Quantcast
Channel: VIJIMAMBO
Viewing all 45984 articles
Browse latest View live

OCEAN ROAD YAPOKEA MSAADA WA VITANDA VINAVYOTUMIA UMEME

$
0
0
Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) ya jijini Dar es Salaam imepokea msaada wa vitanda viwili (2) vya umeme kutoka nchi ya Jamhuri ya Muungano wa Czech wakishirikiana na kampuni ya Gama Pharmaceutical kwaajili ya kumsaidia mgonjwa na muuguzi bila kutumia nguvu.

Akizungumza mara aada ya kupokea msaada huo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani (ORCI), Dkt.Julius Mwaiselage jijini Dar es Salaam leo Oktoba 07, 2021 amesema kuwa msaada walioutoa Serikali ya jamuhuri ya Czech ni dola 8000 ambazio ni sawa na shilingi milioni 18.

Dkt. Mwaiselage amesema kuwa mahitaji ya taasisi hiyo ni vitanda 25 vinavyotumi umeme au vya kieletrniki, vilivyokuwepo ni 8 sasa huku bado kuna mahitaji ya vitanda vingine 17 ili kutimia 25.

“Mahitaji ya vitanda hivi vinavyotumia umeme ni 25 sasa tuanavyo 8 tunahitaji vitanda vingine 17 vinavyotumia umeme, vitanda vingine vipo lakini sio vya umeme.” Amesema Dkt. Mwaiselage

Hata hivyo Dkt. Mwaiselage ameiomba kampuni ya kitanzania ya Gama Pharmaceutical iliyoshirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Czech kusaidia kupata vitanda vingine 17 ili kuendelea kutoa huduma inastahili kwa wagonjwa hospitalini hapo.

Amesema kuwa vitanda hivyo vinahitajika Zaidi katika hospitali hiyo kwani wagonjwa wa Saratani wameongezeka nchini kwa asilimia 60 hadi 70 wanaenda hospitali wakiwa na hali mbaya hadi hawawezi kutembea, hivyo vitanda hivyo vinaweza kufanya kazi nyingi vyenyewe vitakuwa ni mhimu zaidi.

Dkt.Mwaiselage amesema kuwa vitanda hivyo vitatumia umeme kwaajili ya kumpandisha mgonjwa juu au chini, vinabinuka kulingana na inavyotakiwa na Muuguzi.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Magonjwa yasiyoambukiza kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Omary Ubuguyu amesema kuwa vitanda vinavyotumia umeme vinahitajika Zaidi katika hospitali zinazotoa huduma ya dharura, sehemu ambazo zinatolewa huduma za wagonjwa mahututi.

TANZANIA, CZECH ZAAHIDI KUIMARISHA BIASHARA NA UWEKEZAJI

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Czech Mhe. Miloslav Staŝek akiongea na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) wakati walipokutana leo kwa mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) akimueleza jambo Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Czech Mhe. Miloslav Staŝek wakati walipokutana leo kwa mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Majadiliano baina ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Czech Mhe. Miloslav Staŝek akiongea na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) yakiendelea wakati wa mazungumzo leo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Czech Mhe. Miloslav Staŝek akiongea akipokea zawadi ya picha ya Mlima Kilimanjaro kutoka kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) leo Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Czech Mhe. Miloslav Staŝek katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) leo Jijini Dar es Salaam

Na Mwandishi wetu, Dar

Katika jitihada za kukuza na kuendeleza diplomasia ya uchumi, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Czech zimeahidi kukuza na kuimarisha sekta ya biashara na uwekezaji.

Ahadi hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Czech Mhe. Miloslav Staŝek wakati alipokutana kwa mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk leo katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.

Mhe. STAŜEK amesema kuwa wamejadili masuala mbalimbali ya kukuza na kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Czech hasa katika sekta ya biashara na uwekezaji wa viwanda hapa nchini………..”na leo nimeambatana na wafanyabiashara mbalimbali kutoka Czech ambao wamekuja kuangalia fursa za biashara zinazopatikana hapa Tanzania” amesema Mhe. Staŝek.

“Pia tunajitahidi kuleta teknolojia mpya hapa Tanzania kuinua uchumi, ambapo tunaamini itasaidia kutangaza fursa mbalimbali katika sekta ya biashara na uwekezaji,” Ameongeza Mhe. Staŝek

Kwa Upande wake, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk amesema katika mazungumzo yake na Waziri wa Jamhuri wa Czech Mhe. Staŝek yamejikita zaidi katika kukuza uhusiano wa uchumi hasa masuala ya biashara na uwekezaji.

Leo Mhe. Waziri ameambata na ujumbe wa wafanyabiashara waliokuja kujione fursa mbalimbali hapa nchini ili kuinua sekta ya biashara na uwekezaji…………..”leo pia watakuwa na mkutano ambao utawakutanisha na wafanyabiashara wa Tanzania ili kuona fursa za ushirikiano baina ya Tanzania na Czech,” Amesema Balozi Mbarouk.

“Tumeongelea suala la kuongeza uhusiano katika sekta ya elimu kwa kutoa fursa za masomo kwa wanafunzi wa Tanzania kwenda kusoma Czech ambapo wamekubali na kuahidi kuongeza nafasi za masomo kwa wanafunzi wa Tanzania ili kutoa fursa ya watanzania wengi kunufaika na elimu,” Ameongeza Balozi Mbarouk.

Pia viongozi hao wamejadili suala la kukuza sekta ya utalii hapa nchini ambapo Czech ipo katika mchakato wa kuanzisha safari ya ndege ya kuja Tanzania moja kwa moja ili kukuza na kutangaza Utalii lakini pia kukuza biashara kwa maslahi mapana ya pande zote mbili.

Kadhalika, Balozi Mbarouk amemuahidi Mhe. Staŝek kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kuhakikisha inalinda na kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia uliopo baina yake na Jamhuri ya Czech kwa kuwa uhusiano wa mataifa hayo mawili ni wa muda mrefu na wenye maslahi ya mataifa yote mawili.

UBA EXPANDS ON ITS SERVICES, CUSTOMER SERVICE WEEK.

$
0
0

 

 Being a special celebration of the year,” United Bank for Africa (UBA) Tanzania joins the rest of the world in celebrating Customer Service Week themed “The Power of Service” aiming at celebrating the importance of customer service and the people who offer best services to customers amidst the pandemic on a daily basis.

In line with the theme “The power of service” branches engaged with customers by delivering high quality customer experience as the bank is committed to consistently go an extra mile in delighting the customers at every interaction.

It is at this period where the bank collects feedback from the customers to measure satisfaction in order to improve the quality of products and services offered towards meeting their expectations and create a happy experience.

Marking the end of Customer Service Week, UBA Chief Operation Officer, Flavia Kiyanga expressed her sincere gratitude to customers for the opportunity to bank and serve them with trust.

This was accompanied by awarding appreciation certificates to customers to keep connecting and strengthening the level of commitment for business growth.

Flavia said that, “as we continue the engagement with our customers, UBA has been investing in expanding the bank network to bring services closer to our customers by opening Mwanza and Kijitonyama branches to cater customers need in line with their expectations, because our number one goal is excellent services.”

“We remain grateful to our customers, we promise to continue to win their hearts and minds and strive to expand our branch network further to other parts of the country but also constantly innovate and improve our digital banking channels to adopt to the change in times and consumer tastes and make banking part of our customer’s lifestyle by ensuring convenience and secured transaction anytime, anywhere.”

Speaking during the event also, Head Marketing and corporate communication Ms. Brendansia Kileo said; “UBA is driven by excellent core values that gears towards customer service thus; Excellence, Execution and Enterprise and a very firm customer first Philosophy that trains every staff from the executive level to junior levels on the importance of excellent customer service. Apart from that UBA has invested heavily on seamless digital solutions that are user friendly, fast, secured and convenient to ensure customers are delighted at every interaction.”

UBA anticipates in improving customers’ perceptions by treating them with respect and always listen with intent to serve and resolve.

Our customers always come first.

UBA Tanzania Chief Operation Officer Flavia Kiyanga serves one of the banks long serving customer Mohsin Somji as way of celebrating customers service week.

TUME YA TAIFA YA UMWAGILIAJI YANADI TOZO ZA UMWAGILIAJI KATIKA MAONESHO, KUELEKEA KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI.

$
0
0

 

Na Mwandishi Wetu – Moshi

Ushiriki wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji katika maonesho yanayofanyika mjini Moshi kuelekea maadhimisho ya siku ya chakula Duniani, yameipa fursa ofisi hiyo kunadi sera zake kwa wananchi zinazowataka kisheria wakulima, kulipa tozo za kilimo cha umwagiliaji.

Akizungumza na baadhi na wananchi waliotembelea banda la taasisi hiyo, Bw. Mohamed Mcheni Afisa Kilimo Mwandamizi amesema kuwa, taratibu zote za ukusanyaji wa ada umekamilika  na kutangazwa katika gazeti la serikali, “Kwa mwaka huu wa fedha na miaka inayoendelea tutaendelea kukusanya asilimia tano (5%), na kabla ya kulipa, skimu inatakiwa isajiliwe.” Alisisitiza.

Aidha, Bw. Mcheni alisema kuwa Asilimia tano hiyo ni sawa na wastani wa gunia moja kwa hekari kwa zao la mpunga na aliendelea kufafanua kuwa, chama cha wakulima katika skimu za kilimo cha umwagiliaji zinatakiwa kulipa ada ya usajili kiasi cha shilingi laki moja na elfu sabini na tano (175,000/-) ambapo shilingi laki moja ni ada ya mwaka na shilingi elfu sitini ni ada ya usajili, na shilingi elfu kumi na tano ni ada ya maombi ya usajili.

Alitoa wito kwa wakulima kulipa ada ya asilimia tano (5%) ya wastani wa mavuno kwa msimu wa mwaka kwa hekari.

Maonesho kuelekea maadhimisho ya kilele cha siku ya Chakula Duniani yenye kauli mbiu unayosema inayosema  “Zingatia Uzalishaji na Mazingira Endelevu kwa lishe na Maisha Bora” yanafanyika Mjini Moshi mkoani Kilimanjaro katika kiwanja cha shule ya msingi Mandela.

kushoto Afisa Mazingira kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bi Christina Mwasaka akifafanua jambo kwenye kipeperushi kwa washiriki wa Ofisi hiyo katika Banda, ndani ya Maonesho yanayoendelea Mjini Moshi katika viwanja vya shule ya Msingi Mandela, kuelekekea maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani.

Afisa Kilimo Mwandamizi kutoka Idara ya Uendeshaji Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Mohamed Mcheni, akifafanua Jambo kwa waandishi wa Habari hawapo katika picha, kwenye maonesho yanayoendelea mjini Moshi kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya chakula Duniani.




BALOZI MBAROUK ATETA NA DKT. MATHUKI

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassoro Mbarouk (Mb) amekutana kwa mazungumzo na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dkt. Peter Mathuki leo katika Ofisi za Jumuiya hiyo leo Jijini Arusha.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassoro Mbarouk (Mb) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dkt. Peter Mathuki leo katika Ofisi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, Jijini Arusha
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassoro Mbarouk (Mb) akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dkt. Peter Mathuki leo katika Ofisi za Jumuiya hiyo Jijini Arusha.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dkt. Peter Mathuki akimueleza jambo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassoro Mbarouk (Mb) leo katika Ofisi za Jumuiya hiyo Jijini Arusha.


RAIS SAMIA AHUTUBIA TAIFA KILELE CHA MBIO ZA MWENGE CHATO

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akilihutubia Taifa kwenye kilele cha mbio za Mwenge Maalum wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021 zilizofanyika leo Oktoba 14,2021 katika Uwanja wa Magufuli Wilayani Chato Mkoani Geita.

PICHA NA IKULU

KURUDI KWA MV VICTORIA MKOANI KAGERA KWA WANUFAISHA WAFANYA BIASHARA

$
0
0
Na Silvia Mchuruza,Bukoba, Kagera.

Kufuatia kurudi kwa meli ya Mv Victoria Baadhi ya wafanyabiashara mkoani Kagera wamesema walipiti kipindi kigumu cha kusafirisha bidhaa kutoka mkoani humo kwenda mkoa wa Mwanza kutokana na meli ya NEW MV VICTORIA HAPA KAZI TU kusitisha safari zake kwaajiri ya kufanyiwa matengenezo.

Akizungumza na Fullshangwe Blog Bwana Amri Athuman mfanya biashara wa ndizi, palachichi pamoja na mazao mbalimbali kutoka Bukoba kwenda Mwanza alisema kurudi kwa Mv Victoria itawasaidi sana kuepukana na gharama kubwa walizokuwa wakitumia kipindi meli hiyo ipo kwenye matengenezo.

“ Kukosekana kwa meli hii imepelekea sisi kama wafanyabiashara kutumia gharama kubwa kusafirisha bidhaa zetu kutoka Kagera kwenda Mwanza kwani tumekuwa tukitumia usafiri wa maroli ambavyo ukiangalia gharama zake nikubwa ukilinganisha na gharama za meli katika sualazima la usafirishaji”.

Nae mkuu wa mkoa wa kagera Meja Jenerali Charles Mbuge amesema kuwa safari za meli hiyo inayofanya safari zake kati ya Bukoba na Mwanza itarejea rasmi Octor 15 mwaka huu.

Kauli ameitoa jana akiwa ofisini wakati aluipokuwa akizungumza na waandishi wa habari na kuwataka wananchi sasa kuwa tayali kwa mapokezi mazuri ya meli hiyo.

“Meli ya NEW MV VICTORIA hapa kazi tu iliyositisha safari zake kwaajiri ya kufanyiwa matengenezo inatarajia kurejea Octoba 15 mwaka huu na itaanza safari zake kama kawaida”. Amesema Mbuge.

Hata hivyo ameongoza na kusema kuwa Ikumbukwe kuwa, meli ya NEW MV VICTORIA HAPA KAZI TU ilisitisha safari zake mnamo tarehe 27 septemba mwaka huu.

NAIBU WAZIRI MWANAIDI APOKEA MAGARI NA VIFAA KUTOKA MFUKO WA ABBOTT FUND KWA AJILI YA MAKAO YA TAIFA YA WATOTO KIKOMBO DODOMA

$
0
0
NAIBU Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Mwanaidi Ali Khamis,akiwasili katika Makao ya Taifa ya Watoto yaliyopo eneo la Kikombo nje kidogo ya jiji la Dodoma kwa ajili ya Kupokea Magari,Samani za Ofisi na Vifaa vya Tehama kutoka Mfuko wa ABBOTT FUND hafla iliyofanyika leo Oktoba 14,2021.
NAIBU Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Mwanaidi Ali Khamis,akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa (ABBOTT FUND) Tanzania Bi. Natalie Lebou wakati kukabidhiwa Magari,Samani za Ofisi na Vifaa vya Tehama kutoka Mfuko wa ABBOTT FUND hafla iliyofanyika leo Oktoba 14,2021 katika Makao ya Taifa ya Watoto yaliyopo eneo la Kikombo nje kidogo ya jiji la Dodoma.
NAIBU Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Mwanaidi Ali Khamis,akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhiwa Magari,Samani za Ofisi na Vifaa vya Tehama kutoka Mfuko wa ABBOTT FUND hafla iliyofanyika leo Oktoba 14,2021 katika Makao ya Taifa ya Watoto yaliyopo eneo la Kikombo nje kidogo ya jiji la Dodoma.
Kaimu Katibu Mkuu Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw.Patrick Golwike,akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya Magari,Samani za Ofisi na Vifaa vya Tehama kutoka Mfuko wa ABBOTT FUND hafla iliyofanyika leo Oktoba 14,2021 katika Makao ya Taifa ya Watoto yaliyopo eneo la Kikombo nje kidogo ya jiji la Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa (ABBOTT FUND) Tanzania Bi. Natalie Lebou,akieleza jinsi walivyoamua kukabidhi Magari,Samani za Ofisi na Vifaa vya Tehama katika Makao ya Taifa ya Watoto yaliyopo eneo la Kikombo nje kidogo ya jiji la Dodoma leo Oktoba 14,2021.
Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bw.Ikusubisya Kasebele,akiwatambulisha baadhi ya viongozi kutoka Wizara ya Afya wakati w makabidhiano ya Magari,Samani za Ofisi na Vifaa vya Tehama kutoka Mfuko wa ABBOTT FUND hafla iliyofanyika leo Oktoba 14,2021 katika Makao ya Taifa ya Watoto yaliyopo eneo la Kikombo nje kidogo ya jiji la Dodoma.
Baadhi ya washiriki pamoja na watoto wakifatilia hotuba mbalimbali wakati wa makabidhiano ya Magari,Samani za Ofisi na Vifaa vya Tehama kutoka Mfuko wa ABBOTT FUND hafla iliyofanyika leo Oktoba 14,2021 katika Makao ya Taifa ya Watoto yaliyopo eneo la Kikombo nje kidogo ya jiji la Dodoma.
NAIBU Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Mwanaidi Ali Khamis,akikata Keki wakati wa hafla ya makabidhiano ya Magari,Samani za Ofisi na Vifaa vya Tehama kutoka Mfuko wa ABBOTT FUND hafla iliyofanyika leo Oktoba 14,2021 katika Makao ya Taifa ya Watoto yaliyopo eneo la Kikombo nje kidogo ya jiji la Dodoma.
Watoto wanaoishi katika Makao ya Tsifa ya Watoto Kikombo wakitoa burudani wakati wa Makabidhiano hafla iliyofanyika leo Oktoba 14,2021.
NAIBU Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Mwanaidi Ali Khamis,akiwa katika picha na watoto mara baada ya hafla ya makabidhiano ya Magari,Samani za Ofisi na Vifaa vya Tehama kutoka Mfuko wa ABBOTT FUND hafla iliyofanyika leo Oktoba 14,2021 katika Makao ya Taifa ya Watoto yaliyopo eneo la Kikombo nje kidogo ya jiji la Dodoma.
NAIBU Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Mwanaidi Ali Khamis,akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa (ABBOTT FUND) Tanzania Bi. Natalie Lebou wakati wa makabidhiano ya Magari,Samani za Ofisi na Vifaa vya Tehama kutoka Mfuko wa ABBOTT FUND hafla iliyofanyika leo Oktoba 14,2021 katika Makao ya Taifa ya Watoto yaliyopo eneo la Kikombo nje kidogo ya jiji la Dodoma.
NAIBU Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Mwanaidi Ali Khamis,akikata utepe kuashiria makabidhiano ya Magari,Samani za Ofisi na Vifaa vya Tehama kutoka Mfuko wa ABBOTT FUND hafla iliyofanyika leo Oktoba 14,2021 katika Makao ya Taifa ya Watoto yaliyopo eneo la Kikombo nje kidogo ya jiji la Dodoma.
NAIBU Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Mwanaidi Ali Khamis,akiwa ndani ya gari mara baada ya kukabidhiwa na Mfuko wa ABBOTT FUND hafla iliyofanyika leo Oktoba 14,2021 katika Makao ya Taifa ya Watoto yaliyopo eneo la Kikombo nje kidogo ya jiji la Dodoma.
NAIBU Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Mwanaidi Ali Khamis na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa (ABBOTT FUND) Tanzania Bi. Natalie Lebou wakiwa ndani ya gari wakipongezana mara baada ya makabidhiano ya Magari,Samani za Ofisi na Vifaa vya Tehama kutoka Mfuko wa ABBOTT FUND hafla iliyofanyika leo Oktoba 14,2021 katika Makao ya Taifa ya Watoto yaliyopo eneo la Kikombo nje kidogo ya jiji la Dodoma.
Muonekano wa Magari,Samani za Ofisi na Vifaa vya Tehama yaliyotolwa na Mfuko wa ABBOTT FUND katika Makao ya Taifa ya Watoto yaliyopo eneo la Kikombo nje kidogo ya jiji la Dodoma hafla iliyofanyika leo Oktoba 14,2021.
NAIBU Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Mwanaidi Ali Khamis akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kituo cha Makao Makuu ya Taifa ya Watoto Kikombo baada ya makabidhiano ya Magari,Samani za Ofisi na Vifaa vya Tehama kutoka Mfuko wa ABBOTT FUND hafla iliyofanyika leo Oktoba 14,2021 katika Makao hayo .

Na.Alex Sonna,Dodoma

NAIBU Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Mwanaidi Ali Khamis amepokea magari,samani za ofisi na vifaa vya Tehama kwa ajili ya matumizi katika Makao ya Taifa ya Watoto Kikombo Mkoani Dodoma kutoka Mfuko wa (ABBOTT FUND).

Akizungumza leo Oktoba 14,2021 wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo katika Makao ya Taifa ya Watoto Kikombo Mkoani Dodoma,Naibu Waziri Mwanaidi amesema kupatikana kwa msaada wa magari mawili kwa ajili ya usafiri wa Watoto na Watumishi kutaondoa changamoto zilizokuwepo za Watoto kuchelewa kufika shuleni.

Amesema uwepo wa Samani za ofisi,mabwenini na zile za nyumba za watumishi zinadhihirisha wazi ubora wa Makao haya kwa Watoto na Walezi.

Aidha,Dawa na vifaa tiba katika Zahanati na vifaa vya TEHAMA vitaongeza tija katika kutoa huduma stahiki kwa Watoto kama ilivyokusudiwa.

“Hii inakwenda sambamba na dhamira ya Wizara na Serikali kwa ujumla ya kuhakikisha watoto wanaokumbwa na changamoto ya kupata maeneo ya kuishi wanahudumiwa ipasavyo kwa lengo la kuhakikisha wanapata ulinzi na usalama katika makuzi yao,”amesema Naibu Waziri Mwanaidi

Mwanaidi ameushukuru Mfuko wa Abbott kwa kutoa magari samani za ofisi na vifaa vya Tehama kwa ajili ya matumizi katika Makao ya Taifa ya Watoto Kikombo Mkoani Dodoma.

“Kwa namna ya pekee napenda kuishukuru Idara ya Ustawi wa Jamii pamoja na Mfuko wa Abbott ambao wamefanya kazi kubwa ya maandalizi na hatimaye kufanikisha shughuli hii ya leo.

“Aidha, sina budi kuwashukuru washiriki wote kwa kuacha kazi zenu muhimu na kuamua kushiriki nasi katika shughuli hii muhimu ya makabidhiano rasmi ya magari na vifaa kwa ajili ya kuongeza ufanisi katika utendaji kazi wa kila siku,”amesema Naibu Waziri Mwanaidi

Amesema Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto ina jukumu la kusimamia na kuratibu utoaji wa huduma kwa makundi maalum wakiwemo Watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.

Amesema utoaji na upatikanaji wa huduma hizi unaenda sambamba na upatikanaji wa nyenzo zitakazoweza kurahisisha huduma kwa walengwa kama vile vyombo vya usafiri pamoja na vitendea kazi ikiwamo vifaa vya TEHAMA.

“Ninafahamu kwamba Makao ya Watoto Kikombo yamewezesha upatikanaji wa huduma mbalimbali kwa watoto zikiwamo huduma za Michezo,Elimu Afya,msaada wa kisaikolojia na kijamii na ushauri nasaha,”amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa (ABBOTT FUND) Natalia Lebou amesema wametoa Magari mawili na vifaa vya IT kwa watoto kujifunza pamoja na vifaa vya Dispensary.

Amesema Mwaka huu ni mara ya kwanza kufika Kikombo na wamefurahi kushirikiana na Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto kuhakikisha wanapanga mipango ya kufikiria mbele kuhusiana na makao hayo ya watoto.

“Sisi tumefurahi kuwa kwenye ushirikiano na Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto tunajua kuna kazi sana ambayo tunafanya pamoja kupanga mipango na kufikiria mbele na hii kazi ni kubwa na tumeendelea na tutakuwepo kwa miaka ya mbele.Na pia tutaweza kusaidia kujenga na kutoa huu msaada kwa watoto,”amesema Bi.Natalia

AFRIKA YAJIANDAA KUZALISHA CHAKULA CHA KUTOSHA

$
0
0
Na. Mwandishi Maalum, Addis Ababa

Mkutano wa 39 wa Kawaida wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Umoja wa Afrika umefunguliwa leo jijini Addis Ababa, Ethiopia ambapo pamoja na mambo mengine, Mawaziri watapitia Andiko na mikakati ya utekelezaji wa kaulimbiu ya Mwaka 2022 ya “Lishe na Usalama wa Chakula barani Afrika”. Kaulimbiu hiyo inalenga kusisitiza umuhimu wa lishe bora kwa ajili ya ukuaji na ustawi wa watoto barani Afrika, bara ambalo kwa miaka mingi limekuwa linakabiliwa na uzalishaji mdogo wa chakula. Hivyo, nchi za Afrika zinashauriwa kutekeleza mapendekezo ya Progarmu ya Afrika ya Maendeleo ya Kilimo na Azimio la Malabo kuhusu kilimo ili kuondokana na changamoto ya lishe duni.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula anaongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo na katika mijadala yake, pamoja na mambo mengine,
anatarajiwa kusisitiza umuhimu wa kukifanya Kiswahili kuwa moja ya lugha ya kazi katika Umoja wa Afrika.

Mhe. Mulamula atakumbusha na kulisisitiza suala hilo kwa sababu limeainishwa katika kaulimbiu ya mwaka 2021 ambayo pamoja na mambo mengine, imehimiza matumizi ya lugha za kiafrika na
Kiswahili ni moja ya lugha hizo ambayo inakuwa kwa kasi na kuzungumzwa na watu wengi barani Afrika na duniani kwa ujumla.

Aidha, Waheshimiwa Mawaziri watapokea taarifa kuhusu ugonjwa wa UVIKO-19 ambapo katika hotuba ya ufunguzi ya Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje
wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo alisistiza umuhimu wa nchi wanachama kuzingatia tahadhari za maambukizi ya UVIKO-19 ikiwa ni pamoja na kuhamasisha watu wao kupata chanjo ya ugonjwa huo, huku jitihada zikiendelea kuhakikisha kuwa nchi za Afrika zinapata idadi ya kutosha ya chanjo kwa ajili ya watu wake.

Katika Mkutano huo pia, Mawaziri wa Mambo ya Nje watapitia na kupitisha bajeti ya Mwaka 2022 ya
Kamisheni ya Umoja wa Afrika na kufanya uchaguzi wa nafasi mbalimbali za uongozi, zikiwemo za makamishna wawili wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Rais na Makamu wa Rais wa Chuo Kikuu cha Pan Africa, wajumbe wanne wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika ya Haki za Binadamu na Watu na wajumbe wanne wa Bodi ya Ushauri ya Afrika ya Kupambana na Rushwa.

Vile vile, Mkutano wa 39 wa Mawaziri utapitia na kupitisha miundo ya taasisi saba za Umoja wa Afrika, ukiwemo muundo wa Sekretarieti ya Eneo Huru la Biashara barani Afrika ambalo
Tanzania imeridhia Mkataba wake hivi karibuni. Kupitishwa kwa miundo hiyo itakuwa ni fursa zikiwemo za ajira kwa nchi wanachama, hivyo, Balozi Mulamula amewataka Watanzania kuzichangamkia, pindi zitakapotangazwa.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (kushoto) na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Bi. Eliza Rwitunga wakiwa katika kikao cha kujiandaa na ujumbe wa Tanzania kabla ya kuingia kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Umoja wa Afrika.
Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Umoja wa Afrika ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo akisoma hotuba ya ufunguzi katika Mkutano wa 39 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Afrika unaofanyika jijini Addis Ababa, Ethiopia tarehe 14 na 15 Oktoba 2021
Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Naimi Aziz (kulia) na Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria, Balozi Caroline Chipeta wakisikiliza hotuba ya ufunguzi ya Mkutano wa 39 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Afrika unaofanyika jijini Addis Ababa, Ethiopia tarehe 14 na 15 Oktoba 2021
Ujumbe wa Tanzania katika kikao cha maandalizi na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula
ujumbe wa Tanzania ukijumuisha maafisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia wakiwa katika kikao cha maandalizi na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula.
Picha ya pmoja ya Mawaziri wa nchi za Umoja wa Afrika wanaoshiriki Mkutano wa 39 wa Kawaida wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za AU jijini Addis Ababa, Ethiopia.

RAIS SAMIA AWASILI MKOANI KILIMANJARO KUANZA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU TATU

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu Mkoani Kilimanjaro leo Oktoba 14,2021, akitokea Mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akisalimiana na Viongozi mbalimbali wa Serikali alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu Mkoani Kilimanjaro leo Oktoba 14,2021, akitokea Mkoani Geita.

PICHA NA IKULU

IGP SIRRO AKABIDHI UNYEKITI EAPCCO

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amekabidhi rasmi uwenyekiti wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi Mashariki Mwa Afrika EAPCCO na kumkabidhi uwenyekiti huo Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Congo IGP Dieudonne Bahigwa.
Hafla ya kukabidhi unyekiti huo imefanyika Oktoba 14, 2021 nchini Congo ambapo jumla ya nchi 14 wanachama wa shirikisho hilo wamehudhuria hafla hiyo ya makabidhiano. IGP Sirro ameliongoza Shirikisho hilo kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo ambapo wakati wa uongozi wake amesaidia shirikisho hilo katika kukabiliana na uhalifu unaovuka mipaka, usafirishaji wa dawa za kulevya, ugaidi pamoja na matishio mengine ya kiusalama.
Aidha, kufuatia ushirikiano wa wakuu hao wa Polisi kumewezesha kufanyika kwa operesheni za pamoja sambamba na ubadilishanaji wa taarifa za uhalifu na wahalifu.

BUTIKU:’TUTAENDELEA KUENZI UONGOZI ULIOACHWA NA HAYATI MWL NYERERE KWA KUONDOA TOFAUTI ZA KIKABILA’

$
0
0
MKURUGENZI wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Mh.Joseph Butiku,akizungumza wakati wa Kongamano la Vijana na Mwalimu Nyerere ambalo liliwashirikisha baadhi ya watu waliowahi kufanya kazi na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya kifo chake lililofanyika Oktoba 14,2021 jijini Dodoma.
MKURUGENZI wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Mh.Joseph Butiku,akisisitiza jambo kwa washiriki wakati wa Kongamano la Vijana na Mwalimu Nyerere ambalo liliwashirikisha baadhi ya watu waliowahi kufanya kazi na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya kifo chake lililofanyika Oktoba 14,2021 jijini Dodoma.
Aliyekuwa Mbunge Mhe.Steven Wasira,akichagia mada wakati wa Kongamano la Vijana na Mwalimu Nyerere ambalo liliwashirikisha baadhi ya watu waliowahi kufanya kazi na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya kifo chake lililofanyika Oktoba 14,2021 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Taasisi ya “Sisi Tanzania” ambao ndiyo waandaaji wa kongamano hilo Medoti Mashaka Medoti,akielezea lengo la Kongamano la Vijana na Mwalimu Nyerere ambalo liliwashirikisha baadhi ya watu waliowahi kufanya kazi na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya kifo chake lililofanyika Oktoba 14,2021 jijini Dodoma.
Mbunge wa Viti Maalumu anayewakilisha Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Mhe. Neema Lugangira,akizungumza wakati wa Kongamano la Vijana na Mwalimu Nyerere ambalo liliwashirikisha baadhi ya watu waliowahi kufanya kazi na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya kifo chake lililofanyika Oktoba 14,2021 jijini Dodoma.
Mbunge wa Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde,akizungumza wakati wa Kongamano la Vijana na Mwalimu Nyerere ambalo liliwashirikisha baadhi ya watu waliowahi kufanya kazi na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya kifo chake lililofanyika Oktoba 14,2021 jijini Dodoma.
Mbunge wa kundi la vijana Mkoa wa Singida Nusrat Hanje,akizungumza wakati wa Kongamano la Vijana na Mwalimu Nyerere ambalo liliwashirikisha baadhi ya watu waliowahi kufanya kazi na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya kifo chake lililofanyika Oktoba 14,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakifatilia mada mbalimbali wakati wa Kongamano la Vijana na Mwalimu Nyerere ambalo liliwashirikisha baadhi ya watu waliowahi kufanya kazi na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya kifo chake lililofanyika Oktoba 14,2021 jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna,Dodoma

MKURUGENZI wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Mh.Joseph Butiku amesema miaka 22 bila uwepo wa muasisi wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, watanzania wataendelea kuuenzi uongozi wake usiolea sumu kwenye uongozi na kuondoa tofauti za kikabila zilizokuwa zikiitafuna nchi kwa wakati ule.

Hayo ameyasema leo Oktoba 14,2021 Jijini Dodoma wakati wa Kongamano la Vijana na Mwalimu Nyerere ambalo liliwashirikisha baadhi ya watu waliowahi kufanya kazi na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya kifo chake kilichotokea miaka 22 iliyopita nchini Uingereza katika Hospitali ya St.Thomas mwaka 1999.

Butiku ,amemtaja mwl Nyerere kama shujaa wa ujamaa na kujitegemea hivyo kuwataka watanzania kujitegemea na kuacha uvivu utakaokwamisha maendeleo ya familia zao .

Aidha ameeleza kuwa maisha yake yalikuwa ni tunu kwa watanzania kwa kuwa aliishi kwa kusimamia uzalendo,umoja,mshikamano na kujitoa hata kwa kuhatarisha maisha yake.

Hata hivyo Butiku amesema vijana wa kitanzania wanapaswa kusimama katika nguzo hizo kwa kuzingatia malezi Bora ya wazazi wao na hatimaye kuwa na Taifa linalozingatia utu na maadili .

“Malezi yanawandaa watanzania wenye maadili na utii na kuwa na nafasi ya kukubali kusahihisha au kusahihishwa pale ambapo ni lazima,”amesema Butiku.

Aidha amefafanua kuwa katika kipindi chote alichafanya kazi na Mwl.Nyerere alimshuhudia akiwajali wanawake kwa vitendo na kuwapa usawa hali iliyowaondolea dhana ya kudharauliwa .

Kwa kufanya hivyo amesema Nyerere aliamua kuandika kitabu cha wanawake ili kuhamasiaha jamii kutambua mchango wa wanawake katika harakati za maendeleo ya taifa.

“Tumeshuhudia Mwalimu akiwapa nafasi za uongozi baadhi ya wanawake akiwepo Titi Mohamed “amesema

Kwa upande wake Mhe.Steven Wasira ameweka wazi kufurahishwa na jinsi vijana wanavyomuenzi Mwl Nyerere kwa kujifunza mambo mengi aliyoyafanya katika kipindi cha uhai wake.

“Nimefurahi kuona kuwa kuna watu wanaomjua vizuri Mwalimu kama waliishi naye na hii inaonyesha wazi kwamba watanzania wanapenda Viongozi shupavu wanaojali uwajibikaji na uwazi Kama alivyofanya Baba wa Taifa,”amesema Mhe.Wasira

Mbali na hilo ameeleza kuwa Mwalimu Nyerere aliwajali vijana kwa vitendo kwa kumpa kazi kwa nafasi ya ukuu wa Mkoa akiwa na miaka 27 tu.

“Vijana wasioelewa vizuri maono ya mwalimu wanaweza wakababaishwa kutokana na Dunia ya sasa ya mitandao,maisha mnayoishi sasa mnahitaji kukuwa zaidi kwa kuzingatia ukweli na hapo mtakuwa mmemuenzi ,”ameeleza.

Aidha amesema kutokana na mapenzi na nchi yake Mwalimu alianza harakati za utetezi akiwa bado mwanafunzi Ili kuondoa udini na ukabila ulioanzishwa na Wakoloni .

“Mwalimu alichukia ubaguzi wa kidini ulioanzishwa na wakoloni,wakoloni waliuchukia uislamu kitu ambacho Mwalimu aliopingana nacho na kuanzisha harakati za kupigania uhuru na hatimaye kuwa Taifa huru lisilo na udini,”amesema.

Naye Mbunge wa Viti Maalumu anayewakilisha Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Mhe. Neema Lugangira, ametumia nafasi hiyo kuikumbusha jamii kumuenzi Mwl.Nyerere kwa kuzingatia kilimo chenye tija kwa uhakika wa chakula na lishe.

“Mwalimu Nyerere alipenda sana kilimo,aliamini kuwa kilimo ni uti wa mgongo wa Taifa letu,hii ilijidhihirisha wakati akitoa mada maalumu huko Roma-Italia ambapo alisisitiza kuwa asilimia 97 ya watanzania kwa wakati ule wengi walitegemea sekta ya kilimo,”anasema.

Mbunge wa kundi la vijana Mkoa wa Singida Nusrat Hanje amesema katika kumuenzi Hayati Mwl.Nyerere lazima kuwaenzi pia Waandishi wa vitabu kwa sababu wamewezesha kizazi cha sasa kumjua vizuri.

“Wengi hatumjui Nyerere lakini kupitia Vitabu tunaweza kumuelezea sifa zake na kumuelewa,kupitia Waandishi wetu mahiri tuaishi kupitia maisha yake”amesema

Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya “Sisi Tanzania” ambao ndiyo waandaaji wa kongamano hilo Medoti Mashaka Medoti ameeleza lengo la kuandaa jukwaa hilo ni kuwapa fursa watanzania na hasa vijana kumuenzi Baba wa Taifa, kutafakari maisha yake na kuishirikisha jamii kuona ni kwa namna gani maisha yake yanakuwa chachu katika uchumi wa nchi.

“Tumelipa kongamano hili jina la Vijana na mwalimu Nyerere,tunatumia jukwaa hili kutoa mustakabali wetu kama vijana kwa kuziishi fikra zake hasa kwa kuzingatia katika harakati zake alitumia nusu ya maisha yake kuhudumia watanzania kwa kujitoa na kufanya misingi ya ujenzi wa Taifa letu kuwa na dhana ya kuheshimu utu wa binadamu,”amesisitiza

Hata hivyo Bw.Medoti amesema kwa miaka 22 bila uwepo wa Hayati Baba wa Taifa hilO, watanzania wana kila sasababu za kujivunia kama taifa lenye mshikamano uliorithishwa.

“Katika hili tuna deni la kulipa kwa kushikamana kushirikiana katika kukemea ujinga na maradhi,tunamuenzi na kumkumbuka zaidi kwa uongozi wake usiolea sumu kwenye taifa letu na kuondoa tofauti za kikabila zilizokuwa zikiitafuna nchi kwa wakati huo,”amesema .

NYERERE DAY 2022 WANAFUNZI IKUNGI KUPIGWA MSASA MAENDELEO YA TAIFA

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Jerry Muro ambaye alikuwa mgeni rasmi akizungumza na Wanafunzi katika Bonanza la michezo mbalimbali ikiwa ni Maadhimisho ya kumbukizi ya Baba wa Taifa Hayati Julius Kambarage Nyerere ambayo yalifanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Ikungi mkoani Singida.
Afisa Michezo wa wilaya hiyo Rachel Maliwa, akiongoza kufanya mazoezi.
Mwanafunzi Rehema Peter wa Shule ya Sekondari Ikungi akizungumza kwenye bonanza hilo.
Mwanafunzi Glory Malecela wa Shule ya Sekondari Ikungi akizungumza kwenye bonanza hilo.
Jogging ikifanyika.
Mazoezi yakiendelea.
Mazoezi yakiendelea.
Afisa Ustawi wa Jamii wa wilaya hiyo Haruni Yasin Haruni akiongoza kufanya mazoezi.
Mazoezi yakiendelea.
Wanafunzi wakisakata rhumba.
Wanafunzi wakisakata rhumba.
Wanafunzi wakiwa kwenye bonanza hilo.
Michezo ikiendelea
Michezo ikiendelea
Mashabiki wakifuatilia michezo.
Wanafunzi wakiwa katika foleni ya kupima afya.
Upimaji afya ukiendelea.
Upimaji afya ukiendelea.
Michezo ikiendelea.
Wanafunzi wakiangalia michezo.

Na Dotto Mwaibale, Ikungi

SERIKALI wilayani Ikungi mkoani Singida imesema Maadhimisho ya Siku ya Kumbukizi ya Baba wa Taifa Hayati Julius Nyerere yatakayofanyika mwakani yatakuwa ya kipekee ambapo midahalo ya kuwafundisha wanafunzi kuhusu maendeleo ya Taifa itatolewa.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Jerry Muro ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Bonanza la michezo mbalimbali ikiwa ni Maadhimisho ya kumbukizi ya Baba wa Taifa Hayati Julius Kambarage Nyerere ambayo yalifanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Ikungi.

” Ndugu zangu niwashukuru ninyi nyote mliojitokeza kuja kushiriki michezo mbalimbali tangu asubuhi kwa ajili ya kumbukizi hii ya kuadhimisha siku ambayo mhasisi wa Taifa letu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alifariki,” alisema Muro.

Muro aliwashukuru washiriki wote wa bonanza hilo wakiwemo viongozi wa wilaya hiyo, wanafunzi pamoja na Afisa Michezo wa wilaya hiyo Rachel Maliwa kwa kuratibu bonanza hilo.

Alisema wanapo maliza kumbukizi hiyo wao kama Serikali ndio mwanzo wa maandalizi mapya ya kuandaa Tamasha lingine la mwaka ujao kwani alifika kwenye bonanza hilo kuona na kujifunza.

Alisema maandalizi ya kumbukizi nyingine ya Mwalimu Nyerere inayokuja wataanza maandalizi yake mapema na kwa muda mrefu wakisaidiana na Walimu, Afisa Utumishi, Afisa Michezo, Afisa Elimu Sekondari na Msingi.

Alisema katika tamasha hilo itafanyika midahalo ya kitaaluma baada ya kutengeneza mada mbalimbali watakazopewa wanafunzi ambazo zitaelezea mtazamo na maendeleo ya Taifa na kuzishindanisha shule zote za Sekondari zilizopo kwenye wilaya hiyo na washindi watapatiwa zawadi zitakazopendekezwa.

Alisema michezo itaanza wiki mbili kabla ya siku ya maadhimisho hayo kwa kuzishindanisha timu za shule na za mitaani na siku ya kilele watatoa vikombe, zawadi na kwa wanafunzi watapatiwa vyeti na kwa shule itakayofanya vizuri sana itapatiwa zawadi nono na ya kipekee ambayo ni siri yake na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo.

Muro alitumia nafasi hiyo kuwataka wanafunzi kuzingatia masomo na kuacha mambo mengine yote yatakayoweza kuwakwamisha wasiweze kumaliza masomo yao na kushindwa kutimiza ndoto za maisha yao.

Afisa michezo wa wilaya hiyo Rachel Maliwa alisema katika kumbukizi ya Mwalimu Nyerere waliona wafanye bonanza la michezo mbalimbali kukimbia (Jogging) kilometa mbili, mazoezi ya viungo, mpira wa miguu, kikapu, Netball na mingine mingi ambayo ilichezwa na Watumishi wa Serikali Kuu, Halmashauri na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ikungi.

Alisema bonanza hilo lilifanyika sambamba na upimaji wa afya kama kupima uzito, urefu, damu, Ukimwi, uchangiaji wa damu salama na chanjo ya Uviko 19.

Alisema kazi hiyo ya upimaji wa afya ilifanywa na Wafanyakazi kutoka Idara ya Afya wilaya humo.

Wanafunzi wa Sekondari ya Ikungi Glory Malecela na Rehema Peter wakizungumza kwa nyakati tofauti katika bonanza hilo walisema michezo inawafanya wafurahi, kujumuika na watu mbalimbali, inawafanya kuwa vizuri katika masomo na wakatoa shukurani zao kwa waandaaji wa bonanza hilo.

RAIS SAMIA AANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI KILIMANJARO

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwasili katika eneo la Sanya Juu Wilayani Siha Mkoani Kilimanjaro leo Octoba 15,2021. Kwa ajili ya kuzindua rasmi Barabara ya Lami yenye urefu wa kilomita 32.2. 15,2021. Mhe. Rais Samia yupo Mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya kutembelea, kukagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo ya Wananchi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiondoa kitambaa kuzindua rasmi Barabara ya Lami yenye urefu wa kilomita 32.2 katika eneo la Sanya Juu Wilayani Siha Mkoani Kilimanjaro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikata utepe kuzindua rasmi Barabara ya Lami yenye urefu wa kilomita 32.2 katika eneo la Sanya Juu Wilayani Siha Mkoani Kilimanjaro leo Octoba 15,2021. Mhe. Rais Samia yupo Mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya kutembelea, kukagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo ya Wananchi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Waziri wa Ujenzi Mhe. Makame Mbarawa pamoja na baadhi ya watendaji Wakuu wa Wizara hiyo mara baada ya kuzindua rasmi Barabara ya Lami yenye urefu wa kilomita 32.2 katika eneo la Sanya Juu Wilayani Siha Mkoani Kilimanjaro
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Wananchi wa Kijiji cha Sanya Juu Wilayani Siha Mkoani Kilimanjaro mara baada ya kuzindua rasmi Barabara ya Lami yenye urefu wa kilomita 32.2 katika eneo la Sanya Juu Wilayani Siha Mkoani Kilimanjaro
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiondoa kitambaa kuweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Jengo la Huduma ya Afya ya Mama na Mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa katika Eneo la Mawezi Mkoani Kilimanjaro leo Octoba 15,2021. Mhe. Rais Samia yupo Mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya kutembelea, kukagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo ya Wananchi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiondoa kitambaa kuweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Daraja la Rau linalojengwa katika Eneo la Rau Halmashauri ya Moshi Mjini Mkoani leo Octoba 15,2021. Mhe. Rais Samia yupo Mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya kutembelea, kukagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo ya Wananchi.

PICHA NA IKULU.

KILIMO CHA UMWAGILIAJI KUKABILIANA NA ATHARI NA MADHARA YATOKANAYO NA MABADILIKO YA TABIANCHI

$
0
0

 NA Mwandishi Wetu – Moshi

Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imejipanga kimkakati kupitia mpango kambambe wa Taifa wa Umwagiliaji wa mwaka 2018, kukabiliana na athari na madhara yatokanayo na mabadiliko ya Tabia nchi katika sekta ya Kilimo.

Hayo yamesemwa leo mjini Moshi katika maonesho yanayoendelea kuelekea maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani na Mhandisi Naomi Mcharo, kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.

Mhandisi Naomi amesema kuwa,mabadiliko ya tabianchi yamesababisha ukame na wakati mwingine mafuriko yanayosababisha madhara katika mashamba na uharibifu wa miundombinu ya umwagiliaji, “ kwa hivyo sisi Tume ya Taifa ya Umwagiliaji tuna Mpango kabambe ambao tumeanisha kuanzia miaka 10 mpaka 20 ya kukabiliana na mabadilio ya Tabia nchi, kwa maana ya kwamba tumepanga kuwa na Ujenzi wa mabwawa nchi nzima takribani mabwawa 88, ambayo yapo kimakakati katika maeneo kame.” Alisisitiza.

Aidha, Mhandisi alibainisha kuwa mabwawa hayo yatajengwa katika maeneo ambayo yanapata ukame kwa muda mrefu na mvua zenye kuleta madhara.

Alibainisha kuwa, maeneo mbayo yatajengwa na yamejengwa mabwawa hayo kama vile katika wilaya ya Kwimba yanasaidia kukabiliana na athari na madhara yatokano na mabadiliko ya Tabia nchi.

Awali Mhandisi Naomi alieleza kuwa, Fedha zinazoingia katika mfuko wa Taifa wa Umwagiliaji zinatoka katika vyanzo mbali mbali vya mapato, ikiwa ni pamoja na ukodishwaji wa mitambo inayomilikiwa na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, ambapo fedha hizo zinatumika katika  kazi ya matunzo, matengenezo na ujenzi wa Miundombinu katika skimu za kilimo cha umwaguliaji nchini, akitolea mfano wa ukarabati wa skimu  ya Pawaga, na Dakawa unaoendelea, Ruaha Mbuyuni ambapo ukarabati wa kingo ya mto Lukosi ulioacha njia umekamilika, na Urumwi Ujenzi unaendelea wa mfumo shirikishi kwa wananchi yaani  force account.

Picha ikionesha mtambo maarufu kwa jina la kijiko ukifanya kazi katika Skimu ya Kilimo cha umwagiliaji Urumwi mkoani kilimanjaro.

Picha ikionesha Fundi ujenzi akifanya kazi katika skimu ya kilimo cha umwagiliaji Urumwi mkoani Kilimanjaro,ambapo ujenzi huo shirikishi kwa wananchi unaendelea.

Pichani Mhandisi, Naomi Mcharo akizungunza na waandishi wa habari hawapo katika picha,, kuhusiana na namna sekta ya kilimo cha umwagiliaji ilivyojipanga katika kukabiliana na athari na madhara yatokananyo na mabadiliko ya Tabianchi.



BIRTHDAY YA MTOTO JACOB, OCEAN CITY, MARYLAND

$
0
0

Mtoto Jacob akifurahia siku ya kumbukizi ya kuzaliwa kwake aliyofanyiwa na wazazi wake siku ya Jumamosi Oktoba 16, 2021 Ocean City, Maryland, Kama kawaida NDMV family ambazo hukutana katika kuungana mkono katika shughuli mbalimbali aidha za wazazi au watoto wao na kusherehekea pamoja kama wanafamilia moja ikiwemo watoto wao waliojijengea urafiki na ukaribu wa kucheza pamoja mara wanapokutana.
Mtoto Jacob akizima mishumaa katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.
Mtoto Jacob akikata keki/
Mtoto Jacob akimlisha keki mama yake.

Mtoto Jacob akimlisha keki baba yake
Mtoto Jacob akimlisha keki mdogo wake.
Mtoto Jacob akimlisha keki dada yake.
Kwa picha zaidi bofya soma zaidi
Mtoto Jacob akimlisha keki bibi yake.

Mtoto Jacob akimlisha keki babu yake
Mtoto Jacob akisakata rhumba.
Picha juu na chini ni mapema siku ya jumamosi NDMV Family wakiwa kwenye bwawa la kuogelea.
Picha juu na chini NDMV Family wakijumuika pamoja kwenye sherehe ya Birthday na chakula cha jioni.
Picha juu na chini NDMV family wakipata chai day two.

Picha juu na chini wakiwa kwenye bwawa la kuogelea kabla kila familia kurejea makwao.



WANANCHI WASHAURIWA KUUNGA MKONO HUDUMA BORA NA ZA KIDIGITALI ZINAZOTOLEWA NA POSTA TANZANIA

$
0
0
Kaimu postamasta mkuu wa shirika la Posta Tanzania, Macrice Mbodo (katikati)akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha .
Meneja Tehama wa shirika la Posta Tanzania ,Inspekta Reuben Komba akizungumza na vyombo vya habari jijini Arusha

(Happy Lazaro)

Happy Lazaro,Arusha

Arusha.Wananchi wametakiwa kupenda kutumia huduma za posta ya hapa kwetu nchini huku wakitakiwa kupenda vitu vya nyumbani kwani posta ya Sasa imebadilika hivyo ni vizuri wakaunga mkono kutumia huduma za posta hapa kwetu kwani kwa Sasa huduma zimeboreshwa kidigitali kupitia Tehama .

Hayo yamesemwa na Kaimu postamasta Mkuu shirika la posta Tanzania,Macrice Mbodo wakati akizungumza katika mkutano wa wadau wa Tehama unaofanyika mjini hapa.

“kwa nini tukatumie maposta ya nchi zingine wakati tuna Posta yetu hapa nyumbani na Posta yetu Sasa hivi imebadilika Sana tunatoa huduma zote kidigitali hivyo nawaomba Sana wananchi waunge mkono kwa kutumia huduma za nyumbani za Posta.”amesema Mbodo.

Ameongeza kuwa ,huduma zinazotolewa na Posta Sasa hivi ni za kidigitali na zinatoa mwanya wa kila mwananchi kupata huduma popote pale alipo kwani wao ndo wanamfuata mwananchi na hawasubiri mwananchi awafuate.

Amesema kuwa,Serikali ya awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Samia suluhu Hassan imejipanga kutumia Tehema kurahisisha utoaji wa huduma za serikali kwa wananchi kupitia vituo vya huduma pamoja.

Ameongeza kuwa,Serikali imejipanga kupitia shirika la posta Tanzania kuhakikisha kuwa huduma mbalimbali za serikali zinatolewa chini ya dari Moja kupitia vituo vya huduma pamoja.

“madhumuni makuu ya kushiriki mkutano huu ni ili kuonyesha fursa ya kidigitali zinazotumiwa na posta kwani posta tuliyonayo .sasa hivi sio ile ya zamani ,hivyo wananchi wanapaswa kuitumia kwa shughuli mbalimbali.”amesema .

Ameongeza kuwa ,posta ya kidigitali inamwezesha mwananchi kuwa na duka mtandao ambapo inamwezesha mwananchi kuuza na kununua bidhaa zao kote duniani kupitia.duka hilo .

Amefafanua kuwa,posta ya sasa ipo kwa ajili ya kumfuata mwananchi kwani huduma za shirika zinapatikana kupitia simu za mkononi ambapo sasa hivi mwananchi anaweza kutumia namba ya simu kuwa anuani yake tofauti na zamani kwenda ofisi za posta.

Mbondo amesema kuwa, kwa Sasa hivi kuna mabadiliko makubwa ambayo yamepatikana kwani unaweza kuagiza bidhaa mbalimbali mikoa nyingine na unafikishiwa hapo hapo ulipo kila mmoja anapaswa kutambua kuwa hii ni posta ambayo imebadilika .

“Ukituma mzigo wako leo ukaweka namba ya simu utapokea meseji kuwa mzigo umepata hii ni zaidi ya Posta tofauti na kipindi kile hivyo naomba wananchi waitumie Posta vizuri.”amesema

Amefafanua kuwa, kama shirika wana fursa ya kukua zaidi kwa kuhakikisha wao ndo wasafirishaji wakuu hapa Tanzania lengo kuhakikisha usafirishaji ndani ya Tanzania unafanyika kupitia shirika la Posta.

Ameongeza kuwa, hapa Arusha Tanzania ni makao makuu ya Umoja wa posta Afrika na wamejipanga kuhakikisha posta ya Tanzania inakuwa mfano wa kuigwa kwa posta zote za Umoja wa Afrika ili waje kujifunza hapa.

Kwa upande wake Meneja Tehama wa shirika la Posta Tanzania ,Inspekta Reuben Komba amesema kuwa, Posta wameunganisha ofisi katika maeneo mbalimbali na zinatoa huduma kidigitali na zimeweza kupiga hatua kubwa kwa kufikia watu mbalimbali.

Komba amesema kuwa,kupitia huduma za duka mtandao zinawawezesha wafanyabiashara wadogo kuweza kujisajili na kuuza huduma zao sehemu yoyote mtandaoni na mwitikio ni mkubwa Sana.

“kwa kweli kupitia huduma ya kimtandao inasaidia kuunganisha wateja mbalimbali na kuweza kupata fursa ya kuuza na kununua bidhaa zao duniani kupitia duka mtandao “amesema Inspekta Komba.

MAJALIWA: RAIS SAMIA AMEDHAMIRIA KUENDELEZA MICHEZO NCHINI

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Rais wa awamu ya sita Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan anapenda na kuthamini michezo mbalimbali nchini na atahakikisha inaendelea kushamiri na kuongeza tija.

Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa ametumia fursa hiyo kuwahakikishia wadau wa michezo na wanamichezo wote nchini kwamba Serikali itaendelea kuunga mkono shughuli zote za michezo ukiwemo mchezo wa mpira wa miguu.

Mheshimiwa Majaliwa aliyasema hayo jana usiku (Alhamisi, Oktoba 21, 2021) katika hafla ya utoaji wa tuzo kwa wanamichezo waliofanya vizuri msimu wa 2020/2021 zilizoandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

“Mheshimiwa Rais Samia anawahakikishia kuwa Serikali anayoiongoza imedhamiria kuendeleza michezo na itaongeza nguvu ili kuhakikisha mchezo wa mpira wa miguu nchini unakuwa na viwango bora.”

Waziri Mkuu aliupongeza uongozi wa TFF kwa kuandaa wa tuzo hizo ambazo zinatoa motisha kwa wachezaji, walimu, viongozi wa vilabu na waamuzi. “Tuzo hizi zinaongeza hamasa kwa wengine kushiriki kikamilifu.”

“…Katika vipindi vyote, sasa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania limetufikisha mahali ambapo tunaona muelekeo wa soka letu. Viongozi wa TFF wametufikisha mahali pazuri, tunapaswa kuwapongeza kwa hatua hii.”

Wakati huo huo, Mheshimiwa Majaliwa alimuagiza Mkurugenzi wa Michezo nchini Yusuph Singo ahakikishe timu zinazoliwakilisha Taifa katika mashindano mbalimbali ya kimataifa zinawezeshwa kushiriki kikamilifu bila ya kukwama.

Katika hafla hiyo, Mheshimiwa Majaliwa alitoa tuzo kwa timu na wachezaji waliofanya vizuri katika makundi mbalimbali. Baadhi ya tuzo zilizotolewa ni na ya mchezaji bora VPL 2020/ 2021 ambaye ni John Bocco kutoka klabu ya Simba; Mchezaji bora wa Kombe la Shirikisho, Feisal Salum kutoka Yanga Sports Club, mchezaji bora anayechipukia ambayo iliyochukuliwa na Abdul Sopu wa Coastal Union na tuzo ya mhamasishaji bora iliyochukuliwa na Nick Reynolds maarufu kama Bongo Zozo.

Tuzo nyingine ni ya timu yenye nidhamu iliyochukuliwa na Timu ya Coastal Unioan, tuzo ya heshima kwa soka la wanawake iliyopokelewa na Mjane wa marehemu, Dkt. Maneno Tamba

Rais wa Shirikisho la Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia alimkabidhi Waziri Mkuu tuzo ya heshima kutokana na mchango wake mkubwa katika kuendeleza mpira wa miguu nchini. Pia Waziri Mkuu alimkabidhi Alhaji Abdallah Kibadeni tuzo ya mchezaji gwiji



Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo hizo Alhaji Ahmed Msafiri amesema kuwa utoaji wa tuzo hizo umezingatia haki na usawa kutoka kwa majaji na pia zimetolewa kulingana na vigezo vilivyowekwa ikiwemo ushiriki wa kila mmoja katika eneo husika.

MKUU WA WILAYA YA MTWARA AIPONGEZA SERIKALI KWA KUANDAA MAFUNZO KWA WASAFIRISHAJI

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Mtwara Mheshimiwa Dustan Kyobya akifungua Semina ya mafunzo kwa wadau wa uasafirishaji (hawapo pichani), kuhusu Sheria ya Udhibiti Uzito wa Magari ya mwaka 2016 na kanuni zake za mwaka 2018 inayofanyika katika ukumbi wa Chuo cha VETA Mtwara
Baadhi ya washiriki wa semina ya mafunzo kwa wadau wa usafirishaji kuhusu Sheria ya Udhibiti Uzito wa Magari ya mwaka 2016 na kanuni zake za mwaka 2018 inayofanyika katika ukumbi wa Chuo cha VETA Mtwara wakifurahia jambo.
Baadhi ya washiriki wa semina ya mafunzo kwa wadau wa usafirishaji kuhusu Sheria ya Udhibiti Uzito wa Magari ya mwaka 2016 na kanuni zake za mwaka 2018 inayofanyika katika ukumbi wa Chuo cha VETA Mtwara, wakimsikiliza mgeni rasmi Mheshimiwa Dustan Kyoba, Mkuu wa wilaya ya Mtwara (hayupo pichan), wakati wa ufunguzi wa semina hiyo.
Washiriki wa semina ya mafunzo kwa wadau wa usafirishaji kuhusu Sheria ya Udhibiti Uzito wa Magari ya mwaka 2016 na kanuni zake za mwaka 2018 inayofanyika katika ukumbi wa Chuo cha VETA Mtwara, wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi Mheshimiwa Dustan Kyoba, Mkuu wa wilaya ya Mtwara, wakati wa ufunguzi wa semina hiyo.

Picha na WUU

Mkuu wa wilaya ya Mtwara Dustan Kobya, ameipongeza Serikali kwa kuandaa mafunzo kwa wasafirishaji kuhusu Sheria ya Udhibiti Uzito wa Magari ya mwaka 2016 na kanuni zake za mwaka 2018.

Ametoa pongezi hizo wakati akifungua semina ya mafunzo ya sheria hiyo kwa wadau wa usafirishaji yaliyoandaliwa na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), yanayofanyika kwa siku moja mkoani Mtwara katika ukumbi wa Chuo cha VETA.

“Ni matumaini yangu kuwa mafunzo haya yataongeza uelewa kwa Sheria hii ya Udhibiti Uzito wa Magari ya mwaka 2016 na kanuni zake za mwaka 2018 kwa wasafirishaji hali itakayopelekea barabara zetu kudumu na kupitika nyakati zote na hivyo kuipunguzia Serikali mzigo mkubwa wa gharama za matengenezo ya barabara mara kwa mara”, amesema Dustan Kobya.


Aidha Mkuu wa Wilaya huyo aliitaka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kupitia TANROADS, kuandaa vipindi maalumu, majarida na vipeperushi vitakavyotoa uelewa zaidi kwa wadau wa usafirishaji, ili kupunguza au kuondoa kabisa changamoto ya uzidishaji uzito wa magari barabarani.

Akimkaribisha mgeni rasmi, Meneja wa TANROADS mkoa wa Mtwara, Mhandisi Dotto John amesema kuwa, mafunzo hayo yanalenga kutoa uelewa kwa wasafirishaji ili kupunguza changamoto mbalimbali zitokanazo na uelewa mdogo wa Sheria ya Udhibiti Uzito wa Magari inayotumiwa na nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki yaani ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Sudani Kusini.

Kwa upande wake msimamizi wa Mizani kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Leonard Saukwa amesema kuwa mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo wasafirishaji na wamiliki wa magari ya mizigo ili waweze kuelewa sheria ya udhibiti uzito ya Afrika Mashariki na kanuni zake na kwamba watazunguka nchi nzima katika vituo 13 kwa ajili ya kutoa elimu hiyo

Mafunzo hayo ambayo yanashirikisha wadau mbalimbali wa usafirishaji yamepangwa kufanyika katika Mikoa 13 ikiwemo Dar es Salaam, Mtwara, Morogoro, Dodoma, Njombe, Mbeya, Rukwa, Ruvuma, Kigoma, Geita, Tabora, Mwanza, Arusha na Tanga.

MAKAMU WA RAIS KUFUNGA SHIMIWI KESHO UWANJA WA JAMHURI MOROGORO

$
0
0
Mshambuliaji Mkoma Watson wa timu ya RAS Mara akijaribu kupita mbele ya mlinzi Issa wa NFRA katika mchezo wa soka wa michuano ya Idara na Wizara za Serikali (SHIMIWI), uliofanyika leo kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, ambapo RAS walishinda kwa magoli 6-0.
Mchezaji Lightnes Mlay (mwenye mpira) wa timu ya Hazina akitafuta njia ya kumpita Apsa Mohamed (mwenye jezi ya zambarau) wa Wizara ya Afya katika mchezo wa netiboli katika michuano ya Michezo ya Idara na Wizara za Serikali (SHIMIWI) uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro.ambapo Hazina walishinda kwa magoli 18-13
Timu ya Uchukuzi (pichani) ikijiandaa kuvuta Kamba na wenzao wa RAS Ruvuma katika mchezo wa michuano ya Shirikisho la Michezo ya Idara na Wizara za Serikali (SHIMIWI) uliofanyika leo kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. Uchukuzi walishinda kwa mivuto 2-0.
Wachezaji wa timu ya Polisi Tanzania (kulia) wakivutana na Wizara ya Mambo ya Nje katika michuano ya Shirikisho la Michezo ya Idara na Wizara za Serikali (SHIMIWI) uliofanyika leo kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, ambapo Polisi waliibuka washindi kwa mivuto 2-0.
Timu ya Wakala wa Jiolojia na Utafiti wa Madini (GST) (kushoto) wakiwavuta bila huruma Wizara ya Habari na Mawasiliano mivuto 2-0 kwenye michuano ya Shirikisho la Michezo ya Idara na Wizara za Serikali (SHIMIWI) uliofanyika leo kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Na Mwandishi Wetu, Morogoro

WAKATI Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango kesho atafungua rasmi michuano ya Shirikisho la Michezo ya Idara na Wizara za Serikali (SHIMIWI) inayoendelea kwenye viwanja mbalimbali mkoani Morogoro, timu za Wizara ya Mambo ya Nje za soka na netiboli zimeng’ara kwa kupata ushindi.

Michuano hiyo inayoendeshwa kwa mtindo wa makundi katika michezo ya soka, netiboli na Kamba tayari ilianza tarehe 20 Oktoba, 2021 lakini kesho itafunguliwa rasmi.

Timu ya soka ya Mambo ya Nje iliibuka washindi kwa kuwafunga Tume ya Uchaguzi kwa magoli 4-0 mchezo uliofanyika uwanja wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kampasi ya Mazimbu; ambapo magoli ya washindi yalifungwa na Fidelis Chipamba matatu na Mikidadi Nnoa bao 1. Nayo timu ya Ofisi ya Waziri Mkuu iliibuka washindi kwa kuwafunga Ujenzi kwa magoli 2-0 yaliyofungwa na Joseph John na Frank Mwakitalu, mchezo huu umefanyika kwenye Chuo Kikuu cha Jordan.

Nao Madini waliwafunga Tume ya Uchaguzi (NEC) kwa magoli 2-1 katika mchezo uliochezwa SUA kampasi ya Mazimbu, ambapo magoli yote ya washindi yalifungwa na Madilu Ngusi huku la NEC lilifungwa na Desmond Haukira. Wakati mchezo mwingine Sanaa wametoshana nguvu na Sheria na Katiba kwa kutoka suluhu; nao Wizara ya Kilimo waliwafunga Maliasili kwa bao 1-0 lililofungwa na Tanziru Mhando.

Kwa upande wa dada zao wa netiboli timu ya Nje waliwafunga RAS Mara kwa magoli 15-11. Hadi mapumziko washindi walikuwa mbele kwa magoli 5-4; nayo RAS Moro waliwafunga Wizara ya Viwanda na Biashara kwa magoli 3-1.

Katika mchezo mwingine wa soka uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri timu ya RAS Mara iliwaadabisha NFRA kwa kuwafunga magoli 6-0, yaliyofungwa na Mkoma Pastor manne, Watson Ntimwa bao 1 na beki Marco wa NFRA alijifunga na kukamilisha idadi ya magoli 6; nazo Hazina na Nishati zilitoshana nguvu kwa kutoka suluhu.

Katika michezo mingine ya netiboli timu ya Wizara ya Maji waliwafunga Mahakama kwa magoli 16-14. Hadi mapumziko washindi waliongoza kwa magoli 10-5; huku Nishati wakiwachapa Tume ya Walimu kwa magoli 14-9; nayo Hazina iliwacharaza Wizara ya Afya kwa magoli 18-13; wakati Hazina waliwafunga Mifugo magoli 29-10.

Nayo Tamisemi waliwafunga Mambo ya Nje kwa magoli 48-6; huku Ikulu wakiwachezesha rumba Wizara ya Maji kwa kuwafunga magoli 68-7; nayo Sanaa waliwashinda Nishati kwa magoli 23- 21 na Wizara ya Elimu waliwaadhibu Tume ya Uchaguzi kwa kuwafunga magoli 49-12.

Kwa upande wa mchezo wa kuvuta kamba kwa wanawake timu ya Uchukuzi iliwavuta RAS Ruvuma kwa mivuto 2-0; huku Wizara ya Kilimo ikiwavuta Wizara ya Maji kwa mivuto 2-0; nayo RAS Iringa wakiwavuta Hazina kwa mivuto 2-0; huku Sanaa wakiwavuta RAS Kilimanjaro kwa mivuto 2-0.

Michezo mingine Wizara ya Maliasili na Utalii waliwavuta Tume ya Walimu kwa mivuto 2-0; nayo Wizara ya Katiba na Sheria waliibuka washindi kwa kuwavuta kwa mbinde Tume ya Uchaguzi kwa mivuto 1-0; huku Tamisemi wakitoshana nguvu na Madini kwa kutoka sare ya mvuto 1-1.

Kwa upande wa wanaume timu ya Wizara ya Kilimo waliwavuta Tume ya Walimu kwa mivuto 2-0; huku Wizara ya Mambo ya Ndani waliwavuta Ujenzi kwa mivuto 2-0; nayo Mifugo waliwavuta Ukaguzi kwa mivuto 2-0; huku Polisi wakiwavuta Mambo ya Nje kwa 2-0; pia Wizara ya Maliasili waliwavuta Hazina kwa 2-0 na Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini waliwavuta Habari na Mawasiliano kwa mivuto 2-0.

Michuano hiyo ambayo inashirikisha michezo ya soka, netiboli, kuvuta Kamba, bao, karata, draft, darts, riadha, kuendesha baiskeli na kufukuza kuku inaendelea kwenye viwanja mbalimbali na itafikia kilele tarehe 2 Novemba, 2021
Viewing all 45984 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>