Job Ndugai, alikaririwa akisema yeye ndiye mwenye dhamana ya kuwaapisha wabunge hivyo, wabunge wa Chadema wanaoingia bungeni wasitishwe na mtu yeyote.

MTANZANIA lilimtafuta Msekwa kujua tafsiri za maamuzi hayo lakini alisisitiza kuwa uamuzi wa spika hauhojiwi.

“Haina tafsiri yoyote, ni spika amesema sasa unataka kutafsiri maneno ya spika, ametoa uamuzi wake sasa unauhoji uamuzi wa spika kwanini, una haki gani ya kuhoji maamuzi ya spika…si sahihi.

“Kwanini msihoji uamuzi wa wale waliofukuzwa, si wamewafukuza kwa madaraka waliyonayo…kwa katiba waliyonayo,” alisema Msekwa.

Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCO), Profesa Gaudence Mpangala, alisema Spika anapaswa awe mstari wa mbele kusimamia sheria na katiba za nchi ili kudumisha mshikamano.

“Moja kwa moja wamepoteza ubunge kufuatana na katiba na sheria za Tanzania kwa sababu sheria ya nchi yetu mbunge lazima awe amedhaminiwa na chama cha siasa.

“Utawala wa sheria na katiba ndiyo msingi wa kuleta heshima ya nchi na mshikamano sasa tunashangaa spika anapindisha sheria na katiba za nchi kwa sababu tu ya kisiasa, si jambo zuri anapaswa awe mstari wa mbele kusimamia sheria na katiba za nchi,” alisema Profesa Mpangala.

Akizungumza kwa njia ya mtandao juzi, Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika alisema katika kikao chake kilichofanyika Mei 9 na Mei 10 kwa njia ya video, kwa mujibu wa katiba ya chama, sifa za uanachama wa Chadema kwenye kifungu cha 5.15 cha katiba kinasema mwanachama wa Chadema lazima awe anakubaliana na itikadi na falasafa ya chama.

“Kwa hiyo Komu na Selasini kwa nyakati tofauti walijitokeza mbele ya waandishi wa habari na kutangaza kwamba haakubaliani na itikadi ya Chadema na wanakubaliana na itikadi ya chama kingine na baada ya hapo wameendelea kutoa lugha za kejeli dhidi ya chama na uongozi wake. Hivyo Kamati Kuu ya chama katika kikao chake kimefikia uamuzi wa kuwafuta uanachama,” alisema.

Mnyika alisema wabunge David Silinde (Momba) na Wilfred Lwakatare (Bukoba Mjini) siyo tu wamekiuka maagizo ya chama, bali pia wamekuwa wakijitokeza kwenye vyombo vya habari na njia nyingine za mawasilianao na kutoa maneno ya kashfa na kejeli dhidi yamaagizo ya chama na ya viongozi wa chama.

Katibu Mkuu huyo wa Chadema, alisema kuwa azimio la nne la kamati kuu iliamua kuhusu wabunge wengine ambao walikwenda kinyume na maagizo na makubaliano ya chama na wabunge lakini hawajaonesha utovu wa nidhamu wa ama kukikashifu au kukikejeli chama na uongozi wake.

“Hawa kamati kuu ya chama imeazimia kwamba watakiwe kujieleza ni kwa vipi wasichukuliwe hatua zaidi kwa kukiuka hayo maagizo na makubaliano ya chama na wabunge wafuatao wanaingia kwenye kundi hili.

“Hao ni Suzan Masele, Joyce Sokombi, Latifa Chande, Lucy Mlowe, Sware Semesi, Jafari Michael, Peter Lijualikali, Willy Kambalo, Rose Kamili, Sabrina Sungura na Anne Gideria ambao watatakiwa kujieleza kuhusu uamuzi wao wa kukiuka makubaliano kati ya wabunge na uongozi wa chama.

“Hao wamepewa nafasi hiyo ya ziada kwa sababu tu baada ya kukiuka huko maagizo hawajaonekana mbele ya vyombo vya habari wakihujumu chama,” alisema.

Kuna Watu Hawapendeki, Wasikuumize Kichwa!

$
0
0
KWA uwezo wake Mwenyezi Mungu tumeiona tena Jumatatu hii njema, Mola ametuwezesha tumeweza kukutana pamoja hapa kwenye kilinge chetu cha kupeana elimu ya uhusiano.

Kutokana na jinsi hali ilivyo, ni vyema wapendanao mkachukua hatua za kujilinda na janga hili la Corona.

Mlinde mpenzi wako ili naye akulinde wewe. Kumuacha akiwa hayupo salama, hakumaanishi wewe utakuwa salama, bali ni hatari kwako pia. Jukumu la kujilinda ni la kwenu wote wawili, chukueni hatua stahiki.

Tukirudi kwenye elimu yetu ya uhusiano, kama mada inavyojieleza hapo juu. Kwenye maisha ya uhusiano wa kimapenzi, kila mmoja anaitafuta amani ya moyo wake. Hakuna mtu ambaye anatamani kuishi kwenye shida za uhusiano.

Na katika hali ya kawaida, maisha ya uhusiano yanahitaji kuwa rafiki. Ili muweze kuwa na mafanikio, ni vizuri sana mkawa kwenye ulimwengu ule usiokuwa na makelele. Ulimwengu ambao kila mmoja wenu atafurahia uhusiano wenu.

Kinyume na hapo, maisha ya uhusiano wa kimapenzi yatakuwa magumu mno. Yatakuwa ni mateso. Kuishi kwenye mateso kunapunguza hata siku za kuishi. Kuishi kwenye ulimwengu huo ni sawa na kujipalia kaa la moto. Utateseka sana!

Bahati mbaya sana, licha ya kuwa kila mtu anakuwa na tabia zake, lakini kwa kweli kuna baadhi ya watu wao huwa ni kama wameumbwa kuwa sehemu ya kero kwa mwenzake. Kuna watu ambao unaweza kusema wao kuwa kwenye makelele au ugomvi ni sehemu ya furaha kwao.

anapokaa siku mbili au tatu bila kusababisha jambo ambalo litakutoa kwenye mstari na kukuondolea amani ya moyo, hajisikii raha. Mazungumzo yake siku zote siyo ya kujenga. Zaidi ni kukukera tu ilimradi akuondolee amani ya moyo. Hawa ndiyo watu ambao namaanisha kwamba hawapendeki, hata ufanye nini, huwezi kumbadilisha tabia.

Utafanya kila njia ili angalau kuweza kumbadilisha tabia, lakini mwenzako habadiliki chochote. Yeye ni kawaida yake kukukera. Sasa mtu wa aina hii wa nini kuendelea kuwa naye kwenye uhusiano wa kimapenzi? Mtu ambaye yeye hakupi furaha zaidi ya kero wa nini?

Watu wa aina hii tupo nao kwenye jamii zetu. Wakati mwingine ni vigumu kuwajua, lakini ni lazima tujifunze kuwabaini mapema. Tuwatambue na ikiwezekana kama hujaingia naye kwenye hatua kubwa kama uchumba na ndoa, basi uachane naye mapema.

Mtu ambaye anakuwa si msaada, anakuwa kero huyo ni shida. Unamueleza jambo jema, lakini yeye halimuingii akilini. Jambo ambalo analitamani ni kukupanikisha ili mgombane utadhani vile moyoni anafurahia ugomvi.

Ndugu zangu, maisha ya uhusiano yanahitaji utulivu. Kwa kawaida maisha yamejaa shida na changamoto za kila namna hivyo mahali pekee ambapo mtu anatengemea kupata faraja ni kwa mwenza wake.

Kama una mwenza ambaye hakupi faraja kila siku, huyo ujue kabisa hakufai. Hakuna sababu ya kuishi kwa kudundana au kutoana ngeu ndiyo maisha yaende, jaribuni sana kuepuka hilo mapema. Kama mtu unaona hakuelewi sera zako, analifanya penzi lenu kuwa uwanja wa vita, basi ujue huyo hafai.

Amepoteza sifa na ukimbaini mapema, muepuke. Usijipe presha za bure. Chagua kuwa na amani maishani mwako ili uweze kuishi miaka mingi kwa raha mustarehe.

Kwa leo naishia hapa, tukutane wiki ijayo kwa mada nyingine nzuri. Unaweza kunifuata kwenye kurasa zangu za mitandao ya kijamii, Instagram na Facebook: Erick Evarist, Twitter: ENangale.
GPL

Serikali ya Tanzania yatoa siku tisa kwa wanasoka wa kigeni

$
0
0
By Imani Makongoro, Mwananchi

Dar es Salaam.Serikali ya Tanzania imetoa siku tisa kuanzia leo Jumatano kwa wadau wa soka kutoa maoni yao juu ya idadi ya wanasoka wa kigeni kwenye klabu za Tanzania.

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe hivi karubuni aliitaka Baraza la Micheza Tanzania (BMT) kuandaa mwongozo utakaotumiwa na wadau wa michezo kutoa maoni juu ya idadi ya wanasoka wa kigeni katika wanaopaswa kusajiliwa na kila timu kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara.

BMT imeeleza kuanza kupokea maoni hayo leo na zoezi litafungwa Mei 20.

Ofisa habari wa BMT, Najaha Bakari, amesema kutokana na janga la corona, hawataweza kufanya midahalo ya wadau wa michezo, hivyo watapokea maoni hayo kupitia mitandao ya Baraza la Michezo.

"Zoezi la kupokea maoni litafungwa Mei 20, maoni yatapokelewa kupitia tovuti ya Baraza, akaunti ya facebook na instagram sanjari na kwenye barua pepe ya BMT," amesema.

Mpaka sasa klabu zinaruhusiwa kusajili wanasoka 10 wa kigeni, huku klabu za Simba, Yanga na Azam ndizo zikionekana kufikisha idadi hiyo kwenye usajili wake.

Mwamnyeto rasmi Yanga mchakato umemalizika hivi

$
0
0
By Mwandishi wetu
KWA dili lilivyo, Mwanaspoti linaweza kuthibitisha kwamba imebaki kutangazwa tu Bakari Nondo Mwamnyeto kuwa mchezaji mpya wa Yanga, baada ya wadhamini wa klabu hiyo GSM kumaliza shoo yote.

Awali, Simba walikuwa wamepania kumaliza ishu ya beki huyo, lakini vigogo wa Coastal Union wakaja na masharti magumu huku wakala wa mchezaji akidai thamani yake si chini ya Sh100milioni.

Kigogo aliyesimamia shoo hiyo ya Mwamnyeto, imebainika kuwa ni Mhandisi Hersi Said wa GSM kwa niaba ya Yanga ya Mwenyekiti Msomi, Dk Mshindo Msolla.

Inaelezwa kuwa Dk Msola anaiva sana na Mwamnyeto na alishampa maneno matamu muda mrefu ila ishu ikawa kimya

Mwanaspoti linafahamu kwamba Hersi alitinga barakoa yake na kuwasha gari mpaka Tanga kuweka ishu sawa na klabu ya mchezaji huyo kimya kimya huku Simba wakiwa wametulia zao ndani wakisubiri corona imalizike ingawa tayari walishapeleka ofa yao kwa njia ya mazungumzo ya simu na ikakataliwa kwa madai kuwa ni ndogo.

“Ninachofahamu ni kuwa msimu ujao GSM watatudhamini Coastal Union ikiwa ni moja ya makubaliano ya dili hili la Mwamnyeto na kila kitu kiko wazi,” alisema mmoja wa mabosi wa klabu hiyo mwenye ushawishi mkubwa.

Habari zinasema Coastal Union watapata udhamini wa Sh70milioni kila mwaka kutoka GSM ambayo ni makubaliano tofauti na mchezaji, ambaye sasa wameshapewa ruksa na wanamalizana naye juu kwa juu kuhusu maslahi binafsi.

Mwamnyeto amebakiza takribani miezi 13 katika mkataba wake na Coastal.

Jana, Mwanaspoti lilimsaka Mwamnyeto katika kupata uhakika huo ambapo, licha ya kukwepakwepa alithibitisha kwamba yuko katika hatua za mwisho msimu ujao kuvaa jezi za Yanga.

“Tunaendelea vizuri na kila kitu kipo sawa, najua uongozi wa Coastal Union ulishamaliza upande wao na Yanga na sasa bado huku kwetu kidogo tu tutamaliza,” alithibitisha beki huyo ambaye ni beki wa Taifa Stars.

Ingawa gharama kamili ya usajili huo haijawekwa wazi taarifa kutoka ndani ya familia ya beki huyo ni kwamba, Mwamnyeto ataitumikia Yanga kwa miaka mitatu kuanzia msimu ujao huku gharama kubwa zikitumika kuanzia usajili mpaka mshahara wake.

Kitendo cha Yanga kumchukua Mwamnyeto ni kama kombora la kwanza walilorirusha kwa Bilionea wa Simba, Mohamed Dewji ‘MO’ ambaye bodi yake ndio ilitangulia kumhitaji beki huyo lakini wakachelewa kisa gharama ni kubwa.

Hata hivyo, kutokamilika kwa dili hilo Coastal Union wametaja kuwa ni utata wa meneja wa Mwamnyeto, Kassa Mussa ambaye kwa sasa yupo nchini Italia.

Inadaiwa kuwa kupanda bei ya beki huyo kumetokana na msimamo wa Mussa, ambaye amekuwa akibadilika kila kukicha huku Mwamnyeto mwenyewe kitambo alishakubali kila kitu.

Habari zinasema kwamba Mussa anataka Mwamnyeto aende kucheza soka la kulipwa Ulaya.

Rais Magufuli agawa usafiri kwa maafisa tarafa Rukwa huku wakikisitizwa kutimiza majukumu ya serikali hasa kutoa elimu ya Corona.

$
0
0
Maafisa tarafa za Tarafa 12 za mkoa wa Ruk2wa wakiwa kila mmoja amesimama nyuma ya Pikipiki tayari kwa kukabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kwa niaba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli. 
Afisa Tarafa wa Tarafa ya Namanyere Wilayani Nkasi Kasim Ibrahim akitia saini hati ya Makabidhiano mbele ya Mkuu wa mkoa wa Rukwa pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa ili kukabidhiwa Pikipiki aliyoahidiwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Katibu Tawala wa MKoa wa Rukwa Benard Makali akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo bahasha yenye funguo za Pikipiki ili aweze kutoa Pikipiki kwa Afisa Tarafa (hayupo pichani)kwa niaba ya maafisa tarafa wenzie.
Uongozi wa Mkoa wa Rukwa ukiongozwa na Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Tarafa wa mkoa baada ya makabidhiano ya Pikipiki zilizotolewa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Katika hatua za kuboresha utendaji kazi wa Maafisa Tarafa nchini Rais Wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli ametoa pikipiki 12 kwa Maafisa Tarafa mkoani Rukwa ili ziweze kuwasaidia kutekeleza majukumu yao ya kiserikali katika kata wanazozihudumia.

Pikipiki hizo zimetolewa ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliyoitoa tarehe 04.06.2019 baada ya kufanya kikao kazi na Maafisa Tarafa wote nchini alipokutana nao Ikulu Jijini Dar es salaam.

Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi pikipiki hizo Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo alimshukuru Rais kwa kutimiza ahadi hiyo huku akiwasisitiza maafisa hao kuzitumia pikipiki hizo kwa malengo yaliyokusudiwa na Rais ikiwemo kusimamia mapato, miradi ya maendeleo iliyopo kwenye maeneo yao pamoja na kusikiliza kero za wananchi.

Alieleza kuwa katika ziara zake alizozifanya katika maeneo ya vijijini, alibaini kuwepo kwa mwamko mdogo wa wananchi juu ya ugonjwa hatari wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na virusi vya Corona (Covid-19) hivyo kuwataka maafisa hao kuhakikisha wanavitumia vyombo hivyo kufikisha elimu ya ugonjwa huo hatari.

“Ni Imani yangu kuwa tutavitumia vyombo hivi vya usafiri kuhakikisha kuwa tunawafikia wananchi wetu kwenye maeneo yao ili tuweze kuwahamasisha kujikinga na ugonjwa huu hatari ikiwa ni pamoja na kuvaa barakoa, kunawa mikono kwa maji tiririka mara kwa mara na kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima,” Alisema

Aidha, Alimtaka Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa kuhakikisha anachukua hatua kali za kisheria na kiutumishi kwa Afisa Tarafa yeyote atakayetumia pikipiki hiyo kinyume na malengo ya serikali ikiwemo kutumia kama Bodaboda na kuongeza kuwa pikipiki hizo zina namba za serikali, hivyo, kuzitumia kinyume na malengo yake ni ukosefu wa maadili.

Kwa upande wake Katibu Tawala huyo wakati akieleza mgawanyo wa pikipiki hizo alisema kuwa Mkoa wa Rukwa una Tarafa 16 ambapo Tarafa 4 kati ya hizo zina pikipiki ambazo zimekaguliwa na ziko salama zinaendeelea kufanya kazi na hivyo kuwasisitiza maafisa hao kutekeleza majukumu yao kama yalivyoainishwa katika Waraka Namba 1 wa Maendeleo ya Utumishi wa Umma wa Mwaka 2007.

“Tarafa ambazo hazikuwa na usafiri kwa wilaya ya Kalambo ni Tarafa ya Matai, Kasanga, Mwimbi, Mwazye na Mambwenkoswe zilikuwa hazina usafiri. Kwa Wilaya ya Sumbawanga ni Tarafa ya Itwelele, Kipeta, Lwiche na Mtowisa na Wilaya ya Nkasi ni Tarafa ya Chala, Kate na Namanyere na tarafa ambazo zilikuwa na pikipiki kwa Wilaya ya nkasi ni Wampembe na Kirando na Wilaya ya Sumbawanga ni Laela na Mpui,” Alisema.

Wakati akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Maafisa Tarafa wenzake, Afisa Tarafa ya Kasanga Andrew Ngindo baada ya kumshukuru Rais Magufuli, alimuomba Mkuu wa Mkoa kuona uwezekano wa kutengewa bajeti ya mafuta pamoja na matengezo kwa pikipiki hizo ili ziendelee kuwarahisishia utekelezaji wa majukumu yao.

“Kuwa na Pikipiki ni jambo moja lakini pikipiki ikiwa bila ya Mafuta bila ya uwezeshwaji wa kutosha ni kama tembo mweupe ndani ya nyumba, mimi niwaombe sana wakuu wa wilaya, sisi ndio wawakilishi wao katika maeneo yale ambayo wao wasipofika sisi tukifika maana yake Mkuu wa Wilaya amefika na tayari tumekuwa tumetekeleza makujumu yao, kwahiyo Wakuu wa wilaya watusaidie kupata bajeti hiyo,” Alisema.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli aliahidi kuwapa usafiri maafisa tarafa wote nchini wasio na usafiri na hivyo kutoa pikipiki 448 kote nchini kwaajili ya maafisa hao ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake.

SERIKALI YARIDHISHWA NA UTENDAJI KAZI WA BODI ZA PAROLE NCHINI

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe. Hamad Masauni(Mb) akitoa hotuba katika hafla fupi ya uzinduzi wa Bodi ya Taifa Parole Taifa, leo Mei 14, 2020 katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango, jijini Dodoma.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Suleiman Mzee ambaye pia ni Katibu wa Bodi ya Taifa Parole akitoa maelezo mafupi kuhusiana na utendaji kazi wa Bodi za Parole nchini tangu kuanzishwa kwake mwaka 1994. Leo Mei 14, 2020 katika hafla fupi ya uzinduzi wa Bodi ya Taifa Parole Taifa, katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango, jijini Dodoma.
Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia uzinduzi wa Bodi ya Taifa Parole leo Mei 14, 2020 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Parole Taifa, Mhe. Dkt. Augustino Mrema akisoma taarifa fupi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi azindue Bodi ya Taifa Parole leo Mei 14, 2020 jijini Dodoma.
Mjumbe wa Bodi ya Taifa Parole, Mchungaji wa Kanisa la KKKT Dodoma, Marco Kinyau akijitambulisha mbele ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe. Hamad Masauni(Mb) kabla ya uzinduzi wa Bodi ya Taifa Parole leo Mei 14, 2020 jijini Dodoma. Kulia kwake ni baadhi ya wajumbe wa bodi hiyo.
Meza kuu wakifuatilia utambulisho wa wajumbe wapya wa Bodi ya Taifa Parole. Katikati ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe. Hamad Masauni(kulia) ni Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Suleiman Mzee(kushoto) ni Mwenyekiti wa Parole Taifa, Mhe. Augustino Mrema.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe. Hamad Masauni(meza kuu katikati aliyeketi) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya Taifa Parole(waliosimama). Wa pili toka kulia aliyeketi meza kuu ni Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Suleiman Mzee(Wa pili toka kushoto aliyeketi meza kuu) ni Mwenyekiti wa Parole Taifa, Mhe. Augustino Mrema(Picha zote na Jeshi la Magereza).

Na ASP. Lucas Mboje, Dodoma

SERIKALI imeridhishwa na kiwango cha kazi zinazofanywa na Bodi ya Taifa ya Parole pamoja na Bodi za Parole mikoa katika utekelezaji wa Sheria ya Bodi ya Parole nchini licha uwepo wa changamoto mbalimbali.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe. Hamad Masauni(Mb)katika hafla ya uzinduzi rasmi wa Bodi ya Taifa ya Parole iliyofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango, leo Mei 14, 2020 jijini Dodoma ambapo amewataka kutekeleza wajibu wao ipasavyo kama Rais Dkt. John Pombe Magufuli alivyowaamini na kuwapa jukumu hilo.

“Serikali inaridhishwa sana na kiwango cha kazi mnazozifanya kikamilifu katika urekebishaji wa wahalifu kwa kuwapa wafungwa fursa ya kutumikia sehemu ya adhabu zao wakiwa nje ya magereza kwa usimamizi wa jamii nzima. Hongereni sana”, amesema Naibu Waziri Masauni.

Waziri Masauni amesema kuwa ustarabu wa nchi zote duniani hupimwa kwa kuzingatia namna zinavyoshughulikia uhifadhi salama na urekebishaji wa wahalifu katika magereza.

Aidha, ameongeza kuwa nyenzo kubwa ya msingi zitakazowawezesha wajumbe wa Bodi hiyo ni kujenga uewelewa wa mpango wa Parole , uelewa wa dhana na filosofia yake na umhimu wake katika jamii.

“ Ni muhimu sana ninyi wajumbe wa bodi hii ya Taifa Parole kuielewa sheria yenyewe na taratibu zake kiutekelezaji, dhana yenyewe, filosofia ya mpango wa Parole na manufaa yake katika jamii”, amesisitiza Naibu Waziri Masauni.

Wakati huo huo, Naibu Waziri Masauni amewaasa wafungwa wote wa Parole nchini ambao wamenufaika na utaratibu huo kuwa na nidhamu na washirikiane vema na jamii inayowazunguka ili kudhihirisha kwamba wamebadilika tabia na kuaacha uhalifu.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa Parole, Dkt. Augustino Mrema amesema kuwa atahakikisha kuwa anafanya kazi kwa weledi mkubwa huku akishirikiana na wajumbe wote na atahakikisha bodi hiyo inasonga mbele na si kurudi nyuma. Aidha, ametoa shukrani za dhati kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kumteua kuwa Mwenyekiti wa bodi hiyo.

“Napenda nitoe shukrani zangu za kipekee kwa Rais Magufuli kwa kuniteua kwa mara nyingine kuiongoza bodi hii, kuteuliwa kwangu ni ishara ya imani katika kulibeba jukumu hili la kijamii”, amesema Mwenyekiti Parole Taifa, Dkt. Mrema.

Kwa upande wake, Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Suleiman Mzee ambaye pia ni Katibu wa Bodi ya Taifa Parole amempongeza Mhe. Dkt. Augustino Mrema kwa kuteuliwa tena kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa Parole pamoja na wajumbe wote na kuongeza kuwa hiyo inadhihirisha imani kubwa ya Serikali katika kubeba dhamana hiyo.

Kamishna Jenerali Mzee amesema kuwa tangu bodi hiyo ya Parole Taifa ianze kutekeleza Sheria ya Parole nchini mpaka sasa wamefanikiwa kujadili wafungwa 6,237, wafungwa walionufaika kwa Parole ni 5,535, na wafungwa waliokataliwa kwa sababu mbalimbali 702. Aidha, mpaka sasa ni wafungwa 25 tu ndio waliokiuka masharti ya Parole na kurudishwa magerezani.

“Mhe. Naibu Waziri mpaka sasa jumla ya vikao 41 vimeshafanyika tangu ianzishwe Sheria ya Bodi za Parole nchini na imewezesha kujadili wafungwa hawa walionufaika na wale ambao hawakunufaika”, amesema Kamishna Jenerali Mzee.

Bodi ya Taifa Parole ni tasnia muhimu sana katika urekebishaji wa wahalifu kwa kuishirikisha jamii. Tangu kuanzishwa kwa bodi hiyo mwaka 1994 mafanikio makubwa yameonekana kutokana na baadhi ya wafungwa kuachiliwa kupitia utaratibu huu hivyo kupunguza sehemu ya changamoto ya msongamano magerezani.

Mwisho.

Qwihaya yalikumbuka jeshi la Polisi vita dhidi ya corona

$
0
0
Abichi Masanga, Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilayani Mufindi akipokea vifaa vya kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona kutoka kwa Meneja wa Qwihaya General Enterprises Co Ltd, kampuni inayozalisha nguzo za umeme ya mjini Mafinga. Qwihaya kwa sasa inamiliki viwanda mkoani Iringa na Kugoma

Na Mwandishi wetu, Mafinga

Kampuni inayozalisha nguzo za umeme ya Qwihaya General Enterprise Co Ltd imelikumbuka jeshi la Polisi mjini Mafinga, Wilayani mfindi kwa kutoka vifaa vya kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona vinavyo sababisha ugonjwa wa covid 19.

Msaada huo ni mwendelezo wa ziara ya Qwihaya katika kukabidhi vifaa hivyo maeneo mbalimbali na tayari zaidi ya Sh65 zimetumika kwa kazi hiyo tangu janga hilo lianze.

Akikabidhi msaada huo, Meneja wa Qwihaya, Ntibwa Mjema amesema kampuni hiyo imeamua kushiriki kwa vitendo vita dhidi ya corona ikiunga mkono jitihada za Serikali katika kupambana.

Tumetoa vitakasa mikono, barakoa na sabuni ili wenzetu polisi wanapotekeleza majukumu yao wawe kwenye mazingira salama,” amesema Mjema.

Kwa upande wake, Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Mufindi, Abichi Masanga aliishukuru kampuni hiyo na kuziomba kampuni nyingizi ziige mfano huo.

“Tunashukuru kwa huu msaada na bado tunahitaji msaada mwingine, hapa wanakuja raia wengi na watuhumiwa wakiwa hapa wanahitaji barakoa na sanitaiza kwa hiyo, mahitaji makubwa” amesema Kamanda Masanga.

Kwa sasa kampuni ya Qwihaya inamilikiwa na Mzalendo, ndugu Leonard Mahenda ina viwanda vya kuzalisha nguzo za umeme katika mikoa ya Iringa na Kigoma huku mkakati ukiwa kumaliza uhaba wa bidhaa hiyo ambayo awali ilikuwa ikiingizwa kutoka nje ya nchi unamalizika.

Qwihaya umeme unawaka vijijini kama mijini

Mwisho.

KATA YA KITWIRU BARABARA ZAKARABATIWA,WANANCHI WAPONGEZA

$
0
0
Diwani wa kata ya Kitwiru Baraka Kimata akiwa na burudoza likikarabati baadhi ya Barbara za mitaa ya kata ya Kitwiru.

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.


Wananchi wa kata ya kitwiru wapongeza juhundi za diwani wa kata hiyo kwa kurekebisha miundombinu ya barabara ambayo itasaidia kukuza maendeleo ya wananchi.

Wakizungunza wakati wa ukarabati barabara za mitaa mbalimbali katika kata hiyo ya Kitwiru walisema jambo analolifanya diwani huyo ni kuhakikisha wananchi wanafanya shughuli za kimaendeleo bila ya vikwazo vyovyote vile.

Walisema kuwa mvua za msimu huu zimearibu barabara kwa asilimia kuwa na kupelekea kufifia kwa kazi za kimaendeleo kwa wananchi.

"Uwepo wa miundombinu bora ya barabara kunachangia kwa kiasi kikubwa shughuli za kimaendeleo kufanyika bila changamoto hiyo na kuleta maendeleo kwa kukuza uchumi wa wananchi "walisema

Wananchi hao waliongeza kuwa wanachangamoto ya kukosekana kwa usafiri wa moja kwa moja wa kutoka Iringa mjini hadi Mitaa ya Nyamuhanga ambako asilimia kubwa ya wananchi wanaishi huko huku shughuli za kiuchumi wanazifanya Iringa mjini kwa asilimia kubwa.

Kwa upande wake diwani wa kata ya Kitwiru Baraka Kimata alisema kuwa jukumu kubwa ni kuwatumikia wananchi ili wafanye shughuli za kimaendeleo wakiwa hawana changamoto za miundombinu ya barabara.

Alisema kuwa huo ni mkakati endelevu wa uihakikisha wanaboresha miundombinu ya barabara kwenye mitaa yote ya kata ili kurahisiha shughuli za kimaendeleo za wananchi wote.

Kimata alisema kuwa juhudi za kukarabati miundombinu ya barabara inatokana na juhudi za kwake kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa manispaa ya Iringa mjini wanaopenda maendeleo ya wananchi wa kipato cha chini.

"Tumeanza ukarabati huu wa miundombinu ya barabara utakuwa endelevu kila uchwao ili kuhakikisha barabara zote za kata yangu ya Kitwiru zinapitika kirahisi na kurahisisha shughuli za kimaendeleo kwa wananchi" alisema kimata

Kimata alisema kuwa mvua za msimu huu ziliharibu miundombinu ya barabara kwa kiasi kikubwa na kukwamisha juhudi za maendeleo kwa wananchi wa kata ya KiKitwiru.

Kuhusu changamoto ya Usafiri wa dala dala na bajaji kutofika katika maeneo hayo Kimata alisema alikwisha zungumza na wamiliki wa magarinili waanzishe safari kupitia njia inayokatiza mitaa ya Nyamuhanga na kupatiwa kibari lakini changamoto iliyokuwapo awali ni hadi ya miundombinu chakavu hivyo ukarabati huo wa barabara utafungua fursa ya kuwapo kwa dala dala na bajaji zitakazoanza safari katika maeneo hao.

Kimata aliwahimiza wamiliki wa vyombo vya usafiri wa Umma kutumia fursa ya uhitaji wa usafiri katika maeneo hayo ili kujiongezea kipato na kuondosha kero ya usafiri kwa wananchi wa Nyamuhanga na kata ya Kitwiru kwa ujumla

KAMPUNI YA EVERWELL CABLE AND ENGINEERING CO. LTD YACHANGIA SH. MILIONI 100 KUKABILIANA NA CORONA

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akipokea hundi ya Sh. 100,000,000/= kutoka kwa kampuni ya Everwell Cable and Engineering Co. Ltd, ikiwa ni mchango kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali za mapambano dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu- COVID – 19. Makabidhiano hayo yamefanyika kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Mei 13, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akizungumza baada ya kupokea hundi ya Sh.100,000,000/=, ikiwa ni mchango kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali za mapambano dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu- COVID – 19. Makabidhiano hayo yamefanyika kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Mei 13, 2020. ( Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, akizungumza kwenye makabidhiano ya hundi ya Sh. 100,000,000/= , ikiwa ni mchango kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali za mapambano dhidi ya ugonjwawa homa kali ya mapafu- COVID – 19. Makabidhiano hayo yamefanyika kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Mei 13, 2020. ( Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (Kushoto) pamoja na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge), Tixon Nzunda wakati wa kupokea hundi ya Sh. 100,000,000/=, ikiwa ni mchango kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali za mapambano dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu- COVID – 19. Makabidhiano hayo yamefanyika kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Mei 13, 2020. ( Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana, na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb), amepokea msaada wa hundi yenye thamani ya sh. milioni 100 iliyotolewa na kampuni ya Everwell Cable and Engineering Co. Ltd, inayojishughulisha na uzalishaji wa nyaya za kusafirisha umeme kwenye miradi mbalimbali ya umeme hapa nchini, kwa ajili ya kusaidia mapambano dhidi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona (COVID- 19).

Waziri amepokea mchango huo kwa niaba ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa leo tarehe 13 Mei, 2020 katika Ofisi ya Waziri Mkuu Mlimwa, Jijini Dodoma.

Akizungumza wakati wa kupokea mchango huo Waziri Mhagama ameipongeza kampuni hiyo kwa kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuhakikisha inapambana na janga la ugonjwa wa COVID-19.

“Kwa niaba ya serikali nawashukuru sana kwa kuwa sehemu ya watanzania katika kipindi hiki cha mapambano ya janga la COVID-19. Tunawashukuru sana kwa kuendelea kuwa sehemu ya shida na raha za Taifa hili,” ameeleza Waziri Mhagama.

Aidha, Waziri Mhagama amewahakikishia watanzania kuwa michango hiyo inasimamiwa vyema na serikali kwa kuitumia michango hiyo katika kushughulikia majukumu yaliyopangwa ya kupambana na janga la ugonjwa wa COVID-19.

Awali, Waziri wa Nishati Dkt. Medadi Kalemani ameipongeza kampuni hiyo kwa mchango wao kwa Serikali kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19.

“Kampuni hii ni moja ya wawekezaji waliojenga Kiwanda hapa nchini, lakini pamoja na shughuli za uwekezaji wameguswa katika kipindi hiki wakati serikali inapambana na janga hili la ugonjwa wa COVID-19, tunawashukuru sana kwa mchango wenu kwa watanzania ”amesema Dkt. Kalemani.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Everwell Cable and Engineering Co. Ltd, Bw. Jiaopeng Lu ameeleza kuwa Kampuni hiyo imekuwa ikishirikiana na watanzania katika uzalishaji wa bidhaa za kiwanda kabla ya Janga hili la Ugonjwa wa COVID-19, hivyo hawana budi kuhakikisha watanzania wanakuwa salama ili waendelee kushirikiana nao katika shughuli za uzalishaji

Spika Ndugai azuia wabunge 15 Chadema

$
0
0
SPIKA wa Bunge, Job Ndugai

Na MWANDISHI WETU-DODOMA, Mtanzania

SPIKA wa Bunge, Job Ndugai, amewazuia wabunge 15 wa Chadema kuhudhuria bungeni, iwapo hawatakamilisha masharti mawili muhimu.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Spika jana, ilieleza kuwa wabunge hao watatakiwa kutimiza masharti hayo kwa kuwa hawajulikani waliko na wamekuwa wakihesabiwa kama watoro tangu walipoacha kuingia bungeni Mei 1, mwaka huu.

“Ofisi ya Bunge inatoa taarifa kwamba katika siku za hivi karibuni baadhi ya wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamekuwa watoro kwa kutohudhuria vikao vya Bunge bila ruhusa ya Spika kwa muda wa wiki mbili, kinyume na masharti ya Kanuni ya 146 inayosisitiza wajibu wa kila mbunge kuhudhuria vikao vya Bunge.

“Aidha, tunapenda ifahamike kwamba wabunge hao walisusia vikao vya Bunge huku wakiwa wamelipwa posho ya kujikimu ya kuanzia Mei 1-17, 2020.

“Kwa mujibu wa masharti ya Kanuni ya 5 ya Kanuni za Bunge, Spika alitoa masharti mawili kwa wabunge hao,” ilieleza taarifa hiyo.

Ilieleza kuwa sharti la kwanza ni kuwataka wabunge hao kurejea bungeni au kurudisha fedha walizolipwa mara moja na sharti la pili ni kwa kuwa haijulikani wabunge hao walipo, watalazimika kuwasilisha ushahidi kwamba wamepimwa na hawana maambukizi ya virusi vya corona kabla ya kuruhusiwa kuingia bungeni.

Taarifa hiyo iliwataja wabunge hao kuwa ni Freeman Mbowe, Ester Bulaya, Halima Mdee, John Heche, Joseph Mbilinyi, Peter Msigwa, Rhoda Kunchela, Pascal Haonga, Catherine Rage, Devotha Minja, Joyce Mukya, Aida Khenan, Upendo Peneza, Grace Kiwelu na Joseph Haule.

“Hivyo basi, kwa taarifa hii, na kwa mujibu we Kanuni ya 144 ya Kanuni za Kudumu za Bunge inayohusu usalama katika maeneo ya Bunge, Spika ameagiza Kitengo cha Usalama cha Bunge kutowaruhusu wabunge waliotajwa hapo juu kuingia katika maeneo ya Bunge kuanzia leo (jana) Jumatano Mei 13, 2020 mpaka watakapotimiza masharti tajwa hapo juu,” ilieleza taarifa hiyo.

Hatua hiyo ni utekelezaji wa maagizo ya Spika Ndugai aliyoyatoa Mei 6, mwaka huu akisema wabunge hao waliojipa karantini ya siku 14 ni watoro na wanatakiwa kurudi bungeni haraka ili waendelee na kazi.

Pia aliwataka wabunge hao ambao wamelipwa fedha za kujikimu za kuanzia Mei Mosi hadi 17, mwaka huu kama hawatarudi bungeni mara moja, wakati watakaporudi baada ya siku 14 hawatapokewa hadi wawe na vyeti vya kuonyesha wamepimwa corona na pia wawe wamerudisha kwenye akaunti ya Bunge fedha hizo.

Spika Ndugai alisema endapo hawatafanya hivyo hawataruhusiwa kuingia bungeni na majina yao yatapelekwa kwenye vyombo vya ulinzi na usalama kwa hatua zaidi kwa sababu watakuwa wamefanya wizi wa fedha hizo.

Agizo hilo lilitokana na hatua ya uongozi wa Chadema kuwaagiza wabunge wake kuacha kuhudhuria vikao vya Bunge na kukaa mbali na majengo ya Bunge ya Dodoma na Dar es Salaam ili kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona.

Hivi karibuni akisoma maamuzi ya Kamati Kuu ya Chadema iliyofanywa kwa njia ya mtandao, Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika, aliwataka wabunge hao kutorudisha fedha hizo na waendelee kuwa karantini kama chama kilivyoelekeza.

Mnyika aliwasisitiza wabunge wao wote walioko Dodoma wasiende majimboni au mikoani bali wabaki Dodoma kwenye karantini hadi itakapothibitika kuwa ni salama na au kupata maelekezo mengine yoyote yaliyo rasmi.

Siku 14 za wabunge hao kujiweka karantini zilikamilika jana.

KUHUSU POSHO

Hata hivyo pamoja na maagizo ya awali kuhusu wabunge wa Chadema kurejesha posho za siku 14 ambazo walishalipwa, chama hicho kimekaidi maelekezo hayo na kueleza kuwa hakuna mbunge aliyefanya kosa kwa kupokea posho hizo.

Mnyika alisema kuwa Kamati Kuu ilijadili kwa kina kuhusu madai ya Spika Ndugai kwamba wabunge wa Chadema waliopewa posho za kujikimu Dodoma ni wezi na ilifikia uamuzi kwamba madai hayo ni ya uongo na chama kutoa rai kwa wabunge kuwa kwa sababu siyo wezi, wasitekeleze yale yaliyoelekezwa na Spika ambayo yanakwenda kinyume cha sheria, Katiba ya nchi na utaratibu wa Bunge.

“Kwa hiyo kimsingi Kamati Kuu imepitia madai hayo na kuona kwamba wabunge wa Chadema siyo wezi kama alivyojaribu kudai Spika,” alisema Mnyika.

Pamoja na mambo mengine, kikao hicho cha Kamati Kuu kiliazimia kuwafuta uanachama wabunge wake wanne, wakiwamo Joseph Selasini (Rombo), Antony Komu (Moshi Vijijini) ambao wote kwa nyakati tofauti walitangaza kujiunga na Chama cha NCCR-Mageuzi mara baada ya Bunge kumaliza muda wake.

Mbali na hao pia kikao hicho kiliwavua unachama wabunge Wilfred Lwakatare (Bukoba Mjini) na Davidi Silinde (Momba) huku Mbunge wa Viti Maalumu, Mariam Msabaha ambaye alikuwa mjumbe wa Kamati Kuu akivuliwa nyadhifa zake zote ndani ya chama na kutakiwa kujieleza kwanini asichukuliwa hatua.

Aidha, wabunge wengine ambao wanaendelea kuhudhuria vikao vya Bunge wametakiwa kujieleza ni kwa vipi wasichukuliwe hatua zaidi kwa kukiuka hayo maagizo na makubaliano ya chama.

Waliotakiwa kujieleza kwa kukiuka makubaliano hayo ni Suzan Masele, Joyce Sokombi, Latifa Chande, Lucy Mlowe, Sware Semesi, Jafari Michael, Peter Lijualikali, Willy Kambalo, Rose Kamili, Sabrina Sungura na Anne Gideria.

Hata hivyo, akizungumza bungeni mwanzoni mwa wiki, Spika Ndugai alisema yeye ndiye mwenye mamlaka ya kuwaapisha wabunge, hivyo wabunge wa Chadema wanaoingia bungeni wasitishwe na mtu yeyote na kwamba vikao vinavyoendelea ni vya majungu tu.

“Lakini niseme wabunge mnaapishwa na Spika, wakati nawaapisha hapa na wabunge wangu niliowaapisha wala msiwe na wasiwasi, vikao ni vya majungu wala msiwe na wasiwasi.

“Eti mtu mmoja anajifanya ana mamlaka ya kuburuza wabunge anavyotaka, haiwezekani. Biashara itaishia huko huko, sio kwa hii Tanzania, unafanya unavyotaka, mara kushoto geuka, kulia sawa, kushoto sawa, nyuma geuka sawa, ukipata mshahara haya lete huku.

“Kweli mmekuwa watumwa wa mtu, hili jambo halipo duniani wala Tanzania, muendelee kutulia msiwe na shaka,” alisema Ndugai.

Dk. Shein Aipongeza Redio Jamii ya Micheweni Pemba

$
0
0
RADIO Jamii iliyopo Micheweni Pemba imepongezwa kwa mchango wake mkubwa wa kutoa elimu kwa jamii juu ya tahadhari ya ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Corona kisiwani humo.

Pongezi hizo zimetolewa wakati viongozi wa Mikoa miwili ya Pemba walipokutana na na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein huko Ikulu ndogo, Chake Chake, Mkoa wa Kusini Pemba.

Akisoma taarifa ya Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mkuu wa Mkoa huo Omar Khamis Othman alisema kuwa Redio Jamii iliyopo Micheweni imeweza kutoa vipindi mbali mbali ikiwa ni pamoja na uvaaji wa barakoa, umuhimu wa kunawa maji tiririka na sabuni kama njia ya kujihadhari na ugonjwa huo.

Kiongozi huyo alieleza kuwa jumla ya wananchi 7,689 wananoishi maeneo ya kisiwa cha Fundo, Kokoa, Njau, Kojani, Makangale,Kifundi, Msuka, Micheweni, Shanake na Kiuyu kwa Manda, Tondooni, Tumbe, Shumba Mjini, Maziwa Ngombe, Michenzani, Kiuyu Mbuyuni wamepata elimu ya kuelewa ugonjwa wa Corona na hatua za kujikinga na ugonjwa huo.

Alieleza kuwa redio hiyo imeweza kusaidia jitihada hizo za kutoa elimu katika maeneo hayo yakiwemo yale ya visiwa na maeneo mengineyo ikiwa ni pamoja na kueleza katika vipindi vyake juu ya umuhimu wa kutoa taarifa pale wanapogundua kuna mtu ama watu wameingia kutoka nje ya nchi.

Mkuu wa Mkoa huo alieleza kuwa elimu iliyolenga kuutambua ugonjwa wa Corona na mbinu zote muhimu za kujikinga na ugonjwa huo imetolewa kupitia mikutano ya jamii kwa Shehia 61 za Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Aidha, aliongeza kuwa elimu kwa wachuuzi na wanunuzi wa samaki 2,651 ilitolewa katika Shehia nne ambazo zina bandari za kuuzia samaki ikiwemo Msuka, Kiuyu, Shumba Mjini, Wete, Mtambwe, Gando na Tumbe.

Vile vile, Mkuu wa Mkoa huyo alieleza kuwa Mkoa huo umetoa elimu kwa makundi tofauti wakiwemo Maimamu, Mashehe, Watu maarufu, Madalali na Kamati za afya za Shehia kwa Shehia zote 61 za Mkoa wa Kaskazini Pemba ambapo elimu imetolewa juu ya kuelewa ugonjwa wa Corona.

Ambapo pia kiongozi huyo alieleza kuwa hatua muhimu za kujikinga na ugonjwa huo zikiwemo uvaaji wa barakoa, kutekeleza maelekezo ya Serikali pamoja na umhimu wa kutoa taarifa pale wanapogundua kuna mtu ama watu wana dalili za maradhi ya Corona.

Kwa maelezo ya Mkuu wa Mkoa huyo juhudi zimechukuliwa za kufanya ukaguzi na uchunguzi wa wasafiri wanaotoka nje ya Kisiwa cha Pemba sambamba na kufanya usimamizi wa kambi ambazo zilifunguliwa kwa ajili ya kuwaweka wasafiri waloingia nchini kutoka Kenya.

Pamoja na hayo, kiongozi huyo alieleza hatua zilizochukuliwa katika kufanya ukaguzi wa bandari bubu ambapo Mkoa huo una jumla ya bandari bubu 172 ambazo zinatumiwa na wananchi kwa shughuli mbali mbali.

Aliongeza kuwa Shehia 17 zenye bandari bubu zilikaguliwa na kufuatiliwa ambapo jumla ya wananchi 725 walipitia bandari zisizo rasmi walipatikana ambapo pia, juhudi zilifanywa za ziara katika maeneo hatarishi yenye mikusanyiko ya watu.

Nae Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Hemed Suleiman Abdallah alieleza kuwa Mkoa huo kwa kushirikiana na Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kupitia Idara ya Habari Maelezo umeweza kutoa taaluma ya kutosha katika maeneo mbali mbali mjini na vijijini kwa kutumia gari la matangazo.

Aliongeza kuwa kwa kushirikiana na wataalamu wa afya vipindi mbali mbali vimeweza kutengeneza katika redio za Jamii ikiwemo redio hiyo ya Micheweni pamoja na Redio Istiqama na Redio pamoja na Televisheni ya ZBC.

Aidha, alieleza kuwa mashirikiano makubwa baina ya uongozi wa Kusini Pemba na Mkoa wa Tanga katika kufuatilia wananchi wanaotoka Mombasa ili kujikinga na ugonjwa wa Corona yamefanyika kwa mafanikio

Mkuu huyo wa Mkoa aliongeza kuwa hali ya upatikanaji wa chakula kwa kipindi hichi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni nzuri ambapo mahitaji ya vyakula vya msingi ukiwemo mchele, sukari, unga wa sembe na ngano yanaendelea kupatikana madukani na vipo vya kutosha.

Aliongeza kuwa kutokana na uhamasishaji na uimarishaji wa huduma za kilimo wananchi wameweza kuzalisha mazao ya ndizi na muhogo kwa wingi na kwa sasa Mkoa huo tatizo la upatikanaji wa chakula halipo.

Kuhusu bei ya vyakula, Mkuu wa Mkoa huyo alisema kuwa bado haijabadilika na Serikali ya Mkoa inaendelea kufuatilia kwa karibu ili kuhakikisha kwamba bei hazipandi kiholela lwa kisingizio cha mwezi wa Ramadhani ama maradhi ya Corona.

Pamoja na hayo, Mkuu huyo wa Mkoa alieleza kuwa katika utekelezaji wa mikakati ya kupambana na janga la Corona Mkoa huo umeweza kuchukua hatua mbali mbali katika maeneo yote ya mikusanyiko kama vile masoko,maeneo ya biashara, maeneo ya michezo, sehemu za ibada, vituo vya daladala na katika Taasisi za Serikali na binafsi ili kuthibiti ugonjwa huo.

Kwa maelezo ya kiongozi huyo alieleza kuwa Afisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kusini Pemba kwa kushirikiana na vikosi vyengine vya Ulinzi na Usalama vya Mkoa wa Kusini kwa kushirikiana na Masheha na Madiwani imefanya doria maalum ya kuzikagua na kuzitambua bandari bubu zote 253 kwa Mkoa wa Kusini.

Sambamba na hayo, viongozi hao walieleza hali ya amani na utulivu iliyopo katika Mikoa yote miwili na kueleza kuwa wananchi wanaendelea kufanya shughuli zao za kijamii na kiuchumi kama kawaida pamoja na kushirikiana na Serikali katika kufanikisha shughuli mbali mbali za kijamiii na kimaendeleo.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

: WAZIRI MKUU ATEMBELEA MRADI WA SGR MKOANI PWANI

WAZIRI MKUU AFURAHISHWA NA KASI YA UJENZI MRADI MKUBWA WA UMEME WA JULIUS NYERERE WA MW 2115

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (katikati, mstari wa mbele) akiongozana na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kushoto) na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Zena Said (kulia) wakati akitembeela ujenzi wa mradi wa umeme wa maji wa Julius Nyerere (JNHPP) kwenye mto Rufiji mkoani Pwani.

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Kassim Majaliwa ameridhishwa na hatua mbalimbali za ujenzi wa Mradi mkubwa wa Kufua Umeme kwa maji wa Julius Nyerere (JNHPP) unaotekelezwa kwenye mto Rufiji.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo Mei 14, 2020, baada ya kufanya ziara kwenye eneo la mradi unaotarajiwa kuzalisha jumla ya Megawati 2115“ utakapokamilika 2022.

Waziri Mkuu ambaye alifuatana na Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo mhandisi Zena Said watendaji wa TANESCO wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji TANESCO, Dk.Tito Mwinuka, alisema ziara yake ililenga kupata picha halisi ya hali ya mradi na hatua iliyofikiwa.

“Nimefarijika sana kuona hatua iliyofikiwa toka mradi umeanza mwezi Juni mwaka Jana mpaka leo ni ya kuridhisha.” Alisema Waziri Mkuu.

Alisema ziara yake imempa fursa ya kujionea jinsi kazi zinavyoendelea na nimatumaini yake
utakamilika kwa wakati

“Nimepata fursa ya kuona eneo lote la mradi na kazi mbalimbali zikiendelea, wakandarasi wanafanya vizuri na sisi Kama Serikali kupitia Wizara na TANESCO tumekuwa karibu nao kuhakikisha wanafanya vizuri na hayo ndio matarajio ya watanzania.” alisema Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu amewahakikishia watanzania kuwa mradi huo utakamilika katika muda uliopangwa na kuwapongeza wakandarasi kampuni ya Elsewedy na Arab contractor kutoka Misri kwa kazi nzuri.

Alisema licha ya changamoto ya mvua za masika bado kazi ya ujenzi iliendelea.
Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa ujenzi wa mradi huo Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani alisema, ujenzi ulianza 15/6/2020 na utakamilika 14/6/2022.

“Mradi unashughuli kubwa saba kati ya hizo muhimu sana ni nne, ujenzi wa njia ya kuchepusha maji, kujenga bwawa lenyewe, kujenga kingo nne zitakazowezesha maji kuhifadhiwa na ya mwisho ni kujenga power house.”. alifafanua Dkt. Kalemani.

Dkt.Kalemani alisema Hadi sasa mkandarasi ameshalipwa shilingi trilioni 1.29 ya jumla ya shilingi trilioni 6.5 ya mkataba mzima. “Malipo hayo ni sawa na asilimia 100 ambayo inahusu malipo ya awali asilimia 15 na malipo ya kazi alizofanya Hadi sasa.” Alifafanua Dkt. Kalemani.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (kulia) akiwa na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, akizungumza wakati alipotembeela eneo la ujenzi wa mradi wa umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) wa MW 2115 huko Rufiji Mkoani Pwani
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitazama maendeleo ya ujenzi wa mradi wa kufua umeme wa maji wa Julius Nyerere kwenye mto Rufiji mkoani Pwani.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO (Anayeshughulikia Miundombinu na Uwekezaji) Mhandisi Khalid James), akiteta mwakilishi wa kampuni iliyopewa kandarasi ya ujenzi wa mradi wa JNHPP ya El Sewedy Electric kutoka Misri.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Zena Said, akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ziara hiyo.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (kushoto), akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO Dkt. Tito Mwinuka (kulia) mara baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea ujenzi wa mradi wa kufua umeme wa majai wa Julius Nyerere (JNHPP) kwenye bonde la mto Rufiji mkoani Pwani Alhamisi 14/5/2020.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia) akizungumza na wakandarasi wanaotekeleza ujenzi wa mradi wa umeme wa Julius Nyerere, Arab Contractors na Elsewedy kutoka nchini Misri, wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo utakaozalisha MW 2115 za umeme. Waziri Mkuu alitembeela mradi huo Alhamisi 14/5/2020.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (wakwanza kushoto), akiteta jambo na Mkurugenzi qa TANESCO Dkt. Tito Mwinuka (aliyevaa nguo nyeusi), Katibu Mkuu Wizara ya Nishatio Mhandisi Aziza Said (wapili kushoto) na wakandarasi wa kampuni za Arab Contractors na Elsewedy zote kutoka Misri, wakati wa ziara ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kutembelea mradi wa umeme wa maji wa Julius Nyerere (JNHPP) huko Rufiji Mkoani Pwani 14/5/2020.
Taswira ya baadhi ya maeneo ya ujenzi wa mradi wa JNHPP leo Mei 14, 2020
Taswira ya baadhi ya maeneo ya ujenzi wa mradi wa JNHPP leo Mei 14, 2020

Naibu Waziri Nyongo Awataka viongozi wa vijiji kushiriki kutoa elimu ya uwekezaji katika sekta ya madini kupunguza migogoro

$
0
0
Mkurugenzi wa Kampuni ya Busolwa Mining LTD, Baraka Ezekiel akielezea jambo kwa ujumbe ulioambatana na Naibu Waziri Nyongo wakati wa ziara ya kukagua kusikiliza na kutatua changamoto za mwekezaji huyo.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kushoto) akiambatana na ujumbe wake wakati wa ziara katika mgodi wa uchimbaji wa kati wa madini unaomilikiwa na Kampuni ya Busolwa Mining LTD. Kulia ni Mkurugenzi wa mgodi huo, Baraka Ezekiel akielezea namna mitambo iliyosimikwa katika eneo hilo itakuwa ikifanya kazi mara baada ya ujenzi wake kukamilika
Mkurugenzi wa Kampuni ya Busolwa Mining LTD, Baraka Ezekiel akielezea jambo kwa ujumbe ulioambatana na Naibu Waziri Nyongo wakati wa ziara ya kukagua kusikiliza na kutatua changamoto za mwekezaji huyo. (Picha na Wizara ya Madini).

Na Nuru Mwasampeta, WM

NAIBU Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo ameutaka uongozi wa Kijiji cha Buhunda maarufu kama Lushokela kilichocho wilayani Misungwi mkoani Mwanza kutoa elimu ya uwekezaji kwa wananchi wake ili kuwa na uelewa juu ya masuala ya uwekezaji katika sekta ya madini.

Naibu Waziri Nyongo alitoa maelekezo hayo Aprili 12, 2020 alipotembelea mradi mpya wa uchimbaji wa madini unaomilikiwa na Kampuni ya Busolwa Mining LTD uliopo katika Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, baada ya kuelezwa ugumu wa mwananchi katika kupisha mradi kwa mwekezaji huyo na kudai naye anataka kuchimba
katika eneo hilo.

“Hapa ni suala la uelewa tu, elimu ya uwekezaji katika sekta ya madini inatakiwa kwa wananchi, na watoaji wa elimu wa kwanza ni ninyi viongozi wa Serikali za vijiji na mitaa.

"Mchimbaji akiomba na kupewa leseni mmiliki wa ardhi anapaswa kulipwa fidia na kupisha eneo hilo ili kupisha shughuli za uchimbaji,"Nyongo alisisitiza.

Kufuatia changamoto ya utoaji wa mizigo bandarini, Naibu Waziri Nyongo ameahidi kufanya mazungumzo na uongozi wa Shirika la Taifa la Usafirishaji (TASAC) kuhakikisha inaharakisha taratibu za utoaji wa mizigo bandarini ili vifaa hivyo vitolewe kwa wakati kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo na kuwafanya wawekezaji kukamilisha miradi yao kama walivyokusudia.

Kutokana na changamoto ya ugonjwa wa Corona unaoikabili Dunia, uliopelekea baadhi ya vifaa vinavyohitajika kwa ajili ya ukamilishaji wa ufungaji wa mitambo mgodini hapo kutokupatikana kwa wakati, Naibu Waziri Nyongo alisema, changamoto hiyo inaelekea ukingoni kwani nchi ya China ambako ndiko vilikiagizwa vifaa hivyo tayari viwanda mbalimbali vimefunguliwa na vinazalisha hivyo watarajie ukomo wa changamoto hiyo ndani ya muda mfupi.

Kwa upande wake Mkurugenzi na mwekezaji wa migodi ya Busolwa Mining, Baraka Ezekiel alisema wameshakusanya mchanga wa dhahabu utakaoweza kuchenjuliwa katika mgodi wao mpya wa Misungwi kwa muda wa mwaka mmoja na kubainisha kuwa, kwa sasa wanasubiri kukamilika kwa ujenzi wa mradi huo uliokwamishwa kwa kiasi kikubwa na mlipuko wa janga la corona duniani.

Akifafanua suala hilo, Baraka alisema, baadhi ya vipuri vya kukamilisha ufungaji wa mitambo katika mgodi huo ulisimama kutokana na uzalishaji wa vipuri, hivyo nchini China kusimama, lakini pia wataalamu waliokuwa wakisaidia ufungaji wa mitambo hiyo hawakuweza kurudi mara baada ya kusherehekea sikukuu za mwaka mpya wa Kichina kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa corona uliopelekea mipaka nchini humo kufugwa.

Pamoja na hayo ameeleza changamoto nyingine kuwa ni pamoja na ucheleweshwaji wa kutoa mizigo bandarini, umeme mdogo kwa ajili ya kuendeshea mitambo yao, na mgogoro wa eneo baina yake na mwananchi anayedai kutaka kuchimba madini katika eneo la leseni hiyo.

Akizungumzia suala la ajira, Baraka alisema mgodi huo unatarajia kuajiri watumishi wa kudumu wapatao 88 miongoni mwao saba watatoka nje ya nchi kwa ajili ya kusaidia kuelekeza wazawa namna ya kuendesha mitambo hiyo na pia itatoa ajira zisizo rasmi kwa watu 200 hivyo kufungua fursa za ajira kwa watanzania.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Juma Sweda ameiomba Serikali kufungua soko la madini wilayani humo na kubainisha kuwa tayari ofisi yake kwa kushirikiana na Ofisi ya Madini wamekwisha andaa jengo kwa ajili ya soko hilo na kubainisha kuwa kinachokosekana ni mashine za kupimia purity ya madini ya dhahabu sokoni hapo.

Sweda alisema, kufunguliwa kwa soko hilo kutaisaidia Serikali katika suala zima la ukusanyaji wa mapato, lakini pia kuwapa fursa wachimbaji wadogo waliopo katika eneo hilo kuuza madini yao sokoni hapo kuliko kusafiri mpaka Mwanza jambo ambalo linahatarisha usalama wao.

Akijibu hoja hiyo ya Mkuu wa Wilaya Sweda, Naibu Waziri Nyongo alimwagiza Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Mwanza kuhakikisha soko hilo linawezeshwa mapema na kufunguliwa ili kuwezesha biashara ya madini wilayani hapo kufanyika sokoni hapo.

Fedha za FIFA hazitoenda kwa klabu-TFF

Burundi yawatimua maofisa wa WHO

$
0
0
BUJUMBURA, BURUNDI, BBC

SHIRIKA la Afya Duniani (WHO) liko katika harakati za kuwahamisha wafanyakazi wake wanne kutoka nchini Burundi baada ya kuambiwa waondoke na Serikali.

Mkurugenzi wa kieneo barani Afrika, Dk Matshidiso Moeti, amethibitisha habari hiyo kwenye mkutano na waandishi wa habari, lakini akaongeza kuwa hajui ni kwanini viongozi walichukua hatua hiyo.

Hata hivyo Dk Moeti alisema kuwa licha ya kufukuzwa bado WHO itashirikiana na viongozi wa Burundi katika kukabiliana kwao na janga la virusi vya corona vinavyosababisha homa ya mapafu ikulikanayo kana Covid-19.

Hatua hiyo inajiri baada ya ujumbe kutoka Wizara ya Mambo ya Nje nchini Burundi, uliotumwa mtandaoni kuwataka wawakilishi wa WHO kuondoka nchini humo ndani ya saa 48.

Dk. Walter Kazadi Mulombo ambaye alikuwa mwakilishi wa WHO nchini Burundi pamoja na wataalamu wengine Pr. Tarzy Daniel, Dk. Ruhana Mirindi Bisimwa na Dk. Jean Pierre Murunda Nkatawana wamepatiwa hadi Mei 15, 2020 kuondoka.

Katika mahojiano ya simu, Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi Ezechiel Nibigira hakukataa wala kuthibitisha hatua hiyo.

Mfanyakazi wa wizara hiyohiyo alithibitishia BBC Idhaa ya Great Lakes uhalisia wa agizo hilo.

Sababu ya kufukuzwa kwa maofisa hao wa afya haikutajwa, licha ya juhudi za BBC kuzungumza na Walter Kazadi Mulombo.

Serikali ya Burundi inakabiliwa na ukosoaji mkubwa kwa kuandaa uchaguzi katika mazingira ya janga la corona, licha ya kuripoti kuwa na wagonjwa 27 na kifo cha mtu mmoja.

Kampeni ya wagombea urais zinafanyika kote nchini humo kabla ya uchaguzi utakaofanyika Jumatano, bila ya kuwa na utaratibu wa kukabiliana na maambukizi ya virus ya corona.

Hali hiyo imezua hofu ya kusambaa kwa virusi via ugonjwa wa Covd-19 katika taifa hilo dogo la Afrika Mashariki.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari kuhusi hali ya Burundi, siku ya Jumatano, Shirika la Kimataifa la kushughulikia hali ya dharura (International Crisis Group) lilisema Serikali ya Burundi halijakubali kuwepo kwa corona na kuongeza kuwa kutilia shaka idadi ya wagonjwa wa corona iliyotangazwa.

Mei 10, Serikali ya Burundi ilisema kwamba wachunguzi wote wa uchaguzi utakaofanyika Mei 20, 2020 watalazimika kufuata maagizo ya kukabiliana na virusi vya corona.

Hii ina maana kwamba wachunguzi wote ambao wanalenga kwenda katika taifa hilo ili kusimamia uchaguzi huo watalazimika kwenda karantini kwa siku 14 kuanzia siku watakapowasili nchini humo.

Na tangazo hilo lilitolewa wakati ikiwa ni siku 10 tu ndio zilizosalia kabla ya shughuli hiyo ya kidemokrasia kufanyika, hatua hiyo ilimaanisha kwamba wachunguzi kutoka mataifa ya kigeni hawataweza kuingia nchini humo.

Hatahivyo Jumuiya ya Afrika Mashariki ilisema kwamba italazimika kuwatumia maofisa wake waliopo nchini humo kusimamia shughuli hiyo.

Serikali ya Burundi imefunga mipaka yake ili kuzuwia kusambaa kwa virusi, na kuruhusu shehena za malori ya mizigo tu kuingizwa nchini kutoka mataifa jirani.
Viewing all 45918 articles
Browse latest View live