Quantcast
Channel: VIJIMAMBO
Viewing all 45912 articles
Browse latest View live

Makamu wa Rais Akutwa na Corona

$
0
0
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Sudan Kusini, Riek Machar na mkewe, Angelina Teny, ambaye ni Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo wamekutwa na maambukizi ya Covid-19 jana (Jumatatu).

Taarifa zilizopo zinasema watu hao walipata maambukizi hayo baada ya kukutana na watu walio katika tume maalum ya kupambana na ugonjwa huo.

Pia wafanyakazi kadhaa wa ofisi za viongozi hao, wakiwemo walinzi, pia wamepata maambukizi hayo japokuwa majina yao hayakuchapishwa.

Waziri Biteko: Sekta ya Madini inaongoza kwa ukuaji wa uchumi nchin

$
0
0
Waziri wa Madini, Doto Biteko akizungumza na wajumbe wa warsha iliyoandaliwa kwa lengo la kuandaa kitabu cha viashiria hatarishi (Risk Registry) vya Wizara ya Madini iliyofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Madini Dodoma leo Mei 18, 2020. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila na Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango Augustine Ollal.
Kamishna wa Madini, Mhandisi David Mulabwa (kushoto) akifuatiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Madini, Issa Nchasi na wajumbe wengine wakifuatilia mafunzo juu ya uandaaji wa daftari la viashiria hatarishi.
Waziri wa Madini, Doto Biteko (kulia) na Katibu Mkuu wa Madini Prof. Simon Msanjila wakiteta jambo wakati wa warsha iliyoandaliwa kwa lengo la kuandaa kitabu cha viashiria hatarishi vya wizara ya madini iliyofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Madini Dodoma
Wajumbe wa warsha iliyoandaliwa kwa lengo la kuandaa kitabu cha viashiria hatarishi vya Wizara ya Madini iliyofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Madini Dodoma leo Mei 18, 2020 wakimfuatilia Waziri wa Madini, Doto Biteko. Mbele ni Mwezeshaji Dkt.Ernest Mwasalwiba. (Picha na Wizara ya Madini).

Nuru Mwasampeta na Tito Mselem,WM- Dodoma

WAZIRI wa Madini, Doto Biteko amesema ukuaji na mchango wa Sekta ya Madini kwenye pato la taifa unakua kwa kasi na kuwa mwaka 2019 mchango huo umeongezeka na kufikia asilimia 17.7 kutoka ukuaji wa asilimia 1.5 kwa mwaka 2018.

Amesema, kwa ukuaji huo sekta ya madini imeongoza sekta zote kwa ukuaji ikifuatiwa na sekta ya ujenzi ikiwa na ukuaji wa asilimia 14.1.

Ameongeza kuwa, wizara yake imekuwa ikikusanya kiasi cha wastani wa shilingi bilioni 39 kwa mwezi ,lakini kwa mwezi Aprili makusanyo hayo yamepaa na kufikia kiasi cha shilingi bilioni 58 jambo ambalo linaonesha mafanikio makubwa ya kisekta.

Hata hivyo, Waziri Biteko ametaka ukuaji huo wa Sekta ya Madini usaidie katika kukuza sekta nyingine za kiuchumi na hapo ndipo manufaa ya sekta ya madini yatakuwa na manufaa zaidi.

Waziri Biteko amebainisha hayo leo Mei 18, 2020 alipokuwa akifungua warsha ya maandalizi ya kitabu cha viashiria hatarishi (Risk register) cha wizara inayofanyika kwa siku tano katika ukumbi wa Chuo cha Madini Dodoma (MRI) na baadaye kuja na kitabu hicho kama matokeo ya warsha hiyo.

Biteko ameongeza kuwa, wizara inapoendelea kutekeleza majukumu yake, yumkini kuna viashiria hatarishi ambavyo endapo havitadhibitiwa vitakwamisha juhudi za wizara kufikia malengo, hivyo wizara imeamua kuandaa kitabu kitakachosaidia kubaini viashiria hivyo na kuvifanyia kazi ili kuyafikia malengo iliyojiwekea.

Akizungumza na washiriki wa warsha hiyo, Biteko amewataka wajumbe kubaini viashiria hatarishi vinavyoikabili wizara, kubuni mikakati madhubuti ya kudhibiti viashiria hivyo na kuandaa daftari la viashiria hatarishi la wizara kwa muda wa siku tano watakazokuwepo katika warsha hiyo.

Amesema, kwa kufanya hivyo, uhakika wa wizara pamoja na wadau wake wa malengo mkakati ya wizara kufikiwa utakuwa mkubwa kwani viashiria hatarishi vitakuwa vimepangiwa mikakati ya kuidhibiti kabla ya kutokea na kukwamisha juhudi za wizara.

Biteko amesema, maandalizi ya kitabu cha viashiria hatarishi ni utekelezaji wa maelekezo yaliyotolewa katika Waraka wa Hazina namba 12 wa mwaka 2013 ukielekeza taasisi zote za umma zikiwemo wizara kuwa na mfumo thabiti wa kudhibiti viashiria hatarishi (Risk Management) na kuandaa daftari la viashiria hatarishi (Risk register)

Ameendelea kusema suala la udhibiti na usimamizi wa viashiria hatarishi ilianzishwa mwaka 2010 kupitia Sheria ya Fedha ya mwaka 2010 iliyofanyiwa marekebisho kati sura 348 ya Sheria ya Fedha za Umma ya mwaka 2001.

Waziri Biteko amesema usimamizi wa viashiria hatarishi kwenye taasisi za umma ni takwa la kisheria ambapo chimbuko lake ni marekebisho katika sura ya 348 ya Sheria ya Fedha za umma ya mwaka 2001 yaliyofanyika mwaka 2010 na hivyo kuanzishwa kwa Idara ya Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali ambapo moja ya majukumu yake ni kusimamia mifumo ya udhibiti wa viashiria hatarishi vya malengo katika taasisi za umma.

Aidha, Waziri Biteko amewataka watendaji wa wizara kuendelea kuwakumbusha wachimbaji na wafanyabiashara wa madini kuendelea kufuata sheria na taratibu zinazosimamia Sekta ya Madini ili iendelee kuzalisha kwa faida.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila amewataka washiriki wote kufuatilia kwa umakini mafunzo hayo ili kuvitambua viatarishi na kuviepuka kabla havijawa tatizo.

WAMILIKI WA VIWANDA NCHINI WAELEKEZWA KUKATA BIMA ZA MOTO.

$
0
0
Waziri wa viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa{aliyevaa koti} akiongea na uongozi wa kiwanda kukoboa kahawa cha Amri Amir AL-HABSSY kilichoungua kwa moto Mei 07, 2020 ambacho chanzo chake ni hitilafu ya umeme iliyotokana na radi kubwa iliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha siku hiyo iliyosabisha hasara ya takribani Tsh.1,328,940,000.00 Karagwe, Kagera
Waziri wa viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa{aliyevaa koti} akikagua kiwanda kukoboa kahawa cha Amri Amir AL-HABSSY kilichoungua kwa moto Mei 07, 2020 ambacho chanzo chake ni hitilafu ya umeme iliyotokana na radi kubwa iliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha siku hiyo iliyosabisha hasara ya takribani Tsh.1,328,940,000.00 kushoto ni mmilioki wa kiwanda Karim Amri, kulia ni Mkuu wa wilaya Karagwe Godfrey Muheruka. Karagwe, Kagera
{Picha na Eliud Rwechungura – Wizara ya Viwanda na Biashara}

Na Eliud Rwechungura – Wizara ya Viwanda na Biashara
Waziri wa viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa amewataka wamiliki wa viwanda nchini kuhakikisha wanakata bima za moto ili pale wanapokumbwa na ajali za moto wapate wepesi wa kulipwa fidia za mali zao.

Bashungwa alitoa wito huo akiwa ziarani Karagwe mkoani Kagera 17 mei 2020, baada ya kutembelea na kukagua kiwanda cha kukoboa kahawa cha Amri Amir AL-HABSSY kilichoungua kwa moto Mei 07, 2020 nakuona mashine zilivyoharibika baada ya kuunguzwa na moto ambao chanzo chake ni hitilafu ya umeme iliyotokana na radi kubwa iliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha siku hiyo.

Akiongea baada ya kukagua Mhe. Bashungwa alitoa pole kwa mkurugenzi wa kiwanda hicho Karim Amri pamoja na wafanyakazi ambao kwasasa wamepoteza ajira zao, ambapo alirithishwa na hatua ambazo zimekwishachukuliwa na wamiliki wa kiwanda hicho ambazo ni kufatilia bima kwaajili ya kulipwa fidia.

“Tunapokuwa na viwanda hatujui mambo ya kesho na keshokutwa, mambo ya ajari unaweza kupanga kila kitu lakini hakuna anayetegemea ajari itatokea muda gani, kwahiyo kupitia kiwanda hiki nitoe wito kwa viwanda vyote nchini tuwe tunakata bima, maana kiwanda hiki kimeungua lakini walikuwa na bima ya moto.”

Awali meneja wa kiwanda hicho Daniel Ndayanse akitoa taarifa kwa Waziri alieleza hasara walioipata baada ya kufanya tathimini ya hasara iliyotokana na kuungua kwa kiwanda hicho kuwa ni mashine za kiwanda ni takribani Tsh.1,328,940,000.00 na jingo la takribani Tsh. 49,275,750.00 na kuongeza kuwa kiwanda kilikuwa na waajiliwa wa kudumu 16 ambao wapo kwa kipindi chote cha mwaka na wakati wa msimu huwa kinaajili watu kuanzia 800 hadi 1000 kulingana na kazi ya siku.
Aidha, Meneja alieleza kuwa “Kiwanda chetu tulikuwa tumekiimalisha kwa kukifanya cha kisasa ambapo tuliweza kuzalisha kati ya tani 50 hadi tani 65 za kahawa safi ambazo ni takribani gunia kati ya 800 hadi 1,000 kwa masaa 24, kwa kukoboa kahawa maganda kati ya tani 115 hadi tani 140 kwa masaa hayo 24 kama hakuna tatizo la umeme.”

Kwaupande wake mmiliki wa kiwanda Bw.Karim Amri alimshukuru Mhe.Rais John Pombe Magufuli kwa kuendelea kuimarisha na kuweka sera bora za viwanda kwa wawekezaji nchini, ambapo alitumia fursa hiyo kutoa maombi maalumu kwa Mhe.Waziri Bashungwa.

“Tunakuomba wewe Mhe.Waziri kuweka msukumo kwa watu wa bima BRITAM INSURANCE ambao tulikata bima kwao waweze kutufanyia haraka watulipe ili tuweze kununua mashine kufikia mwezi julai mwaka huu kiwanda kianze kufanya kazi”.

Alisema kuwa pamoja na mafanikio waliyo nayo kwa upande wa viwanda wilayani Karagwe alifafanua changamoto kubwa inayowasumbu mara kwa mara kuwa ni tatizo la umeme ambalo limekuwa tatizo sugu kwa wenye viwanda ambapo alisema kuwa kuna siku umeme unakatika na kuwaka Zaidi ya mara 20 hivyo husababisha kuungua kwa Motors,taa, na mitambo mingine.

Kufatia kukithiri kwa matukio ya moto wilayani Karagwe, kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo ikiongozwa na mwenyekiti wake mkuu wa wilaya Godfrey Muheruka imeamua kujenga kituomcha zima moto na uokoaji ambacho kitakuwa kikisaidia kwenye ajali za moto pale zinapotokea.

Hata hivyo kitendo cha kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya karagwe kuamua kujenga jingo la zima moto na uokoaji kikamshawishi waziri Bashungwa kuchangia mifuko 200 ya saruji na kuwataka wadau wa maendeleo kuchangia ili kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwa wakati.

MKUCHIKA AZINDUA BODI YA USHAURI YA WAKALA YA NDEGE ZA SERIKALI NA KUITAKA IHAKIKISHE ATCL INAKUWA IMARA KIUSHINDANI

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Wakala ya Ndege za Serikali (hawapo pichani) mara baada ya kuzindua Bodi hiyo mapema leo Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi Mhandisi John W. H. Kijazi ambaye pia ni Mwenyekiti ya Bodi ya Ushauri wa Wakala ya Ndege za Serikali akitoa neno la shukrani mara baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) kuzindua rasmi bodi hiyo mapema leo Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akimsikiliza Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi Mhandisi John W. H. Kijazi ambaye pia ni Mwenyekiti ya Bodi ya Ushauri wa Wakala ya Ndege za Serikali wakati akitoa neno la utangulizi kabla ya uzinduzi rasmi wa Bodi ya Wakala ya Ndege za Serikali uliofanyika mapema leo Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

James K. Mwanamyoto - Chamwino Dodoma
Tarehe 19 Mei, 2020.


Serikali imezindua Bodi ya Ushauri ya Wakala ya Ndege za Serikali ambayo itakuwa na jukumu la kumshauri Waziri mwenye dhamana juu ya namna bora ya kuboresha wakala hiyo ili kuwa na mipango na mikakati endelevu itakayoleta tija katika usafiri wa anga.

Akizindua bodi hiyo mapema leo Ikulu ya Chamwino, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) ameitaka bodi kuhakikisha Tanzania inakuwa na Shirika la Ndege imara litakaloweza kushindana na mashirika mengine ya kikanda na kimataifa kwa kuanzisha na kuendesha safari nyingi za ndani ya nchi, za kikanda na za kimataifa.

Mhe. Mkuchika amesema, suala la kuimarisha usafiri wa anga kwa kulifufua Shirika la Ndege la Tanzania ni moja ya utekelezaji wa ahadi za Chama cha Mapinduzi iliyopo kwenye ilani yake ya Uchaguzi ya Mwaka 2015.

Mhe. Mkuchika ameitaka Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA) na Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kufanya kazi kwa ushirikiano wenye tija ikiwa ni pamoja na kujengeana uwezo na uzoefu kiutendaji.

Aidha, Mhe. Mkuchika amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kulipa uzito mkubwa jukumu la usimamizi wa TGFA kwa kumteua Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi Mhandisi John W. H. Kijazi kuwa Mwenyekiti ya Bodi ya Ushauri wa Wakala ya Ndege za Serikali.

Kwa upande wake, Mhe. Balozi Mhandisi John W. H. Kijazi, amemshukuru Mhe. Rais kwa kumuamini na kumpa jukumu la kuongoza bodi hiyo ili iweze kutekeleza majukumu yake kikamilifu.

Mhe. Balozi Kijazi ameahidi kutekeleza maelekezo yote yaliyotolewa na Waziri Mkuchika ili kuiwezesha Wakala ya Ndege za Serikali kutekeleza majukumu yake ikiwa ni pamoja na kuliimarisha Shirika la Ndege ya Tanzania kuwa imara na la kiushidani.

Wakala ya Ndege za Serikali ilianzishwa rasmi tarehe 17 Mei, 2002 kupitia Sheria ya Wakala za Serikali Na. 30 ya Mwaka 1997 kama ilivyorekebishwa Mwaka 2009. Wakala hii, ilikuwa chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ambapo tarehe 23 Aprili, 2018, Serikali iliamuia kuihamishia Ofisi ya Rais, Ikulu kwa Tangazo la Serikali Na. 252 la tarehe 8 Juni, 2018.

James K. Mwanamyoto,
Afisa Habari-Ofisi ya Rais UTUMISHI
0713 360 813
19 Mei, 2020.

TANZANIA YAFUNGUA ANGA YAKE, SASA RUKHSA NDEGE ZA KIMATAIFA KUINGIA NA KUTOKA

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe, akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani), alipokutana nao kutoa taarifa ya kuruhusu anga la Tanzania kutumika kwa ndege za abiria, biashara na mizigo, jijini Dodoma Mei 18,2020
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini, Mhandisi Julius Ndyamukana (kulia), wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe (hayupo pichani), jijini Dodoma wakati alipokutakana na waandishi wa habari kuruhusu anga la Tanzania kutumika kwa ndege za abiria, biashara na mizigo.

NA WUUM, DODOMA
Serikali ya Tanzania imefuta rasmi zuio la safari za ndege baada ya taathimini ya mambukizi ya COVID -19 iliyofanywa nchini kubaini kupungua kwa maambukizi na idadi ya wagonjwa na kurejesha huduma za usafiri kama ilivyokuwa awali.
Akifuta zuio hilo jijini Dodoma Mei 18, 2020 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe ameziagiza Mamlaka ya Usafiri wa Anga Nchini (TCAA), Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), Kampuni ya Kusimamia na kuendeleza Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KADCO) na Kampuni ya Ndege Nchini (ATCL) kuanza kutoa huduma bila kikwazo na kuzingatia taratibu za kiafya zilizotolewa na Shirika la Afya Ulimwenguni na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Nchini.
“Kupitia Tangazo hili natamka kuwa ndege zote za kibiashara, misaada, kidiplomasia, dharura na ndege maalum zinaruhusiwa kuruka na kutua katika viwanja vyetu nchini kama ilivyokuwa awali” Amesema Waziri Mhandisi Kamwelwe.
Waziri Mhandisi Kamwelwe amezitaka Taasisi hizo kuhakikisha abiria wote wanaoingia nchini wanapimwa joto ili kuendelea kujikinga na maambukizi yanayoweza kutokea kutokana na muingiliano wa watu.
Waziri Mhandisi Kamwelwe ameongeza kuwa kufunguliwa kwa anga hilo kutarejesha fursa za kibiashara hasa katika eneo la utalii na kuinua pato la Taifa.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilitoa tamko la kufunga rasmi ndege za abiria za mashirika ya ndege ya kimataifa kuingia nchini Mei 2020 baada ya kujiridhisha kuwepo na ongezeko la kuenea kwa Virusi vya Korona
Katika hatua nyingine Waziri Mhandisi Kamwelwe amesema kwa upande wa Usafiri wa Malori kati ya Tanzania na Rwanda Serikali za nchi hizo zimekubaliana masharti nane ili kuendelea kudhibiti kuenea kwa virusi kati ya nchi hizo mbili.
Waziri Mhandisi Kamwelwe amesema pamoja na mambo mengine Serikali hizo zimekubaliana mizigo inayoelekea Rwanda kushuhushwa katika vituo maalum ikiwemo Rusumo na Kagitumba isipokuwa mzigo wa mafuta, Magari yanayokwenda Nchini Demokrasia ya Kongo (DRC) kupitia Rwanda itasindikizwa bure hadi kwenye mpaka wa Rwanda na DRC.
Magari ya mizigo yataruhusiwa kusafiri kuanzia sa 12.00 asubuhi hadi 12.00 jioni, kuboresha taratibu za upakiajia na upakuaji wa mizigo katika mipaka, kupunguza vituo vya kusimama.
Waziri Mhandisi Kamwelwe ameongeza kuwa madereva wote wanaosafirisha mizigo watapimwa mwanzoni mwa safari na kwenye mipakani baada ya kuwasili.
Aidha, amewataka wadau wote wa usafirishaji kuhakikisha changamoto zote zinazowakabili ziwasilishwa Wizarani ili kufanyiwa kazi kabla ya kuathiri biashara katika mipaka yote nchini.

MBUNGE CHUMI KUTATUA CHANGAMOTO ZA SOKO LA MASHUJAA MAFINGA

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi akiongea na wananchi wa jimbo la Mafinga(PICHA KUTOKA MAKTABA)

NA FREDY MGUNDA,MAFINGA.

WAFANYABIASHARA wa soko la Mashujaa katika Halmashauri ya Mji wa Mafinga wametakiwa kuendelea kufanya biashara huku kero zao zikiendelea kutatuliwa ili biashara ziendelee kufanyika kwa uhuru na kukuza uchumi wa wananchi wa Halmashauri hiyo.

Akizungumza kwa njia ya simu kutokea jijini Dodoma,Mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi alisema kuwa amejipanga kuhakikisha anatatua kero ya wafanyabishara hao ili kuendeleza shughuli za kiuchumi kufanyika kwa mujibu wa sheria za nchi.

Chumi alisema kuwa atahakikisha anatatua tatizo la umeme katika soko la Mashujaa kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanafanya shughuli za kibiashara kwa masaa mengi kama alivyoomba Bungeni kuwa wafanyabiashara wa Mji wa Mafinga wanatakiwa kufanya biashara kwa masaa ishirini na Nne.

“Nikiwa bungeni nilisema kuwa kuna miji ambayo ipo katika barabara ya Daresalaam Zambia na Malawi kufanya biashara kwa masaa ishirini na nne kulinga na taswira ya biashara ambapo kuna mzunguko mkubwa wa fedha katika mazingira hayo” alisema Chumi

Alisema miji midogo kama Mlandizi,Chalinze,Morogoro mjini,Mikumu,ruaha Mbuyuni,Ilula,Ipogolo,Ifunda,Mafinga na Makambako wanatakiwa kufanya biashara kwa masaa ishirini na nne kulinga na kuwa na jografia ya kibiashara.

Chumi alisema anaungana mkono hoja za wafanyabishara wa Mji wa Mfinga kwa kuhakikisha wanafanya biashara masaa ishirini na nne ili kukuza uchumi kwa kasi kubwa kama ilivyo kwa uongozi wa awamu ya tano ambao unawataka wananchi kufanya kazi kukuza uchumi.

Mji wa mafinga ni mji wa kibiashara kama ilivyo kwenye baadhi ya jiji la Nairobi kuna maeneo wanafanya biashara kwa masaa hao ndio maana wanakuza uchumi kwa kasi kubwa hata Mafinga panatakiwa kuwa hivyo.

Chumi alisema wafanyabishara kufanya biashara kwa masaa mengi kunachangia kuongeza kipato hivyo hata ulipaji wa ushuri mbalimbali na tozo zinaongezeka kwenye mapato ya serikali na kukuza uchumi wa nchi.

Aidha Chumi alisema kuwa huduma ya maji na choo ataifanyika kazi licha kuwa uongozi wa soko unatakiwa kuwasilisha maombi kwa uongozi wa Halmashauri ya Mji wa Mfinga ili kuanza kulitafutia ufumbuzi tatizo hilo.

Awali wakilalamika wafanyabiashara wa soko hilo la Mashujaa walisema kuwa soko hilo linakosa huduma ya Maji,Umeme,na Choo vitu ambavyo ni muhimu kuwepo kwenye maeneo ya kibiashara kama ilivyo kwenye soko hilo la Mashujaa.

Soko hili linakabiliwa na changamoto ya kukosekana kwa huduma ya ya Choo,Maji na umeme vitu vinavyofanya wafanyabishara wengi kufanya biashara kwa mashaka huku wakiofia afya zao na wateja.

MSIBA DMV NA DELAWARE

$
0
0
Familia ya Bandawe ikishirikiana na
JUMUIYA YA ATC/ DMV inasikitika kutangaza msiba wa mpendwa wao, Mr. Emmanuel Bandawe, Mwana DMV kwa zaidi ya miaka 20,uliotokea Delaware siku ya Jumamosi May 16, 2020 katika Hospital ya Delaware Memorial.

Marehemu anatarajiwa kuzikwa Delaware Mei 22.

Makadirio ya gharama ya Funeral home na maziko ya mpendwa wetu ni $13,500.

Tunaomba tuunganishe nguvu tumpumzishe mpendwa wetu, tafadhali Tuma rambirambi kupitia
*CashApp/Zelle*
*Lysa (Elizabeth)Bantu*(919) 452-2746*
Rambirambi

1. Vitalis Gunda $75
2. Ibra Nyagali $50
3. Linda Mwamba $50
4. Fellah & Lina $100
5. Joyce Cottrell $100
6. Richard and Melissa $100
7. Zelda & Tony Mwingira $100
8. Lulu $100
9. Irene Bomani $50
10. Pili Mnzavas-Wood $50
11. Lusajo Kibonde $50
12. Alu and Julius Nyangoro $100
13. Sia Makundi $50
14. Stella $60
15. Peter Kirigiti $100
16. Nunu Mwilima $100
17. Arthur Gao $50
18. Fadhili Malima $100
19. Mariam Kalala & Pendo Nyangoro $200
20. Doris & Abbas Mattaka $200
21. Neesha Jurobi $100
22. Saada Gaddies $100
23. Loveness Mamuya $100
24. Sunday & Elinita $100
25. Ally & Mariam Idowa $150
26. Peace Kachuchuru $100
27. Janice & Julius Manase $50
28. Khadija Riyami $50
29. Mariam Aranga $50
30. Danny & Ummy $100
31. Mwamoyo Hamza $100
32. Jabiri Jongo $60
33. Honest Mulamula $50
34. Mch John Mbatta $75
35. KC & Thecla $200
36. Adam Fred Tenga $100
37. Saidi Mwamende $30
38. Donacian & Eliserena $50
39. Asha N. & Baghdellah $100
40. Gatty & Keith Tate $120
41. Lucy Bowe $50
42. Saidi Mateso $100
43. Jabil & Aisha Kiegemwe $100
44. Deogratius Mosha $50
45. Aziza Farahani $50
46. Edwin Waluye $50
47. Alawi & Family $50
48. Bernadeta Kaiza & Mr. Sackstus $100
49. Fundi & Santina $200
50. Amide Mutaboyerwa $100
51. Samora Tofiki Nnauye $100
52. The Muhanjis $100
53. Deep Williams $100
54. Hajji Khamis $100
55. Mganga Muhombolage $50
56.Valerian Kisanga $100
57. Eric Mahai $100
58. Nambai & Family $100
59. Mr. & Mrs. Matope $400
60. Lulu & Elvis Saria $50
61. Kennedy Kishumbua $50
62. Poul & Josephine Basondole $100
63. Amran Kilemile $50
64. Liban Newa $50
65. Mr. & Mrs. Kocha Mateso $50
66. Belinda Nkya $50
67. Lemmy Muhando $50
68. Shaillah Kishumbua $100
69. Iska & Jojo $50
70. Salum Mkamba $100
71. Jaha Juma & Neville Lema $100
72. Ahmed Kufakunoga $100
73. Mercy & Peter Ligate $100
74. Najma Talib $50
75. Francisca Benedict $100
76. Ronald Mtawali $50
77. Augustina Charles $50
78. Mnkande Florah $30
79. Dickinson Sipemba $201
80. Isaac Mungongo $500
81. Rose Kachuchuru $40
82. Seif A. Al Rashidy $50
83. Hadiatou $100
84. Asteria Montgomery $150
85. Pac Livery Svc Inc $100
86. Juliano Daraja $100
87. Alice Brice $52
88. Katule & Family $100
89. Dorothy Soukou $500
90. Betty Mbatta $50
91. Rosemary Mziray Commodore $50
92. Farida & Issah $100
93. Juliana & Steve Mkanyia $200
94. Hamisi Msendo $50
95. Marge & Emeldee Mutafa $50
96. Goodluck Majollo $50
97. Abraham Kishumbua $100
98. Alex & Jennifer Kumwembe $100
99. Clara Lema $50
100. Anita Mwemenzi & Frank Mutafungwa $100
101. Margareth Mfugale $50
102. Leah Nyaki $40
103. Cleopatra J. Kulasi $50
104. Mr. & Mrs Mujunangoma $100
105. Zain Hamza $50
106. Mr. Mohamed Matumla $50
107. Hidaya Mahita $50
108. Joseph Adams (Djjoe) $50
109. Abdul $50
110. Tina & Elias Magembe $100
111. Collin Onjiko $50
112. Rashida Masesa $50
113. Abdul Kufakunoga $250
114. Ally Omary $100
115. Cosmas Kileo $40
116. Mr. & Mrs. Mungasi $50
117. Suleiman Baajun $50
118. Lawa's Family $40
119. Neema Ngwilulupi $50
120. Helen & Katie Kombe $50
121. Daniel & Wazaino Makuza $50
122. Hassan $100
123. Eliud & Grace Mbowe $100
124. Nunu & Yacob Kinyemi $50
125. Esther Traore $100
126. Eunice Magonya $500
127. Shaaban K. Fundi $50
128. Edward Taji $50
129. Hariet Tarazo $50
130. Mariam Mashaka $100
131. Nathan Chiume $50
132. Sophia & Abdul $100
133. Joyce Mshana $50
134. Fofo Madete $50
135. Dorothy Pambe $50
136. Mathias Choma $100
137. Lindah Mhando $100
138. George Kombe $100
139. Joha Nyang'anyi $100
140. David Y. Mbaga $100
141. Moddy Kiluvia $100
142. Hajji Helper $50
143. Mariam Mkama $50
144. Bi Fatuma $20
145. Caroline Mdee $100
146. Peter Kapanga $50
147. Caroline Mdee Muwonge $100
148. Flora M. & Rashid Kamugisha $100
149. Tino Malindi & Mary Mgawe $100
150. Bishop & Mama Maturlu $60
151. Elizabeth & Amos $75
152. Dr. Patrick Nhigula $50
153. Julie & Leslie Kombe $50
154. Bukhite Aljabry $50
155. Irene & Peter $200
155. Dr. Secelela & Given Malecela $500
156. Lulu & Shabby $101
157. Happiness Kariuki $50
158. JChe $20
159. Alamin Othman $50
160. Baraka Bitariho $75
161. Rosemary Mshana $50
162. The Sheriff $50
163. Sophia Mgaza $50
164. Jeffy Deo Nkanda & Family $50
165. Ruth Mukami $50
166. Warashi Khamis $50
167. Juster & Pius Mutalemwa $50
168. Joseph Ngocho $50
169. Rama & Sartana Kamguna $100
170. Fortunatus Mwakipesile $50
171. Mariam Kurtiz $50
172. Neema Babu $40
173. Amina Hassan $25
174. Eliufoo Kishumbua $200
175. Maria Nyatenga $50
176. Uwezo Tandau $50
177. Reza Matovu $50
178. Mather Masukuzi $30
179. Jane Nyamunga $150
180. Catherine Mukami $50
181. Julius Tesha $100
182. Samira Yasin $20
183. Lulu & Liberatus $60
184. Terry Shomari $50
185. Anazako & Lindah Mhando $100
186. Mathias Choma $100
187. Roble Abdul $50
188. Baraka Derua $50
189. Geraldine Ngowi & Grace Mlingi $100
190. Sabrina Chikumoghumra $200
191. Arthur Chacha $50
192. Frida & Jerome Kassembe $100
193. Melissa Makota $50
194. Raphael Ernest $20
195. Ally Idowa $20
*Total received $15,811*
Kwa mawasiliano zaidi:
Mr. Lucas Mukami +1 443-401-6554
Cleopatra Kulasi +1 202-378-8079
Dorothy Soukou (805) 708-0012
Abdul Kufakunoga (248) 515-5509
Abbas Mataka +1 (301) 537-7854
Dr. Mwamoyo Hamza (301) 922-0618
Liberatus Mwang'ombe
+1 240-423-3331
Tunatanguliza shukurani na Mwenyezi Mungu akuongezee pale ulipopunguza.
BWANA AMETOA, BWANA AMETWAA NA JINA LAKE LIHIMIDIWE
*Update as of 5:50pm next update at 10pm 5/19*

SAO HILL: MAZIWA YA NYUKI YA KINGA YA BINAADAM KUZEEKA

$
0
0
Mhifadhi wa shamba la Miti la Sao Hill kitengo cha Nyuki Wilayani Mufindi Said Abubakari moja kati ya mazao ya Nyuki katika shamba la miti la serikali ao Hill
Wavunaji wa mazo ya Nyuki katika shambva la miti la miti sao Hill Wilayani Mufindi
Baadhi ya waandishi mkoani Iringa wakifuatia zoezi la ufunaji wa mazao ya mdudu Nyuki 

NA FREDY MGUNDA,MUFINDI
.

WAKALA wa huduma za misitu Tanzania TFS kupitia shamba la miti la Sao hill Mkoani Iringa wanatarajia kuanzisha Mpango maalumu wa uvunaji wa sumu na maziwa ya nyuki yanayotajwa na watafiti wa masuala ya afya za binaadam kuwa na manufaa makubwa kiafya na fursa muhimu kiuchumi kupitia mazao yatokanayo na nyuki.

Mhifadhi wa shamba la Miti la Sao Hill kitengo cha Nyuki Wilayani Mufindi Said Abubakari Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa maandalizi ya maadhimisho ya siku ya Nyuki Duniani kwa upande wa mkoa wa Iringa na maeneo yaliyo chini ya wakala wa misitu Tanzania kupitia shamba hilo alisema mazao hayo yatachangia kuongeza pato la maduhuri ya serikali na ukuaji wa pato la wananchi wagao nyuki kutokana na mazao hayo kuhitajika zaidi katika matumizi ya mwili wa binadamu.

Alisema Maziwa ya nyuki pamoja na sumu inayozalishwa na Nyuki ni fursa muhimu kiuchumi katika soko la mazao yazalishwayo na wadudu hao huku akitanabaisha kuwa tafiti zinaeleza kuwa Maziwa ya nyuki yana Protini ya kiwango cha juu zaidi kuliko inayopatikana katika vyakula vingine na usaidia watu wanayoyatumia kutozeeka haraka, huku akiitaja sumu ya nyuki kuwa tiba muhimu ya binadam hasa kuhusu maradhi yanayohusisha tatizo la uvimbe kwa akina mama.

Abubakari alisema kwa mujibu wa tafiti mbalimbali sumu ya Nyuki inasaidia kutibu watu wenye uvimbe hasa hasa wanawake waliotoka kujifugua,ukipata dawa vizuri kwa mujibu ya wataalam uvimbe hupungua kila uchwao kutoka na dawa hiyo kufanya kazi kwa haraka.

“Uvimbe huo huanza kupungua taratibu kutoka matumizi bora ya dawa hiyo, Tupo katika hatua za awali za utafiti kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali na tukianza uzalishaji huo utakuwa na faida kubwa kwa wananchi wa Tanzania na nje ya Tanzania kwa kuwa hadi hivi sasa uvunaji wa sumu ya mdudu Nyuki inafanyika Tabora tu na sisi hapa tutafaata hivi punde” alisema Abubakari

Aidha Abubakari alisema Mpango wa SAO HILL ni kuwawezesha wafugaji Nyuki kupata mafunzo maalum ya uzalishaji wa maziwa kupitia malikia ambaye huzaa Nyuki wadogo ambao ndio hasa huzalisha zao la maziwa ya mdudu huyo.

“Maziwa ya mdudu nyuki huzalishwa na Nyuki wadogo ambao wanakuwa wamezalishwa kwa siku moja hadi siku mbili ndio ambao hasa ndio huwa wanakuwa na uwezo wa kuzalisha maziwa hayo” alisema Abubakari

Alisema kuwa pamoja na fursa hiyo kuwapo kwa wafugaji wa nyuki wanapaswa kutambua kuwa ulizalishaji wake unahitaji gharama kiasi huku na uhifadhi wa maziwa ya nyuki ukiwalazimu kuwa na vifaa maalum ambavyo vitawasaidia kuhifadhi maziwa hayo yatakayokuwa yamezalishwa na nyuki wadogo.

Akisisitiza kuhusu umuhimu wa maziwa ya nyuki Abubakari alisema kuwa maziwa ya hayo ni chakula ambacho kinaprotini isiyopatikana kwenye aina yeyote ya Maharage au Nyama, na zao hilo utumiwa zaidi katika nchi zilizoendelea kutokana na umuhimu wake hasa juu ya virutumisho vinavyowasaidia watumiaji kutozeeka haraka kutokana kutokana na utumiaji wa virutubishi vilivyomo katika maziwa hao.

Abubakari aliongeza kuwa kando ya mazao ya hayo nyuki wamekuwa na manufaa makubwa kutokana na uchevushaji wanauofanya katika mimea mbali mbali huku akibainisha kuwa asali ni muongoni mwa mazao muhimu kwa afya ya binaadam ambayo katika maeneo mbalimbali ulimwenguni imekuwa ikitumika huku akiwataka wafugaji nyuki kuzingatia ubora ili kuiongezea thamani ili koboresha soko lenye kuaminika katika zao hilo.

Nao baadhi ya wafugaji wa Nyuki walisema kuwa wamekuwa wakipata faida kubwa kutokana na mazao wanayovuna kutokana na Nyuki hasa kupitiaa zao la Asali baada ya kupatiwa mafunzo kupitia wataalam wa shamaba la miti la Srikali la SAO HILL hatua iliyowawezesha kuzalisha mazao bora ya nyuki na kuwaongezea soko la uhakika ndani na nje ya nchi.

“Tumepata fursa ya kufuga Nyuki na tunawashukuru wenzet wa shamba la miti la Serikali SAO HILL kwa kweli kwa elimu waliyotupatia kwa kushirikiana na wakala wa Misitu Tanzania TFS imetusaidia sana kukuza vipato vyetu na mpaka sasa miongoni mwetu imekuwa ni ajira rasmi inayokidhi mahitaji yote muhimu” walisema

Ikumbukwe Kupitia lengo namba moja la kutokomeza umasikini lililomo kwenye ajenda ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 2030, serikali zinahimizwa kutafuta mbinu mbadala kuwawezesha wananchi kupitia miradi mbalimbali ili kujikwamua na umasikini ifikikapo mwaka 2030.

Lengo hili linakwenda sambamba na mikakati ya Shamba la miti la Serikali SAO HILLl katika kuendeleza shughuli za ufugaji wa nyuki na kuongeza thamani ya mazao yatokanayo na nyuki

Kwa mujibu wa taarifa ya mwaka jana ya shirika la chakula ulimwenguni FAO asilimia 75 ya matunda na mbogamboga visingekuwepo bila nyuki na ni bidhaa ambazo ni muhimu sana kwa uhakika wa chakula na bayoanuai ya dunia.

Maadhimisho ya kimataifa ya siku ya nyuki duniani yalipitishwa rasmi na Baraza Kuu la Umoja wa mwaka 2017 na sasa yanaadhimishwa ulimwenguni kote kila ifikapo Mei 20 kila mwaka

WAZIRI MKUU AWASIMAMISHA KAZI WATUMISHI WATATU TEMESA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiangalia ghala la spea za magari, katika yadi ya TEMESA, jijini Dodoma, May 19, 2020, wakati alipotembelea karakana ya mitambo ya wakala hao wa Ufundi na Umeme (TEMESA). Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiangalia magari, katika yadi ya TEMESA, jijini Dodoma, May 19, 2020, yaliyofika kwa ajili ya matengenezo, wakati alipotembelea karakana hiyo ya mitambo ya wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiangalia ghala la spea za magari, katika yadi ya TEMESA, jijini Dodoma, May 19, 2020, wakati alipotembelea karakana ya mitambo ya wakala hao wa Ufundi na Umeme (TEMESA). Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiangalia magari, katika yadi ya TEMESA, jijini Dodoma, May 19, 2020, yaliyofika kwa ajili ya matengenezo, wakati alipotembelea karakana hiyo ya mitambo ya wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiangalia mashine ya kupimia matairi, wakati alipotembelea karakana ya mitambo ya wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), jijini Dodoma, May 19, 2020, ( Picha na Ofisi ya Waziri 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akimsikiliza, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, wakati alipotembelea karakana ya mitambo ya wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), jijini Dodoma, May 19, 2020, ( Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza na watumishi wa TEMESA, baada ya kukagua karakana ya mitambo ya wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), jijini Dodoma, May 19, 2020, ( Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akimpa onyo, Mtendaji Mkuu wa TEMESA, Mhandisi Japhet Maselle, baada ya kutoridhishwa na utendaji wake, wakati alipotembelea karakana ya mitambo ya wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), jijini Dodoma, May 19, 2020, katikati ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe. ( Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, baada ya kukagua karakana ya mitambo ya wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), jijini Dodoma, May 19, 2020, ( Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

NA OWM, DODOMA
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi watumishi watatu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kwa tuhuma za kuhusika na upotevu wa sh. milioni 780 zinazotokana na zabuni.
Vile vile, Waziri Mkuu ametoa muda wa miezi miwili kwa taasisi zote za Serikali zinazodaiwa na TEMESA kiasi cha sh. bilioni 25.88 ziwe zimeshalipa na iwapo kuna taasisi itashindwa kulipa deni lake hadi Julai 30, 2020 apewe taarifa.
Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo leo (Jumanne, Mei 19, 2020) alipotembelea karakana ya mitambo ya TEMESA jijini Dodoma na amewasisitiza watumishi hao wafanye kazi kwa uadilifu na Serikali haihitaji wala haitowavumilia watumishi wazembe.
Vile vile, Waziri Mkuu ametoa muda wa miezi miwili kwa taasisi zote za Serikali zinazodaiwa na TEMESA kiasi cha sh. bilioni 25.88 ziwe zimeshalipa na iwapo kuna taasisi itashindwa kulipa deni lake hadi Julai 30, 2020 apewe taarifa.

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo leo (Jumanne, Mei 19, 2020) alipotembelea karakana ya mitambo ya TEMESA jijini Dodoma na amewasisitiza watumishi hao wafanye kazi kwa uadilifu na Serikali haihitaji wala haitowavumilia watumishi wazembe.
Kufuatia hali hiyo, Waziri Mkuu amemuonya Mtendaji Mkuu wa TEMESA, Japhet Maselle kutokana na usimamizi wake usioridhisha, ambapo amesema Mtendaji huyo alikuwa anajua kuhusu upotevu wa fedha katika wakala huo na hakuchukua hatua kwa wahusika.

“…si mzuri kwenye usimamizi unapenda kuacha watu wanaofanya maovu wakiwemo na watumishi hawa watatu. Mtendaji ulikuwa unajua, ulikuwa hauchukui hatua hadi uliposikia nakuja, hii si sahihi sheria zipo na maelekezo ya Serikali yapo. Upotevu wa sh. milioni 780 katika taasisi ni doa.”
Waziri Mkuu amesema kufuatia na matumizi mabaya ya fedha yanayofanywa TEMESA, amemuagiza Mdhibiti na Makaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) akafanye ukaguzi katika wakala huo kutokana na upotevu wa sh. milioni 780 zilizotakiwa zipelekwe Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Wakati huo huo, Waziri Mkuu amezitaka taasisi zote za Serikali zinazodaiwa na wakala huo ziwe zimelipa madeni yote katika kipindi cha miezi miwili ili kuiwezsha TEMESA kuweza kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

“Tukishapata bilioni 25 TEMESA hii tukapeleka walau bilioni moja moja kila mkoa watanunua mitambo, watanunua vipuri na magari yatatengenezwa kwa haraka. Magari yote ya Serikali lazima yatengenezwe TEMESA kwa sababu ya uhakika wa usalama wake.”
Pia, Waziri Mkuu ameuagiza uongozi wa wakala huo ufanye maboresho makubwa kiutendaji ikiwa ni pamoja na kufanya marekebisho ya sehemu ya magari kwa kuwa inalalamikiwa zaidi hususani suala la utengenezaji wa magari yanayopelekwa.

Waziri Mkuu amesema kuwa Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa wanalalamikia gharama kubwa wanazotozwa kwa ajili ya utengenezaji wa magari, hivyo lazima ziangaliwe kama ni halisi.
Hata hivyo, Waziri Mkuu ameuagiza uongozi wa wakala huo ujiridhishe kila kivuko kama ni kizima ili kuepusha madhara makubwa yanayoweza kutokea na wavifanyie ukaguzi wa mara kwa mara.

Awali, Mtendaji Mkuu wa TEMESA alisema wakala huo unakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo madeni makubwa yanayotokana na huduma zao kutolipwa kwa wakati au kutolipwa kabisa.
“…kwa mfano hadi mwezi Machi 2020 tunazidai taasisi za Serikali kiasi cha shilingi 25,882,593,038 na wakati huo huo tukidaiwa na wazabuni mbalimbali kiasi cha shilingi 18,959,630,408.”

Changamoto nyingine aliyoitaja ni uchakavu wa karakara nyingi zinazomilikiwa na wakala huo katika makao makuu ya mikoa mbalimbali nchini, hivyo kuathiri ufanisi katika matengenezo ya magari ya Serikali.

EMANUEL BANDAWE (Mwamba). A man who need no introduction. Life Well Lived – You Will Be Missed Forever.

$
0
0
BY MOHAMED MATOPE

This year, 2020, has been a tough year for many people all around the world. The coronavirus pandemic has fundamentally transformed our sense of humanity and possibly forever changed our way of life. For now, we can’t hug, we can’t shake hands or even visit our loved ones at time when they need us the most, when they are sick in the hospital. Here in Washington DC and its metropolitan area (DMV), this year has been disproportionally somber and will probably go down as the darkest and saddest year in the history of the region and our communities. We are saddened by the passing of our dear fellow and colleague, Mr. Emanuel Bandawe, a.k.a Mr. Mwamba.

From the time I heard of Mwamba’s passing on Saturday afternoon, I was so heartbroken that I just felt compelled to go back to my photo albums to look at all the pictures I have of him. I could not believe what had just happened. So many specific memories came to my mind instantly. This was a man of personality and remarkable characteristics. He had undying and unquestionable love for his family. He loved music, great food, and had a passion for enjoying life. In most ways, this man was exceptional. His acceptance of everyone and refusal to judge or dismiss anyone unnecessarily was impeccable. As a people person, he enjoyed being with people, making people laugh, analyzing sports, and telling funny stories. I cannot stop hearing the sound of his laugh. The bottom line is, Mwamba’s life was never short on excitement.

Mr. Emmanuel Bandawe was one of the very first people I met when I first came to the United States. In the winter of 1997, on February 7, to be specific, I met Mwamba at the Dulles International Airport on my arrival to this great land of opportunity. I remember our very first encounter as if it was yesterday. I greeted Mwamba with shikamoo, and he replied Marahaba. That day, Mr. Bandawe, together with other friends, picked me up from the airport in Virginia and dropped me off in Silver Spring, Maryland.

The following week Mwamba came to our apartment in Bladensburg, where I was staying with Terry Shomari and Daniel Nyambibo. Our apartment was roughly about 8 Kilometers from his place in Hyattsville. He offered to take me to the social security offices in Wheaton, Maryland. On that day, I also greeted him with Shikamoo, and again he responded with Marahaba. From that day on, Mr. Bandawe was a frequent visitor to our apartment and always took me out for a car ride to light up my eyes, showing me different places in Maryland, Virginia, and Washington DC. The first time I explored the region, was with Mwamba. That experience alone was humbling.

Needless to say, every time we met, I always greeted him with Shikamoo. But after the third week of hanging out with him, I involuntarily stopped greeting him with Shikamoo. He never told me to stop; neither did he disapprove it, but Shikamoo just looked old, and suddenly it just didn’t fit in our relationship. Showing respect to him did not require Shikamoo anymore. He made me feel comfortable around him. He became a friend, someone I strongly trusted and could easily confide in. That was Mr. Bandawe. He could magically make you feel comfortable and belonging.

Besides making people feel easy and comfortable around him, he also made people laugh. Mwamba was charming, and his presence everywhere he went was felt like an earthquake. I remember back in those days; we would walk into a place with Mwamba, whether it is in a party, repass, funeral, or any other gathering, and the moment Mwamba walked into the crowd – the mood, the ambiance – everything changed. He would light up the room with his smile and jokes.

You know, there is one thing I will never forget about Mwamba. Back in the days when he was taking me around the city, we frequently made several stops in different houses and apartments. Sometimes he would say: “oh, we need to pull over here to see brother So-So,” sometimes it was just something as simple as “oh, I see So-So’s car in the parking lot, he must be in his apartment. Let’s go say, Hi”. Just like that, in many instances, we would end up spending plenty of time visiting deferent folks. It was because of him that I got to meet most of the folks I have come to know in the DMV Tanzanian community. Through him, I have made plenty of relationships and friendships. He was superb social connector.

In the summer of 1997, I met one of my terrific friends through Mwamba’s connections. On that day, Mwamba took me to Hyattsville Chillum Road apartment complex to visit his friend; something was going on that day. Several Tanzanian guys in that apartment ware having fun. And Mwamba and I walked in, he introduced me to every person, went to the kitchen and made some delicious baked fish and rice – more of the food a bit later on in this story – and continued with his introductions, and that is how I came to know Mr. Erick Mahai. He has remained a good friend till today. When I tell you, Mwamba was a GIANT – you would not even begin to understand the deep meaning behind that statement. He stood TALL for everyone, and he would come through for you, even when you thought no one could do.

I mentioned about his love and passion for cooking, and how he enjoyed eating good food. Oh yes, Mwamba was a food lover. This is probably prevalent to everyone who knew Mwamba well. I remember back when we were in our bachelor apartment; he used to pop up in the middle of the day, take me out to the grocery store, collect some ingredients/items and come back home straight to the kitchen. He would enter the kitchen, and when he was done, the food was simply amazing. Talk about good African food: coconut rice and beans, chicken stew, baked fish, fried chicken gizzards, and so forth. It was always a variety of dishes and never a dull moment. It got to the point where one day, my roommate complained that we cooked too much food and that we should think about saving money. To which, Bandawe answered: “we only live once!” and yes, of course, he did finish up his remarks with a lousy joke. Oh boy, that fella could cook!

One day he spontaneously came to the apartment and said, “Mwanangu, I need to take you out shopping. You need to start dressing like you are in America now. We need to replace your entire wardrobe”. I thought he was joking, but I was wrong. That’s the day I found out, not only did he love cooking and good food, but the guy was also into fashion. Every day he would come up with a new style of fashion. Even though I have never been into his room, I assumed that his closet was full of designer clothing. Bandawe took fashion cues from everywhere, the likes of Kanda Bongoman and Tyson Beckford. I am telling you, if this guy were Congolese, he would have been a “Sapeur.” His style was nothing short of elegant!

I remember this one time when I went to pick him up from his house to honor an invitation for an occasion held at the ambassador’s residence in Potomac. This guy came out looking crisp and sharp like a knife. He had on a dark blue suit with a matching dark brown tie with a pocket square fold. I will never forget that day. With the suite, he wore a plain white shirt with an overly shiny black moccasin shoes matching his belt. I felt so bad for myself. He made me look like his gatekeeper. We got to the ambassador’s place, and the moment we entered the house, the whole place suddenly got some extra light in it. He certainly drew everybody’s attention with his swagger. Mwamba was so good in making explosive entrances.

Sadly, to say, now that looking back into my friendship with Bandawe, I feel so hurt and guilty at the same time. I last spoke with him over six months ago. In that conversation, he gave me his updated cell phone number and invited me to visit him in Delaware. I promised him that I would and got carried away with life and never managed to follow through on my promise. It is not an excuse that life got in the way, and it breaks my heart that I didn’t make time to visit him. I haven’t seen him in person for over three years, and this by itself kills my conscious. I wish I had made the extra effort to go and visit him. This is probably the biggest lesson to many of us around here in the DMV. We tend to forget – Life is short, and sometimes death is sudden. We should meet more frequently and spend more time with not only our families but also great friends like Mwamba.

Significantly, you just couldn’t underestimate his love for his motherland country. Although Mwamba had lived in America for over 25 years, he always considered Tanzania his home. He never left behind his Tanzanian roots and culture. He was big fan of Yanga and, what photographic memory he had when it comes to the description of old Tanzanian football matches. He loved to talk about Tanzania politics and general welfare.

Mwamba passed away on Saturday, May 16, 2020, at Delaware Memorial Hospital, he succumbs to short illness. Mwamba’s legacy will live on through his wife, two biological children, and one adopted child. Emmanuel Billy Bandawe, my dear eternal friend, we will miss you beyond eternity. Go with the angels and Rest in Peace, Mwamba!

The End.
May 19, 2020

DKT. MAGUFULI AWASALIMIA WANANCHI WA NZEGA TABORA PAMOJA NA WANANCHI WA SINGIDA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Nzega mkoani Tabora (hawaonekani pichani) wakati akielekea mkoani Singida.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Nzega mkoani Tabora (hawaonekani pichani) wakati akielekea mkoani Singida.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Singida mjini (Kwenye Mataa) mara baada ya kuwasili wakati akitokea Nzega Mkoani Tabora.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwandri mara baada ya kuwasili Nzega Mkoani Tabora.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na mtoto aliyejulikana kwa jina moja la Rahma mara baada ya kuwasalimia Wananchi katika eneo la Mataa 
mkoani Singida. (PICHA NA IKULU).

BODI YA UTALII TANZANIA: TUPO TAYARI KUANZA KUPOKEA WATALII

$
0
0
Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii (TTB), Jaji Mstaafu Thomas Mihayo akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani Jijini Dar es Salaam, kuhusu kurejeshwa kwa huduma za utalii nchini.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii (TTB), Bi. Devota Madachi akiandika swali kutoka kwa waandishi wa habari katika Mkutano wa Waandishi wa habari na Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii, Jaji Mstaafu Thomas Mihayo pichani Jijini Dar es Salaam, kuhusu kurejeshwa kwa huduma za utalii nchini.
Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii (TTB), Jaji Mstaafu Thomas Mihayo akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani Jijini Dar es Salaam, kuhusu kurejeshwa kwa huduma za utalii nchini, kushoto ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa TTB, Bi. Devota Madach

Na Mwandishi Wetu, MAELEZO
BODI ya Utalii Tanzania (TTB) imesema ipo tayari kuanza kupokea watalii wakati wowote kuanzia sasa kufuatia hatua ya Serikali kuruhusu kuendelea kwa shughuli za utalii nchini hatua iliyotokana na kupungua kwa kasi ya mlipuko wa ugonjwa wa homa kali ya mapafu (CORONA) duniani.
Hayo yamesemwa leo Jumatano (Mei 20, 2020) Jijini Dar es Saalam na Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Jaji mstaafu Thomas Mihayo wakati wa mkutano wake na Waandishi wa Vyombo vya Habari kuelezea mikakati endelevu ya TTB katika kutangaza shughuli za utalii nchini.
Jaji Mihayo alisema kufuatia kikao baina ya wadau wa utalii na Serikali kilichofanyika hivi karibuni Jijini Arusha, Wizara ya Maliasili na Utalii imeandaa mwongozo mahsusi wa namna ya uendeshaji wa shughuli za utalii nchini na unaotarajiwa kutafsiriwa kwa lugha mbalimbali na kusambazwa katika masoko ya utalii sehemu mbalimbali duniani.
‘Bodi ya Utalii Tanzania imeshiriki kikamilifu kwenye kikao hicho na mwongozo uliotolewa utahakikisha kuwa Watanzania wanakua salama na watalii pia wanatalii kwenye vivutio vilivyo na usalama na kuhakikisha kuwa shughuli za kutangaza utalii hazisimami kutokana na janga la corona duniani’’ alisema Jaji Mihayo.
Kwa mujibu wa Jaji Mihayo alisema TTB pia imepanga kufanya kufanya ukaguzi wa maeneo mbalimbali ya kupokelea na kulaza watalii ili kujiridhisha kuwa maeneo hayo yana huduma mbalimbali za dharura kulingana na mwongozo ulitolewa na Serikali ili kuhakikisha kuwa utalii wa Tanzania unaendelea kuwa salama.
Aidha Jaji Mihayo alisema mara baada ya zoezi hilo kukamilika TTB itaanza kufanya mazungumzo na Ofisi za Ubalozi wa Tanzania na Balozi za masoko ya utalii wa Tanzania zilizopo nchini ili kuwahakikishia hatua zilizochukuliwa na Serikali kuhusiana na udhibiti wa mlipuko wa virusi vya COVID-19 kabla ya kuruhusu watalii kuanza kuwasili nchini.
Akifafanua zaidi Jaji Mihayo alisema TTB kwa kushirikiana na sekta binafsi imetengeneza filamu mbalimbali za vivutio vya utalii nchini ili kuhakikisha kuwa shughuli za kutangaza utalii hazisimami kutokana na janga la CORONA, ikiwemo kampuni ya Great Migration Camp walioanzisha kipindi cha ‘Serengeti Live Show’ kinachorushwa katika mitandao yote ya kijamii ya TTB na Serengeti Live YouTube Channel.
‘Nitoe wito kwa wafanyabiashara wa sekta ya utalii, kujitolea kwa hali na mali kutangza filamu hizi ambazo zimesaidia kutangaza utalii wa Tanzania duniani, na televisheni zetu za ndani zinaweza kuzipata filamu hizi bure bila malipo hapa TTB ili mkaziongeze kwenye ratiba za vipindi vyenu kama sehemu ya kutoa elimu’ alisema Jaji Mihayo.
Kwa upande Mkurugenzi Mwendeshaji wa TTB, Devota Mdachi alisema mwishoni mwa mwezi huu, ndege ya kwanza inatarajia kutua nchini ikiwa na watalii ambapo hadi sasa tayari wadau wote wa utalii wamekamilisha miongozo mbalimbali inayotakiwa kufuatwa ili kuwakinga watalii na maambukizi ya virusi vya COVID-19.
Aidha Mdachi alisema Serikali pia i imefanya mawasiliano na Ofisi za Ubalozi wa Tanzania katika nchi za Israel, China na Malaysia ili kuhamasisha makundi makubwa ya watalii wa nchi hizo waliopanga kuja Tanzania mwanzoni mwa mwaka huu kufufua mipango yao ya safari ya kutembelea vivutio vya utalii nchini.
Aidha Mdachi alisema kwa kuzingatia mwongozo uliopo Serikali tayari imeanza kufanya mazungumzo na makampuni za uwakala wa utalii katika nchi India, Malaysia na Israel.

YANGA YENYE SURA MPYA YAANZA KUSAKWA

$
0
0

WINFRIDA MTOI – DAR ES SALAAM , Mtanzania

KLABU ya Yanga, imezindua rasmi mchakato wa kuelekea katika mfumo wa mabadiliko ya uendeshaji wa klabu hiyo.

Mchakato huo utasimamiwa na kamati ndogo inayoongozwa na Mwanasheria, Alex Mgongolwa.

Kampeni hiyo ilizinduliwa jana jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Yanga, Dk Mshindo Msolla, ikiwa ni rasmi kuanza kupokea maoni ya wanachama.

Yanga imefikia hatua hiyo, baada ya kukamilisha makubaliano na wataalamu kutoka Ligi Kuu Hispania (La Liga), Hispania, kupitia andiko la awali la kamati ya ndogo ya mabadiliko.

Akizungumzia uzinduzi huo, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Hassan Bumbuli, alisema wanakwenda katika mfumo wa mabadiliko ilikuwa moja ahadi za viongozi wa klabu hiyo wakati wanagombea.

Alisema mchakato huo utafadhiliwa na wadhamini wao, kampuni ya GSM na kauli mbiu yake ni ‘Twenzetu Kwenye Mabadiliko,” alisema Bumbuli.

Alieleza kuwa uzinduzi huo ni mwanzo wa mambo mazuri yanayokuja katika klabu hiyo.

Katika video ya Mwenyekiti wa Yanga, Dkt. Mshindo Msolla, iliyowekwa na katika mtandao wa klabu hiyo, alisikika akisema “Moja ya dhamila yangu wakati nagombea ni kubadilisha muundo wa uendeshaji wa klabu, nadhani ndoto hiyo inakwenda kukamilika.

“Ombi la viongozi kwa wanachama na wapenzi wa Yanga, tuwe

kitu kimoja, tuungane na uongozi na wadhamini ili tuweze kufanikisha hilo, Yanga moja katika Twenzetu Kwenye Mabadiliko,” alisema.

Alisema uzinduzi huo, ni mwanzo wa kuelekea katika mabadiliko ambao utakuwa muda rasmi wa mchakato wa kufika kule wanakotaka kwenda.

Kwa upande wake, Mkugenzi wa uwekezaji wa GSM, Hersi Said, alisema watajitoa kwa hali na mali kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa kama walivyoahidi kudhamini mchakato huo katika hatua ya awali.

Alisema kilichokuwa kinasubiriwa ni makubaliano ya kimkataba ya pande mbili, kati ya watu kutoka La Liga na Yanga, jambo ambalo limeshakamilika.

“Kama tulivyoahidi kusaidia katika mchakato huu wa mabadiliko, tutafanya hivyo kuhakikisha mabadiliko yanakwenda vizuri na kila Mwanayanga anapata nafasi ya kutoa maoni yake,”alisema.

Alisema hatua, iliyofikiwa ni nzuri kutokana na vikao vilivyokuwa vinafanyika muda mefu, kuweka mipango sawa, anaamini kila kitu kitakwenda vizuri baada ya uzinduzi.

Katika udhamini huo wa mchakato wa mabadiliko, GSM waliahidi kutoa ofisi itakayotumiwa na wataalam hao kutoka Hispania, pindi wakatapowasili nchini.

DC JOKATE APOKEA MSADA WA THAMANI YA SHILINGI MILIONI 76.8 KUTOKA PLAN INTERNATIONAL KUSAIDIA WILAYA KISARAWE

$
0
0
Meneja wa Shirika la Plan International Wilaya ya Kisarawe Marcely Madubi akifafanua kuhusu msaada wa vifaa mbalimbali vya kukabiliana na Corona ambavyo wamevitoa kwa ajili ya Wilaya ya Kisarawe.
Sehemu ya matanki ya maji ya ujazo wa lita 500 kila moja ambayo yametolewa na Shirika la Plan International kwa ajili ya kuiwezesha Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe kukabiliana vema na janga la Corona ambapo matanki hayo yatagawiwa kwenye vituo vyote vya afya wilayani Kisarawe.
Na Mwandishi Wetu

HALMASHAURI ya Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani limekabidhiwa msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya Sh.milioni 76.8 kwa ajili ya kukabiliana na janga la Corona kutoka Shirika la Plan International.
Msaada huo umekabidhiwa na Meneja wa Shirika hilo Kisarawe Marcely Madubi kwa Mkuu wa Wilaya hiyo, Jokate Mwegelo ambaye ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa vita dhidi ya Corona Tanzania imefanikiwa kushinda kwa asilimia kubwa.
Vifaa hivyo ambavyo idadi yake ipo kwenye mabano ni vipima joto vya mionzi(8), matenki ya maji yenye ujazo wa Lita 500(20), glovu boksi (80),galoni za lita tano za vitakasa mikono (5), vitakasa mikono (210), aproni (80), barakoa FFP2 (30), maboksi ya taulo za kike (100), miwani za kujikinga (30), viatu (120), vifuniko vya mwili (10), mabango (18) na vipeperushi (1500) kwa ajili ya kusambaza elimu.
Akizungumza baada ya kupokea vifaa hivyo leo katika Hospitali ya Walaya ya Kisarawe mkoani Pwani Mkuu wa Wilaya hiyo Jokate Mwegelo amelishukuru shirika hilo kwa msaada walioutoa ambao utasaidia kuimarisha mapambano ya Corona.
"Plan International kwa kushirikiana na Shirika la Champion Chanzige (CCO),wametoa msaada wa vifaa hivi pamoja na kutoa elimu kwa njia ya matangazo kwa jamii itakayoambatana na wasanii wa wilaya yetu kundi la Kibajaji, kwa kuzunguka kata 17.Utoaji huo wa elimu utakwenda sambamba na ugawaji aa vipeperushi na ubandikaji wa mabango katika ofisi za kata na maeneo mengine muhimu,"amesema.
Pia alisema Shirika la Plan International litawezesha mafunzo kwa wataalam na viongozi wa ngazi ya wilaya, kata na vijiji wapatao 488 pamoja na kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kuandaa vipindi vitakavyotoa elimu rafiki kwa watoto kupitia runinga na redio.
Jokate ametumia nafasi hiyo kuiomba jamii ya Wilaya ya Kisarawe kuhakikisha inamlinda mwanafunzi wa kike hasa kipindi hiki ambacho wako majumbani ili kuwaepusha kupata mimba kwani Serikali inatumia gharama kubwa ya uwekezaji kwa ajili ya kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu, hivyo waachwe watimize ndoto zao.
Pia ameeleza namna ambavyo Wilaya hiyo imefanikiwa katika mapambano dhidi ya Corona na kubwa zaidi Tanzania imefanikiwa kushinda vita dhidi ya ugonjwa huo kutokana na maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na Rais Dk.John Magufuli kuhusu mbinu bora na sahihi za kuukabili ugonjwa huo.
Kwa upande wake Meneja wa Shirika la Plan International Madubi amefafanua jumla ya msaada wote ambao wameutoa kwa ajili ya Wilaya ya Kisarawe una thamani ya Sh.milioni 76.8 na katika fedha hizo kuna mgawanyo kulingana na aina ya msaada ambao wameutoa.
Amesema kuwa vifaa vilivyotokewa kwa ajili ya hospitali vina jumla ya thamani ya Sh. milioni 34.2 na Sh. milioni 42.5 zitatumika kwa ajili ya kutoa elimu kwa jamii dhidi ya Corona, kukarabati gari la wagonjwa na kuendesha mafunzo wataalam wa afya, walemavu, viongozi wa dini na wa serikali wapatao 488.
"Tunaamini vitakasa mikono, sabuni na matenki ya maji yatakayowekwa vituo vya afya na shule tunazotekeleza ujenzi wa vyoo na madarasa vitasaidia jamii na maeneo hayo kujikinga na maambukizi ya Corona. Maboksi 100 ya taulo za kike zitasaidia wasichana wapatao 1,200 hususan waishio kwenye mazingira magumu," amesisitiza.
Pia Madubi amewaomba wazazi,walezi na jamii kwa ujumla kuhakikisha wanawaondoa watoto kwenye hali ngumu ikiwa ni pamoja na unyanyasaji wa kijinsia na kubebeshwa majukumu mengine ya kifamilia badala ya kujisomea.
Ametoa rai kwa jamii kuwa licha ya wanafunzi kuwa wako nyumbani lakini wanatakiwa kuendelea kusoma kwa kujisomea kila siku ili kutosahau waliyofundishwa shuleni kabla ya Corona kuingia nchini.Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo akipata maelezo kuhusu matanki ya maji yaliyotolewa na Shirika la Plan International baada ya kukabidhiwa kwa ajili ya Wilaya hiyo.Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo(kulia) na Meneja wa Shirika la Plan International (kushoto) katika Wilaya hiyo Marcely Madubi(kushoto) wakioneshwa na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani Stanphod Mwakatabe moja ya vifaa vya msaada ambavyo vimetolewa na Shirika hilo kwa ajili ya mapambano dhidi ya Corona ndani ya wilaya hiyo.Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo(kulia) na Meneja wa Shirika la Plan International (kushoto) katika Wilaya hiyo Marcely Madubi(kushoto) wakioneshwa na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani Stanphod Mwakatabe moja ya vifaa vya msaada ambavyo vimetolewa na Shirika hilo kwa ajili ya mapambano dhidi ya Corona ndani ya wilaya hiyo.Jokate Mwegelo ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani akifafanua jambo baada ya kupokea msaada wa vifaa mbalimbali vya kukabiliana na Corona vyenye thamani ya Sh.milioni 76.8.04:Katibu Tawala Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani Tella Mwampamba (aliyesimama) akizungumza kabla ya Shirika la Plan International kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vyenye zaidi ya Sh.milioni 76.8 kwa ajili ya kukabiliana na Corona katika Wilaya hiyoMeneja wa Shirika la Plan International Wilaya ya Kisarawe Marcely Madubi akifafanua kuhusu msaada wa vifaa mbalimbali vya kukabiliana na Corona ambavyo wamevitoa kwa ajili ya Wilaya ya Kisarawe.Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani Stanphod Mwakatabe(aliyesimama) akielezea umuhimu wa vifaa vya kukabiliana na Corona ambavyo vimetolewa kwa ajili ya kuwezesha watoa huduma za afya katika Wilaya hiyo kutekeleza majukumu yao ya kuhudumia wagonjwa bila ya kupata maambukizi

WAZIRI UMMY AMKABIDHI RC DODOMA VIFAA VYA HOSPITALI

$
0
0
Katika kuhakikisha mapambano dhidi ya KifuaKikuu TB yanaendelea leo Mei 20, 2020, Zahanati ya Buigiri - Chamwino jijini Dodoma imemkabidhiwa Hadubini za Kisasa (LED Microscope) 57 kwa ajili ya vituo vya huduma za Afya mkoa wa jiji la Dodoma. Lengo ni kuimarisha huduma za upimaji na ugunduzi wa TB, Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu amesema wakati akimkabidhi RC Dodoma Dkt. Mahenge
Hadubini hizi ni sehemu ya Hadubini (Microscope) 941 zilizonunuliwa na Wizara ya Afya kwa thamani ya Tsh.bilioni 3.3 ikiwa ni sehemu ya jitihada za Serikali ya Awamu ya 5 chini ya Rais Mhe Dkt. John Pombe Magufuli ili kuboresha huduma za Afya nchini. "Ni faraja kuona kuwa Jitihada zetu zinazaa matunda ikiwemo
kupungua kwa maambukizi mapya ya wagonjwa wa TB kwa mwaka kutoka wagonjwa 160,000 (2015) hadi 142,000. Kupungua kwa vifo vitokanavyo na TB kwa mwaka kutoka vifo 30,000 (2015) hadi vifo 22,000". Amesema Waziri Ummy. Pia Waziri huyo ameishukuru GlobalFund kwa kuunga mkono jitihada za serikali katika kutokomeza maradhi hayo.
Pamoja na kuendelea na mapambano dhidi ya COVID19, Kipaumbele cha Wizara sasa ni kuhakikisha Mwendelezo wa huduma muhimu za Afya (Continuity of Essential Health Services) ikiwemo Huduma za Mama na Mtoto (RCH), Chanjo, Udhibiti wa magonjwa mengine kama TB, Malaria, HIV 


VIONGOZI WA DINI WILAYANI KARAGWE WAANDAMANA KUMSHUKURU RAIS MAGUFULI KWA KURUHUSU IBAADA DC AWAPOKEA KWA NIABA YAKE NA KUTOA NENO.

$
0
0
Viongozi wa dini wilayani Karagwe wakiwa katika maandamano ya amani kumshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli kuruhusu kuendelea na Ibada katika misikiti na makanisa kuendelea na Ibada zao.
Na, Allawi Kaboyo, Karagwe.
Viongozi wa mathehebu mbalimbali ya dini wilayani Karagwe mkoani Kagera wamefanya maandamano ya Amani yenye lengo la kumshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kuruhusu kuendelea kufanyika kwa ibaada makanisani na misikitini kote nchini katika kipindi hiki cha mlipuko wa gonjwa hatali la COVID-19 linalosababishwa na virusi vya Corona.
Maandamano hayo yamefanyika leo yakitokea ofisi za mkuu wa wilaya hiyo na kupokelewa na mlezi wa kamati ya Amani ya wilaya hiyo Mwashamu Baba Askofu Almachius Vicent Rweyongeza wa jimbo la katoriki Kayanga pamoja na mkuu wa wilaya Mhe.Godfrey Muheruka katika viwanja vya nyumba ya vijana (ANGAZA) wilayani humo.
Kiongozi wa maandamano hayo mwenyekiti wa kamati ya maadili ya wilaya Karagwe Mchungaji Selesitin John wa kanisa la FPCT Kayanga amesema kuwa wameguswa na kauli ya Rais magufuli aliyoitoa mei 17 mwaka huu baada ya kushiri ibaada ya jumapili wilayani Chato.
Amesema kuwa suala la Rais Magufuli kuruhusu watanzania kuendelea kuabudu kwa kuliombea taifa na janga la Corona kwa kutofunga nyumba za ibaada linawapa msukumo mkubwa wa kuendelea kumshukuru na kumombea kwa mungu.
“Sisi viongozi wa dini wilayani Karagwe tunaungana na Rais Magufuli katika kipindi hiki cha Corona kuendelea kufanya ibaada huku tukichukua tahathali zote zinazotolewa na wataalamu wa afya, Magufuli alichaguliwa na mungu kuja kutuokoa sisi watanzania hivyo tunayo kila sababu ya kumuunga mkono na kuzidi kuliombe taifa letu libaki salama, niwaombe watanzania tuendelee kumuamini na kumuombea Rais wetu hili nalo litapita.” Amesema Mchungaji Selesitin.
Kwaupande wake Askofu Almachius baada ya kupokea maandamano hayo amewashukuru viongozi hao kwa mshikamano na umoja walioudumisha kwa maslahi ya wanakaragwe na watanzania kwa ujumla ambapo amesema kuwa kitendo cha kujitokeza hadharani na kumpongeza Rais Magufuli ni kitendo cha kizalendo nay eye kama mlezi wao amelipokea kwa nia njema.
Asikofu ameongeza kuwa nchi ya Tanzania ilimuhitaji mtu kama Rais magufuli ambaye mpaka sasa amekuwa mfano wa kuigwa kwa mataifa ya Africa na ulimwenguni kwa ujumla, na kuongeza kuwa kupitia maumbi na dua zinazoendelea kufanyika katika makanisa na misikiti katika kipindi hiki cha ugonjwa wa Covid-19 yamelifanya Taifa kuanza kuuepuka ugonjwa huu kama Rais alivyosema tunaendelea vizuri.
“Tumekuwa tukimsikia Rais Magufuli akituomba viongozi wa dini kuendelea kuliombea taifa na kuwasihi waumini wetu kufunga na kusali tukimuomba mungu wetu aweze kutunusuru na janga hili, sasa kupitia maombi na dua zetu mungu ameanza kutujibu ni wajibu wetu kama viongozi wa dini kudumisha Amani na mshikamano wetu bila kujali mathehebu yetu.” Asikofu Almachius amesema.
Asikofu amesisitiza kuwa wataendelea kuungana na Rais kwa kuwasihi waumini wao kufunga na kusali ili kumshukuru mungu kama Rais alivyotangaza siku tatu za maombezi ya shukurani yatakayofanyika kuanzia ijumaa ya tarehe 21 hadi jumapili ya tarehe 23 kwa makanisa yote wilayani humo.
Kwaupande wake Alhaji Sheikh Mustapha Muyonga Amiri wa wilaya Karagwe kutoka taasisi ya kiislamu JASUTA amesema kuwa licha ya kuwepo kwa janga la Corona waumini wa dini hiyo wameendelea kufanya ibaada mbalimbali ikiwemo kushiriki vipindi vya swala katika misikiti yao huku wakichukua tahadhali mbalimbali.
Amesema suala la Rais Magufuli kutofunga nyumba za ibaada limeliongezea daraja kubwa kwa mungu Taifa hili la Tanzania kwa uchamungu unaoendelea katika maeneo mbali mbali na kuongeza kuwa janga la Corona sio janga la kwanza Duniani maana yalikuwepo majanga mengi na makubwa kabla yetu.
“Kitendo cha Rais magufuli kuwaacha watanzania waendelee kuabudu ni kitendo cha kishujaa sana hivyo watanzania kwa imaani zetu tuendelee kumuombea Rais wetu na taifa letu, Kabla yetu yalikuwepo majanga tena makubwa lakini nyumba za ibaada hazikuwahi kufungwa hata nyakati za mitume, na mungu alishatwambia katika kitabu chake kitukufu Qur-an kuwa niombeni name nitawaitikieni hivyo tuzidi kumuomba na kumshukuru kila siku, sisi tumefunga na sasa tunaelekea kumaliza mfungo wetu wa mwezi mtukufu wa Ramadhan na Inshaallah tutaswali na idd tukiwa salama. Amesema Alhaji Muyonga.
Mkuu wa wilaya Karagwe Godfrey Muheruka Baada ya kuwapokea viongozi wa dini amesema viongozi wa dini wilayani humo wamekuwa mfano wa kuigwa kwa kuhubiri Amani na mshikamano kwa wanakaragwe ambapo amewahakikishia Amani na usalama wakati wakiliombea taifa.
Muheruka amesema kuwa kuwa mbele kwa viongozi wa dini katika kuliombea taifa ni jambo la kizalendo kwa nchi yao na hilo ndilo analolihubiri Rais Magufuli kwa watanzania wote kuendelea kuomba na kusali ili tuweze kuepushwa na janga la Corona.
“Kwaniaba ya Mhe.Rais John Pombe Magufuli mimi Godfrey Muheruka mkuu wa Wilaya ya Karagwe na wapokea viongozi wa dini waliojitokeza kufanya maandamano ya kumpongeza Rais Magufuli kwa kuwaruhusu kuendelea kufanya ibaada katika nyumba za ibaada, niwahakikishi viongozi wangu wa dini sitawaangusha tutaendelea kuwa pamoja katika mapambano dhidi ya Corona.”
Mkuu huyo ameongeza kuwa wananchi kupitia viongozi wa dini wandelee kufanya ibaada huku wakifuata taratibu zote zinazotolewa na wataalamu wa afya katika maeneo mbalimbali na kuongeza kuwa Corona ipo lakini wanatakiwa kutokuwa na hufu huku akisistiza kuendelea kufanya kazi kwa kulijenga taifa lao.
“Mimi niseme tu wapo baadhi ya viongozi walitangaza kufunga makanisa hapa wilayani suala lililowapelekea wananchi kutishia kulichoma kanisa hilo, lakini tulivyoona hali hiyo tulijitahidi kuizui hali hiyo na kanisa halikuchomwa, hivyo nitoe wito kwa viongozi wa dini waacheni waumini wenu wafanye ibaada maana gonjwa hili ni gonjwa kama magonjwa mengine na sio kila anayeumwa anaumwa Corona, niwahakikishieni kwa wilaya Kargwe mpaka sasa tupo salama hatuna mshukiwa wala mgonjwa wa Corona tuendeleeni kuomba na kufanya kazi.” Amesema Muheruka.
Viongozi hao wamesema kuwa wataungana na watanzania wote pamoja na Rais Magufuli katika kufanya ibaada ya Shukrani kwa mungu kwa ambayo itadumu kwa siku tatu kama Rais Magufuli alivyotangaza kwa lengo la kumshukuru mungu kwa namna anavyolibariki taifa la Tanzania

TANZIA NYUMBANI TANZIA

$
0
0
*TANZIA*
Familia ya Beatrice na Erick Lemunge inasikitika kutangaza kifo cha mama mzazi wa Erick, mama Laura Lemunge, kilichotokea Tanzania saa saa sita na dkk 24 usiku kule Arusha (saa kumi na moja na nusu ya Minnesota).

Mipango ya kusafirisha kwenda Rombo kwa mazishi inafanywa.

Kwa ajili ya kutoruhusiwa mikusanyiko ya watu wengi, hatutakuwa na mkusanyiko wowote nyumbani kwa Beatrice na Erick. 
Kama kutakuwa na utaratibu wa kukusanyika hapo baadaye, tutawapa taarifa.

Unaweza kuwasalimia Erick na Beatrice kwa kupitia 
namba 
651-398-1861 
na 
763-334-8505.

Kama ungependa kutoa rambirambi kwa wafiwa, tafadhali tuma rambirambi yako kwa wafiwa kwa njia zifuatazo:
1. CashApp
•$ErickLemunge 
2. Bank Account: Zelle
•Beatrice H. Laizer
8455484926

Kwa taarifa zaidi, unaweza kuwasiliana pia na Emma Kasiga kwa namba 
612-229-4050

Mungu amlaze mahali pema peponi Mama yetu Laura Lemunge. 

Amina

UNITED STATES GOVERNMENT TO PROVIDE TANZANIA AN ADDITIONAL $2.4 MILLION DOLLARS TO HELP RESPOND TO COVID-19 OUTBREAK

$
0
0
U.S. Embassy Dar es Salaam
U.S. Embassy Dar es Salaam
TANZANIA


May 22, 2020

FOR IMMEDIATE RELEASE


UNITED STATES GOVERNMENT TO PROVIDE TANZANIA AN ADDITIONAL $2.4 MILLION DOLLARS TO HELP RESPOND TO COVID-19 OUTBREAK

Dar es Salaam: The United States has announced an additional $2.4 million (5.6 billion Tanzanian shillings), through the United States Agency for International Development (USAID) in health assistance funds for the strengthening of laboratory capacity for optimal diagnostics, risk-communications, water and sanitation, the prevention and control of infections, public health messaging, and more. This support complements the $1 million recently announced COVID-19 relief funds, for a total of $3.4 million in new resources for Tanzania. In addition, the U.S. government has directed existing $1.9 million to address COVID-19 for a total of $5.3 million (12.2 billion Tanzanian shillings).

The United States has invested more than $7.5 billion total in Tanzania over the past 20 years, nearly $4.9 billion for health. Since 2009, the United States government has funded more than $100 billion in health assistance and nearly $70 billion in humanitarian assistance globally. The United States government continues to be the single largest health and humanitarian donor for both long-term development and capacity building efforts with partners, and emergency response efforts in the face of recurrent crises, and we are leading the world’s humanitarian and health assistance response to the COVID-19 pandemic.

The United States continues to demonstrate global leadership in the face of the COVID-19 pandemic. The American people have given more than $10 billion that will benefit the global COVID-19 response, and we continue to ensure that the substantial U.S. funding and scientific efforts on this front remain a central and coordinated part of the worldwide effort against COVID-19. Months into fighting this pandemic at home and abroad, the United States continues to lead a global response—building on decades of leadership in life-saving health and humanitarian assistance.

To request more information, please call the U.S. Embassy Dar es Salaam Press Office at Tel: +255 22 229-4000 or email: DPO@state.gov.

Naibu Waziri wa Afya Awasili Ofisini Kwake Dodoma

$
0
0
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Godwin Oloyce Mollel akitia saini kitabu mara baada ya kuwasili ofisini kwake Mtumba Jijini Dodoma leo tarehe 21 Mei, 2020 baada ya kuapishwa kushika nafasi hiyo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Godwin Oloyce Mollel akisalimiana na watumishi wa Wizara hiyo mara baada ya kuwasili ofisini kwake Mtumba Jijini Dodoma leo tarehe 21 Mei, 2020 baada ya kuapishwa kushika nafasi hiyo. Kushoto ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu.

Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW

SIMBA SC, TAASISI YA MO DEWJI WATOA MSAADA HOSPIATLI YA TAIFA MUHIMBILI, MOI NA JKCI KUPAMBANA NA CORONA

$
0
0
Simba Sports Club Kwa kushirikiana na Mo Dewji Foundation imekabidhi msaada wa lita 500 za sabuni na vipukusi (sanitizers) pamoja na kufanya uzinduzi wa eneo la kunawia mikono lililojengwa na taasisi ya Mo Dewji Foundation kwenye maeneo ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Taasisi ya Mifupa (MOI)l na Taasisi Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Lengo la msaada huo ni kusaidia kupambana na ugonjwa wa corona.

Viewing all 45912 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>