Quantcast
Channel: VIJIMAMBO
Viewing all 45984 articles
Browse latest View live

RAIS SAMIA APOKEA RAIS WA BURUNDI NDAYISHIMIYE KUANZA ZIARA YA SIKU NCHINI

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 22 Oktoba, 2021 kwa ziara ya kikazi ya siku 3.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama pamoja na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye wakati nyimbo za Mataifa mawili Tanzania na Burundi pamoja na wimbo wa Afrika Mashariki zikipigwa mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye akikagua Gwaride la Heshima lililoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 22 Oktoba 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimtambulisha mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye kwa Viongozi mbalimbali wa Serikali mara kuwasili katika viwanja vya Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 22 Oktoba 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evareste Ndayishimiye Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza ujumbe wa Tanzania katika mazungumzo Rasmi na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye aliyekuwa akiongoza ujumbe kutoka Burundi katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evareste Ndayishimiye akizungumza kwenye mkutano na Waandishi wa Habari Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 22 Oktoba 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza kwenye mkutano na Waandishi wa Habari wakati wa ujio wa Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evareste Ndayishimiye Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evareste Ndayishimiye akizungumza kwenye mkutano na Waandishi wa Habari Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.

PICHA NA IKULU.

TUVUNJE UKIMYA KWA KAZI ZA NDANI NA NDOA ZA UTOTO, TUPATE ELIMU-UDAA

$
0
0
Na Joseph Lyimo

MSICHANA wa jamii ya kidatoga wa Kata ya Bassotu Wilayani Hanang’ Mkoani Manyara, Neema John (Udaa) siyo jina lake halisi amesema aliamua kuachana na uamuzi wa wazazi wake wa kulazimishwa kufanya kazi za ndani na kuamua kupata elimu.

Udaa anaeleza kuwa wazazi wake walitaka akafanye kazi za ndani Katesh ili awe anawatumia fedha ila alikataa na kuamua kuendelea na masomo baada ya kuhitimu darasa la saba na kuchaguliwa kuendelea na sekondari.

Anasema baadhi ya wazazi na walezi wa watoto wa eneo hilo ambao ni jamii ya wafugaji hawapendi watoto wapate elimu hiyo huwashinikiza wakafanye kazi za ndani au kuolewa ili wapewe mahari ya ngombe ila yeye aligoma.

“Mimi nina ndoto ya kuwa mwalimu hivyo baada ya kuchaguliwa kuendelea na elimu ya sekondari nilikuwa najiandaa ndipo wazazi wakaniambia nikafanye kazi za ndani Katesh ila nikakataa,” amesema Udaa.

Amesema aliwaeleza wazazi wake kuwa kuna shirika lisilo la kiserikali analolifahamu wakiendelea kumkataza asiendelee na masoko akafanye kazi za ndani atatoa taarifa ndipo wakamkubalia.

Amesema yeye binafsi ametambua haki yake ya kupata elimu ndiyo sababu aliwaeleza wazazi wake kwa kuwaambia kuwa wamuache asome la sivyo atawashitaki ndipo wakamkubalia.

“Mwamko wa wazazi wangu hivi sasa umebadilika kwani awali hawakutaka nisome ila baada ya mimi kuonyesha msimamo kuwa napenda elimu walikubali niendelee na masomo na nisiajiriwe kufanya kazi za ndani,” amesema Udaa.

Amesema baadhi ya wazazi na walezi hufanya makubaliano na watoto wao kwenda kufanya kazi za ndani au kuacha masomo ili wakaolewe na kuacha haki zao za kupata elimu ila kwake alisimama kidete.

Mratibu wa uwezeshaji jamii kisheria wa kituo cha msaada wa sheria wa wanawake na watoto, Consolata Chikoti amesema jamii inatakiwa kutoa ushirikiano, wasiwaone maadui, wajue kuwa wana nia njema ya kusaidia jamii na pia mpango kazi wa Taifa ujulikane kwa wadau wote.

“Tumeamua kuja Hanang’ na kukutana na jamii ya eneo hili kwa sababu tumeona hii jamii ina uhitaji wa aina yake, ina watoto wenye vipaji, lakini kuna vikwazo vikiwemo mila na desturi kandamizi kwa watoto wa kike na wanawake,” amesema Chikoti.

Amesema katika kukabiliana na vitendo hivi vya kikatili suala la ushahidi nalo limekuwa kikwazo, kwani sheria ina mapungufu makubwa, kuna matatizo mengine yanahitaji mbinu mbadala ikiwemo sheria yenyewe ilivyo.

“Pamoja na Serikali kupanga bajeti kutekeleza mpango huu, bado ina mambo mengi, hivyo wadau tajwa waone haja ya kuchangia kufanikisha zoezi hilo na kutokomeza kwa ajili ya manufaa ya wasichana na wanawake kwa ujumla,” amesema Chikoti.

Hivi karibuni mkuu wa mkoa wa Manyara, Charles Makongoro Nyerere alifanya ziara kwenye wilaya mbalimbali za mkoa huo na kuwataka wazazi, walezi wenye wanafunzi kuhakikisha wanaendelea na masomo.

“Kama una mtoto anayesoma shule ya msingi au sekondari uhakikishe anahitimu masomo yake na endapo akiolewa au kukatizwa masomo yake tutawachukulia hatua kali za kisheria,” amesema Makongoro.

BILLIONI 7.4 ZATENGWA KUBORESHA HUDUMA KATIKA MAKAZI YA WAZEE NCHINI

$
0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akiwasilisha taarifa kuhusu Makazi ya Wazee nchini mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Mwanaidi Ali Khamis akifafanua jambo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Stanslaus Nyongo akielezea jambo wakati wa Uwasilishajiwa taarifa kuhusu Makazi ya Wazee nchini mbele ya Kamati hiyo jijini Dodoma.
Baadhi ya Wabunge wakifuatilia hoja ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima wakati akiwasilisha taarifa kuhusu Makazi ya Wazee nchini mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii jijini Dodoma.

MAJALIWA AFUNGUA MKUTANO WA TANO WA TEHAMA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Wadau wa Sekta ya TEHAMA wakati alipofungua Mkutano wa Tano wa Mwaka wa TEHAMA Tanzania uliofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC) jijini Arusha,
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha nakala za mwongozo wa usajili wa watalaamu wa Tehama baada ya kuuzindua, katika Mkutano wa Tano wa Mwaka wa Tehama Tanzania uliofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC) jijini Arusha, Oktoba 22, 2021. Kushoto ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Tekinolojia ya Habari, Dkt. Ashatu Kijaji
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokea kwa Tuzo kutoka kwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Tekinolojia ya Habari, Dkt. Ashatu Kijaji kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ya kutambua mchango wake katika kukuza sekta ya TEHAMA Nchini. katika Mkutano wa Tano wa Mwaka wa Tehama Tanzania uliofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC) jijini Arusha
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza, Mkurugenzi wa Masuala ya Sekta kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Emmanuel Manasseh (kushoto) wakati alipotembelea banda la TCRA katika Mkutano wa Tano wa Mwaka wa TEHAMA Tanzania uliofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC) jijini Arusha, Oktoba 22, 2021. Wa pili kushoto ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Ashatu Kijaji, kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Zainab Chaula na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella.
Wadau wa Sekta ya TEHAMA wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Mkutano wa Tano wa Mwaka wa TEHAMA Tanzania uliofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC) jijini Arusha, Oktoba 22, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA

$
0
0

KUKAMATWA KWA MTUHUMIWA WA KUTUPA MTOTO.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limefanikiwa kumkamata mwanamke JANETH PETER [32] Mkazi wa Kiwira Wilayani Rungwe kwa tuhuma za kutupa mtoto mchanga jinsi ya kike anayekadiriwa kuwa na umri wa siku tatu ambaye alikutwa tayari amefariki dunia baada ya kutupwa ndani ya shimo la choo.

Mtuhumiwa amekamatwa Oktoba 20, 2021 majira ya saa 19:00 jioni baada ya Jeshi la Polisi mkoani hapa kufanya msako mkali huko Kata ya Kiwira, Tarafa ya Ukukwe, Wilaya ya Rungwe na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa ambaye amehojiwa na kukiri kutenda kosa hilo.

Awali mnamo Oktoba 20, 2021 majira ya saa 09:00 asubuhi huko Mtaa wa Makaburini uliopo Kata ya Kiwira, Tarafa ya Ukukwe katika Halmashauri ya Rungwe, Mwili wa kachanga ulikutwa ndani ya shimo la choo kilichopo nyumbani kwa SALOME LUTENGANO [36] Mkazi wa Mtaa wa Makaburini na ndipo jitihada za kuutoa zilianza lakini tayari alikuwa amefariki dunia. Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.

WAZIRI MKUU APONGEZA JUHUDI ZA TCRA KUSIMAMIA MASAFA

$
0
0
Mkurugenzi wa Masuala ya Kisekta Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Emmanuel Manasseh akitoa maelezo mbele ya Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa kuhusu shughuli za TCRA kwenye banda la maonyesho katika viwanja vya AICC, Arusha. Picha na: TCRA

Na Mwandishi Wetu

Serikali imeitaka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuongeza juhudi katika usimamizi wa Rasilimali za Mawasiliano nchini, zikiwemo namba za mawasiliano ya simu, mfumo wa postikodi na rasilimali adimu za masafa.

Akizungumza kwenye viwanja vya Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa AICC wakati alipotembelea banda la maonesho la TCRA kwenye Mkutano wa Mwaka wa Wataalam wa TEHAMA uliofanyika jijini Arusha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) alisisitiza kuwa ni muhimu TCRA ikaongeza juhudi katika kazi yake nzuri ya kusimamia rasilimali hizo kwa kuzingatia kuwa Tanzania kwa sasa inajielekeza kujenga Uchumi wa Kidijitali unaotegemea sekta pana ya mawasiliano.

Pamoja na maelekezo hayo Waziri Mkuu ameipongeza TCRA kwa kazi nzuri ya kusimamia sekta ya mawasiliano nchini na kusisitiza kuwa rasilimali adimu za masafa zilindwe kwa kadri inavyopaswa. Waziri Mkuu alitoa maelekezo hayo baada ya kupata maelezo ya utendaji wa TCRA kutoka kwa Mkurugenzi wa Masuala ya Kisekta Dkt. Emmanuel Manasseh ambae alimweleza kuwa TCRA inajikita kuhakikisha usimamizi wa rasilimali za mawasiliano hasa rasilimali adimu unafanyika kwa ufanisi mkubwa.

Akiwahutubia washiriki wa Mkutano huo Waziri Mkuu alisisitiza kuwa serikali iko thabiti katika kutekeleza azma yake ya kujenga uchumi wa Kidijitali ifikapo mwaka 2025 huku Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ikiwa nyenzo muhimu ya kufikia azma hiyo.

“Lengo la Serikali ni kuhakikisha tunaimarisha uchumi wa kisasa unaotegemea TEHAMA na ninyi kama wataalam wetu mnayo nafasi ya kutufikisha kwenye uchumi huu” alisisitiza Waziri Mkuu.

Aidha, Waziri Mkuu Majaliwa Majaliwa alibainisha kuwa, serikali ipo tayari kupokea changamoto zote ambazo wataalam hao wataziainisha ili kuzipatia ufumbuzi.

“Nia ya Serikali ni kuhakikisha katika kipindi cha Miaka Mitano ijayo Tanzania inatambulika kote barani Afrika na Duniani kama nchi iliyojiimarisha katika uchumi wa kidijitali”alisisitiza Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu alisisitiza kuwa mifumo yote ya TEHAMA ikiwemo ya kutoa huduma na kuwezesha utendaji wa serikali itawafikia wananchi wote walioko mijini na vijijini, ili kuhakikisha Taifa linafikia azma ya kujenga uchumi wa Kidijitali.

Alibainisha kuwa katika kusambaza huduma kupitia TEHAMA serikali itahakikisha kila kona ya nchi inafikiwa na huduma za intaneti kupitia mkongo wa Taifa

Katika hatua nyingine Majaliwa alibainisha kuwa Serikali ipo katika hatua za awali za kujenga kituo kikubwa cha TEHAMA kitakachowezesha umahiri, ubunifu na utafiti katika sekta ya TEHAMA; kituo hicho kinatarajiwa kujengwa jijini Dodoma.

Kuhusu anuani za makazi Waziri Mkuu aliagiza Wizara ya Habari, Mawasiliano na TEHAMA kuhakikisha inaharakisha mchakato wa kukamilisha uwekaji wa anuani za makazi kote nchini ambazo zitaunganishwa na TEHAMA kutoa huduma kwa wananchi kote nchini.

Akizungumzia uwekezaji kwenye TEHAMA, Waziri Mkuu aliiagiza Wizara kwa kushirikiana na kituo cha uwekezaji nchini kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji kwenye TEHAMA ili kuhakikisha lengo la kujenga uchumi wa Kidijitali linafikiwa mapema.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Ashatu Kijaji akiwasilisha hotuba kwa wataalam wa TEHAMA mbele ya Waziri Mkuu alibainisha kuwa ifikapo mwaka 2025 Tanzania itakuwa imeunganishwa kwa mkongo wa taifa kwa sehemu kubwa.

“wizara imeweka mkakati wa kuhakikisha mkongo wa taifa wa mawasiliano unatandazwa maeneo yote ya nchi ili kuwezesha uzalishaji wa fursa nyingi zaidi za kiuchumi hapa nchini” alibainisha na kusisitiza Waziri Kijaji.

Kijaji alibainisha kuwa serikali imeandaa muongozo wa usajili wa wataalam wa TEHAMA nchini ikiwa ni utekelezaji wa matakwa ya kisera ili kuhakikisha wataalamu wote wa TEHAMA nchini wanasajiliwa kuwezesha azma ya serikali kujenga uchumi wa kidijitali ambapo lengo ni kuhakikisha kabla ya mwaka 2025 angalau wataalam 5000 wa TEHAMA wasajiliwe chini ya mpango huo.

Aidha Wizara imesisitiza nia ya serikali kuwawezesha vijana wabunifu katika TEHAMA kukuza tija na vipaji.

“Tunahitaji kuwekeza kwenye utafiti na kuwashika mkono vijana wetu wanaojishughulisha na TEHAMA” alisisitiza Waziri Kijaji.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mheshimiwa Selemani Kakoso (Mb) alisisitiza umuhimu wa Mamlaka ya Mawasiliano kufikisha elimu kwa umma juu ya matumizi sahihi ya TEHAMA.

Mkutano huo ulioratibiwa na Wizara ya Habari, Mawasiliano na TEHAMA umehudhuriwa na wataalam wa TEHAMA zaidi ya 800 kutoka maeneo mbalimbali nchini na nje ya Tanzania ukilenga kuyaleta pamoja mawazo ya kitaalam katika TEHAMA yatakayowezesha ukuaji wa sekta hiyo; Waziri Kijaji alitumia fursa hiyo kubainisha kuwa mkutano kama huo mwaka 2023 utafanyika Zanzibar.

RAIS ALHAJ DK. MWINYI AFUNGUA IJITIMAI YA KIMATAIFA KIDOTI MKOA WA KASKAZINI UNGUJA

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj. Dk. Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Viongozi wa Dini alipowasili katika Masjid Fiysabilillahi Tabligh Markaz Zanzibar Kidoti Mkoa wa Kaskazini Unguja kwa ajili ya ufunguzi wa Ijitimai ya Kimataifa 2021, inayofanyika leo 22-10-2021.(Picha na Ikulu)
WAUMINI wa Dini ya Kiislam Zanzibar wakiitikia Dua ikisomwa na Amiri Lulu kutoka Dar es Salaam, baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa iliofanyika katika Masjid Fiysabilillahi Tabligh Markaz Zanzibar, kabla ya ufunguzi wa Ijitimai ya Kimataifa iliofanyika leo.(Picha na Ikulu)
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe Haroun Ali Suleiman, akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa Ijitimai ya Kimataifa iliofanyika katika Masjid Fiysabilillahi Tabligh Markaz Zanzibar Kidoti Mkoa wa Kaskazini Unguja.(Picha na Ikulu)
Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi akizungumza kabla ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi, kufungua Ijitimai ya Kimatifa, inayofanyika katika Masjid FDiysabilillahi Tabligh Markaz Zanzibar Kidoti Mkoa wa Kaskazini Unguja.(Picha na Ikuu)RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwahutubia Waumini wa Dini ya Kiislam katika hafla ya Ufunguzi wa Ijitimai ya Kimataifa inayofanyika katika Masjid Fiysabilillahi Tabligh Markaz Zanzibar Kidoti Mkoa wa Kaskazini Unguja leo 22-10-2021.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua maalum iliyosomwa na Amiri Lulu kutoka Gongolamboto Dar es Salaam, baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa na (kulia kwa Rais) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Saleh Omar Kabi na Amiri Mkuu Ali Khamis Mwalim na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria Utumishi na Utawala Bora Mhe.Haroun Ali Suleiman.(Picha na Ikulu)

MAJALIWA: SERIKALI IMETENGA SH. BILIONI 170 UJENZI MKONGO WA TAIFA

$
0
0

 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Wadau wa Sekta ya TEHAMA wakati alipofungua Mkutano wa Tano wa Mwaka wa TEHAMA Tanzania uliofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC) jijini Arusha, Oktoba 22, 2021.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan imetenga shilingi bilioni 170 kwa ajili ya ujenzi wa Mkongo wa Taifa katika mwaka wa fedha 2021/2022.

“Lengo letu ni kuwawezesha watoa huduma za mawasiliano kutumia miundombinu hii kuboresha huduma za mawasiliano nchini na kurahisisha ufikishwaji wa intaneti kwenye ofisi mbalimbali za sekta ya umma na binafsi”

Ameyasema hayo leo (Ijumaa, Oktoba 22, 2021) wakati alipofungua Mkutano wa Tano wa Mwaka wa TEHAMA Tanzania uliofanyika katika katika ukumbi wa mikutano wa AICC, jijini Arusha. Amesema fedha hizo zitawezesha kujenga kilomita 4,244 za Mkongo ili kufikisha jumla ya kilomita 12,563.

Mheshimiwa Majaliwa ametumia fursa hiyo kuiagiza Wizara ya Habari, Sayansi na Teknolojia ya Habari isimamie kwa karibu mradi wa upanuzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ili wananchi wengi zaidi washiriki katika ujenzi wa uchumi wa kidijitali.

“Hivi sasa Serikali imejenga kilomita 8,319 za Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano hadi mwezi Septemba 2021. Malengo yetu kama Serikali ni kujenga hadi kilomita 15,000 ifikapo mwaka 2024/2025. Hili linahitaji uwekezaji mkubwa na Serikali imejipanga kuwekeza vilivyo lakini pia tunakaribisha wabia na wawekezaji katika eneo hili pamoja na maeneo mengine ya TEHAMA.”

Amesema kuwa miundombinu ya TEHAMA ni uti wa mgongo wa maendeleo ya kidijitali, hivyo nchi inahitaji kuongeza idadi ya watumiaji wa intaneti kufikia zaidi ya asilimia 80 nchi nzima kutoka asilimia 45. “Serikali imejiwekea lengo la kuongeza mtandao wa urefu wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ili kufikisha huduma bora na zenye gharama nafuu kwa wananchi wote.”

Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa katika kipindi cha miaka mitano ijayo Serikali imedhamiria kuipeleka Tanzania kwenye ramani ya Ulimwengu kama moja ya nchi ambayo TEHAMA imeleta mageuzi makubwa ya kiuchumi.

Pia, Waziri Mkuu ameiagiza Tume ya TEHAMA ihakikishe inaweka mikakati mahsusi ya kusajili wataalamu wa TEHAMA ili kufikia lengo la usajili wa wataalamu 5,000 ifikapo mwaka 2025.

“Wizara ya Habari, Sayansi na Teknolojia ya Habari pia ishirikiane na Sekta binafsi katika kuongeza ufanisi wa kiutendaji. Angalieni pia uwezekano wa kufanya kazi na makampuni makubwa yaliyobobea katika sekta hii ili kujenga uchumi wa kidijitali.”

Baada ya kufungua mkutano huo Mheshimiwa Majaliwa pia amezindua mwongozo wa usajili wa wataalamu wa TEHAMA na kutoa vyeti kwa baadhi ya wataalamu wa TEHAMA ambao wamesajiliwa.

Mhe. Majaliwa pia ameitaka Wizara ya habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari washirikiane na Eizara ya mambo ya ndani katika kuhakikisha wanaweka Kamera za Usalama katika miji ili kukabiliana na changamoto ya uhalifu

Naye, Waziri wa Habari, Sayansi na Teknolojia ya Habari Dkt. Ashatu Kijaji amesema wizara yao imejipanga kujenga kituo mahiri cha kukuza utaalamu na tafiti nchini ambacho kitajengwa jijini Dodoma kwa kupitia Mradi wa Tanzania ya Kidijitali “Digital Tanzania”.

Amesema Wizara yao itakuwa mstari wa mbele kwa upande wa masuala ya kidijitali kwa kuangalia na kushauri sheria, kanunina na taratibu hitajika ili ziweze kuchochea na kuvutia ubunifu wa bidhaa na huduma za kidijitali zenye tija kiuchumi na zinazozingatia maadili ya Taifa.

Pia, Dkt. Kijaji amesema katika kuchochea ujenzi wa Taifa la kidijitali, wamebuni utaratibu wa kutoa tuzo maalum kwa wizara, idara, halmashauri, taasisi, kampuni na wabunifu wanaofanya kazi nzuri na jamii ikanufaika na matunda ya kazi na ubunifu wao kupitia TEHAMA.

Miongoni mwa waliotunukiwa tuzo ni pamoja na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kulibeba suala la TEHAMA kwa nguvu zake zote na kuliweka kwenye vipaumbele vya Serikali ya awamu ya sita ambayo anaiongoza.

Amesema wizara yao inaamini kwa kupitia utaratibu huo utakaokuwa unafanyika kila mwaka utatoa ushawishi mkubwa hasa katika eneo la ubunifu na kuchochea matumizi ya kidijitali ili Tanzania iweze kuwa Taifa la kidijitali.


BITEKO ARAHISISHA BIASHARA YA MADINI ULANGA

$
0
0
Waziri wa Madini Doto Biteko Akizungumza na wadau mbalimbali katika Tamasha la Kuhamasisha Fursa za Uwekezaji katika wilaya ya Ulanga iliyofanyika tarehe 22 Oktoba, 2021
Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Ngollo Malenga Akizungumza na wadau mbalimbali katika Tamasha la Kuhamasisha Fursa za Uwekezaji katika wilaya ya Ulanga iliyofanyika tarehe 22 Oktoba, 2021
Waziri wa Madini Doto Biteko akitiembelea mabanda mbalimbali wakati Akifungua Tamasha la Kuhamasisha Fursa za Uwekezaji wilayani Ulanga


Ulanga yaainisha fursa za uwekezaji Sekta ya Madini

Na Steven Nyamiti-WM

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameiagiza Tume ya Madini kuanza kutoa vibali vyote vya madini kwa wafanyabiashara wa madini katika eneo la Mahenge Ulanga ili kuondoa usumbufu wa kusafiri umbali mrefu wa zaidi ya kilomita 300 hadi mkoani Morogoro kwa ajili ya kufunga mizigo yao.

Ameelekeza agizo hilo lianze kutekelezwa Novemba Mosi, 2021 ili wafanyabiashara wa madini wapate huduma zote muhimu kuanzia kufanyiwa uthaminishaji, upimaji, ukataji, ufungaji na uongezwaji wa thamani ili manufaa hayo yabaki kwa wananchi wa Ulanga.

Waziri Biteko ametoa agizo hilo leo Oktoba 22, 2021 wakati akifungua Tamasha la Kuhamasisha Fursa za Uwekezaji linalofanyika katika Wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro.

Aidha, Waziri. Biteko amesema, mchakato wa kuanzisha Mkoa wa Kimadini wa Mahenge Ulanga unaendelea ili kurahisisha shughuli za uchimbaji wa madini kwa wanachi wa Mahenge kwa kuwasogezea huduma karibu.

Akizungumzia umuhimu wa Sekta ya Madini, Waziri Biteko amesema kuwa,uwepo wa shughuli za madini zina mchango mkubwa katika maendeleo ya Taifa, hususan katika utoaji wa ajira na mapato yatokanayo na shughuli hizo.

“Uwepo wa shughuli za madini zina mchango mkubwa sana kwa maeendeleo ya Taifa, hasa katika utoaji wa ajira na mapato yatokanayo na shughuli hizo,”amesema Waziri Biteko.

katika kuhamasisha Fursa za Uwekezaji, Waziri Biteko amepongeza uongozi wa Wilaya ya Ulanga kwa kuanzisha na kufanikisha Tamasha la Kuhamasisha Fursa la Uwekezaji kwa kushirikiana na wadau wengine.

Amesema, kupitia tamasha hilo, kutachochea uwekezaji katika Wilaya ya Ulanga kwa kwa kuleta maendeleo ya kwa wananchi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ulanga, Bi. Ngollo Malenya amesema, Wilaya ya Ulanga ina fursa za uwekezaji katika uchimbaji wa madini, ubia na wamiliki wa leseni za maeneo ya madini ambao wana leseni lakini hawana mitaji, vifaa na teknolojia ya uchimbaji wa madini.

“Kuna fursa ya kuanzisha viwanda vidogo na vikubwa vya kukata na kuchakata madini, kutoa huduma katika migodi, mikopo kwa wachimbaji wakubwa na wadogo na kunufaika na Soko la Madini la Ulanga,”amesisitiza Malenya.

Aidha, ameeleza madini yanayopatikana katika Wilaya ya Ulanga ni pamoja na madini ya Kinywe (graphite) ambapo madini hayo yamekuwa yakihitajika sana duniani katika utengenezaji wa betri, madini ya Spinel, Rubi na Dhahabu.

Tamasha la Kuhamasisha Fursa za Uwekezaji linalofanyika katika Wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro linakwenda na Kauli Mbiu isemayo “Amazing Ulanga” kauli mbiu inayoashiria uhalisia wa Wilaya ya Ulanga.

Aidha, tamasha hilo limehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, wakuu wa wilaya na wadau mbalimbali wa sekta nyingine ili kujadili kwa pamoja fursa za maendeleo zinazopatikana katika Wilaya ya Ulanga.

TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE YAIBUKA KINARA MATUMIZI YA TEHAMA SEKTA YA AFYA

$
0
0
Na: Mwandishi wetu – Arusha

23/10/2021 Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imepewa tuzo ya Taasisi ya mabadiliko Tehama bora katika utoaji wa huduma za afya nchini.

Tuzo hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Zainab Chaula wakati wa kongamano la tano la siku tatu kwa maafisa TEHAMA Tanzania lililomalizika Jana Jijini Arusha.

Akizungumza wakati wa kufunga kongamano hilo Bi. Chaula alisema kuwa JKCI ni miongoni mwa Taasisi za serikali ambayo inatoa huduma nzuri ya matibabu ya moyo kwa wagonjwa kupitia mifumo ya Tehama.

“Lengo la serikali ni pamoja na kuiwezesha nchi ya Tanzania kuendana na kasi ya mabadiliko ya Tehama duniani jambo ambalo JKCI inalifanya kuendana na matumizi ya Tehama”, alisema Bi. Chaula.

Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hiyo Mkuu wa Kitengo cha Tehama wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Raymond Machary aliishukuru serikali kwa kutambua na kuthamini huduma zinazotolewa na Taasisi hiyo kupitia mfumo wa Tehama.

Machary ambaye pia ni mbobezi kwenye tasnia ya Tehama alisema hivi sasa taasisi hiyo imekua ikitoa huduma zake nyingi ikiwemo huduma za wagonjwa kupitia mfumo wa Tehama na kupunguza matumizi ya karatasi.

“Kwa takwimu za wagonjwa wanaofika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete kwa mwezi ni takribani 9000 na zaidi ambapo kwa siku ni wastani wa wagonjwa 300 hadi 500. Kutokana na idadi hii ya wataka huduma kuwa kubwa suala la matumizi ya Tehama halikuweza kuepukika”,

“JKCI pamoja na mambo mengine, ilifanya maamuzi ya kusudi kuwa Tehama itumike katika uendeshaji wa Taasisi hivyo kuifanya kuwa chachu ya kuboresha huduma zinazotolewa, haikuwa kazi kubwa kwa Idara ya Tehama kuhakikisha Tehama inatumika kwenye maeneo yote ya ofisi hivyo kurahisisha huduma na kupunguza gharama za karatasi na muda”, alisema Machary.

Aidha Machary alisema kuwa kutokana na mwamko mkubwa wa matumizi ya Tehama, Idara ya Tehama iliweza kuandaa mifumo mingi ambayo inatumika hadi sasa na Taasisi hiyo ikiwa ni pamoja na mfumo wa utoaji wa huduma za kitabibu (eHealth), usimamizi wa vifaa na madawa, mfumo wa kukusanya changamoto za mifumo, mifumo kwa ajili ya tafiti ndogo ndogo, pamoja na mfumo wa kukusanya changamoto za wagonjwa.

“Mifumo iliyopo mingi iliandaliwa na wataalamu wa ndani kulingana na mahitaji yetu, mifumo yote iliyoandaliwa imeleta mafanikio na tija kubwa kwa Taasisi yetu”,

“Mafanikio haya yote ni kutokana na dhamira ya serikali kuona umuhimu wa Tehama, tunaishukuru sana Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, tume ya Tehama, Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mamlaka ya Serikali Mtandao kwa kushirikiana na Taasisi yetu kuongeza ubunifu katika kutoa huduma bora kwa watanzania”, alisema Machary.


MWISHO –

DC JOKATE ATOA MAELEKEZO KWA TANROADS ,TARURA BAADA YA AMEND KUWEKA ALAMA ZA BARABARANI SHULE YA MSINGI MADENGE, RUVUMA

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam Jokate Mwegelo akiwa na wanafunzi wa Shule za Msingi Madenge na Ruvuma pamoja na maofisa kutoka TARURA, na Amend wakati akikata utepe kuashiria kuzindua alama za usalama barabarani katika Shule hizo ambazo zimetengengenezwa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Amend.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam Jokate Mwegelo akizungumza wakati wa uzinduzi wa alama za barabarani kwa Shule ya Msingi Madenge na Ruvuma zilizopo katika wilaya hiyo.Alama hizo zimewekwa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Amend .

Na Mwandishi Wetu

MKUU wa Wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam Jokate Mwegelo, ametoa maelekezo kwa Wakala wa Barabara (TANROADS) na Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA), kuzingatia uwekaji wa alama za usalama barabarani katika maeneo ya shule wakati wa kiandaa michoro ya ujenzi wa barabara hizo na katika utekelezaji wake.

Aliyasema hayo, Dar es Salaam, alipokuwa akizindua alama za usalama barabarani katika Shule za Madenge na Ruvuma wilayani humo, ambazo zimetengengenezwa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Amend huku akitaka pia jeshi la Polisi wilayani humo, kuhakikisha linasimamia kikamilifu masuala ya usalama barabarani huku akisisitiza pia jamii kufuata sheria hizo.

“Naelekeza TARURA na TANROADS, wakati mkiandaa michoro ya barabara na katika utekelezaji mzingatie kuweka alama hizi katika maeneo muhimu hasa ya shule. Zingatieni hili ili tupunguze ajali hizi zinazosababisha vifo na ulemavu,”amesema.

Kuhusu Jeshi la Polisi Jokate ameisitiza wasimamie kikamilifu sheria za usalama barabarani na kuchukua hatua stahiki kwa watu wanao vunja sheria hizo.

“Serikali yetu inaboresha kwa kiasi kikubwa barabara .Wilaya yetu ya Temeke pia imepata barabara nzuri. Lakini halii imekuwa changamoto. Watu hawazingatii sheria za usalama barabarani. Wanaendesha vyombo vya usafiri kwa kasi bila kujali kuna watumiaji wengine wa barabara,”amsema.

Akiizungumzia Amend, Jokate amewapongeza kwa ujitolea kuweka alama za barabarani katika maeneo ya shule hizo za Madenge na Ruvuma pamoja na kutoa elimu kwa wanafunzi na watumiaji wa barabara.

“Amend kwa kweli mmetusaidia mno Temeke.Mmelinda uhai wa watoto wetu.Mmefanya jambo zito na niwahakikishie serikali itaunga mkono jitihada zenu hizi kwa asilimia miamoja,”alieleza Jokate.

Kwa upande wake Meneja wa Amend hapa nchini, Simon Kalolo, amesema wamekuwa wakijitolea kutoa elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi katika mikoa mbalimbali nchini na kuweka alama hizo ili kuzua ajali.

“Dhamira yetu ni kuona wanafunzi ,wadau wa elimu na jamii yote inakuwa salama dhidi ya ajali za barabarani. Katika shule za Madenge n a Ruvuma, tumejitolea kuandaa michoro ya usalama barabarani, vivuko na kuwapa elimu wanafunzi ili wawe mabalozi wazuri wa usalama barabarani, “amefafanua Kalolo.

Wakati Diwani wa Kata ya Temeke, Omari Babu, ametumia nafasi hiyo kuipongeza Amend kwa msaada wa alama hizo na kueleza kuwa zitasaidia kupunguza ajali za barabarani huku akiitaka jamii kuzingatia sheria.

TANZANIA YANG’ARA MCHEZO WA KARATE NCHI ZA MAZIWA MAKUU

$
0
0
 
Na Mwandishi Maalum, DRC

Timu ya Taifa ya Karate ya Tanzania imeng’ara katika mashindano ya kimataifa ya Karate kwa Nchi za Maziwa Makuu yaliyofanyika nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na kumalizika leo Jumamosi.

“Kwa ujumla tumepata medali 27 kwa categories tofauti tofauti ambapo wanawake wameleta medali 13 na wanaume ni medali 14,” alisema kiongozi wa Chama cha Karate nchini na kuongeza:

“Katika medali hizo tuna Gold 7, Silver 8 na Bronze 12.” Timu hiyo iliondoka nchini kupitia Rwanda baada ya Serikali ya Tanzania kupitia Wizara yenye dhamana na Michezo kukwamua changamoto ya usafiri na vibali kwa ajili ya Timu hiyo kuvuka kupitia mpaka wa Rwanda uliokuwa umefungwa.

WAZIRI NDUMBARO “KAMPENI YA ROYAL TOUR HAIPOI, TUNAKUJA NA MKUTANO WA MASOKO NA UTALII WA KIMATAIFA”

$
0
0
Waziri wa Maliaslili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza kuhusiana na kufanyika kwa mkutano wa kimataifa wa utalii na masoko wakati akifanya mahojiano maalum ya jinsi Wizara ya Maliasili na Utalii ilivyojipanga kutangaza vivutio vya utalii ilivyonavyo kimataifa kwa lengo la kuongeza idadi ya watalii nchini kutoka watalii milioni 1.5 hadi kufikia watalii milioni 5 kama ilani ya CCM inavyoelekeza ifikapo mwaka 2025

Kabla ya Kipindi maalum cha kutangaza utalii maarufu cha ‘Royal Tour’ kilichoanzishwa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan hakijapoa kwa mara nyingine tena Wizara ya Maliasili na Utalii imesema inatarajia kufanya mkutano mkubwa wa Kimataifa wa Utalii na Masoko (Tourism Marketing) katika Jiji la Arusha, wiki ya pili ya mwezi Novemba mwaka huu.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro ametoa kauli hiyo leo Jijini Dar es Salaam wakati akifanya mahojiano maalum ya jinsi Wizara hiyo ilivyojipanga kutangaza vivutio vya utalii ilivyonavyo kimataifa kwa lengo la kuongeza idadi ya watalii nchini kutoka watalii milioni 1.5 hadi kufikia watalii milioni 5 kama ilani ya CCM inavyoelekeza ifikapo mwaka 2025

Waziri Ndumbaro amesema lengo la mkutano huo utakaofanyika kwa muda siku mbili utajadili namna ya kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini kwa kuwakutanisha wadau wa utalii wa ndani na nje ya nchi wakiwemo wamiliki wa makampuni ya Kimataifa ya kutangaza utalii duniani pamoja na Wataalam kutoka Shirika la Umoja wa Kimataifa linaloshughulikia masuala ya utalii Duniani ( UNWTO)

Akizungumzia Washiriki hao, Dkt.Ndumbaro amesema mkutano huo wa kimataifa utatoa fursa kwa Washiriki duniani kote hata kwa wale watakaoshindwa kufika nchini wataweza kushiriki kwa njia ya mtandao pia.

Akizungumzia sababu iliyopelekea Wizara hiyo kuamua kufanya mkutano huo, Dkt.Ndumbaro amesema kama nchi imejaliwa kuwa na vivutio vingi vya utalii na vya kipekee ambavyo havipatikani mahali popote duniani isipokuwa Tanzania lakini vivutio hivyo vimekuwa havijulikani Kimataifa.

” Nilipofika Wizarani baada ya kufanya kazi kwa muda wa mwezi mmoja tu nikawambia wenzangu kwamba kama ningekuwa natoa ‘marks’ kwenye maeneo mawili kwenye uhifadhi na utalii, kwenye uhifadhi ningetoa marks mia kwa mia lakini kwenye utalii ningetoa moja ya mia kwani kwa vivutio vya utalii tulivyonavyo Tanzania tumeshindwa kuvitangaza, tungevitangaza vizuri mapato yetu yangekuwa sio ya hapa” amesisitiza Dkt.Ndumbaro.

Dkt.Ndumbaro amesema nchi ya Tanzania katika suala la vivutio vya utalii ipo vizuri ila kwenye suala la ”marketing” ya vivutio vya utalii haipo vizuri

“Tunaona kwenye suala la kujitangaza ndio kuna ugonjwa ndio maana Mimi na Wenzangu tunajitahidi kupigania kuleta mikutano mikubwa ifanyike nchini pamoja na kuanzisha mazao mengine ya utalii kama njia kutangaza vivutio vya utalii tulivyonavyo” amesisitiza Dkt.Ndumbaro.

Dkt.Ndumbaro amesema uamuzi wa kufanya mkutano huo wa masoko na utalii ni moja ya mikakati maalum ambayo kama Wizara ni kuhakikisha jitihada alizozianzisha Rais Samia Suluhu Hassani za kuitangaza utaliii nchini kupitia kipindi chake maarufu cha “Royal Tour” hazipoi na kusisitiza kuwa kampeni hiyo inazidi kuwa ya moto kila kukicha.

Kufuatia hali hiyo, Dkt.Ndumbaro ametoa wito kwa sekta binafsi kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhakikisha mkutano huo unafanikiwa kufanyika ili sekta ya utalii iweze kuinuka tena kufuatia wimbi la UVIKO -19

Amesema mkutano huo utakuja na mbinu mbadala kwa kuhakikisha sekta ya utalii nchini inapaa kwa kuyafanyia kazi mawazo yatakayotolewa katika mkutano huo haraka kadiri iwezekanavyo ili kuongeza idadi ya watalii wa ndani na nje ya nchi.

Katika hatua nyingine, Dkt.Ndumbaro amesema kufanyika kwa mkutano huo kutasaidia kujua udhaifu upo wapi katika kutangaza vivutio vya utalii nchini kwa kuweza kuondokana na taswira mbaya ambayo muda mwingine imekuwa ikifanywa na baadhi ya watu kwa maslahi yao binafsi

Amesema kuna baadhi ya watu wamekuwa wakiharibu taswira ya nchi kwa maslshi yao binafsi na huku wengine kwa sababu za kisiasa bila kujua hali hiyo imekuwa ikiiathiri sekta ya utalii moja kwa moja.

” Kuna baadhi ya Watanzania ambao ni wapuuzi wamekuwa wakijisikia fahari kuisema nchi yake vibaya na kuisifia nchi nyingine vizuri” alisitiza Dkt.Ndumbaro.

MTAMA WAINGIZIA WAKULIMA SH.BILIONI 9

$
0
0
Mkuu wa Ofisi Ndogo ya Shirika la Mpango Chakula Duniani (WFP), Neema Mina Sitta akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Program ya Kilimo Himilivu cha Mtama (CSA), ilivyotengeneza mamilionea kwenye wilaya za Bahi, Kongwa na Mpwapwa mkoani Dodoma.
Ofisa Ufuatiliaji Msaifizi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), William Laswai akimuonesha Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Mwananchi, Janeth Joseph Mtama bora uliozashwa na wakulima wa mkoa wa Dodoma kupitia Program ya Kilimo Himilivu cha zao hill.

Na Mwandoshi Wetu, Dodoma

WAKULIMA 22,000 wa zao la Mtama, kutoka Wilaya za Kongwa, Bahi na Mpwapwa, wameuza tani 17,000 za zao hilo kwa msimu wa mwaka huu na kufanikiwa kujipatia Sh bilioni 9.

Wakulima hao wamenufaika na kilimo hicho kupitia Program ya Kilimo Himilivu cha Mtama (CSA), inayotekelezwa na Mpango wa Chakula Duniani (WFP), kupitia Mpango Mkakati wa 2017 hadi 2022.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa mwishoni mwa wiki, Mkuu wa Ofisi Ndogo ya WFP, Neema Mina Sitta alisema kwa sasa wamefikia vijiji 203 kati ya zaidi ya 700 vilivyopo.

Alisema WFP ni mpango ambao unafanya kazi kwa mtazamo wa kibinadamu kama kusaidia sekta ya kilimo, maendeleo, wakimbizi, afya na lishe ambapo kwa Dodoma wameweza kusaidia wakulima wa zao la Mtama kuongeza usalishaji.

Sitta alisema WFP iliandika mradi wa kilimo himilivu katika wilaya za mkoa wa Dodoma na kupata ufadhili wa Sh. bilioni 1.7 kutoka Shirika la Maendeleo la Ireland (Irish Aid) ambapo matunda yameshaonekana kwa wakulima zaidi 22,000 kujpatia Sh bilioni 9.

Alisema uamuzi wa WFP kuingia katika kilimo himilivu cha Mtama wameweza kuunganisha wakulima na soko moja kwa moja na kuondoa madalali au watu wac katikati walikuwa wanachangia kushusha bei ya zao.

Mkuu huyo alisema kwa sasa bei ya zao la Mtama kilo moja inaunzwa hadi Sh 550 kutoka Sh 250 ya awali hivyo kuongeza kipato kwa wakulima na kuhamsisha kilimo hicho.

Alisema wamekuwa wakitoa elimu kwa wakulima namna ya kulima kilimo bora na endelevu ambacho kitaweza kuingiza mapato yao na nchi.

Sitta alisema kilimo cha Mtama ambacho kinalimwa katika mkoa wa Dodoma kinazingatia mfumo wa kilimo hai jambo ambalo linachangia kuwepo na uhakika wa soko kote duniani.

Mkuu huyo wa ofisi ndogo alisema ushiriki wao kwenye kilimo ni kuhakikisha mkulima ananufaika na kilimo lakini pia ardhi inakuwa endelevu kwa vizazi vijavyo.

“WFP kupitia ufadhili wa Irish Aid, tumefanikiwa kuongeza uzalishaji wa zao la Mtama ambapo kwa msimu huu wakulima wamezalisha zaidi ya tani 17,000 na kujipatia Sh bilioni 9 lakini hitaji ni kubwa zaidi hasa kutoka ndani na nchini Sudani Kusini,” alisema.

Alisema kwa msimu ujao wanatarajia uzalishaji kuongezeka kutokana na kuongezeka kwa wilaya za Chemba, Kondoa, Dodoma na Chamwino.

Sitta alisema katika kutekeleza CSA wamekuwa wakishirikiana na Serikali kwa kutumia watalam wao wa kilimo hali ambayo inaleta ufanisi mzuri.

Halikadhalika alisema wamepokea ombi la Serikali katika kuanzisha program zakuongeza uzalishaji kwenye zao la alizeti ambapo matarajio yao ni kuingiza kwenye Mpango Mkakati wa WFP wa 2022 hadi 2027.

Aidha, alisema WFP imekuwa ikinunua mazao mengine kama mahindi kwa ajili ya kupeleka katika ofisi za WFP za nchi nyingine na kwenye kambi za wakimbizi za Nduta na Nyarugusu.

Sitta alisema hadi sasa wamefanikiwa kununua zaidi ya tani laki saba kwa ajili ya kusambaza katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi.

WATUMISHI WAPYA SEKTA YA UJENZI WAFUNDWA

$
0
0
Afisa Utumishi Mkuu kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Bw. Stanley Madyaga, akiwaasa watumishi wapya wa Sekta hiyo (hawapo pichani), kufanya kazi kwa ubunifu na nidhamu wakati wa semina elekezi iliyofanyika jijini Dodoma.
Afisa Utumishi kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Bi. Hindu Augossy (kulia), akizungumzia umuhimu wa watumishi wapya kufuata maadili ya utumishi wa umma katika semina elekezi iliyoandaliwa na Sekta hiyo kwa waajiriwa wapya jijini Dodoma. Kushoto ni Bi. Esther Mwina, Afisa Utumishi akifuatilia.
Baadhi ya watumishi wapya wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), wakifuatilia semia elekezi kutoka kwa mtaalam kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma (hayupo pichani), jijini Dodoma.
Afisa Utumishi Mkuu kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Bw. Stanley Madyaga (wan ne kushoto), katika picha ya pamoja na watumishi wapya wa Sekta hiyo mara baada ya kufungua rasmi semina elekezi, jijini Dodoma.

RAIS DKT.MWINYI AZUNGUMZA NA MABALOZI WALIOTEULIWA KUIWAKILISHA TANZANIA NCHI ZA NJE

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akizungumza na Mabalozi waliopishwa hivi karibuni kwenda kuiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tannzania katika Nchi mbali mbali walipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha leo (pichani wa pili kulia) Mhe.Balozi Anisa Mbega Nchini India (katikati) MheInnocent Shiyo Nchini Afrika ya Kusini na (kushoto) Mhe.Togolani Mavura Nchini Korea Kusini
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akizungumza na Mabalozi waliopishwa hivi karibuni kwenda kuiwakilisha Tannzania Nchi mbali mbali walipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi waliopishwa hivi karibuni kwenda kuiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tannzania Nchi katika mbali mbali walipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha leo,(kushoto) Mhe.Balozi Togolani Mavura Nchini Korea Kusini,Mhe.Anisa Mbega Nchini India na Mhe.Innocent Shiyo Nchini Afrika ya Kusini pia na Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Injinia Zena Ahmed Said (kulia).[Picha na Ikulu

#TheJoint Se. 01 Ep. 11 Guest Starring: Lulu Diva & Bi. Chau

#TheJoint Se. 01 Ep. 13 Guest Starring: Navy Kenzo(Nahreel & Aika)

PITA PITA YA VIJIMAMBO BLOG USO KWA MACHO NA NY EBRA AKIWA KWENYE HARAKATI ZA NAWAZA TU 2025..

$
0
0
Hapa ni Ny Ebra Akiwa na wananchi baada ya kuwaandalia bonanza la mpira wa miguu hii ni katika harakati za kuchukua jimbo 2025. Ny Ebra ni mdau mkubwa wa mpira wa miguu kwaiyo ndo maana kwake imekuwa rahisi kuanza na jambo hili kwa kuwakusanya vijana pamoja na kuwatengenezea mazingira ya umoja. Bonanza hili lilikutanisha timu ya veterani na vijana na mshindi alipata mipira na jersey kwa timu zote baada ya mchezo. Na jambo hili litakuwa endelevu kwani kutakuwa na ligi itakayo shirikisha timu za maeneo hao. Ligi hiyo itaitwa  #NAWAZA TU 2025# Kwa taswira zaidi nenda chini.

Ny Ebra akiwaonesha vijana kuwa na yeye bado yumo licha ya umri kusogea machweo.

Ny Ebra akipata ukodak na timu zote mbili kabla ya mchezo kuanza, Ny Ebra anatema huu ni mwanzo tu
 

VIONGOZI WA SKIMU ZA UMWAGILIAJI WATAKIWA KUSIMAMIA UKUSANYAJI WA ADA NA TOZO.

$
0
0

 Na Mwandishi Wetu – Pawaga Iringa.


Mhandisi wa Umwagiliaji Mkoa wa Iringa ONESMO KAHOGGO amewataka viongozi katika Skimu za Umwagiliaji kusimamia kikamilifu zoezi la ukusanyaji ada na tozo kwa lengo la kutunisha mfuko wa Umwagiliaji.

Akizungumza mjini IRINGA Bw, KAHOGGO amesema endapo wakulima katika Skimu za Umwagiliaji watachangia fedha za ada ya usajili na matunzo kwa wakati, itasaidia kuharakisha ukarabati wa Skimu zilizoharibika kutokana na athari zitokanazo na madhara ya mabadiliko ya tabia nchi pamoja na kujenga Skimu mpya nchini.

Ametolea mfano zoezi la kuurejesha mto Ruaha Mdogo katika njia yake ya asili limegharimu fedha kutoka mfuko wa Umwagiliaji ambao unahitaji kuwezeshwa na wakulima hao.

Kwaupande wake Bi, KATARINA RASHIDI MLAGA mkulima mkazi wa kijiji cha Magozi ameishukuru serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kwa kazi kubwa iliyofanya wa kurejesha mto Ruaha Mdogo katika njia yake ya asili, nakusema kuwa wakulima katika kijiji hicho hutegemea Zaidi kilimo cha umwagiliaji, na wamepata elimu ya kutosha kuhusu uchangiaji wa tozo za umwagiliaji na wapo tayari kuchangia.

Awali akiongea kijijini hapo Diwani wa kata ya ILOLO MPYA Bw, FUNDA MIHAYO amemshukuru Mkurugenzi wa Tume ya taifa ya Umwagiliaji Bw, DAUDI KAALI kwa kuwezesha wataalam wa tume kurekebisha miundombinu ya mifereji ya kupeleka maji katika mashamba ya wakulima pamoja na zoezi la usanifu linaloendelea katika Skimu ya Liganga ambapo lengo ni kuwezesha maji kunyweshea Skimu ya Magozi na Mkombilenga.


Mhandisi Umwagiliaji Mkoa wa Iringa Bw. Onesmo Kahoggo akingumza kuhusu Viongozi wa skimu za kilimo cha Umwagiliaji Nchini, kusimamia ukusanyaji wa ada na Tozo za Umwagiliaji.
Bi Katarina Rashid Mlaga, mkulima mkazi wa kijiji cha Mgozi akiishuru Serikali kwa kurejesha mto Ruaha Mdogo katika njia yake ya asili.
Picha Ikionesha mto Ruaha mdogo baada ya kurejeshwa katika njia yake ya asili.

Picha ikionesha Roli la kubebea mchanga likiwa kazini wakati wa ukarabati wa mto Ruaha mdogo.
Viewing all 45984 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>