Quantcast
Channel: VIJIMAMBO
Viewing all 45984 articles
Browse latest View live

MAJALIWA: VIONGOZI WA DINI ENDELEENI KUIUNGA MKONO SERIKALI

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza wakati wa tukio la uzinduzi wa mradi wa Kanisa Katoliki wa mapambano dhidi ya UVIKO 19, unaofadhiliwa na Serikali ya Marekani, katika hospitali ya Cardinal Rugambwa iliyopo Ukonga, Dar es Salaam, Oktoba 27, 2021. Kulia ni Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania Askofu Mkuu Gervas Nyaisonga na katikati ni Balozi wa Marekani nchini Donald Wright. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua mradi wa Kanisa Katoliki wa mapambano dhidi ya UVIKO 19, unaofadhiliwa na Serikali ya Marekani, katika hospitali ya Cardinal Rugambwa iliyopo Ukonga, Dar es Salaam, Oktoba 27, 2021. Wengine kutoka kushoto ni Jane Manyahi Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Cardinal Rugambwa na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na uzazi, Balozi wa Marekani nchini Donald Wright, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania Askofu Mkuu Gervas Nyaisonga, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Dkt. Godwin Mollel na kulia ni Mbunge wa Ukonga Jerry Slaa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiagana na Balozi wa Marekani nchini Donald Wright wakati wa tukio la uzinduzi wa mradi wa Kanisa Katoliki wa mapambano dhidi ya UVIKO 19, unaofadhiliwa na Serikali ya Marekani, katika hospitali ya Cardinal Rugambwa iliyopo Ukonga, Dar es Salaam, Oktoba 27, 2021. kushoto ni Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania Askofu Mkuu Gervas Nyaisonga na watatu kushoto ni Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Stephano Msomba. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa wito kwa viongozi wa dini nchini waendelee kuiunga mkono Serikali katika mapambano ya UVIKO 19 sambamba na kuelimisha umma umuhimu wa kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo.

Amesema hadi kufikia tarehe 22 Oktoba 2021, jumla ya wananchi 981,297 walikuwa wamechanjwa na jumla ya wagonjwa 26,154 na vifo 725 vilitolewa taarifa tangu ugonjwa huo uliporipotiwa kuingia nchini kwa mara ya kwanza tarehe 19 Machi 2020.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano, Oktoba 27, 2021) wakati akizindua Mradi wa Mpango wa Kanisa Katoliki wa Mapambano dhidi ya UVIKO-19 katika Hospitali ya Cardinal Rugambwa iliyopo Ukonga, Dar es Salaam.

Mradi huo unatekelezwa kupitia vituo 12 vya kutolea huduma za afya vya Kanisa Katoliki vilivyopo kwenye maeneo mbalimbali nchini ili kusaidia kujaziliza kazi kubwa inayofanywa na Serikali katika kudhibiti maambukizi ya UVIKO 19.

Amesema licha ya Tanzania kuudhibiti mlipuko huo, bado ugonjwa upo na wagonjwa pamoja na vifo vinavyotokana na ugonjwa huo vinaendelea kufuatiliwa na kutolewa taarifa huku Serikali ikitekeleza afua mbalimbali za kupambana na janga hilo pamoja na kuimarisha uchumi na huduma za jamii.

“Hivyo basi, tuendelee kuchukua tahadhari za kujikinga na ugonjwa huu kwa kujijengea utamaduni wa kuvaa barakoa safi na salama, kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni au kutumia vitakasa mikono pamoja na kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima.”

TANZANIA INATARAJIA KUWAKILISHA TAARIFA YAKE YA UTEKELEZAJI WA HAKI ZA BINADAMU.

$
0
0
Na Mwandishi wetu,

Tanzania inatarajia kuwakilisha taarifa yake ya utekelezaji wa haki za binadamu na kufanyiwa tathimini chini ya mfumo wa Umoja wa Mataifa kwa kipindi maalum (Universal Periodic Review-UPR) huko Geneva kuanzia tarehe 1-12 Novemba 2021.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula(Mb) ameyasema hayo Mkoani Morogoro wakati akifungua mafunzo ya watendaji waandamizi wa Taasisi za Serikali zinazosimamia haki za binadamu kuhusu kuongeza utekelezaji wa tamko la Marrakesh.

Ameongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imedhamiria kutekeleza wajibu wake wa kikatiba na kutekeleza wajibu ilionao kupitia Mikataba ya Kimataifa na kikanda ambayo imeridhia na kwamba inatambua umuhimu wa watetezi wa haki za binadamu kama wadau wakubwa wa kulinda, kukuza na kudumisha haki za binadamu.

Balozi Mulamula amesema hatua ya Tume ya haki za binadamu na Utawala Bora ya Tanzania kutajwa kuwa miongoni mwa Tume bora 23 Barani Afrika kwa kusimamia na kuzingatia mikataba ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa nay a kujivunia na kwamba Serikali itaendelea kusimamia na kutekeleza mikataba hiyo hapa nchini.

Pia amesema Serikali inawategemea watetezi wa haki za binadamu kama “Whistleblowers” pale kunapotokea ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na Taasisi za Serikali au watu binafsi na pia katika kubaini matumizi mabaya ya madaraka kwa Serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali.

Balozi Mulamula ameongeza kuwa Serikali ineheshimu tamko la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu na Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kijamii na kisiasa ambayo inatoa wajibu kwa Serikali kulinda na kudumisha haki za binadamu pamoja na kuwalinda watetezi wa haki za binadamu.

Ametoa kwa wadau kushirikiana ili kuondoa mtazamo hasi uliopo duniani kote ya watetezi wa haki za binadamu kuonekana kama adui wa Serikali na Sio walinzi wa watu kwamba Serikali inatambua wajibu wa kuweka mazingira wezeshi ya kisheria na kitaasisi ya kuhakikisha kuwa watetezi wa haki za binadamu wanaweza kufanya kazi zao kwa uhuru.

Ameishukuru Wizara ya Katiba na Sheria na wadau wote kwa kushiriki ipasavyo kwenye maandalizi ya Taarifa hiyo ambayo inaenda kukamilisha wajibu wa Tanzania kutoa taarifa kuhusu utekelezaji wa haki za binadamu nchini.

Awali akizungumza wakati akimkaribisha Balozi Mulamula Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Jaji Mstaafu Methew Mwaimu amesema tume anayoingoza itaendelea kusimamia na kutekeleza kikamilifu mikataba ya haki za binadamu na utawala bora ya Kitaifa,Kikanda na Kimataifa.



Ameishukuru Serikali kwa ushirikiano inayoitoa kwa tume hiyo jambo la linaloiwezesha kuendelea kutekeleza majukumu yake kikamilifu.

MHE. RAIS SAMIA APOKEA KOMBE LA USHINDI WA COSAFA KUTOKA KWA TIMU YA TAIFA YA WANAWAKE TWIGA STARS

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Viongozi na Wachezaji wa Timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya Wanawake Twiga Stars mara baada ya kupokea Kombe la Ubingwa wa Cosafa kwa Timu hiyo leo tarehe 27 Oktoba, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea Kombe la Ubingwa wa Cosafa kutoka kwa Nahodha wa Timu ya Taifa ya Wanawake Twiga Stars Amina Ali Bilali leo tarehe 27 Oktoba, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na baadhi ya Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Wanawake Twiga Stars mara baada ya kupokea Kombe la Ubingwa wa Cosafa kutoka kwa Wachezajia wa Timu ya hiyo leo tarehe 27 Oktoba, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika Picha ya pamoja na Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Wanawake Twiga Stars mara baada ya kupokea Kombe la Ubingwa wa Cosafa kutoka kwa Wachezajia wa Timu ya hiyo leo tarehe 27 Oktoba, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam

SERIKALI YAPONGEZWA KWA KUBUNI MIFUMO YA TEHAMA YA KUTATUA KERO ZA WANANCHI

$
0
0
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Abdallah Chaurembo akiongoza kikao kazi cha kamati yake na Uongozi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakati wa ziara ya kamati hiyo kwenye Kituo cha Utafiti na Ubunifu cha Mamlaka ya Serikali Mtandao jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akijibu hoja za Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo na Uongozi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kilichofanyika kwenye Kituo cha Utafiti na Ubunifu cha Mamlaka ya Serikali Mtandao jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao, Mhandisi Benedict Ndomba akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya taasisi yake kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo na Uongozi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kilichofanyika kwenye Kituo cha Utafiti na Ubunifu cha Mamlaka ya Serikali Mtandao jijini Dodoma.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakifuatilia taarifa ya utekelezaji wa Mamlaka ya Serikali Mtandao iliyokuwa ikiwasilishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Mhandisi Benedict Ndomba wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo na Uongozi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kilichofanyika kwenye Kituo cha Utafiti na Ubunifu cha Mamlaka ya Serikali Mtandao jijini Dodoma.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa Mhe. Saasisha Mafuwe akiwasilisha hoja wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo na Uongozi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kilichofanyika kwenye Kituo cha Utafiti na Ubunifu cha Mamlaka ya Serikali Mtandao jijini Dodoma.
Naibu Mkatibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael akitoa ufafanuzi wa hoja za kiutumishi zilizowasilishwa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo na Uongozi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kilichofanyika kwenye Kituo cha Utafiti na Ubunifu cha Mamlaka ya Serikali Mtandao jijini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Abdallah Chaurembo akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati yake na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora mara baada ya kuhitimisha ziara ya kamati hiyo kwenye Kituo cha Utafiti na Ubunifu cha Mamlaka ya Serikali Mtandao jijini Dodoma.

Na. James K. Mwanamyoto-Dodoma

Tarehe 27 Oktoba, 2021

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Abdallah Chaurembo ameipongeza Serikali kupitia Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) kwa kubuni mifumo ya utoaji huduma kwa wananchi na kutatua kero zinazowakabili pindi wanapohitaji huduma katika taasisi za umma.

Mhe. Chaurembo ametoa pongezi hizo leo wakati wa kikao kazi cha kamati yake na Uongozi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kilichofanyika katika Kituo cha Utafiti na Ubunifu cha Mamlaka ya Serikali Mtandao jijini Dodoma.

Mhe. Chaurembo amesema, kamati yake inaridhika na utendaji kazi wa Ofisi hiyo hasa katika kubuni mifumo ya TEHAMA inayosaidia kuondoa malalamiko ya wananchi.

Mhe. Chaurembo amesema kamati yake itaendelea kutoa ushirikiano kwa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na kuwasisitiza wajumbe wa kamati yake kutoa elimu ya matumizi ya mifumo hiyo kwa wananchi wanapokuwa kwenye maeneo yao ya utawala.

“Mambo mazuri sana yamefanywa na Ofisi hii pamoja na taasisi zake, hasa hili la kubuni mifumo ya TEHAMA inayoondoa malalamiko, hivyo wajumbe wa kamati hii tuwasaidie kutoa elimu ya umuhimu wa mifumo hii kwa wananchi, tuwasisitize wananchi watumie mifumo hii kuondoa malalamiko,” Mhe. Chaurembo amesisitiza.

Akitoa neno la utangulizi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema, Serikali kupitia wataalam wa ndani wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) imekuwa ikibuni mifumo mbalimbali kwa lengo la kusogeza huduma za Serikali karibu na wananchi na kuwaweka wananchi karibu na Serikali yao.

Mhe. Mchengerwa amesema kuwa Ofisi yake iliona ni vema kufanya ubunifu wa kutengeneza mifumo ya TEHAMA ya utoaji huduma kutokana na changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikiwakabili Watumishi wa Umma na wananchi kwa kipindi cha muda mrefu.

Akifafanua jinsi mfumo mmojawapo uliobuniwa na wataalam hao ujulikanao kwa jina la Sema na Waziri wa UTUMISHI unavyofanya kazi, Mhe. Mchengerwa amesema, mfumo huu unamuwezesha mwananchi kuwasilisha kero au lalamiko lake moja kwa moja kwake na kulifanyia kazi.

Mhe. Mchengerwa amewaomba Wajumbe wa Kamati ya USEMI kutoa elimu ya faida za mfumo huu kwa watumishi na wananchi katika maeneo yao ili utumike kutatua changamoto zinazowakabili.

“Mkiwa kama wawakilishi wa wananchi, tunaomba mtusaidie kupeleka ujumbe kwa wananchi kuhusu faida za mfumo huu kwani tunataka kupunguza kabisa malalamiko na kutatua changamoto za kiutumishi zinazowakabili Watumishi wa Umma kwa muda mrefu.” Mhe. Mchengerwa ameongeza.

Sanjari na hilo, Mhe. Mchengerwa ameishukuru kamati kwa kuiongoza na kuishauri vema ofisi yake na kuahidi kuendelea kutekeleza maelekezo yote yanayotolewa na kamati hiyo kwa maslahi ya taifa.

Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA), Mkurugenzi Mkuu wa eGA, Mhandisi Benedict Ndomba amesema Kituo cha Utafiti na Ubunifu cha Mamlaka ya Serikali Mtandao kimelenga kwenye ubunifu na utafiti katika TEHAMA ili kuwa na mifumo itakayoboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Mhandisi Ndomba amesema falsafa ya Kituo hicho ni kutumia wataalam wa ndani katika kujenga mifumo hiyo ya TEHAMA ili kuweza kutatuta matatizo yetu wenyewe.

MHE. RAIS SAMIA AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA UONGOPZI WA ULINGO.

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Uongozi wa Asasi ya Tanzania Women Cross-Party Platform (T-WCP-ULINGO) wakati Uongozi huo ulipofika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 27 Oktoba, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Asasi ya Tanzania Women Cross-Party Platform (T-WCP-ULINGO) mara baada ya kumaliza mazungumzo na Uongozi huo leo tarehe 27 Oktoba, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam.

DKT.GWAJIMA AFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI WA SAYANSI, TEKNOLOJIA NA UBUNIFU WA UGANDA.

$
0
0
Na.WAMJW- DAR

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima leo amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu wa Uganda Dkt. Monica Musenero Masanza aliyeambatana na Wataalamu kutoka Wizara hiyo ya Uganda.

Katika Mkutano huo kwa pamoja wamekubaliana kushirikiana katika mapambano dhidi ya magonjwa mbalimbali ikiwemo ugonjwa wa UVIKO-19 ili kulinda afya za wananchi wa Tanzania na Uganda.

Aidha, Dkt. Gwajima amemhakikishia utayari wa Wizara yake kushirikiana na Wizara yake nchini Uganda ili kuboresha utoaji huduma kwa wananchi na kuleta matokeo chanya katika Sekta ya Afya baina ya nchi hizo.

Naye Waziri wa Sayansi, Teknlojia na Ubunifu nchini Uganda Dkt. Monica Musenero amesema, Uganda iko tayari kushirikiana na Tanzania katika katika mapambano dhidi ya magonjwa mbalimbali ikiwemo ugonjwa wa UVIKO-19.

Kikao hicho kimefanyika katika kituo cha mikutano ya kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

WIZARA YA MAJI KUNUNUA VIFAA VYA KISASA KWA AJILI YA KUFANYA UTAFITI WA MAJI ARDHINI

$
0
0
WAZIRI wa Maji Mhe.Jumaa Aweso ,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Oktoba 27,2021 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kuhusu matumizi ya fedha za Mgao wa kutekeleza miradi katika athari za uviko -19.
Baadhi ya Watendaji wa Wizara ya Maji wakifatilia hotuba ya Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso (hayupo pichani) wakati akitoa taarifa kuhusu matumizi ya fedha za Mgao wa kutekeleza miradi katika athari za uviko -19 leo Oktoba 27,2021 jijini Dodoma
Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga ,akizungumza kabla ya kuingia Mkataba na Kampuni ya CRJE East Afrika Limited kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Wizara hiyo ujenzi utakaogharimu kiasi cha shilingi bilioni 22.9 hadi utakapo kamilika
Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga akisaini Mkataba na Kampuni ya CRJE East Afrika Limited kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Wizara hiyo Mtumba ujenzi utakaogharimu kiasi cha shilingi bilioni 22.9 hadi utakapo kamilika.
Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga akibadilishana Mkataba mara baada ya kuingia na Kampuni ya CRJE East Afrika Limited kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Wizara hiyo Mtumba ujenzi utakaogharimu kiasi cha shilingi bilioni 22.9 hadi utakapo kamilika.

Na.Alex Sonna,Dodoma

WAZIRI wa Maji Mhe.Juma Aweso amesema kupitia fedha za mradi wa mapambano dhidi ya athari za uviko -19 Wizara hiyo imepanga kununua seti nne za vifaa vya kisasa kwa ajili ya kufanya utafiti wa maji ardhini ili kuondoa kadhia ya awali ya kutumia fedha nyingi kuchimba visima katika maeneo mbalimbali bila kuwa na uhakika wa kupata maji.

Kauli hiyo ameitoa leo Oktoba 27,2021 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu matumizi ya fedha za Mgao wa kutekeleza miradi katika athari za uviko -19, ambapo Wizara hiyo imepata kiasi cha shilingi bilioni 139.4 ambapo kiasi kati ya fedha hizo zitatumika kununua vifaa hivyo vya kufanya utafiti wa maji ardhini na kutekeleza miradi 218 nchi nzima.

Aweso amesema wizara imeeelekeza Sh 17,613,853,330 kwa ajili kununua sekta tano za mitambo ya ujenzi wa mabwawa na seti nne za vifaa vya kisasa vya utafiti wa maji chini ya ardhi.

” Kwa muda mrefu Serikali na wadau wameekuwa wakichimba visima maeneo mbalimbali nchini bila kuwa na uhakika wa kupata maji kwa kutambua umuhimu wa utafiti maji chini ya ardhi kabla ya kuanza kuchimbia tunanunua vifaa vya kisasa vya utafiti.”amesema Aweso

Aidha Aweso amesema kuwa wamepanga kununua seti 25 ya mitambo ya kuchimbia visima ambavyo kila mkoa utapata mtambo mmoja, lengo likiwa ni kukabiliana na uhaba wa vitendea kazi na kusisitiza kuwa Wizara itahakikisha mitambo hiyo inatunzwa.

” Tumekuwa na uhaba wa vitendea kazi hususani mitambo ya kuchimbia visima ambapo husababisha kuchelewesha utekelezaji wa miradi na hatimaye upatikanaji wa huduma za maji kwa wananchi.”amesema Aweso

Katika hatua nyingine Mhe. Aweso ameagiza watendaji wote watakao simamia miradi hiyo kusimamia kwa weledi na Wizara itafuatilia kwa ukaribu sana utekelezaji wa miradi hiyo.

” Mimi na viongozi wengine wa wizara tutafuatilia kwa karibu utekelezaji wa Mpango huu na kwa yeyote ambaye atakwamisha malengo hatutavumilia na tutachukua hatua kali”amesisitiza

Wakati huo huo Wizara ya Maji imesaini mkataba na Kampuni ya CRJE East Afrika Limited wa ujenzi wa jengo la Wizara hiyo ujenzi utakaogharimu kiasi cha shilingi bilioni 22.9 hadi utakapo kamilika.

Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga ameitaka Kampuni hiyo kuzingatia ubora katika utekelezaji wa mradi huo.

SPIKA NDUGAI AIPONGEZA WIZARA YA MADINI

$
0
0
SPIKA wa Bunge Job Ndugai,akizungumza wakati wa hafla ya utoaji leseni ya uchimbaji mkubwa wa Madini kwa kampuni ya Tembo Nickel Corporation Limited na uzinduzi wa Taarifa ya Uhamasishaji,uwazi na uwajibikaji katika Rasilimali Madini,mafuta na gesi asilia (TEITI) ya mwaka 2018/19 hafla iliyofanyika leo Oktoba 27,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Madini Dotto Biteko,akielezea jinsi wizara ilivyojipanga katika kutekeleza majukumu yake wakati wa hafla ya utoaji leseni ya uchimbaji mkubwa wa Madini kwa kampuni ya Tembo Nickel Corporation Limited na uzinduzi wa Taarifa ya Uhamasishaji,uwazi na uwajibikaji katika Rasilimali Madini,mafuta na gesi asilia (TEITI) ya mwaka 2018/19 hafla iliyofanyika leo Oktoba 27,2021 jijini Dodoma.
Spika Mstaafu wa Bunge Anna Makinda,akizungumza wakati wa hafla ya utoaji leseni ya uchimbaji mkubwa wa Madini kwa kampuni ya Tembo Nickel Corporation Limited na uzinduzi wa Taarifa ya Uhamasishaji,uwazi na uwajibikaji katika Rasilimali Madini,mafuta na gesi asilia (TEITI) ya mwaka 2018/19 hafla iliyofanyika leo Oktoba 27,2021 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya Madini na Nishati Danstan Kitandula,akizungumza wakati wa hafla ya utoaji leseni ya uchimbaji mkubwa wa Madini kwa kampuni ya Tembo Nickel Corporation Limited na uzinduzi wa Taarifa ya Uhamasishaji,uwazi na uwajibikaji katika Rasilimali Madini,mafuta na gesi asilia (TEITI) ya mwaka 2018/19 hafla iliyofanyika leo Oktoba 27,2021 jijini Dodoma.
Naibu katibu Mkuu Chama Cha Mapinduzi CCM Christina Mdeme ,akizungumza wakati wa hafla ya utoaji leseni ya uchimbaji mkubwa wa Madini kwa kampuni ya Tembo Nickel Corporation Limited na uzinduzi wa Taarifa ya Uhamasishaji,uwazi na uwajibikaji katika Rasilimali Madini,mafuta na gesi asilia (TEITI) ya mwaka 2018/19 hafla iliyofanyika leo Oktoba 27,2021 jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato,akizungumza wakati wa hafla ya utoaji leseni ya uchimbaji mkubwa wa Madini kwa kampuni ya Tembo Nickel Corporation Limited na uzinduzi wa Taarifa ya Uhamasishaji,uwazi na uwajibikaji katika Rasilimali Madini,mafuta na gesi asilia (TEITI) ya mwaka 2018/19 hafla iliyofanyika leo Oktoba 27,2021 jijini Dodoma.
Baadgi ya washiriki wakifatilia hafla ya utoaji leseni ya uchimbaji mkubwa wa Madini kwa kampuni ya Tembo Nickel Corporation Limited na uzinduzi wa Taarifa ya Uhamasishaji,uwazi na uwajibikaji katika Rasilimali Madini,mafuta na gesi asilia (TEITI) ya mwaka 2018/19 hafla iliyofanyika leo Oktoba 27,2021 jijini Dodoma.
SPIKA wa Bunge Job Ndugai,akizindua Taarifa ya Uhamasishaji,uwazi na uwajibikaji katika Rasilimali Madini,mafuta na gesi asilia (TEITI) ya mwaka 2018/19 hafla iliyofanyika leo Oktoba 27,2021 jijini Dodoma.
SPIKA wa Bunge Job Ndugai,akionyesha kitabu mara baada ya kuzindua Taarifa ya Uhamasishaji,uwazi na uwajibikaji katika Rasilimali Madini,mafuta na gesi asilia (TEITI) ya mwaka 2018/19 hafla iliyofanyika leo Oktoba 27,2021 jijini Dodoma.


Na.Alex Sonna,Dodoma

SPIKA wa Bunge Job Ndugai ameitaka wizara ya nishati kuhakikisha kunakuwepo na umeme wa uhakika ili kuwezesha sekta ya uchimbaji madini nchini.

Spika Ndugai, amesema hayo leo wakati wa hafla ya utoaji leseni ya uchimbaji mkubwa wa Madini kwa kampuni ya Tembo Nickel Corporation Limited na uzinduzi wa Taarifa ya Uhamasishaji,uwazi na uwajibikaji katika Rasilimali Madini,mafuta na gesi asilia(TEITI) ya mwaka 2018/19.

Ndugai, amesema katika uchimbaji huo mkubwa ni muhimu kuwepo na umeme wa uhakika ili kutokwamisha shughuli hiyo.

“Kukatika kwa umeme kwa saa 10 ni hasara kubwa kwa uwekezaji hivyo wizara mnatakiwa kuhakikisha kuwa umeme unakuwepo wa uhakika sisi kule Kongwa tulishazoea kukaa bila umeme hata siku 10 siyo habari,”amesema Ndugai

Aidha amesema Taifa linakwenda kushuhudia uwekezaji mkubwa utakao liletea fedha nyingi.

” Nimpongeze Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira mazuri ya kufanikisha uwekezaji huu Mkubwa uwekezaji nchini”amesema Spika Ndugai

Amesema kuwa awali ilikuwa ngumu sana kupitisha bajeti ya wizara ya Nishati na Madini kutokana na imani ya watanzania na wabunge kuwa ndogo sana kwenye sekta hii. Sera zetu huko mwanzo zilikuwa hazitufikishi popote tuliona tunaliwa tu.

”Tunashukuru kwamba sasa tumekuwa na mikataba inayoeleweka, tumetunga sheria zinazoweza kusimamia rasilimali zetu vizuri, tunapeana leseni hadharani tukiwa tunajua nini kinachokwenda kufanyika tukiwa na maoteo ya nini tutakachokwenda kunufaika nacho”amesisitiza

Kwa upande wake Waziri wa Madini Dotto Biteko amesema kuwa Tanzania inatarajia kutengeneza ajira 987 na mapato ya Dola za marekani bilioni 7.54 sawa na fedha za Tanzania takribani Trilioni 17.35 Kutokana na ubia muendelezo na makampuni ya Madini.

Ameeleza kuwa mapato hayo yanatokana na gawio la hisa huru za Serikali, tozo na Kodi mbalimbali zitakazotokana na Madini yatakayozalishwa kwa kipindi chote Cha uhai wa mgodi huo.

“Mafanikio mengine ni pamoja na ujenzi wa kiwanda Cha ubia Cha usafirishaji Madini ya metali (multi-metal Refinery Plant) kinachotarajiwa kujegwa katika wilaya ya kahama, mkoani shinyanga.

Pia, amesema kuwa kiwanda hicho kitahitaji malighafi mbalimbali ikiwa ni pamoja na chokaa,magadi soda,sulphuric acid na hydrochloric acid zitakazochochea kukua na kuanzisha kwa viwanda vya uzalishaji kemikali na kuendelea kufunguliwa kwa migodi mipya ya kuzalisha malighafi hizo.

Waziri Biteko amewataka wananchi kujiandaa kufanya uwekezaji katika sekta mbalimbali zitakazohudumia katika mgodi,na kuwaeleza wawekezaji kuzingatia Sheria,kanuni,taratibu na miongozo inayosimamia sekta ya Madini ikiwemo ushirikishwaji wa watanzania kwenye fursa mbalimbali za kibiashara.

Amesema manufaa mengine ni kukua kwa mchango wa sekta ya Madini katika Pato la Taifa,kuchochea kukua kwa sekta nyingine za uchumi kama vile viwanda,biashara na sekta za kifedha,kuongezeka kwa fedha za kigeni Kutokana na mauzo ya Madini yaliyosafishwa nje ya Nchi,huduma za bima na Sheria Kutokana na kufungamanisha sekta ya Madini na sekta hizo.

“Hadi septemba 2021 leseni hai ambazo zimeshatolewa ni leseni 1,044 za utafutaji wa Madini,lesseni 15 za uchimbaji mkubwa,leseni 161 za uchimbaji wa Kati,leseni 34,000 za uchimbaji mdogo,leseni 1561 za biashara ya Madin.

“Kutolewa kwa leseni hizi ni pamoja na kuendeleza kusimamia shughuli za uchimbaj, ambapo Serikali imeweza kupata mapato zaidi,”amesema Biteko

Naibu katibu Mkuu Chama Cha Mapinduzi CCM Christina Mdeme amesema chama hicho kitaendelea kusimamia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ili kuhakikisha kupitia Wizara ya Madini inatekelezwa ipasavyo.

“Ndugu zangu Madini yetu ni uchumi wetu hivyo tunakila sababu yakuyatunza ili yaendelee kupandisha uchumi wa nchi yetu.

“CCM inaomba tusiruhusu ulasimu katika uwekezaji Kwenye sekta hii kwani uwekezani ni mapato Madini ni utalii ni jukumu letu watanzania kuendelea kuyatunza Madini haya na ni vyema tukaendeela kutoa leseni kubwa na ndogo ili kuweza kuwanufaisha watanzania wengi kwani sekta hii inatoa ajira kwa vijana wengi,”amesema Mdeme.

Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya Madini na Nishati Danstan Kitandula amesema jitihada ambazo zimekuwa zikifanywa na Serikali zimewezesha sekta ya Madini kukuwa.

Amesema uzinduzi wa ripoti ya TEITI na utoaji wa leseni kwa kampuni ya TEMBO ni jambo ambalo walilitamani muda mrefu kama kamati na kuona kwamba yale waliyokuwa wanayahitaji katika sekta ya Madini yanakwenda kutekelezwa.

“Hii ilikuwa ndoto yetu kubwa sana kwetu kama kamati ya na kutokana na hili tumefurahi sana sasa tunaamini ndoto zetu zinakwenda kutimia,”amesema

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AZINDUA KAMPENI YA MADAWATI 1000 YA BENKI YA EXIM

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (Kushoto) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Tanzania Bw Jaffari Matundu wakiwa wameketi katika moja ya madawati yaliyotolewa na benki ya Exim Tanzania kwa ajili ya Mkoa wa Lindi yakiwa ni sehemu kampeni ya ugawaji madawati 1000 yaliyofadhiliwa na benki hiyo kwa ajili ya shule za msingi katika mikoa mbalimbali ikiwemo Dodoma, Mtwara, Lindi, Mbeya, Mwanza na Tanga wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo iliyofanyika Mkoani Lindi jana. Wanaoshuhudia ni pamona na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bi Zainabu Telack (Kulia) na Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Exim Bw Stanley Kafu (Kushoto)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (Katikati) akikata utepe kuashiriki uzinduzi wa kampeni ya ugawaji madawati 1000 ya Benki ya Exim Tanzania kwa ajili ya shule za msingi katika mikoa mbalimbali ikiwemo Dodoma, Mtwara, Lindi, Mbeya, Mwanza na Tanga wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo iliyofanyika Mkoani Lindi jana. Wanaoshuhudia ni pamona na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Bw Jaffari Matundu (wa tatu kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bi Zainabu Telack (wa tatu kulia) na Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Exim Bw Stanley Kafu (wa pili kushoto)

LINDI; Oktoba 26, 2021: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, hii amezindua rasmi kampeni ya ugawaji madawati 1000 yaliyofadhiliwa na Benki ya Exim Tanzania kwa ajili ya shule za msingi katika mikoa mbalimbali ikiwemo Dodoma, Mtwara, Lindi, Mbeya, Mwanza na Tanga.

Hatua hiyo inalenga kuunga mkono jitihada za serikali katika kukabiliana na uhaba wa madawati katika baadhi ya shule hapa nchini sambamba na kuboresha sekta ya elimu.

Hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo imefanyika Mkoani Lindi mapema jana na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi waandamizi wa serikali, baadhi ya wabunge wa mkoa wa Lindi, wananchi, wanafunzi pamoja na viongozi wa benki hiyo.

Akizungumza jana katika Uzinduzi huo Waziri Mkuu Majaliwa alisema pamoja na kuipongeza benki hiyo kwa jitihada hizo alisema hatua hiyio itasaidia sana katika kupinguza idadi ya wanafunzi wanaokabiliwa na chjangamoto ya ukosefu wa madawati huku akibainisha kuwa kwasasa serikali inaendelea na jitihada mbalimbali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuimaliza kabisa changamoto hiyo.

“Jitihada hizi za Benki ya Exim zimekuja wakati muafaka wakati pia serikali inaendelea kutoa fedha kwa ajili ya elimu katika kujenga vyumba vya Madarasa Nchini na kuboresha Miundombinu ya elimu Nchini.Lengo ni kuhakikisha kwamba pamoja na ongezeko hili la wanafunzi kutokana na mpango wa elimu lakini wanaketi kwenye madawati,’’ alisema Waziri Mkuu Majaliwa

Katika hafla hiyo ilishuhudiwa Waziri Mkuu Majaliwa akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bi Zainab Telack Madawati 200 kwa ajili ya Mkoa wa huo ikiwa ni sehemu ya mpango huo huku akiwaomba wadau mbalimbali kuiga mfano wa benki ya Exim kwa kujitokeza kwa wingi kuunga mkono jitihada hizo.

Awali akizungumza kuhusu kampeni hiyo Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Bw Jaffari Matundu alisema ni mwendelezo wa mkakati wa benki hiyo katika kusaidia jamii unaofahamika kama Exim Cares na dhamira ya benki hiyo katika kuisaidia serikali kukabiliana na upungufu wa madawati katika baadhi ya shule hapa nchini.

“Uzinduzi wa kampeni hii muhimu unalenga kuunga juhudi za Serikali kuboresha miundo mbinu ya elimu hapa nchini. Kampeni itahusisha utoaji wa madawati 1000 katika mikoa mbalimbali hapa nchini Dodoma, Mtwara, Lindi, Mbeya na Mwanza na ugawaji wake utazingatia hali ya uhitaji,’’ alisema Bw Matundu katika taarifa yake mbele ya Waziri Mkuu Majaliwa.

“Kama ambavyo benki ya Exim tumejizatiti kutanua huduma zetu katika mikoa mbalimbali hapa nchini ndivyo ambavyo pia tumejipanga kuhakikisha kwamba uwepo wetu kwenye maeneo hayo unakwenda sambamba na uchangiaji wa huduma za kijamii ikiwemo elimu, afya na uhifadhi wa mazingira ambapo mwezi katikati ya mwaka huu tulishirikiana na Waziri Mkuu Mstaafu Mh Mizengo Pinda katika kufanikisha kampeni ya upandaji miti zaidi ya10,000 katika eneo la Zuzu jijini Dodoma,’’. Aliongezea.

Akizungumza kwenye hafla hiyo Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bi Zainabu Telack aliishukuru benki hiyo kwa msaada huo huku akiiomba iendelee kutazama pia sekta nyingine ikiwemo afya.

“Nimefurahi kusikia kwamba mkakati wa benki ya Exim katika kupanua huduma zake zake katika maeneo mbalimbaliunakwenda sambamba na upanuzi wa mkakati wake katika kusaidia jamii. Huu ni mfano wa kuigwa na ni matarajio yangu kwamba kupitia jitihada kama hizi pia wananchi wa Lindi wataendelea

BALOZI SOKOINE AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KWENYE MKUTANO WA 15 WA TUME YA PAMOJA YA KUDUMU KATI YA TANZANIA NA RWANDA

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine akitoa hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu (JPC) kati ya Tanzania na Rwanda kwa Ngazi ya Makatibu Wakuu uliofanyika katika Ukumbi wa Wakimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Rwanda Bi. Shakilla K. Mutoni, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine, na Balozi Naimi Azizi Mkuruegenzi wa Idara ya Afrika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia Mkutano uliokuwa ukiendelea.
Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu kati ya Tanzania na Rwanda kwa Ngazi ya Makatibu Wakuu uliokuwa ukiendelea JNICC jijini Dar es Salaam
Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu kati ya Tanzania na Rwanda kwa Ngazi ya Makatibu ukiendelea JNICC jijini Dar es Salaam
Picha pamoja ya washiriki wa Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu kati ya Tanzania na Rwanda kwa Ngazi ya Makatibu ulifanyika JNICC jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bw. Dotto James akichangia jambo kwenye Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu kati ya Tanzania na Rwanda kwa Ngazi ya Makatibu Wakuu uliofanyika JNICC jijini Dar es Salaam

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine leo tarehe 27 Oktoba 2021 ameongoza ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu (JPC) kati ya Tanzania na Rwanda kwa Ngazi ya Makatibu Wakuu uliofanyika katika Ukumbi wa Wakimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

Pamoja na mambo mengine Mkutano wa Makatibu Wakuu umepitia na kuthibitisha agenda mbalimbali zilizowasilishwa kwao na Wataalam kabla ya agenda hizo kuwasilishwa na kupitishwa kwenye Mkutano wa Mawaziri unaotarajiwa kufanyika jijini hapa tarehe 28 Oktoba 2021.

Akizungumza wakati wa hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano huo, Balozi Sokoine amewapongeza Wataalam kutoka Tanzania na Rwanda kwa kukamilisha taarifa kwa wakati na ufanisi na kuwezesha mkutano wa makatibu wakuu kufanyika.

“Mkutano huu wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ni jukwaa muhimu katika kukuza ushirikiano baina ya Nchi zetu hizi mbili jirani na rafiki, kwani hutoa fursa ya kuangalia maeneo ya ushirikiano kwa upana wake pamoja na kutoa nafasi ya kubainisha maeneo ya kipaumbele na kuainisha mpango wa utekelezaji ili kuharakisha maendeleo ya wanachini kupitia programu na miradi tunayokubaliana kuitekeleza” Balozi Sokoine

Aliongeza kusema, Mkutano huo wa 15 utatoa nafasi kwa nchi hizi kutathmini namna makubaliano ya awali yalivyotekelezwa, kuainisha changamoto zilizojitokeza kwenye utekelezaji na kutoa suluhu ya namna ya kuzitatua ili kuimarisha ushirikiano uliopo kwa manufaa ya nchi hizi mbili.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Rwanda Bi. Shakilla K. Mutoni, ameeleza kuwa pamoja na kupiga hatua kwenye utekelezaji wa maazimio mengi yalifikiwa kwenye Mkutano wa mwisho wa Tume hiyo uliofanyika mwezi Julai, 2016 nchini Rwanda. Mkutano huu wa 15 huo ulemeleta chachucha ya kuongeza kasi ya utelezaji wa maeneo ambayo yalikuwa bado yaponyuma kiutelezaji. Aidha, ameipongeza Tanzania kwa kutekeleza ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) ambayo baada ya kukamilika kwa ujenzi itarahisisha usafirishaji wa bidhaa kuelekea nchini Rwanda.

Mkutano huu wa Makatibu Wakuu ni mwendelezo wa maandalizi ya Mkutano wa 15 wa Tume ya Kudumu ya Ushirikiano unaotarajiwa kuhitimishwa na Mkutano wa Mawaziri hapo tarehe 28 Agosti 2021.

JIEPUSHENI KUTUMIA USAFIRI WA WANAOSHITAKIANA MABARAZA YA ARDHI-NAIBU WAZIRI MABULA

$
0
0
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (Wa tatu kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela wakishuhudia kuapa kwa mmoja wa Wajumbe wa Baraza la Ardhi na Nyumba la wilaya ya Morogoro tarehe 27 Oktoba 2021 baada ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo.
Mmoja wa Wajumbe wa Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Morogoro (kulia) akiapa wakati wa uapisho wa wajumbe wanne wa Baraza hilo uliofanywa na Mkuu wa mkoa wa Morogoro Martine Shigela
Mjumbe wa Baraza la Ardhi na Nyumba la wilaya ya Morogoro Elia Petro Mpesa akisaini baada ya kuapa kuwa mjumbe wa baraza hilo
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (kushoto aliyekaa) na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela wakiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe Baraza la Ardhi na Nyumba la wilaya ya Morogoro tarehe 27 Oktoba 2021. Kushoto ni Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Morogoro Frank Minzikunte na wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi na Nyumba wilaya ya Morogoro Mwanahawa Kassim.


Na Munir Shemweta, WANMM MOROGORO

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amewataka Wajumbe wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya kujiepusha kutumia usafiri wa wananchi wanaoshitakiana wakati wa kwenda uwandani ili kuepuka tuhuma za kufanya upendeleo wakati wa kusikiliza mashauri.

Dkt Mabula alitoa kauli hiyo tarehe 27 Oktoba 2021 mkoani Morogoro wakati akishuhudia uapishwaji wajumbe wapya wa Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Morogoro uliofanywa na Mkuu wa mkoa huo Martine Shigela. Baraza la Ardhi na Nyumba la Morogoro linahudumia halmashauri tatu za Mvomero, Morogoro Vijijini na Manispaa ya Morogoro.

‘’Ninaomba hili mliepuke sana maana linaleta changamoto kubwa, na mwingine anaweza akakata rufaa akidai mwenzake alikuwa anawapeleka wajumbe uwandani, suala hilo limekuwa likileta shida sana’’ alisema Dkt Mabula.

Wajumbe wa Baraza la Ardhi na Nyumba la wilaya wana jukumu la kusikiliza kesi na kutoa maoni juu ya shauri husika kwa maandishi na wakati wa kusikiliza shauri wana wajibu wa kuhoji maswali ya ufafanuzi ili kupata uelewa zaidi.

Maoni ya wajumbe yanatumika kumsaidia Mwenyekiti wa Baraza kutoa maamuzi ingawa ni lazima Mwenyekiti ajikite katika sheria hivyo anaweza kuyakubali maoni hayo au kuyakataa lakini lazima atoe sababu za kuyakataa.

Dkt Mabula alisema, Wizara inachoshauri ni Mwenyekiti wa Baraza awe na ratiba ya mwezi mzima kuhusiana na safari za kwenda uwandani na taarifa iwasilishwe kwa Mkuu wa wilaya pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri husika ili inapofika siku ya kwenda uwandani basi watumie usafiri wa serikali.

Aliongeza kwa kusema kuwa, kutumia usafiri wa serikali kutaepusha minong’ono na kumkosesha amani mmoja wa miongoni mwa wanaoshitakiana kwa kuhisi kuwa anaweza kuwa anaonewa.

Aidha, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ametaka mashauri katika Mabaraza ya Ardhi kumalizika katika kipindi kisichozidi miezi sita labda kwa yale mashauri ambayo yanaweza kucheleweshwa kwa sababu za mawakili.

‘’Naomba katika kupangilia kesi zisiwe zinapelekwa mbali sana kiasi cha kujikuta mtu anasota mwaka mmoja, miaka miwili kesi haijaisha tutakuwa hatiujawatendea haki’’ alisema Dkt Mabula.

Mkuu wa mkoa wa Morogoro Martine Shigela aliwapongeza wajumbe wa Baraza walioteuliwa na kuwaeleza kuwa uteuzi walioupata umezingatia uadilifu na weledi wao na ana matumaini wajumbe hao wataenda kutenda haki kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa.

‘’Nina matumaini katika nafasi hii mliyoipata mtaenda kutenda haki katika mashauri kwa watu watakaofika kwenye Baraza la Ardhi na Nyumba na hatutarajii kuona uadilifu unapungua mahali ambapo wananchi wanaenda kupata haki kuwa sehemu ya kuilalamikia’’ alisema Shigela.

Jumla ya wajumbe wanne wa Baraza la Ardhi na Nyumba la wilaya ya Morogoro waliapishwa kuhudumu kwenye baraza hilo na sababu ya Mabaraza ya Ardhi na Nyumba kuketi na wajumbe katika kusikiliza mashauri ni kushirikisha jamii kwenye utatuzi wa migogoro ya ardhi na wajumbe hao wana msaada mkubwa katika utatuzi wa migogoro ya ardhi.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Morogoro Mwanahawa Kassim hadi kufikia septemba 2021 katika wilaya ya morogoro Manispaa, Morogoro Vijijini na Mvomero kuna jumla ya mashauri 1,220 ambapo kati ya mashauri hayo yaliyofunguliwa kwa mwezi septemba pekee ni 57 na yaliyoisha mwezi huo ni mashauri 114.

TMA YATANGAZA UTABIRI WA HALI YA HEWA , UKAME WATISHIA

$
0
0
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam kuelezea utabiri wa mvua za msimu kwa maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka. Kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri Mamlaka ya Hali ya Hewa TMA, Dkt. Hamza.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam kuelezea utabiri wa mvua za msimu kwa maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka. Kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri Mamlaka ya Hali ya Hewa TMA, Dkt. Hamza.
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) leo imetoa utabiri wa mvua za msimu kwa maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka huku ikionesha mikoa mingi ya maeneo hayo yakitarajiwa kuwa na mvua za chini ya wastani hadi wastani.

Akizungumza na vyombo vya habari kutoa utabiri huo, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi ameitaja mikoa ya Kigoma, Tabora, Katavi, Singida, Dodoma, Rukwa, Songwe, Mbeya na Iringa kuwa inatarajia kuwa na mvua za chini ya wasta hadi wastani.

Dk. Kijazi amesema kwa mikoa ya Njombe, Ruvuma, Lindi, Mtwara na kusini mwa mkoa wa Morogoro inatarajiwa kuwa na mvua za wastani hadi chini ya wastani, huku akiitaja mikoa ya Kigoma, Tabora, Katavi, Singida, Dodoma, Rukwa, Songwe, Mbeya na Iringa ikitarajia kupata mvua za chini ya wastani hadi wastani.

“…Aidha, Vipindi virefu vya ukavu vinatarajiwa kati ya mwezi Novemba, 2021 na Januari, 2022. Ongezeko kidogo la mvua linatarajiwa mwezi Machi 2022, mvua zinatarajiwa kuanza katika wiki ya tatu ya mwezi Novemba, 2021 katika maeneo mengi na kuisha kati ya wiki ya pili na ya tatu ya mwezi Aprili, 2022.” Alieleza Mkurugenzi, Dk. Kijazi.

Alibainisha kuwa mwelekeo wa msimu wa vuli kwa miezi ya Oktoba hadi Disemba 2021 kwa maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua ikiwemo mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Mara, Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Dar es Salaam, kaskazini mwa mkoa wa Morogoro, Pwani kijumuisha kisiwa cha Mafia mvua zinatarajiwa kuwa za chini ya wastani hadi wastani.

Tayari TMA imetoa ushauri na tahadhari kwa wadau wa sekta mbalimbali wanaotumia taarifa za hali ya hewa katika utekelezaji wa majukumu yao kama vile kilimo na usalama wa chakula, mifugo na uvuvi, maliasili, wanyamapori na utalii, pamoja na sekta ya afya ili kuchukua taadhari kuepusha athari zozote zitakazoweza kujitokeza.

WAZIRI NDAKI: TUMIENI UTAALAM WENU KUWAELIMISHA WAFUGAJI NA WAVUVI

$
0
0
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki akifungua Mkutano wa 44 wa Wataalam wa Uzalishaji Mifugo Tanzania ambapo amewataka wataalam hao kutumia utaalamu wao kuwaelimisha wafugaji na wavuvi ili waweze kufuga kisasa. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Olasiti Garden Hotel Jijini Arusha.
Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Huduma za Ugani, Dkt. Angello Mwilawa akiwasalimia wajumbe wa Mkutano wa 44 wa Wataalam wa Uzalishaji Mifugo Tanzania ambapo pia alisema mkutano huo unawasaidia wataalam kutoka maeneo tofauti kubadilishana uzoefu. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Olasiti Garden Hotel Jijini Arusha.
Mwenyekiti wa Chama cha Wataalam wa Uzalishaji wa Mifugo Tanzania (TSAP), Dkt. Daniel Komwihangilo akitoa maelezo mafupi kuhusu chama hicho kwenye Mkutano wa 44 wa chama hicho ambapo amesema moja ya malengo yake ni kuhimiza maendeleo katika sayansi ya uzalishaji na uendelezaji wa mifugo hapa nchini. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Olasiti Garden Hotel Jijini Arusha.
Msajili wa Bodi ya Maziwa nchini ambaye pia ni Katibu Msaidizi wa TSAP, Dkt. George Msalya akiwatambulisha wajumbe walioshiriki Mkutano wa 44 wa Wataalam wa Uzalishaji Mifugo Tanzania kwa mgeni rasmi Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Olasiti Garden Hotel Jijini Arusha.
Wajumbe wa Mkutano wa 44 wa Wataalam wa Uzalishaji Mifugo Tanzania wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa katika mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Olasiti Garden Hotel Jijini Arusha.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki (kulia) akipokea zawadi ya maziwa kutoka kwa wawakilishi wa Kampuni za Kilimanjaro Fresh na Asas Dairies Ltd mara baada ya kumaliza kufungua Mkutano wa 44 wa Wataalam wa Uzalishaji Mifugo Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa Olasiti Garden Hotel Jijini Arusha.
Picha ya Pamoja ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki (wanne kutoka kushoto waliokaa) na Wajumbe wa Mkutano wa 44 wa Wataalam wa Uzalishaji Mifugo Tanzania mara baada ya kumalizika kwa ufunguzi wa mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Olasiti Garden Hotel Jijini Arusha.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki amewataka wataalamu wa mifugo na uvuvi kutoa elimu ya kitaalam kwa wafugaji na wavuvi ili waweze kufuga kwa tija.

Waziri Ndaki aliyasema hayo leo (27.10.2021) wakati akifungua Mkutano wa 44 wa Wataalam wa Uzalishaji Mifugo Tanzania (TSAP) wenye kauli mbiu ya Uzalishaji Endelevu wa Mifugo na Samaki wakati wa janga la UVIKO 19 uliofanyika kwenye ukumbi wa Olasiti Garden Hotel jijini Arusha.

Kutokana na janga la UVIKO 19, wataalam wametakiwa kuongeza kasi katika utoaji elimu kwa wafugaji na wavuvi ili kuwapa mbinu bora zitakazowasaidia kuongeza uzalishaji na kuweza kukidhi soko la nyama na samaki ambalo kwa sasa linazidi kukua kutokana na kufunguka kwa masoko ya nje ya nchi kutokana na jitihada kubwa zinazofanywa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan za kufungua fursa za masoko ya mifugo na samaki nchi za nje haswa kwenye masoko ya Uarabuni, Ulaya na China.

Pia amewasihi wataalam walioshiriki mkutano huo kuishauri serikali haswa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuhusu namna bora ya kuongeza uzalishaji na kupunguza migogoro ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi. Waziri Ndaki amesema kuwa Wizara itaendeleza jitihada za kuhakikisha kuna kuwa na mazingira bora ya kufuga, kusindika na kufanya biashara ya mazao ya mifugo na uvuvi.

Lakini pia Waziri Ndaki amewasisitiza wafugaji kuendelea kununua maeneo kihalali kwa ajili ya shughuli za ufugaji na kuhakikisha wanayapima na kuyamiliki ili waondokane na migogoro. Vilevile amewasisitiza kuendelea kupanda malisho katika maeneo watakayoyamiliki ili kuondokana na tatizo la malisho kwa mifugo.

Naye Mwenyekiti wa Chama hicho cha TSAP, Dkt. Daniel Komwihangilo alisema lengo la chama hicho ni kuhimiza maendeleo katika sayansi ya uzalishaji na uendelezaji wa mifugo hapa nchini, kutoa fursa kwa wadau wote wa tasnia ya mifugo kukutana ili kubadilishana mawazo na uzoefu, na kushirikiana na wataalam na wanachama wa waliopo katika vyama vya taaluma chini katika sekta ya mifugo na uvuvi ili kuendeleza sekta hizo. Chama hicho kwa sasa kina wanachama zaidi ya 300 ambao wapo hai kutoka katika sekta mbalimbali.

Aidha, amemuomba Waziri kuangalia uwezekano wa kuunda chombo maalum cha kutambua na kuisimamia kada hiyo kisheria. Vilevile amemshukuru Waziri kwa ushirikiano anaoutoa katika kusimamia sekta ya mifugo na uvuvi na kwamba wao kama chama wataendelea kutoa ushirikiano kwa serikali katika kuhakikisha uzalishaji unaongezeka.

WATAALAM MIPANGOMIJI WATAKIWA KUTENGA MAENEO YA WAFANYABIASHARA

$
0
0
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akisisitiza jambo wakati wa kufunga Mkutano wa Saba wa Wataalam wa Mipangomiji uliofanyika katika hoteli ya Nashera mkoani Morogoro
Sehemu ya wajumbe wa Mkutano wa Saba wa Wataalam wa Mipangomiji wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (Hayupo pichani) wakati wa kufunga mkutano huo katika Hoteli ya Nashera mkoani Morogoro.
Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wataalamu wa Mipangomiji Profesa Wilbard Kombe (Wa tatu Kushoto) pamoja na viongozi wengine wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (hayupo pichani) wakati wa kufunga mkutano wa Saba wa Wataalam wa Mipangomiji katika Hoteli ya Nashera Morogoro.

Na Munir Shemweta, WANMM MOROGORO

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amewataka Wataalam wa Mipangomiji nchini kuhakikisha wanapopanga mipango yao kwenye maeneo mbalimbali nchini wanatenga maeneo ya wafanyabiashara wa kawaida ili waweze kufanya biashara katika mazingira rafiki na yaliyo bora.

Alisema, baada ya Wataalam hao kutekeleza wajibu wao wa kupanga, halmashauri nchini ambazo ni mamlaka za upangaji ziweke miundombinu ili wafanyanyabiashara hao wapatikane kwenye maeneo maalum yaliyotengwa.

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, maeneo yatakayotengwa kwa ajili ya wafanyabiashara wa kawaida ni sharti yawe na huduma zote muhimu kama vile maji, umeme na barabara ili kuwawezesha kufanya biashara zao hata usiku kwenye maeneo maalum yaliyotengwa.

‘’Mnapoandaa michoro yenu ya mipangomiji zingatieni taaluma huku mkikumbuka kuna makundi maalum kama vile Mamalishe, Machinga, Bodaboda na watanzania wa kawaida na muwawekee utaratibu maalum wa kupata ardhi kwa gharama nafuu ili nao waweze kushiriki kujenga maeneo yaliyopangwa’’ alisema Naibu Waziri Dkt Mabula

Akizungumza wakati wa kufunga Mkutano Mkuu wa Saba wa Wataalamu wa Mipangomiji uliofanyika tarehe 27 Oktoba 2021 mkoani Morogoro, Naibu Waziri Mabula alisema, mipango ya uendelezaji miji na michoro ya mipangomiji inapoandaliwa ipelekwe mitaani katika lugha ambayo wana mitaa wanaweza kuielewa.

‘’Mipango ya uendelezaji miji inapoandaliwa iletwe mitaani katika lugha ambayo wana mitaa wanaweza kuielewa ili waweze kusimamia, sababu wao ndiyo wadau na watasaidia hata katika development control’’ alisema Dkt Mabula.

Aidha, aliwataka Wataalam wa Mipangomiji kushirikisha watendaji kata, mitaa na vijiji katika mipango ya uendelezaji mji kwa kuwa wao ndiyo wadau muhimu na kusisitiza kuwa wadau hao ni nguvu kazi itakayosaidia kupunguza ujenzi holela kwenye maeneo ya mijini na vijijini.

Naibu Waziri wa Ardhi aliwaasa Wataalam Mipangomiji kuwa wabunifu na kuandaa miradi shirikishi isiyokuwa na suala la fidia na kubainisha kuwa miradi hiyo ni lazima itafanikiwa kwa kuwa itakuwa imeshirikisha wananchi watakaojiona kama sehemu ya wamiliki wa miradi hiyo.

Pia aliitaka Bodi ya Usajili wa Wataalamu wa Mipangomiji kuendelea kusimamia nidhamu, maadili na uwajibikaji kwa wataalamu wa sekta hiyo ili kuleta ufanisi katika sekta ya mipangomiji.

Awali Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wataalamu wa Mipangomiji Profesa Wilbard Kombe alimueleza Naibu Waziri wa Ardhi kuwa, katika maazimio yake wajumbe wa mkutano huo walipendekeza kufanyika mabadiliko kwenye sheria namba nne kwenye kifungu kinachohusu mfuko wa fidia ili watumiaji wakubwa wa ardhi wachangie mfuko huo.

‘’Tumeona huu ni wakati muafaka kwa watumiaji wakubwa wakachangia katika huu mfuko ili kuipa nguvu wizara kumudu gharama zinazotokana na fidia hasa baada ya ardhi kuwa na thamani, kutegemea wizara moja kumudu jukumu hili ni ngumu sana hivyo tumeona ni wakati muafaka kufanya mabadiliko kwenye sheria hiyo’’ alisema Kombe.

Mkutano huo wa Wataalam wa Mipangomiji nchini wenye kauli mbiu ‘Mipangomiji na Uwekezaji Shirikishi Tanzania’ ulishirikisha Wataalamu wa Mipangomiji 230 kutoka mikoa mbalimbali nchini na ulifunguliwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi.

BENKI KUU KUANZA KUCHUKUA HATUA DHIDI YA MATUMIZI MABAYA YA NOTI

$
0
0

Hivi karibuni kuimeibuka wimbi la vitendo vya matumizi mabaya ya noti katika shughuli mbalimbali za kijamii hususan kwenye sherehe za harusi ambapo watu wamekuwa na tabia ya kutunza wahusika wa matukio kwa kuwarushia noti zinazoanguka sakafuni na muda mwingine kukanyagwa, kuziviringisha katika maumbo mbalimbali na kutumia kama mapambo, kuweka kwenye mwili wa mtu ulio loa jasho na matukio yote yanayofanana na hayo.

Matendo haya yanatweza fedha ya Tanzania ambayo ni moja ya tunu za taifa letu.Vitendo hivyo vinaendelea kutokea licha ya Benki Kuu ya Tanzania na viongozi mbalimbali wa Serikali kwa nyakati tofauti kuvikemea.

Hivyo basi, Benki Kuu ya Tanzania inatoa onyo kwa wananchi ambao bado wanakaidi onyo hili ambalo limetolewa mara kadhaa kuhusu namna sahihi ya kutunza noti za Tanzania zinazokuwa mikononi mwao kwa kuzitumia kinyume na maadili pamoja na matakwa ya kisheria.

Kwa taarifa hii, Benki Kuu ya Tanzania itaanza kuchukua hatua dhidi ya wale wote watakaohusika na vitendo vya matumizi mabaya ya noti za Tanzania kwa njia yoyote ile ikiwamo kuweka pesa sakafuni au sehemu yoyote ambayo siyo nadhifu. Vitendo hivyo vinachangia kutweza fedha zetu na kusababisha uchakavu hivyo kuiongezea Serikali gharama kubwa za kuchapisha fedha zingine.

Aidha, Benki Kuu inawashauri washiriki katika matukio yote ambayo yanahusisha matumizi ya fedha kuandaa vyombo maalum vya kuweka fedha hizo badala ya kufanya vitendo ambavyo havikubaliki.

Wananchi wote mnahamasishwa kutoa taarifa mara moja kwa Benki Kuu au Vyombo vya Usalama pale mnapobaini matumizi yasiyo sahihi ya fedha zetu ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi ya wahusika.

Tukitunza fedha zetu tunachangia kuzifanya zitumike kwa muda mrefu na hivyo kuipunguzia Serikali

MSAJILI HAZINA AKAGUA UPANUZI KIWANDA CHA SUKARI KILOMBERO

$
0
0
Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Sukari cha Kilombero anayeshughulikia Fedha, Fakihi Fadhili akitoa ufafanuzi kwa Msajili wa Hazina, Mgonya Benedicto namna mitambo ya kuzalisha sukari kiwandani hapo inavyofanya kazi wakati wa ziara ya Msajili wa Hazina hivi karibuni mkoani Morogoro. Msajili alikwenda kiwandani hapo kujionea kuanza kwa utekelezaji wa mradi wa upanuzi wa kiwanda unaotarajiwa kupaisha uzalishaji wa sukari kutoka tani 127,000 hadi 271,000 ifikapo mwaka 2023.
Msajili wa Hazina, Mgonya Benedicto akikagua moja ya bidhaa za sukari inayozalishwa na Kiwanda cha Sukari cha Kilombero kilichopo Morogoro kutoka kwa Meneja Mkuu anayeshughulikia Fedha, Fakihi Fadhili wakati wa ziara ya Msajili wa Hazina aliyetembelea kiwandani hapo hivi karibuni kujionea kuanza kwa utekelezaji wa mradi wa upanuzi wa kiwanda unaotarajiwa kupaisha uzalishaji wa sukari kutoka tani 127,000 hadi 271,000 ifikapo mwaka 2023.
Msajili wa Hazina, Mgonya Benedicto akipokea maelezo ya ubora wa sukari inayozalishwa na Kiwanda cha Sukari cha Kilombero kilichopo mkoani Morogoro kutoka kwa Meneja Mkuu anayeshughukia Fedha, Fakihi Fadhili wakati wa ziara ya Msajili wa Hazina aliyetembelea kiwandani hapo hivi karibuni kujionea kuanza kwa utekelezaji wa mradi wa upanuzi wa kiwanda unaotarajiwa kupaisha uzalishaji wa sukari kutoka tani 127,000 hadi 271,000 ifikapo mwaka 2023.
Msajili wa Hazina, Mgonya Benedicto akitoa maelekezo kwa Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Sukari Kilombero anayeshughukia Fedha, Fakihi Fadhili kuhusu namna bora ya kuongeza ufanisi katika uzalishaji wa sukari katika kiwanda hicho wakati wa ziara yake ya hivi karibuni mkoani Morogoro. Msajili wa Hazina alitembelea kiwandani hapo kujionea kuanza kwa utekelezaji wa mradi wa upanuzi wa kiwanda unaotarajiwa kupaisha uzalishaji wa sukari kutoka tani 127,000 hadi 271,000 ifikapo mwaka 2023.
Meneja Mradi wa Upanuzi wa Kiwanda cha Sukari cha Kilombero, Dennis Mdoe akitoa maelezo kwa Msajili wa Hazina, Mgonya Benedicto kuhusu utekelezaji wa mradi wa upanuzi wa kiwanda hicho wakati wa ziara ya Msajili wa Hazina aliyetembelea kiwandani hapo hivi karibuni kujionea kuanza kwa utekelezaji wa mradi wa upanuzi wa kiwanda unaotarajiwa kupaisha uzalishaji wa sukari kutoka tani 127,000 hadi 271,000 ifikapo mwaka 2023..

(Picha na Ofisi ya Msajili wa Hazina)

Na Mwandishi Maalumu, Morogoro

SERIKALI kwa kushirikiana na Kampuni ya Sukari ya Kilombero imeanza utekelezaji wa mradi wa upanuzi wa Kiwanda cha Sukari cha Kilombero kitakachokuwa na uwezo wa kuzalisha tani 144,000 za sukari kwa mwaka.

Mradi huo wenye gharama ya Shilingi bilioni 584 ulioanza kutekelezwa Mei mwaka huu unatarajiwa kukamilika Juni 2024 na kuwezesha kiwanda hicho kufikisha tani 271,000 kwa mwaka. Kwa sasa kiwanda hicho kinazalisha tani 127,000 kwa mwaka.

Akizungumza kuhusu mradi huo alioutembelea hivi karibuni Kilombero mkoani Morogoro, Msajili wa Hazina, Mgonya Benedicto aliagiza kasi na ufanisi katika utekelezaji wake ili kufanikisha juhudi za serikali za kuondoa uhaba wa sukari nchini na pia kuongeza pato la serikali na wananchi wanaozunguka mradi huo.

Aliongeza kusema; ” Nataka muongeze juhudi katika utendaji kazi, kuimarisha usimamizi wa mradi na na Serikali tunaahidi kutoa ushirikiano utakaohitajika katika kufanikisha mradi huu muhimu kwa uchumi wa Taifa.”

Serikali ina hisa ya asilimia 25 katika Kampuni ya Sukari ya Kilombero, hisa nyingine zinamilikiwa na Kampuni ya Illovo Sugar Africa .

Msajili wa Hazina, Mgonya aliishukuru Menejimenti kwa kuunga mkono juhudi za Serikali katika uwekezaji huo wa kihistoria unaolenga kuongeza uzalishaji wa sukari nchini na kupunguza pengo la la mahitaji ya sukari nchini.

Naye Meneja Mkuu wa kampuni hiyo ya Sukari Kilombero anayeshughulikia Fedha, Fakihi Fadhili alisema mradi wa upanuzi wa kiwanda hicho utaongeza kiwango cha miwa kutoka kwa wakulima wadogo wa Bonde la Mto Kilombero kutoka tani 600,000 za hivi sasa mpaka kufikia tani 1,700,000.

Alisema kwa upanuzi huo, wakulima wataondokana na usumbufu wa soko la miwa na hivyo kuongeza mara tatu ya kipato cha wakulima hao kufikia Shilingi bilioni 300 ifikapo mwaka 2028.

Aidha idadi ya wakulima wadogo watakaojihusisha na uzalishaji wa miwa inatarajiwa itaongezeka kutoka 8,000 hadi 16,000 na kunufaisha wananchi 100,000 wa maeneo yanayozunguka bonde la Kilombero.

Kwa upande wa ajira, Fakihi alisema kutakuwa na ongezeko la ajira ya moja kwa moja ya zaidi ya watu 2,000 na ongezeko maradufu ya kodi kutoka Sh bilioni 50 zinazolipwa sasa na kampuni hiyo.

Mradi huo pia umelenga kuzalisha umeme wa megawati 10 kwa ajili ya matumizi ya kiwanda na wa ziada kuingizwa katika gridi ya taifa.

Aidha, inatazamiwa kuwa mchango wa Kampuni ya Sukari ya Kilombero kwa uchumi wa nchi utaongezeka maradufu kutoka Sh bilioni 340 kwa mwaka hadi kufikia wastani wa Sh bilioni 750 kiwanda kipya kitakapoanza uzalishaji.

WATALAAM KUTOKA BARA NA ZANZIBAR WAKUTANA

$
0
0
Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Nishati, Petro Lyatuu ( mbele-kushoto), Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Maendeleo ya Mafuta na Gesi Asili Zanzibar (ZPDC), Mikidadi Rashidi(mbele-kulia) wakiendesha kikao cha Ushirikiano baina ya Wizara hizo kilichofanyika Oktoba 27,mwaka huu katika ofisi za Wizara ya Nishati zilizopo katika Mji wa Serikali jijini Dodoma
Washiriki kutoka Wizara ya Nishati Pamoja na Taasisi zilizopo chini yake wakiwa katika kikao cha Ushirikiano baina ya Wizara ya Nishati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kilichofanyika Oktoba 27, mwaka huu katika ofisi za Wizara ya Nishati zilizopo katika Mji wa Serikali jijini Dodoma.
Washiriki Kutoka Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi na Taasisi zilizopo chini yake wakiwa katika kikao cha Ushirikiano baina ya Wizara ya Nishati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kilichofanyika Oktoba 27, mwaka huu katika ofisi za Wizara ya Nishati zilizopo katika Mji wa Serikali jijini Dodoma.
Picha mbalimbali za matukio katika kikao na baada ya kikao cha Ushirikiano baina ya Wizara ya Nishati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kilichofanyika Oktoba 27, mwaka huu katika ofisi za Wizara ya Nishati zilizopo katika Mji wa Serikali jijini Dodoma.

Hafsa Omar-Dodoma

Wataalam kutoka Wizara ya Nishati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na wa kutoka katika Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wamefanya kikao cha Ushirikiano kwa ngazi ya wataalam.

Kikao hicho cha Ushirikiano baina ya Wizara hizo kimefanyika Oktoba 27, mwaka huu katika ofisi za Wizara ya Nishati zilizopo katika Mji wa Serikali jijini Dodoma.

Kikao hicho, kimeongozwa na Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Nishati, Petro Lyatuu na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Maendeleo ya Mafuta na Gesi Asili Zanzibar (ZPDC), Mikidadi Rashidi na kuhudhiriwa na Wajumbe kutoka Wizara ya Nishati na Taasisi zake pamoja na wajumbe kutoka katika Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi na Taasisi zilizopo chini yake.

Wajumbe wa kikao, walijadili ajenda mbalimbali ambazo ni hatua zilizofikiwa katika kukamilisha hati ya Mashirikiano(MoU) kati ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) na Mamlaka ya Udhibiti Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta Asilia, Zanzibar (ZPRA), hatua iliyofikiwa katika kukamilisha hati ya mashirikiano (MoU) kati ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Kampuni ya Maendeleo ya Mafuta na Gesi Asili Zanzibar (ZPDC) na masuala mengine mbalimbali.

Wakati akifungua kikao, Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Nishati, Petro Lyatuu, aliwataka wajumbe hao kutoa michango yao kwa ufanisi.

Kikao hicho ni moja ya vikao ambavyo vinafanyika kwa kuzingatia muongozo uliotolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais, ambavyo hupaswa kufanyika mara nne kwa mwaka.

WAZIRI ATOA MSAMAHA NA USALIMISHAJI WA SILAHA ZINAZOMILIKIWA KINYUME NA SHERIA

$
0
0
30/10/2021 DODOMA

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. George Simbachawene ametoa msamaha na usalimishaji wa silaha kwa wanaomiliki kinyume na sheria na kuwataka kuzisalimisha silaha hizo kwenye vituo vya Polisi na wahusika kutoshitakiwa endapo watazisalimisha silaha hizo haramu kwa hiari na kwa muda uliopangwa.

Waziri Simbachawene ametoa msamaha huo leo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa zoezi la usalimishaji wa silaha haramu kwa hiari nchi nzima litafanyika kuanzia tarehe 01 Novemba 2021 na baada ya muda uliowekwa kupita, msako mkali utafanyika kwa nchi nzima ili kuwakamata wote waliokaidi nafasi ya msamaha waliopewa.

RC MJEMA AZINDUA KITUO CHA USAMBAZAJI MBEGU MKOA WA SHINYANGA..APOKEA MBEGU BORA KUTOKA ASA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema (kushoto), Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude na Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA), Dkt. Sophia Kashenge (wa pili kulia) wakiwa wameshikilia mbegu bora za alizeti na mahindi wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Usambasaji wa mbegu za kilimo Mkoa wa Shinyanga.

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema amezindua Kituo cha Usambasaji wa mbegu za kilimo Mkoa wa Shinyanga pamoja na kupokea Shehena ya zaidi ya tani 100 (kilo 190,000) ya mbegu bora za Mahindi na Alizeti kutoka Wakala wa Mbegu za Kilimo (Agricultural Seed Agency – ASA).

Uzinduzi huo umefanyika Ijumaa Oktoba 29,2021 katika Ghala la Chakula (NFRA) Mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa kilimo mkoa wa Shinyanga.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mhe. Mjema amesema Kituo cha Usambazaji wa mbegu za kilimo itawezesha upatikanaji wa mbegu bora kwa bei nafuu huku akiwataka Maafisa Kilimo kutokaa ofisini bali waende kwa wakulima ili mbegu hizo zitumike vizuri kwa malengo yaliyokusudiwa.

“Mbegu hizi bora za kilimo zimekuja katika wakati muafaka kwani msimu wa kilimo umeanza. Shinyanga kuna ukame hivyo ni lazima tulime kimkakati. Tunamshukuru Mhe. Rais Samia katurahisishia kwa kutuletea mbegu hizi za kimkakati ambazo ni za muda mfupi tu alizeti miezi mine na mahindi miezi mitatu tu unavuna”,amesema.

“Tunashukuru kupata mbegu hizi bora, twendeni tukalime ili tuwe na chakula. Tunataka tulime ili tusiwe na njaa, haitakubalika hapa Shinyanga tuonekane hatuna chakula wakati mbegu bora tumeletewa. Shinyanga tunataka mtetemo wa maendeleo (Vibe)”,ameongeza Mhe. Mjema.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Shinyanga ametumia fursa hiyo kuishukuru ASA kwa kuleta shehena ya mbegu bora za kilimo na kuiomba kuendelea kuleta mbegu za mazao yanayostahimili ukame huku akiwasihi wananchi kutumia mbegu hizo ili kuondokana na umaskini.

“Mbegu bora za kilimo zitakuwa zinauzwa kwenye maghala ya chakula na tutahakikisha wakulima waliopo pembezoni wanapata mbegu hizi ili waweze kulima kwa tija na kuondokana na umaskini”,amesema Mjema.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA), Dkt. Sophia Kashenge amesema kwa kuona umuhimu wa matumizi ya mbegu bora katika eneo la Kanda ya Ziwa umeona ni vyema kuwa na eneo maalumu litakalotumika kusambaza mbegu hivyo kwa kuanzia wamezindua Kituo cha Shinyanga ili kuwezesha upatikanaji wa mbegu bora kwa bei nafuu kwa eneo hilo la Kanda ya Ziwa.

“Kwa awamu ya kwanza tumeleta shehena ya kilo 190,000 za mbegu za kilimo ambapo ni kwa mara ya Kwanza kwetu kusafirisha kwa kutumia Treni. Kati ya hizo kilo 20,000 ni mbegu bora za Alizeti (Standard seeds) ambazo zimeongezwa uwezo wa mkubwa wa kustahili visumbufu mbalimbali na kilo moja ya alizeti itauzwa shilingi 3500. Lakini kilo 89,000 ni za Mbegu bora ya mahindi (Situka M1) ambayo yanayostahimili ukame ambapo kilo moja ya mbegu hizi za mahindi itauzwa shilingi 2700”,ameeleza Dkt. Kashenge.

“ASA ina vituo mbalimbali vya usambazaji wa mbegu bora zinazozalishwa katika mashamba yake. Miongoni mwa vituo hivi vya usambazaji ni pamoja na vituo vyote vya uzalishaji katika mikoa mbalimbali na sasa kituo hiki cha Shinyanga kitakuwa msaada kwa maeneo ya Kanda ya Ziwa”,amesema Dkt. Kashenge.

Dkt. Kashenge ametumia fursa hiyo kuwashauri wakulima kutumia mbinu bora za kilimo ili mbegu hizo ziweze kuleta tija huku

Amesema ASA ambayo makao makuu yake yapo Mkoani Morogoro, kupitia mashamba yake 18 huzalisha mbegu za mazao zaidi ya 40 yakiwemo mahindi, mpunga,alizeti, soya, michikichi, maharage,mbogamboga,ufuta, karanga,mtama, kunde,choroko,mbaazi na mbegu za pamba kulingana na uwezo na mahitaji kwa wakati husika.

Aidha amesema ASA inahitaji eneo la Hekta 200,000 ili iendelee kuzalisha mbegu za kilimo nyingi zaidi ili kuhakikisha kuwa kila mkulima analima kilimo chenye tija akitumia mbegu bora.

Akifafanua zaidi Dkt. Kashenge ameeleza kuwa Tasnia ya mbegu nchini Tanzania inaundwa na sekta ya umma na binafsi ili kuhakikisha mbegu bora zinapatikana katika ngazi zote kwa wakati ambapo sekta ya umma inajumuisha Taasisi za TARI yenye jukumu la kuzalisha mbegu mama, TOSCI yenye jukumu la kudhibiti ubora wa mbegu na ASA yenye jukumu la kuzalisha na kusambaza mbegu bora.

Hata hivyo amesema changamoto ya matumizi bora ya mbegu bora kwa wakulima imetokana na uelewa mdogo wa matumizi ya mbegu bora pamoja na uwezo mdogo wa wakulima kununua mbegu bora hivyo kufanya matumizi ya mbegu bora nchini kuwa chini.

“Licha ya kwamba matumizi ya mbegu bora bado ni changamoto kwa wakulima wengi kutokana na upatikanaji mdogo wa mbegu bora, ongezeko kubwa la uhamasishaji wa matumizi ya mbegu bora za kilimo umesababisha hamasa kubwa kwa wakulima kuhitaji mbegu bora za kilimo. Hali hii imesababisha uhitaji mkubwa wa mbegu za mazao mbalimbali ikiwemo mbegu za mafuta”,amesema Dkt. Kashenge.

Nao Wakuu wa wilaya Jasinta Mboneko (Shinyanga) na Joseph Mkude (Kishapu) wameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongoza na Rais Samia Suluhu kwa kuwapatia mbegu bora za kilimo huku wakiahidi kuwa watapeleka mbegu hizo kwa wakulima maeneo ya vijijini kwa bei ile ile ya shilingi 3500 kwa kilo moja ya mbegu za alizeti na shilingi 2700 kwa mbegu za mahindi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA), Dkt. Sophia Kashenge (kulia) akizungumza wakati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema (mwenye kiremba chekundu) akipokea Shehena ya tani 100 ya mbegu bora za Mahindi na Alizeti kutoka Wakala wa Mbegu za Kilimo (Agricultural Seed Agency – ASA) Ijumaa Oktoba 29,2021 katika Stesheni ya Mjini Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mabehewa yaliyosheheni mbegu bora za mahindi na alizeti kutoka Wakala wa Mbegu za Kilimo (Agricultural Seed Agency – ASA)
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema (mwenye kiremba chekundu) akikata utepe wakati akipokea Shehena ya mbegu bora za Alizeti kutoka Wakala wa Mbegu za Kilimo (Agricultural Seed Agency – ASA). Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akifuatiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA), Dkt. Sophia Kashenge. Wa kwanza kulia ni Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Esther Makune akifuatiwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema (mwenye kiremba chekundu) akikata utepe wakati akipokea Shehena ya mbegu bora za Alizeti kutoka Wakala wa Mbegu za Kilimo (Agricultural Seed Agency – ASA). Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akifuatiwa na Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mhe. Agnes Bashemu. Wa kwanza kulia ni Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Esther Makune akifuatiwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema (mwenye kiremba chekundu) akikata utepe wakati akipokea Shehena ya mbegu bora za Mahindi kutoka Wakala wa Mbegu za Kilimo (Agricultural Seed Agency – ASA).
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema (mwenye kiremba chekundu) na viongozi mbalimbali wakipiga makofi baada ya kukata utepe wakati akipokea Shehena ya mbegu bora za Alizeti kutoka Wakala wa Mbegu za Kilimo (Agricultural Seed Agency – ASA).
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema (mwenye kiremba chekundu) akizungumza baada ya kupokea Shehena ya mbegu bora za Mahindi na Alizeti kutoka Wakala wa Mbegu za Kilimo (Agricultural Seed Agency – ASA).
Muonekano wa ya mbegu bora za Mahindi na Alizeti kutoka Wakala wa Mbegu za Kilimo (Agricultural Seed Agency – ASA).
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema (mwenye kiremba chekundu) akikata utepe kuzindua Kituo cha Usambasaji wa mbegu za kilimo Mkoa wa Shinyanga katika Ghala la Chakula Mjini Shinyanga (NFRA) ambapo mbegu bora za kilimo kutoka Wakala wa Mbegu za Kilimo (Agricultural Seed Agency – ASA) zitakuwa zinauzwa kwa bei nafuu kwa wakulima wa Mkoa wa Shinyanga na mikoa ya jirani.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema (kushoto), Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude na Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA), Dkt. Sophia Kashenge (wa pili kulia) wakiwa wameshikilia mbegu bora za alizeti na mahindi wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Usambasaji wa mbegu za kilimo Mkoa wa Shinyanga katika Ghala la Chakula Mjini Shinyanga (NFRA) ambapo mbegu bora za kilimo kutoka Wakala wa Mbegu za Kilimo (Agricultural Seed Agency – ASA) zitakuwa zinauzwa kwa bei nafuu kwa wakulima wa Mkoa wa Shinyanga na mikoa ya jirani.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema (mwenye kiremba chekundu), Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude na Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA), Dkt. Sophia Kashenge (wa pili kulia), Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Esther Makune (wa kwanza kushoto) akifuatiwa na Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Mhe. Agnes Bashemu na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko wakiwa wameshikilia mbegu bora za alizeti na mahindi wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Usambasaji wa mbegu za kilimo Mkoa wa Shinyanga katika Ghala la Chakula Mjini Shinyanga (NFRA).
Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA), Dkt. Sophia Kashenge akionesha mbegu bora za alizeti
Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA), Dkt. Sophia Kashenge akionesha mbegu bora za mahindi
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Usambasaji wa mbegu za kilimo Mkoa wa Shinyanga
Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA), Dkt. Sophia Kashenge akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Usambasaji wa mbegu za kilimo Mkoa wa Shinyanga

Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

RAIS DKT.MWINYI AMEWAAPISHA VIONGOZI ALIOWATEUWA

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akimuapisha Nd.Mwanamkaa Abdulrahman Mohammed kuwa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka wakati wa hafla iliyofanyika leo Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.[Picha na Ikulu] 30 /10/2021.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akimuapisha Nd.Salma Ali Hassan kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka wakati wa hafla iliyofanyika leo Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.[Picha na Ikulu] 30 /10/2021.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akimuapisha Mhe. Muumin Khamis Kombo kuwa Jaji wa Mahkama Kuu Zanzibar katika hafla iliyofanyika leo Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.[Picha na Ikulu] 30 /10/2021.
Majaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar wakifuatilia hafla ya kuapishwa Mhe.Muumin Khamis Kombo kuwa Jaji wa Mahkama Kuu Zanzibar katika hafla iliyofanyika leo Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.[Picha na Ikulu] 30 /10/2021.
Viewing all 45984 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>