Quantcast
Channel: VIJIMAMBO
Viewing all 45984 articles
Browse latest View live

SERIKALI KUFUNGA RADA SABA ZA HALI YA HEWA NCHINI

$
0
0
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara, akizungumza katika kikao kazi chake na uongozi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa, Dkt. Agnes Kijazi akitoa taarifa ya Mamlaka hiyo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara, wakati alipotembelea na kukagua utendaji kazi wa Mamlaka hiyo, jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri wa Hali ya Hewa kutoka Mamlaka ya Hewa (TMA), Dkt. Hamza Kabelo, akimuonesha Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara, namna wanavyosoma taarifa za hali ya hewa katika Mamlaka hiyo, jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Buruhani Nyenzi, akizungumza mbele ya Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara, wakati alipotembelea na kukagua utendaji kazi wa Mamlaka hiyo, jijini Dar es Salaam.

Serikali imeingia mkataba kwa ajili ya ujenzi wa rada mbili za mwisho za Hali ya Hewa ili kufikisha mtandao wa rada saba zinazotarajiwa kufungwa katika mikoa ya Dodoma na Kilimanjaro kwa ajili ya kuboresha ukusanyaji na utoaji wa taarifa za hali ya hewa nchini.

Aidha, Serikali imekwishafunga rada tano za hali ya hewa ambapo kati ya hizo rada tatu zimeshafungwa katika mikoa ya Dar es Salaam (Bangulo), Mwanza (Kiseke) na Mtwara (Mikindani) na tayari zimeshaanza kufanya kazi na rada mbili zitakazofungwa katika mikoa ya Mbeya (Kawetire) na Kigoma (Nyamoli) ziko katika hatua za mwisho za utekelezaji.

Ameyasema hayo, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara akiwa jijini Dar es Salaam wakati alipotembelea Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), ambapo pamoja na mambo mengine ameipongeza Mamlaka hiyo kwa ufanisi na utendaji kazi mzuri ndani na nje ya nchi.

“Niwapongeze uongozi na watumishi wa Mamlaka hii kwani utendaji wenu umekidhi mahitaji ya ndani na nje ya nchi na kutunikiwa vyeti vya ubora wa huduma”, amesema Naibu Waziri Waitara.

Naibu Waziri Waitara amewataka watumishi wa Mamlaka hiyo kutobweteka na mazuri yanayoendelea kutekelezwa na Mamlaka hiyo na badala yake kuendeleza kubaini na kufatilia mwenendo wa hali ya hewa, vimbunga baharini, hali mbaya ya hewa, upepo mkali kwa ajili ya sekta za usafiri wa anga, majini, ulinzi, kilimo, uvuvi, utunzaji wa misitu na utalii.

“Taarifa mnazozitoa zinaleta tija kwa sekta zote kwani nimejaribu kufatilia sana hata watu wa meli, anga, kilimo na ujenzi wa miundombinu inayoendelea wanapata taarifa zote na kwa usahihi”, amesisitiza Naibu Waziri Waitara.

Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya TMA, Dkt. Buruhani Nyenzi, ameishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa fedha za miradi ya maendeleo na kuisimamia taasisi hiyo kwa ustawi wa maendeleo ya nchi yetu hasa katika karne ya sasa ambayo masuala ya tabia nchi yamekuwa mtambuka.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi, amesema kuwa taasisi hiyo imeanzishwa mwaka 2019 chini ya Sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Na. 2 ya mwaka 2019 ikiwa na majukumu ya kutoa, kuratibu na kudhibiti huduma za hali ya hewa nchini.

Ameongeza kuwa Mamlaka hiyo ina mitambo ya kisasa pamoja na wataalamu ambao wamesaidia kuboresha sana utabiri kwani kiwango cha utabiri usahihi wake umefikia zaidi ya asilimia 80 hapa nchini.

Naibu Waziri Waitara yuko jijini Dar es Salaam kwa ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuzungumza na uongozi na watumishi wa Taasisi zilizo chini ya Wizara yake.

RAIS DK.MWINYI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA BALOZI WA NIGERIA NCHINI TANZANIA MHE HAMISU UMAR IKULU ZANZIBAR

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ai Mwinyi akimsikiliza Balozi wa Nigeria Nchini Tanzania Mhe. Hamisu Umar Takamawa, alipofi Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na mgeni wake Balozi wa Nigeria Nchini Tanzania Mhe Hamisu Umar Takamawa, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiongazana na mgeni wake Balozi wa Nigeria Nchini Tanzania Mhe. Hamisu Umar Takamawa, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake Balozi wa Nigeria Nchini Tanzania Mhe.Hamisu Umar Takamawa, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.5-10-2021.(Picha na Ikulu)

MAJALIWA: RAIS SAMIA AMETOA SH. BILIONI 2.46 UKARABATI VITUO VYA MIZANI NCHINI

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa bilioni 2.469 kwa ajili ya kuvifanyia maboresho vituo 42 vya mizani nchini kikiwemo na kituo cha Mingoyo kilichopo eneo la Mnazi Mmoja kwenye barabara ya Mtwara-Mingoyo-Masasi mkoani Lindi.

Pia, Mheshimiwa Majaliwa ametoa muda wa miezi miwili kuanzia leo Oktoba 5, 2021 hadi Novemba 30, 2021 uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi uwe umetenga eneo kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha mabasi na maegesho ya malori.

Ameyasema hayo leo (Jumanne, Oktoba 5, 2021) wakati akizungumza na wananchi katika eneo la Mnazi Mmoja mkoani Lindi baada ya kukagua kituo cha Mizani cha Mingoyo akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika mkoa huo.

Mheshimiwa Majaliwa amesema Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi imetenga bajeti katika mwaka wa fedha 2021/2022 kwa ajili ya kufunga Load Cells za kisasa (electronic Load Cells) katika vituo vyote 42 vya mizani nchni.

Pia, Mheshimiwa Majaliwa ametumia fursa hiyo kumuagiza Meneja wa TANROADS mkoa wa Lindi, Mhandisi Efatha Mlavi akifanyie maboresho kituo cha Mizani cha Mingoyo ili kurahisisha utendaji kazi katika mizani hiyo ikiwemo uingiaji na utokaji wa magari.

Akizungumzia kuhusu ujenzi wa kituo cha mabasi cha Mnazi Mmoja Waziri Mkuu amesema eneo hilo linakuwa kwa kasi na linahitaji liwe na kituo cha mabasi pamoja na kituo cha kuegeshea malori ili kupunguza msongamano uliopo sasa. “

Baada ya Waziri Mkuu kutoa agizo hilo wakazi wa Mnazi Mmoja waliishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia kwa kuwajali na kwamba wanaahidi kuendelea kuiunga mkono.

Kadhalika, Waziri Mkuu amekagua maendeleo ya maradi wa ujenzi wa barabara ya Hingawali-Navanga (km 14.1) na Navanga-Pangabuhi (km 8), Mkoani Lindi inayojengwa kwa kiwango cha changarawe ambao ujenzi wake umefikia asilimia 40.

Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa ujenzi wa barabara hiyo ambayo inajengwa kwa gharama ya shilingi milioni 299.9 utakuwa mkombozi kwa wananchi wa maeneo hayo kwa kuwa utarahisisha usafirishaji.

WAZIRI KIJAJI AKUTANA NA WAKUU WA TAASISI BAADA YA WIKI TATU TANGU KUAPISHWA KWAKE

$
0
0
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza na wakuu wa taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo katika ukumbi wa Ofisi za Wizara hiyo zilizopo Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma. Kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Kundo Mathew na Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Zainab Chaula.
Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew akizungumza wakati wa kikao kazi cha Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Ashatu Kikaji (katikati) na wakuu wa taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo katika ukumbi wa Ofisi za Wizara hiyo zilizopo mji wa Serikali Mtumba, Dodoma. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Zainab Chaula.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Zainab Chaula akizungumza wakati wa kikao kazi cha Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Ashatu Kikaji (kushoto) na wakuu wa taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo (hawapo pichani) katika ukumbi wa Ofisi za Wizara hiyo zilizopo mji wa Serikali Mtumba, Dodoma
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabir Kuwe akizungumza wakati wa kikao kazi cha Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Ashatu Kikaji (hayupo pichani) na wakuu wa taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo katika ukumbi wa Ofisi za Wizara hiyo zilizopo mji wa Serikali Mtumba, Dodoma
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) Macrise Mbodo akizungumza wakati wa kikao kazi cha Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Ashatu Kikaji (hayupo pichani) na wakuu wa taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo katika ukumbi wa Ofisi za Wizara hiyo zilizopo mji wa Serikali Mtumba, Dodoma
Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Justina Mashiba akizungumza akizungumza wakati wa kikao kazi cha Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Ashatu Kikaji (hayupo pichani) na wakuu wa taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo katika ukumbi wa Ofisi za Wizara hiyo zilizopo mji wa Serikali Mtumba, Dodoma
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Daphrosa Kimbory akizungumza wakati wa kikao kazi cha Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Ashatu Kikaji (hayupo pichani) na wakuu wa taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo katika ukumbi wa Ofisi za Wizara hiyo zilizopo mji wa Serikali Mtumba, Dodoma
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA (ICTC) Samson Mwela akizungumza wakati wa kikao kazi cha Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Ashatu Kikaji (hayupo pichani) na wakuu wa taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo katika ukumbi wa Ofisi za Wizara hiyo zilizopo mji wa Serikali Mtumba, Dodoma
Katibu Mtendaji wa Baraza la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano (TCRA-CCC) Mary Msuya akizungumza wakati wa kikao kazi cha Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Ashatu Kikaji (hayupo pichani) na wakuu wa taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo katika ukumbi wa Ofisi za Wizara hiyo zilizopo mji wa Serikali Mtumba, Dodoma
Kaimu Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Tuma Abdallah akizungumza wakati wa kikao kazi cha Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Ashatu Kikaji (hayupo pichani) na wakuu wa taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo katika ukumbi wa Ofisi za Wizara hiyo zilizopo mji wa Serikali Mtumba, Dodoma

Prisca Ulomi na Faraja Mpina
*Asema Wizara yake ni Wezeshi kwa maendeleo ya Taifa
*Awataka watumishi wawe wazalendo
*Watekeleze Mkataba baina ya CCM na Serikali kwa kuhudumia wananchi

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Ashatu Kijaji amekutana na Wakuu wa taasisi zilizo chini ya Wizara katika kikao kazi kilichofanyika jana tarehe 04/10/2021 katika ofisi za Wizara hiyo zilizopo mji wa Serikali Mtumba, Dodoma baada ya wiki tatu tangu alipoteuliwa na kuapishwa kuongoza Wizara hiyo

Dkt. Kijaji amesema kuwa kikao hicho kilikuwa na lengo la kufahamiana, kukumbushana na kutambua majukumu yao katika Taifa kwa kuitumikia Serikali iliyopo madarakani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambayo iliingia Mkataba mahsusi na wananchi kupitia Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 – 2025

“Wizara hii ni sehemu ya Serikali na tuna jukumu la kuhakikisha Mkataba ambao chama cha CCM kiliingia na wananchi unatekelezeka ipasavyo katika tasnia za Habari, Mawasiliano na TEHAMA kwa kutekeleza jukumu kubwa la kuwawezesha watanzania kupata mawasiliano na habari ambazo zina athari chanya kwenye maisha yao kijamii na kiuchumi”, amezengumza Dkt. Kijaji

Amesema kuwa Wizara hiyo ni Wizara wezeshi lakini imekuwa ikichangia pato la Taifa kwa asilimia 1.5 kwa miaka minne mfululizo kitu ambacho anakiona hakijakaa sawa hasa ukizingatia kama Taifa tunaelekea kwenye uchumi wa dijitali ambapo Wizara hiyo pamoja na taasisi zake wanapaswa kuangalia upya na kuleta mabadiliko ya mchango wao kwa pato la Taifa

Ameongeza kuwa watendaji wakuu wa taasisi za Wizara yake wahakikishe wanakuwa wazalendo na kuleta tafsiri sahihi ya viti walivyoaminiwa na Serikali kuvikalia kwa kuhakikisha wanawafikishia watanzania huduma zenye viwango na ubora unaohitajika

Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Zainab Chaula amezungumzia kikao hicho kuwa kilikuwa ni kikao cha Waziri kufahamiana na Wakuu wa taasisi na kukumbushana kutimiza wajibu kwa watendaji hao kuwajibika kwa matokeo ambayo ni kutoa huduma bora kwa wananchi na kuhakikisha taarifa za utekelezaji wa matokeo chanya zinamfikia mwananchi

Naye Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Macrise Mbodo amesema kuwa kikao hicho kimetengeneza uelewa wa pamoja kati ya utendaji wa taasisi na matamanio na matarajio ya Waziri huyo ya utendaji wa taasisi hizo kwa matokeo ambapo wakuu wa taasisi hizo walipata fursa ya kueleza majukumu ya msingi ya taasisi zao, zilipotoka na zinapoelekea

Kikao hicho kilihudhuriwa na wakuu wa taasisi za Wizara hizo ambazo ni Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Shirika la Posta Tanzania (TPC), Tume ya TEHAMA (ICTC) na Baraza la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano (TCRA-CCC).

WIZARA YA ELIMU KUJENGA MAABARA ZA MUDA KATIKA TAASISI YA SAYANSI ZA BAHARI YA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM ZANZIBAR

$
0
0
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Profesa Joyce Ndalichako, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa James Mdoe, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na viongozi Waandamizi wa chuo hicho wakikagua eneo zitakapojengwa maabara za muda za Taasisi ya Sayansi za Bahari katika kampasi ya Buyu.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa William William Anangisye akimuonesha Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako vifaa mbalimbali vya maabara za Taasisi ya Sayansi za Bahari vilivyoteketea kwa Moto.
Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mhe Profesa Joyce Ndalichako akiangalia uharibifu wa miundo mbinu ya maabara za Taasisi ya Sayansi za Bahari ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam zilizoteketea kwa moto Oktoba 2 , 2021 katika eneo la Mizingani Bandarini Zanzibar.
Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mhe Profesa Joyce Ndalichako na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Simai Mohamed Said pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa James Mdoe wakikagua Maabara za Taasisi ya Sayansi za Bahari ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam zilizoteketea kwa moto Jana Oktoba 4 , 2021 katika eneo la Mizingani Bandarini Zanzibar.

Na WyEST,Zanzibar

Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako, amesema Wizara itahakikisha Taasisi ya Sayansi za Bahari ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam iliyoko Zanzibar inajengewa Maabara za muda na kuwekewa vifaa baada ya moto kuteketeza maabara zote na vifaa siku ya Jumamosi Oktoba 2, 2021 ili kuwezesha wanafunzi kuendelea na masomo watakapofungua chuo.

Akizungumza mjini Zanzibar Oktoba 4, 2021 baada ya kukagua uharibifu uliotokea kwenye jengo la maabara la Taasisi hiyo lililoko eneo la Mizingani Bandarini, Waziri Ndalichako amesema pamoja na kujenga maabara za muda Wizara ina mpango wa kujenga maabara za kudumu na kwamba tayari Serikali kupitia Wizara ilishatoa Shilingi bilioni moja kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa maabara mpya, hivyo ameagiza sehemu ya fedha hizo zitumike kununua vifaa muhimu vya maabara zitakazotumika kwa muda.

“Sisi kama Wizara tunaendelea kutekeleza kwa vitendo maono ya Mhe. Rais ya kuhakikisha elimu yetu inatoa vijana wenye ujuzi katika eneo hili la sayansi za bahari na ndio maana wiki iliyopita tumetoa kwa Taasisi hii Shilingi bilioni moja kwa ajili ya kukamilisha maabara mpya, hivyo pateni kibali cha kutumia sehemu ya fedha hizo kununua vifaa,” amefafania Waziri Ndalichako.

Aidha, Prof. Ndalichako amemuagiza Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa William Anangisye kuhakikisha Chuo kinafunguliwa Oktoba 25, 2022 kama ilivyopangwa ili kutoathiri mzunguko wa Mwaka wa Masomo na kuwataka wanafunzi wa Chuo hicho kutokuwa na hofu .

Ndalichako ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Jeshi la Polisi, Idara ya Zimamoto kikosi cha Bandarini na Kamisheni ya Maafa iliyoko chini ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar pamoja na Raia wema kwa kazi kubwa ya kudhibiti na kuzima moto huo.

Kwa upande wake Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe. Simai Mohamed Said amemshukuru Prof. Ndalichako kwa kufika katika eneo hilo na kuahidi kushirikiana na chuo hicho kuhakikisha shughuli za Masomo zinaendelea kutokana na umuhimu wa Taasisi hiyo kwa uchumi wa nchi.

“Sote tunatambua umuhimu wa Taasisi hii ambayo ni chachu na kitovu cha kuimarisha uchumi wa Buluu na maabara hizi zilikuwa tegemeo si kwa Tanzania tu bali hata nchi za jirani hivyo tutashirikiana kuhakikisha zinarejea katika kipindi kifupi,” amesema mhe. Simai.

Naye Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam amesema moto huo ulizuka Jumamosi mchana katika jengo la maabara eneo la Mizingani Bandarini na kuteketeza maabara zote 3 pamoja na vifaa, vyumba vya madarasa 3, ofisi 2 na chumba cha “Server”.

Amesema Taasisi mbalimbali na jeshi la polisi zinaendelea na uchunguzi ili kubaini hasara halisi na kuongeza kuwa Chuo tayari kimeandaa mpango wa kuwezesha masomo kuendelea mara kipindi cha masomo kwa mwaka 2021/2022 kitakapoanza Oktoba 2021. Amesema mpango huo ni Pamoja na kujenga maabara za muda katika eneo la Buyu yalipo makao makuu ya Taasisi hiyo.

Taasisi ya Sayansi za Bahari ya Chuo Kikuu cha Dar es Salam iliyopo Zanzibar ina wanafunzi zaidi ya 100 wa Shahada ya Awali, Umahiri na Uzamivu kutoka Tanzania na nje ya Tanzania.

WAZIRI UMMY AKABIDHI GARI LA KUBEBEA WAGONJWA KITUO CHA AFYA MIKANJUNI ,ATOA MAAGIZO KWA DED TANGA

$
0
0
MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi kulia akimkabidhi Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurhamani Shiloo kushoto gari la kubebea Wagonjwa (Ambulace) kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Mikanjuni ambalo limetolewa na Mbunge huyo mapema leo kulia anayeshuhudia ni Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Mikanjuni Mwajame Bausy wa pili kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Spora Liana
Gari la Kubeba wagonjwa Ambulance ambalo limetolewa na Mbunge wa Jimbo la Tanga Ummy Mwalimu kama linanyoonekana
Mbunge wa Jimbo la Tanga Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada yua makabdhiano hayo leo
Mbunge wa Jimbo la Tanga Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi akizungumza na wananachi waliofika kwenye kituo cha Afya Mikanjuni Jijini Tanga mara baada ya kukabidhi gari la kubebea wagonjwa ambalo amelitoa kulia ni Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurhamani Shiloo wa wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Spora Liana
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abduraham Shiloo akizungumza wakati wa halfa hiyo kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Tanga(CCM) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi na kulia ni Diwani wa Kata ya Mabawa
Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Mikanjuni Mwajame Bausy akitoa taarifa ya kituo hicho kwa Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi
Diwani wa Kata ya Mabawa akizungumza

NA OSCAR ASSENGA, TANGA

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Ummy Mwalimu amemtaka Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Spora Liana kutokumuonea aibu Afisa wa Afya yoyote ambaye atakwenda kunyume na miongozo na taratibu za utoaji huduma kwenye vituo vya afya Tanga Jijini humo.

Aliyasema hayo leo wakati akikabidhi gari maalumu ya kubebea wagonjwa (Ambulace) kwenye kituo cha Afya Mikanjuni ambapo limetolewa na Waziri Ummy Mwalimu ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM)

Hatua hiyo ya mbunge huyo kutoa msaada huo wa gari ni kuondosha kero ambazo zilikuwa zinawakabili wananchi hususani wagonjwa ambazo walikuwa wakikumbana nazo wakati wakihitaji kupata huduma ya dharura.

Alisema kwa sababu Rais anataka kuwatumikia wananchi wa Tanga na watanzania wanyonge sasa kama dawa zinakuja na watu wanaambiwa hakuna na wanafanya mambo kijanjajanja wasivumiliwe hata kidogo

“Ndugu zangu Tanga Jiji haitakiwi vituo vya kutolea huduma vikakosa dawa Mkurugenzi lisimamieni tunataka dawa ziwepo kwenye vituo vya afya na zahanati na mjitathimini tusianze kutafutana uchawi Je mnakwenda sahihi na miongozo ya Serikali?Alihoji Waziri Ummy.

Alisema wanachotaka ni wahakikishe huduma bora zinapatikana lakini niwapongeze pia watumishi na wahudumu wa afya kwa kazi nzuri wanayofanya kwa kuhakikisha wananchi wanapata matibabu.

“Lakini niwaambie Rais Marehemu Magufuli amelala lakini kazi yake inaonekana na Rais Samia Suluhu ataendeleza hivyo wana Tanga tuendelee kumuunga mkono kwani amedhamini kuleta maendeleo makubwa”Alisema

Hata hivyo alisema yeye kama mbunge aliamua kutoa msaada huo baada ya kupokea kero kutoka kwa Diwani Kata ya Mabawa na wananchi kuhusu gari la kubebea Wagonjwa (Ambulance) kwa sababu mgonjwa anatakiwa kupelekwa bombo gari haiji kwa wakati na hivyo kupelekea uwepo wa changamoto”Alisema

Hata hivyo alisema aliona njia nzuri ya kuweza kuondosha kero hiyo ni kuwanunulia gari hilo kutokana na kata hiyo ni miongoni mwa kata zilizomuunga mkono .

“lakini pia niwaashe mhakikishe mnaitunza gari hii na Mkurugenzi mtafanya taratibu za kuihamisha iwe sm na tutakabidhi funguo na atatufwe dereva kwa ajili ya kuiendesha na niwaahaidi kwamba nitaenda kutafuta kwa ajili ya vituo vya afya nyengine”Alisema

Awali akizungumza Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurhamani Shiloo amesema katika vituo vya afya kila mwananchi anaapopata huduma kwenye vituo vya afya au zahanati kuhakikisha anapewa risiti za kieletroni kutokana na fedha aliyopewa na hakuna lugha mbadala.

Alitoa wito kwa wananchi ili waweze kuunga mkono juhudi za mbunge ili fedha ziweze kuleta tija na maslahi mapana kwa wagonjwa ili waweze kununua vifaa tiba na dawa ili wagonjwa waweze kuhudumiwa.

“Pili niombe vifaa vitakavyokuwa vikitolewa na vinavyotolewa vitumike kwa maslai mapana na wananchi wa Jiji la Tanga ili kuunga mkono juhudi za mbunge kwa sababu yeye ameamua kushughulika na matatizo ya wananchi wa Tanga ili kuhakikisha anaondosha kero zao.

Naye Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Mikanjuni Mwajame Bausy aliishukuru Serikali ya awamu ya sita na uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga kwa upanuzi mkubwa uliofanyika kwenye kituo hicho .

Alisema katika upanuzi huo majengo matatu yamejengwa kwa gharama ya sh milioni 400 na yamekamilika na yameanza kutumika na kutoa huduma kwa wananchi.

“Hali hii imeongeza ubora wa huduma zinazotolewa kwenye kituo na kuongeza mapato yatokana na huduma za afya na robo ya mwisho mwaka 2020/2021 kituo kilikusanya miloni 14.2 ukilinganisha na mapato ya robo ya mwaka ya mwaka wa fedha 2021/2022 kituo kilikiusanya kiasi cha milioni 22.2”Alisema

DK. KHALID AFUNGUA MKUTANO WA KUTHIBITISHA RHASIMU YA SERA YA KINGA YA USAFIRISHAJI WA HARAMU WA BINAADAMU.

$
0
0
Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano wa kuthibitisha Rasimu ya Sera ya Kinga ya Usafirishaji Haramu wa Binaadamu na Kinga ya Uhamiaji Haramu katika Bara la Afrika wakifuatilia mkutano huo uliyofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Madinatul Bahari Mbweni Zanzibar. Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Sera, Uratibu na Braza la Wawakilishi Dkt. Khalid Salum Mohammed akifungua Mkutano wa kuthibitisha Rasimu ya Sera ya kinga ya Usafirishaji Haramu wa Binaadamu na Kinga ya Uhamiaji Haramu katika bara la Afrika,hafla iliyofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Madinatul Bahari Mbweni Zanzibar.Mkurugenzi Mkuu Idara ya Maendeleo ya Jamii, Michezo Utamaduni, Kazi, Ajira na Uhamaji Bw. Sabelo Mbokazi, akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano wa Kuthibitisha Rasimu ya Sera ya Kinga ya Usafirishaji Haramu wa Binaadamu na Kinga ya Uhamiaji haramu katika Bara la Afrika, uliofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Madinatul Bahari Mbweni Zanzibar.
Waziri wa Nchi, Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Sera, Uratibu na Baraza La Wawakilishi Dkt. Khalid Salum Mohammed akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kufungua Mkutano wa kuthibitisha Rasimu ya Sera ya kinga ya Usafirishaji Haramu wa Binaadamu na Kinga ya Uhamiaji Haramu katika Bara la Afrika,hafla iliyofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Madinatul Bahari Mbweni Zanzibar.

PICHA NA FAUZIA MUSSA -MAELEZO ZANZIBAR.

Issa Mzee – Maelezo Zanzibar 06/10/2021

Kamisheni ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Afrika (AU), imeamuwa kuweka sera ya kinga dhidi ya usafirishaji haramu wa binadamu, na uhamaji haramu kwa lengo la kupiga vita uvunjifu wa Haki za Binadamu unaofanywa Barani Afrika.

Akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano wa Kuthibitisha sera hizo katika ukumbi wa Hotel ya Madinatul Bahri Mbweni Zanzibar ,Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi, Dk, Khalid Salum Mohamed amesema umefika wakati wa kuhakikisha uhalifu huo unapotea Afrika.

Alisema kwa muda mrefu Barani Afrika kumekuwa na matukio ya uvunjifu wa haki za binadamu kwa kusafirisha watu kwenda nje ya Afrika jambo ambalo huwaletea madhara makubwa wanapofika ugenini.

Alieleza kuwa, ni jambo lisilopingika kuwa, Nchi nyingi za Afrika ikiwemo Tanzania zinaathirika vibaya kutokana na usafirishaji haramu wa binadamu, licha ya kuwepo sheria ya kimataifa inayokataza uhalifu huo.

“Uhalifu huu huwaathiri na kuwakumba zaidi wanawake na watoto na kupelekwa nchi mbalimbali ikiwemo Mashariki ya Kati na hata Barani Ulaya ambapo hukutana na vitendo mbalimbali vya uvunjifu wa haki za binadamu ikiwemo mauaji” alisema Waziri huyo.

Hivyo ,alisema uthibitishwaji wa sera ya Kinga ya Usafirishaji Haramu wa Binadamu na Kinga Ya Uhamaji Haramu katika Bara la Afrika ni hatua muhimu na itasaidia katika kuondoa uhalifu huo.

Nae Mwakilishi wa Shirika la kimataifa la Wahamaji(IOM) Tanzania, Qassim Sufi,alisema shirika hilo linatambua madhara ya uhalifu huo ambao kwa kiasi kikubwa husababishwa na hali ya kukosekana kwa amani na utulivu katika baadhi ya mataifa ya Afrika.

Alisema licha ya kuwepo kwa sera hizo, ipo haja kwa kila Nchi mwanachama wa Jumuiya ya Afrika kuweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha Raia wanalindwa hasa wanawake na watoto.

Aidha alieleza kuwa, Shirika linaloshughulikia Wahamaji Duniani (IOM),linapenda kuona haki za binadamu zinalindwa hasa kwa wahamaji, kwani ni haki ya kila mwanadamu kuheshimiwa na kupewa haki zake popote Duniani.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Michezo Utamaduni, Kazi, Ajira na Uhamaji kutoka Umoja wa Nchi za Afrika(AU), Bw.Sabelo Mbokazi, alisema Bara la Afrika haliwezi kuwa na amani wala maendeleo ikiwa uhalifu wa kusafirisha binadamu unaendelea kuwepo.

Alieleza kuwa, upatikanaji wa haki za binadamu na uwepo wa sera na sheria madhubuti, utasaidia katika kuhakikisha Raia wa Afrika wanabaki salama katika Mataifa yao.

Alisema utekelezaji wa sera mbili zinazotarajiwa kuthibitishwa katika mkutano huo ni miongoni mwa hatua madhubuti zinaweza kusaidia katika kutokomeza uhaklifu huo Barani Afrika.

Hata hivyo, alisema umefika wakati wa kuhakikisha wahalifu wote wanaohusika nauhalifu huo wanafikishwa katika vyombo vya sharia na kufunguliwa mashataka ili kukomesha vitendo hivyo.

Mkutano huo uliolenga kuthibitisha Sera ya Kinga ya Usafirishaji Haramu wa Binadamu na Kinga ya Uhamaji Haramu umehudhuriwa na nchi mbalimbali za Umoja wa Afrika ikiwemo Zambia, Algeria,Mauritania na Tanzania.

WAZIRI MWAMBE ALITAKA BARAZA LA UWEZESHAJI KUFANYA UTAFITI WA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji Mhe.Geoffrey Mwambe akiongea na Bodi Pamoja na menejimenti ya Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi jijini Dodoma.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Bibi. Beng’i Issa akiongea wakati wa kikao cha Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji Mhe.Geoffrey Mwambe a Bodi Pamoja na menejimenti ya Baraza hilo jijini Dodoma.
Baadhi ya wajumbe wa Bodi na Menejimenti ya Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi wakiwa katika kikao Pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji Mhe.Geoffrey Mwambe jijini Dodoma .


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji Mhe.Geoffrey Mwambe amelitaka Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), kufanya tafiti kuhusiana na suala la mitaji na masuala ya riba hali ambayo itasaidia kuonyesha namna mitaji inavyoweza kupatikana, athari za riba kubwa na njia za kusaidia kuzipunguza kama namna ya kuwawezesha Watanzania kuimarika kiuchumi.

Mhe. Mwambe ameyasema hayo wakati alipokutana na kuzungumza na Bodi pamoja na Menejimenti ya Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi jijini Dodoma. Aidha, amefafanua kuwa sera ya uwezeshaji ni mtambuka na inamhusu kila mtu na sekta zote hivyo kuna umuhimu wa Baraza kuwaelewesha wananchi na kila sekta ili watambue kuwa wanalo jukumu la kuitekeleza sera hiyo.

Amefafanua Baraza lina kazi kubwa ya kuwalea wajasiriamali wanaofanya vizuri na kutoa ajira kwa watu wengine. Amesiistiza kuwa wapewe ushauri na kuwapendekeza kupata mikopo nafuu na kusaidiwa vitendea vya kisasa ili kuongeza uzalishaji na kutoa ajira kwa wananchi wengi.

Awali akiongea katika kikao hicho, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Bibi. Beng’i Issa amebainisha kuwa mipango ya Baraza hilo ni kuhakikisha inafanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwawezesha wananchi kwa kuandaa sera ya Taifa ya ushiriki wa watanzania katika Uwekezaji na miradi ya kimkakati kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu,

Ameongeza kuwa Mipango ya Baraza hilo ni kuendeleza vituo vya uwezeshaji katika ngazi ya Mikoa na Halmashauri, kuratibu utendaji wa jukwaa la wanawake kiuchumi katika ngazi ya Mikoa na Halmashauri na ujenzi wa jengo la Ofisi kwa ajili ya matumizi ya Baraza.

Kwa niaba ya Bodi ya Baraza, Prof. Lucian Msambichaka alimhakikishaia alimshukuru Mhe. Waziri kuwa maelekezo aliyoyatoa watayatekeleza kwa wakati ili kuhakikisha wananchi wanawezeshwa kiuchumi.

Kikao hicho kilihudhuriwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu- Uwezeshaji Prof. Godius Kahyarara Pamoja na Watumidhi wa Idara ya Uwezeshaji Ofisi ya Waziri Mkuu- Uwekezaji.

DKT. MAHENGE: TUTATUMIA KILA MBINU WANANCHI WAPATE CHANJO YA UVIKO SINGIDA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa Singida Dkt.Binilith Mahenge akizungumza kwenye kikao cha kamati ya afya ya msingi ya jamii (PHC) Mkoa wa Singida kilicho keti leo kuhusu utekelezaji wa mpango shirikishi na harakishi kwa ajili ya utoaji wa chanjo dhidi ya ugonjwa wa Uviko 19. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Alhaj Juma Kilimba na Mganga Mkuu Mkoa wa Singida Victorina Ludovick.
Mganga Mkuu Mkoa wa Singida Victorina Ludovick akizungumza kwenye kikao hicho.
Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dorothy Mwaluko akizungumza kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali ya Mitaa (TAMISEMI) Idara ya Jamii na Lishe, Dinah Atinda (kulia) na Richard Magodi kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakiwa kwenye kikao hicho.
Viongozi wa dini wakiwa kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Mratibu wa Health Promotion Mkoa wa Singida, Habibu Mwinory akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskas Muragili akichangia jambo kwenye kikao
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo akichangia jambo kwenye kikao
Mwakilishi kutoka Shirika la Sema na Mjumbe wa Taifa wa Baraza la Mashirika yasiyo ya Kiserikali Mkoa wa Singida Peter Lissu akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Mratibu wa TASAF Mkoa wa Singida, Patrick Kasango akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Mchungaji wa Kanisa la Anglikana Joseph Kyense akichangia jambo kwenye kikao hicho

Na Dotto Mwaibale, Singida

MKUU wa Mkoa wa Singida Dkt.Binilith Mahenge amesema watatumia kila mbinu ili kuona wananchi wa mkoa huo wanapata chanjo ya Uviko-19.

Dkt.Mahenge ameyasema hayo leo kwenye kikao cha kamati ya afya ya msingi ya jamii (PHC) Mkoa wa Singida kilicho keti kuhusu utekelezaji wa mpango shirikishi na harakishi kwa ajili ya utoaji wa chanjo dhidi ya ugonjwa wa Uviko 19.

“Tumekwisha anza kuona matokeo mazuri ya watu kujitokeza kupata chanjo, hii inatokana na kazi nzuri na mbinu mbalimbali za uhamasishaji naomba tusimame hapo na twende tukaeneze hizo juhudi ninachohitaji ni kuona watanzania wengi wanapata chanjo,”. alisema Mahenge.

Alisema zitatumika kila mbinu katika kukamilisha kazi hiyo kwani kwenye msafara wa mamba kenge hawakosekani hivyo ni wajibu wetu tufanye kila liwezekanalo ili wabaki mamba na kuachana na hao kenge ambao wanazohofisha jitihada hizo.

Alisema kazi hiyo inawezekana hasa baada ya hizi siku chache kuongezeka kwa idadi ya wananchi kujitokeza kupata chanjo hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo alisema muitikio wa wananchi kupata chanjo hiyo ni mkubwa zaidi maeneo ya vijiji tofauti na mijini ambapo alitolea mfano wa Singida Mjini ambayo imepitwa na Singida Vijijini hivyo akaomba uhamasishaji katika maeneo ya mijini uongezewe nguvu.

Mchungaji wa Kanisa la Anglikana Joseph Kyense aliiomba Serikali iendelee kuleta chanjo nyingi zaidi ili kila mwananchi aweze kuchagua chanzo atakayoipenda badala ya kuwa na moja tu.

Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskas Muragili alisema kupitia mpango huo Shirikishi na Harakishi wananchi wamekuwa na muitikio hasa baada ya kueleweshwa umuhimu wa chanjo hiyo.

Mwakilishi kutoka Shirika la Sema na Mjumbe wa Taifa wa Baraza la Mashirika yasiyo ya Kiserikali Mkoa wa Singida Peter Lissu alisema kesho kwa kushirikiana na Civil Society Foundation watakuwa na kikao na Mashirika 50 ya mkoani hapa kwa ajili ya kuona mchango wao wa uhamasishaji wananchi kujitokeza kupata chanjo hiyo.

Mwenyekiti wa Dini mbalimbali Mkoa wa Singida Sheikh Hamisi Kisuke alisema zoezi la kwenda kuhamasisha nyumba kwa nyumba ili watu wajitokeze kupata chanjo limefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa kuongeza idadi ya watu tofauti na mwanzo.

RAIS SAMIA AMEDHAMIRIA KUMSHUSHA MAMA NDOO KICHWANI – MAJALIWA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Maji cha Swahili cha Nangurukuru wilayani Kilwa, Hosseah Hopaje wakati alipotembelea kiwanda hicho, Oktoba 6, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama maji yaliyowekwa kwenye chupa wakati alipotembelea kiwanda cha Swahili cha Nangurukuru wilayani Kilwa, Oktoba 6, 2021. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda hicho, Hosseah Hopaje. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama chupa kubwa za maji wakati alipotembelea kiwanda cha maji cha Swahili katika eneo la Nangurukuru wilayani Kilwa, Oktoba 6, 2021. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda, Hosseah Hopaje. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu kiwanda cha maji cha Swahili cha Nangurukuru wilayani Kilwa kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda, Hosseah Hopaje wakati alipotembelea kiwanda hicho, Oktoba 6, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kilwa, kufanya utafiti wa kina wa maeneo ambayo yatawezesha upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo yote yenye changamoto ya maji katika wilaya hiyo.

Amesema Serikali inayoongozwa na mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuhakikisha huduma ya maji safi na salama inapatikana katika kila kijiji ikiwa ni utekelezaji wa kampeni yake ya kumtua mama ndoo kichwani.

Ametoa maagizo hayo leo (Jumatano Oktoba 6, 2021) wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na wakazi wa vijiji vya Nasaya, Chumo na Kipatimu akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo katika Mkoa wa Lindi.

“Utafiti lazima ufanyike ili tujue wapi tunapa maji, Rais Samia anatoa pesa kwa ajili ya kuwahudumia wananchi, piteni mpime maeneo yote mtafute vyanzo na mtuambie maji yako kiasi gani, mitambo na wataalam tunao.”

Awali, akizungumza na wananchi wa kijiji cha Chumo, Waziri Mkuu ametoa onyo kwa wafugaji wenye tabia ya kuingiza mifugo katika mashamba ya wakulima. “Viongozi wekeni utaratibu wa kukutana na wafugaji na kuwaelimisha ili wafuge kulingana na ukubwa wa maeneo yao.”

Waziri Mkuu amesema kuwa Serikali inaendelea na mpango wake wa kuunganisha mtandao wa barabara Wilaya kwa Wilaya baada ya kukamilika kwa mpango wa kuunganisha makao makuu ya mikoa kwa barabara za lami.

“Meneja wa TANROADS nimeona ukarabati unaoendelea hakikisha barabara hii inafanyiwa ukarabati wa mara kwa mara na iwe inapitika kipindi chote.”

Akiwa katika kijiji cha Miteja Waziri Mkuu alimuagiza Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Zainab Kawawa asimamia ujenzi wa Kituo Shikizi cha Masaninga ambacho kimejengwa kwa nguvu ya wananchi hadi kufikia hatua ya upauaji.

Amesema hadi kufikia tarehe 4 ya mwezi Novemba shule hiyo iwe imekamilika na kuchangia shilingi milioni tano ikiwa ni hatua ya kuunga mkono jitihada za wananchi wa kijiji hicho.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu alitembelea kiwanda cha kusindika vinywaji cha Hopaje kilichopo Nangurukuru Wilayani Kilwa, ambapo amesema Mheshimiwa Rais Samia ameendelea na utekelezaji wa sera ya viwanda na kuvutia wawekezaji ili kukuza uchumi kwa kuweka mazingira bora ya uwekezaji.

MIONGOZO ADA ZA UKUSANYAJI TOZO ZA UMWAGILIAJI WAKAMILIKA

$
0
0

 Na Mwandishi Wetu – Dodoma


Katika kutekeleza agizo la Serikali linalowataka wakulima wote wanaojishughulisha na shughuli za kilimo cha umwagiliaji kuachangia asilimia tano katika mfuko wa maendeleo ya kilimo cha Umwagiliaji, Tume ya taifa ya Umwagiliaji imekamilisha Miongozo kanuni na taratibu za ukusanyaji wa tozo za Kilimo cha Umwagiliaji.

Hayo yamesemwa Mapema Leo jijini Dodoma na Kaimu Mkurugenzi mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Daudi Kaali alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake.

Bw. Kaali alisema mapema mwezi July Mwaka huu Serikali kupitia Waziri wa Fedha ilitoa agizo ya wakulima waliyopo katika skimu za kilimo cha umwagiliaji kuchangia asilimia tano kwa kila hekta na fedha hizi ziingizwe katika mfuko wa umwagiliaji kwa ajili ya kugharamia matunzo, matengenezo pamoja na uendeshaji wa skimu za kilimo cha umwagiliaji.

Aidha Mkurugenzi Kaali amesema kuanzia mwezi huu wa kumi Tume ya Taifa ya Umwagiliaji inaanza kampeni maalum ya kutoa elimu kuhamasisha wananchi mbali mbali wachangie watoe hizi ada kwa ajili a kuendeleza kilimo cha umwagiliaji, “Hivyo watumishi mbalimbali kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji na viongozi mbali mbali wa serikali watakwenda katika maeneo mbalimbali ya nchi,kwa ajili ya kuelemisha na kuhamasisha utoaji wa ada hizi za umwagiliaji.” Alisema Kaali

Bw. Kaali wamewaasa wakulima wanaojihusisha na kilimo cha Umwgiliaji kuchangia ada za umwagiliji kwani amesema ni fursa nzuri ssaa ambayo imetolewa na Serikali kuchangia fedha katika mfuko wa umwagiliaji ili kuweza kutatua changamoto kubwa katika skimu mbalimbali hapa nchini.

Kwa pande wake Kaimu Mkurugenzi uendeshaji Bwana Enterbet Nyoni amesema katika skimu za kilimo cha umwagiliaji zisozendelezwa mgawanyo wa Ada ya tozo ya asilimia tano ya tozo, utahusisha asilimia sabini na tano (75%) kubakia katika skimu husika na asilimia ishirini na tano (25%) itakwenda katika mfuko wa maendeleo ya kilimo cha umwagiliaji


Kaimu Mkurugenzi Mkuu Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Daudi Kaali akizungumza na waandishi wa Habari Ofisini kwake jijini Dodoma kuhusiana na uchangiaji wa Tozo katika sekta ya Kilimo cha Umwagiliaji.

SERIKALI HAITOWAVUMILIA WATUMISHI WA UMMA WATAKAOSHINDWA KUTIMIZA WAJIBU

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mtakatifu Martin ya Kipatimu wilayani Kilwa, Dkt. Christina Kasyama (kulia) kuhusu mashine ya X-ray wakati alipotembelea hospitali hiyo
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wauguzi wa Hospitali ya Mtakatifu Martin ya Kipatimu wilayani Kilwa wakati alipoitembelea, Oktoba 6, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan haitawavumilia watumishi wa umma watakaoshindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

“…Rais anahitaji kuona watumishi wa umma wakifanya kazi kwa weledi na kwa kuzingatia maadili. Pia anataka kuona watumishi wakiwafuata wananchi katika maeneo yao ya makazi na kusikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi.”

Ameyasema hayo leo (Jumatano, Oktoba 6, 2021) wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Kipatimu wilayani Kilwa baada ya kutembelea Hosptali ya Mission ya Kipatimu akiwa kwenye ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo mkoani Lindi.

Mheshimiwa Majaliwa amewataka watumishi hao wahakikishe wanatekeleza majukumu yao ya kuwahudumia wananchi kwa kufuata taratibu zilizowekwa pamoja na kusimamia vizuri fedha za miradi ya maendeleo zinazopelekwa katika maeneo yao.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Dkt. Kheri Kagya ahakikishe mtaalamu wa X-ray anapelekwa katika Hosptali ya Mtakatifu Martin iliyopo Kipatimu ili kuwapunguzia wananchi wa maeneo hayo kutembea umbali mrefu kufuata huduma hiyo.

Ametoa agizo hilo baada ya uongozi wa hospitali hiyo ambayo inaendeshwa kwa ushirikiano kati ya Serikali na Kanisa Katoliki kumueleza Waziri Mkuu kwamba hospitali hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya ukosefu wa mtaalamu wa X-ray licha ya kuwa na kifaa hicho.

Pia, Waziri Mkuu amemuagiza Dkt. Kagya ahakikishe hospitali hiyo ambayo kwa sasa ina daktari mmoja iongezewe daktari mwingine ili kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi.

Awali, Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt. Christina Kasyama alisema hospitali hiyo ambayo inamilikiwa na Jimbo Katoliki la Lindi inafanya kazi kwa ushirikiano na Serikali kupitia mkataba wa huduma (PPP) na inahudumia wakazi takribani 50,000 wa Kilwa Kaskazini na maeneo ya jirani.

TANZANIA NA BENKI YA KIARABU WASAINI MKATABA WA UJENZI WA BARABARA YA ZANZIBAR

$
0
0
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Kiarabu ya Maendeleo ya Kiuchumi Afrika (BADEA), Dkt. Sidi Ould Tah, wakisaini marekebisho ya mkataba wa Mradi wa Bararaba ya Wete – Chake Chake, Pemba katika hafla iliyofanyika, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Kiarabu ya Maendeleo ya Kiuchumi Afrika (BADEA), Dkt. Sidi Ould Tah, wakionesha marekebisho ya mkataba wa Mradi wa Bararaba ya Wete hadi Chake Chake, Pemba baada ya kusainiwa katika hafla iliyofanyika, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akimsindikiza Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Kiarabu ya Maendeleo ya Kiuchumi Afrika (BADEA), Dkt. Sidi Ould Tah, baada ya kumaliza hafla ya utiaji saini marekebisho ya mkataba wa mradi wa bararaba ya Wete hadi Chake Chake, Pemba iliyofanyika, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Kiarabu ya Maendeleo ya Kiuchumi Afrika (BADEA), Dkt. Sidi Ould Tah, baada ya kumaliza hafla ya utiaji saini wa marekebisho ya mkataba wa mradi wa bararaba ya Wete hadi Chake Chake, Pemba iliyofanyika, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Kiarabu ya Maendeleo ya Kiuchumi Afrika (BADEA), Dkt. Sidi Ould Tah, zawadi ya picha ya Mlima Kilimanjaro ikiwa na baadhi ya Wanyama, baada ya kumaliza hafla ya utiaji saini wa marekebisho ya mkataba wa Mradi wa Bararaba ya Wete hadi Chake Chake, Pemba iliyofanyika jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Kiarabu ya Maendeleo ya Kiuchumi Afrika (BADEA), Dkt. Sidi Ould Tah, baada ya kumaliza hafla ya utiaji saini wa marekebisho ya mkataba wa Mradi wa Bararaba ya Wete hadi Chake Chake, Pemba iliyofanyika jijini Dodoma.

(Picha na WFM – Dodoma)

WATAALAM KUFANYA TATHMINI KUBAINISHA MIPAKA PORI LA AKIBA MKUNGUNERO

$
0
0
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza na wakazi wa kijiji cha Bereko wilayani Kondoa mkoa Dodoma wakati wa ziara ya mawaziri wa kisekta kutafuta ufumbuzi wa migogoro ya ardhi kwenye maeneo ya hifadhi.
Sehemu ya wananchi wa Bereko wilayani Kondoa mkoa wa Dodoma wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Mawaziri wa kisekta wakati wa ziara ya kutafuta ufumbuzi wa migogoro ya ardhi kwenye maeneo ya hifadhi.
Mbunge wa Jimbo la Kandoa ambaye ni Waziri wa Habari, Mwasiliano na Teknolojia Dkt Ashatu Kijaji akizungumza wakati wa ziara ya mawaziri wa kisekta kutafuta ufumbuzi wa migogoro ya ardhi katika maeneo ya hifadhi kwenye kijiji cha Bereko wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mery Masanja akizungumza na wananchi wa Bereko wilayani Kondoa mkoa Dodoma wakati wa ziara ya mawaziri wa kisekta kutafuta ufumbuzi wa migogoro ya ardhi katika maeneo ya hifadhi.
Picha inayoonesha eneo la Pori la Akiba la Mkungunero kwenye kijiji cha Bereko wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma.

Na Munir Shemweta, WANMM KONDOA

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amesema timu ya wataalamu itapelekwa katika Pori la Akiba la Mkungunero lililopo wilayani Kondoa mkoa wa Dodoma kufanya tathmini na kuweka mipaka upya kwa lengo la kuepusha kuvamiwa.

Waziri Lukuvi alibainisha hayo tarehe 6 oktoba 2021 wilayani Kondoa mkoani Dodoma wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Bereko akiwa katika ziara ya Mawaziri wa kisekta ya kutoa mrejesho wa utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 920.

“Katika Pori la Akiba la Mkungunero tutafanya tathmini upya na kuweka mipaka upya ili wananchi wajue eneo lililohifadhiwa linaanzia wapi na linaishia wapi” alisema Lukuvi.

Kwa mujibu wa Waziri Lukuvi, baada ya kufanyika tathmini upya na mipaka kupimwa hatarajii kuona wananchi wakivamia maeneo ya hifadhi na mapori ya akiba na kueleza kuwa, Rais Samia Suluhu Hassan ameamua kumaliza migogoro ya matumizi ya ardhi katika maeneo mbalimbali nchini.

Akielezea mgogoro wa matumizi ya ardhi eneo la Bereko wilayani Kondoa, Lukuvi alisema, eneo hilo halina mgogoro mkubwa ukilinganisha na maeneo mengine kwa kuwa mgogoro uliopo unaohusisha ekari 17.2 pekee.

Hata hivyo, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliwataka wakazi wa Bereko kujiepusha na tabia ya kuvamia maeneo ya vyanzo vya maji na kubainisha kuwa, serikali haitasita kuwaondoa watakaojenga kandokando ya mito.

Mapema Mbunge wa jimbo la Kondoa ambaye ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia Dkt. Ashatu Kijaji aliueleza ujumbe wa Mawaziri nane wa kisekta kuwa wananchi wa eneo la Bereko wana tatizo na msitu wa TFS kwenye mlima Salanka aliouleza kuwa mipaka yake imekuwa haitabiriki kutokana na kuhamahama.

“Msitu katika Mlima Salanka umekuwa kero na wananchi wanaumizwa, msitu una mipaka isiyotabirika kwa kuwa inahamahama na wakati mwingine inasogezwa kwenye mbaazi” alisema Dkt Ashatu.

Timu ya Mwaziri nane ikiongozwa na Waziri Lukuvi imemaliza ziara yake kwenye mkoa wa Dodoma katika wilaya ya Kondoa kwa kutembelea vijiji na mitaa kwenye pori la akiba la Swagaswaga na vijiji vilivyopo kinga la mita 500 katika pori la akiba la Mkungunero na baadaye kuelekea mkoa wa Manyara kuendelea na ziara ya kutoa mrejesho wa utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika maeneo ya hifadhi.

TANROADS YANG’ARA TUZO ZA TAASISI BORA ZA SERIKALI

$
0
0
Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), imeng’ara katika tuzo za taasisi bora za serikali kwa uwezeshaji wananchi kiuchumi baada ya kuwa mshindi wa kwanza na kutunukiwa tuzo na Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC).

TANROADS ilitunukiwa tuzo hiyo Jumatatu, Oktoba 4, 2021 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa katika Kongamano la tano la taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi, lililofanyika jijini Dodoma.

Tuzo hizo hutolewa na NEEC katika kila kongamano la Taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi, zikihusisha makundi mbalimbali yanayoshindania ambapo kwa mwaka huu, yalikuwepo makundi saba.

TANROADS ilishindania tuzo hiyo katika kundi la Taasisi za serikali, lililohusisha taasisi mbalimbali na kuibuka mshindi wa kwanza huku nafasi ya pili ikishikiliwa na Mamlakaya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA).

Utaratibu wa upatikanaji wa mshindi wa tuzo hiyo, kwa mwaka huu, ulihusisha uundwaji wa kamati ya kujitegemea iliyokuwa na wajumbe wanne kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu na TAMISEMI.

Vigezo vinavyohusishwa kushindania tuzo hizo ni kila mshindi anapaswa kupata alama zisizopungua 50 na katika kila kundi hupatikana mshindi wa kwanza, wa pili na mshindiwa tatu.

Kila kundi huwa na washindani watano na ushindani hufanyika kwa kuzingatia vigezo.

Makundi yaliyokuwepo katika tuzo za mwaka huu ni kundi la Mikoa, Wizara, Taasisi za Serikali, Mifuko ya Kijamii, Programu za uwezeshaji, taasisi zilizoshirikiana kutekeleza programu za Baraza, Wajasiriamali na Asasi za kiraia.

TANROADS imekuwa taasisi ya mfano kwa uwezeshaji wananchi kiuchumi kutokana na umahiri katika utekelezaji wa majukumu yake, yakiwemo ya ujenzi wa barabarazinazounganisha Mikoa ambapo miradi inayotekelezwa imeleta faida nyingi za kiuchumi, kijamii na kibiashara kwa wananchi.

Serikali baada ya kuridhika na ufanisi wa TANROADS iliongeza jukumu la ujenzi wa viwanja vya ndege, hatua ambayo imefikiwa baada ya serikali kuamini ufanisi mkubwa wa TANROADS katika miradi ya ujenzi wa Barabara na Madaraja nchini.

Kuongezwa kwa jukumu hilo, ni kielelezo halisi cha utendaji bora na ufanisi wa TANROADS katika kazi ambazo kimsingi zinabeba dhima ya kuhudumia wananchi.

AKAMATWA NA SILAHA AINA YA RIFLE INAYODHANIWA KUTUMIKA KWENYE UJANGILI-ACP MALULU

$
0
0

Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
JESHI la polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji , linamshikilia mtuhumiwa mmoja jina linahifadhiwa ,kwa kukutwa na silaha aina ya Rifle yenye no.373 inayodhaniwa kutumika kwenye matukio ya ujangili.

Kamanda wa polisi Mkoa wa kipolisi Rufiji ACP Kungu Malulu alithibitisha ,kukamatwa kwa mtu huyo, huko katika Kijiji cha Mwangaei Kibata kata ya Kitamba Tarafa ya Kipatimu wilaya ya Kilwa mkoa wa Lindi wakati askari polisi mkoa wa Kipolisi Rufiji kwa kushirikiana na kikosi cha kuzuia na kupambana na ujangili nchini wakiwa katika msako.

“Walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja mwanaume mwenye umri wa miaka 43,mkulima mkazi wa Mwangei akiwa na silaha aina ya Rifle yenye no 373 ambayo alikuwa akimiliki kinyume cha sheria na kutumia katika ujangili.”
Katika hatua nyingine Kamanda Malulu alisema ,walimkamata mtuhumiwa mmoja mwanaume akiwa na silaha aina ya Gobore alilokuwa kaliticha juu ya dali la nyumba yake ,katika kijiji Kitembo wilayani Kibiti .
Hata hivyo ,wamewakamata watuhumiwa wengine wawili wakazi wa Dar es Salaam wanaume ,wakisafirisha viroba vitano vinavyodhaniwa kuwa ni madawa ya kulevya aina ya bangi yenye uzito wa kg 130 .

“Watuhumiwa hawa walikuwa wakitumia gari aina ya T 559BJL Toyota Corona watuhumiwa wote wanahojiwa kwa upelelezi na watafikishwa mahakamani”

Kungu Malulu alisema ,watuhumiwa wote majina yanahifadhiwa kutokana na sababu za kiupelelezi.

Kufuatia matukio hayo ,Malulu alitoa wito kwa wananchi ,kuzingatia taratibu za kumiliki silaha bila kutumia pasipo uhalali na wale wanaomiliki kihalali wahakikishe wanazingatia matumizi sahihi ya silaha zao.

WAZIRI MAKAMBA AANZA KUTEKELEZA AGIZO LA MAKAMU WA RAIS MKOANI KIGOMA

$
0
0
Waziri wa Nishati, January Makamba akiwa katika chumba cha kuongozea mitambo ya umeme katika Kituo cha kuzalisha umeme kilichopo Kigoma mjini tarehe 06 Oktoba, 2021. Kushoto kwa Waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Ester Mahawe.
Waziri wa Nishati, January Makamba (Wa Tatu kutoka kulia) akitazama moja ya mitambo ya kuzalisha umeme katika Kituo cha kuzalisha umeme kilichopo wilayani Kasulu mkoa wa Kigoma tarehe 06 Oktoba, 2021. Kushoto kwa Waziri ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji (Uzalishaji) kutoka TANESCO, Mhandisi Pakaya Mtamakaya.
Waziri wa Nishati, January Makamba (Wa Tatu kutoka kulia) akiwa katika kituo cha kuzalisha umeme kwa kutumia Jua wilayani Kigoma Mkoa wa Kigoma kinachomilikiwa na kampuni ya Nextgen Solawazi. Kulia kwa Waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Ester Mahawe. Wengine katika picha ni Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Maharage Chande (wa kwanza Kushoto), na Wa Pili kutoka kushoto ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji (Uzalishaji) kutoka TANESCO, Mhandisi Pakaya Mtamakaya.
Waziri wa Nishati, January Makamba akizungumza na Wataalam kutoka TANESCO wanaofanya kazi katika Kituo cha kuzalisha umeme kilichopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma wakati alipofika mkoani humo kutatua changamoto ya upatikanaji umeme wa uhakika.
Waziri wa Nishati, January Makamba (Wa Pili kushoto) akitazama baadhi ya mitambo ya umeme katika Kituo cha kuzalisha umeme kilichopo wilayani Kasulu mkoa wa Kigoma tarehe 06 Oktoba, 2021. Kushoto kwa Waziri ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji (Uzalishaji) kutoka TANESCO, Mhandisi Pakaya Mtamakaya na kulia kwa Waziri ni Mkuu wa Kituo cha umeme cha Kasulu, Masanja Nkuba.

Na Teresia Mhagama, Kigoma

Waziri wa Nishati, January Makamba ameanza kutekeleza agizo lililotolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Philip Mpango tarehe 22 Septemba 2021 la kutatua changamoto ya kukatika umeme mara kwa mara mkoani Kigoma.

Katika ziara yake ya kikazi mkoani Kigoma aliyoifanya tarehe 06 Oktoba 2021, Waziri Makamba alibainisha kuwa, kuna mipango ya muda mfupi, kati na mrefu ambayo inalenga kuhakikisha kuwa Mkoa wa Kigoma unakuwa na umeme wa uhakika na hivyo kuondoa kero hiyo ya umeme kukatika mara kwa mara.

Alibainisha kuwa, katika mipango ya muda mfupi, Kituo cha umeme cha Kigoma chenye uwezo wa megawati 6.25 kitaongezewa mashine mbili zitakazozalisha jumla ya megawati 2.5 kwenye kituo husika ambapo mashine ya kwanza yenye uwezo wa megawati 1.25 itakamilika kufungwa tarehe 15 Novemba 2021.

Aliongeza kuwa, mashine ya pili yenye uwezo wa megawati 1.25 itafungwa na kukamilika tarehe 25 Novemba 2021.

Aidha, alieleza kuwa miradi ya muda wa kati na mrefu itaunganisha Kigoma na umeme wa gridi na kupelekea Mkoa huo kuwa na umeme mwingi na wa bei nafuu kwani kwa sasa Kigoma inatumia umeme unaotokana na mafuta na hivyo inatumia shilingi Bilioni 3 kwa mwezi kuzalisha nishati hiyo huku mapato yakiwa ni shilingi bilioni 1.5.

Miradi hiyo ya muda wa kati na mrefu itakayounganisha Kigoma na gridi ya Taifa ni ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme itakayotoka Nyakanazi-Kakonko hadi Kibondo itakayokamilika Machi 2022

Mradi mwingine ni ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kV 132 kutoka Tabora hadi Kigoma ambayo inatarajiwa kukamilika Oktoba 2022.

Aidha, mradi mwingine ni ujenzi wa njia kubwa ya umeme ya msongo wa kV 400 kutoka Nyakanazi hadi Kigoma ambapo utekelezaji wa mradi huo unatarajiwa kukamilika mwaka 2023

Vilevile mradi mwingine wa umeme unaotarajiwa kuboresha hali ya umeme mkoani Kigoma ni mradi wa kufua umeme wa maji wa Malagarasi utakaozalisha megawati 49.5 na Serikali imeshapata fedha kutoka Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) na mwakani atatafutwa mkandarasi kwa ajili ya ujenzi.

Akiwa mkoani Kigoma, Waziri Makamba alikagua mitambo ya kuzalisha umeme iliyopo wilayani Kigoma pamoja na wilayani Kasulu ambapo akiwa wilayani Kasulu alikuta changamoto ya mitaa mingi kukosa umeme ambapo ili kutatua changamoto hiyo alieleza kwamba utafanyika utaratibu ndani ya Wizara ili kuiwezesha TANESCO kupeleka umeme kwenye mitaa hiyo.

Katika hatua nyingine, Waziri wa Nishati alitembelea kituo cha umeme wa Jua cha Nextgen Solawazi ambacho kwa sasa kinazalisha umeme wa kiasi cha megawati 1.8 na kupeleka kwenye kituo cha kuzalisha umeme cha TANESCO ambapo kampuni hiyo ya Nextgen inatarajia kuongeza uzalishaji na kufikia megawati 4.3 ifikapo tarehe 8 Oktoba 2021.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa TANESCO, Maharage Chande, alisema kuwa, Mkoa wa Kigoma utaanza kupata umeme wa gridi ya Taifa ifikapo Machi 2022.

Katika ziara hiyo Waziri wa Nishati aliambatana na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Kigoma wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Ester Mahawe ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Kigoma.

RAIS DKT.MWINYI AONGOZA MAPOKEZI YA NDEGE MPYA ZA SHIRIKA LA NDEGE TANZANIA ATCL

$
0
0


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akifuatana wasaidizi wake baada ya kumalizika kwa hafla ya sherehe ya mapokezi ya Ndege 2 Mpya za Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) wakati wa mapokezi rasmi zilipowasili leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar . [Picha na Ikulu] 08/10/2021.
Ndege 2 za Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) zikimwagiwa maji kama ishara ya kupata baraka zilipowasili leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, ambapo mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi(hayupo pichani).[Picha na Ikulu] 08/10/2021.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi alipokuwa akitoa hutuba yake katika hafla ya mapokezi ya Ndege 2 mpya za Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibarzilizowasili leo,ambapo Viongozi mbali mbali wa Serikali wamehudhuria akiwepo na Waziri Mkuu wa wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Majaliwa Kassim Majaliwa. [Picha na Ikulu] 08/10/2021.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akisalimiana na Marubani wa Ndege Mpya za Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) wakati wa mapokezi rasmi zilipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar leo [Picha na Ikulu] 08/10/2021.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akisalimiana na Wahudumu wa Ndege Mpya za Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) wakati wa mapokezi rasmi zilipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar leo [Picha na Ikulu] 08/10/2021.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa mgeni rasmin na Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Majaliwa Kassim Majaliwa (katikati) pamoja na Viongozi wengine wakisimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa katika hafla ya sherehe ya mapokezi ya Ndege 2 mpya za Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani karume Zanzibar leo [Picha na Ikulu] 08/10/2021.

RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI MBALIMBALI, SENGATI ATENGULIWA

WAZIRI MCHENGERWA AWATAKA WATUMISHI KUZINGATIA MWONGOZO WA MAVAZI KWA WATUMISHI WA UMMA MAHALA PA KAZI

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akisalimiana na Watendaji na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Simiyu alipowasili katika mkoani humo kwa ziara yake ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji kwa Watumishi wa Umma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akizungumza na Watendaji na Watumishi wa Mkoa wa Simiyu alipowasili katika Mkoa huo kwa ziara yake ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji kwa Watumishi wa Umma.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. David Kafulila akiwasilisha taarifa ya utekelezaji ya Mkoa wake kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya Mhe. Mchengerwa ya kuhimiza uwajibikaji kwa Watumishi wa Umma mkoani Simiyu.
Mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima, Bw. Haruna Taratibu akiwasilisha hoja ya kiutumishi kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. 

Na. James K. Mwanamyoto-Bariadi

Tarehe 08 Oktoba, 2021

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa amewataka Watumishi wa Umma nchini kuzingatia Mwongozo wa Mavazi kwa Watumishi wa Umma kwa mujibu wa Waraka wa Utumishi wa Umma Na.6 wa Mwaka 2020 wanapokuwa mahala pa kazi wakitekeleza majukumu yao.

Mhe. Mchengerwa ametoa wito huo leo mkoani Simiyu alipokuwa akizungumza na Watumishi wa Umma wa Mkoa huo, wakati wa ziara yake ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji kwa Watumishi wa Umma mkoani humo.

Mhe. Mchengerwa amesema, kuna baadhi ya Watumishi wa Umma katika taasisi mbalimbali za umma hawazingatii Mwongozo huo, na badala yake wanavaa mavazi yasiyostahili sehemu za kazi.

“Nawataka Watumishi wote wa Umma nchini kuzingatia Mwongozo wa Mavazi kwa Watumishi wa Umma kwa mujibu wa Waraka wa Utumishi wa Umma Na.6 wa Mwaka 2020 wanapokuwa katika utekelezaji wa majukumu yao kwani kuna baadhi ya Watumishi hawauzingatii Mwongozo huu na kuvaa wanavyojisikia wao, jambo hili sitaki kuliona,” Mhe. Mchengerwa amesisitiza.

Mhe. Mchengerwa ameainisha kuwa, mwongozo huo unafafanua aina ya mavazi yanayoruhusiwa na yasiyoruhusiwa kuvaliwa na Mtumishi wa Umma kulingana na eneo alilopo wakati akitekeleza majukumu yake.

Aidha, Mhe. Mchengerwa amewasisitiza watumishi kuacha matumizi ya simu wanapowahudumia wateja kwani kwa kufanya hivyo wanawakatisha tamaa wananchi wanaofuata huduma na kuijengea taswira mbaya Serikali kwa wananchi wake.

“Kuna baadhi ya watumishi wamekuwa wakitumia simu na hata wakiona wateja bado wanaendelea kufanya hivyo badala ya kuwahudumia, ninawataka muache tabia hiyo mara moja, tufanye kazi kwa weledi, tujitoe kwa ajili ya wananchi, tuwasilikilize wananchi wanapofuata huduma, tuwajali maana nchi hii ni yao na tupo kazini kwa ajili yao,” Mhe. Mchengerwa amesisitiza.

Mhe. Mchengerwa yuko Mkoani Simiyu kwenye ziara ya kikazi ya siku mbili kuhimiza uwajibikaji kwa Watumishi wa Umma na kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF akitokea Mkoani Mwanza na Mara.
Viewing all 45984 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>