Quantcast
Channel: VIJIMAMBO
Viewing all 45984 articles
Browse latest View live

JKCI KWA KUSHIRIKIANA NA HOSPITALI YA WILAYA YA KIGAMBONI WAADHIMISHA SIKU YA MOYO DUNIANI KWA KUPIMA MAGONJWA YA MOYO BILA MALIPO KWA WANANCHI

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Fatma Nyangasa akizingumza na wananchi waliofika katika viwanja vya Hospitali ya wilaya ya Kigamboni iliyopo eneo la Gezaulole jijini Dar es Salaam kwa ajili ya upimaji wa magonjwa ya Moyo bila malipo uliofanywa na wataalamu kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Kigamboni ni maadhimisho ya siku ya moyo Duniani.
Baadhi ya wananchi wa wilaya ya Kigamboni wakimsikiliza mkuu wa wilaya hiyo Fatma Nyangasa wakati akizungumza nao kuhusu umuhimu wa kupima afya wakati wa upimaji wa magonjwa ya moyo bila malipo uliofanyika katika viwanja vya Hospitali ya wilaya ya Kigamboni ikiwa ni maadhimisho ya siku ya moyo Duniani.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Fatma Nyangasa akimsikiliza Alex Kyando kutoka kampuni ya uagizaji na usambazaji wa dawa za binadamu na vifaa tiba ya Ajanta Pharma Limited alipokuwa akimweleza kuhusu aina ya dawa za moyo wanazozitoa kwa watu waliokutwa na matatizo ya moyo wakati wa upimaji wa magonjwa ya moyo bila malipo uliofanywa na wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Kigamboni ikiwa ni maadhimisho ya siku ya moyo Duniani.
Mtafiti kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Makrina Komba akimweleza Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Fatma Nyangasa jinsi wanavyowapima na kupata uwiano wa urefu na uzito wananchi waliofika katika Hospitali ya wilaya hiyo wakati wa upimaji wa magonjwa ya Moyo bila malipo uliofanywa na wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Kigamboni ikiwa ni maadhimisho ya siku ya moyo Duniani.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Fatma Nyangasa akiangalia picha inayoonesha mlo kamili wakati Afisa lishe wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Husna Faraji alipokuwa akimwelezea kuhusu lishe bora wakati wa upimaji wa magonjwa ya Moyo uliofanywa na wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Kigamboni ikiwa ni maadhimisho ya siku ya moyo Duniani.
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Mourice Obwanga akimpima shinikizo la damu (BP) mwananchi aliyefika katika viwanja vya Hospitali ya wilaya ya Kigamboni kwa ajili upimaji wa magonjwa ya Moyo uliofanywa na wataalamu wa Taasisi hiyo kwa kushirikiana na wenzao wa Kigamboni ikiwa ni maadhimisho ya siku ya moyo Duniani.
Mkazi wa Kigamboni akisoma Jarida la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) linalotoa uelewa wa magonjwa ya moyo wakati wa upimaji wa magonjwa ya moyo bila malipo uliofanywa kwa wakazi wa wilaya hiyo na wataalamu JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Kigamboni ikiwa ni maadhimisho ya siku ya moyo Duniani
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Fatma Nyangasa akiangaliza dawa ya moyo iliyokuwa inatolewa bila malipo na kampuni ya uagizaji na usambazaji wa dawa za binadamu na vifaa tiba ya Samiro Pharmaceutical Limited kwa watu waliokutwa na matatizo ya moyo wakati wa upimaji wa magonjwa ya moyo uliofanywa kwa wakazi wa wilaya hiyo. Kulia ni mwakilishi wa kampuni hiyo Faraji Namonde.
Daktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Tulizo Shemu akimwonesha aina ya dawa za moyo alizomwandikia mkazi wa Kigamboni wakati wa upimaji wa magonjwa ya Moyo bila malipo uliofanywa na wataalamu wa Taasisi hiyo kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya wilaya ya Kigamboni ikiwa ni maadhimisho ya siku ya moyo Duniani.
Maafisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Hospitali ya Wilaya ya Kigamboni wakitoa huduma za upimaji wa magonjwa ya Moyo bila malipo kwa wananchi wa wilaya hiyo ikiwa ni maadhimisho ya siku ya moyo Duniani.
Daktari wa Hospitali ya wilaya ya Kigamboni James Mbapila akiwaeleza madhara ya magonjwa ya moyo wananchi waliofika katika viwanja vya Hospitali hiyo jana kwa ajili ya upimaji wa magonjwa ya moyo bila malipo uliofanywa na wataalamu wa Hospitali hiyo kwa kushirikiana na webzao wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) .

Picha na JKCI

RAIS SAMIA AONGOZA WATANZANIA KUAGA MWILI WA HAYATI OLE NASHA JIJINI DODOMA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisaini kitabu cha kumbukumbu ya maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu na Uwekezaji Hayati William Tate Ole Nasha wakati wa kuaga mwili wa Naibu Waziri huyo katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiongoza Watanzania kuaga mwili wa aliyekuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu na Uwekezaji Hayati William Tate Ole Nasha katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma leo Sept 30,2021

PICHA NA IKULU

RAIS SAMIA AYATAKA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI KUZINGATIA MIPANGO NA VIPAUMBELE KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,akizungumza wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Mashirika yasiyo ya kiserikali NGOs uliofanyika leo September 30,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano Mkuu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini wakifuatilia hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali uliofanyika leo September 30,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima,akizungumza wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Mashirika yasiyo ya kiserikali NGOs uliofanyika leo September 30,2021 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dk.John Jingu,akizungumza wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Mashirika yasiyo ya kiserikali NGOs uliofanyika leo September 30,2021 jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Anthony Mtaka,akitoa salamu za Mkoa wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Mashirika yasiyo ya kiserikali NGOs uliofanyika leo September 30,2021 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NaCONGO) Dkt. Lilian Badi,akielezea malengo ya Mkutano wa Mwaka wa Mashirika yasiyo ya kiserikali NGOs uliofanyika leo September 30,2021 jijini Dodoma.
Mbunge wa Viti Maalumu anayewakilisha Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Mhe. Neema Lugangira,akizungumza wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Mashirika yasiyo ya kiserikali NGOs uliofanyika leo September 30,2021 jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizindua taarifa ya mchango wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakati wa Mkutano wa Mwaka wa NGOs uliofanyika leo September 30,2021 jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo ya heshima kutoka kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima wakati wa Mkutano wa Mwaka wa NGOs uliofanyika leo September 30,2021 jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna, Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameyataka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kuzingatia Mipango na Vipaumbele vya Kitaifa katika kutekeleza majukumu na miradi mbalimbali ya maendeleo.

Rais Samia amesema hayo jijini Dodoma wakati akizungumza na wawakilishi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika Mkutano wa Mwaka wa Mashirika hayo.
“Napenda kuyaelekeza Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kuwa na mpango mkakati wa Maendeleo utakaokwenda sambamba mpango wa Taifa wa miaka mitano,” amesema na kuongeza; huko nyuma Mashirika mengine yalikuwa yakifanya kazi kulingana na matukio, ukianzishwa mpango wa mazingira Mashirika yanakimbilia huko ili kushawishi fedha za wafadhili. Ni imani yangu mtajipanga upya kufanya kazi kwa ufanisi” amesema Mhe. Samia.

Aidha, ameyataka Mashirika hayo kuongeza uwazi na uwajibikaji katika utekelezaji wa majukumu yao na miradi mbalimbali kwa kuzingatia tamaduni, mila na desturi za nchi.

Mashirika ya ndani pia wametakiwa kupunguza utegemezi kwa wafadhili na wadau wa Maendeleo kutokana na mabadiliko ya Sera na Agenda za wadau hao bali waanzishe miradi ya kuwatengenezea fedha kwa kushirikiana na Serikali.

Aidha ameyataka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kuhamasisha zoezi la Sensa likatalofanyika nchini mwaka 2022 ili Taifa liweze kujiletea Maendeleo katika sekta mbalimbali.

Kwa upande wake Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amempongeza Rais kwa uongozi wake mahiri uliowezesha Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kupata uongozi.

Ameongeza pia, kupitia mkutano huo Mashirika hayo yamepata semina elekezi kuhusu sheria, kanuni na miongozo hivyo ni matumaini kuwa sasa wamefahamu wanatakiwa kufanya nini.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Dkt. Lilian Badi amesema Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yatazingatia sheria, kanuni na miongozo pamoja na kushirikiana na Serikali ili kutoa mchango wenye tija nchini.

MAJALIWA APOKEA TAARIFA YA TUME YA UCHUNGUZI WA BEI ZA BIDHAA ZA MAFUTA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea Taarifa ya Tume ya Uchunguzi wa Bei za Bidhaa za Mafuta aliyoiunda Septemba 2, 2021 kutoka kwa Mwenyekiti wa tume hiyo, ambaye pia ni Mbunge wa Mkinga, Danstan Kitandula, Ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Septemba 29, 2021. Kulia ni Waziri wa Nishati, January Makamba. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MAJALIWA AZUNGUMZA NA WAZIRI ASHATU KIJAJI.

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Tekinolojia ya Habari, Dkt. Ashatu Kijaji, ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Septemba 30, 2021.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

JESHI LA POLISI KUYAFUTA MAKAMPUNI YASIYOFUATA MASHARTI YA VIBALI

RAIS SAMIA, SPIKA NDUGAI WASHIRIKI MISA YA KUUAGA MWILI WA NAIBU WAZIRI MAREHEMU TATE OLE NASHA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Ngorongoro na Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu (uwekezaji), Marehemu William Tate Ole Nasha tukio lililofanyika leo katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma, Septemba 30, 2021
Katibu wa Bunge, Bi. Nenelwa Mwihambi akiaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Ngorongoro na Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu (uwekezaji), Marehemu William Tate Ole Nasha baada ya misa ya kuombea mwili huo tukio lililofanyika leo katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma, Septemba 30, 2021
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akiweka shada ya maua kwenye jeneza la mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Ngorongoro na Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu (uwekezaji), Marehemu William Tate Ole Nasha tukio lililofanyika leo katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma, Septemba 30, 2021
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango na Mke wake, Bi. Jenisia Mpango wakiaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Ngorongoro na Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu (uwekezaji), Marehemu William Tate Ole Nasha tukio lililofanyika leo katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma, Septemba 30, 2021
Wageni mbalimbali wakishiriki misa ya kuombea mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Ngorongoro Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu (uwekezaji), Marehemu William Tate Ole Nasha tukio lililofanyika leo katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma, Septemba 30, 2021
Waheshimiwa Wabunge wakiaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Ngorongoro na Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu (uwekezaji), Marehemu William Tate Ole Nasha tukio lililofanyika leo katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma, Septemba 30, 2021
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akisaini kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Ngorongoro na Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu (uwekezaji), Marehemu William Tate Ole Nasha tukio lililofanyika leo katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma, Septemba 30, 2021
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akizungumza wakati wa misa ya aliyekuwa Mbunge wa Ngorongoro na Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu (uwekezaji), Marehemu William Tate Ole Nasha tukio lililofanyika leo katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma, Septemba 30, 2021
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza wakati wa misa ya aliyekuwa Mbunge wa Ngorongoro na Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu (uwekezaji), Marehemu William Tate Ole Nasha tukio lililofanyika leo katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma, Septemba 30, 2021.

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

WAZIRI MULAMULA AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA MAKAMPUNI YA THE PULA GROUP JIJINI DAR

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mheshimiwa Balozi Liberata Mulamula (Mb) akihutubia hadhira iliyojitokeza kwenye sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Peace Corps Tanzania yaliyofanyika kwenye viunga vya Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mheshimiwa Balozi Liberata Mulamula akisalimiana na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mhe. Dr. Donald Wright alipowasili kwenye sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Peace Corps Tanzania yaliyofanyika kwenye viunga vya Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mheshimiwa Balozi Liberata Mulamula (katikati), Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mhe. Dr. Donald Wright (kulia) na Mkurugenzi Mkazi wa Peace Corps Tanzania Bi. Stephanie Joseph de Goes (kushoto) wakiwa wamesimama wakati Wimbo wa Taifa la Tanzania na Marekani unaimbwa.
Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mhe. Dr. Donald Wright akihutubia kwenye sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Peace Corps Tanzania yaliyofanyika kwenye viunga vya Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkaazi wa Peace Corps Tanzania Bi. Stephanie Joseph de Goes akizungumza kwenye sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Peace Corps Tanzania yaliyofanyika kwenye viunga vya Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mheshimiwa Balozi Liberata Mulamula (Mb) akizungumza kwenye sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Peace Corps Tanzania yaliyofanyika kwenye viunga vya Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mheshimiwa Balozi Liberata Mulamula, Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mhe. Dr. Donald Wright na Mkurugenzi Mkazi wa Peace Corps Tanzania Bi. Stephanie Joseph de Goes wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Ubalozi wa Marekani na Peace Corps Tanzania.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mheshimiwa Balozi Liberata Mulamula na Rais wa Makampuni ya The Pula Group Dkt. Mary Stith wakiwa kwenye mazungumzo yaliyofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mheshimiwa Balozi Liberata Mulamula akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo na Rais wa Makampuni ya The Pula Group”Dkt. Mary Stith yaliyofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
Muzungumzo yakiendelea
Balozi Mteule Prof. Adelardus Kilangi akisaini kitabu cha wageni alipowasili katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Balozi Liberata Mulamula Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Balozi Mteule Prof. Adelardus Kilangi akisaini kitabu cha wageni alipowasili katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Balozi Liberata Mulamula Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mheshimiwa Balozi Liberata Mulamula na Balozi Mteule Prof. Adelardus Kilangi wakiwa katika mazungumzo


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mheshimiwa Balozi Liberata Mulamula (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Makampuni ya The Pula Group Dkt. Mary Stith katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.

Kampuni ya The Pula Group ni Kampuni ya Kimarekani inayojishughulisha na uchimbaji wa madini ya risasi (graphite) hapa nchini ambayo ni moja ya malighafi muhimu katika uzalishaji wa betri. Pamoja na mambo mengine mazungumzo hayo yalijikita katika kujadili masuala mbalimbali muhimu katika kutangaza fursa kwa lengo la kuvutia wawekezaji wengi zaidi katika sekta hiyo.

Akizungumza baada ya mkutano huo Dkt. Mary ameeleza sambamba na kumshirikisha Waziri Mulamula kuhusu mchango na nafasi ya Kampuni yake katika kutangaza fursa za uwekezaji zinazopatikana nchini hasa kwenye sekta ya madini pia ametumia fursa hiyo kujifunza na kupata uzoefu wa masuala mengi kuhusu Wanawake na Uongozi kutoka kwa Waziri Mulamula.

“Wakati huu ambao Dunia inakabiliana na adhari za madiliko ya Tabianchi, mahitaji ya madini ya ghraphite ambayo ni muhimu katika uzalishaji wa nishati ya umeme yameendelea kuongezeka Duniani kwa sababu ni rafiki kwa mazingira, nafarijika kuona Tanzania ikiwa na kiasi kikubwa cha hifadhi ya madini haya yenye viwango vya kimataifa” Amesema Dkt. Mary.

Aidha Waziri Mulamula kwa upande wake amemwakikishia Dkt. Mary kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi madhubuti wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan itaendelea kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji nchini sambamba na kudumisha ulinzi na usalama.

Kampuni ya The Pula Group ilianza kuendesha shughuli za utafutaji na uchimbaji wa madini ya graphite nchini mwaka 2014.

Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula amekutana na kufanyamazungumzo na Balozi Mteule Prof. Adelardus Kilangi katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam. Prof. Adelardus Kilangi aliteuliwa kuwa Balozi Septemba 12, 2021.

Katika tukio jingine Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula ameshiriki Sherehe ya Maadhimisho ya Miaka 60 ya Peace Corps Tanzania yaliyofanyika kwenye viunga vya Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam. Maadhimisho hayo yaliongozwa na kauli mbiu “Miaka Sitini ya Huduma na Urafiki”.

Akizungumza katika Maadhimisho hayo Waziri Mulamula ameeleza kuwa Tanzania ina thamini sana jitihada na mchango wa Marekani katika maendeleo ya Kijamii na Kiuchumi kwenye maeneo mabalimbali hapa nchini ikiwemo; afya, elimu, miundombinu, maji, teknolojia ya habari na mawasiliano, kuimarisha demokrasia, haki za binadamu, utawala wa sheria na utawala bora.

Waziri Mulamula aliongeza kusema wakati huu ambao nchi hizi mbili zinasherekea Maadhimisho ya Miaka Sitini ya Huduma na Urafiki, ni fursa nyingine ya kutafakari mafanikio yaliyopatikana kutokana na ushirikiano wetu ambayo ni chachu katika kudumisha na kuimarisha ushirikiano wa karibu zaidi baina ya Nchi hizi mbili rafiki. Aidha, Waziri Mulamula amewashukuru Raia wa Marekani ambao kwa muda mrefu wamejitolea kufanya kazi bila kuchoka katika maeneo mbalimbali ya vijijini nchini wakishirikiana na Washirika wa ndani ikiwemo kufundisha hesabu na sayansi katika shule za upili, wakufunzi wa walimu katika teknolojia ya habari na mawasiliano na sekta ya afya.

“Nitumie fursa hii kusisitiza kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kushirikiana na Marekani na itaendelea kufanya kazi kwa ukaribu na Peace Corps Tanzania katika kuleta maendeleo endelevu kwa Nchi yetu”. Alisema Waziri Mulamula.

Peace Corps Tanzania ni Taasisi ya Kimarekani inayochangia nguvu kazi katika shughuli

mbalimbali za maendeleo ya Kijamii na Uchumi kwa kujitolea. Kazi na majukumu ya Peace Corps Tanzaniayanaongozwa na Mkataba uliosainiwa kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Marekani Januari 9, 1979.

Maadhimisho hayo pamoja na washiriki wengine yalihudhuriwa na Mhe. Dr. Donald Wright Balozi wa Marekani nchini Tanzania na Bi. Stephanie Joseph de Goes Mkurugenzi Mkazi wa Peace Corps Tanzania

RAIS MHE.DKT.MWINYI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA WAZIRI MKUU MSTAAFU WA UINGEREZA MHE. TONY BLAIR IKULU ZANZIBAR

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na mgeni wake Waziri Mkuu Mstaaf wa Uingereza Mhe.Tony Blair, mazungumzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
WAZIRI Mkuu Mstaaf wa Uingereza Mhe. Tony Blair akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) baada ya kumaliza mazungumzo yake na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) mazungumzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali (hawapo pichani) baada ya kumaliza mazungumzo yake na Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza Mhe. Tony Blair (kushoto kwake) yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiongozana na mgeni wake Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza Mhe. Tony Blair,baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu) RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na mgeni wake Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza Mhe. Tony Blair, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)

MAKAMU WA RAIS DKT.MPANGO AKUTANA NA UONGOZI WA SHIMMUTA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Shirikisho la michezo la mashirika ya umma na kampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA) mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo. Septemba 30,2021.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akikabidhiwa zawadi ya ngao ya heshima kutoka kwa viongozi wa Shirikisho la michezo la mashirika ya umma na kampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA) akiwa mlezi wa shirikisho hilo mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo. Septemba 30,2021.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akikabidhiwa mavazi ya michezo kutoka kwa viongozi wa Shirikisho la michezo la mashirika ya umma na kampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA) mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo. Septemba 30,2021.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango hii leo Septemba 30, 2021 amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma na Kampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA).

Katika mazungumzo hayo, Makamu wa Rais ametaja Michezo kama njia ya kuleta umoja na undugu katika maeneo ya kazi pamoja na kuondokana na maradhi mbalimbali. Amesema kupitia michezo ndio kunaweza pia kukabiliana na Uviko 19 pamoja na kutoa elimu ya kupata chanjo ya ugonjwa huo.

Makamu wa Rais ametoa rai kwa Shimmuta kutumia michezo wanayoisimamia kutoa elimu ya utunzaji mazingira. Amesema yapo maeneo mengi yanayohotaji upandaji miti pamoja na usafi wa mazingira hivyo Shimmuta inapaswa kuwa chachu ya kuhamasisha utunzaji wa mazingira kwa vitendo.

Aidha Makamu wa Rais ameiasa SHIMMUTA kufanya michezo itakayotoa mchango katika jamii kama vile Riadha zinazofanywa kwa lengo la kupata fedha na kusaidia katika huduma za kijamii.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Shimmuta, Hamis Mkanachi amesema changamoto inayoikabili Shimmuta ni ukosefu wa udhamini katika mashindano yanayoandaliwa pamoja ushiriki mdogo wa Mashirika, Kampuni na taasisi katika michezo hiyo.

Mashindano ya Shimmuta mwaka 2021 yanatarajiwa kufanyika mkoani Morogoro katikati ya mwezi Novemba.

DKT.GWAJIMA AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA PAKISTANI NCHINI TANZANIA

$
0
0

Na.WAMJW- DOM

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima leo amekutana na Balozi wa Pakstani nchini Tanzania Mhe.Muhammad Saleem ambapo wamekubaliana kushirikiana na kubadilishana uzoefu katika uwekezaji na utengenezaji wa viwanda vya dawa na vifaa tiba.

Dkt. Gwajima amemhakikishia utayari wa Wizara yake kushirikiana zaidi na Ubalozi huo kwa kupeleka wataalam wake Pakstani kwa ajili ya mafunzo ya muda mrefu na mfupi ili kuweza kufikia matokeo chanya ya mapinduzi ya uzalishaji wa dawa nchini .

Naye Balozi Muhammad Saleem amesema Pakstani iko tayari kushirikiana na Tanzania katika kuleta matokeo chanya katika sekta ya afya hususani katika swala la miundombinu, vifaa na kuwekeza viwanda vya dawa nchini Tanzania.

Kikao kimefanyika katika ofisi za Wizara zilizopo Jijini Dodoma, kimehudhuriwa pia na Wataalamu kutoka Wizara ya Afya na Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

WAZIRI MCHENGERWA AWATAKA WATUMISHI WALIOSHINDWA KUWAPANDISHA VYEO WENZAO WASHUSHWE VYEO

$
0
0
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais,Utumishi na Utawala Bora Mohammed Mchengerwa,akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali (hawapo pichani) kilichofanyika leo September 30,2021 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais,Utumishi na Utawala Bora Mohammed Mchengerwa,akisisitiza jambo kwa washiriki wakati wa kikao kazi cha Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali (hawapo pichani) kilichofanyika leo September 30,2021 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu, Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome kwa niaba ya Katibu Mkuu-UTUMISHI ,akizungumza wakati wa kikao kazi cha Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali kilichofanyika leo September 30,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali wakimsikiliza Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Utumishi na Utawala Bora Mohammed Mchengerwa,(hayupo pichani) wakati akifungua kikao kazi cha Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali kilichofanyika leo September 30,2021 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Nolasco Kipanda akitoa neno la utangulizi kabla ya Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Utumishi na Utawala Bora Mohammed Mchengerwa,kufungua kikao kazi cha Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali kilichofanyika leo September 30,2021 jijini Dodoma.
Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma, Dkt. Emmanuel Shindika akitoa neno la shukrani kwa niaba ya washiriki kwa Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Utumishi na Utawala Bora Mohammed Mchengerwa,mara baada ya kufungua kikao kazi cha Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali kilichofanyika leo September 30,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Utumishi na Utawala Bora Mohammed Mchengerwa,akiwa katika picha ya pamoja na washiriki mara baada ya kufungua kikao kazi cha Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali kilichofanyika leo September 30,2021 jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna,Dodoma

WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais,Utumishi na Utawala Bora Mohammed Mchengerwa amewaagiza watendaji wa ofisi yake kuwashusha vyeo Maafisa Utumishi katika Taasisi za Umma walioshindwa kuwapandisha vyeo watumishi wenye sifa za kupanda madaraja.

Kauli hiyo ameitoa leo September 30,2021 jijini Dodoma wakati akifungua kikao kazi cha Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watendaji hao.

Amesema,kuwa Afisa Utumishi yeyote aliyezembea na kusababisha Watumishi wa Umma kutopandishwa madaraja achukuliwe hatua kwa kushushwa cheo na kuhamishwa kituo cha kazi ili iwe ni fundisho kwa wengine wanaoshindwa kuwajibika ipasavyo.

“Fanyeni upembuzi na kuwaondoa Maafisa Utumishi wote waliobainika kutotekeleza wajibu wa kuwapandisha madaraja watumishi wenye sifa stahiki, kwani nimekuwa nikipokea malalamiko toka kwa watumishi wa taasisi mbalimbali,” amesema Mhe. Mchengerwa

Aidha amefafanua kuwa, ofisi yake ilifanya kazi usiku na mchana kuhakikisha taarifa za kiutumishi zilizotumwa na waajiri zinafanyiwa kazi kwa lengo la kuwapandisha vyeo watumishi husika.

“Mhe. Rais anatambua kuwa nguzo ya Serikali kiutendaji ni Watumishi wa Umma hivyo haiwezi kufanya vizuri iwapo haitowajali watumishi wake na ndio maana aliagiza wapandishwe madaraja,” Mhe. Mchengerwa amefafanua.

Aidha Waziri Mchengerwa amewataka watendaji hao kutotumia mwanya wa kuajiri vibarua au watumishi wa mkataba kama njia ya kuweka mwanya wa watumishi hewa.

“Ndugu zangu niwaambie katika bajeti ya 2021/2022 serikali iliomba kibali cha kuajiri watumishi 46,000 na mpaka sasa waliojiriwa hawazidi 10,000, hivyo kama watendaji mnauhitaji wa wafanyakazi ombeni kibali cha kuajiri na sio kutumia vibarua au watumishi wa mkataba ili kuweka mwanya wa watumishi hewa,”amesisitiza

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Profesa Sifuni Mchome amesema kuwa lengo la kikao hicho ni kujadili masuala ya wakala ,mafanikio pamoja na changamoto na hatimaye kuzitafutia ufumbuzi wa namna ya kuzitatua.

“Uwepo wa wakala umeleta mafanikio mengi,mojawapo ni wakala nyingi zimeboresha huduma ambapo zinatolewa kwa muda mfupi na bora,wakala nyingi zimeongeza wigo wa mapato ya ndani na kuweza kujitegemea,”amesema

Naye Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma, Dkt. Emmanuel Shindika,akitoa neno la shukrani kwa niaba ya washiriki amemshukuru Mhe. Waziri kwa kukubali wito wa kukutana na Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali na kumuahidi kutekeleza maelekezo yote aliyoyatoa.

WAZIRI MCHENGERWA AELEKEZA KUWABADILISHIA VITUO VYA KAZI MAAFISA UNUNUZI SERIKALINI ILI KUKABILIANA NA VITENDO VYA RUSHWA

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akizungumza na Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali (hawapo pichani) kabla ya kufungua kikao kazi cha watendaji hao kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akifurahia jambo na Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali kabla ya waziri huyo kufungua kikao kazi cha watendaji hao kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akisikiliza utambulisho wa Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali (hawapo pichani) kabla ya waziri huyo kufungua kikao kazi cha watendaji hao kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Nolasco Kipanda pindi alipowasili kufungua kikao kazi cha Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini ACP Ibrahim Mahumi, mara baada ya kufungua kikao kazi cha Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.

Na. James K. Mwanamyoto-Dodoma

Tarehe 01 Oktoba, 2021

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa amewaelekeza watendaji wa ofisi yake kuwa na utaratibu wa kuwabadilishia vituo vya kazi Maafisa Ununuzi na Ugavi wote waliokaa muda mrefu kwenye kituo kimoja ili kukabiliana na changamoto ya maafisa hao kujihusisha na vitendo vya rushwa na ukiukwaji wa taratibu za manunuzi Serikalini.

Mhe. Mchengerwa ametoa maelekezo hayo wakati akifungua kikao kazi cha Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watendaji hao kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.

Mhe. Mchengerwa amesema, wapo Maafisa Ununuzi na Ugavi waliokaa muda mrefu kwenye vituo vya kazi na kuona ofisi ni zao na hatimaye kuanza kufanya kazi kwa mazoea, hivyo ofisi yake inalazimika kuwa na utaratibu wa kuwahamisha ili kuendelea kusimamia uadilifu mahala pa kazi.

“Hakuna Afisa Ununuzi na Ugavi au mtumishi yeyote wa umma mwenye hati miliki ya kukaa muda mrefu kwenye kituo kimoja cha kazi na kuongeza kuwa, ofisi yake itahakikisha inawajibika kuendelea kulinda maadili ya utendaji kazi kwa watumishi wa kada zote,” Mhe. Mchengerwa amesisitiza.

Ameongeza kuwa, Maafisa Ununuzi na Ugavi watakaohamishwa wawe tayari kufanya kazi watakapopelekwa kwani ni jukumu la Watumishi wa Umma kuwatumikia wananchi mahala popote.

Mhe. Mchengerwa amefafanua kuwa, kitendo cha kuwabadilishia Maafisa hao vituo vya kazi kitasaidia sana kuongeza weledi na uwajibikaji mahala pa kazi.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma, Dkt. Emmanuel Shindika amempongeza Mhe. Mchengerwa kwa kutoa maelekezo ya kuwa na utaratibu wa kuwabadilishia vituo vya kazi Maafisa Ununuzi na Ugavi ili waondokane na utendaji kazi wa mazoea unaosababisha wajihusishe na vitendo vya rushwa.

Naye, Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Nolasco Kipanda amesema kwa kuwa takribani asilimia sabini ya matumizi yapo upande wa manunuzi hivyo katika kikao kazi hicho mada ya masuala ya ununuzi na ugavi itawasilishwa ili kujenga uelewa wa pamoja kwa Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali katika eneo hilo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa ameendelea kukemea vitendo vya rushwa kwa Watumishi wa Umma wa kada mbalimbali ikiwemo ya ununuzi na ugavi.

JKCI YATOA HUDUMA ZA VIPIMO VYA MAGONJWA YA MOYO KATIKA MKUTANO WA MWAKA WA MADAKTARI

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Tatizo Waane akielezea huduma zinazotolewa na JKCI wakati Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel alipotembelea banda la JKCI wakati wa Mkutano wa mwaka wa madaktari uliofanyika katika Hoteli ya Malaika Jijini Mwanza.
Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Theophilly Mushi akitoa taarifa ya upimaji uliofanyika katika Mkoa wa Geita wakati Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel alipotembelea banda la JKCI wakati wa Mkutano wa mwaka wa madaktari uliofanyika katika Hoteli ya Malaika Jijini Mwanza.
Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Theophilly Mushi akimpima kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography – ECHO) mwananchi wa Mkoa wa Mwanza aliyetembelea katika banda la JKCI wakati wa mkutano wa mwaka wa madaktari uliofanyika katika Hoteli ya Malaika Jijini Mwanza
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Tatizo Waane akipokea cheti cha utambuzi wa huduma zinazotolewa na JKCI wakati wa Mkutano wa mwaka wa madaktari uliofanyika katika Hoteli ya Malaika Jijini Mwanza.

Picha na: JKCI

MAKAMU WA RAIS WA BENKI YA DUNIA KANDA YA AFRIKA AMALIZA ZIARA YAKE NCHINI

$
0
0
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kulia) akimkabidhi zawadi ya picha ya Mlima Kilimanjaro Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Kusini na Mashariki mwa Afrika, Dkt. Hafez Ghanem, baada ya kumaliza ziara yake nchini Tanzania.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Kusini na Mashariki mwa Afrika, Dkt. Hafez Ghanem wakipeana mikono baada ya Makamu wa Rais huyo kukabidhiwa zawadi ya picha ya Mlima Kilimanjaro, jijini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia (WB) Kanda ya Kusini na Mashariki mwa Afrika, Dkt. Hafez Ghanem na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) wakiteta jambo, baada ya Makamu wa Rais huyo kumaliza ziara yake nchini.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akiteta jambo na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Kusini na Mashariki mwa Afrika, Dkt. Hafez Ghanem, baada ya kumaliza ziara yake nchini Tanzania.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akimuongoza mgeni wake Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Kusini na Mashariki mwa Afrika, Dkt. Hafez Ghanem, alipokuwa akiondoka katika uwanja wa ndege wa Dodoma, baada ya kumaliza ziara yake nchini Tanzania. Mbele ni Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania, Bi. Mara Warwick.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Kusini na Mashariki mwa Afrika, Dkt. Hafez Ghanem, wakiwa katika uwanja wa ndege wa Dodoma, baada ya Makamu wa Rais huyo kumaliza ziara yake nchini Tanzania.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akiagana na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Kusini na Mashariki mwa Afrika, Dkt. Hafez Ghanem, baada ya kumaliza ziara yake nchini Tanzania.

(Picha na WFM, Dodoma)

TAARIFA YA UFAFANUZI KUHUSU MAGARI YA MIZIGO YA TANZANIA YALIYOKWAMA NCHINI MALAWI

MHE. ELSIE KANZA BALOZI MPYA WA TANZANIA NCHINI MAREKANI NA MEXICO AWASILI RASMI MJINI WASHINGTON, D.C.

$
0
0
Mhe. Elsie S. Kanza, Balozi mpya wa Tanzania nchini Marekani na Mexico akiwasili rasmi Mjini Washington D.C kwenye picha akipokewa na Bi. Jean Msabila katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dulles.
Mhe. Elsie S. Kanza, Balozi mpya wa Tanzania nchini Marekani na Mexico awasili rasmi Mjini Washington D.C, kushoto ni Mwambata Jeshi wa Ubalozi wa Tanznia nchini Marekani na Canada, Kanali Festusi J. Mang'wela na kulia ni Bi. Jean Msabila
Picha ya pamoja
Watumishi wa Tanzania House wakiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Balozi Elsie S.Kanza
Kushoto ni Bi Sophia V. Gunda, Mwambata Uhamiaji Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani akiwa katika picha na Mhe. Balozi Elsie S.Kanza siku alipowasili Washington, D.C.
Baadhi ya waatumishi wa Tanzania House wakiwa na Mhe. Balozi Elsie S.Kanza mara tu alipowasili Washington, D.C.
Kwa picha zaidi bofya soma zaidi
Mhe. Balozi Elsie S.Kanza alisalimiana na watumishi wa Tanzania house.
Mhe,Balozi Elsie S. Kanza akiwasili rasmi Kituo chake cha kazi ofisi za Ubalozi wa Tanzania Washington DC.
Mhe. Balozi Elsie S. Kanza akikaribishwa rasmi Tanzania house , Washington D.C na Bi. Jean A. Msabila, Afisa Ubalozi
Mhe. Balozi Elsie S.Kanza, alisalimiana na Watumishi wa Tanzania House- Washington D.C
Mhe. Balozi Elsie S.Kanza, alisalimiana na Watumishi wa Tanzania House- Washington D.C
Mhe. Balozi Elsie S.Kanza, alisalimiana na Watumishi wa Tanzania House- Washington D.C
Mhe. Balozi Elsie S.Kanza, alisalimiana na Watumishi wa Tanzania House- Washington D.C
Mhe. Balozi Elsie S.Kanza, alisalimiana na Watumishi wa Tanzania House- Washington D.C
Mhe. Balozi Elsie S.Kanza asaini kitabu maalum mara baada ya kuwasili Tanzania house, Kituo chake kipya cha kazi , Washington D.C
Mhe. Balozi Elsie Kanza , akipata maelezo mafupi kuhusu kituo chake kipya cha kazi kutoka Menejimenti ya Ubalozi.
Mhe. Balozi Elsie Kanza , akipata maelezo mafupi kuhusu kituo chake kipya cha kazi kutoka Menejimenti ya Ubalozi.
Picha ya pamoja
Picha ya pamoja
Picha ya pamoja
Picha ya pamoja
Picha ya pamoja

BIRTHDAY YA MTOTO TYLAR ILIYOFANYIKA KATIKA HOTELI YA KAFAHARI, PENNSYLVANIA YENYE MANDHARI YA KIAFRIKA NA MBUGA ZA WANYAMA

$
0
0

Keki ya birthday ya mtoto Tylar ikiwa ikimsubili mwenye siku yake aje aikate.
Mtoto Tylar akipata picha ya upendeleo siku wazazi wake walipomfanyia sherehe ya siku yake ya kuzaliwa katika mji wa Pocono Manor ndani ya hoteli kaliya Kalahari yenye mandhari ya kiAfrika na mbuga za wanyama iliyopo Pennsylvania nchini Marekani.
Mtoto Tylar akikata keki.
Mtoto Tylar akikata keku na marafiki zake.
Mtoto Tylar akijiandaa kukata keki.
Mtoto Tylar akiwa katika picha ya pamoja na watoto wenzake.
Mama wakiwa katika picha ya pamoja na Tylar na watoto wao.wa kike.
Kwa picha zaidi bofya soma zaidi
Baba na watoto wao wa kiume katika picha ya pamoja.
Baba na watoto wao wa kike.
Day 2, Juu na chini Watoto katika picha ya pamoja.

 

RAIS SAMIA AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA MKURUGENZI WA BENKI YA KIARABU YA MAENDELEO AFRIKA BADEA,PIA AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA BAADHI YA MAWAZIRI NA WATENDAJI

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Kiarabu ya Maendeleo ya Kiuchumi Afrika (BADEA) Dkt. Sidi Ould Tah, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 05 Oktoba 2021 amekutana na kuzungumza na baadhi ya Mawaziri akiwemo Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Profesa Makame Mbarawa, Waziri wa Tamisemi Mhe. Ummy Mwalimu, Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Profesa Kitila Mkumbo, Waziri wa Nishati Mhe. Januari Makamba pamoja na baadhi ya Watendaji wa Taasisi mbalimbali za Serikali, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 05 Octoba 2021.

PICHA NA IKULU

MAJANGILI YENYE BUNDUKI YAKAMATWA.

$
0
0
Kamnda wa Uhifadhi wa Kanda ya Magharibi kutoka Mamlaka ya ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania(TAWA) Bigilamungu Kagoma akionyesha bunduki aina ya SMG ilikamatwa hivi karibuni katika doria ya kusaka majangili kwenye mapori ya akiba mbalimbali


Na Lucas Raphael,Tabora

MAMLAKA ya Usimammizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Kanda ya Magharibi imewakamata Majangili 11 wakiwa na Bunduki 11 pamoja na Gobore 31 zilizosalimishwa katika Msako Unaoendelea katika Mikoa ya Tabora na Katavi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake jana Kamanda wa Uhifadhi wa Kanda ya Magharibi Bigilwamungu Kagoma alisema Majangili hao wenye Bunduki walikamatwa Wilaya za Kaliua, Sikonge Urambo na Mlele.

Kamanda Kagoma alisema kuwa msako huo ambao ni endelevu ulianza Mapema Mwezi Septemba lengo lake ni kusaka watu wanaojihusisha na Ujangili.

Alisema miongoni mwa bunduki zilizokamatwa moja ni aina ya Short gun na Rifle iliyotengenezwa kienyeji ambazo zilikutwa majumbani mwa majangili wawili.

Aliongeza kuwa kati ya majangili hao mmoja alikutwa kijiji cha Mibono Wilaya ya Sikonge akiwa na bunduki aina ya Rifle 30 06.

Kamanda Kagoma alisema kuwa jangili wa pili alikutwa na Shortgun akiwa ndani ya Hifadhi ya Jumuiya ya Uyumbu Wilaya ya Urambo pia alikamatwa na maganda 15 ya risasi za buinduki na Baruti Gm 200.

Alisema kuwa jangili mwingine alikutwa na Gobore aliweza kuwaonyesha Kiwanda chake cha Kutengenezea Bunduki hizo na vifaa mbali mbali ndani ya Pori jipya la akiba la Inyonga.

Kufuatia hali hiyo aliwaonya wanaojihusisha na Ujangili kuacha vitendo hivyo mara moja pamoja na wanaomiliki bunduki kinyume cha sheria kuzisalimisha kabla hawajakamatwa na kuchukuliwa hatua kali.

Kamanda kagoma pia alitoa wito kwa wananchi waliokuwa wanatumia Mapori ya Inyonga, Wembele na Igombe watoke mara moja kwa kuwa yamepandishwa hadhi na kuwa mapori ya Akiba kwa sasa yanamilikiwa na Tawa.
Viewing all 45984 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>