Quantcast
Channel: VIJIMAMBO
Viewing all 45982 articles
Browse latest View live

WIZARA YA NISHATI YAJIVUNIA MIAKA 60 YA UHURU KUONGEZEKA KWA KUZALISHA UMEME NCHINI

$
0
0
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Mhandisi Felichesmi Mramba,akitoa taarifa ya wizara ya Nishati kwa kwa niaba ya Waziri wa Nishati,Januari Makamba kuhusu mafanikio yaliyopatika kwa kipindi cha miaka 60 ya Uhuru leo November 9,2021 jijini Dodoma
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakifatilia hotuba ya Waziri wa Nishati Januari Makamba iliyowasilishwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Felichesmi Mramba kuhusu mafanikio yaliyopatika kwa kipindi cha miaka 60 ya Uhuru leo November 9,2021 jijini Dodoma

Na.Alex Sonna,Dodoma

KATIKA kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru Wizara ya Nishati imetaja mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya umeme na nishati jadidifu ni kuongezeka kwa uzalishaji wa umeme nchini ambapo hadi kufikia septemba 2021 upatikanaji wa umeme umefikia Megawati 1,609.91 ikilinganishwa na Megawati 17.5 kabla ya uhuru.

Akizungumza leo Novemba 9,2021 jijini Dodoma Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Mhandisi Felichesmi Mramba kwa niaba ya Waziri wa Nishati,Januari Makamba kuhusu mafanikio na maendeleo ya sekta hiyo katika kipindi cha miaka 60.

KUONGEZEKA KWA UZALISHAJI WA UMEME

Mramba amesema katika kipindi cha miaka 60 ya uhuru wa Tanzania Bara mafanikio yaliyopatikana katika Sekta ya Umeme na Nishati Jadidifu ni pamoja na kuongezeka kwa uzalishaji wa umeme nchini ambapo hadi kufikia mwezi Septemba, 2021 upatikanaji wa umeme umefikia MW 1,609.91 ikilinganishwa na MW 17.5 kabla ya Uhuru.

Amesema ,uwezo wa mitambo ya kufua umeme iliyoungwa katika mfumo wa Gridi ya Taifa umefikia MW 1,573.65 ambapo umeme wa nguvu ya maji (36.46%); gesi asilia 57.28(%); Mafuta (5.60%); na Tungamotaka (Biomass) (0.67%) na kwamba uwezo wa mitambo hiyo unajumuisha mitambo inayomilikiwa na TANESCO ambayo huchangia (86.57%) na mitambo ya wazalishaji binafsi (IPPs/SPPs) ambayo huchangia (13.43%).

“Uwezo wa mitambo ya kuzalisha umeme iliyopo nje ya Gridi ya Taifa (off-grid) ni MW 36.26 ambapo TANESCO inamiliki mitambo yenye MW 31.26 na mzalishaji binafsi NextGen Solawazi (Kigoma) MW 5 kwa kutumia nguvu ya jua,ukamilika kwa mitambo wa kuzalisha umeme kwa nguvu ya maji ya: Hale MW 21 (mwaka 1964).

“Na kwa njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kV 11 kutoka hale hadi Dar es salaam; Nyumba ya Mungu MW 8 (mwaka 1969) na njia ya umeme ya msongo wa kV 66 Kutoka nyumba ya Mungu hadi Arusha; Kidatu MW 240 (mwaka 1975- 1981); Mtera MW 80 (mwaka 1988); New Pangani Falls MW 68 (mwaka 1995); na kihansi wa MW 180 (mwaka 2000),”Alifafanua.

Amesema kukamilika kwa ujenzi wa mitambo ya kufua umeme kwa kutumia gesi asili ya Songas MW 189 (mwaka 2004) Ubungo I MW 102 (mwaka 2008), Ubungo II MW 105 (mwaka 2012), Tegeta MW 45 (mwaka 2009), Somanga Fungu MW 7.5 (mwaka 2010), Kinyerezi I MW 150 (mwaka 2016) na ujenzi wa njia za umeme wa kV 220 (Kinyerezi – Kimara) na kV 132 (Kinyerezi – Gongolamboto); Nyakato MW 63 (mwaka 2013), Kinyerezi II MW 248 (mwaka 2018) na Mtwara gas power plant MW 22 (mwaka 2019).

Amesema kukamilika kwa ujenzi wa njia za kusafirisha umeme za kV 66 yenye urefu wa Kilomita 125 kutoka Mbala, Zambia hadi Sumbawanga (mwaka 2001) kV 220 kutoka Singida na Arusha (mwaka 1996) km 300, kV 132 kutoka Ubungo-Makumbusho (mwaka 2010) kilomita 7; kV 132 yenye urefu wa kilomita 80 kutoka Mtwara hadi Mahumbika (Lindi).

“Pamoja na vituo vya kupoza umeme vya Mtwara na Mahumbika, kV 400 kutoka Iringa hadi Shinyanga kupitia Dodoma na Singida km 670 (mwaka 2016), kV 220 kutoka Makambako hadi Songea km 250 pamoja na ujenzi wa vituo vitatu (3) vya kupoza umeme vya Makambako, Madaba na Songea (mwaka 2018); na kV 220 Bulyanhuku Geita km 55 (mwaka 2020).

VITUO VIPYA VYA KUBORESHA UPATIKANAJI WA UMEME

Ameyataja mafanikio mengine yaliyopatikana ndani ya miaka 60 ya uhuru ni kukamilika kwa ujenzi wa vituo vipya vya kupoza umeme kwa ajili ya kuboresha upatikanaji na umeme vya Mbagala, Kipawa, Gongolamboto na Mburahati Mkoani Dar es Salaam, vituo vya kupoza umeme vya Njiro B, Mount Meru, Sakina, Unga Ltd, Kiltex na Themi Mkoani Arusha.

Mramba amevitaja vituo vingine ni vya kupoza umeme vya Bomambuzi na Trade School Mkoani Kilimanjaro; ukarabati wa vituo vya kupoza umeme vya Mikocheni, Oysterbay, City Centre, Gongolamboto, Kariakoo, Mbagala, Chang’ombe, Kipawa na Ubungo Mkoani Dar es Salaam.

“Kukamilika kwa ujenzi wa njia za msongo wa kV 33, kV 11 na kV 0.4 kwa ajili ya kusambaza umeme katika Mikoa ya Dodoma, Iringa, Manyara, Mbeya, Morogoro, Mwanza, Njombe na Tanga kwa ufadhili wa Millenium Challenge Corporation (MCC).

Kukamilika kwa mradi wa kusambaza umeme wa Electricity V (2015) katika Wilaya za Bukombe, Kwimba, Magu, Mbogwe, Misungwi na Sengerema. Mradi huo ulihusu ujenzi wa njia ya kusambaza umeme wa Msongo wa kV 33, kufunga transfoma na kuwaunganishia umeme wateja 8,600,”amesema.

SEKTA YA MAFUTA NA GESI
Amesema kabla ya uhuru biashara ya mafuta ilianza maeneo ya mwambao wakati Smith MacKenzie alipoanza kuingiza mafuta kwenye visiwa vya Zanzibar kama wakala wa Kampuni ya Shell.

Amesema Kampuni hiyo ilipanua shughuli zake hadi maeneo ya Tanzania Bara na pia ilijihusisha na utafutaji wa mafuta hadi mwaka 1964.

“Mwaka 1966, Serikali kwa kushirikiana na kampuni ya Agip iliunda kampuni ya Tanzania and Italian Petroleum Refinery (TIPER) ambayo ilihusika na kuagiza, kusafisha na kuuza mafuta kwa kampuni za usambazaji,”amesema.

Amesema kiasi cha mafuta kilichokuwa kinasafishwa na kampuni hiyo hakikukidhi mahitaji kutokana na sababu hiyo, mwaka 1969 Serikali ilianzisha Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC).

Amesema TPDC pia ilikuwa na jukumu la kusimamia shughuli za utafiti wa awali na utafutaji mafuta kwa kushirikiana na kampuni nyingine chini ya mikataba ya Production Sharing Agreement (PSA).

Amesema Serikali ilitoa leseni ya utafutaji wa mafuta ya petroli kwa Kampuni ya AGIP katika eneo la mwambao wa bahari ya Hindi kutoka Mtwara hadi Tanga.

“Shughuli za utafutaji wa mafuta zilianza rasmi mwaka 1973 na kampuni hiyo ikagundua gesi asilia katika eneo la Songo Songo mwaka 1974. Kwa kuwa lengo lilikuwa ni kupata mafuta, AGIP ilirudisha eneo hilo kwa Serikali mwaka 1975 na kuendelea na utafutaji wa mafuta.

“Wakati AGIP ikiendelea na juhudi za utafutaji mafuta, TPDC ilianza rasmi shughuli za uagizaji mafuta ghafi mwaka 1977,Mwaka 1980, Sheria ya Utafutaji na Uendelezaji wa Mafuta (Petroleum Exploration and Production Act, 1980) ilitungwa ili kuwezesha mikakati ya Serikali ya kuhamasisha ushiriki wa kampuni za kimataifa,”amesema.

MATUKIO MBALIMBALI WAKATI MHE. DKT. NCHEMBA AKIHITIMISHA HOJA ZA MAPENDEKEZO YA MPANGO WA MAENDELEO WA TAIFA KWA MWAKA 2022/23

$
0
0
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akihitimisha hoja za Mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2022/23, bungeni jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiteta jambo na Waziri wa Kilimo Mhe.Dkt.Adolf Mkenda (Mb), kabla ya kuhitimisha hoja za Mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2022/23, bungeni jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiteta jambo na Waziri wa Kilimo Mhe.Dkt.Adolf Mkenda (Mb), kabla ya kuhitimisha hoja za Mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2022/23, bungeni jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb), akifafanua hoja mbalimbali zilizowasilishwa na wabunge wakati wa kuchangia Mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2022/23, bungeni jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akipongezwa na Mbunge wa jimbo la Mchinga Mheshimiwa Salma Kikwete, baada ya kuhitimisha hoja za Mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2022/23, bungeni jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiteta jambo na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb), kabla ya kuhitimisha hoja za Mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2022/23, bungeni jijini Dodoma.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WFM)

MAAGIZO YA NAIBU WAZIRI BASHE KWA TUME YA TAIFA YA UMWAGILIAJI.

$
0
0

 Na Mwandishi Wetu -Dodoma


Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe. Hussein Bashe (MB) ameiagiza Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kupitia wahandisi wa wake wa mikoa kuainisha eneo linalofaa kwa kilimo cha umwagiliaji, na kusema kuwa ni ngumu kuwa na kilimo endelevu cha umwagiliaji kama hakuna mfumo endelevu wa kilimo hicho.

Naibu Waziri Bashe, ameyasema hayo jana jioni jijini Dodoma, alipokuwa katika kikao cha pamoja na wahandisi wa Umwagiliaji wa Mikoa na menejimenti ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.

Bashe alisema kuwa, wahandisi wa Umwagiliaji nchini wanatakiwa kwenda kusajili skimu zote za kilimo ili kuweza kupata picha halisi, na kuzitambua skimu hizo pamoja na eneo lote linalofaa katika kilimo cha umwagiliaji. “Potential areas za miradi zitambulike, na za mabwawa zitambulike, tutenganishe miradi inayoweza kufanywa kwa ujenzi shirikishi yaani force account na miradi mingine.” Alisisitiza Bashe.

Aliendelea kusema kuwa, ni Lazima Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ijue inajenga hekta ngapi mpya za Umwagiliaji, pamoja na kuzifanyia matengenezo skimu nyingine, na kujiekea malengo ili kuweza kufikia lengo la ilani ya Chama cha Mapinduzi inayotaka hekta zaidi ya milioni moja na laki mbili(1,200,000)kumwagiliwa ifikapo mwaka 2025.

Akiongea kuhusu Mitambo iliyopo katika sekta ya kilimo cha Umwagiliaji na kumilikiwa na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Naibu Waziri Bashe alisema, vifaa vyote vifanyiwe matengenezo na uanishwe ununuaji wa mitambo mipya.

Awali Naibu Waziri Bashe, aliagiza Tume hiyo kuwa na Muundo katika sekta ya kilimo cha umwagiliaji utakaoonesha wahandisi wa umwagiliaji wa Wilaya nchini na alisisitiza swala zima la kuandaa budget halisi itakayokidhi mahitaji ya Ofisi hiyo.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe alipokuwa akizungumza na wahandisi wa Umwagiliaji wa Mikoa nchini hawapo pichani Jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Profesa Henri Mahoo, akizungumza wakati wa kikao cha Naibu Waziri Bashe na Wahandisi wa Umwagiliaji wa Mikoa nchini hawapo pichani

Picha ikionesha Sehemu ya washiriki wa kikao, cha Naibu Waziri Bashe jijini Dodoma.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Bw. Daudi Kaali akizungumza wakati wa kikao cha Naibu Waziri Bashe na wahandisi wa Umwagiliaji wa Mikoa nchini. 

KIPI WATANZANIA WAASIA NA WAAJEMI WANAPATIA AMBACHO SISI TUNAKOSEA?

$
0
0
Na Togolani Mavura

Ni kawaida siku hizi kupokea simu, meseji ama ugeni wa ndugu, jamaa na marafiki kukuuliza na kuomba kama unaweza kusaidia kupatikana kwa ajira kwa ajili ya kijana au binti yao ama kufuatwa na kijana au binti mwenyewe. Mara nyingi utaachiwa nakala kivuli za vyeti vya ufaulu kwa ajili ya rejea
.
Pale nawe unapojaribu kupigia wenzako wawili watatu kuomba wakusaidie, unakuta na wao wanamaombi kama yako mengi na wengine wana wenza wao au wadogo zao nao wanatafuta ajira. Wakati mwingine tunaangukia kwenye lawama kuwa sisi si watu wa msaada kwa kuamini kuwa uwezo wa kusaidia tunao ila tu hatuna nia.

Swali lililonijia haraka haraka mawazoni mwangu ni kwa nini siwaoni Watanzania wenye Asili ya Kiasia na Kiajemi wakitembea na bahasha za khaki zenye nakala vivuli nao wakitafuta ajira? Nikajikuta najiuliza tena, mbona ni kama idadi yao katika Vyuo Vikuu vyetu ni ndogo sana? Na pale wanapokuwapo hao wachache mara nyingi huwakuta katika fani fulani fulani tu? Mara nyingi utawakuta kwenye shahada za udaktari na famasia, uhandisi, sayansi ya mifumo ya computer na masuala ya fedha ikiwemo bima, uhasibu, biashara na masoko. Ni nadra sana kuwakuta wenzetu hawa katika masomo ya fani za historia, mambo kale, sayansi ya siasa na utawala, sayansi jamii na sheria.


Juma lililopita nilipata fursa ya kuhudhuria mahafali ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Katika ukumbi ule uliokuwa na wahitimu wapatao 3,000 wa shahada za kwanza, pili na tatu, nilijaribu kuhesabu hawa wenzetu hawakuzidi 10.

Pamoja na kutoonekana kwa wenzetu hawa huko kwenye misururu ya Bodi ya Mikopo, usaili wa ajira serikalini na mahala pa kutolea nakala vivuli (photocopy), wanaonekana kwa wingi katika foleni za benki, TRA, Brela na Bandarini. Hili linafikirisha na limenipa maswali. Kuna kipi wenzetu wanapatia ambacho sisi tunakosea? Kipi tunaweza kujifunza kutoka kwao?

Bila shaka mimi si wa kwanza kujiuliza maswali haya. Wengi wamekuwa nayo. Hata ukitazama matajiri wakubwa hapa nchini utakuta wanatoka katika jamii hiyo hiyo tu. Karibia kila jamii za wenzetu hawa zilizoko nchini zina bilionea wake walau mmoja anayeibeba jamii yao. Iwe Ismailia, Ithna Asheria, Hindu, Bohora. Hali kadhalika Waburushi, Washihiri, Wamanga nk, Ni vigumu kuwataja Watanzania Wafrika katika orodha ya mabilionea nchini. Wengi wao pia ni mabilionea wa msimu na wengine huibuka na kuondoka na awamu ya uongozi wa nchi. Wenzetu hawa wapo tu. Hata ukisikia dili kubwa pia utakuta wapo wao.

Nakumbuka katika utoto wangu kuwasikiliza Marehemu Mchungaji Christopher Mtikila, Mwenyekiti wa Chama cha DP aliyekuja na hoja yake ya mkato na kuwatuhumu kuwa ni wenzetu hawa ni wezi na kuwaita ‘magabacholi’. Baadae nikamsoma Marehemu Mzee Idd Simba ambaye yeye alikuja na ‘Dhana ya Uzawa’ akijaribu kuyajibu maswali hayo katika muktadha wa historia.

Mchango wa Marehemu Mtikila hauwezi kutusaidia sana kwenda mbele. Maana kama hoja ni wizi tu, wenzetu wenye asili ya kiafrika nao wametuhumiwa kuiba na kufisadi nchi sana lakini hakuna cha maana kinachoonekana ama wanachoweza kutuonyesha. Hivyo kwa maoni yangu hii ni hoja muflis. Hoja ya Marehemu Mheshimiwa Idd Simba inayo mashiko. Yeye anadai, ukoloni na baadae Azimio la Arusha, vimechangia kwa kiasi kikubwa kuwanyima fursa Watanzania wa Jamii ya Kiafrika kumiliki mali na kuwa matajiri.

Maelezo ya Marehemu Mheshimiwa Idd Simba ni kuwa, wakoloni hawakuwaandaa Watanganyika Waafrika kwa shughuli za biashara bali kuajiriwa na kutumikishwa. Akadai kuwa hata baada ya uhuru, hapakuwa na jitihada za makusudi za kurekebisha hali hiyo. Azimio la Arusha kwa maelezo yake na vita vya uhujumu uchumi baadae, vilikuwa ni msumari wa mwisho kwenye jeneza la kuwazikia wajasiriamali Watanzania Waafrika. Kutokana na hilo, kukajengwa unyanyapaa dhidi ya Watanzania Waafrika kumiliki biashara na utajiri. Unyanyapaa huu amedai umejificha katika mifumo ya maamuzi na mabenki.

Maelezo ya Marehemu Mheshimiwa Idd Simba yanatusaidia kuelewa ukubwa wa tatizo na chimbuko lake. Hata hivyo, hayatusaidii kujibu tatizo lenyewe kwa ukamilifu wake. Baada ya mjadala ulioamshwa na Mchungaji Mtikila na Mzee Iddi Simba kumekuwepo na jitihada kadhaa za kurekebisha kasoro hizo za historia nchini. Kuundwa kwa Baraza la Uwezeshaji, Mifuko ya Uwezeshaji, Upendeleo kwa Watanzania Waafrika katika mchakato wa Ubinafsishaji na mengineyo yaliibua Watanzania Wazawa kiuchumi. Hata hivyo, baada ya muda, wengi wao walifilisika kwa sababu mbalimbali, wengine biashara zao zimekufa baada ya wao kufariki.

Uzoefu huo unaturudisha tena kwenye swali la msingi, ni kipi basi ambacho bado hatujakipatia sana? Mbona wengi wa hawa Watanzania wa Asili ya Kiasia na Kiajemi nao walikutana na misukosuko ya Uhujumu Uchumi na Utaifishaji huko nyuma? Iweje wameweza kuibuka tena na wenzetu sisi hata wale walioinuka wamerudi chini? Maswali haya yamenifanya nitafakari zaidi na kutizama nje ya lensi ya historia tu.

Binafsi, nimebahatika kuishi, kusoma na kukulia jirani na jamii hizi. Nimejifunza pia mawili matatu kutoka jamii zao ambayo huko awali sikuwahi kuyapa umuhimu mkubwa. Kadri umri unavyokwenda napata ufahamu na uelewa juu ya dhana kadhaa juu yao. Naweza kusema, wengi wao wana kipato cha kawaida sana tena chini ya kipato cha wengi wa jamii yetu. Isipokuwa, wao, mfumo wao wa maisha na utamaduni wao umejijenga katika taratibu kadhaa za maisha ambazo zinawapa faida kadhaa kushinda sisi. Aidha, muono wao juu ya maisha nao unasaidia kuyatafsiri maisha katika namna tofauti na sisi.

Tofauti na Watanzania Waafrika, wenzetu hawa kwa sababu za kihistoria wamejikuta wanasukumwa kutafuta maisha katika sekta binafsi zaidi kuliko sekta ya umma. Kwa sababu za kihistoria, baada ya uhuru kulikuwepo wimbi kubwa la kutoa kipaumbele kwa Watanzania Waafrika ambao walionekana kukosa fursa wakati wa uhuru katika utumishi wa umma (africanization). Matokeo yake ilikuwa ni kuzaliwa kwa ‘unyanyapaa bubu’ (silent discrimination) dhidi yao hali iliyowafanya wasitamani kutafuta ajira katika Serikali na taasisi zake.

Hii kwao ilikuwa ni faida ya kwanza kabisa. Kwa mtazamo wangu, hii iliwafanya wasiione hatima yao katika ajira (employment) ambazo nyingi zilikuwa katika sekta ya umma. Wao wakajikita zaidi katika biashara na kazi (jobs) na ajira chache katika shughuli wanazozimiliki ambazo ni biashara. Ndio maana utawakuta zaidi katika ajira za masoko, uhasibu, menejimenti na baadae mifumo ya computer.

Kutokana na mazingira hayo, hali hiyo ikawapelekea pia kuwekeza zaidi katika elimu ya stadi za kazi na vitendo badala ya nadharia na ufahamu. Kwa lugha nyepesi, kwao hakuna umuhimu sana wa kufika chuo kikuu kama huendi kusomea udaktari, ufamasia, uhandisi na kwa kiasi uhandisi wa mifumo ya computer. Ndio sababu kadiri unavyokwenda kwenye elimu ya sekondari ya juu (Advanced Level Secondary Education) idadi yao inapungua sana. Badala ya kuhangaika na kutegesha michepuo (balancing combination), wao wanaanza kusomea stadi za kazi moja kwa moja. Wengi wanaanza kusomea elimu ya vyeti na utaalam wa masuala mahsusi. Utawakuta kwenye mitihani ya bodi (chartered institutes) za uhasibu za ndani na nje ya nchi, mitihani ya bodi za mifumo ya teknolojia na mifumo ya computer, masuala ya benki, bima, masoko, menejimenti na rasilimali watu, masuala ya forodha (customs clearing and forwarding) na ualimu wa chekechea (Early Childhood Teachers Training). Ndio sababu hutawakuta kwenye msururu wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi. Kwao, hakuna ufahari kuwa na cheti cha shahada ya kwanza ya Chuo Kikuu (University Degree) bali Cheti cha Stadi.

Kwa kuwa kwao ajira (employment) si hatima yao bali hatma yao iko kwenye kazi na shughuli za kutafuta rizki na kipato(jobs), hivyo mfumo wao wa maisha umewaandaa kwa kutafuta kipato (income) na si mshahara (salary). Hii inawafanya kuwaandaa watoto wao kutafuta na kuheshimu kipato. Maana yake, wanawaandaa kwa kazi ama shughuli yoyote. Muhimu kwao ni kupata kipato kuwezesha kuendesha maisha. Tofauti na ajira, kipato si lazima kiambatane na heshima ya kukaa ofisini, kwenye kiyoyozi, kuvaa rasmi sana na kuwa na hadhi. Mara nyingi, hayo ambayo huambatana wakati mwingine na mshahara duni. Kipato si lazima kiwe cha mwezi na anayetafuta kipato anaweza kupata zaidi ya yule anayepata mshahara wa mwezi. Isitoshe, kuishi na kipato kunahitaji pia nidhamu tofauti kuliko kuishi na mshahara.

Mengi ambayo nimeyaandika hapo juu yaweza yasiwe mapya sana. Tunaweza kutoa mifano mingi ya Watanzania Waafrika ambao nao wanayafanya hayo. Hata hivyo, hayo pekee si yanayofanya wenzetu hususan Watanzania wa jamii ya kiasia kupata matokeo tofauti. Siri kubwa iko katika mfumo wa maisha na mfumo wa mbeleko (social support system) walionao. Hapa ndio tofauti kubwa kati yetu na wao ilipo. Hapa ndio njia panda tunayoachania.
Kutokana na mazingira yao na haja ya kujihami (self-help), pengine kutokana na uchache wao, wamejitengenezea mifumo inayohakikisha ustawi wa jamii zao. Wamehakikisha jumuiya zao zinakuwa na uongozi na mifumo ya uendeshaji, wanamiliki huduma za jamii ikiwemo shule, hospitali na hata makaburi. Wamekwenda mbali zaidi kuwa na mifumo inayokusanya na kuhifadhi takwimu na kumbukumbu ya kila mmoja wao (census and data registry), kuwa na mifumo yao fedha na kumiliki mabenki (financial systems), mifuko ya wakfu (endowment funds) wa kusaidia wasiojiweza na mifumo ya usuluhishi wa migogoro na maamuzi (dispute and conflict resolution mechanisms). Kwa lugha nyepesi ni kama wanazo mamlaka na serikali ndogo katika jamii zao. Na mifumo yao huwafanya kila mwana jumuiya kuwa tegemezi zaidi kwa mfumo huo kama ‘samaki na maji’. Kiasi kwamba, kutengwa na jumuiya yako kwa kukiuka miiko na masharti ni jambo ambalo kila mmoja analiepuka.

Kutokana na mifumo hiyo, kila mwana jumuiya yao, hata kama hana fedha, anajikuta anamiliki mtaji jamii (social capital) mkubwa sana wa kuanzia maisha kuliko wenzetu na sisi. Kwa kuwa tu mwanajumuiya, unaaminika, unakopesheka, unaajirika na unadhaminika popote. Nirahisi kwa mwanajumuiya kutafuta na kupata kazi. Kazi itatangazwa kwanza ndani ya jumuiya yao kabla ya kutangazwa nje. Ukihitaji mkopo, ni rahisi kukopesheka na kuminiwa bila kuwa na dhamana yenye thamani kubwa (collateral). Ukiugua, unayo bima ya uhakika ya matlbabu na pale ambapo kuna tozo za huduma, basi tozo kwa wanajumuiya huwa ya chini kuliko ya wasio wanajumuiya katika shule na hospitali zao.
Aidha, mwanajumuiya anapopata tatizo, Jumuiya inayo wajibu wa kumhangaikia. Ukifiwa, huna sababu ya kuwaza kitapikwa nini na marehemu atazikwa wapi. Wajibu wako ni kulia na kuomboleza maana Jumuiya itashughulika. Hali kadhalika, kijana akihitaji kuoa na kuanza maisha. Kila mwana jumuiya ana wajibu kwa wanajumuiya wengine. Haishangazi kuwa ni nadra kuwakuta wamefikishana Polisi na Mahakamani panapotokea kutokuelewana. Na hata anaposhitakiwa na mtu wa nje ya Jumuiya yao, jumuiya humuwekea dhamana. Ndio maana hutawakuta wenzetu hawa kwa wingi katika mahabusu zetu. Ukimkuta, ujue hiyo kesi ni ngumu sana.

Mfumo wao huo wa maisha unawafundisha jambo lingine muhimu sana ambalo sisi tunapungukiwa. Nalo ni nidhamu na utamaduni wa kuweka akiba (saving discipline and culture). Katika kuishi kwangu nao, nimeona namna ambavyo vipaumbele vyao ni tofauti na vyetu. Mathalan, katika utamaduni na mifumo yetu ya maisha tunafuja na kutapakanya sana mali. Vitu kama ndoa za mitala (polygamy) na ‘nyumba ndogo’ na namna tunavyoendesha ndoa hizo, idadi kubwa ya watoto tunaozaa, matumizi makubwa ya anasa, starehe na ulevi, ufahari katika umiliki wa vitu tusivyovihitaji sana katika maisha lakini tunavihitaji zaidi kwa ajili ya kukogana nk. Tunafanya harusi na misiba ya gharama na ni rahisi zaidi kuchangishana kwa harusi ya siku moja na maziko ya kifahari ya siku moja kuliko kumchangia mtoto wa jamii yetu ada, kuanza maisha ama kumtibu anapoumwa. Sisi vipimio na vigezo (metrics) za mafanikio ni kumiliki nyumba ya kifahari na magari (nyingi ya hizi ni mitaji mfu / dead capital), kwao, ni kumiliki biashara na sifa ya jina la familia.

Mfumo wetu wa familia (extended family) nao ni tegemezi sana kwa watu wachache, Ni mfumo unaowaelemea wachache wenye nacho na kuwazuia watu wasiweze kujiwekea akiba. Ni rahisi kukuta mtu mmoja ama familia moja imebeba familia tatu ama ukoo. Kwa wenzetu utamaduni ni kuungishana. Ukiwa na biashara, wa Jumuiya yako watanunua kwanza kwako kabla ya kununua kwingine na hawatakudhulumu ama kukulalia kwa sababu wewe ni rafiki au ndugu. Sisi ni tofauti. Ukianzisha huduma au biashara, ndugu na marafiki ndio ama hawatanunua, ama wakinunua wanakulalia, ama hawakulipi kwa wakati ama hawakulipi kabisa. Aidha, wenzetu wanafungua biashara zenye kuongeza mnyororo wa biashara na thamani (value chain) kutoka pale anapoishia mwenzako na si kuigana (copy cut) na kumalizana wenyewe kwa ushindani usio na afya (unhealthy competition). Matokeo yake, sote hatukui, sana sana baada ya muda, sote tunakufa.

Nimalizie kwa kusema, mtazamo huu si timilifu wala si utafiti wa kitaaluma. Hata hivyo, unaweza kusaidia wanataaluma wetu kupata kwa kuanzia na sisi wengine kupata kutafakari. Kwa kufanya hivyo kutatusaidia kuondokana na dhana fulani fulani ambazo tumezikumbatia ambazo hazitusaidii sana. Ile dhana kuwa wenzetu hawa ni wezi, walibebwa na historia, ni matajiri tu kwa kuzaliwa na wanarithishana utajiri ni dhana ambazo hazitufikishi popote zaidi ya kutujengea chuki, mashaka na kututia ganzi. Jawabu lipo katika kuwasoma na kuwaelewa. Na somo lenyewe ni kuwa nidhamu (discipline) na taasisi imara (robust institutions) ndio jawabu la jamii yoyote yenye mafanikio iwe ya binadamu ama mdudu. Ndio maana nyuki na siafu wanafanya mambo makubwa ya kujenga (constructive) wakati nzi na mbu wanafanya makubwa ya kubomoa (destructive).
Hata katika jamii zetu ambazo zimefanikiwa kiasi kwenye kujenga nidhamu na taasisi imara kama familia na jumuiya, unaiona tofauti. Wenzetu Wapemba, Wakinga na Wachagga wana kiwango fulani cha nidhamu na wanamifumo yao ingawa si kwa mapana kama ya wenzetu na tunaona ambavyo wanapata matokeo chanya. Vivyo hivyo ukishuka kwa baadhi ya koo na familia ukweli huu unajidhihirisha. Ndio maana tunayo kwa mfano, familia ya Marehemu Hubert Kairuki wanaomiiki hospitali ya Kairuki na Chuo Kikuu cha Tiba kwa miaka zaidi ya 25, 19 kati ya hiyo, baada ya kufariki muasisi wa hospitali hiyo. Ni moja ya mifano michache tunayoweza kuitoa. Lipo la kujifunza kutoka kwa wenzetu hawa kama tunataka kutoka hapa tulipo. Bahati mbaya haya si mambo wataalam wetu wa uchumi, jamii na biashara wanatafiti wala kuchapisha.

NAPE;JPM KALA MKOPO

$
0
0

Jpm kala mkopo kwa kujenga mradi wa umeme mkubwa,Bwawa la Rufiji (Bwawa la Mwalimu Nyerere) unaozidi uwezo wa umeme wote unaozalishwa tangu mkoloni,Nyerere,Mwinyi,Mkapa na Kikwete na Sasa hakuna tena mgao wa Umeme,tutapata Umeme na kusaza,tutasahau habari ya iptl,dowans,Richmond na Escrow!.

Jpm kala mkopo kwa kujenga Reli ya Umeme,Reli ya kisasa yenye uwezo mkubwa wa kwenda kwa haraka na kubeba mzigo mkubwa kuliko Reli zote nchini,Treni ambayo itatumia saa moja na nusu toka Dar hadi Morogoro,na Masaa matano tu toka Dar hadi Mwanza,hii imefanya kuharakisha Maendeleo,badala ya kusafiri Masaa 17 toka Dar hadi Mwanza,sasa hivi ni masaa 5 tu kwa treni ya Umeme ya SGR.

Jpm kala mkopo kwa kujenga maghala ya kutunzia vyakula kwa mikoa yote inayozalisha vyakula kwa hifadhi za taifa letu,Sasa Taifa limekuwa na hifadhi ya kutosha ya Mazao ya Chakula.!.

Jpm kala mkopo kwa kufufua shirika la ndege la atcl na ununuzi wa ndege zake kumi na moja kwa ajili ya kukuza na kuboresha sekta ya Utalii,hivi sasa tunashuhudia Watalii zaidi ya 1,000 wakitua nchini.

Jpm kala mkopo kwa kutoa ruzuku ya kielimu ( elimu bure) kwa shule za misingi na sekondari,hivi sasa hakuna mtoto asiyejua kusoma wala kuandika.!.

Jpm kala mkopo kwa kujenga hospitali kwa wilaya zote ambazo hazikuwa na hospitali za wilaya na vituo vya Afya zaidi ya 300 nchini baada ya kuvikuta vituo 67 tu!

Jpm kala mkopo kwa kumalizia miradi iliyoanzishwa na watangulizi wake ambayo ilikwama kuendelea baada ya pesa kupigwa ama ujenzi usioridhisha kama barabara,Madaraja,Viwanja vya ndege vya zamani na Vipya,Kujenga barabara za juu na zile za kukatisha bahari ya hindi na kule ziwa Victoria na vivuko mbalimbali.

Jpm kala mkopo kwa kuendelea kujenga miundombinu ya bandari na ujenzi wa meli mpya kwa maziwa ya Nyasa,Victoria na Tanganyika!.

-Kwa nini Jpm alikula mkopo,

JPM alikula mkopo kwa sababu ni Mzalendo na aliyoyafanya kila Mtanzania ameyaona hata watoto wadogo wanajua,Jpm aliyoyafanya yalikuwa damuni mwakw,ukimchana hivi damu yake inasema Mimi ni Mtanzania,nitapenda kuiona Tanzania ikiwa Taifa kubwa kama China.

-Jpm alikula mkopo mara tu baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuanza miradi mingi nchi nzima,miradi inayoonekana kwa macho na sio miradi hewa ama ya kitapeli kama miradi tuliyowahi kuisikia siku za nyuma,Miradi aliyofanya Jpm inaonekana wazi na Wananchi wanapata faraja,ni miradi ya barabara nchi nzima,meli,vivuko,umeme,maji,afya,utalii,bandari,na viwanja vya ndege,Siku za nyuma tulikuwa tunaambiwa maneno tu ama kuishia kuona ujenzi usioridhisha.

-Mwaka 2016 Jpm alikula mkopo pale alipoanza kwa vitendo kupiga kazi,Wazanzibari walimuita "Bosi kazi" Wazee wa Awamu ya nne waliita nguvu ya soda,lakini siku zilivyozidi kwenda wazee wa kitonga waligundua si povu wala nguvu ya soda bali mtendakazi yupo kazini.Ujenzi ulioanza na kumalizika ulitoa picha ya utendaji wa kutukuka katika awamu ya tano,Mwaka 2016 tulianza kuona matunda halisi ya maneno,ahadi na utendaji kazi wa Awamu ya tano na ukamilishwaji wa ilani ya CCM kwa asilimia 120.

-Jpm kala mkopo katenda haya yafuatayo,wenzangu na Mimi wale walikula mkopo sijui walifanya nini? Nothing to write home about!

1.Hostel za Chuo cha UDSM.

2.Hostel za Askari Magereza.

3.Ununuzi wa Ndege 11 (Nyingine 3 zinakuja mwakani).

4.Ujenzi wa Flyover Tazara na Ubungo.

5.Upanuzi wa Airport Mwanza
Upanuzi barabara ya Moroco Dar es Salaam.

6.Ujenzi wa Meli kubwa 6 katika Ziwa Victoria,Ziwa Tanganyika na Ziwa Nyasa.

7.Kukomesha Rushwa
Kurejesha nidhamu Makazini.


-Mwaka 2017 Jpm alikula mkopo pale tulipoona ujenzi mkubwa miradi mbalimbali ukianza.

-Uzinduzi ujenzi wa reli kwa ajili ya treni ya Umeme.

Ujenzi wa barabara ya Mtwara-Tandahimba

-Jpm alikula mkopo kwa kukomesha Watumishi Wenye Feki hivyo kuokoa Mabilioni ya Fedha.

Barabara ya kuunganisha Wilaya za Kibondo kigoma Kaliua huko Tabora.

Miradi Mikubwa ya Maji,Dar,Morogoro,Dodoma,Kigoma,Tabota,na Shinyanga.

Uwezeshaji Ujenzi Bomba la Mafuta kutoka Hoima mpaka Tanga.

-Jpm alikula mkopo kwa kuwa katika miaka yake mitano kila upitapo ujenzi ulikuwa unaendelea.

Dar es Salaam kila kona Barabara ya Tandale-Sinza- Mawasiliano barabara imejengwa,Mitaa ya Kinondoni hivi ina lami,Ubungo Interchange inajengwa
Madaraja yanajengwa

Upanuzi wa barabara kuu ya Ubungo hadi chalinze unafanywa kwa kiwango cha barabara nane.

-Jpm alikula mkopo kwa ujenzi wa Flyovers zinajengwa pamoja na barabara za ziwani na baharini.

-Jpm alikula mkopo kwa kuisimama vyema miradi ya umeme inajengwa na miradi mingi ni kwa hela za watanzania wenyewe,Miradi wa Umeme wa Gas wa Kinyerezi,na mradi wa Bwawa la Umeme la Rufiji (Bwawa la Umeme la Mwalimu Nyerere)

Miaka yote maeneo ya Mbezi na kimara walikuwa hawapati maji japo yanapita njia hiyo hiyo lakini sasa maji yamefika mbezi, na bado wanaendelea kutandaza mabomba ili kupeleka maji.

Awali waliokuwa wanakula hela za wananchi ni wenye miradi ya kuuza maji kwa magari. Ila sasa wananchi wamekombolewa.

-Jpm kala mkopo kwa kusimamia utendaji kazi na kufanya performance appraisals, Utendaji kazi umeimarika, sasa hivi kila mmoja anaona cheo akipewa ni kama kakalia kaa la moto.Yale mambo ya kupiga hela na kukaa ofisini kupiga usingizi yameisha watu ni kazi la sivyo unawajibishwa.

Madawa sasa yanapatikana hospitali, ile hali ya madawa ya hospitali yanapelekwa katika Pharmas binafsi imeisha.

Hospitali sasa za serikali ukienda mgonjwa anajaliwa sio kama ilivyokuwa awali.

-Jpm kala mkopo kwa kuleta Uwajibikaji,Taasisi za serikali wafanyakazi wamekuwa wanawajibika,hakika nidhamu imeimarika.

-Jpm kala mkopo kwa usimamizi madhubuti wa mapato ya Serikali, sasa taasisi za serikali zinajiendesha kibiashara na si kihasara kama ilivyokuwa awali, ilikuwa ni ulaji tuu wa hela, upigaji dili, taasisi zinakufa, hakuna gawio kwa serikali, ila sasa zinatoa gawio.

Hakika kila kitu ni usimamizi imara, ukicheka na kima utavuna mabua.

-Jpm kala mkopo kwa kusimamia nidhamu kazini,Awali watu walikuwa wanaulilia uongozi, hata wasio kuwa na elimu walikuwa wanagombea kupata uongozi, katika miaka yake mitano uongozi ulikuwa mgumu sababu kama wewe si muwajibikaji una ndoto za kupiga tuu, hupati nafasi, Uongozi umekuwa una hadhi kwa sasa.

@Nape pokea Salaam za mkopo aliokula JPM,hii ni robo tu ya mkopo aliokula JPM.

HAFLA YA UTIAJI SAINI HATI ZA MAKUBALIANO KATIKA NYANJA YA ELIMU, ELIMU YA JUU NA MICHEZO KATI YA TANZANIA NA MISRI IKULU CAIRO MISRI.

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Serikali ya Tanzania na Misri wakati wa hafla ya utiaji saini Hati za makubaliano katika Nyanja ya Elimu, Elimu ya Juu na Michezo kati ya Tanzania na Misri Ikulu Cairo Misri.
Rais wa Misri Mhe. Abdel Fatth Al Sisi, akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Serikali ya Tanzania na Misri wakati wa hafla ya utiaji saini Hati za makubaliano katika Nyanja ya Elimu, Elimu ya Juu na Michezo kati ya Tanzania na Misri Ikulu Cairo Misri.

NAWEKA REKODI SAWA JE PABLO FRANCO MARTIN, ALIWAHI KUWA KOCHA MSAIDIZI WA REAL MADRID?

$
0
0
Pablo amewasili leo asubuhi na kupokewa na Mratibu wa timu, Abbas Suleiman tayari kuanza kuutumikia mkataba wake wa miaka miwili akirithi mikoba ya Mfaransa, Didier Gomes Da Rosa aliyefukuzwa mwezi uliopita.

Taifa limeendelea kudanganywa kwa mara nyingine ,naweza kusema hivyo bila shaka. Pia, udhaifu wa wachambuzi wetu katika kulipokea jambo fulani kisha kulifanyia utafiti wa kina kabla ya kulizungumza ,limewekwa kapuni. Inahuzunisha kwa upande mmoja.

Kama Taifa inapofikia hatua hii, hatuna budi kujitazama upya. Taifa hili si Taifa la wendawazimu...Taifa hili sio Taifa la Vilaza.

Katika maendeleo ya utandawazi wa teknolojia yanayoibadilisha Dunia kila kukicha, ni kazi rahisi kudanganya na ni kazi ngumu vile vile kuficha ukweli...Kwanini?

Wiki hii klabu ya Simba ilimtangaza raia wa hispania aitwaye Pablo Franco Martin kuwa kocha wao mpya akichukua nafasi ya Didier Da Rosa aliyekatishiwa mkataba wake.

Hapana shaka kuwa, Pablo Franco Martin ni kocha msomi mwenye lesen ya Uefa A Pro. Leseni yake ni ya kiwango cha juu Barani Ulaya. Leseni hii katika madaraja ipo sawa na ile ya CAF A kwa upande wa Bara la Afrika.

Makocha wenye ngazi ya leseni hii ,utazamwa kuwa wakufunzi wa wanafunzi wa fani ya ukocha kwa wakati mwingine. Bila shaka yoyote,Pablo Franco Martin amejaza vyeti katika fani hii.
Pamoja na wasifu wa elimu yake, nimejikuta nikibakia na mshangao baada ya kusikia wasifu wa Pablo Franco Martin kuwa amewahi kuwa msaidizi wa Julen Lopetaqui kunako klabu ya Real Madrid. Kwanini nishangae?

Kwanza napenda utambue mgongano wa kimaslahi katika makala hii. Mtoa makala ni shabiki kindaki ndaki wa Real Madrid kwa zaidi ya miaka 20 sasa.

Kuwa shabiki sio kigezo cha kujua mengi kuhusu Real Madrid, ila mimi naweza kusema ni zaidi ya shabiki kwa uwanja wa kuifuatilia kila habari ya timu hii...Je kuna tatizo kwa Pablo Franco Martin?

KAMA TAIFA LIMEDANGANYWA...
Niliposikia jina la Pablo Franco Martin katika wasifu wa kuwahi kuhudumu kama kocha msaidizi wa Real Madrid kati ya Julai 31, 2018 hadi November 2, 2018, nilijiuliza maswali mengi...

Moja ..Hili ni jina geni katika masikio yangu kuwahi kulisikia ndani ya viunga vya Charmatin zilipo ofisi za Real Madrid jijini Madrid na katika viwanja vya Valdebebas mahala ambapo timu ya Real Madrid wanapofanyia mazoezi.

Pia ,jina hili ni geni kunako kiwanja cha Alfredo Di Stefano mahala ambapo Real Madrid Castilla (Madrid B) wanapoutumia kwa mechi zao.

Pia ,jina la Pablo Franco sio jina lenye maana kubwa ndani ya majukwaa la dimba la Santiago Bernabeu. Hii ina maana gani?;

PABLO FRANCO MARTIN HAJAWAHI KUWA KOCHA MSAIDIZI WA REAL MADRID

..Huu ndio ukweli uliofichwa ama unaofichwa makusudi na baadhi ya watu kwa maslahi yao.Mtu huyu anayetajwa kuwa amewahi kuwa kocha msaidizi kunako klabu ya Real Madrid ...ukweli hajawahi kuwa kocha wa Real Madrid ama kuwa mfanyakazi wa kawaida wa klabu ya Real Madrid.

Bahati mbaya porojo hizi, zimewaingia wachambuzi wetu vijana na wakongwe na kuonesha udhaifu mkubwa wa kulipokea jambo na kutolifanyia utafiti kwa kina. Uamuzi kama huu unaweza gharimu Taifa kwa wakati mwingine.

Uthibitisho wao (wachambuzi)ukapokelewa na mashabiki wa soka nchini na kila mmoja akizungumza wasifu huo bila kujua kuwa sio kweli.

Bahati mbaya hata wachambuzi wetu wakubwa nao wakajikuta wakiingia katika mkumbo huo. Wakatangaza kuwa Pablo Franco Martin alipata kuwa msaidizi wa Julen Lopetaqui kunako klabu ya Real Madrid....

UKWELI NI UPI SASA ?
Mnamo Julai 1, 2018..Real Madrid walimtangaza Julein Lopetaqui kuwa kocha wa klabu hiyo. Lopetaqui alichukuliwa toka timu ya Taifa ya Hispania na uamuzi wake huo ukapelekea mkataba wake na Chama cha soka cha Hispania ufikie tamati wa kuifundisha timu ya Taifa. Lopetaqui akaenda zake Real Madrid kwa madaha!

Real Madrid alienda naye Albert Celadez (Huyu ni mchezaji wa zamani wa Real Madrid) ambaye ndiye alikuwa kocha msaidizi namba moja kwa Julen Lopetaqui kunako klabu ya Real Madrid.

Huku msaidizi mwingine wa Lopetaqui alikuwa Pablo Sanz Iniesta. Huku kocha wa Makipa akiwa Juan Canales, msaidizi wake aliitwa Antolin Gonzalo. Timu ya makocha wa viungo ilikuwa chini ya Antonio Pintus (huyu alikuwa hapo tangu enzi ya utawala wa Zinedine Zidane) akiwa mkuu, huku akisaidiwa na Jose Conde, Javier Mallo (Mkufunzi wa viungo na msomaji wa wapinzani), na Oscar Caro. Hili ndio benchi la ufundi la Real Madrid chini ya Julein Lopetaqui.

Benchi hili la ufundi lilihudumu kunako Real Madrid kuanzia Julai 1, 2018 hadi October 28,2018.. na siku moja baadae yaani October 29,2018 baada ya kipigo toka kwa FC Barcelona.

Lopetaqui na benchi lake walifukuzwa kazi isipokuwa kwa Antonio Pintus na Javier Mallo pekee. Hawa wawili waliendelea kuwapo Real Madrid.

Miezi mingi baadae, Albert Celadez alikuja tangazwa kuwa kocha wa Valencia huku Julen Lopetaqui akiwa kocha wa Sevilla yupo na Pablo Sanz Iniesta, Oscar Caro hadi hivi leo.

Ikumbukwe kuwa Albert Celadez ndiye alikuwa kocha msaidizi wa Julen Lopetaqui tangu akiwa FC Porto, kisha wakakutana tena timu ya Taifa ya Hispania.

Albert Celadez akiwa kocha wa Timu ya Taifa ya Vijana na Lopetaqui akiwa kocha wa timu ya wakubwa. Lopetaqui akamfanya kuwa msaidizi wake nambari moja kwa timu ya Taifa ya wakubwa.

Baadae waliondoka wote na kuungana kunako klabu ya Real Madrid.. walipohudumu kwa siku 120 tu kabla ya kufukuzwa.

Julen Lopetaqui na msaidizi wake Albert Celadez waliishia kuiongoza Real Madrid katika mechi 14 tu. Wakishinda 6 wakitoa sare mechi 2 na kufungwa 6.

NI KWELI ALIKUWA MSAIDIZI WA SANTIAGO SOLARI KWA MECHI MOJA HAPO HAPO REAL MADRID?
Inachekesha wakati mwingine. Pablo Franco Martin sio tu hajawahi kuwa kocha msaidizi wa Real Madrid bali pia kufanya kazi kwenye sekta yoyote klabuni hapo.

Alipofukuzwa Julen Lopetaqui. Real Madrid ilimpandisha kocha wao wa timu ya vijana Santiago Solari ambaye pia alimteua Santiago Sanchez kuwa msaidizi wake mara moja.

Hivyo kuanzia October 29, 2018 kocha mkuu wa Real Madrid alikuwa Santiago Solari na msaidizi wake namba moja aliitwa Santiago Sanchez na meneja msaidizi aliitwa Jose Parrales (Msaidizi namba mbili) . Kocha wa makipa alikuwa Robert Vazquez. Huku Antonio Pintus na Javier Mallo waliendelea kuwa makocha wa viungo.

JE UDANGANYIFU HUU UMEANZIA WAPI?

Wasifu wa Pablo Franco Martin kuwa alipata kuwa kocha msaidizi wa Real Madrid, upo kwenye midomo ya wachambuzi wa soka wa Kitanzania na baadhi ya ripota wa habari za soka wachache wa wa kiafrika waliopokea habari kama ilivyo toka nchini kwetu.

Huku pia wasifu huu ukiwa umechomekwa katika mitandao ya "wikipedia na transfer Market " pekee. Mitandao hii miwili mtu yoyote yule ukiwa na account unaweza kurekebisha kwa kupunguza ama kuongeza taarifa bila vikwazo.

Mfumo huu unaifanya wavuti hizi isiwe cha nzo cha uhakika cha kuamini wala kuchukuliwa kama rejeo (reference) na haitambuliki kwenye mifumo ya ushahidi wenye kuthibitisha Duniani kote.

Jina la Pablo Franco Martin halipo kwenye list ya watu waliowahi kuwa makocha wasaidizi wa klabu ya Real Madrid zaidi ya miaka 20 iliyopita.

Inashangaza kuwa jina la Pablo Franco Martin halipo kwenye wavuti, kurasa rasmi za klabu ya Real Madrid za mitandaoni.

Kitu kingine kinachoshangaza pia...Huyu Pablo Franco hata uliandike jina lake "Google" hatambuliki kama aliwahi kuwa kocha wa Real Madrid tofauti na wavuti hizo nilizozitaja.

Katika picha za pamoja za benchi la Ufundi lililotangazwa mwezi Agosti ,2018 na Real Madrid chini ya Julen Lopetaqui halipo jina Pablo Franco Martin wala picha yake...hata katika benchi la ufundi la Santiago Solari halipo jina lake wala picha yake. Unajiuliza inakuwaje?

WAKENYA WANA AKILI SANA...
Wakala wa Pablo Franco Martin aliyemleta Simba nii Mkenya. Ndio, ni mkenya. Bila shaka ,wakenya wanajua akili zetu watanzania zilivyo.

Wanajua kucheza na fursa..wanajua kucheza na hisia zenu. Mwisho wanajua nini tunataka..

Nyuma ya Pablo Franco Martini katika ujio wake kuja Simba, wako watu wanaojua nini wanafanya...ni wenye akili mno. Niwapongeze katika hilo.

Walianza kucheza na wavuti zile ambazo wabongo wengi tunakimbilia kama wikipedia, kisha transfer Market....walipofanikiwa hapa...wakajua kabisa hata wachambuzi wetu wataishia hapa.

Wachambuzi wetu hawakutaka kuzisumbua akili zao. Hata kujaribu kufuatilia je ni kweli aliwahi kuwa kocha msaidizi wa Lopetaqui kunako Real Madrid?

Hawakujaribu hata kutafuta picha zake akiwa kwenye benchi la Real Madrid na wachezaji.

Kama hakuna...katika kila klabu na kila kocha mpya anapokuja kuna utaratibu wa picha rasmi la benchi la ufundi je Pablo Franco Martin yupo?..Hakuna.

Porojo zile zile za Inonga Baka kuitwa timu ya Taifa ya DRC wakati sio kweli ndio hizi hizi za Pablo Franco kuwahi kuwa msaidizi wa Real Madrid. Wakati si kweli...Inahuzunisha!

Nb.Hata Pablo Franco Martini mwenyewe hajui kama aliwahi kuwa kocha msaidizi wa Julen Lopetaqui kunako Real Madrid..ujue...

Ukitaka uthibitisho wa wasaidizi hawa tafuta kurasa rasmi za Real Madrid, wavuti yao, na google kwa ushahidi wa picha hata kutazama youtube ila kote huko hayupo Pablo Franco Martin...Hizi habari za Pablo franco kwa Real Madrid ni Propaganda tu.

@Nihzrath Ntani Jnr (Madridista)
Ukonga-DSM

WAZIRI WA ZANZIBAR ATEMBELEA BANDA LA NSSF KATIKA MAONYESHO YA WIKI YA HUDUMA ZA FEDHA

$
0
0
Mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, Waziri wa Nchi Afisi ya Rais , Fedha na Mipango, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Jamal K. Ali, alipotembelea katika banda la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF). Maonesho ya Wiki ya Huduma za Fedha kitaifa yanaendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja ambapo NSSF inaendelea kutoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa sekta binafsi na sekta isiyo rasmi.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba akipata maelezo kutoka kwa Afisa matekelezo mwandamizi Hawa Godigodi, alipotembelea banda la NSSF wakati wa Maonesho ya Wiki ya Huduma za Fedha kitaifa katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii(NSSF) Masha Mshomba akielezea huduma mbalimbali zinazotelewa na NSSF katika maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa. Katika maadhimisho hayo NSSF inatoa elimu kuhusu hifadhi ya jamii, elimu kuhusu umuhimu wakujiwekea akiba, elimu ya huduma zinazotolewa kwa njia ya mtandao ambapo ndio kipaumbele muhimu cha Mfuko pamoja na kueleza fursa za uwekezaji.
Mkurugenzi wa Idara ya Hifadhi ya Jamii, Ofisi ya Waziri Mkuu, Festo Fute (katikati) akisisitiza jambo alipotembelea banda la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakati wa Maonesho ya Wiki ya Huduma za iFedha kitaifa katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba, kulia ni Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma, Lulu Mengele pamoja na wafanyakazi wa NSSF
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Dkt. John Mduma (kulia), akipata maelezo mbalimbali kuhusu ushiriki wa NSSF katika Maonesho ya Wiki ya Huduma za Fedha kitaifa. Maonesho haya yanaendelea katika viwanja vya Mnazi mmoja, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba akitoa maelezo kwa Waziri wa Nchi Afisi ya Rais , Fedha na Mipango, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Jamal K. Ali kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na NSSF wakati wa Maonesho ya Wiki ya Huduma za Fedha kitaifa katika viwanja vya Mnazi mmoja.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba (wa kwanza mstari wa mbele) akiwa katika ufunguzi wa Maonesho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam
Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Jamal K. Ali (aliyekaa katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Kamishna Uendelezaji wa Sekta ya Fedha kutoka Wizara ya Fedha Dkt. Charles Mwamwaja (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Fatma Nyangasa na viongozi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba, akiwa katika maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa ambapo alipata fursa ya kutembelea na kupata maelezo katika banda la Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF). Mifuko hiyo ipo katika viwanja vya Mnazi mmoja kutoa elimu kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa kwa wanachama wao.

WAZIRI MCHENGERWA ATEMBELEA OFISI ZA TUME YA UCHAGUZI JIJINI DODOMA

$
0
0
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera (kulia) akizungumza jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Mohamed Mchengerwa wakati Waziri na Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma walipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dodoma, Novemba 10,2021. (Picha na Mroki Mroki).
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera (kushoto) akizungumza jambo baada ya kumkabidhi taarifa ya uchaguzi mkuu wa 2020 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Mohamed Mchengerwa wakati Waziri na Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma walipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dodoma, Novemba 10,2021. (Picha na Mroki Mroki).

MADAKTARI WAZAWA WABADILISHA MSHIPA WA DAMU ULIOTANUKA NA VALVU YAKE

$
0
0
Madaktari wazawa mabingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa kubadilisha mshipa mkubwa wa damu (aorta) uliokuwa umetanuka pamoja na valvu yake (Aortic valve insufficiency) bila ya usimamizi wa madaktari kutoka nje baada ya miaka kadhaa ya kujifunza upasuaji huo kutoka kwa wataalam wenzao wanaofika JKCI kwa ajili ya kubadilishana uzoefu.

Kwa mara ya kwanza madaktari wazawa mabingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wamefanya upasuaji wa kubadilisha mshipa mkubwa wa damu (Aorta) uliokuwa umetanuka pamoja na valvu yake (Aortic valve insufficiency) bila ya usimamizi wa madaktari kutoka nje baada ya miaka kadhaa ya kujifunza upasuaji huo kutoka kwa wataalam wenzao wanaofika JKCI kwa ajili ya kubadilishana uzoefu.

Upasuaji huo unaojulikana kwa jina la kitaalamu la Bentall Surgery uliochukua masaa matano kukamilika ulifanyika hivi karibuni ambapo mgonjwa anaendelea vizuri na anatarajia kuruhusiwa wakati wowote kuanzia sasa.

Mgonjwa huyo alikuwa anasumbuliwa na maumivu ya kifua na baada ya uchunguzi aligundulika kuwa mshipa mkubwa wa damu (aorta) unaotoa damu kutoka kwenye moyo na kusambaza damu mwili mzima umepanuka sana na valvu yake ya moyo inavuja damu.

Akizungumzia upasuaji huo Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Upasuaji wa Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Godwin Sharau alisema tatizo hilo mara nyingi huwapata watu wengi wenye umri wa kuanzia miaka ya 50 kwenda juu lakini pia uwapata watu wanaosumbuliwa na shinikizo la damu la muda mrefu hivyo mshipa huo kupoteza umahiri wake wa kuweza kustahimili presha.

Dkt. Sharau ambaye pia ni daktari bingwa wa upasuaji wa moyo kwa watoto alisema kwa mgonjwa ambaye hatapata matibabu husika kwa wakati mshipa huo huendelea kutanuka na hivyo kupelekea kufa ghafla.

“Kwa miaka mingi upasuaji wa Bental operation kwa hapa JKCI umekuwa ukifanyika lakini chini ya usimamizi wa madaktari wenzetu kutoka nje ya nchi, sasa wataalam wetu wameonesha umahiri mkubwa wa kufanya upasuaji huu. Hii ni hatua nzuri sana katika Taasisi yetu”, alisema Dkt. Sharau.

“Upasuaji wa kubadilisha mshipa mkubwa wa damu (Aorta) uliotanuka pamoja na valvu yake huchukua muda mrefu kutokana na ubadilishaji wa mishipa lakini pia baada ya upasuaji huu mgongwa anaweza akavuja damu kwa wingi na wakati mwingine kupoteza maisha”, alisema Dkt. Sharau

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya upasuaji watu wazima wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Evarist Nyawawa alisema mgonjwa huyo baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kina ilionesha yakuwa mshipa mkubwa wa damu (Aorta) ulikuwa umetanuka kiasi cha kwamba muda wowote ungeweza kupasuka.

“Mgonjwa tuliyemfanyia upasuaji wa mshipa wake mkubwa wa damu (Aorta) pamoja na valvu yake (Aortic valve) iliyokuwa inarudisha damu kwenye chemba ya kushoto ya moyo ilikua inamfanya mgonjwa akose nguvu na kushindwa kupumua vizuri”, alisema Dkt. Nyawawa.

“Sasa tuna uzoefu mkubwa naamini tutaendelea kuokoa maisha ya watanzania wengi ambao wanahitaji upasuaji kama huu, na hii itapunguza wagonjwa kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kutafuta huduma za kibingwa za matibabu ya moyo”, alisema Dkt. Nyawawa

Naye Mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji wa kubadilisha mshipa mkubwa wa damu (aorta) uliotanuka pamoja na valvu yake (Bental operation) Benny Mongi aliwashukuru wataalamu hao wa JKCI na kuwapongeza kwa kutumia utaalam wa hali ya juu waliokuwa nao kwa kuokoa maisha yake.

“Nimeambiwa huduma kama hii niliyofanyiwa na madaktari wa JKCI haikuwahi kufanyika kupitia madaktari wazawa lakini kwangu wameweza, nikirejea nyumbani baada ya matibabu haya naenda kutoa ushuhuda wa huduma hii niliyoipata hapa hapa Tanzania ili watanzania wenzangu wafahamu na kutumia vizuri rasilimali zetu ambazo serikali yetu imetuwekea”,.

“Nimekuwa nikitafuta hewa kwa mikono kutokana na matatizo ya moyo niliyokuwa nayo, sikuwa naweza kupumua kabisa mikono yangu muda wote ndio ilikua ikinisaidia kujipulizia ili nipate hewa, sitaacha kumshukuru Mwenyezi Mungu na wataalam hawa kwa kuokoa maisha yangu”, alisema Mongi.

Kwa kipindi cha mwezi mmoja wa Oktoba hadi Novemba 2021 madaktari wazawa mabingwa waupasuaji wa moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wamefanya upasuaji wa kubadilisha mshipa mkubwa wa damu (aorta) uliokuwa umetanuka pamoja na valvu yake (Aortic valve insufficiency) bila ya usimamizi wa madaktari kutoka nje ya nchi kwa mgonjwa mmoja na upandikizaji wa mishipa ya damu ya moyo bila ya kusimamisha moyo kwa wagonjwa watatu.

MHE. RAIS SAMIA AKAMILISHA ZIARA YAKE YA KISERIKALI YA SIKU TATU NCHINI MISRI

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na Waziri wa Nchi anaeshuhulikia masuala ya Uhamiaji na Wamisri nje ya nchi, wa Misri Mhe. Nabila Makram, katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Cairo Misri alipokua akiondoka Misri na kurejea Tanzania baada ya kukamilisha ziara yake ya siku tatu nchini Misri leo tarehe 12 Novemba 2021

RAIS SAMIA SULUHU ATEMBELEA JENGO JJIPYA LA MAKUMBUSHO KATIKA MJI MPYA WA SERIKALI CAIRO NCHINI MISRI

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipata maelezo kuhusu uhifadhi wa nyaraka mbalimbali alipotembelea Jengo jipya la Makumbusho katika mji mpya wa Serikali Cairo nchini Misri jana jioni.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitembelea Jengo jipya la Makumbusho katika mji mpya wa Serikali Cairo nchini Misri jana jioni.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitia saini kitabu cha kumbukumbu alipotembelea Jengo jipya la Makumbusho katika mji mpya wa Serikali Cairo nchini Misri jana jioni.

‘WADAU WA AFYA WEKEZENI KWENYE RASILIMALI WATU’ MHE UMMY

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa kufunga mradi wa usaid boresha afya kanda ya kaskazini, kati na kusini, utakaofanyika tarehe 11 novemba, 2021 katika hoteli ya rafiki jijini dodoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu akikagua maonyesho ya huduma za USAID Boresha Afya wakati wa kufunga mradi wa usaid boresha afya kanda ya kaskazini, kati na kusini, utakaofanyika tarehe 11 novemba, 2021 katika hoteli ya rafiki jijini dodoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu katika picha ya pamoja na wataalaam wa Mradi wa USAID Boresha Afya wakati wa kufunga mradi wa usaid boresha afya kanda ya kaskazini, kati na kusini, utakaofanyika tarehe 11 novemba, 2021 katika hoteli ya rafiki jijini dodoma
Wageni waalikwa wakifuatilia hafla ya kufunga mradi wa usaid boresha afya kanda ya kaskazini, kati na kusini, utakaofanyika tarehe 11 novemba, 2021 katika hoteli ya rafiki jijini dodoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika la Kimataifa la Watu wa Marekani (USAID Tanzania), Kate Samvongsiri, (Pili kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa EGPAF Sajida Kimambo(Kwanza Kushoto), Mkurugenzi wa Deloitte Consulting Limited,Carlton Jones(Kwanza kulia) pamoja na Mkurugenzi wa USAID Boresha Afya Kanda ya Kaskazini na Kati Dr.Marina Njelekela
Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika la Kimataifa la Watu wa Marekani (USAID Tanzania), Kate Samvongsiri akizungumza wakati wa kufunga mradi wa usaid boresha afya kanda ya kaskazini, kati na kusini, utakaofanyika tarehe 11 novemba, 2021 katika hoteli ya rafiki jijini dodoma
Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu amewataka wadau wanaotekeleza Afua za nchini kuwekeza kwenye ajira za watumishi wa Afya ili kukabiliana na upungufu wa watumishi wa kada hiyo uliopo hivi sasa.

Waziri Ummy ameyasema hayo wakati wa kufunga mradi wa USAID Boresha Afya Kanda ya Kaskazini, Kati na Kusuni iliyofanyika leo Jijini Dodoma.

Amesema nimesikia changamoto mbalimbali zilizowasilishwa na wadau ambao wametekeleza kazi za mradi huu ikiwemo upungufu wa watumishi, hii ni changamoto ambayo Serikali inaitambua na inatoa kipaumbele na mpaka sasa tumeshapeleka maombi ya Kibali cha ajira Utumishi ili tuweze kuajiri wataalamu hao.

“Watumishi wa Afya waliopo hivi sasa ni 47% tu ya mahitaji hivyo tuna upungufu wa 53% hata tukiajiri hatuwezi kumaliza tatizo hili hivyo ni vyema na wadau wetu mkatuunga mkono” alisema Ummy.

Kila Mdau akiweka kipengele cha kuajiri wataalam wa Afya hata wawili tu kwa mwaka itasaidia katika kuboresha eneo hilo na kwa pamoja tukazidi kuboresha Afya Nchini.

Akizungumza katika kikao hicho Mkurugenzi wa Huduma za Afya Ustawi wa Jamii na Lishe Dkt. Ntuli Kapologwe amesema mradi wa USAID Boresha Afya umefanikisha kuboresha huduma za Afya Nchini ikiwemo ujenzi wa vituo bora vya Afya, upatikanaji wa vifaa na vifaa tiba, kuboresha na kuwezesha mazingira bora kwa watu wanaoishi na maambukizi ya VVU/UKIMWI kupata huduma katika vituo vyote vya Kutolea huduma za Afya Nchini.

Naye Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika la Kimataifa la Watu wa Marekani (USAID Tanzania) Kate Somvongsiri amesema mpaka mradi huu kwisha wametumishi Dola za Kimarekani Mil. 220 sawa na fedha za Kitanzania Takribani sh bil 450 katika utekelezaji wa kazi mbalimbali za mradi huo.

USAID imeweza kutoa ufadhili wa utekelezaji wa miradi miwili ambayo ni USAID boresha Afya mmoja ukiongozwa na EGPAF na mwingine ukitekelezwa na Deloitte kwa kuahirikiana na waahirika wenza EngenderHealth, MDH na FHI360.

WAZIRI LUKUVI AKUTANA NA MKURUGENZI MKAZI WA USAID TANZANIA

$
0
0
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Marekani (USAID) nchini Tanzania Veeraya Kate Somvongsiri akimkabidhi zawadi Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi alipomtembelea ofisini kwake eneo la Mji wa Serikali Mtumba mkoani Dodoma tarehe 11 Novemba 2021.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Marekani (USAID) nchini Tanzania Veeraya Kate Somvongsiri (Kulia) akizungumza na Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mary Makondo alipokwenda kukutana na Waziri wa Ardhi William Lukuvi ofisini kwake eneo la Mji wa Serikali Mtumba mkoani Dodoma tarehe 11 Novemba 2021.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Marekani (USAID) nchini Tanzania Veeraya Kate Somvongsiri (wa pili kushoto) na viongozi wa Wizara alipotembelewa na Mkurugenzi huyo wa USAID ofisini kwake eneo la Mji wa Serikali Mtumba mkoani Dodoma tarehe 11 Novemba 2021.

Na Munir Shemweta, WANMM

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amekutana na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Marekani (USAID) nchini Tanzania Veeraya Kate Somvongsiri na kumuelezea hatua zinazochukuliwa na serikali katika kuimarisha sekta ya ardhi nchini.

Bi Kate alimtembelea Waziri Lukuvi katika Ofisi za Wizara zilizopo eneo la Mji wa Serikali Mtumba mkoani Dodoma leo tarehe 11 Novemba 2021 kwa lengo la kujitambulisha.

Katika mazungumzo yao, Waziri Ardhi alimueleza Mkurugenzi huyo wa USAID nchini kuwa, Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi iko katika jitihada mbalimbali kuhakikisha ardhi yote ya Tanzania inapangwa na kupimwa.

Kwa mujibu wa Lukuvi, pamoja na juhudi hizo, Wizara yake imeanza pia kuhifadhi kumbukumbu za ardhi kwa kutumia mfumo wa kidigitali na kuachana na ile mifumo ya zamani iliyokuwa ikitumia karatasi nyingi huku ikianza kutoa hati za ardhi za kielektroniki yenye kurasa moja.

‘’Tunataka kwenda mbele zaidi katika teknolojia ya uhifadhi wa kumbukumbu zetu za ardhi na tumeanza kuscan taarifa zetu za ardhi katika teknolojia na tumeanza pia kutoa hati za kielektroniki kwenye mkoa wa Dar es salaam na Dodoma’’ alisema Lukuvi.

Naye Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mary Makondo alisema, pamoja juhudi za Wizara kuhakikisha ardhi inapimwa vipaumbele pia vimeelekezwa kwenye maeneo ya vijijini ikiwemo kutumia njia rahisi ya upimaji na kutoa hati za kimila ili kulinda maeneo pamoja na kuwawezesha wananchi kiuchumi.

‘’Kwa sasa wizara ya ardhi inafanya jitihada kubwa kuhakikisha ardhi inapangwa na kupimwa ili kuepuka migogoro ya ardhi na wakati huo kuwawezesha wananchi kiuchumi pamoja na kuiwezesha serikali kupata mapato.’’ Alisema Mary

Kwa Upande wake Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Marekani USAID Veeraya Kate Somvongsiri aliunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali kupitia Wizara ya Ardhi na kusema kuwa Shirika hilo liko tayari kushirikiana na wizara ya ardhi kusaidia sekta ya ardhi nchini.

‘’Nimetembelea mkoa wa Iringa kunakofanyika mradi wa upimaji ardhi wa teknolojia rahisi vijijini (Feed the Future Tanzania Land Tenure Assistance) na kuona jinsi mradi huo ulivyofanikiwa ambapo niliangalia namna bora ya kusaidia miradi kama hiyo na nimeomba kupatiwa proposal kuhusiana na mafanikio ya mradi’’.alisema Kate

Serikali ya Marekani kupitia Shirika lake la Maendeleo la Marekani USAID imekuwa ikifadhili miradi mbalimbali nchini Tanzania katika nyanja za nishati, uhifadhi wa mazingira, huduma za afya ya uzazi na afya ya mtoto, huduma za kubabiliana na malaria na msaada kwa wakimbizi.

HAPPY BIRTHDAY ISAAC KIBODYA MKUU WA WILAYA

$
0
0

EBra NY akimtakia heri ya siku ya kuzaliwa mkuu wa Wilaya Isaac Kibodya ambayo leo ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake.
Happy Birthday Isaac Kibodya
Ebra NY akiwa na Isaac Kibodya nyumbani kwake Dodoma siku Ebra alipomtembelea Mkuu wa Wilaya Makao makuu ya nchi


 


AMIRI JESHI MKUU WA MAJESHI YA ULINZI NA USALAMA NCHINI ALIPOKUWA AKIFUNGUA MKUTANO MKUU WA TANO KWA MAKAMANDA WA JWTZ

$
0
0
Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama nchini na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, alipokua akifungua Mkutano Mkuu wa Tano wa Makamanda wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) 2021, uliojadili hali ya Jeshi pamoja na Taifa kwa ujumla ili kuweza kutekeleza majukumu yao kwa upeo wa pamoja katika Jeshi hilo. mkutano huo ulifanyika jana katika Kambi ya JWTZ 302 KV Lugalo Jijini Dar es Salaam.

RAIS WA ZANZIBAR DK.MWINYI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA WAWEKEZAJI JIJINI DARBAN

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Ujumbe wa Wawekezaji kutoka Nchini Misri ukiongozwa na Kiongozi Mkuu ya Kampuni ya Elsewedy.Mhandisi Ahmed El Sewedy na (kulia kwa Rais) na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar.Mhe Omar Said Shaban,mazungumzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Hoteli ya “The Oyster Box” Jijini Darban Afrika Kusini, baada ya kumalizika kwa hafla ya ufunguzi wa mkutano wa Maonesho ya Wafanyabiashara wa Nchi za Afrika
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika mazungumzo na Kiongozi Mkuu wa Kampuni ya El Sewedy kutoka Nchini Misri.Mhandisi.Ahmed El-Sewedy na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar.Mhe.Omar Said Shaban na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Tanzania Mhe. Exaud Kigahe, mazungumzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Hotel ya “The 0yster Box “ Darban Nchini Afrika Kusini, baada ya ufunguzi wa Maonesho ya Biashara kwa Wafanyabiashara wa Nchi za Afrika uliofanyika katika Ukumbi wa ICC Jijini Darban Nchini Afrika Kusini.


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Uongozi wa Benki ya Afrexim ukiongozwa na Kiongozi Mkuu wa Benki hiyo Bw.Amr Kamel na (kulia kwa Rais) Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar.Mhe.Omar Said Shaban,mazungumzo hayo yaliofanyika katika ukumbi wa jengo la mikutano la ICC Jijini Darban,baada ya kumalizika kwa mkutano wa ufunguzi wa mkutano wa Maonesho ya Wafanyabiashara wa Nchi za Afrika,uliofanyika katika ukumbi wa ICC Jijini Darban Afrika Kusini.(Picha na Ikulu)

WAZIRI UMMY MWALIMU AWAPONGEZA VIONGOZI HALMASHAURI YA TEMEKE

$
0
0
Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Ummy Mwalimu amewapongeza viongozi wa Temeke, akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mkurugenzi pamoja na watumishi kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya katika kusimamia miradi ya maendeleo.

Ametoa kauli hiyo leo Novemba 15,2021 wakati wa ziara yake ya kutembelea na kuangalia maendeleo ya miradi inayofadhiliwa na benki ya Dunia, kupitia miradi ya kimkakati ya uendelezaji wa jiji la Dar es Salaam (DMDP).

Miradi hiyo ambayo ilikua kwenye awamu ya kwanza ya utekelezwaji wake, kwa sasa imekamilika na imekua chachu kubwa ya maendeleo na faida kwa Wananchi,huku zaidi ya bilioni 650 zikiwa zimetumika katika utekelezwaji wake kwa manispaa ya Temeke.

Waziri Ummy alitabanaisha kwamba kupitia fedha za benki ya Dunia, katika kuboresha huduma za jamii ,miundombinu ya Dar es Salaam ikiwemo kujenga barabara,vituo vya afya na masoko,maeneo mengi katika jiji yamebadilika na kupendeza.

Aidha amewashukuru Benki ya Dunia kwa ushirikiano huo,mbali na shukrani hizo, amewaomba kwamba katika awamu zijazo,waongeza ushirikiano katika kuboresha maeneo mengine ambayo bado hayajafikiwa na mradi huo.

Katika ziara hiyo Ummy amewangozana na viongozi mbalimbali wa benki ya Dunia akiwemo Mari Pangestu ambaye ni mkurugenzi wa sera, maendeleo na ushirikiano wa benki hiyo. Kwa pamoja walitembelea soko la Makangarawe na kituo cha afya Buza.

“Sekta ya afya imeimarika, vituo vipo vizuri, visafi, lakini tangu kituo hicho kimeanza kutoa huduma, hawajapata kifo kinachotokana na ujauzito au uzazi, kwa hilo amewapongeza sana,”amesema Waziri Ummy.

MAKAMU WA RAIS DKT.MPANGO AWASILI SINGAPORE

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza na Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Singapore Mhe.Teo Sieng Seng mara alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Changi Nchini Singapore. Makamu wa Rais yupo Nchini Singapore kuhudhuria Mkutano wa Jukwaa la Majadiliano ya Kiuchumi (Bloomberg New Economy Forum 2021 ). Novemba 15,2021.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza na Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Singapore Mhe.Teo Sieng Seng mara alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Changi Nchini Singapore. Pembeni ni Balozi wa Tanzania nchini India Baraka Luvanda pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Mbarouk. Novemba 15,2021.

BALOZI MULAMULA AMPOKEA MJUMBE MAALUM WA WAZIRI MKUU WA UINGEREZA

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula akimueleza jambo Mjumbe Maalum wa Waziri Mkuu wa Uingereza anayeshugulikia masuala ya biashara Tanzania Bw. Lord Walney walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Mjumbe Maalum wa Waziri Mkuu wa Uingereza anayeshugulikia masuala ya biashara Tanzania Bw. Lord Walney akimsikilza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula akimueleza jambo walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Ujumbe wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (kulia) katika kikao na Mjumbe Maalum wa Waziri Mkuu wa Uingereza anayeshugulikia masuala ya biashara Tanzania Bw. Lord Walney katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwa na Mjumbe Maalum wa Waziri Mkuu wa Uingereza anayeshugulikia masuala ya biashara Tanzania Bw. Lord Walney, katika picha ya pamoja na Balozi wa Uingereza hapa nchini, Mhe. David Concar (mwenye suti ya bluu), kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Amerika na Ulaya katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Swahiba Mndeme
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akimsikiliza Balozi wa Korea ya Kusini aliyemaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini Mhe. Tae-ick Cho wakati alipokwenda kumuaga Mhe. Waziri katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akimueleza jambo Balozi wa Korea ya Kusini aliyemaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini Mhe. Tae-ick Cho katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akimkabidhi zawadi ya picha ya jahazi Balozi wa Korea ya Kusini aliyemaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini Mhe. Tae-ick Cho katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwa na Balozi wa Korea ya Kusini aliyemaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini Mhe. Tae-ick Cho katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Caesar Waitara
Viewing all 45982 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>