Quantcast
Channel: VIJIMAMBO
Viewing all 45912 articles
Browse latest View live

Kampuni za simu zaliza walalahoi ununuzi vifurushi

$
0
0

MWANDISHI WETU -DAR ES SALAAM, Mtanzania

WAKATI kampuni za simu zikiendelea na ushindani wa mauzo ya vifurushi vya bando za data na kuliza walalahoi, Kampuni ya Vodacom inaonekana kuwa ghali zaidi ikiwa mbele kwa zaidi ya mara mbili ikilinganishwa na kampuni nyingine.

Kwa mujibu wa ripoti ya robo mwaka ya sekta ya mawasiliano ya simu kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) inayojumuisha miezi mitatu ya Januari, Februari na Machi mwaka huu, Vodacom ndiyo inayoongoza kwa mauzo ya juu ya vifurushi vya data.

Katika ripoti hiyo iliyotolewa hivi karibuni, Vodacom hutoza Sh 98 kwa MB moja ikiwa imejumuisha kodi ya VAT, ikifuatiwa Kampuni ya Zantel ambayo hutoza Sh 41 kwa kila MB ikiwa ni pamoja na VAT.

Ripoti hiyo ambayo inatokana na data zilizowasilishwa na kila kampuni kwa TCRA, inaonyesha kuwa Kampuni ya Tigo na Airtel zinashika nafasi ya tatu katika tozo hizo kwa kuwa zinatoza Sh 40 kwa kila MB ikijumuishwa VAT.

Katika mtiririko huo, Kampuni ya Halotel inashika nafasi ya nne kwa kutoza Sh 26 kwa kila MB ikijumuisha VAT.

TTCL inatajwa na TCRA kuwa kampuni inayoshika nafasi ya tano katika mtiririko huo kwa kutoza Sh 14 kwa kila MB ikiwa ni nafasi ya pili kutoka mwisho miongoni mwa kampuni saba za simu zilizoorodheshwa katika ripoti hiyo

Ripoti hiyo ya TCRA inaainisha kwamba kampuni inayotoza kiwango cha chini kabisa kwa malipo ya data ni Smile ambayo hutoza Sh 6 kwa MB moja.

WATEJA WA HUDUMA ZA KIFEDHA


Katika suala la utoaji wa huduma za kifedha zinazojumuisha miamala ya kuweka na kutoa fedha kupitia mitandao ya simu, kwa Januari kampuni zote zilizotajwa zilitoa huduma kwa wateja 26,503,777, Februari zilitoa huduma kwa wateja 26,671,082 ikiwa ni ongezeko la wateja 167,305 ikilinganishwa na Januari na Machi zilitoa huduma kwa wateja 26,383,998 ikiwa ni pungufu kwa wateja287,084 ikilinganishwa na Februari.

Katika utoaji wa huduma hizo, Vodacom kupitia huduma ya M-Pesa ndiyo inayoongoza kwa kuwa na wateja wengi ambapo kwa Januari ilihudumia wateja 10,326,928 na Februari wateja 10,157,671 hivyo kupungua wateja 169,257 na Machi ilihudumia miamala 10,102,681 ikiwa ni pungufu ya wateja 54,990 hivyo kupoteza wateja 224,247.

Kampuni iliyofuata kwa kuhudumia wateja wengi ni Tigo kupitia huduma ya Tigo Pesa ambapo Januari ilihudumia wateja 7,959,370 na Februari wateja 7,954,048 ikiwa ni pungufu ya wateja 5,322 ikilinganishwa na Januari, na Machi ilihudumia wateja 8,330,330 ikiwa ni ongezeko la wateja 376,282 na kuifanya kuwa na ongezeko la wateja 370,960 kwa kipindi hicho cha miezi mitatu.

Hivyo, wakati Vodacom ikipoteza wateja 224,247 katika huduma zake za kifedha, Tigo iliongeza wateja 370,960 katika kipindi hicho cha miezi mitatu.

Airtel kupitia huduma ya Airtel Money kwa Januari ilihudumia wateja 5,345,519 na Februari wateja 5,549,511 hivyo kuwa na ongezeko la wateja 203,992 na Machi ilihudumia wateja 5,626,586 hivyo kuwa na ongezeko la wateja 77,075.

Kampuni ya Halotel kupitia Halopesa Januari ilihudumia wateja 1,719,627 na Februari ilihudumia wateja 1,816,078 ikiwa ni ongezeko la wateja 96,451 na Machi ilihudumia wateja 1,853,290 ikiwa ni ongezeko la wateja 37,212 ikilinganishwa na Februari.

TTCL kupitia huduma ya T-Pesa kwa Januari ilihudumia wateja 756,352 na Februari wateja 791,805 sawa na ongezeko la wateja 35,453 ikilinganishwa na Januari, na kwa Machi ilihudumia wateja 82,588 ikiwa imepoteza wateja 709,217 ikilinganishwa na Februari.

Zantel kupitia huduma ya Ezy Pesa Januari ilihudumia wateja 395,981 na Februari wateja 401,969 ikiwa ni ongezeko la wateja 5,988 ikilinganishwa na Januari, na Machi ilihudumia wateja 388,523 ikiwa ni pungufu ya wateja 13,446 ikilinganishwa na Februari.

Kampuni ya Smile haikuhudumia mteja yeyote katika huduma za kifedha katika kipindi hicho cha miezi mitatu.

MIAMALA NA VIWANGO VYA FEDHA VILIVYOHAMISHWA

Katika kupindi chote cha miezi mitatu, wateja wa kampuni zote za simu walifanya miamala 270,509,343 Januari na Februari 239,345,967 ikiwa ni pungufu kwa miamala 31,163,376 ikilinganishwa na Januari na Machi 256,150,335 ikiwa ni ongezeko la miamala 16,804,368 ikilinganishwa na Februari.

Kwa viwango vya jumla vya thamani ya kifedha kwa miezi hiyo, Januari ilifikia Sh 9,335,656,546,643 na Februari Sh 8,306,321,832,279 ikiwa ni pungufu ya Sh 1,029,334,714,364 ikilinganishwa na Januari, na Machi Sh 9,017,884,846,866 ikiwa ni ongezeko la Sh 711,563,014,587 ikilinganishwa na Februari.

Vodacom ndiyo iliyoongoza kwa viwango vikubwa vya uhamishaji fedha kupitia M-Pesa ambapo Januari ilihamisha miamala 124,414,825 na Februari 101,360,184 ikiwa ni pungufu ya miamala 23,054,641 ikilinganishwa na Januari, na na Machi ilifanya miamala 106,352,098 ikiwa ni ongezeko la miamala 4,991,914 ikilinganishwa na Februari.

Miamala hiyo ya M-Pesa kwa Januari ilifikia kiwango cha Sh 5,450,561,266,308 na Februari Sh 4,675,239,545,169 ambayo inaainisha upungufu wa Sh 775,321,721,139 na Machi Sh 5,084,530,555,683 ikimaanisha ongezeko la Sh 409,291,010,514.

Tigo ilifuatia kwa viwango ambapo kupitia Tigo Pesa Januari ilifanyika miamala 78,991,516 na Februari miamala 70,074,203 ikiwa ni upungufu wa miamala 8,917,313 na Machi miamala 75,107,094 ikiwa ni ongezeko la miamala 5,032,891.

Miamala hiyo ya Tigo Pesa kwa Januari ilikuwa na thamani ya Sh 2,051,344,393,852 na Februari Sh 1,846,759,373,602 ikiwa ni upungufu wa Sh 204,585,020,250 na Machi Sh 1,995,840,604,555 ikiwa ni ongezeko la Sh 149,081,230,953.

Airtel ilishika nafasi ya tatu kupitia huduma yake ya Airtel Money ambapo Januari miamala iliyofanyika ilifikia 49,979,065 na Februari 50,643,194 ambayo ni ongezeko la miamala 664,129 na Machi miamala 56,914,579 ambayo ni ongezeko la miamala 6,271,385.

Miamala ya Airtel kupitia Airtel Money kwa Januari ilikuwa na thamani ya Sh 1,568,389,507,046 na Februari Sh 1,511,952,671,962 ambayo ilikuwa ni pungufu kwa Sh 56,436,835,084 na Machi Sh 1,642,225,613,794 ambayo iliakisi ongezeko la Sh 130,272,941,832.

Ilifuatiwa na Halotel ambapo kupitia Halopesa Januari ilifanyika miamala 13,333,676 na Februari 13,585,755 ambayo ni ongezeko la miamala 252,079 na Machi miamala 14,809,315 ambayo ni ongezeko la miamala 1,223,560 ikilinganishwa na Februari.

Miamala hiyo ya Halotel kupitia Halopesa kwa Januari ilikuwa na thamani ya Sh 164,608,868,885 na Februari Sh 173,248,128,211 ambayo ni pungufu kwa Sh 147,284,056,064 ikilinganishwa na Januari na Machi Sh 194,598,762,724 ambayo ni ongezeko la Sh 21,350,634,513 ikilinganishwa na Februari.

Zantel kupitia Ezy Pesa Januari ilifanya miamala inayofikia 2,844,783 na Februari 2,843,962 ikiwa ni pungufu ya miamala 821 na Machi miamala 2,956,294 ikiwa ni ongezeko la miamala 112,332 ilikinganishwa na Februari.

Miamala hiyo ya Zantel kupitia Ezy Pesa kwa Januari ilikuwa na thamani ya Sh 90,994,751,652 na Februari Sh 88,298,671,493 ambayo ni pungufu ya Sh 2,696,080,159 ikilinganishwa na Januari, na Machi ilifikia thamani ya Sh 89,734,186,856 ambayo ni ongezeko la Sh 1,435,515,363 ikilinganishwa na Februari.

TTCL kupitia T-Pesa Januari ilifanya miamala 945,478 na Februari miamala 838,669 ambayo ni pungufu kwa miamala 106,809 ikilinganishwa na Februari, na Machi miamala 10,955 ambayo ni pungufu wa miamala 827,714 ikilinganishwa na Februari.

Miamala hiyo ya TTCL kupitia T-Pesa kwa Januari ilikuwa na thamani ya Sh 9,757,758,900 na Februari Sh 10,823,441,842 ambayo ni ongezeko la Sh 1,065,682,942 ikilinganishwa na Januari, na Machi Sh 10,955,123,254 ambayo ni ongezeko la Sh 131,681,412 ikilinganishwa na Februari.

Kwa kampuni ya simu ya Smile, katika kipindi hicho hakuna muamala wowote uliofanyika.

SERIKALI YATANGAZA BEI ELEKEZI YA CHANJO 13 ZA MAGONJWA YA MIFUGO,WAZIRI MPINA AIPA KIBARUA KIZITO BODI YA TVLA

$
0
0
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akimkabidhi vitendea kazi Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Wakala wa Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA), Profesa Amandus Muhairwa baada ya kuiziduia bodi hiyo na kupokea taarifa ya kutangazwa kwa bei elekezi ya Chanjo Makao Makuu ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mtumba jijini Dodoma 
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akimkabidhi vitendea kazi Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) baada ya uzinduzi wa Bodi ya TVLA Makao Makuu ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mtumba jijini Dodoma.
Wajumbe wa Bodi ya Wakala wa Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalah Ullega mara baada ya uzinduzi wa bodi hiyo Makao Makuu ya Wi

SHIRIKA LA SEMA LATOA ELIMU YA KUJIKINGA NA CORONA KWA ASKARI POLISI WA MKOA WA SINGIDA

$
0
0
Mdau wa mapambano dhidi ya Corona kutoka Taasisi ya Empower Youth Prosperity ( EYP) ya mkoani Mbeya, Ipyana Mwakyusa akitoa elimu ya kujikinga dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa corona kwa Askari Polisi wa Kituo Kikuu cha Mkoa wa Singida leo hii Asubuhi.
Askari Polisi wa Kituo Kikuu cha Mkoa wa Singida, wakipata elimu hiyo.
Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Florence Mwenda, akisisitiza jambo kwa askari wa kituo hicho, wakati wa kutolewa kwa elimu hiyo.
Mdau wa mapambano dhidi ya Corona kutoka Taasisi ya Empower Youth Prosperity ( EYP) ya mkoani Mbeya, Ipyana Mwakyusa, akisisitiza jambo wakati akitoa elimu hiyo.
Maafisa wa Shirika lisilo la Kiserikali la Sustanable Environment Management Action (SEMA) la Mkoa wa Singida, Gerson Janga (kushoto) na Witness Anderson wakitoa elimu hiyo kwa askari hao kwa njia ya mabango.
Askari hao wakiwa wamesimama kwa tahadhari ya kuacha mita zaidi ya moja kama njia ya kujikinga na maambukizi ya Corona.

Na Dotto Mwaibale,Singida


SHIRIKA lisilo la Kiserikali la Sustanable Environment Management Action (SEMA) kwa kushirikiana na wadau kutoka Taasisi ya Empower Youth Prosperity ( EYP) ya mkoani Mbeya wamtoa elimu ya kujikinga dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa corona kwa Askari Polisi wa Kituo Kikuu cha Polisi Mkoa wa Singida leo hii Asubuhi.

Akizungumza wakati wa utoaji wa elimu hiyo, Mdau wa mapambano dhidi ya Corona kutoka Taasisi ya Empower Youth Prosperity ( EYP) ya mkoani Mbeya, Ipyana Mwakyusa alisema elimu hiyo ililenga kukumbusha namna ya kujikinga na ugonjwa huo.

"Kila mtu anajua uwepo wa ugonjwa huu tunatoa elimu hii kwenu kwa ajili ya kukumbusha tukizingatia nyie wenzetu huwa mnakutana na watu wengi" alisema Mwakyusa.

Akielezea jinsi ya kujikinga na homa ya Virusi vya corona Mwakyusa alitoa tahadhari kwa askari hao kukaa mbali angalau mita 1 au 2 na mtu wakati wakiwa kazini.

Tahadhari nyingine alioitoa ni pamoja na kufunika mdomo na pua wakati wa kukohoa kwa kutumia kitambaa safi au sehemu ya mbele ya kiwiko cha mkono, kuepuka kugusana, kusalimiana kwa kushikana mikono.

Tahadhari nyingine ya jinsi ya kujikinga pamoja na mambo mengine ni kuepuka kugusa macho, pua au mdomo baada ya kunawa.

"Safisha mikono yako mara kwa mara kwa maji tiririka na sabuni au kwa dawa ya kutakasa mikono" alisema Mwakyusa.

Akizungumzia ugonjwa huo, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Florence Mwenda, alisema kwa upande wao wamechukua tahadhari zote za kujikinga pamoja na watu wanao wahudumia.

Kampeni ya utoaji wa elimu hiyo inafanywa kwa ufadhili wa Shirika la Stromme East Africa Foundation lenye Makao Makuu Kampala nchini Uganda huku ufadhili mkuu wa mashirika hayo ukitolewa na Shirika la Stromme Foundation la Norway kupitia mradi wa uwezeshaji jamii kiuchumi unaowalenga vijana wa kiume, wa kike, watoto na wakina mama.

WATANZANIA WALIOKWAMA INDIA WATUA BONGO

$
0
0

UBALOZI wa Tanzania nchini India, kwa kushirikiana na Shirika la Ndege la Tanzania [Air Tanzania] pamoja na diaspora wa Tanzania nchini India wamefanikisha safari ya kwanza ya kuwarejesha nchini Watanzania waliokuwa wamekwama katika miji mbalimbali nchini India kutokana na zuio la kuingia na kutoka ndege za kimataifa lililowekwa na Serikali ya India kama hatua mojawapo ya kudhibiti kuenea kwa maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19.

Ndege maalum ya Boeng 787-8 ya Dreamliner ya Air Tanzania ilitumwa na Serikali jijini Mumbai kwenda kuwachukua watu hao tangu Machi 22, 2020, lilipowekwa zuio hilo.

Ndege hiyo iliondoka India jana Mei 15, 2020, saa 2 asubuhi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Chhatrapati Shivaji International Airport, Mumbai, ikiwa imebeba jumla ya raia wa Tanzania 246, miongoni mwao ni waliokuwa wameenda India kwa ajili ya matibabu, wahitimu kutoka vyuo mbalimbali na wanafunzi ambao wanalazimika kurudi nyumbani kwa kuwa vyuo vimefungwa hadi mwezi Agosti/Septemba 2020.

Ndege hiyo imewasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere [JNIA] saa 6 mchana leo Ijumaa tarehe 15 Mei 2020.

Takriban Watanzania 410 walijiandikisha katika Ubalozi wa Tanzania, New Delhi, na kuelezea utayari wao wa kuchangia gharama.

Kwa kuwa idadi yao ilikuwa kubwa zaidi ya walioweza kusafiri katika awamu hii ya kwanza, Serikali inaangalia uwezekano wa kutuma ndege nyingine maalum ya Air Tanzania kwendakuwachukua waliosalia ndani ya mwezi huu.

Gharama ya tiketi ya ndege hiyo, namna ya kulipa, mahali ambapo ndege itatua pamoja na tarehe za kuwasili kwa ndege hiyo nchini India zitatangazwa na ubalozi mapema iwezekanavyo.

Ubalozi unapenda kuwashukuru diaspora wa Tanzania nchini India kwa kufanikisha zoezi hili kwa weledi mkubwa na uongozi wa Wizara za Mambo ya Nje za India na Tanzania na serikali, kwa ujumla, kwa miongozo mbalimbali wakati wa zoezi hili.

Kabla ya ndee hiyo kuwasili katika uwanja wa ndee wa JNIA wazazi, ndugu na jamaa watu hao walionekana wakiwa na nyuso za furaha wakiwasubiri ndugu zao.

Mmoja wa wanafunzi waliokuwa wanasoma India, Sulemani Khalidi, ameishukuru serikali kwa kuwarejesha.

“Kwa kweli naishukuru sana Serikali yangu kwa kusirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini India kwa kutusaidia sisi sote hadi kufika hapa nchini leo,” amesema .

MAJANGA: Haya ndio yaliyomkuta bondia Class Marekani

$
0
0
By IMANI MAKONGORO, MWANASPOTI

VIJANA wengi wanatamani kuishi Marekani, bila shaka simulizi za maisha ya kule na namna wanavyoona kwenye mitandao ya kijamii na kwenye runinga yanawapa mzuka wa kuishi huko hasa wale ambao, hawajawahi kufika huko.

Ndivyo ilikuwa kwa bondia Ibrahim Class, ambaye mwishoni mwa mwaka 2018, bingwa huyu wa dunia wa Global Boxing Council (GBC) alipata ofa ya kwenda kuishi Marekani ambako alikaa kwa zaidi ya mwaka mmoja kabla ya kurejea nchini.

Class anasema aliletewa mkataba mnono ambao, ulimshawishi kutoka Dar es Salaam kwenda kuanza maisha mapya.

“Tuliondoka nchini na Chaurembo Palasa, mwenyeji wetu kule alikuwa mtu mmoja raia wa huko aliitwa Napolio. Safari yetu ilikuwa nzuri na tulifuata taratibu zote za kuingia nchini humo.

“Napolio alitupokea vizuri tukawa tukiishi kwake mjini Washington DC, tulikaa kama mwezi mmoja, maisha yakaanza kubadilika,” anasimulia Class.

Ingawa hapa nchini ziliibuka taarifa kuwa, Class amekwenda Marekani kuwa bondia wa mazoezi (sparing patner) wa bei rahisi, wengine wakavumisha kuwa anafanya vibarua kwenye maduka makubwa.

Anasema mkataba wake ulikuwa wa kwenda kufanya mazoezi kule na kutafutiwa mapambano ambayo angepigana akitokea nchini humo na Napolio ndiyo angekuwa meneja wake.

“Kile ambacho kiliwekwa kwenye mkataba kikawa tofauti, tukiwa pale nyumbani kwa Napolio nikawa nawasiliana na rafiki yangu mmoja anaitwa God yupo Texas, tukamueleza changamoto tunazopitia akakubali twende kwake.”

Anasema yeye na Chaurembo walihamia kwa God ambako walikaa kama wiki mbili, mwenyeji wao akawatafutia gym ya kufanyia mazoezi, walifanikiwa akaanza mazoezi kule.

Anasema baadaye God aliwaunganisha kwa ndugu yao anaitwa Eddy kwa ajili ya kufanya mazoezi na kucheza mapambano, ambako walikaa mwezi mmoja kabla ya kupata pambano nchini Afrika Kusini.

“Tulikwenda Afrika Kusini na Palasa, baada ya lile pambano, Palasa alisema anarudi Tanzania, mimi nikarudi Marekani.

KUJITEGEMEA

Class anasema baada ya kurejea Marekani alizungumza na Eddy akamwambia anahitaji kujitegemea kwa kuwa mwenyeji wake alikuwa na familia na tayari alikuwa amewapa hifadhi ya muda mrefu.

“Nilipanga nyumba ambayo kwa mwezi nilikuwa nikilipa dola 1,300 (Sh2.9mil), ambayo ilijumuisha bili ya umeme na maji, nikaanza kujitegemea.”

Anasema akiwa nchini humo, mbali na ngumi lakini pia alitafuta kibarua akawa anafanya ambacho kilikuwa kikimuingizia fedha.

“Maisha Marekani yalikuwa ni gharama, ni kweli nilikuwa nikipata fedha, lakini gharama za maisha ziko juu sana nchini humo, nilikaa mwaka mmoja.

Anasema akiwa Marekani alipata pambano mjini Califonia ambako ni mitaa ya Floyd Mayweather, hivyo alikwenda kupiga kambi mjini humo.

YEYE NA PACQUIAO

Akiwa Califonia, alijifua kwenye gym ya kocha wa Manny Pacquiao, ambaye alimsaidia katika mazoezi kabla ya kupanda ulingoni kuzichapa kwenye pambano hilo ambalo alipoteza kwa Technical Knock Out (TKO).

“Nilijifua kwenye gym ya kocha Fred Rochie ambaye ni kocha wa Pacquiao hadi siku ya pambano, ingawa kocha wangu binafsi, ambaye nilitoka nao Texas nilikuwa nikimlipa,” anasema.
Anasema kutokana na juhudi ya mazoezi aliyokuwa akiionyesha kule Texas, kocha alimpa ofa ya kutumia gym bure na alikuwa akimlipa akijiandaa kucheza pambano
“Mara ya mwisho kocha wangu nimemlipa dola 6,000 (Sh 13 milioni) kwenye pambano langu, Marekani maisha ni ghali kidogo, tofauti na huku kwetu, lakini pia michongo ya kupata pesa ipo,” anasema.
Class, ambaye pambano lake la ubingwa wa dunia lililopewa sapoti na serikali kabla ya kwenda Marekani, aliingiza Sh 18 milioni anasema kwa maisha ya Marekani ukiwa na kipaji, ngumi zinalipa.
“Kibongo bongo siwezi kumlipa kocha 13 milioni kwa pambano, lakini Marekani nililipa pesa hiyo tena kocha akinisaidia tu, kwani ilikuwa ni kwenye pambano na gharama za gym nilipewa ofa,” anasimulia.
Bondia huyo, ambaye anajiandaa kucheza ubingwa wa dunia nchini baada ya janga la corona kupita, anasema gharama za maisha nchini Marekani pia ziko juu.
Class, ambaye alianza ngumi mwaka 2010 anasema katika maisha yake ya ngumi hawezi kulisahau pambano lake la Mei Mosi, 2013 alipocheza na Amos Mwamakula.
“Mpinzani wangu alinitambia mno, si yeye tu, hadi mashabiki wake na hata wangu walijua nitapigwa, nilielezwa sifa zake kila siku tangu siku niliposaini kuzichapa naye hadi siku ya pambano,” anasimulia.
Class anasema sifa kubwa ya Mwamakula bondia kutoka Mbeya aliambiwa ni kuwa ana nguvu nyingi, hivyo ni bondia mwenye ngumi nzito na kamwe hatomuweza, ingawa alishinda pambano hilo ambalo lilimpa ujasiri hadi sasa.
Class, 29, anasema alianza kujifunza ngumi akiwa na miaka 10, wakati huo alipenda kuufuatilia mchezo huo.
“Siku moja nilimuomba Chaku Master (Said), anisaidie nijifunze, alinipeleka kwa Kinyogoli (Habibu) akaanza kunifundisha,” anasimulia.
Anasema kwa kuwa alipenda kujifunza, alifuata maelekezo yote ya kocha na Kinyogoli amekuwa msaada mkubwa katika safari yake hiyo.

UBINGWA WA DUNIA
Julai Mosi, 2017, Class alitwaa ubingwa wa dunia nchini Ujerumani, baada ya kumchapa Jose Ferero kwa pointi na kuutetea ubingwa huo miezi minne baadaye jijini Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Uhuru alipomchapa Koos Sibiya wa Afrika Kusini.
Anasema alicheza pambano hilo akiwa kwenye kiwango bora, kabla ya kwenda Ujerumani alifanya mazoezi na mabondia tofauti tofauti nchini akiwamo Abdallah Pazi na Cosmas Cheka.
“Nilipokuwa nikitetea ubingwa wangu, bahati mbaya niliumia mguu, hakuna aliyekuwa akifahamu hili, nilicheza kwa tabu, lakini namshukuru Mwenyezi Mungu alinisimamia hadi nikashinda nyumbani,” anasimulia
Bondia huyo ambaye ni wa pili nchini kwenye uzani wa super feather na wa 75 kati ya mabondia 1586 duniani anasema ngumi zimemsaidia mambo mengi kwenye maisha yake ikiwamo kujenga mjengo wake Kimara, jijini Dar es Salaam.
Tangu 2010 alipoingia rasmi kwenye ngumi za kulipwa, Class amecheza mapambano 29, ameshinda 23 (11 kwa KO), amepigwa mara 6 (3 kwa KO).

TAMKO LA WAZIRI UMMY MWALIMU KUHUSU SIKU YA FAMILIA DUNIANI, BADILISHENI CORONA KUWA FURSA KWA MALEZI YA FAMILIA

$
0
0
15 Mei, 2020
Mwandishi wetu, WAMJW

Wazazi na walezi nchini wametakiwa kufanya tathimini juu ya fursa na changamoto zilizopo katika familia zao hususani kipindi hiki ambacho jamii inakabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona vinavyosababisha ugojwa wa homa kali ya mapafu (COVID-19).

Wito huo umetolewa leo jijini Dar Es Salaam na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akizungumza kuhusu Siku ya Familia Duniani ambayo huadhimishwa kila tarehe 15 ya Mwezi Mei.

Waziri Ummy amesisitiza wazazi na walezi kuhakikisha wanatumia kipindi cha mapambano dhidi ya Corona kuwa karibu na familia zao huku wakifanya ufuatiliaji wa karibu hasa kwa watoto na Wazee kwa kufuatilia hali zao za lishe na endapo kuna mabadiliko wachukue hatua stahiki ya kutoa taarifa na kuwapeleka Katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Waziri Ummy ameziasa familia zisiwanyanyapae waliopata maambukizi ya Corona tabia ambayo inaweza kupunguza upendo na utu miongoni mwa Watanzania wakati huu wa mapambano dhidi ya COVID-19.

“Niwaombe wazazi na walezi muwe karibu na familia zenu hasa watoto na wazee na punde mnapobaina dalili za ugonjwa wa Corona watoe taarifa ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa” alisema

Amesema wakati wa maadhimisho ya Siku ya Familia wazazi pia wanawajibika kubuni michezo mbalimbali kwa ajili ya watoto ili waendelee kujifunza wakiwa nyumbani itakayokuwa kivutio kwa watoto na hivyo kubaki nyumbani badala ya kuranda mtaani.

Ameongeza kuwa kipindi hiki wakati shule zimefungwa ikiwa ni njia ya kuwaepusha na maambukizi ya virusi vya corona, watoto waandaliwe mazingira bora yatakayowawezesha kuendelea kufuatilia masomo kupitia vyombo vya habari na njia ya mtandao.

“Familia ni msingi wa ustawi wa Jamii yoyote ile hivyo ni muhimu kuilinda ili kufikia maendeleo endelevu na kuhakikisha tunailinda na maambukizi ya Virusi vya Corona” alisema

Aidha, amesema kutokana na umuhimu wa familia kwa ustawishi wa jamii, Wazazi na walezi wana kila sababu ya kubadilisha tabia, mitazamo na kuongeza maarifa huku wakiongeza mbinu za kuiwezesha familia kukabiliana na changamoto mbalimbali zikiwemo maambukizi ya Virusi vya Corona.

Amesisitiza umuhimu wa Watanzania kuendelea kufuata kanuni na maelekezo ya wataalam wa afya ili kujikinga na kuwakinga wengine dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19 ambayo ni kujiepusha na mikusanyiko, kunawa mikono kwa kutumia sabuni na maji tiririka, kutumia vitakasa mikono kuzingatia umbali wa mita moja na kuendelea kati ya mtu na mtu pamoja na kuvaa barakoa.

Pia Waziri Ummy amezitaka Mamlaka za Mikoa na Serikali za Mitaa kuhakikisha wanaadhimisha Siku ya Familia Duniani kwa kutoa elimu kwa familia kuhusu namna ya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona.

Tanzania inaungana na Mataifa mengine ulimwenguni kila tarehe 15 mwezi Mei kuadhimisha Siku ya Familia Duniani ambayo kwa Mwaka huu inaongozwa na Kauli Mbiu isemayo “Familia ni Msingi katika kutokomeza Corona, tuilinde na tuwalinde wengine”

MWISHO.

BADILISHENI CORONA KUWA FURSA KWA MALEZIYA FAMILIA

KEYDOLI; MREMBO KUTOKA KENYA AMWAGIA SIFA HARMONIZE

$
0
0

MOMBASA, KENYA, MTANZANIA 


ONGEZEKO la wasanii wapya halipo Bongo pekee bali mpaka nchini Kenya, mashabiki wameendelea kushuhudia vipaji vipya kila siku.

Swaggaz tumekutana na KeyDoli, mrembo kutoka Mombasa nchini Kenya anayefanya vyema kwa sasa na wimbo, Infinity aliomshirikisha rapa Country Boy akitumia staili ya Afro Arabic Soul.

Swaggaz: KeyDoli ni nani na lini ulianza kujihusisha na muziki?

KeyDoli: Jina langu halisi ni Yusriyah Ahawa, nilianza muziki nikiwa mdogo sana kama miaka 14 hivi, ilikuwa mwaka 2002.

Nilipata kutambulishwa na prodyuza mmoja anayeitwa Bruce Othiambo ambaye alikuwa rafiki wa baba yangu kwa sababu walikuwa wanafanya kazi sehemu moja.

Prodyuza Bruce ambaye sasa ni marehemu alikuwa kwenye studio zinaitwa Johari Cleff na ndio ilikuwa inasimamia wasanii wakubwa kutoka Kenya.

Ngoma yangu ya kwanza iliitwa Nipe na baba yangu ndio alirekodi akishirikiana na prodyuza Bruce, wimbo huo ulinipa umaarufu sio tu hapa Kenya bali na Afrika Mashariki na Uingereza.

Swaggaz: Wanamuziki gani walikuvutia mpaka ukaingia kwenye muziki?

KeyDoli: Nilizaliwa kwenye familia ya muziki ndiyo maana nikajikuta napenda kuimba kwa kuwa hata baba yangu alikuwa anapenda muziki.

Nikawa nasikiliza muziki wa Yondo Sister, Mbilia Bel na Franco huku Madonna akiwa ni msanii wangu pendwa na haipiti siku sijamsikiliza.

Swaggaz: Kwanini uliamua kutangaza muziki wako Tanzania kwa kumshirikisha rapa Country Boy?

KeyDoli: Toka zamani ilikuwa ndoto yangu nifike Tanzania. Kwa hadithi za mama aliniambia amezaliwa Bongo pia nilikuwa nikiwasikia kina Juma Nature, Lady Jay Dee na Ray C kwahiyo nilikuwa natamani nifike.

Nilitamani kufika Tanzania nikiwa mdogo ila kwa sababu nilikuwa shule nilishindwa lakini nashukuru Machi 1, mwaka huu nilifika Dar es Salaam na kuweza kutimiza ndoto yangu kufanya kazi na Country Boy.

Swaggaz: Ukiwa kama msanii wa kike na mrembo sana, changamoto zipi unapitia kwenye muziki wako?

KeyDoli: Sio rahisi ila mimi nilifunzwa toka nikiwa mdogo kuwa wakati wa biashara ni biashara tu, ukiwa na mazungumzo ya biashara hakuna mtu anaweza kukutongoza ndio maana nikiwa nakwenda kwenye studio kurekodi au redioni au kwenye Tv huwa nakuwa na mtu kando yangu ili kukwepa hizo changamoto.

Swaggaz: Mbali na Country Boy, wasanii gani wengine wa Tanzania unatamani kufanya nao kazi?

KeyDoli: Harmonize au Darassa lakini Harmonize zaidi maana mashallah yuko na moyo mweupe na nilipata bahati ya kumwona hana dharau wala kiburi na uimbaji wake ni mzuri pia Darassa navutiwa na floo zake.

Swaggaz: Changamoto zipi zipo kwenye tasnia ya muziki hapa Kenya?

KeyDoli: Mimi naona sapoti hamna sana lakini siwezi kulaumu vyombo vya habari kwa sababu kuna wengine hawajafikishiwa kazi pia mashabiki nao hawajafikishiwa muziki kwa usahihi ili waweze kuusapoti.

Swaggaz: Baada ya kuachia ngoma yako na Country Boy, mashabiki watarajie nini kutoka kwako?

KeyDoli: Niko na ngoma mpya nitaiachia Mei 21, mwaka huu nikiwa nimemshirikisha msanii mkubwa wa Tanzania. Huo wimbo upo kwenye albamu yangu yenye jumla ya nyimbo 12.

Pia niko na EP yenye nyimbo nne ambazo zote nimeshirikisha Country Boy na tayari zina video ambazo nilifanyia Tanzania.

Mashabiki waendelee kunitafuta kwenye mitandao ya kijamii kama Facebook, Instagram, YouTube naitwa Keydoli ili wapate kunifahamu zaidi nawapenda sana Watanzania.

Pia nawakumbusha tuendelee kuvaa barakoa na kunawa mikono na kutumia sanitaiza mara kwa mara ili Mungu atulinde na ugonjwa wa corona.

Zoom yashtakiwa na kanisa baada ya mafunzo ya bibilia kuvamiwa kwa picha za ngono

$
0
0
CALIFONIA, MAREKANI

WAKATI watumiaji wa mtandao wa Zoom wakiongezeka kutoka milioni 10 kwa siku hadi milioni 200, Kanisa moja huko Califonia linashtaki kampuni hiyo baada ya mvamizi mmoja kuvamia darasa la mafundisho ya bibilia yaliokuwa yanaendelea mtandaoni na kutuma picha za unyanyasaji wa watoto kingono.

Mvamizi huyo alivamia mkutano huo na kuchezesha picha za video zenye kutatiza akili”, kulingana na kesi iliyowasilishwa na Kanisa la Lutherani la Saint Paulus.

Viongozi wa kanisa la San Francisco waliwasiliana na kampuni ya Zoom kutafuta usaidizi lakini kampuni hiyo haikuchukua hatua yoyote.

Katika taarifa, msemaji wa kampuni ya Zoom ameshtumu tukio hilo baya na la kiovu.

“Tunahuzunika pamoja na wale walioathirika,”kampuni hiyo imesema, “Siku hiyo hiyo tulipogundua tatizo hili, tulimtambua aliyetekeleza kitendo hicho, tukachukua hatua kwa kumfungia asiweze kuingia kwenye mtandao wetu na kuwasilisha taarifa kwa mamlaka husika.”

Kampuni hiyo imezungumzia hatua za kiusalama walizochukua hivi karibuni katika mtandao wao”, na kuongeza kwamba watumiaji wa kampuni ya Zoom hawastahili kushirikisha watu wengi sana namba zao za siri za kuwawezesha kufanya mkutano kama ilivyoonekana kwa kundi hilo la kanisa.

Umaarufu wa mikutano kwa njia ya video kupitia mtandao wa Zoom umeongezeka sana katika miezi ya hivi karibuni hasa kwa wafanyakazi na hata kwa shughuli za kibinafsi wakati ambapo nchi kadhaa zimechukua hatua ya kusalia ndani kama njia ya kukabiliana na virusi vya corona.

Utumiaji mkubwa wa mtandao huo wa zoom umekumbwa na mashaka ya kiusalama na faragha ya watu, ambapo wavamizi wamekuwa wakivamia mikutano ya watu bila kualikwa na wakati mwingine wakituma ujumbe wa chuki, kibaguzi, unyanyasaji au hata picha za ngono.

Kanisa la Saint Paulus – moja ya makanisa ya zamani huko San Francisco – limesema kwamba kesi hiyo iliyowasilishwa katika mahakama moja iliyopo San Jose Jumatano, inalalamikia tukio la Mei 6 wakati wa mafundisho ya bibilia ambayo yalivamiwa na mtu aliyefahamika – ambaye pia ameripotiwa kwa mamlaka mara kadhaa.

Wanafunzi wanane wanaojifunza mafundisho ya bibilia, wengi wao wakiwa wale wanaopokea malipo ya uzeeni, mfumo wao wa kompyuta ulikatishwa wakati mvamizi huyo alipocheza video za ngono.

Wakati ambapo programu ya zoom imeendelea kupata umaarufu, imekumbwa na ukosoaji mkubwa kwasababu za kiusalama.

“Video hizo zilikuwa mbaya na ilikera zaidi kuonesha watu wakubwa wakijihusisha na vitendo vya ngono miongoni mwao, kufanya vitendo vya ngono dhidi ya watoto na wale wachanga, pamoja na kuwanyanyasa kimwili,” kesi hiyo inasema

Wakati wanafunzi hao walipojaribu kufunga video hiyo na kuanza tena, mvamizi huyo alivamia tena, kesi hiyo inaongezea.

Kanisa hilo limewasilisha mashtaka likitaka hatua kuchukuliwa dhidi ya kampuni ya Zoom yenye makao yake San Jose.

Katika kesi hiyo, waliowasilisha mashtaka wanataka kufidiwa kwa madai ya kupuuzwa, kukiukwa kwa mkataba, ukosefu wa haki na tabia zisizofaa katika biashara.

Kampuni ya Zoom iliandika kwenye blogu kwamba imechukua hatua zaidi za kiusalama wiki hii na kuahidi hatua za kuimarishaji usalama ikiwemo mipango ya kumzuia mtu wa kando kuingilia mawasiliano ya mtumiaji.

Awali, kampuni hiyo ilikosolewa kwa kudai kwamba tayari hatua za kumzuia mtu wa kando kuingilia data ya mtumiaji zipo kumaanisha kuwa ni mtumiaji pekee anayeweza kufikia ujumbe wake na video zake.

Kile kilichoikumba kanisa hilo ndicho kilichotokea katika kikao cha bunge cha Afrika Kusini wiki moja iliyopita.

Mkutano wa kamati ya bunge kwa njia ya mtandao Afrika Kusini uliwahi kuvamiwa na wadukuzi na spika kudhalilishwa.


Kikao hicho kilikuwa tu ndio kimeanza picha za ngono zilipojitokeza kwenye skrini huku sauti ya mwanamume ikisikika kumtusi Spika Thandi Modise, ambaye alikuwa mwenyekiti wa kikao hicho.

Spika huyo aliyeshikwa na hasira alipaza sauti akisema hiyo ndio sababu anapinga mikutano ya mitandaoni.

“Hiki kilichotokea ni kilekile nilichokuwa ninakisema kuhusu kufanya mikutano kwa njia ya Zoom!” Modise amenukuliwa akisema hivyo na tovuti ya Times Live.

Wabunge walielezea tukio hilo kama lenye kukera na kutatiza akili, kulingana na Tovuti ya habari ya Eyewitness.

Iliwalazimu wahandisi wa Bunge kutuma kiunganishi kingine ambapo wabunge waliungana tena na kuendelea na kikao chao.

Kampuni ya mtandao wa Zoom imekuwa ikikosolewa kimataifa kwa taarifa kwamba kuna wavamizi wanaotuma picha za ngono au maudhui ya matusi wakati wa mikutano.

Kuvamiwa kwa mtandao kwa njia ya Zoom kumekuwa kukifanyika mara kwa mara katika wiki za hivi karibuni wakati ambapo watumiaji wengi wapya wameanza kutumia mtandao huo kama njia moja ya kukabiliana na kusambaa kwa ugonjwa wa Covid-19 na kuahirishwa kwa mikutano na matukio ambayo awali ilikuwa ifanyike ana kwa ana.

WIZARA YA FEDHA YAWASILISHA BAJETI YAKE KWA MWAKA WA FEDHA 2020/2021 BUNGENI JIJINI DODOMA MEI 15, 2020

$
0
0
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, akiwasilisha Hotuba ya makadirio na mapato ya bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa mwaka wa fedha wa 2020/2021 bungeni Jijini Dodoma Mei 15, 2020

MAELEZO YA MHESHIMIWA DKT. PHILIP I. MPANGO (MB.), WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO WAKATI AKIWASILISHA BUNGENI HOTUBA YA MAKADIRIO YA MAPATO NA
MATUMIZI YA WIZARA YA FEDHA NAMIPANGO
KWA MWAKA 2020/21


1.0 TANGULIZI

1. Mheshimiwa Spika, kutokana na taarifa iliyowasilishwa ndani ya Bunge lako Tukufu na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, iliyochambua bajeti za mafungu ya Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi kwa mwaka 2020/21, naomba kutoa hoja kwamba, Bunge lako Tukufu sasa lipokee na kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa mwaka 2019/20 na kuidhinisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya mafungu saba (7) ya Wizara pamoja na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi kwa mwaka 2020/21.

2. Mheshimiwa Spika, awali ya yote, napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu, kwa kutujalia afya njema pamoja na kutuwezesha kuendelea kutekeleza majukumu yetu kwa Taifa na leo amenipa kibali kusimama mbele ya Bunge lako Tukufu kuwasilisha Mpango na Bajeti ya Wizara yangu kwa mwaka ujao wa fedha.

3. Mheshimiwa Spika, kwa moyo wa dhati kabisa, napenda kutoa shukrani zangu kwa kiongozi wetu, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuniamini kusimamia Wizara ya Fedha na Mipango kwa kipindi chote cha muhula wa kwanza wa Serikali yake.

Ni heshima kubwa kwangu kufanya kazi chini ya Kiongozi Mkuu wa nchi huyu ambaye ana upeo mkubwa sana, mchapa kazi, mwenye uzalendo wa kweli na ambaye ameistaajabisha dunia kwa kutekeleza mambo makubwa ya kimaendeleo kwa kipindi kifupi.

Itoshe tu kusema namshukuru sana, naendelea kumuombea afya njema yeye na familia yake ili kazi kubwa aliyoianza ya kuwaletea maendeleo makubwa wananchi wa Tanzania iweze kukamilika. Ahadi yangu kwa Mheshimiwa Rais na Watanzania ni kuwa, nitaendelea kuchapa kazi katika kipindi chote cha utumishi wangu ili kuenzi nafasi hii adhimu niliyokabidhiwa ya kutoa mchango wangu kwa mama Tanzania.

4. Mheshimiwa Spika, vilevile, napenda nitumie jukwaa hili kuwashukuru na kuwapongeza kwa dhati kabisa, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mhe. Kassim M. Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa namna walivyojitoa katika kuwahudumia Watanzania.

Nimefurahi kufanya kazi chini yao na ninawasihi Watanzania kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupatia wasaidizi hawa waandamizi wa Mheshimiwa Rais ambao ni makini na wenye mapenzi ya dhati kwa nchi yao. Tuendelee kwa pamoja kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu ili waendelee kuwa na afya njema na pia hekima na busara katika kazi zao za kumsaidia Kiongozi Mkuu wa Nchi.

5. Mheshimiwa Spika, napenda kukupongeza wewe binafsi, kwa kusimamia mhimili huu wa Bunge kwa umahiri mkubwa sana.

Aidha, ninakupongeza pamoja na Mheshimiwa Naibu Spika na Wenyeviti wote wa Bunge kwa kuongoza vyema majadiliano ya Bajeti za Wizara mbalimbali. Naomba pia nitumie fursa hii kuishukuru kipekee Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Mashimba Mashauri Ndaki (Mb.), kwa maoni, ushauri na mapendekezo mazuri waliyotupatia wakati wa kuchambua mapendekezo ya Bajeti ya Wizara yangu kwa mwaka 2020/21.

Nakiri kwamba mimi binafsi, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.), Naibu Waziri na Watendaji wa Wizara yetu na taasisi zake tumejifunza mambo mengi mazuri kutokana na hoja na ushauri wa Kamati hii nyeti.

Vile vile, napenda nitumie fursa hii, kuwapongeza sana Waheshimiwa Mawaziri wote wa Serikali ya Awamu ya Tano kwa kusimamia majukumu ya Wizara zao vizuri na kupelekea kupatikana kwa mafanikio makubwa katika utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi 2015 – 2020.

6. Mheshimiwa Spika, naomba nitumie pia nafasi hii kumpongeza sana Comred Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb.) kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria. Aidha, natoa pole kwa Bunge lako Tukufu kwa kumpoteza Mhe. Balozi Dkt. Augustine Philip Mahiga aliyekuwa Mbunge wa Kuteuliwa – CCM na Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Rashid Ajali Akbar, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Newala Vijijini-CCM, Mhe. Mchungaji Dkt. Getrude Pangalile Rwakatare, aliyekuwa Mbunge Viti Maalum – CCM na Mhe. Richard Mganga Ndassa (Senator) aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Sumve-CCM. Tunawaombea ili wapate rehema kwa Mungu, wapumzike kwa amani. Amina.

7. Mheshimiwa Spika, namshukuru sana Mheshimiwa Dkt. Ashatu Kachwamba Kijaji, Mbunge makini wa Kondoa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, kwa msaada mkubwa anaonipatia katika kutekeleza majukumu ya Wizara. Nampongeza sana kwa uchapakazi na kujitoa kwake na napenda niwaombe Wananchi wa Jimbo la Kondoa wamrejeshe kwa kishindo mama huyu Hodari katika Bunge lijalo.

Aidha, nawashukuru sana watumishi wote wa Wizara ya Fedha na Mipango wakiongozwa na Katibu Mkuu ambaye pia ni Mlipaji Mkuu wa Serikali, Bw. Doto M. James, Naibu Makatibu Wakuu Bi. Amina Kh. Shaaban, Bw. Adolf H. Ndunguru na Bi. Mary N. Maganga kwa ushirikiano wanaonipatia katika kutekeleza majukumu ya Wizara. Vile vile, nawashukuru Wakuu wa Mashirika na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango (CAG, BOT, TRA, NBS, TR, TRAT, TRAB, Benki za Serikali, Taasisi 5 za mafunzo ya Elimu ya Juu na Bodi za Kitaaluma na Kitaalam) pamoja na watumishi wote wa taasisi hizo kwa ushirikiano walionipatia katika kipindi chote cha utumishi wangu kama Waziri wa Fedha na Mipango.

8. Mheshimiwa Spika, naomba sasa nijielekeze kwenye hoja yangu. Nitaanza kwa kuelezea mapitio ya utekelezaji wa mpango na bajeti ya Wizara kwa mwaka 2019/20, maeneo ya kipaumbele pamoja na mikakati mbalimbali ambayo itatekelezwa na Wizara kwa mwaka 2020/21. Aidha, nitawasilisha Mpango na Bajeti ya mwaka 2020/21 kwa mafungu saba (7) ya Wizara ambayo ni Fungu 7 – Ofisi ya Msajili wa Hazina, Fungu 10 – Tume ya Pamoja ya Fedha, Fungu 13 – Kitengo cha Udhibiti wa Fedha Haramu, Fungu 21 – HAZINA, Fungu 22 – Deni la Taifa na Huduma Nyingine, Fungu 23 – Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali na Fungu 50 – Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Fungu 45 – Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi.

2.0. MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA MPANGO NA BAJETI YA WIZARA KWA MWAKA 2019/20 NA MALENGO YA MWAKA 2020/21
Mapitio ya Mapato na Matumizi

9. Mheshimiwa Spika, mapitio ya mapato na matumizi ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2019/20 ni kama inavyooneshwa katika hotuba yangu kuanzia ukurasa wa 5 hadi ukurasa wa 8.
Utekelezaji wa Majukumu kwa mwaka 2019/20 na Mpango wa Mwaka 2020/21

10. Mheshimiwa Spika, naomba kulielekeza Bunge lako Tukufu kwa ufupi juu ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara kwa kipindi cha kuanzia Julai 2019 hadi Machi 2020 pamoja na Mpango na Bajeti ya mwaka 2020/21. Maelezo ya kina yapo katika hotuba yangu ukurasa wa 8 hadi wa 33.

(i) Kubuni na Kusimamia Utekelezaji wa Sera za Uchumi Jumla

11. Mheshimiwa Spika, Pato la Taifa limekua kwa asilimia 7.0 mwaka 2019, kama ilivyokuwa mwaka 2018. Sekta zilizoongoza katika ukuaji ni pamoja na Uchimbaji wa Madini na Mawe asilimia 17.7, Ujenzi asilimia 14.1, Sanaa na Burudani asilimia 11.2 na Usafirishaji na Uhifadhi wa Mizigo asilimia 8.7. Sekta zilizokuwa na mchango mkubwa katika Pato la Taifa kwa mwaka 2019 ni: Kilimo (asilimia 26.6); Ujenzi (asilimia 14.3); Biashara na Matengenezo (asilimia 8.8); Viwanda (asilimia 8.5) na Usafirishaji na Uhifadhi mizigo (asilimia 6.9). Aidha, mfumuko wa bei umeendelea kubaki katika wigo wa tarakimu moja ambapo kwa mwezi Machi 2020, ulikuwa asilimia 3.4.

12. Mheshimiwa Spika, kutokana na uchambuzi wa awali, shabaha za uchumi jumla katika mwaka 2020/21 ni kama ifuatavyo: Pato halisi la Taifa linatarajiwa kukua kwa asilimia 4.0 mwaka 2020; mfumuko wa bei kubaki katika wigo wa tarakimu moja; nakisi ya bajeti ya Serikali kufikia asilimia 2.8; mapato ya ndani asilimia 14.5 ya Pato la Taifa; na mapato ya kodi asilimia 12.5 ya Pato la Taifa. Matarajio haya yanatarajiwa kupungua kutegemea ukubwa wa athari za mlipuko wa ugonjwa wa homa kali ya mapafu (unaosababishwa na Virusi vya CORONA) kwenye sekta mbalimbali.

(ii) Uandaaji, Utekelezaji na Usimamizi wa Mikakati, Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Bajeti ya Serikali

13. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia mwezi Machi 2020, Wizara ilifanikiwa kuandaa Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2020/21; kuandaa taarifa ya Hiari ya Nchi Kuhusu Utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030 (SDGs); kuunda mfumo wa kitaasisi wa ufuatiliaji na utoaji wa taarifa za utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030 pamoja na mfumo wa awali (prototype) wa Kanzidata ya Kuhifadhi na Kutoa Taarifa za Miradi ya Maendeleo.

14. Mheshimiwa Spika, Wizara imechukua hatua za kimkakati za kuimarisha ukusanyaji wa mapato kama zinavyoonekana katika hotuba yangu ukurasa wa 11 hadi wa 14. Hatua hizo zimeiwezesha Serikali kukusanya mapato ya ndani ya jumla ya shilingi trilioni 16.06 katika kipindi cha Julai 2019 hadi Machi 2020, sawa na asilimia 92.4 ya lengo. Mapato ya ndani yameongezeka kutoka shilingi trilioni 14.07 hadi shilingi trilioni 16.06, sawa na asilimia 14.2 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2018/19.

15. Mheshimiwa Spika, kati ya Julai 2019 na Machi 2020, Wizara imefanikisha upatikanaji wa fedha za misaada na mikopo nafuu ya jumla ya shilingi trilioni 2.04 sawa na asilimia 93 ya lengo la kipindi hicho la shilingi trilioni 2.78. Aidha, Wizara imefanikisha mkopo wa kiasi cha shilingi trilioni 3.44 kutoka katika soko la ndani, sawa na asilimia 101.5 ya lengo la kukopa shilingi trilioni 3.39 na mkopo wa shilingi trilioni 1.82 kutoka soko la nje sawa na asilimia 78.66 ya lengo la kukopa shilingi trilioni 2.32.

16. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia mwezi Machi 2020, jumla ya shilingi trilioni 24.65 zilitolewa kwa ajili ya kugharamia utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Serikali. Kati ya kiasi hicho, shilingi trilioni 1.16 zimetolewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya kielelezo na shilingi bilioni 597.54 kwa ajili ya kulipa madai yaliyohakikiwa. Aidha, jumla ya shilingi bilioni 33.98 sawa na asilimia 84.95 ya bajeti iliyotengwa zimetolewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi 18 ya kimkakati inayotekelezwa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

(iii) Kubuni, Kuunda na Kusimamia Mifumo ya Usimamizi wa Fedha na Mali za Umma

17. Mheshimiwa Spika, Wizara imeboresha Mfumo wa Ukusanyaji wa Mapato ya Serikali (GePG) kwa kuongeza huduma kwa njia ya simu za kiganjani (GePG application mobile) na kwa kuunganisha mfumo huo na mifumo ya Mamlaka ya Mapato Tanzania ya ukusanyaji wa mapato. Utekelezaji wa jukumu la kubuni, kuunda na kusimamia mifumo ya usimamizi wa fedha na mali za umma umefafanuliwa kwa kina katika hotuba yangu ukurasa wa 14 hadi wa 15.

(iv) Usimamizi wa Sekta ya Fedha

18. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia mwezi Machi 2020, Wizara imefanikiwa kukamilisha uandaaji wa Kanuni za Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya Mwaka 2018 ambapo zilianza kutumika rasmi mwezi Novemba 2019. Aidha, Wizara imeanza kutekeleza Mpango Maalum wa Elimu kwa Umma kuhusu sekta hii ili kujenga uelewa kwa wananchi. Vile vile, Wizara imekamilisha kuandaa Mpango Kabambe wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha pamoja na Kanuni za Kumlinda Mtumiaji wa Huduma za Fedha. Ukurasa wa 16 -17 wa hotuba yangu unaainisha kwa kina kazi nyingine zilizofanyika katika kutekeleza jukumu hili muhimu kwa uchumi wetu kati ya Julai 2019 na Machi 2020.

(v) Usimamizi wa Deni la Serikali

19. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia mwezi Machi 2020, Serikali ilifanikiwa kulipa deni lake lote lililoiva lenye thamani ya shilingi trilioni 6.19. Kati ya kiasi hicho, Deni la Ndani ni shilingi trilioni 4.06 ikijumuisha riba shilingi trilioni 1.09 na mtaji shilingi trilioni 2.98. Aidha, Deni la Nje ni shilingi trilioni 2.13 ikijumuisha riba ya shilingi bilioni 636.75 na mtaji shilingi trilioni 1.49.

(vi) Ubia kati ya Sekta ya umma na sekta binafsi

20. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia mwezi Machi 2020, Wizara imefanikisha kutungwa kwa Kanuni za Sheria ya Ubia za Mwaka 2020 na kutangazwa katika Gazeti la Serikali Na.37. Aidha, Wizara imeendelea kupokea, kuchambua na kutoa ushauri kwa Mamlaka za Serikali zinazotekeleza miradi ya PPP ipatayo 10 ambayo ipo katika hatua za awali za kutafuta wabia, washauri elekezi, kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina.

21. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2020/21, Wizara inatarajia kukamilisha taratibu za kuanzisha kituo cha ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi – PPP Center.
(vii) Usimamizi wa Taasisi na Mashirika ya Umma

22. Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Msajili wa Hazina imeendelea kutekeleza jukumu lake la Usimamizi wa Taasisi na Mashirika ya Umma kama inavyooneka katika hotuba yangu ukurasa wa 23 -24. Aidha, hadi kufikia mwezi Machi 2020, Mfuko Mkuu wa Serikali umepokea jumla ya shilingi bilioni 612.87 kutoka kwenye Taasisi na Mashirika ya Umma kama gawio na michango ya Mashirika.

(viii) Taasisi za Mafunzo ya Elimu ya Juu na Bodi za Kitaaluma na Kitaalamu

23. Mheshimiwa Spika, Wizara inasimamia Taasisi tano (5) za mafunzo ya elimu ya juu na Bodi mbili (2) za kitaaluma na kitaalamu ambazo ni: Chuo cha Usimamizi wa Fedha -IFM; Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini – IRDP; Taasisi ya Uhasibu Tanzania – TIA; Chuo cha Uhasibu Arusha –IAA; Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika – EASTC; Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi – PSPTB na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu – NBAA. Utekelezaji wa majukumu ya taasisi hizo na mpango wa utekelezaji kwa mwaka 2020/21 ni kama inavyoonekana katika kitabu cha hotuba yangu ukurasa wa 24 -27.

(ix) Mafao ya Wastaafu na Mirathi

24. Mheshimiwa Spika, kati ya mwezi Julai 2019 na Machi 2020, Wizara imelipa mafao na pensheni kwa wastaafu wa Serikali 57,605, mirathi kwa warithi 1,006 na malipo ya kiinua mgongo kwa watumishi 457 wa Serikali walio kwenye mikataba. Aidha, Wizara imeandaa vitambulisho vipya vya wastaafu vya kielektroniki katika mfumo wa “smart cards” na kuboresha Mfumo wa unaotumika kutoa huduma kwa njia ya mtandao na kudhibiti fedha za mirathi zinazotoka HAZINA kwenda moja kwa moja kwenye akaunti za warithi (Tanzania Pensioners Payment System – TPPS).

(x) Tume ya Pamoja ya Fedha

25. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/20, Tume ya Pamoja ya Fedha imefanya stadi maalum kuhusu Mfumo wa Biashara kati ya Tanzania Bara na Zanzibar na Mwenendo wa Mapato ya Muungano. Aidha, Tume imefanya uchambuzi wa taarifa na takwimu halisi za Mapato na Matumizi ya Muungano kwa mwaka 2017/18, mwaka 2018/19 na 2019/20. Taarifa ya uchambuzi wa takwimu hizo ilijadiliwa na Sekretarieti ya Tume mwezi Februari, 2020 na Serikali za pande zote zinaendelea kufanyia kazi mapendekezo yaliyomo katika taarifa hiyo.

(xi) Sekta ya Michezo ya kubahatisha

26. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia mwezi Machi 2020, Wizara imewezesha marekebisho ya Sheria ya Michezo ya Kubahatisha SURA 41 ili kuipa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha mamlaka ya kuratibu, kusimamia na kudhibiti matangazo ya michezo ya kubahatisha. Aidha, Bodi inaendelea kuunda na kuunganisha mifumo ya TEHAMA ili kuimarisha udhibiti wa michezo ya kubahatisha.

(xii) Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi

27. Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha uwazi na uwajibikaji kwenye matumizi ya rasilimali za umma, hadi kufikia Machi 2020, Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi imefanya ukaguzi kwa mafungu 66 ya Wizara na Idara za Serikali; Wakala 33; Taasisi 48; Balozi 42; Vyama vya Siasa 19; Bodi za Mabonde ya Maji 14; Hospital za Rufaa 27, Mashirika ya Umma 150; Mamlaka za Serikali za Mitaa 185; Mikoa 26; na Mifuko Maalumu 16. Aidha, ofisi imefanikiwa kufanya ukaguzi wa usimamizi wa mikataba ya ujenzi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa 19. Vile vile, ukaguzi umefanyika kwa miradi ya maendeleo 435 ikijumuisha miradi 65 ya Serikali Kuu na miradi 370 ya Serikali za Mitaa.

28. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2020/21, Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi imepanga kuimarisha ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo hadi ngazi za Tarafa, Kata na Vijiji; kufanya ukaguzi wa miradi mikubwa ya maendeleo (Reli ya Kisasa, Vivuko, Bomba la Gesi Mtwara na Ukarabati wa Reli ya Kati); kupanua mawanda ya ukaguzi katika eneo la uchimbaji wa madini, mafuta na gesi ikiwemo kuimarisha ukaguzi wa kiuchunguzi na kiufundi; na kuendelea kufanya ukaguzi wa Serikali Kuu, Serikali za Mitaa, Mashirika ya Umma pamoja na kufanya ukaguzi wa ufanisi.

Changamoto na Mikakati ya Kukabiliana nazo

Changamoto


29. Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa majukumu ya Wizara unakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo tunaendelea kukabiliana nazo kwa kushirikiana na wadau wengine ili zisilete athari hasi katika malengo tuliyojiwekea. Baadhi ya changamoto hizo ni:

(i) Kasi ndogo ya ufuatiliaji na tathmini ya miradi na programu za maendeleo katika Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala, Taasisi za Umma, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa;
(ii) Mabadiliko ya mara kwa mara ya teknolojia ya mifumo ya usimamizi na ukusanyaji wa mapato yanayoleta uhitaji wa upatikanaji wa teknolojia mpya na kuboresha na kuhuisha teknolojia ya mifumo iliyopo ili kuongeza ufanisi;
(iii) Kuongezeka kwa gharama za mikopo kwenye masoko ya fedha duniani kutokana na mabadiliko ya sera za fedha katika nchi zilizoendelea (hususan Marekani na Nchi za Ulaya);
(iv) Uharibifu wa miundombinu ya barabara na madaraja kutokana na mafuriko; na
(v) Mlipuko wa ugonjwa wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na virusi vya corona (COVID-19).

Mikakati ya Kukabiliana na Changamoto

30. Mheshimiwa Spika, Baadhi ya hatua zinazochukuliwa na Wizara katika kukabiliana na changamoto za utekelezaji wa majukumu yake ni pamoja na:

(i) Kuanza mchakato wa kutunga sera na mkakati wa ufuatiliaji na tathmini ya miradi na programu za maendeleo;
(ii) Kujenga uwezo wa wataalam wa ndani katika kubuni, kuunda na kuhuisha teknolojia ya mifumo ya usimamizi na ukusanyaji wa mapato;
(iii) Kuhamasisha wadau wa ndani kuendelea kushiriki katika minada ya dhamana za Serikali pamoja na kutafuta vyanzo vingine vya mikopo ya nje vyenye riba nafuu; na
(iv) Wizara imekamilisha uchambuzi wa taarifa mbalimbali za kisekta ili kubaini kiwango cha athari zitokanazo na mlipuko wa ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona (COVID-19) katika uchumi na kuainisha mikakati ya muda mfupi, wa kati na mrefu ya kukabiliana nazo. Taarifa jumuishi ya mikakati ya kupambana na CORONA imewasilishwa kwenye ngazi za maamuzi Serikalini.

3.0 MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA 2020/21


(i) Makadirio ya Mapato

31. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2020/21, Wizara inakadiria kukusanya maduhuli ya kiasi cha shilingi bilioni 973.02 kutoka katika vyanzo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na gawio, kodi za pango, marejesho ya mikopo, michango kutoka katika taasisi na mashirika ya umma, mauzo ya leseni za udalali na nyaraka za zabuni. Mchanganuo wa maduhuli yanayokadiriwa kukusanywa umeoneshwa katika kitabu cha hotuba ukurasa wa 34 katika Jedwali Na. 4.

(ii) Makadirio ya Matumizi

32. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2020/21, Wizara ya Fedha na Mipango inaomba kuidhinishiwa jumla ya shilingi trilioni 12.39 kwa mafungu yote saba (7) kwa ajili ya matumizi ya kawaida na maendeleo. Kati ya kiasi hicho, shilingi trilioni 11.73 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi bilioni 659 kwa ajili ya matumizi ya maendeleo. Kati ya matumizi ya kawaida, shilingi trilioni 10.48 kwa ajili ya deni la Serikali, shilingi bilioni 750.29 matumizi mengineyo na shilingi bilioni 510 kwa ajili ya mishahara na marekebisho ya mishahara. Aidha, matumizi ya maendeleo yanajumuisha shilingi bilioni 624.7 fedha za ndani na shilingi bilioni 34.61 fedha za nje.

33. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2020/21, Fungu 45 – Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi inaomba kuidhinishiwa kiasi cha shilingi bilioni 80.5 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na ya maendeleo. Kati ya kiasi hicho, shilingi bilioni 68.87 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi bilioni 11.66 matumizi ya maendeleo. Matumizi ya kawaida yanajumuisha shilingi bilioni 14.88 kwa ajili ya mishahara na shilingi bilioni 53.99 matumizi mengineyo. Aidha, matumizi ya maendeleo yanajumuisha shilingi bilioni 6.70 fedha za ndani na shilingi bilioni 4.96 fedha za nje. Mchanganuo wa kiasi kinachoombwa kwa kila fungu umeainishwa katika Jedwali Na. 5 lililopo katika hotuba yangu ukurasa wa 35.

4.0 HITIMISHO

34. Mheshimiwa Spika, kama nilivyotangulia kusema awali, Mkutano huu wa Bunge ni wa mwisho katika muhula huu wa kwanza wa Serikali ya Awamu ya Tano. Napenda kutumia fursa hii kukiri kuwa, katika kipindi chote cha muhula huu, Wizara imenufaika sana na maoni na ushauri kutoka kwa Waheshimiwa Wabunge wote ambao umesaidia kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi na kuimarisha uchumi wa nchi yetu.

35. Mheshimiwa Spika, kwa mara nyingine, naomba nirudie kumshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kufanya kazi yake hii ya Waziri wa Fedha na Mipango aliyonipa kupitia Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha, namshukuru tena Mheshimiwa Rais, kwa kuendelea kuniamini katika nafasi hii ngumu kwa miaka mitano mfululizo. Vilevile, napenda kuwashukuru wananchi wote wa Tanzania hususan kwa kufanya kazi na kulipa kodi ili kujenga uchumi wa nchi yetu. Nawaomba Watanzania tuendelee kuchapa kazi kama anavyotuasa Mheshimiwa Rais wetu na kuitekeleza kwa vitendo kaulimbiu ya “HAPA KAZI TU”.

36. Mheshimiwa Spika, kutokana na janga la mlipuko wa ugonjwa wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na virusi vya corona (COVID-19), napenda kuchukua fursa hii kutoa pole kwa wananchi wote waliopatwa na madhara yanayotokana janga hili na kuwaasa kuendelea kuchukua hatua za kujikinga na ugonjwa huu kama inavyoelekezwa na wataalamu wa afya. Aidha, napenda kuwapongeza kwa dhati madaktari na watumishi wote wa Afya walio mstari wa mbele siku zote katika kutoa huduma kwa wananchi hasa wanyonge na hususan katika kipindi hiki cha mlipuko wa COVID-19 nchini.

37. Mheshimiwa Spika, mwisho kabisa, napenda nikushukuru tena kwa kunipa nafasi ya kuwasilisha hoja hii pamoja na Waheshimiwa Wabunge wote kwa kunisikiliza. Aidha, nawashukuru wote walioshiriki katika maandalizi ya hotuba hii na kuhakikisha inakamilika kwa wakati. Hotuba hii inapatikana katika tovuti ya Wizara kwa anuani ya www.mof.go.tz.

38. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.

NAIBU SPIKA MGENI RASMI KATIKA MAADHIMISHO YA KILELE CHA WIKI YA WAUGUZI JIJINI DODOMA

$
0
0
Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson akikata utepe kuzindua Wodi ya Upasuaji ya Wanawake katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma ambayo ilikuwa katika marekebisho wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya Wauguzi. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge na kushoto kwake ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dkt. Ernest Ebenzi.
Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson akikata utepe kuzindua Wodi ya Upasuaji ya Wanawake katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma ambayo ilikuwa katika marekebisho wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya Wauguzi. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge na kushoto kwake ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dkt. Ernest Ebenzi. 
Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya Wauguzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge na kushoto kwake ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dkt. Ernest Ebenzi.
Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson akikagua ukarabati uliofanyika katika Wodi ya Watoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya Wauguzi. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge na Wakwanza kulia ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dkt. Ernest Ebenzi.
Baadhi ya Wauguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma wakila kiapo cha utendaji kazi wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya Wauguzi Duniani.
Baadhi ya Wauguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma wakimsikiliza Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya Wauguzi Duniani.
(PICHA NA BUNGE)

Takukuru yaiweka mtu kati TFF

$
0
0
By Elizabeth Edward, MWANASPOTI

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru), imefichua kuanza uchunguzi juu ya matumizi mabaya ya fedha kiasi cha zaidi ya Shilingi 1 bilioni kilichotolewa na serikali na wadau wengine kwa ajili ya kufanikisha Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Vijana chini ya Umri wa miaka 17 (Afcon U17) zilizofanyika mwaka jana.

Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbung'o alisema kuwa fedha hizo ambazo kiasi kikubwa kilitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli, hakikutumika vizuri na wamegundua viashiria vya ubadhilifu.

"Lakini baada ya Mheshimiwa Rais kuonyesha mfano wa kuchangia, wako wadau wengine waliojitokeza.Kuna mashirika mbalimbali yalihusika kuchangia fedha.

Sasa zile fedha kweli zimetumika vibaya na taasisi inazo taarifa. Imechukua hatua za kufanya uchunguzi. Na huu uchunguzi uko vizuri. Tunawaita watu wote wanaohusika au wanaohisiwa kuhusika kwa namna yoyote ile ya ugawaji au usimamiaji wa hizo fedha.

Tunawaita wanakuja hapa, tunawahoji. Tunaendelea kukusanya nyaraka mbalimbali zinazoonyesha ukusaji wa ile fedha na matumizi yake zilivyotumika.Kwa hiyo niseme tu kwamba uchunguzi unaendelea na huu ni uchunguzi wa kijinai. Hawa watu wana hiari ya kuanza kurejesha hizo fedha lakini uchunguzi upo na unafanyika na wahusika wote wanaitwa Takukuru," alisema Brigedia Jenerali Mbung'o.

Rais Magufuli alitoa mchango huo wa fedha kulisaidia Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuandaa fainali hizo zilizofanyika kuanzia Aprili 14 hadi 18 mwaka jana.
Cameroon waliibuka mabingwa wa mashindano hayo baada ya kuichapa Guinea kwa mikwaju ya penati 5-3 kufuatia timu hizo kutoka sare tasa katika dakika 120 za mchezo.

MSIBA DMV NA DELAWARE

$
0
0
Taswira inaweza kujumuisha: Mtu 1, uwezekano wa matini yanayosema 'va RIP Bro Emmanuel Bandawe'
Familia ya Bandawe ikishirikiana na
JUMUIYA YA ATC/ DMV inasikitika kutangaza msiba wa mpendwa wao, Mr. Emmanuel Bandawe, Mwana DMV kwa zaidi ya miaka 20,uliotokea Delaware siku ya Jumamosi May 16, 2020 katika Hospital ya Delaware Memorial.

Marehemu anatarajiwa kuzikwa Delaware tarehe na siku inategemea na michango ya rambirambi itakavyokwenda.

Makadirio ya gharama ya Funeral home na maziko ya mpendwa wetu ni $10,500.

Tunaomba tuunganishe nguvu ya pamoja tumpumzishe mpendwa wetu, tafadhali Tuma rambirambi kupitia
*CashApp/Zelle*
*Lysa (Elizabeth)Bantu*(919) 452-2746*

Rambirambi
1. Vitalis Gunda $75
2. Ibra Nyagali $50
3. Linda Mwamba $50
4. Fellah & Lina $100
5. Joyce Cottrell $100
6. Richard and Melissa $100
7. Zelda & Tony Mwingira $100
8. Lulu $100
9. Irene Bomani $50
10. Pili Mnzavas-Wood $50
11. Lusajo Kibonde $50
12. Alu and Julius Nyangoro $100
13. Sia Makundi $50
14. Stella $60
15. Peter Kirigiti $100
16. Nunu Mwilima $100
17. Arthur Gao $50
18. Fadhili Malima $100
19. Mariam Kalala & Pendo Nyangoro $200
20. Abbas Mattaka $200
21. Neesha Jurobi $100
22. Saada Gaddies $100
23. Loveless Mamuya $100
24. Sunday & Elinita $100
25. Ally & Mariam Idowa $150
26. Peace Kachuchuru $100
27. Janice & Julius Manase $50
28. Khadija Riyami $50
29. Mariam Aranga $50
30. Danny & Ummy $100
31. Mwamoyo Hamza $100
32. Jabiri Jongo $60
33. Honest Mulamula $50
34. Mch John Mbatta $75
35. KC & Thecla $200
36. Adam Fred Tenga $100
*Total received $3,271*
Kwa mawasiliano zaidi:
Mr. Lucas Mukami +1 443-401-6554
Cleopatra Kulasi +1 202-378-8079
Dorothy Soukou (805) 708-0012
Abdul Kufakunoga (248) 515-5509
Abbas Mataka +1 (301) 537-7854
Dr. Mwamoyo Hamza (301) 922-0618
Liberatus Mwang'ombe
+1 240-423-3331
Tunatanguliza shukurani na Mwenyezi Mungu akuongezee pale ulipopunguza.
BWANA AMETOA, BWANA AMETWAA NA JINA LAKE LIHIMIDIWE
*Update as of 8:20pm next update at 1pm 5/18*

Standard Chartered Bank becomes the first Bank to announce COVID-19 Relief Measures for its clients

$
0
0
Standard Chartered Bank Tanzania has become the first Bank in Tanzania to announce relief measures for its Individual and Business Clients whose income and cash flows have been affected by the COVID-19 pandemic. 

In a statement issued by the Bank, Mr. Ajmair Riaz, the Bank’s Country Head of Retail Banking, said that his team has been working very closely with the Bank’s clients in the Individual and Business segments to understand the financial challenges that they are facing during this unprecedented time.      

“During this unprecedented period, we understand the challenges that prevail including from a financial aspect. In this regard, we have been reaching out to our clients to discuss how the pandemic is affecting them and the various challenges that they are facing. 

We have, therefore, based on discussions with our various clients, decided to take proactive actions to introduce relief measures that will ease the financial burden for our Individual and Business Clients whose income and cash flows have been impacted by the COVID-19 pandemic.” Mr. Riaz said.    


Mr. Riaz added that his Bank has looked into a number of options for supporting its clients and had narrowed down to two effective measures which comprise of either a payment holiday or tenor extension for loan repayments. 
He highlighted that these options are open to Individual clients who have Personal Loans or Mortgages with the Bank, as well as Business Clients, mainly in the SME sector, who have taken loans from the Bank. He also added that the relief measures which will be granted to the Bank’s clients, will be based on a criteria that will consider financial impact arising from cases such as unpaid leave, salary reduction, job loss, infected customers, loss of business and other reasons that the Bank may find reasonable during this unprecedented time.

Speaking about the specific options of the relief measures Mr. Riaz explained that clients who opt for the option of a payment holiday will get a three-month moratorium, and the option of the extension of the Loan Tenure entails a twelve-month additional period to make repayments, resulting into smaller repayment instalments that the Bank’s clients can bear. 

“Our Clients continue to be the reason why we are in business, and why we are ‘Here for good’ as per our Brand Promise. We are also committed to enhancing prosperity for our clients. As we go through this unprecedented period, we remain committed to supporting them to come out of it with minimal impact, if any, on their financial status. We, therefore, believe that the options of a three-month moratorium, and a twelve-month extension on the loan repayments tenure will go a long way in minimizing the financial impact to our clients, and we will discuss these options with them accordingly as and when we receive their requests.” Mr. Riaz added.  

As the country continues to combat the spread of the pandemic, Mr. Riaz urged the Bank’s clients to further leverage on the Bank’s Digital capabilities. He highlighted that the Bank’s Full Digital Bank on Mobile offers more than seventy banking services thus enabling users to carry out all their transactions without needing to come to any of the Bank’s branches. 

“As we go through this period, the health of our clients is our priority. In this regard, we continue to advocate for, and drive branchless and cashless banking. With our Full Digital Bank on Mobile our clients need not visit any of our branches. They can make their utility payments, move money from their accounts to their mobile phone accounts, and vice versa, they can carry out foreign currency transactions as well as manage their Debit Cards, from activating to deactivating them. All these can be done from the safety of our clients’ premises.” Mr. Riaz said. 

Touching on the Bank’s SME clients, Mr. Riaz said that the Bank’s enhanced Straight2Bank Digital Platform enables business owners to fully carry out their financial obligations including payment of salaries, Tax payments as well as payment to vendors, among other obligations, at the safety of their premises. 

“I’d like to remind our clients to continue using our Digital Banking capabilities to reduce physical interaction at branches and decrease the handling of cash.  We should also continue to follow the Government’s and Medical Experts’ precautionary measures. I believe that we will make it through when we stay diligent, keep our hope towards the future, and foster cooperation. We continue to be committed to doing the best we can for our clients in these unprecedented times.” Mr. Riaz concluded.

Rais Magufuli Afiwa na Dada Yake

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitoa heshima za mwisho msibani katika mtaa wa Msilale Chato mkoani Geita wakati wa kuaga mwili wa Marehemu Dada yake Gaudensia Felician Marko Msangwa aliyefariki Dunia jana tarehe 17 Mei 2020, Chato mkoani Geita


KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA AWAPATIA TANZANIA PRISONS SPORTS CLUB BASI JIPYA DOGO AINA YA COSTA

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Magereza, Suleiman Mzee(katikati) akionesha kadi ya gari jipya la Tanzania Prisons SC hivi karibuni katika Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Dodoma kabla ya kumkabidhi Mkuu wa Sehemu ya Michezo katika Jeshi la Magereza, SSP. Matilda Mlawa(wa kwanza kulia). Kushoto ni Kaimu Kamishna Divisheni ya Sheria na Uendeshaji wa Magereza, SACP. George Mwambashi.
ni Muonekano wa Basi jipya dogo la Klabu ya mpira wa miguu ya Jeshi la Magereza(Tanzania Prisons Sport Club) lilonunuliwa kwa thamani ya Tsh. Milioni 75.
ni Muonekano wa Basi jipya dogo la Klabu ya mpira wa miguu ya Jeshi la Magereza(Tanzania Prisons Sport Club) lilonunuliwa kwa thamani ya Tsh. Milioni 75.
ni Muonekano wa Basi jipya dogo la Klabu ya mpira wa miguu ya Jeshi la Magereza(Tanzania Prisons Sport Club) lilonunuliwa kwa thamani ya Tsh. Milioni 75.

Na ASP. Lucas Mboje, Dodoma.

KATIKA kutatua changamoto ya usafiri kwa Klabu ya mpira wa miguu ya Jeshi la Magereza(Tanzania Prisons SC). Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Suleiman Mzee ameipatia Klabu hiyo Basi dogo aina ya Costa lenye thamani ya Tsh. Milioni 75 kwa ajili ya kuisafirisha Timu kwenda mikoa mbalimbali nchini.

Akizungumza katika makabidhiano ya gari hilo hivi karibuni jijini Dodoma, Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Suleiman Mzee amesema kuwa kwa muda mrefu Klabu hiyo haikuwa na usafiri hivyo iliwalazimu Uongozi wa Klabu kukodi magari hivyo kuongeza gharama za uendeshaji wa Klabu.

"Nimefanya maamuzi ya kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa changamoto ya usafiri kwa Timu yetu na katika kupunguza gharama za kukodi magari hivyo nimewapatia Basi dogo jipya kwa ajili ya Timu ili waweze kulitumia kwenda sehemu mbalimbali nchini kwa mujibu wa ratiba za Ligi Kuu", amesema Kamishna Jenerali Mzee.

Kwa upande wake Mkuu wa Sehemu ya Michezo, Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, SSP. Matlida Mlawa akizungumza kwa niaba ya Uongozi wa Klabu hiyo amemshukru sana Kamishna Jenerali wa Magereza Suleiman Mzee kwa kutatua changamoto hiyo ya usafiri lakini pia kwa kuthamini tasnia ya michezo Jeshini.

"Nichukue nafasi ya kipekee kumshukru Kamishna Jenerali Suleiman Mzee kwa kutupatia usafiri huu na nina imani kubwa kwamba ataleta mageuzi makubwa ndani ya Jeshi la Magereza", amesema SSP. Mlawa.

Klabu ya Jeshi la Magereza Tanzania Bara ilianzishwa mwaka 1996 na imekuwa na historia kubwa katika tasnia ya mchezo wa mpira wa miguu nchini ambapo Mwaka 1999 Timu ya Tanzania Prisons SC iliweza kuchukua ubingwa wa Ligi ya Muungano chini ya Kocha Mkuu Boniphace Mkwasa. Klabu hiyo ina makazi yake jijini Mbeya na inashiriki Ligi Kuu Tanzania Bara iliyosimama kufuatia uwepo wa ugonjwa wa Corona nchini - COVID19.

Mbunge Lijualikali Aangua Kilio Bungeni I Asema Amechoka Kutumika CHADEMA I Aomba Kujiunga CCM

BUNGE LA 11 KUVUNJWA JUNI 19, 2020: SPIKA NDUGAI ASEMA

$
0
0
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na waandishi wa habari katika kikao kilichofanyika nyumbani kwake uzunguni Jijini Dodoma Mei 18, 2020. Mhe. Ndugai ametangaza mabadiliko ya ratiba ya shughuli za Bunge la 11 ambapo bajeti kuu ya serikali itasomwa tarehe 11 Juni 2020 na shughuli za Bunge zitamalizika Juni 19, 2020 ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli atatoa hotuba ya mwisho ya kulivunja bunge.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akiongoza kikao cha kamati ya uongozi kilichokaa ili kupokea Mapendekezo ya Mabadiliko ya Ratiba ya Mkutano wa 19 wa Bunge leo nyumbani kwake uzunguni Jijini Dodoma Mei 18, 2020.

NAIBU WAZIRI MABULA ATAKA WADAIWA SUGU KODI YA ARDHI KUBANWA

$
0
0
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akimsikiliza Mtaalamu Mshauri wa Mradi wa Kurasimisha Ardhi Vijijini unaotekelezwa na Shirika la Feed the Future Bw. Malaki Msigwa (Kulia) alipotembelea Masijala ya Ardhi ya Halmashauri ya wilaya ya Iringa wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi na kufuatilia wadaiwa sugu wa kodi ya ardhi tarehe 16 Mei 2020.
Naibu Waziri wa Adhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akimkabidhi Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka mkoa wa Iringa (IRUWASA) Gilbert Kayange taarifa inayoonesha kiasi cha kodi ya pango la ardhi inachodaiwa Mamlaka hiyo tarehe 16 Mei 2020 wakati wa zoezi lake la kuwafikia wadaiwa sugu wa kodi ya ardhi katika mkoa wa Iringa.
Naibu Waziri wa Adhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akimsikiliza Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka mkoa wa Iringa (IRUWASA) Gilbert Kayange baada ya kumpatia taarifa inayoonesha kiasi cha kodi ya pango la ardhi inachodaiwa Mamlaka hiyo wakati wa zoezi lake la kuwafikia wadaiwa sugu wa kodi ya ardhi katika mkoa wa Iringa tarehe 16 Mei 2020. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akioongozwa na Kamishna Msaidizi wa Ardhi mkoa wa Iringa Wenslaus Mtui kutoka katika Tawi la Benki ya CRDB Iringa wakati wa zoezi lake la kuwafikia wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi katika mkoa wa Iringa tarehe 16 Mei 2020.

Na Munir Shemweta, WANMM IRINGA
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angelina Mabula amezitaka halmashauri zote nchini kuhakikisha zinapeleka hati za madai ya kodi ya pango la ardhi kwa wadaiwa sugu wa kodi hiyo kuanzia jumatatu tarehe 18 Mei 2020 na watakaokaidi kulipa kwa hiari wafikishwe kwenye Mabaraza ya Ardhi ya Nyumba ya Wilaya.
Dkt Mabula alitoa maagizo hayo tarehe 16 Mei 2020 akiwa katika ziara yake mkoani Iringa kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi sambamba na kufuatilia wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi katika baadhi ya Taasisi zilizopo katika halmashauri za Manispaa na wilaya ya Iringa.
Katika ziara yake Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliwafikia wadaiwa sugu wakubwa wa mkoa wa Iringa ambao ni Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka mkoa wa Iringa (IRUWASA) , Shirika la Umeme mkoa wa Iringa, Benki ya CRDB, Hoteli ya Peacoc na kituo cha Radio cha EBONY ambao kwa pamoja wanadaiwa zaidi ya milioni 128.
Dkt Mabula alizitaka idara za ardhi katika halmashauri zote nchini kupitia kumbukumbu za wadaiwa wa kodi ya pango la ardhi vizuri na kuwaandikia Hati za Madai zitakazowataka wadaiwa kulipa kwa hiari madeni yao na watakaokaidi wafikishwe katika Mabaraza ya Ardhi ya Nyumba ya Wilaya.
‘’ Wdaiwa wote sugu wa kodi ya pango la ardhi baada ya hati ya madai kupelekwa wawe wamelipa kodi hiyo kwa hiari ndani ya siku kumi na nne na wakishindwa wafikishwe kwenye mabaraza ya ardhi ya nyumba ya wilaya, tunataka Ikifika juni 30, 2020 Wizara iwe imekamilisha kukusanya Bilioni 180 kama ilivyojiwekea katika malengo yake’’ alisema Dkt Mabula
Akiwa ofisi za Shirika la Umene mkoa wa Iringa, Naibu Waziri wa Ardhi alimueleza Meneja wa mkoa wa Shirika hilo Richard Swai kuwa, shirika lake linadaiwa milioni 384 kama kodi ya pango la ardhi kwa kushindwa kulipa kodi hiyo katika kipindi cha miaka mitatu katika eneo inalomiliki la Mtera na kutaka kupewa ahadi ya maandishi itakavyofanikisha kulipa deni hilo.
Meneja wa TANESCO Iringa Swai alieleza kuwa, eneo linalodaiwa liko chini ya idara ya Uzalishaji Makao Makuu na malipo yake hufanywa huko ambapo alimuahidi Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kulifanyia kazi suala hilo.
Kwenye ofisi za Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Iringa (IRWASA) Dkt Mabula baada ya kumueleza Mkurugenzi wake Gilbert Kayange kuhusiana na deni la Mamlaka hiyo katika maeneo ya Gangilonga na Itamba linalofikia milioni 104.1, Mkurugenzi huyo alisema, Mamlaka yake imekuwa ikilipa kodi hiyo ingawa kuna tofauti ya kiwango cha deni walichopelekewa na kumbukumbu walizo kuwa nazo jambo alilolieleza kuwa limeifanya Mamlaka yake kutaka kukaa pamoja na halmashauri husika ili kufanya uhakiki.
Katika hatua nyingine, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameitaka idara ya ardhi katika halmashauri ya wilaya ya Iringa kuhakikisha kufikia ijumaa tarehe 22 Mei 2020 inazipeleka Hati 110 katika Ofisi ya Kamishna Msaidizi wa Ardhi mkoa wa Iringa kwa ajili ya kukamilishwa ili wamiliki wake wapatiwe hati.
Hatua hiyo inafuatia Dkt Mabula kufanya upekuzi katika Majalada ya ardhi aliyoyakuta katika ofisi ya Masijala ya Ardhi ya halmashauri ya wilaya ya Iringa ambapo baadhi ya majalada hayo hayajakamilishwa toka mwaka 2019 jambo lilillomsikitisha na kuamuru majadala hayo kufanyiwa kazi haraka.
‘’Yaani hati ziko hapa tangu mwaka jana eti mnamsubiri Kamishna, huu ndiyo ucheleweshaji hati unaolalamikiwa na wananchi, nataka kufikia ijumaa ijayo majalada yote 110 yawe yamepelekwa kwa Kamishna kwa ajili ya kuandaliwa hati’’ alisema Dkt Mabula
Aidha, aliitaka ofisi ya Msajili wa Hati mkoa wa Iringa kuhakikisha mara baada ya kukamilika uandaaji hati za ardhi, ofisi hiyo iwasiliane na halmashauri husika kwa ajili ya kuzipeleka hati hizo katika maeneo hayo kwa lengo la kuwaondolea usumbufu wananchi kuzifuata mkoani.
Wakati huo huo, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amembana Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Hamid Njovu kurejesha kiasi cha milioni 368,100,000/= ikiwa ni sehemu ya fedha ilizokopeshwa halmashauri yake kwa ajili ya mradi wa kupanga na kupima viwanja katika manispaa hiyo.
Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ilikopeshwa shilingi milioni 418,100,000 kwa jili ya mradi wa kupanga na kupima viwanja katika eneo la Igumbilo ambapo jumla ya viwanja 253 vilipimwa na kuuzwa na halmashauri hiyo ilifanikiwa kuuza viwanja 197 na kupata shilingi 692,667,000/= lakini ikarejesha kiasi cha milioni 50 pekee.
Naibu Waziri wa Ardhi alisema, mkopo uliokopeshwa halmashauri hiyo pamoja na halmashauri nyingine nchini unatakiwa kurejeshwa kwa asilimia mia moja lakini kati ya halmashauri 24 zilizokopeshwa ni halmashauri nne pekee ndizo zilizorejesha mkopo huo kwa asilimia mioa moja na kuagiza halmashauri zilizokopeshwa kurejesha fedha hizo kama inavyoelekeza katika masharti ya mkopo.

MRADI WA WA MAJI WA ZAIDI YA BILIONI 9 WASAINIWA

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Leonard Msenyele (kulia) na Mhandisi Mradi wa Kampuni ya CCECC, Mhandisi He Jun wakisaini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji wa Kyaka-Bunazi utakaogharimu zaidi ya bilioni 9.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Leonard Msenyele (wa pili kushoto) akisisitiza jambo kabla ya kusaini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji wa Kyaka- Bunazi wenye thamani ya zaidi ya bilioni 9.

NA MWANDISHI WETU.
Serikali kupitia Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza (MWAUWASA) imesaini mkataba na Mkandarasi Kampuni ya China Civil Engineering Construction Cooperation (CCECC) ya China kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa maji wa Kyaka- Bunazi wenye thamani ya shilingi 9,414,739,257.50.
Akizungumza hivi karibuni wakati wa kusaini mkataba huo kwenye Ofisi za MWAUWASA, Jijini Mwanza, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Leonard Msenyele aliipongeza kampuni hiyo kwa kushinda tenda na alibainisha kwamba ujenzi wa mradi huo utachukua miezi 13.
Alisema mkataba unahusisha ujenzi wa chanzo cha maji kwenye Mto Kagera chenye uwezo wa kuzalisha lita za maji 6,574,000 kwa siku; ulazaji wa bomba kuu kutoka kwenye chanzo hadi kwenye kituo cha tiba ya maji; ujenzi wa kituo cha tiba ya maji kitakachokuwa na tenki la kuhifadhia maji.
Alibainisha kwamba kukamilika kwa mradi huo kutanufaisha wananchi wa maeneo ya Kyaka, Bunazi na maeneo mengine yanayozunguka mradi Wilayani Missenyi.
Mhandisi Msenyele alimsisitiza Mkandarasi kuhakikisha anakamilisha ujenzi huo kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa kama ilivyo kwenye mkataba. “Ni vyema Mkandarasi ukatambua suala la muda, hakikisha mradi unakamilika kwa wakati, wananchi wanausubiri huu mradi kama walivyoahidiwa,” alisisitiza Mhandisi Msenyele.
Mara baada ya kusaini mkataba, Mhandisi Msenyele alimtaka Mkandarasi kuelekea eneo la mradi kwa ajili ya kufanya maandalizi ya kuanza ujenzi hasa ikizingatiwa kwamba ujenzi wa mradi ulipaswa kuwa umekwisha anza.
“Hakuna sababu ya kuchelewa, mipango yote ipo tayari na kwakuwa tumekwisha saini mkataba ni vyema ukafika eneo la mradi na kujipanga ukiwa huko huko, suala la muhimu kwa sasa ni nyinyi kufika eneo la mradi,” alisisitiza Mhandisi Msenyele.
Kwa upande wake Mhandisi Mradi wa Kampuni ya CCECC, Mhandisi He Jun alimhakikishia Mhandisi Msenyele kwamba watahakikisha wanakamilisha mradi kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa kama ilivyo kwenye mkataba.
Ujenzi wa mradi wa maji Kyaka Bunazi ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa Julai 11, 2019.
Akiwa njiani akitokea Wilayani Karagwe kuelekea Wilayani Chato, Rais Magufuli alisimama katika Mji Mdogo wa Kyaka kusalimiana na wananchi ambao walimueleza kero ya muda mrefu ya upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama.
Kufuatia hali hiyo, Rais Dkt. Magufuli alimuelekeza Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa kuhakikisha anafika eneo hilo ili kutazama namna ya kuwa na mradi utakaotumia maji kutoka Mto Kagera.
Waziri Mbarawa alifika eneo hilo na alielekeza Mamlaka ya Maji Mwanza (MWAUWASA) kushirikiana na Mamlaka ya Maji Bukoba na Wakala wa Maji Vijijini kuratibu upatikanaji wa mradi huo.
MWAUWASA ilipewa jukumu la kusimamia hatua zote za ujenzi wa mradi kwa niaba ya Wizara ya Maji kuanzia mchakato wa upatikanaji wa Mkandarasi atakayeutekeleza.
Aidha, Mhandisi Msenyele alibainisha kwamba japo agizo lilikuwa kuwapelekea maji wananchi wa eneo la Kyaka lakini baada ya kufanyika kwa tathmini ilionekana kuwa hata mji wa Bunazi ambao ndiyo Makao Makuu ya Wilaya ya Missenyi napo palikuwa na uhitaji mkubwa wa maji.
Aliongeza kuwa kufuatia tathmini hiyo, ilibidi usanifu na utayarishaji wa mradi uhusishe pia maeneo hayo mengine yaliyokuwa na uhitaji wa maji ili kujengwe mradi wenye uwezo wa kuhudumia maeneo yote na kwamba suala hilo limechangia kuchelewa kuanza kwa ujenzi wa mradi
Viewing all 45912 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>