Quantcast
Channel: VIJIMAMBO
Viewing all 45982 articles
Browse latest View live

SPIKA NDUGAI AONGOZA SEMINA YA KAMATI ZA KUDUMU ZA BUNGE ZA VIWANDA, BIASHARA NA MAZINGIRA, BAJETI NA KAMATI YA UONGOZI KATIKA MAJADILIANO NA VIONGOZI WA SHIRIKISHO LA WENYE VIWANDA TANZANIA (CTI)

$
0
0
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) akiongoza semina ya kamati za kudumu za Bunge za Viwanda, Biashara na Mazingira, Bajeti na Kamati ya uongozi katika majadiliano na viongozi wa Shirikisho la wenye viwanda Tanzania (CTI) kuhusu athari za stempu za kodi za elektroniki (ETS) katika biashara nchini iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma, Oktoba 30, 2021, Wa pili kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba (kushoto), Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mhe. Daniel Sillo (wapili kulia) na Mwenyekiti wa Bunge na Kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira, Mhe. David Kihenzile
Wajumbe wa kamati za kudumu za Bunge za Viwanda, Biashara na Mazingira, Bajeti na Kamati ya uongozi wakishiriki semina na majadiliano na viongozi wa Shirikisho la wenye viwanda Tanzania (CTI) kuhusu athari za stempu za kodi za elektroniki (ETS) katika biashara nchini iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma, Oktoba 30, 2021
Mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira na Mbunge wa Kisesa, Mhe. Luhaga Mpina akichangia jambo wakati wa semina ya kamati za kudumu za Bunge za Viwanda, Biashara na Mazingira, Bajeti na Kamati ya uongozi katika majadiliano na viongozi wa Shirikisho la wenye viwanda Tanzania (CTI) kuhusu athari za stempu za kodi za elektroniki (ETS) katika biashara nchini iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma, Oktoba 30, 2021
Mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti na Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Halima Mdee akichangia jambo wakati wa semina ya kamati za kudumu za Bunge za Viwanda, Biashara na Mazingira, Bajeti na Kamati ya uongozi katika majadiliano na viongozi wa Shirikisho la wenye viwanda Tanzania (CTI) kuhusu athari za stempu za kodi za elektroniki (ETS) katika biashara nchini iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma, Oktoba 30, 2021
Wadau mbalimbali kutoka Shirikisho la wenye viwanda Tanzania (CTI) wakiwa katika semina ya kamati za kudumu za Bunge za Viwanda, Biashara na Mazingira, Bajeti na Kamati ya uongozi katika majadiliano na viongozi wa Shirikisho la wenye viwanda Tanzania (CTI) kuhusu athari za stempu za kodi za elektroniki (ETS) katika biashara nchini iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma, Oktoba 30, 2021
Mshirika Mwanzilishi wa Bankable Tanzania, Ndg. Ivan Tarimo akiwasilisha mada wakati wa semina ya kamati za kudumu za Bunge za Viwanda, Biashara na Mazingira, Bajeti na Kamati ya uongozi katika majadiliano na viongozi wa Shirikisho la wenye viwanda Tanzania (CTI) kuhusu athari za stempu za kodi za elektroniki (ETS) katika biashara nchini iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma, Oktoba 30, 2021.

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

WAZIRI SIMBACHAWENE ATOA SIKU 30 KWA WATU WOTE WANAOMILIKI SILAHA KINYUME NA SHERIA KUZISAMILISHA, ATOA MSAMAHA KWA WATAKAO ZISAMILISHA SILAHA HIZO

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akizungumza na waandishi jijini Dodoma, leo Oktoba 30, 2021, kuhusu msamaha na usalimishaji wa silaha kwa wamiliki wa silaha kinyume na sheria. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Ramadhani Kailima. Ametoa siku 30 kwa wamiliki haramu wa silaha hizo kuzisalimisha katika vituo vya polisi, ofisi za serikali za Mitaa na kwa watendaji wa Kata. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akiwaonyesha waandishi wa Habari (hawapo pichani) sheria ya kudhibiti silaha na risasi ya Mwaka 2015, Sura ya 223, baada ya kutangaza msamaha na usalimishaji wa silaha kwa wamiliki wa silaha kinyume na sheria, jijini Dodoma, leo. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Ramadhani Kailima. Ametoa siku 30 kwa wamiliki haramu wa silaha hizo kuzisalimisha katika vituo vya polisi, ofisi za Serikali za Mitaa na kwa Watendaji wa Kata. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kushoto) akisalimiana na Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mbaraka Semwanza, wakati alipokuwa anawasili kuzungumza na waandishi wa Habari, jijini Dodoma, leo. Katikati ni naibu katibu Mkuu, ramadhani kailima, wapili kulia ni Kamishna wa Polisi wa Operesheni na Mafunzo, Lebaratus Sabas. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kulia) akimsikiliza Kamishna wa Polisi wa Operesheni na Mafunzo, Lebaratus Sabas katika kikao na waandishi wa habari kilichifanyika jijini Dodoma, leo. Ametoa siku 30 kwa wamiliki haramu wa silaha hizo kuzisalimisha katika vituo vya polisi, ofisi za Serikali za Mitaa na kwa Watendaji wa Kata. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AZUNGUMZA NA MJUMBE MAALUM WA WAZIRI MKUU WA UINGEREZA KATIKA MASUALA YA BIASHARA KATI YA TANZANIA NA UINGEREZA MHE. LORD WALNEY, GLASGOW, SCOTLAND

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mjumbe Maalum wa Waziri Mkuu wa Uingereza anayeshugulikia masuala ya Biashara kati ya Tanzania na Uingereza Mhe. Lord Walney wa kwanza kulia katika mji wa Glasgow, Scotland leo tarehe 31 Oktoba, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mjumbe Maalum wa Waziri Mkuu wa Uingereza katika masuala ya Biashara Mhe. Lord Walney wa kwanza kulia katika mji wa Glasgow, Scotland leo tarehe 31 Oktoba, 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Mjumbe Maalum wa Waziri Mkuu wa Uingereza katika masuala ya Biashara kati ya Tanzania na Uingereza Mhe. Lord Walney mara baada ya kuzungumza naye katika mji wa Glasgow, Scotland leo tarehe 31 Oktoba, 2021. Wengine katika picha wa kwanza (Kushoto) ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberatha Mulamula na wa kwanza (kulia) ni Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Dkt. Asha Rose Migiro
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Mjumbe Maalum wa Waziri Mkuu wa Uingereza katika masuala ya Biashara kati ya Tanzania na Uingereza Mhe. Lord Walney mara baada ya kuzungumza naye katika mji wa Glasgow, Scotland leo tarehe 31 Oktoba, 2021. Mhe Rais Samia ameshawasili Glasgow kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 26 wa Umoja wa Mataifa utakaojadili athari za mabadiliko ya tabianchi (COP 26). PICHA NA IKULU

DKT. GWAJIMA ATOA WITO WATAALAMU KUTOA ELIMU YA USONJI KWA JAMII.

$
0
0
Na WAMJW-DSM

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima amesema kuwa, wataalam wetu wa afya na elimu na wengine wote walioshiriki katika hafla ya uelimishaji jamii kuhusu Usonji, kutumia elimu hiyo waliopata kuwaelimisha wengine.

Dkt. Gwajima amesema hayo wakati akifungua hafla ya uelimishaji jamii kuhusu Usonji, uliyoambatana na uchangishaji fedha kwaajili ya kuwawezesha vijana wenye usonji kupata mafunzo ya kilimo mahiri yaliyoandaliwa na Lukiza Autism Foundation, Jijini Dar es Salaam.

“Nitoe rai kwa wataalam wetu wa afya na elimu au wawakilishi wao, madaktari, Ustawi wa jamii, walimu wa watoto wenye uhitaji maalum, waandishi wa habari na wengine wote mlioshiriki katika hafla hii, kutumia elimu na uelewa uliopatikana leo kuwaelimisha wengine” Amesema Dkt. Gwajima.

Dkt. Gwajima amesema kwa mujibu wa Takwimu zilizotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) za mwaka 2020 zinaonesha kuwa katika kila watoto 132 Duniani, mtoto mmoja ana Usonji.

“Tanzania, takwimu zilizopo ni za idadi ya Watoto wenye usonji waliofanyiwa usaili katika shule maalum na wale walioonwa katika vituo vya kutolea huduma. Takwimu za mwaka 2018 zinaonesha kuwa, wanafunzi 1416 wana Usonji na walimu 157 katika shule 18 za Msingi”, ameeleza Waziri Gwajima.

Aidha, Dkt.Gwajima ametoa rai kwa wataalam wa afya na elimu wakiwemo madaktari, Ustawi wa jamii, walimu wa watoto wenye uhitaji maalum, waandishi wa habari na wengine wote waliopata fursa ya kushiriki katika hafla ya elimu ya Usonji, kutumia ujuzi huo kuwaelimisha wengine ili kuepuka unyanyapaa dhidi ya watu wenye changamoto hiyo.

Pia katika hatua nyingine Dkt Gwajima amewataka washiriki wa hafla hiyo ya Elimu ya Usonji kuyafanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa katika hafla huyo ili kuona tunaishi kwa upendo na bila kuwabagua na kuwanyanyapaa watu wenye tatizo la Usonji.

Dkt. Gwajima ametoa wito kwa Taasisi mbalimbali za Serikali na zisizo za Kiserikali kufanya tafiti kuhusu tatizo la usonji, na kuweka wazi kuwa, Serikali itatoa ushirikiano kuhakikisha kuwa tafiti hizi zinafanyika na matokeo ya tafiti hizo yanatumika kuimarisha huduma kwa watoto wenye Usonji nchini.

“Ninatoa wito na kuhimiza Taasisi mbalimbali za Serikali na zisizo za Kiserikali kufanya tafiti kuhusu tatizo la usonji na serikali itatoa ushirikiano kuhakikisha kuwa tafiti hizi zinafanyika na matokeo ya tafiti hizo yanatumika kuimarisha huduma kwa watoto wenye Usonji”, ameeleza Waziri Gwajima.

KATIBU MKUU WIZARA YA FEDHA AFUNGUA KIKAO KAZI KATI YA WAHARIRI NA WIZARA YA FEDHA JIJINI DODOMA

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu Serikali Bw. Emmanuel Tutuba akifungua Kikao Kazi kati ya Wizara ya Fedha na Wahariri wa Vyombo vya habari mbalimbali nchini, Kikao hicho pamoja na mambo Kadhaa kinajadili kuhusu Sekta ya Fedha na Maadhimisho ya wiki ya Huduma za Kifedha Kitaifa ambacho kinafanyika kwenye ukumbi wa Kambarage Ofisi ya Hazina jijini Dodoma.
Kamishna Idara ya Maendeleo ya Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha Dkt. Charles Mwamwaja akitoa maelezo ya kikao kazi hicho kabla ya kufunguliwa kati ya Wizara ya Fedha na Wahariri wa Vyombo vya habari mbalimbali nchini, Kikao hicho pamoja na mambo Kadhaa kinajadili kuhusu Sekta ya Fedha na Maadhimisho ya wiki ya Huduma za Kifedha Kitaifa ambacho kinafanyika kwenye ukumbi wa Kambarage Ofisi ya Hazina jijini Dodoma.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Fedha Bw. Benny Mwaipaja akitoa ratiba ya kikao kazi hicho kabla ya kuanza rasmi.
Mwenyekiti wa Wahariri kutoka Vyombo vya Habari wanaoandika Habari za Wizara ra Fedha Bw. Benny Mwang’onda akitoa shukurani zake mara baada ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu Serikali Bw. Emmanuel Tutuba kufungua Kikao Kazi kati ya Wizara ya Fedha na Wahariri .
Baadhi ya Picha zikionesha Wahariri kutoka Vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika Kikao Kazi hicho kati yake na Wizara ya Fedha na Mipango.
Baadhi ya maofisa Mawasiliano kutoka Taasisi mbalimbali zilizo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango wakiwa katika kikaokazi hicho,
Bi Angella Mziray Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na masoko Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF kushoto akiwa na maafisa wengine katika kikaokazi hicho.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu Serikali Bw. Emmanuel Tutuba wa pili kutoka kulia na Kamishna Idara ya Maendeleo ya Sekta ya Fedha Dkt. Charles Mwamwaja wakimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Fedha Bw. Benny Mwaipaja wakati akitoa ratiba ya kikao kazi hicho kulia ni Mtoa Mada Kamishna Msaidizi Wizara ya Fedha Janeth Hiza na kushoto ni Mtoa mada Kamishna Msaidizi Wizara ya Fedha Dioninsia Mjema kushoto.
Baadhi ya waandishi wakishiriki kikao kazi hicho.
Baadhi ya maofisa wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha wakiwa katika kikao kazi hicho.
Kutoka kulia ni Suleiman Jongo kutoka Uhuru, Musfafa kutoka Wasafi TV na Dk. Kahyoza kutoka Gazeti la Lajiji.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri TEF Bw. Deodatus Balile na Mkurugenzi wa Gazeti la Jamhuri akichangia mada katika kikao kazi hicho.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu Serikali BKAw. Emmanuel Tutuba na Kamishna Idara ya Maendeleo ya Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha Dkt. Charles Mwamwaja wakiwa katika picha ya pamoja na wahariri baada ya kufunguliwa kwa kikao kazi hicho.


Na. John Bukuku,Dodoma

Kutokana na umuhimu wa sekta ya fedha katika kuchangia malengo ya serikali ya kuleta maendeleo na kupunguza umasikini, wizara ya fedha na mipango imeandaa mpango mkuu wa maendeleo ya sekta ya fedha wa mwaka 2020/21- 2029/30.

Akizungumza leo Novemba 1,2021 jijini Dodoma Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Emmanuel Tutuba amesema hayo wakati akifungua kikao kazi na wahariri wa vyombo vya habari kwaajili ya kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya fedha

“Wizara ya fedha imeandaa maadhimishe ya huduma za fedha kitaifa lengo ikiwa ni kuwapa elimu wananchi juu ya matumizi bora ya fedha ikiwemo usimamizi wake, mambo ya Bima,malipo, kuweka akiba na kadhalika. alisema,” Tutuba

Katika hatua nyingine katibu mkuu wizara ya fedha na mipango, akatumia fursa hiyo kubainisha lengo la serikali katika kutatua changamoto mbalimbali ndani ya jamii

“Wananchi wakipatiwa elimu ya matumizi ya fedha itwasaidia kupata njia bora ya kupambana na maisha na hatimaye watapata njia ya kupambana na umasikini katika maeneo yao”. Alisema Tutuba

Katika kuhakikisha wanafikia malengo yaliyokusudiwa serikali kupitia wizara ya fedha na mipango imeandaa maadhimisho ya wiki ya huduma za fedha kitaifa yatakayofanyika kuanzia tarehe 8 hadi 14 mwezi huu, 2021.

DHANA YA MAGEREZA KUJITEGEMEA IBORESHE MIRADI

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti akikata utepe kuashiria uzinduzi wa nyumba mpya ya kuishi askari kwenye Gereza Moro wilaya ya Sumbawanga. Kulia ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Rukwa ACP Motrais Mwakiluma na kushoto ni Mkuu wa Gereza Mollo SP Nicostratus Magori.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti (wa pili toka kushoto) akiwasili Gereza la Kilimo Mollo wilayani Sumbawanga kwa ziara ya kuzindua miradi ya maendeleo juzi.
Nyumba mpya ya kuishi familia za askari (Two in One) iliyojengwa katika Gereza la Kilimo Mollo wilayani Sumbawanga kama inavyoonekana wakati wa uzinduzi juzi ambapo imegharimu shilingi Milioni 55.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti akifungua koki ya maji kuashiria uzinduzi wa mradi wa maji safai na salama juzi kwenye Gereza la Kilimo Mollo wilaya ya Sumbawanga.
Mkuu wa Gereza la Kilimo Mollo SP Nicostratus Magori akitoa taarifa ya miradi ya gereza kwa Mkuu wa Mkoa (hayupo pichani) wakati wa hafla ya ufunguzi mradi wa nyumba bora za kuishi askari.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkrikiti akikabidhi funguo ya nyumba kwa askari B1632 S’SGT Jabil Mohamed Mkwazu akiwa na mkewe (kushoto) wakati wa hafla iliyofanyika Gereza Mollo Sumbawanga mwishoni mwa wiki.
(Habari na Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)

Jeshi la Magereza nchini limepongezwa kwa kubuni utaratibu mzuri wa kujiendesha kimapato kupitia miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa nyumba bora kwa gharama nafuu.

Pongezi hizo zimetolewa mwishoni mwa wiki na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti wakati alipozindua mradi wa nyumba za kuishi askari na mradi wa maji kwenye gereza la kilimo Mollo wilaya ya Sumbawanga.

Mkirikiti alifurahishwa kuona mradi wa nyumba ya kuishi familia mbili iliyojengwa kwa shilingi Milioni Hamsini na Tano na aliwapongeza kwa kutekeleza dhana ya Magereza Kujigemea kwa kuwa inaongeza tija kwa mkoa kupitia miradi inayotekelezwa.

“Kama Magereza imeweza kujenga nyumba moja ya familia (Two in One) kwa gharama ya shilingi Milioni 57, huu ni mfano mzuri wa ubunifu. Wito wangu Halmashauri za Rukwa waige mfano huu kwenye utekelezaji miradi ya ujenzi ili kupunguza gharama za fedha za serikali “alisisitiza Mkirikiti.

Awali akitoa taarifa ya miradi, Mkuu wa Gereza la Kilimo Mollo Mrakibu wa Magereza (SP) Nicostratus Magori alisema mradi wa nyumba za kuishi askari umetekelezwa kwa lengo la kupunguza uhaba wa makazi bora ya askari .

Aliongeza kusema gharama halisi za mradi wa nyumba hiyo ni shilingi Milioni 55 ambapo gereza kupitia miradi yake limechangia shilingi Milioni 17.3 na Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) alichangia shilingi Milioni 38

Kuhusu mradi wa maji safi na salama SP Magori alisema jumla ya shilingi Milioni 7.6 imetumika kufufua mradi huo ambapo fedha zote zimetokana na miradi ya gereza Mollo.

SP Magori alitoa ombi kwa Mkuu wa Mkoa kuwa gereza lisaidie kupata miradi mbalimbali kwa lina nguvu kazi na utaalam hatua itakayosaidia kutekeleza miradi kwa ubora huku gereza likiongeza uwezo wake wa kujitegemea kimapato.

“Miradi hii licha ya kutuimarisha kiuchumi, inasaidia pia kutoa mafunzo ya ujuzi kwa wafungwa ili watakapomaliza vifungo vyao itawasaidia kuwa raia wema kwa kufanya kazi halali za kujitegemea” alisema SP Magori.

Gereza la Kilimo Mollo lilianzishwa mwaka 1967 ambapo lina eneo la ukubwa ekari 8,989 na kwa sasa lina miradi ya ujenzi wa nyumba ya kulala wageni, ujenzi wa bwalo, ujenzi wa fremu 11 za maduka na ujenzi wa viwanda vidogo vya kuchaka mazao ya ngano, alizeti na mahindi.

SERIKALI YAZINDUA NEMBO YA MAADHIMISHO YA SHEREHE YA MIAKA 60 YA UHURU JIJINI DODOMA

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama,akizungumza wakati wa uzinduzi wa nembo na kaulimbiu ya maadhimisho ya sherehe ya miaka 60 ya Uhuru uzinduzi huo umefanyika leo November 1,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi, Dkt. Khalid Mohammed Salum,akizungumza wakati wa uzinduzi wa nembo na kaulimbiu ya maadhimisho ya sherehe ya miaka 60 ya Uhuru leo November 1,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya viongozi na waandishi wa habari wakifatilia hotuba mbalimbali wakati wa uzinduzi wa nembo na kaulimbiu ya maadhimisho ya sherehe ya miaka 60 ya Uhuru uzinduzi huo umefanyika leo November 1,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama,akizindua rasmi nembo na kaulimbiu ya maadhimisho ya sherehe ya miaka 60 ya Uhuru uzinduzi huo umefanyika leo November 1,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama,akiwa katika picha ya pamoja mara baada kuzindua nembo na kaulimbiu ya maadhimisho ya sherehe ya miaka 60 ya Uhuru uzinduzi huo umefanyika leo November 1,2021 jijini Dodoma.


Na.Alex Sonna,Dodoma

SERIKALI imezindua rasmi nembo na kaulimbiu ya maadhimisho ya sherehe ya miaka 60, ya Uhuru wa Tanzania bara zitakazofanyika Disemba 9, mwaka huu katika uwanja wa Uhuru mkoani Dar es Saalam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo,Novemba mosi 2021,Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri mkuu Sera, Uratibu, Kazi, Vijana na Ajira Jenista Mhagama,amesema kutokana na umuhimu wa maadhimisho hayo mwaka huu serikali imeazimia kuwa na shughuli zitakazofanyika maeneo mbalimbali ya nchi.

“Lengo ni kutafakari kwa pamoja na kukumbuka tulikotoka, tulipo na tunakoelekea na hasa mafanikio tuliyopata yanayoonyesha dhahiri maendeleo ya miaka 60, ya uhuru wa nchi yetu na watu wake,”amesema.

Amesema shughuli za maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru zitahusisha Wizara na Taasisi zote za serikali kuelezea hatua ambazo kila sekta imepiga tangu Uhuru, tuliposasa na tunapoelekea.

Waziri huyo amesema ratiba ya mikutano ya Mawaziri na vyombo vya habari kuhusu historia ya nchi tangu ilipotoka uhuru hadi sasa kwa kila sekta itaanza Novemba 2, Novemba 2021,ambapo amedai mikutano hiyo inaratibiwa na Idara ya Habari – MAELEZO kwa kushirikiana na sekta husika 2021.

Pia amesema kutakuwa na mahojiano maalum kati ya vyombo vya habari na viongozi mbalimbali wa serikali walioko madarakani na wastaafu, watu mashuhuri, sekta binafsi na wananchi.

Amesema Mahojiano hayo yatahusisha viongozi na wananchi kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.

Vilevile amesema maadhimisho hayo yatahusisha mashindano ya insha kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari, michezo kama mpira wa miguu, kikapu, wavu, riadha na mashindano ya baiskeli.

Pia kutakuwepo na maonyesho ya sanaa na ngoma za jadi, Makongamano ya Kikanda na Kitaifa, Mdahalo wa kitaifa, Maonesho ya Maalum ya Vijana kuonesha Ubunifu na ujuzi katika sekta mbalimbali pamoja na Maonesho ya Biashara ya Kitaifa yatakayotanguliwa na Mkutano wa uwekezaji.

Amesema matukio hayo yatafanyika katika Mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar kuanzia leo hadi Novemba 30, 2021.

Amesema Disemba 2, 2021 utafanyika uzinduzi rasmi wa Juma la Kilele cha sherehe za miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara.

“Uzinduzi huu utafanyika Jijini Dodoma na Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”amesema

Amesema kuwa pia kutakuwepo na uzinduzi wa miradi mbalimbali ya Maendeleo itakayozinduliwa na viongozi wa Kitaifa wakiwemo wa mihimili ya Bunge na Mahakama wakiongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Amesema kutakuwa na mkutano wa uwekezaji ambao utafuatiwa na maonesho ya kitaifa ya biashara utakaojumuisha wafanyabiashara wa pande zote mbili za Muungano.

“Mkutano na Maonesho hayo yatafanyika Zanzibar kuanzia Disemba 3, 2021 na Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mheshimiwa Dk. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi”amesema.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi, Dkt. Khalid Mohammed Salum amesema kuwa uhuru wa Tanganyika wa mwaka 1961 ndiyo baba wa muungano.

“Tunashukuru sana sisi Zanzibar tumehusishwa katika hili kwani Uhuru wa Tanganyiaka ndiyo baba wa Muungano wetu lakini pia na sisi tutahakikisha Januari tunaishirikisha vilivyo Tanzania bara katika maadhimisho ya miaka 58 ya Mapinduzi”amesema Dk. Salum

MAJALIWA: WATANZANIA WANATAMANI TIMU ZAO ZIFANYE VIZURI

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa (wa nne kushoto), Uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na wadau wa mpira wa miguu nchini kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Novemba 1, 2021. Wa tatu kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Caspar Mmuya. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa , Uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na wadau wa mpira wa miguu nchini kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Novemba 1, 2021. Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Caspar Mmuya pia alihudhuria kakao hicho. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa (wa nne kulia), Uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na wadau wa mpira wa miguu nchini kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Novemba 1, 2021. Wa tatu kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Caspar Mmuya. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa GSM, Gharib Mohamed (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Hasa Customs Clearance Company Limited, Salim Abdallah ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Oktoba 1, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa GSM, Gharib Mohamed (kushoto)na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Hasa Customs Clearance Company Limited, Salim Abdallah baada ya mazungumzo mafupi, ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Novemba 1, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Watanzania wanatamani kuona timu zao za Taifa za michezo mbalimbali zinafanya vizuri katika mashindano ya Kimataifa.

Amesema kuwa uwezekano wa timu ya Taifa ya soka ya Tanzania (Taifa Stars) kufanya vizuri katika michuano ya kufuzu kombe la Dunia itakayofanyika nchini Qatar 2022 ni mkubwa kutokana na matokeo mazuri ambayo imeyapata katika michezo ya minne ya awali.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatatu, Novemba Mosi, 2021) wakati wa kikao na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa , uongozi wa TFF pamoja na wadau wa mpira wa miguu kilichofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma.

“Tukifanikiwa kushinda mechi hizo mbili zilizobaki kati ya timu ya Taifa na Congo pamoja na mechi ya timu ya Taifa na Madagascar ambayo itachezwa ugenini, itatupa matumaini ya kushiriki katika michuano ya kombe la dunia, hivyo Serikali inaamini ushirikiano kati ya wadau na Uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ni muhimu katika kufanikisha lengo hilo.”

Akiongea na wadau hao, Mheshimiwa Majaliwa amesema michuano ya kombe la dunia ni fursa kwa wachezaji wetu kwani itawasaidia kutambulika katika mataifa mbalimbali duniani hivyo kupata nafasi ya kuhitajika na vilabu vikubwa duniani.

“Tukishinda mechi hizi mbili pamoja na kuvuka hatua ya mtoano itakayotuwezesha kushiriki kombe la dunia tutakuwa tumewasaidia wachezaji wetu kupanua soko lao kimataifa kwa kuwa wataonekana na hata tutakapoita timu ya Taifa tutakuwa tunaita wachezaji wengi wa kimataifa tofauti na sasa ambao ni watatu tu nao ni Mbwana Samatta, Simon Msuva na Novatus Dismas”.

Waziri Mkuu amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema anatamani kuona timu ya Taifa soka ya wanaume (Taifa Stars) inafanya vizuri kama ilivyo kwa timu ya Taifa ya soka wanawake ambayo hivi karibuni ilichukuwa ubingwa kwenye mashindano ya kombe la COSAFA 2021 yaliyofanyika nchini Afrika Kusini.

SERIKALI YAPOKEA DOZI 500,000 ZA SINOPHARM.

$
0
0
Na WAMJW-DSM.

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto leo imepokea dozi 500,000 za Chanjo ya Sinopharm kutoka Serikali ya Jamhuri ya watu wa China ikiwa ni msaada unaotokana na Ushirikiano bora baina ya nchi hizo mbili.

Shehena hiyo imepokelewa leo Novemba 1, 2021 na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima aliyeambatana na viongozi wengine wa kitaifa na Mkoa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere.

Katika tukio hilo Dkt. Gwajima ameipongeza Serikali ya Jamhuri ya watu wa China kwa ushirikiano wanaoendelea kuonesha ikiwa ni pamoja na kusaidia kuboresha Sekta ya Afya nchini ikiwemo Katika mapambano dhidi ya magonjwa mbali mbali ikiwemo ugonjwa wa UVIKO-19.

“Shukrani za pekee ziwaendee Serikali China hususani katika kujali afya za Watanzania kwa kutupatia Chanjo hizi aina ya Sinopharm Dozi 500,000 ambazo zitatusaidia kuwakinga watanzania 250,000 dhidi ya mapambano ya Ugonjwa wa Virusi vya Corona (UVIKO-19).” Amesema Dkt. Gwajima.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inathamini sana afya za Watanzania. Ndiyo maana tumeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuboresha huduma za kinga nchini. Alisisitiza Dkt. Gwajima.

Aliendelea kusema kuwa, Serikali ilipata jumla ya Chanjo Dozi 1,058,400 aina ya Janssen (Johnson and Johnson) ambazo zilishaisha na Sinopharm Dozi 1,065,600 kutoka shirika la COVAX ndiyo hivi sasa zimeendelea kutolewa katika vituo vyote nchini na kupitia huduma ya mkoba na kusisitiza, wananchi wote,wenye miaka 18 na kuendelea waendelee kupata huduma hiyo.

Aidha Dkt. Gwajima amesema, Wizara ilitoa Mwongozo wa Chanjo unaofafanua vyema taratibu za utoaji wa chanjo hizi wenye lengo la kufikia uchanjaji wa asilimia 60 ya watanzania wenye umri wa miaka 18 na kuendelea.

“Wizara ilitoa Mwongozo wa Chanjo unaofafanua vyema taratibu za utoaji wa chanjo hizi wenye lengo la kufikia uchanjaji wa asilimia 60 ya watanzania wenye umri wa miaka 18 na kuendelea.” Amesema.

Pia, Dkt. Gwajima ameipongeza mikoa mitano ambayo inaongoza kwa kasi ya utoaji wa chanjo ya Sinopharm ambayo ni Ruvuma, Mbeya, Mtwara, Dodoma na Kagera.

Hata hivyo, Dkt. Gwajima ametoa wito kwa Jamii nzima kujitokeza kupata chanjo hii dhidi ya UVIKO-19 ili kupunguza milipuko ambayo inaweza kutokea mara kwa mara na kuepuka madhara makubwa kama kifo na kulazwa kwenye oksijeni kwa muda mrefu.

Mbali na hayo amewaomba wadau wote wenye nia ya kusaidia eneo hili la huduma ya Chanjo kujitokeza na kufuata utaratibu wa mwongozo wa Serikali ili kutoa msaada huo.

“Nitumie fursa hii kuwaomba wadau wengine wote wenye nia ya kusaidia eneo hili kujitokeza na kufuata utaratibu wa mwongozo wa serikali kuhusu suala la kuwezesha msaada huo.”Amesema Dkt. Gwajima.

RAIS SAMIA ASHIRIKI MKUTANO WA COP26 UNAOFANYIKA GLASGOW,SCOTLAND LEO

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akielekea kwenye ukumbi wa Mkutano kwa ajili ya kuhudhuria ufunguzi wa Mkutano wa 26 wa Umoja wa Mataifa utakaojadili athari za mabadiliko ya tabianchi (COP26) unaofanyika Glasgow, Scotland leo tarehe 01 Novemba, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Kupambana na Mabadiliko ya Tabianchi Green Climate Fund (GCF) Yannick Glermarec kabla ya ufunguzi wa Mkutano wa 26 wa Umoja wa Mataifa utakaojadili athari za mabadiliko ya tabianchi (COP 26) unaofanyika Glasgow, Scotland leo tarehe 01 Novemba, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Kupambana na Mabadiliko ya Tabianchi Green Climate Fund (GCF) Yannick Glermarec mara baada ya kuzungumza nae Glasgow, Scotland leo tarehe 01 Novemba, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Malawi Dkt. Lazarus Chakwera kabla ya kuanza kwa Mkutano wa wa 26 wa Umoja wa Mataifa utakaojadili athari za mabadiliko ya tabianchi (COP 26) unaofanyika Glasgow, Scotland leo tarehe 01 Novemba, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Malawi Dkt. Lazarus Chakwera kabla ya kuanza kwa Mkutano wa wa 26 wa Umoja wa Mataifa utakaojadili athari za mabadiliko ya tabianchi (COP 26) unaofanyika Glasgow, Scotland leo tarehe 01 Novemba, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha na Waziri Mkuu wa Uingereza Mhe. Boris Johnson (kushoto) pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres (kulia) mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Mikutano mjini Glasgow, Scotland kwa ajili ya ufunguzi wa Mkutano wa COP26 leo tarehe 01 Novemba, 2021.

MSIMAMO WA TANZANIA KATIKA COP 26

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akilakiwa na ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo katika Mkutano 26 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi unaoendelea mjini Glasgow, Uingereza.
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Dkt. Asha Rose Migiro akiteta jambo na ujumbe wa Tanzania katika mkutano 26 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi unaoendelea Glasgow, Uingereza. Kushoto ni Dkt. Andrew Komba Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais.
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Dkt. Asha Rose Migiro akiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 26 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi unaoendelea Glasgow, Uingereza. Ujumbe huo ni kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais na Benki ya CRDB.
Bi. Emelda Teikwa Afisa Mazingira Mkuu (aliekaa), Bi. Hadija Kayera (wa kwanza kushoto) Afisa Mazingira na Dkt. Emma Liwenga Msaidizi wa Makamu wa Rais (Mazingira) wakiwa katika Mkutano wa 26 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi unaoendelea Glasgow, Uingereza. Kulia ni Bi. Zaninabu Sheuya Afisa Mazingira kutoka Wizara ya Kilimo.

Na Mwandishi Wetu,

Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoshiriki Mkutano wa ishirini na sita wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi. Mkutano huu unafanyika katika Jijini la Glasgow nchini Uingereza kuanzia tarehe 31 Oktoba mpaka tarehe 12 Novemba 2021.

Lengo la Mkutano huu ni kujadili athari zitokanazo na Mabadiliko ya Tabianchi na kuweka Mikakati ya pamoja kama Dunia kukabiliana na athari hizi. Agenda ambazo zinatarajiwa kujadiliwana hatimaye kufikia Makubaliano ya kupambana na athari za Mabadiliko ya tabianchi ni pamoja na kuweka mikakati ya kutafuta Rasilimali Fedha kutoka nchi zilizoendelea kwenda kwa nchi zinazoendelea ambazo zinaathiriwa zaidi na mabadiliko ya tabianchi, takribani kiasi cha dola bilioni 100 kila mwaka za kupambana na changamoto ya Mabadiliko ya Tabianchi kidunia kutoka katika Mifuko ya Jamii za Kimataifa ikiwemo Global Environmental Facility (GEF), Gren Climate Fund (GCF), Adaptation Fund (AF), Least Developed Countries Fund (LDCF).

Agenda zingine zitakazojadiliwa ni pamoja na mikakati ya kuhimili athari za Mabadiliko ya tabianchi (adaptation), upunguzaji wa uzalishaji wa gesijoto (mitigation), kilimo na mabadiliko ya tabianchi, muda wa utekelezaji wa michango ya Taifa ya kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Nationally Determined Contributions Common Timeframes-NDC), Upatikanaji wa Masoko ya Hewa Ukaa chini ya Ibara ya 6 ya Makubaliano ya Paris (Carbon Markets) ili kuweza kupata fedha za kuchangia kwenye mfuko wa kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi (Adaptation Fund).

Majadiliano katika Mkutano huu pia yatahusu Mpango wa Taifa wa Kuhimili Athari za Mabadiliko ya tabianchi (National Adaptation Plans-NAPs), Ubadilishanaji wa Teknolojia baina ya Nchi zilizoendelea na zinazoendelea (Technology Development and Transfer), Ujengaji Uwezo (Capacity Building), Masuala ya Jinsia na Mabadiliko ya Tabianchi (Gender and Climate Change) na Tafiti na Uzalishaji wa Taarifa (Research and Systematic Observation).

Katika Mkutano huu Tanzania inashiriki kikamilifu katika majadiliano ya masuala yenye maslahi mapana kwa nchi na kuweka msimamo katika masuala ya Rasilimali fedha kwa ajili ya utekelezaji wa Mkataba na Makubaliano ya Paris kwa kuzitaka nchi zilizoendelea kutimiza wajibu wao wa ahadi ya kutoa fedha hizi kama ilivyokubaliwa katika mikutano iliyopita.

Katika agenda ya Kujenga Uwezo Tanzania inahimiza nchi zilizoendelea pamoja na mashirika ya kimataifa kutilia mkazo suala la kujenga uwezo wa nchi zinazoendelea ili ziweze kutoa mchango wake kifedha, kiteknolojia na kiutaalamu katika kupunguza uzalishaji wa gesijoto duniani.

Katika nyanja ya Kilimo na Mabadiliko ya Tabianchi katika Mkutano huu unaoendelea Tanzania inasisitiza kuwa sekta ya kilimo isijumuishwe katika sekta zinazotakiwa kupunguza gesi joto kwa kuwa kilimo kinaathirika sana na athari za mabadiliko ya tabianchi kutokana na kutegemea mvua. Agenda hii imekuwa na maoni kinzani kati ya nchi zilizoendelea na zinazoendelea kuhusu kujumuisha sekta ya kilimo katika sekta zinazotakiwa kupunguza uzalishaji wa gesijoto.

Masuala mengine yatakayojadiliwa ni pamoja na Uendelezaji na usambazaji wa teknolojia, Mchango wa Taifa wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi, Upunguzaji gesijoto kwa kutumia biashara na Jinsia na Mabadiliko ya Tabianchi

Ushiriki wa Tanzania katika mkutano wa COP 26 una faida kubwa kwa nchi ikiwa ni pamoja na kupata rasilimali fedha na utaalamu utakaowezesha utekelezaji wa miradi na shughuli mbalimbali ya kupunguza na kuhimili athari za mabadiliko ya tabia nchi. Aidha, ushiriki katika mkutano huo utasaidia kufungua uwekezaji wa sekta binafsi na kuongeza miradi ya Asasi za Kiraia katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Leo tarehe moja na kesho tarehe mbili mwezi huu wa kumi na moja ni siku ambazo viongozi mbalimbali duniani wakiwemo Wakuu wa Nchi watahutubia dunia kupitia Mkutano huu.

ZAIDI YA BILIONI 1.8 KUTUMIKA KUJENGA VYUMBA VYA MADARASA NA MIRADI YA MAJI LUDEWA

$
0
0
Na Damian Kunambi, Njombe.

Mkuu wa wilaya ya Ludewa Andrea Tsere amewataka madiwani pamoja na watendaji wa kata zote za wilaya hiyo kusimamia vyema fedha za miradi za UVIKO – 19 bilioni 1.8 ambapo milioni 920 kwaajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 47 na zaidi ya milioni 978 miradi ya maji.

Akizungumzia mradi wa vyumba vya madarasa amesema wilaya hiyo ina shule za sekondari 17 hivyo kila shule inatakiwa kujengewa vyumba vya madarasa visivyopungua viwili kwa gharama ya shilingi milioni 20 kwa kila chumba.

Ameongeza kuwa anaweka ushindani kwa kila eneo litakalojenga vyumba hivyo kwa wakati ambapo ujenzi huo unatakiwa kumalizika December 15 hivyo watapangwa washindi kulingana na muda waliotumia kumaliza ujenzi na watatangazwa hadharani.

“Leo kwa pamoja tunakubaliana hapa kuwa tunaweka ushindani, itakapofika muda wa kutangaza washindi na wewe ulioshindwa tutakutangaza sasa usije ukasema mkuu wa wilaya ananidhalilisha wakati wewe ndo umejidhalilisha maana hii kazi tunaanza pamoja kwanini wewe ubaki nyuma? “, Amese Tsere.

Aidha kwa upande wa mkurugenzi wa halmashauri hiyo Sunday Deogratias amesema kuwa fedha hizo tayari zimeshafika wilayani na utekelezaji wake tayari umeanza ambapo baadhi ya kata tayari wameanza hatua za awali za kukusanya mawe pamoja na mchanga.

Pia ameunga mkono suala la kushindanisha shule zitakazomaliza ujenzi kwa mapema na kuongeza kuwa wataangalia uwezekano wa kuandaa vyeti kwaajili ya kuwakabidhi washindi hao kuanzia wa kwanza hadi wa tatu.

” Lengo letu ni kushika nafasi ya kwanza kwa mkoa wa Njombe kwani tayari tulishapewa maagizo kutoka kwa mkuu wa mkoa hivyo kwakuwa wanaludewa ni wapenda maendeleo natumai suala hili tutalisimamia vyema”, amesema Deogratias.

Wise Mgina ni mwenyekiti wa halmashauri hiyo amesema fedha za mradi wa maji zimegawanywa katika kata mbili ambapo kata ya Ludewa mjini imepata kiasi cha shilingi milioni 450 ambazo zitatumika kurekebisha mifumo ya maji na zaidi ya milioni 528 zimeelekezwa katika kata ya Madope kwaajili ya kukamilisha mradi wa maji.

Amesema kuwa fedha hizo zimegawiwa maeneo mawili ili kupunguza changamoto za maji kwa awamu kwani wakisema wagawe kila mahali kidogo kidogo hawawezi kumaliza tatizo hivyo ni bora kuweka nguvu sehemu moja na kumaliza tatizo sehemu moja kwenda nyingine.

KATIBU MKUU WIZARA YA MADINI PROF. SIMON MSANJILA ATEMBELEA BANDA LA TANZANIA EXPO 2020 DUBAI

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila (katikati) akitembelea mabanda mbalimbali ya Tanzania kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Tanzania Expo 2020 yanayoendelea Dubai tarehe 1 Novemba, 2021

Mkurugenzi wa Banda la Tanzania kwenye maonesho ya Expo 2020 Dubai Bi. Getrude Ng’weshemi kutoka TanTrade amempokea Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila ambaye ametembelea banda la Tanzania kwenye maonesho ya Kimataifa ya Expo 2020 Dubai. Katika ziara hii Prof. Msanjila aliambatana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Dkt. Venance Mwase, Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Madini Bw. Augustine Ollal, na Kaimu Meneja wa Uwekezaji na Mipango kutoka Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Bi. Nsalu Nzowa.

Dhumuni la ziara hii ilikuwa ni kujionea na kutahmini hali halisi ya maonesho ya Expo 2020 Dubai ili kuweka mkakati bora zaidi ya ushiriki wenye tija wa Sekta ya Madini na namna bora zaidi ya kuendelea kuzitangaza fursa katika sekta hii kote ulimwenguni kupitia maonesho ya Expo 2020 Dubai.

Katika kutekeleza mikakati hiyo Prof Msanjila aliangalia namna Sekta ya Madini Tanzania inavyoweza kushirikiana na nchi nyingine zinazofanya biashara ya madini ili kufikia masoko mengi makubwa zaidi na ya uhakika, na pia uwezekano wa kupata nafasi ya kukutana ana kwa ana na wadau wa uwekezaji.

Ziara hii ni mwanzo mzuri wa maandalizi ya ushiriki rasmi wa Sekta ya Madini katika maonesho ya Expo 2020 Dubai ambapo kutakuwa na program ya Wiki ya Madini inayoandaliwa na TanTrade ambao ni waratibu maonesho haya kwa kushirikiana na Wizara ya Madini na Taasisi zake. Programu hiyo inatarajiwa kuanza tarehe 23 Februari, 2022 hadi tarehe 03 Machi, 2022.

Prof. Simon Msanjila alitumia nafasi hii kutembelea baadhi ya mabanda ya nchi mbalimbali zinazoshiriki kwenye maonesho haya ya Expo 2020 Dubai akianza na mabanda ya Umoja wa Falmeza Kiarabu – Mobility, India na Senegal. Lengo la kutembelea mabanda haya ni kujionea fursa ambazo nchi hizo zimeleta katika maonesho haya. Maonesho haya yanatoa fursa ya kipekee kwa nchi mbalimbali za Afrika kujifunza, kupata uzoefu, kujitangaza kupitia sekta mbalimbali.

Aidha Mkurugenzi wa banda la Tanzania Bi. Getrude Ng’weshemi ameendelea kusisitiza kuwa ushiriki wa sekta nyingine zinazochochea maendeleo ya kiuchumi ikiwemo Sekta ya Madini ni wa muhimu sana katika kuhakikisha kuwa miradi mikubwa na fursa adhimu na zinazohitaji wawekezaji zinapata nafasi ya kujitangaza kupitia ushiriki huu. Ushiriki huu wa pamoja kama taifa utaibua fursa mbalimbali ulimwenguni za uwekezaji na maendeleo endelevu baina ya Tanzania, nchi nyingine za Afrika na Mataifa mbalimbali ulimwenguni.

RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI WA MKURUGENZI MKUU WA NDC

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. Nicolaus Herman Shombe kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC).

Kabla ya uteuzi huo Dkt. Shombe alikuwa Kamishna wa Mipango, Wizara ya Fedha na Mipango.

Dkt. Shombe anachukua nafasi ya marehemu Prof. Damian Gambagambi ambaye alifariki akiwa katika nafasi hiyo.

Uteuzi huo umeanza tarehe 29 Oktoba, 2021.

Jaffar Haniu

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.

HOW BURNA BOY’S MODERN AFRO-BEATS MUSIC AND SUPER PERFORMANCES SET THE BAR HIGH FOR OTHER AFRICAN ARTISTS AND AFRICAN MUSIC WORLD-WIDE

$
0
0
About 3 months ago, my wife and I were looking for a West African artist concert to go to, and that's how we ended up checking out Burna Boy. Based in Atlanta, Burna Boy is a very talented Nigerian artist who has managed to capture so many different audiences worldwide. One thing that obviously stood out to me while scouring through his music and concert lineups was that almost all his concerts were sold out for both his Europe and USA tours, even for those scheduled 3+ months ahead. This included his major shows in Atlanta, New York, and Los Angeles.

And that is what caught my attention. In the back of my mind, I wondered if an African artist like him could captivate so many different people to the point of selling out his concerts 3 months ahead of time, in multiple/different time zones. Being that I had never been a fan of his music, mainly due to the lack of exposure, I figured there must be something extraordinary in him as an entertainer, artist, and performer, that made it possible for him to reach such a massive audience. It took me a while, but finally, I managed to get a couple of tickets for one of his concerts in Houston, Texas.

This concert we attended was almost like a festival. It took place in an open arena, and about 6,000 people pulled up to the event. We were fortunate to get seats on the first row in touching distance away from Burna. On a side note, I love musical performances, and I have been to a few African artist performances in the past few years. My biggest surprise of this specific show, though, came when Burna Boy showed up at his exactly scheduled time, 9pm. And as soon as he entered the stage, the crowd went wild! It was a very curiously and interestingly entertaining night.

First, let me take you back a little and talk about his mother and manager, Bose Ogulu. She showed up on the stage about 5 minutes before the show started in matching brown dress pants and top. She wore short hair colored in yellow and made her presence well known to the audience. She walked up to where the main DJ was set up and bluntly told him and his crew to pack up and leave the stage.

Their set for the night was over. Of course, they were not needed there. Typically, they wanted to take advantage of the pre-show performances they were conducting to stay up there and enjoy a better view of the Burna concert. However, Burna was set to perform with a live band and the DJs were an unnecessary crowd to deal with in his space during the performance. The stage was a piece of a state of the art, big, wide, and well-built with an A/V Media system that was one of its kind and built to handle/cater to big artists, performances, and audiences.

After everyone was kicked out by Burna's mama, the stage was left with only a backup singer and Burna's band crew. The location was now set and ready for the man of the hour. Burna showed up on the stage about 10 minutes after nine (allowing time for quick introductions and hype) and put up an electrifying uninterrupted performance for a full hour, in what I thought was a very satisfying and monumental performance. In that hour of his performance, I saw no one go to the bathroom or sit down; everyone's eyes were on the stage. We were all glued and, at the moment with Burna, and if I must say so, I believe we all had knowingly handled all our other distracting business (bathroom breaks, drinks, etc.) before his performance came. The only thing that accompanied us were our phones, and then we lit up the entire arena.

If you have never seen Burna Boy perform, well, maybe you can't understand, but to my experience, and compared to other concerts I have been to, I can tell you that this fella can entertain. I was impressed with his performance and the kind of following that he has, judging by the audience at the show.

It was very peculiar to me to see that about 70 percent of the attendees were young African Americans, and most of them knew the full lyrics to his songs. This made the entire experience even more impressive. This made me realize how much Nigerian artists have broken through the U.S.A music scene, a lengthy and arduous journey. It used to be that the significant foreign music that was popular to most Americans (especially African Americans) was Jamaican. But now, with Afro-beats, pop Artists like Burna Boy, Wiz Kid, are becoming heavy hitters on the American Music Scene, with such songs as Wiz Kid's “Essence “becoming the first African song to hit the U.S Billboard chart ever.

I believe that Burna's performance was breathtaking and a great experience for three main reasons: His supercharged energy on the stage, great song setlist, and his skillful connection to the audience. It was a one-of-a-kind performance. One that I hardly see in most of the African music concerts that I have gone to. Furthermore, his music composition is another attribute to his uniqueness. The blending in of the original Afro-beat from legendries like Fela Anikulapo Kuti and Sonny Okosun and a little glimpse of R&B beats crosses over not only geographical boundaries , rather, current existing generations.

If there is something one can learn to put up a well-coordinated and successful concert, Burna Boy and his team can surely be able to teach it. For those that have never seen his performances, I encourage you to go on YouTube and just search for Burna Boy's live performance, and even from that, you will be able to see how exciting this artist is. I am very proud to see that the African Music stage is getting bigger and has a broader audience. I hope that more and more upcoming African artists, not just from Nigeria, can help break the scene and take over the international music sphere in the USA.

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN ANAGUSA MAISHA YA KILA MTANZANIA KUPITIA TASAF - Mhe. Ndejembi

$
0
0
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Chenene wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika kijiji hicho.
Mwananchi wa Kijiji cha Chenene Bw. Amiri Mamba akiwasilisha hoja kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo yenye lengo la kukagua utekelezaji wa shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika kijiji hicho.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akijibu hoja za wananchi wa Kijiji cha Chenene wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika kijiji hicho.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kwahemu wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika kijiji hicho.
Wananchi wa Kijiji cha Kwahemu wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo yenye lengo la kukagua utekelezaji wa shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika kijiji hicho.
Mratibu wa TASAF Wilaya ya Chamwino Bw. Sehewa Msagatwa akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ya Kijiji cha Kwahemu kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo ya kukagua utekelezaji wa shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika kijiji hicho.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akimkabidhi fedha mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Chenene kwa ajili ya kununua mpira wa miguu utakaowawezesha wanafunzi wa shule hiyo kufanya mazoezi ya kujenga afya zao ili waweze kushiriki masomo kikamilifu.

Na. Veronica Mwafisi-Chamwino
Tarehe 09 Novemba, 2021

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amesema Serikali inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan inagusa maisha ya kila Mtanzania kupitia utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini nchini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ambao unaziwezesha kaya zote maskini nchini kupata ruzuku inayozisaidia kuboresha maisha yao.

Mhe. Ndejembi amesema hayo kwa nyakati tofauti wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Chenene na Kwahemu, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF III) wilayani Chamwino.

Mhe. Ndejembi amesisitiza kuwa, TASAF inamgusa kila mtu kwani kama kaya yako haipo basi ya jirani yako inanufaika, na kama binafsi haunufaiki basi ndugu yako yeyote ananufaika.

“Kama kaya yako hainufaiki, ya ndugu yako inanufaika na kama wewe binafsi haunufaiki basi Shangazi, Mjomba, Babu au Bibi ananufaika na TASAF,” Mhe. Ndejembi amefafanua.

Katika kuhakikisha fedha za mradi zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na Serikali, Mhe. Ndejembi amewaasa wanufaika wa TASAF kutumia ruzuku wanayoipata kuboresha maisha yao badala ya anasa.

“Serikali haijamkataza mnufaika wa TASAF kunywa pombe, lakini ahakikishe hanywi pombe kwa kutumia fedha zinazotolewa na Serikali kupitia TASAF kwani fedha hizo zinatolewa kwa ajili ya kuboresha maisha ya kaya maskini na si kustarehe,” Mhe. Ndejembi amesisitiza.

Ameongeza kuwa TASAF ni mradi kama ilivyo miradi mingine, kuna siku utafikia ukomo hivyo walengwa wanapaswa kuutumia vema ili wasijute kwa kutotumia fedha hizo kuboresha maisha yao.

Sanjali na hilo, Mhe. Ndejembi amewataka walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kuweka mkakati wa kuboresha maisha yao kupitia TASAF kwani haoni sababu ya wanaonufaika kutumia fedha hizo tofauti na malengo yaliyokusudiwa na Serikali.

Mhe. Ndejembi amesema, Serikali inatarajia baada ya mradi wa TASAF kufikia tamati, wanufaika wa TASAF wamshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan na Serikali yake kwa kuwawezesha kufanya shughuli mbalimbali zikiwemo za ufugaji wa ng’ombe, mbuzi, kuku ikiwa ni pamoja na kuboresha makazi yao kwa kujenga nyumba bora za kuishi.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amefanya ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika Kijiji cha Chenene na Kwahemu vilivyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino.

WAZIRI NCHEMBA AZITAKA HALMASHAURI 55 ZILIPOKEA MIKOPO YA FEDHA YENYE THAMANI YA SH.BILIONI 50 KUZITUMIA KWA MALENGO YALIYOKUSUDIWA

$
0
0
Waziri wa Fedha na Mipango, Mwigulu Nchemba (katikati) akisaini makubaliano ya utoaji wa Fedha za mikopo ya utekelezaji wa programu ya kupanga,kupima na kumilikisha ardhi nchini.Kulia ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi.kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Ummy Mwalimu hafla hiyo imefanyika leo November 8,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Mwigulu Nchemba akiwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi (kulia) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Ummy Mwalimu (kushoto) wakionyesha mikataba mara baada ya kusaini makubaliano ya utoaji wa Fedha za mikopo ya utekelezaji wa programu ya kupanga,kupima na kumilikisha ardhi nchini hafla iliyofanyika hiyo leo November 8,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Mwigulu Nchemba,akizungumza mara baada ya kusaini makubaliano ya utoaji wa Fedha za mikopo ya utekelezaji wa programu ya kupanga,kupima na kumilikisha ardhi nchini hafla iliyofanyika hiyo leo November 8,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Ummy Mwalimu ,akizungumza mara baada ya kusaini makubaliano ya utoaji wa Fedha za mikopo ya utekelezaji wa programu ya kupanga,kupima na kumilikisha ardhi nchini hafla iliyofanyika hiyo leo November 8,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi ,akizungumza mara baada ya kusaini makubaliano ya utoaji wa Fedha za mikopo ya utekelezaji wa programu ya kupanga,kupima na kumilikisha ardhi nchini hafla iliyofanyika hiyo leo November 8,2021 jijini Dodoma.
katibu Mkuu Wizara ya fedha na Mipango Emmanuel Tutuba,akizungumza mara baada ya kusaini makubaliano ya utoaji wa Fedha za mikopo ya utekelezaji wa programu ya kupanga,kupima na kumilikisha ardhi nchini hafla iliyofanyika hiyo leo November 8,2021 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi. Mary Makondo,akitoa maelezo kuhusu programu ya kupanga,kupima na kumilikisha ardhi wakati wa hafla ya utiaji wa saini ya makubaliano ya utoaji wa Fedha za mikopo ya utekelezaji wa programu ya kupanga,kupima na kumilikisha ardhi nchini hafla iliyofanyika hiyo leo November 8,2021 jijini Dodoma.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Antony Mtaka,akizungumza wakati wa hafla ya utiaji wa saini ya makubaliano ya utoaji wa Fedha za mikopo ya utekelezaji wa programu ya kupanga,kupima na kumilikisha ardhi nchini hafla iliyofanyika hiyo leo November 8,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya watendaji wakifatilia hafla ya utiaji wa saini ya makubaliano ya utoaji wa Fedha za mikopo ya utekelezaji wa programu ya kupanga,kupima na kumilikisha ardhi nchini hafla iliyofanyika hiyo leo November 8,2021 jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna,Dodoma

WAZIRI wa Fedha na Mipango,Dk.Mwigulu Nchemba amezitaka Halmashauri 55 zilizopokea mikopo ya fedha yenye thamani ya shilingi bilioni 50 kuhakikisha wanazitumia vizuri kwa malengo yaliyokusudiwa na kuzirudisha kwa wakati ili Halmashauri zingine zipate fursa za kukopa.

Akizungumza leo Novemba 8,2021,Jijini Dodoma wakati wa hafla ya utiaji saini ya makubaliano wa utoaji wa fedha za mikopo ya utekelezaji wa programu ya kupanga ,kupima na kumilikisha ardhi nchini,Waziri Nchemba amezitaka Halmashauri hizo kuzitumia kwa malengo yaliyokusudiwa fedha hizo.

Waziri Nchemba amesema serikali imetoa kiasi cha sh bilioni 50 kwa halmashauri 55 nchini kupitia wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi ili kusaidia upimaji wa ardhi kwenye maeneo yao.

Amesema lengo la Serikali kutoa mikopo hiyo ni kuziwezesha halmashauri hizo kupima ardhi ili kupima ardhi na kuondoa ujenzi wa holela kwenye maeneo hayo

“Serikali itaendelea kutoa fedha hizo kutokana na hali ya bajeti itakavyokuwa imepangwa hivyo waliopata mikopo hiyo wanatakiwa kuonyesha mifano kwa wengine watakaohitaji,”amesema.

Kwa upande wake Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeeo ya Makazi ,William Lukuvi amesema kupitia fedha hizo Halmashauri zitaweza kutengeneza bilioni 41 huku akitolea mfano Halmashauri ya Meru imekopa sh.bilioni 1.6 na inatarajia kuingiza sh bilioni 7.8.

Waziri Lukuvi amesema siku za nyuma Halmashauri zilikuwa zikiomba mikopo kutoka taasisi za kifedha lakini awamu hii serikali imechuku jukumu hilo.

Amesema mikopo hiyo imetolewa na serikali kutokana na andiko lililoandikwa na halmashauri husika kuhusu kazi za fedha hizo

Amesema kuwa jumla ya halmashauri 78 ziliomba mikopo hiyo lakini waliofanikiwa ni halmashauri hizo 55 na watakuwa wakitoa mikopo hiyo ku

Naye,Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Ummy Mwalimu ameagiza mapato ya ndani ya maendeleo katika Halmashauri kutumika pia katika kupima na kupanga miji bila kutaja asilimia ambazo zinatakiwa kutengwa.

Hatua hiyo ilikuja kufuatia Waziri Lukuvi kumuomba Waziri Ummy Halmashuri zitenge fedha kidogo kwa ajili ya kupima na kupanga maeneo.

Waziri Ummy amesema kupatikana kwa fedha hizo imeongeza vipaumbele alivyokusudia kwenye utendaji wake wa kazi alivyojiwekea wakati anaingi kwenye wizara hiyo.

Amevitaja vipaumbele hivyo kuwa ni huduma za afya ,elimu msingi ,kuwawezesha wananchi kiuchumi hasa akinamama ,walemavu na vijana,ujenzi wa miundombinu ya barabara

Waziri Mwalimu amesema kwa sasa ameongezewe kipaumbele cha tano kilichongezewa hiyom jana kuwa ni upimaji ardhi kwenye halmashauri mbalimbali nchini.

“Upatikanaji wa fedha hizo zitaenda kuchochea ukuaji wa uchumi kwa wanachi pamoja na halmashauri husika,”amesema

SERIKALI YATOA NDEGE KWA STARS KUIFUATA MADAGASCAR

$
0
0
KATIKA kuweka mkazo wa kufuzu kombe la Dunia nchini Qatar 2022, Serikali ya Jamhuri wa Muungano Tanzania imetoa ndege ‘Air Bus’ kwa ajili ya mchezo wa Stars dhidi ya Madagascar.

Stars itakuwa na kibarua dhidi ya Madagascar mchezo utakaopigwa Novemba 14 baada ya kumaliza kucheza na DR Congo Novemba 11.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Katibu mkuu wa Wizara ya utamaduni, sanaa na michezo, Dk Hassan Abas amesema Serikali itatoa ndege kwa ajili ya mchezo huo ikiwa ni mkazo wa kuhakikisha timu inafanya vizuri.

“Labda tu niwaambie Serikali katika kuhakikisha tunasapoti michezo tutatoa ndege ya kwenda na kurudi kwa ajili ya mchezo huo, ndege hiyo itabeba wachezaji na benchi lote la ufundi, viongozi, wadau wa soka na waandishi wa habari kwa lengo la kwenda kuhabarisha watanzania”. ,” amesema Abas

Naye Katibu mkuu wa TFF, Wilfred Kidao amesema tayari wameshaanza maandalizi ya mchezo wao ujao dhidi ya Madagascar.

“Tayari tumeshaanza maandalizi ya mchezo wetu ujao dhidi ya Madagascar, lengo ni kuhakikisha tunapata ushindi”.

Stars inaongoza kundi J ikiwa na pointi 7 sawa na Benin huku nafasi ya tatu ikishikiliwa na DR Congo wenye pointi 5.

Mwanaspoti

RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AELEKEA NCHINI MISRI KWA ZIARA YA SIKU 3

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwapungia mkono viongozi mbalimbali waliomsindikiza katika uwanja wa Ndege wa Dodoma wakati akielekea Cairo nchini Misri kwa ajili ya Ziara ya Kiserikali ya siku tatu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango katika uwanja wa Ndege wa Dodoma kabla ya kuondoka nchini kuelekea Cairo, Misri kwa ajili ya Ziara ya Kiserikali ya siku tatu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango wakati akielekea kupanda Ndege kwenda Cairo, Misri kwa ajili ya Ziara ya Kiserikali ya siku tatu. PICHA NA IKULU

MBUNGE WA CHADEMA ACHACHAMAA BUNGENI KUHUSU DENI LA MSD

$
0
0
Na.Mwaandishi Wetu DODOMA

MBUNGE wa Viti Maalumu Agnesta Lambert ( CHADEMA), amesema Bohari Kuu ya Dawa Nchini (MSD) ina hali mbaya kifedha hivyo amependekeza Serikali iwapatie Sh. billion 600 ili iweze kutimiza majukumu yake kwa ufanisi.

Lambert ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma wakati akichangia mpango wa maendeleo wa mwaka 2022/2023 ambapo alisema MSD inahitaji mtaji mkubwa ili iweze kufanya shughuri zake vizuri.

” Mwenyekiti MSD ilikuwa ikiidai Serikali Sh. Billion 269, lakini baada ya Kamati ya PAC kupiga kelele Serikali iliipa MSD Sh. Billioni 39, hivyo ikabaki deni la Sh. Billioni 230″, alisema Lambert.

Mbunge huyo alinukuu kifungu alichosoma Waziri Nchemba katika UK. 14 na UK. 15 ambayo alisema upatikanaji wa dawa muhimu zilisambazwa katika vituo vya Afya kwa asilimia 94.

Alisema Waziri huyo aliendelea kusema Serikali ilitoa Sh. Billioni 234 kwaajili ya kununua dawa na Sh. Billioni 26.3 ya vifaa Tiba hiyo siyo halisi.

Mbunge huyo aliendelea kusema kwa mujibu wa taarifa ya mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Seriki ( CAG) ilisema MSD ina Hali mbaya hivyo inahitaji kuongezwa nguvu.

Aidha Kamati ya Bajeti nayo ilisema MSD Ina hali mbaya hivyo ilipendekeza MSD ipewe Sh. Billioni 363.39 ili iweze kufanya kazi zake vizuri.

” Kwakweli Kamati ya Bajeti imenifurahisha kwa kazi nzuri,kwa kupendekeza MSD iongezewe fedha hizo yaani kwa msemo wa Sasa tunaweza kusema Kamati hiyo imeupiga mwingi”, alisema Lambert.

Pia Mbunge huyo aligongelea msumari wa mwisho kwa kusema hata Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Oktoba 10 mwaka huu aliongea mbele ya vyombo vya habari na kusema huko Mikoani hali mbaya hivyo aliwapa Wiki moja MSD iwe imepeleka dawa Mikoani.

” Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa MSD na Naibu Waziri wa Afya aliongea kwenye vyombo vya habari baada ya kutoka kwenye ziara Mikoani alisema Mikoani hali mbaya dawa hakuna”, alisema Lambert.

” Kamati ya Bajeti ilipendekeza MSD ipewe shilingi Billioni 150 kati ya shilingi Billioni 363.39, ambayo ndio mahitaji halisi ya mtaji ili angalau iweze kutekeleza baadhi ya majukumu”

Hata hivyo, Mbunge huyo alisema kiasi hicho cha fedha kinachopendek zwa na Kamati ya Bajeti kupelekwa MSD (bilioni 150) ni kidogo mno ukilinganisha na mahitaji halisi ya mtaji. Aidha, badala ya kiasi hicho kuisaidia MSD kutekeleza majukumu yake, kitaiongezea STRESS kutokana mzigo mkubwa wa madeni.

Aidha, kutokana na kukinzana kwa taarifa ya Waziri wa Fedha iliyosema upatikanaji wa dawa na vafaa tiba nchini umefikia asilimia 94, huku taarifa za Kamati ya Bajeti, Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) pamoja na maelekezo ya Waziri Mkuu yakionyesha kuwa Kuna uhaba wa dawa na MSD iko hoi kifedha, Mbunge huyo aliitaka Serikali kutoa ufafanuzi kuhusu usahihi wa taarifa hizo!

“Mheshimiwa Mwenyekiti, tuamini taarifa ipi, hotuba ya Waziri wa Fedha, au taarifa za Kamati ya Bajeti na PAC au taarifa ya Waziri Mkuu? Mbunge huyo alihoji.

Aidha Mbunge huyo alisema kutokana na sintofahamu hiyo alipendekeza Serikali katika fedha zilizotolewa na Benki ya Dunia (IMF) sh. Trilioni 1.3, itoe Sh. billioni 600 wapewe MSD ili iweze kulipa madeni na fedha itakayobaki itumike Kama mtaji.

Mbunge huyo alisisitiza kuwa, Serikali iweke kwenye mpango wa Maendeleo wa 2022- 2023 mkakati wa kulipa deni lake kwa MSD kwa mkupuo mmoja sambaba na kuipatia MSD mtaji wa kutosha ili iweze kuzalisha,kununua na kusambaza dawa na vifaa tiba kwa ajili ya kulinda afya za watanzania
Viewing all 45982 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>