Quantcast
Channel: VIJIMAMBO
Viewing all 45982 articles
Browse latest View live

MHE. RAIS SAMIA AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA MKURUGENZI MTENDAJI WA MAENDELEO SERA NA UBIA BENKI YA DUNIA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Sera na Ubia katika Benki ya Dunia (WB) Prof. Mari Pangestu, wakati Mkurugenzi Pangestu alipofika Ikulu, Jijini Dar es Salaam leo tarehe 15 Novemba, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Sera na Ubia katika Benki ya Dunia (WB) Prof. Mari Pangestu, wakati Mkurugenzi Pangestu alipofika Ikulu, Jijini Dar es Salaam leo tarehe 15 Novemba, 2021. PICHA NA IKULU.

KIKWETE AND CO-CHAIR MICHELLE JEAN SUBMIT ICPD25 FIRST REPORT TO THE UNFPA

$
0
0
Former President of Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete and the former Governor General of Canada, and former Secretary General of the International Organization of the Francophonie, H.E. Michaëlle Jean (right) hand over the ICPD25 report to the UNFPA Executive Director, Dr. Natalia Kanem, during the second anniversary of the conference held on Monday in New York.

By a Correspondent

The first report of the High-Level Commission on the Nairobi Summit of the International Conference on Population and Development (ICPD25) Follow-up has been submitted to the UNFPA Executive Director, Dr. Natalia Kanem, during the second anniversary of the conference held on Monday in New York.

The report was presented by co-chairs of the Commission, former President of Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete and the former Governor General of Canada, and former Secretary General of the International Organization of the Francophonie, H.E. Michaëlle Jean.

The report consists of twelve core, overarching commitments, that encapsulate the over 1,300 voluntary commitments made by Governments and other stakeholders at the landmark Nairobi Summit on ICPD25 that took place in November 2019.

It finds progress on some of the Nairobi commitments, but overall notes a harrowing setback in sexual and reproductive health and rights around the world, and calls for ambitious, deliberate and comprehensive action to achieve sexual and reproductive justice for all, in particular women and girls.

It highlights sexual and reproductive rights as a basic prerequisite for achieving the commitments, while also pointing to the fragility of rights, which remain far out of reach for many people, and argues for a comprehensive agenda for sexual and reproductive justice.

The report notes that the global COVID-19 pandemic has laid bare the glaring inequities of people who face different, intersecting forms of discrimination based on their gender, race, age, disability, poverty, and status as a migrant or refugee.

The first report has found out that while there has been progress on some commitments, this progress has been insufficient, and that to urgently change course, the Commission has called for sexual and reproductive justice.

“It’s an agenda that goes beyond promising sexual and reproductive health and rights. It delivers these in people’s lives”, the report outlines.

The hybrid format event, that included both on-site and online speakers and panelists, consisted of eminent leaders from diverse sectors, from around the world and was formed to track progress on the commitments in the Nairobi Statement.

The report notes that the global COVID-19 pandemic has laid bare the glaring inequities of people who face different, intersecting forms of discrimination based on their gender, race, age, disability, poverty, and status as a migrant or refugee.

It also considers constraints on quality, accessible sexual and reproductive health care due to the pandemic that have undermined or delayed progress on the 12 commitments. At the same time, the report highlights innovations born out of necessity that have kept services going and even offered new models that can be more widely replicated.

The report also takes up the financing of the ICPD agenda and the financial commitments, both domestic and international, reflected in the Nairobi Statement, calling attention concerning developments to defund sexual and reproductive health and rights.

In the last chapter of the report the Commission looks into forces propelling and pushing back against advances on the Nairobi commitments, and the levels of accountability that will keep progress on track towards sexual and reproductive justice.

WAZIRI MAKAMBA AKUTANA NA BALOZI WA UGANDA

$
0
0
Waziri wa Nishati, January Makamba ( kulia) akizungumza na Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Balozi Richard Kabonero wakati wa mazungumzo yaliyofanyika katika ofisi ndogo za Wizara ya Nishati zilizopo jijini Dar es Saalam
Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Balozi Richard Kabonero(katikati) katibu wa Ubalozi Uganda nchini Tanzania, Comfort Amviko, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini Francis Nanai wakimsikiliza Waziri wa Nishati(hayupo pichani) wakati wa kikao baina ya Waziri wa Nishati na balozi wa Uganda kilichofanyika katika ofisi ndogo za Wizara Nishati jijini Dar es Saalam
Waziri wa Nishati, January Makamba(kulia) akiwa katika picha ya Pamoja na Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Balozi Richard Kabonero mara baada ya kumaliza kikao kilichofanyika katika ofisi ndogo za Wizara Nishati jijini Dar es Saalam
Kamishna wa Petroli na Gesi, Michael Mjinja ( katikati) katibu wa Waziri Danford Mpelumbe wakimsikiliza Waziri wa Nishati, January Makamba(hayupo pichani) kwenye kikao baina ya Waziri wa Nishati na Balozi wa Uganda nchini Tanzania kilichofanyika katika ofisi ndogo za Wizara Nishati jijini Dar es Saalam,

Hafsa Omar-Dar Es Saalam

Waziri wa Nishati, January Makamba amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Balozi Richard Kabonero.

Mazungumzo hayo, yamefanyika Novemba 15, 2021 katika ofisi ndogo za Wizara ya Nishati zilizopo jijini Dar es Saalam.

Katika kikao hicho ambacho walijadili maandalizi ya ziara ya Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ambae anatarajiwa kuanza ziara nchini Tanzania hivi karibuni.

Aidha, Makamba alisema kuwa Uhusiano mzuri uliopo baina hizo nchi hizi mbili umepelekea kurahisisha ujenzi wa Bomba la kusafirisha mafuta ghafi la Afrika Mashariki ( EACOP) na Marais wa nchi hizo mbili watahakikisha kuwa mradi huo unakamilika.

Pia, alisema mradi wa EACOP ni muhimu sana katika nchi hizo mbili na mpaka sasa upo kwenye hatua nzuri.

“Tunafurahi hatua kubwa iliyofikiwa katika mradi na tunajua umuhimu wa mradi huu kwa nchi zetu zote mbili,” alisisitiza Waziri Makamba.

Kwa upande wake, Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Balozi Richard Kabonero ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano waliotoa kwa kuhakikisha mradi wa Bomba la mafuta unafanikiwa.

MAKAMU WA RAIS AFANYA MAZUNGUMZO NA NAIBU WAZIRI MKUU WA SINGAPORE

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza na Naibu Waziri Mkuu wa Singapore Mhe. Heng Swee Keat, mazungumzo yaliofanyika katika Ukumbi wa Treasury 100 eneo la Shenton Way Nchini Singapore. Makamu wa Rais yupo nchini Singapore kuhudhuria Mkutano wa Jukwaa la Majadiliano ya Kiuchumi (Bloomberg New Economy Forum 2021 ).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akimkabidhi zawadi ya picha yenye mchoro wa Mlima Kilimanjaro Naibu Waziri Mkuu wa Singapore Mhe. Heng Swee Keat mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao yaliofanyika eneo la Shenton Way Nchini Singapore.
Naibu Waziri Mkuu wa Singapore Mhe. Heng Swee Keat akimkabidhi zawadi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao yaliofanyika Shenton Way nchini Singapore.
Naibu Waziri Mkuu wa Singapore Mhe. Heng Swee Keat akimuonesha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango Mandhari pamoja na namna nchi ya Singapore ilivyopangiliwa katika ujenzi wa Majengo na Miundombinu katika eneo la Shenton Way. Novemba 16, 2021.

SAFU YA MILIMA YA LIVINGSTONE YATEKETEZWA NA MOTO NA KUPOTEZA UOTO WA ASILI-DKT.GWAMAKA

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Mhandisi Dkt. Samuel Gwamaka pamoja na watumishi wa NEMC Kanda ya Nyanda za Juu Kusini wakiwa katika picha ya Pamoja na Prof. Mark Mwandosya walipofanya ziara Wilaya ya Kyela katika Safu ya Milima ya Livingstone.
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Mhandisi Dkt. Samuel Gwamaka akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ikombe Wilaya ya Kyela Mkoa wa Mbeya kuhusu uchomaji moto katika Milima ya Livingston.

Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na usimamizi wa Mazingira (NEMC) Mhandisi Dkt. Samuel Gwamaka afanya ziara katika safu ya milima ya livingstone Wilaya ya Kyela Kata ya Matema Mkoani Mbeya na kubaini Kuna uchomaji moto katika milima hiyo na kusababisha uchafuzi mkubwa wa Mazingira na uoto wa asili kupotea.

Dkt. Gwamaka akiwa katika Kijiji cha Ikombe eneo la lyulilo amezungumza na wananchi wa Kijiji hiko na kuwaeleza kuwa shughuli za uchomaji moto katika milima hiyo ni uharibifu wa Mazingira na unaathari kubwa kwa viumbe hai wanaoishi katika Hifadhi ya milima hiyo.

Aidha ameendelea kusema kuwa Milima ya Livingstone inagusa Mikoa mitatu ikiwemo Njombe ,Iringa na Mkoa wa Mbeya hivyo inapaswa kuwa na ushirikiano kati ya Mikoa hiyo ili kuweza kupambana na uharibifu wa Mazingira katika milima hiyo. Amesema kuwa Baraza linaendelea kutoa elimu kwa jamii ili wafahamu kuwa madhara ya uchomaji moto katika milima hiyo ni makubwa kwani itaathiri kizazi kilichopo na kijacho, kama tunavyoona hali iliopo sasa joto limeongezeka kwa kiasi kikubwa kutokana na ukataji miti hovyo. Pia itambulike kuwa milima hiyo ndio kichocheo kikubwa cha upatikanaji wa maji katika mito yetu hivyo kunahaja ya kutunza na kuilinda

“Niwaombe wananchi wa Kijiji hiki na vingine kuhakikisha wanashirikiana na Serikali katika kusimamia hifadhi ya milima ya Livingstone ili kukilinda kizazi chetu na Taifa letu kwa ujumla. Kama tulivyo msikia Rais wetu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Hassan Suluhu akisisitiza Kila Wilaya kupanda miti million 1.3 na sio kupanda tu bali ni lazima miti hiyo itunze ili kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi. Hivyo mazingira ni yetu sote tuhakikishe tunashirikiana na mamlaka husika kama Wakala wa Misitu na Mamlaka ya Hifadhi ya wanyama pori ili kuendelea kuhakikisha maeneo ya Misitu na Hifadhi tunaendelea kulinda kwa Mustakabali wa Nchi yetu pamoja na vizazi vinavyokuja” Amesema Dkt. Gwamaka

Kwa upande wake Mtendaji wa Kata ya Matema Bw. Charles Mwamamba amemshukuru Dkt. Gwaka kwa ujio wake kwani imeongeza nguvu kwa jamii na wananchi wa kijiji cha Ikombe na amesema kuwa matumaini yake elimu aliyotoa kwa wana kijiji hao itasaidia kuelewa kuwa wanapochoma moto wanasababisha madhara makubwa sana katika Mazingira. Ameendelea kusema kuwa historia ya Milima ya Livingstone ilikuwa na uoto wa kutosha lakini shughuli za kibinadamu ikiwemo kilimo, ukataji miti kwa ajili ya mkaa pamoja na uwindaji ndio zilizopelekea uharibifu huo kutokea.

Naye Meneja wa Kanda Nyanda za Juu Kusini NEMC Bi.Glory Kombe amesema kuwa milima ya Livingstone ni maeneo muhimu sana ambayo yanahitaji kuhifadhiwa hivyo sisi kama NEMC tutashirikiana na Halmashauri ya Njombe, Rudewa, Makete Rungwe na Kyela kuhakikisha tatizo hili la moto kutotokea tena kwa miaka ijayo na tutahakikisha milima hii inaifadhiwa ipasavyo. Pia tutahakikisha Sheria ya Mazingira inatekelezwa na kuwachukulia hatua wale wote watakaobainika wanafanya uharibifu wa Mlima huu.

UHUSIANO WA KIMATAIFA NI KIPAUMBELE CHA RAIS SAMIA – MAJALIWA

$
0
0
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza katika kongamano la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Uingereza kwenye ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano ya Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Uingereza nchini, David Concar, katika kongamano la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Uingereza, lililofanyika kwenye ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano ya Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa katika kongamano la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Uingereza lililofanyika kwenye ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano ya Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam,
Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo akizungumza katika kongamano la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Uingereza kwenye ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano ya Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam
Waziri wa Uwekezaji Geofrey Mwambe akizungumza katika kongamano la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Uingereza kwenye ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano ya Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam,
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Liberata Mulamula akizungumza katika kongamano la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Uingereza kwenye ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano ya Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam, Novemba 16, 2021 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

*Lengo ni kukuza uchumi na uwekezaji nchini

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuboresha uhusiano wa kimataifa ili kuchochea uwekezaji na kukuza uchumi wa nchi.

“Mheshimiwa Rais ameniagiza niwaambie kuwa Serikali anayoiongoza ipo tayari kuwapokea, kuwasikiliza na kushirikiana nanyi katika kuimarisha shughuli za uwekezaji na biashara nchini.”

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumanne Novemba 16, 2021) wakati akifungua kongamano la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Uingereza katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

Waziri Mkuu amesema katika kipindi kifupi Mheshimiwa Rais Samia ameboresha mahusiano na nchi mbalimbali ikiwemo Uingereza ikiwa ni sehemu ya mkakati wake wa kukuza uchumi.

Amesema Rais Samia ameongeza usimamizi wa sera za soko huria, sera za kiuchumi na kifedha zenye mwelekeo wa kuimarisha mazingira ya biashara na uwekezaji.

Amesema kwa kipindi cha Machi hadi Agosti 2021, Tanzania imeongoza kwa kuvutia kiwango kikubwa zaidi cha uwekezaji kutoka nje kwa ukanda wa Afrika Mashariki ambapo kiwango cha uwekezaji kutoka nje kilifikia Dola za Marekani bilioni 2.9.

Mheshimiwa Majaliwa amesema licha ya janga la UVIKO19, Tanzania katika mwaka 2020 ilipokea uwekezaji kutoka nje wa Dola za Marekani bilioni moja. “Hili limefanikiwa kutokana na juhudi za makusudi zinazochukuliwa na Serikali katika kuimarisha mazingira ya uwekezaji.”

Akizungumzia kuhusu mahusiano ya kibiashara kati ya Tanzania na Uingereza, Waziri Mkuu amesema Uingereza imeendelea kuwa mshirika wa asili, wa kihistoria na wa muda mrefu wa kibiashara wa Tanzania.

Waziri Mkuu ametoa wito kwa mamlaka husika za pande mbili kushughulikia vikwazo vya kibiashara visivyokuwa vya kikodi ili kurahisisha shughuli za kibiashara na huduma kwenye jamii zetu bila kuathiri misingi ya ushindani.

“Uchumi wa Tanzania umeendelea kukua kwa wastani wa asilimia 6.5 kutoka mwaka 2016 hadi 2020 na hivyo, kuifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zenye uchumi unaokua kwa kasi barani Afrika.”

Ameongeza kuwa hivi karibuni Serikali imeendelea kushuhudia uwekezaji mkubwa kutoka kwa makampuni ya Uingereza ikiwemo miradi 956 kutoka Uingereza yenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 5.5 imesajiliwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania pamoja na mradi wa upanuzi wa Kiwanda cha Sukari cha Kilombero (Dola za Marekani milioni 238) na kupatikana kwa leseni ya uchimbaji wa madini ya nickel ya Kabanga

Waziri Mkuu amemshukuru, , Mwakilishi Maalumu wa Waziri Mkuu wa Uingereza wa masuala ya kibiashara Lord Walney kwa kuitangaza Tanzania kuwa sehemu sahihi kwa ajili ya uwekezaji na biashara hususan kwa makampuni kutoka Uingereza.

Naye, Mwakilishi Maalumu wa Waziri Mkuu wa Uingereza, Bw. Walney, amesema Uingereza itaendelea kuwa mdau muhimu wa maendeleo na uwekezaji nchini Tanzania na wataendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali katika kukuza uchumi na uwekezaji.

Kwa Upande wake, Waziri wa Viwanda na Biashara, Mheshimiwa Kitila Mkumbo, amesema Mkutano huo utakuwa na manufaa makubwa kwa wafanyabiashara wa Tanzania kwani unalenga kuongeza kiwango cha usafirishaji wa bidhaa kutoka nchini Tanzania kwenda Uingereza ili kuweka usawa katika bidhaa zinazoingia na kuuzwa miongoni mwa Nchi hizo mbili.

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Geoffrey Mwambe, amesema lengo la kongamano hilo ni kupokea mrejesho wa wafanyabiashara na wawekezaji kutoka nchini Uingereza kuhusu mazingira ya ufanyaji wa biashara pamoja na kuboresha maeneo ambayo yana changamoto katika uwekezaji na kwa pamoja kuwa na maadhimio ambayo yatatengeneza fursa za kukuza uchumi na usawa wa kibiashara kwa nchi zote.

Waziri Mwambe amesema, Wizara ya Uwekezaji itaendelea kuendesha makongamano ya uwekezaji na wadau wa Sekta Binafsi pamoja na nchi washirika katika kuhakikisha wanatengeneza fursa na mazingira bora ya uwekezaji kwa kusikiliza mawazo na changamoto zinazowakabili wawekezaji.

Naibu Waziri Wa Nchi Ofisi ya Rais Zanzibar, anayeshugulikia Kazi, Uchumi na Uwekezaji Bw. Nurdin Solaga, ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji kutoka nchini Uingereza kuwekeza katika sera ya Uchumi wa Bluu ambapo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetengeneza Mazingira bora ya Kiuwekezaji kwa wawekezaji hususan katika Sera ya Uchumi wa Bluu.

Waziri Mkuu alihitimisha kwa kuwashukuru Washiriki wote wa kongamano hilo na kuwahamasisha kuendelea kuwekeza nchini Tanzania kwani Serikali imeendelea kuimarisha mazingira ya uwekezaji na biashara kwa kutoa vivutio vya kisera na visivyo vya kisera sambamba na cheti cha uwekezaji mahiri. Hatua nyingine ni kuhakikisha huduma zote muhimu ikiwemo vibali, leseni na baadhi ya vivutio vinapatikana kwenye kituo cha huduma cha pamoja.

RAIS MHE.DK. MWINYI AREJEA NCHINI TANZANIA LEO BAADA YA KUMALIZIKA KWA UFUNGUZI WA MKUTANO MAONESHO YA BIASHARA KWA NCHI ZA AFRIKA ULIOFANYIKA JIJINI DARBAN.

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na kuagana Balozi wa Tanzania Nchini Afrika Kusini Meja Jenerali (Mst) Gaudance Milanzi na (kushoto kwake) Kiongozi wa Juu wa Serikali ya Afrika Kusini Mhe.Mashego Dlamini na ( kulia kwake) Mkurugenzi wa Idara ya Diplomasia ya Uchumi Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Edwin Lutageruka, wakati akiondoa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa King Shaka Jijini Darban Afrika Kusini leo 16-11-2021. akirejea Nchini Tanzani.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakisalimiana na kuagana na Balozi wa Tanzania Nchini Afrika Kusini Mhe. Meja Jenerali (Mst) Gaudance Milanzi na Kiongozi wa Juu wa Serikali ya Afrika Kusini Mhe. Mashego Dlamini, alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa King Shaka Darban Jijini Afrika Kusini, baada ya kumalizika kwa mkutano wa Ufunguzi wa Maonesho ya Biashara kwa Nchi za Afrika uliofanyika katika ukumbi wa ICC Darban.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na mwenyeji wake Kiongozi wa juu wa Serikali ya Afrika Kusini Mhe. Mashego Dlamini, akikagua gwaride maalum aliloandaliwa wakati akiondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa King Shaka Jijini Darban Afrika Kusini leo 16-11-2021, akirejea Nchini Tanzania baada ya kumalizika kwa mkutano wa Ufunguzi wa Maonesho ya Biashara kwa Nchi za Afrika, uliofanyika katika ukumbi wa ICC Darban.(Picha na Ikulu)

KAMPUNI YA GOPA CONTRACTORS YAOMBA RADHI WAKULIMA HANANG KWA KUCHELEWA KUANZA UJENZI SKIMU YA ENDAGAW.

$
0
0

 


Meneja wa Kampuni ya GOPA CONTRACTORS Godfrey John, amewaomba radhi Wakulima katika Skimu ya Endagaw kwa kuchelewa kuanza ujenzi wa Miundombinu ya Mifereji na Ukarabati wa Bwawa kwa zaidi ya miezi miwili.

Akizungumza katika kikao kilichowashirikisha, Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Bi Janeth Mayanja, watendaji wa Tume na Wakulima wa Skimu hiyo, Meneja wa kampuni ya GOPA CONTRACTORS Bw, Godfrey John amekiri kampuni yake kushindwa kuanza shughuli za ujenzi katika Skimu hiyo kwa mujibu wa mkataba wa makubaliano na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji na kwamba zoezi la ujenzi litaanza hivi karibuni kwa ubora na viwango vilivyoainishwa kwenye mkataba baada ya kutatua changamoto zilizoikabili kampuni yake.

Mhandisi wa Tume ya Taifa Umwagiliaji Bw, Juma Hamsini, ametoa onyo kali kwa mkandarasi huyo na kuongeza kuwa endapo kampuni yake itarudia kutenda kosa kama hilo, Tume ya taifa ya Umwagiliaji itaiweka kampuni hiyo katika orodha ya makampuni yanayotiliwa shaka kiutendaji hali itakayosababisha kampuni hiyo kukosa fursa ya ujenzi wa Miradi ya Miundombinu ya Umwagiliaji inayoratibiwa na Tume.

Kwaupande wake Mkuu wa Wilaya ya Hanang Bi, Janeth Mayanja, amemtaka Mkandarasi huyo kujenga Miundombinu kwa viwango na ubora kwa mujibu wa mkataba na kwamba atafuatilia ujenzi wa Mradi huo kwa karibu hadi utakapo kamilika.

Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ilisaini makubaliano na kampuni ya Gopa Contractors ya jijini Dar es Saalam, kujenga Mfereji mpya wenye urefu wa Mita Elfu mbili na Mianne (2,400) sanjari na kuongeza urefu mfereji wa zamani kwa kujenga Mita Miasaba na Sabini (770) pamoja na kuondoa Tope ndani ya bwawa linalotumika kumwagilia Skimu ya Endagaw.

Mkataba wa ujenzi wa miundombinu hiyo baina ya Tume na Mkandarasi Gopa Contractors ni wa zaidi ya Shilingi Milioni Miatisa Themanini.( Milioni 980) na ulisainiwa tarehe 31.08. 2021.
Bakari Khamis – Diwani wa Endagaw akiwaonyesha Wahandisi wa Tume changamoto zilizopo katika Bwawa la Endagaw linalotumika kumwagilia Skimu ya Endagaw.

Mkuu wa Wilaya ya Hanang Bi, Janeth Mayanja (Katikati waliosimama),Mkurugenzi wa Kampuni ya Gopa Contractors (wa tano kulia(aliyevaa miwani) pamoja na Watendaji wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji katika eneo la kuhifadhia mitambo ya Mkandarasi mara baada ya kulikagua na kujiridhisha



MHE. RAIS SAMIA AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA MJUMBE MAALUM WA MASUALA YA BIASHARA WA WAZIRI MKUU WA UINGEREZA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mjumbe Maalum wa Waziri Mkuu wa Uingereza Mhe. Boris Johnson, anyeshugulikia masuala ya Biashara kati ya Uingereza na Tanzani Bw. Lord Walney mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 17 Novemba 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mwenyekiti wa Mabenki ya Umoja wa Afrika (UBA) Dkt. Tony Elumelu, mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 17 Novemba 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Ujumbe kutoka Kampuni ya DP World uliongozwa na Mwenyekiti wa Kampuni hiyo kutoka Falme za Kiarabu (UAE) Bw. Sultan Ahmed Bin Sulayem, wakati Ujumbe huo ulipofika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 17 Novemba 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza kwa njia ya mtandao na Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya Equinor Anders Opedal, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

RAIS DK.HUSSEIN ALI MWINYI AKUTANA NA MADAKTARI KUTOKA ‘HACKLAND UNIVERSITY HOSPITAL’ YA NCHINI NORWAY,

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akizungumza na Ujumbe wa Madaktari kutoka ‘Hackland University Hospital’ ya nchini Norway, ambao wamesaidia ujenzi wa Hospital ya Wagonjwa wa Akili Kidongochekundu Wilaya ya Mjini,walipofika Ikulu Jijini Zanzibar.[Picha na Ikulu] 17/11/2021.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) akizungumza na Ujumbe wa Madaktari kutoka ‘Hackland University Hospital’ ya Nchini Norway (kushoto), ambao wamesaidia ujenzi wa Hospital ya Wagonjwa wa Akili Kidongochekundu Wilaya ya Mjini,walipofika Ikulu Jijini Zanzibar.[Picha na Ikulu] 17/11/2021.

WAZIRI UMMY: TEGEMEENI MAKUBWA UJENZI WA BARABARA ZA VIJIJINI

$
0
0
Na. Angela Msimbira Mwanga

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Ummy Mwalimu amesema dhamira ya dhati ya Serikali ya awamu ya sita ni kuhakikisha inajenga miundombinu ya barabara maeneo ya vijijini kwa kuongeza bajeti ya ujenzi wa barabara maeneo ya vijijini kupitia wakala wa barabara Mijini na Vijijini (TARURA)

Akikagua ujenzi wa barabara ya Kisangara – Shighatini na kifula – Butu katika Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Leo Waziri Ummy amesema bajeti ya Tarura katika Halmashauri hiyo imeongezeka kutoka shilingi milioni 695 kwa mwaka wa fedha 2020 hadi kufikia shilingi bilioni 3.5 kwa mwaka wa fedha 2021

Amesema kuwa wananchi wategemee mabadiliko makubwa katika suala zima la ujenzi wa miundombinu kwenye maeneo ya vijijini lengo likiwa ni kuwapunguzia adha wananchi na kufungua uchumi wa wakazi wa Mwaga kwa kuwa barabara nyingi zitafunguliwa,

Amemuagiza Mkandarasi anayejenga barabara hiyo Elerai Construction Co Limited kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa barabara hizo kwa wakati kwa kuhakikisha wanafuata viwango vilivyowekwa na Serikali

Aidha, ujenzi wa barabara ya Kisangara – Shighatini (km3. 57) na Kifula – Butu (km 3.57) itajengwa kwa kiwango cha lami na itagharimu zaidi ya shilingi milioni 441.

RAIS SAMIA AMEDHAMIRIA KUIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA MAMA NA MTOTO – MAJALIWA

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akifafanuliwa jambo na Mganga Mkuu Msaidizi, Taasisi ya NEST 360 – Ifakara, Dot. Robert Tillya, wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Kisayansi wa Huduma za Afya ya Uzazi, Mtoto, Vijana na Lishe ,uliofanyika katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, jijini Dar es salaam
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akioneshwa moja ya zana ya uzazi wa mpango na Muuguzi Mkunga wa Kituo cha Tabata NBC, Flora Amosi, wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Kisayansi wa Huduma za Afya ya Uzazi, Mtoto, Vijana na Lishe uliofanyika katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, jijini Dar es salaam, Novemba 17, 2021. Kutoka kulia ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Kikwete, Mke wa Rais Mstaafu Mama Salma Kikwete, Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akifafanuliwa jambo na Meneja wa Ukuaji wa Vijana Balehe, Angela Damas kutoka Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Kisayansi wa Huduma za Afya ya Uzazi, Mtoto, Vijana na Lishe uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, jijini Dar es salaam
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akifafanuliwa jambo na Meneja Miradi na Utoaji wa Huduma kutoka Taasisi ya Benjamin Mkapa, Dkt. Adeline Saguti, wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Kisayansi wa Huduma za Afya ya Uzazi, Mtoto, Vijana na Lishe uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, jijini Dar es salaam
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiteta jambo na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Kikwete wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Kisayansi wa Huduma za Afya ya Uzazi, Mtoto, Vijana na Lishe uliofanyika katika Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, jijini Dar es salaam
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akihutubia kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Kisayansi wa Huduma za Afya ya Uzazi, Mtoto, Vijana na Lishe uliofanyika katika Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, jijini Dar es salaam, Novemba 17, 2021 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuimarisha huduma za afya ya mama na mtoto na kuzitoa bila malipo ili kupunguza vifo vya akinamama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano.

“Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais wetu Samia Suluhu Hassan inaonekana wazi katika kuimarisha huduma ya mama na mtoto. Tunajenga Vituo vya afya ambavyo vimewekwa miundombinu muhimu katika kutoa huduma ikiwemo jengo la mama na mtoto na chumba cha upasuaji.”

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano. Novemba 17, 2021) wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Kisayansi wa Huduma za Afya ya Uzazi, Mtoto, Vijana na Lishe unaofanyika mkoani Dar es Salaam. Mheshimiwa Majaliwa amefungua mkutano huo kwa niaba ya Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.

“Mtakumbuka kuwa mwezi Novemba mwaka 2018 Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan wakati akiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, alizindua Kampeni ya “Jiongeze Tuwavushe Salama” ambayo ilikuwa na nia ya kuongeza uwajibikaji katika kuhakikisha mama mjamzito na mtoto mchanga wanakuwa salama.”



Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa ametumia fursa hiyo kuielekeza Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee wa Watoto ifanye mapitio ya mwongozo wa uendeshaji wa Vituo vya Afya kuhusu upatikanaji wa watumishi ili Madaktari Bingwa wapatikane hadi ngazi ya Wilaya.

“Wizara ya Elimu ihakikishe mitaala na shule zetu zinawekeza katika kufundisha somo la uzazi kulingana na umri wa wanafunzi. Pia Mamlaka za Serikali za Mitaa zisimamie mpango wa lishe kwa wanafunzi wa shule za kutwa. Lishe ni muhimu sana katika suala zima la kuimarisha afya ya uzazi.”

Pia, Mheshimiwa Majaliwa ameielekeza Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na wadau wote kuimarisha upatikanaji wa huduma kwa ajili ya watoto wachanga ikiwa ni pamoja na uwepo wa vyumba maalum kwa ajili ya watoto wachanga wagonjwa, vifaa tiba na watoa huduma wenye ujuzi.

“Wadau wote katika ngazi zote, kuwekeza ipasavyo kwenye mifumo ya huduma za afya ya uzazi na mtoto ili tufikie malengo endelevu ifikapo 2030, ya kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi hadi 70 kwa kila vizazi hai 100,000 na vifo vya watoto wachanga kufikia 12 kwa kila vizazi hai 1,000.”

Kwa upande wake, Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto amesema uzazi wa mpango ni afua muhimu katika upunguzaji wa vifo vitokanavyo na uzazi na unasaidia katika kuboresha afya ya mama na kumfanya ashiriki vema katika ujenzi wa Taifa na kuongeza kipato kwa familia.



“Uzazi wa mpango unasaidia kumpa mama nafasi ya kumnyonyesha motto wake angalau kwa miaka miwili kama inavyoshauriwa kiafya. Wizara kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo imeendelea kuwekeza na kutoa huduma kwenye afua hii na kwa sasa matumizi ya uzazi wa mpango kwa takwimu za ndani unafikia asilimia 39 tukiwa na lengo la kitaifa la kufika asilimia 47 ifikapo mwaka 2023.”



Amesema Serikali imewekeza kwa kiasi kikubwa kwenye upatikanaji wa huduma za dharura za afya ya uzazi na mtoto mchanga hapa nchini kwa kujenga na kuweka vifaa tiba vya kuwezesha kutoa huduma za dharura za uzazi na mtoto, kutoa dawa ya ganzi/usingizi na kufanya upasuaji wa kumtoa mtoto tumboni.



Dkt. Gwajima amesema Tanzania ina jumla ya vituo vya afya 911 na kati yake vituo 491 sawa na asilimia 51 vinatoa huduma za dharura za uzazi na mtoto timilifu ikiwa ni pamoja na upasuaji wa kumtoa mtoto tumboni.



“Vituo hivi vipya vimeanza kufanya kazi baada ya kuhakikisha kuwa vinapata watumishi stahiki ikiwa ni pamoja na watumishi waliopata mafunzo ya kutoa dawa za ganzi na usingizi katika shule za MUHAS, KCMC na Bugando.”



Naye, Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui amesema Serikali inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Hussein Mwinyi imeweka mikakati thabiti katika kuhakikisha inapunguza vifo vya mama na mtoto na hiyo imechangiwa na uboreshaji mkubwa wa huduma za afya kuanzia ngazi ya chini.

WAZIRI MKUMBO AELEZEA MAFANIKIO YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA TANGU UHURU

$
0
0
WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo,akizungumza na waandishi wa habari leo November 17,2021 jijini Dodoma kuhusu mafanikio ya Sekta ya Viwanda na Biashara katika kipindi cha miaka 60, ya uhuru wa Tanganyika.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo,(hayupo pichani) wakati akiwasilisha mafanikio ya Sekta ya Viwanda na Biashara katika kipindi cha miaka 60, ya uhuru wa Tanganyika leo November 17,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo ,akijibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo November 17,2021 jijini Dodoma wakati akizungumzia mafanikio ya Viwanda na Biashara katika kipindi cha miaka 60, ya uhuru wa Tanganyika.

Na.Alex Sonna,Dodoma

WIZARA ya Viwanda na Biashara imesema katika kipindi cha miaka 60 ya uhuru wa Tanzania Bara imepata mafanikio ndani ya miaka 60 msukumo mkubwa wa ujenzi wa uchumi wa viwanda, idadi ya ajira imeongezeka zaidi na kufikia ajira 482,601 mwaka 2021.

Hayo yameelezwa leo Jumatano ,Novemba 17,2021 jijini Dodoma na na Waziri wa Viwanda na Biashara,Prof. Kitila Mkumbo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu mafanikio ya Sekta ya Viwanda na Biashara katika kipindi cha miaka 60, ya uhuru wa Tanganyika.

AJIRA NA VIWANDA
Waziri Kitila amesema ajira katika Sekta ya Viwanda imeendelea kuongezeka ambapo mwaka 1961 Sekta ya Viwanda ilichangia asilimia 9 ya ajira zote nchini. Hadi kufikia mwaka 2015, ajira katika Sekta ya Viwanda zilikuwa zimeongezeka na kufikia ajira 254,786.

Aidha, kutokana na msukumo mkubwa wa ujenzi wa uchumi wa viwanda, idadi ya ajira imeongezeka zaidi na kufikia ajira 482,601 mwaka 2021.

“Viwanda vyetu vingi vinamilikiwa na watanzania lakini katika sekta biashara sio muhimu nani anamiliki muhimu kwetu ni uwekezaji upo hapa Tanzania bila kujali anatoka nchi gani,muhimu sisi awe ameajiri watanzania,”amesema

Waziri Kitila amesema watanzania wengi wamepata ajira za moja kwa moja rasmi na zisizo rasmi kupitia sekta ya viwanda.

“Tumefanya hesabu katika viwanda vyetu walioajiriwa ni asilimia 99,ukija kwenye viwanda vikubwa pia wengi ni watanzania na muhimu sio nani anamiliki,kikubwa analipa kodi hela inazunguka ndani ya Tanzania.

“Kwa ujumla watu ambao wameajiriwa katika viwanda ni 400,000 lakini uzuri wa viwanda vinazalisha ajira za moja kwa moja zisizorasmi,”amesema

VIWANDA NA PATO LA TAIFA

Waziri huyo amesema mchango wa Sekta ya Viwanda kwenye Pato la Taifa umekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka ambapo wakati wa Uhuru mwaka 1961, Sekta ya Viwanda ilikuwa ikichangia asilimia 3.5 ya Pato la Taifa (GDP). Amesema hadi kufikia mwaka 2015 mchango wa sekta hiyo ulikuwa asilimia 7.9.

Amesema kutokana na jitihada za Serikali za kuhamasisha ujenzi wa viwanda mchango wa sekta ya viwanda kwenye Pato la Taifa uliongezeka na kufikia asilimia 8.5 ya Pato la Taifa mwaka 2019. Mwaka 2020 mchango wa sekta ulishuka kidogo hadi asilimia 8.4.

SERIKALI HAIFANYI BIASHARA

Aidha,Waziri Kitila amesema Serikali haifanyi biashara na wala haiwezi kuibana sekta binafsi katika utendaji kazi wake bali kumekuwa na tofauti ya tafsiri.

TANZANIA NA BURUNDI KUONGEZA USHIRIKIANO KATIKA KUKUZA SEKTA YA POSTA.

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabiri Bakari akizungumza na ujumbe wa Maafisa Waandamizi kutoka Shirika la Posta Burundi wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Posta Burundi Bi. Lea Ngabire walipotembelea Mamlaka hiyo kwa ziara ya mafunzo. Picha na: TCRA
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Posta Burundi Bi. Lea Ngabire akisaini Kitabu cha Wageni wakati alipotembelea Makumbusho ya Mawasiliano iliyopo Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). Katika ziara hiyo ya mafunzo Ingabire aliambatana na Maafisa Waandamizi wa Posta Burundi. Picha na: TCRA

Na: Mwandishi wetu

Shirika la Posta la nchini Burundi limeweka bayana dhamira yake ya kushirikiana na Tanzania katika kukuza sekta ya Posta nchini humo ikiwa ni pamoja na kuongeza ufanisi zaidi katika usimamizi wa masuala ya Posta.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa masuala ya posta wa Burundi Bi. Lea Ngabire wakati alipozuru Ofisi za Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania akiambatana na ujumbe wa Maafisa waandamizi wa Posta Burundi katika ziara ya mafunzo.

“Tumefika hapa TCRA na kujionea shughuli mbalimbali za mawasiliano na lengo letu ni kuona namna nchi zetu mbili zinavyoweza kushirikiana katika kukuza na kuendeleza sekta ya posta” alibainisha Ngabire.

Ujumbe wa Maafisa hao umejumuisha Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA wa Posta Burundi Nyayishimiye Olivier na Mkuu wa masuala ya Barua Misirakuba Deo.

Akipokea ujumbe huo mnamo Jumatano Tarehe 17 Novemba 2021 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Dkt. Jabiri Bakari aliwakaribisha na kuwaeleza kuwa TCRA kama mdhibiti wa sekta ya Mawasiliano nchini Tanzania inatambua umuhimu wa ushirikiano wa mawasiliano hasa kikanda na imekuwa mshirika muhimu wa mawasiliano katika ukanda wa Afrika Mashariki.

“Lengo letu ni kuhakikisha sekta ya mawasiliano nchini Tanzania inasimamiwa kwa uthabiti na kwa upande wa posta TCRA imekuwa ikishirikiana na taasisi mbalimbali za kikanda na kimataifa na kama mnavyofahamu pia Makao Makuu ya Posta Afrika yapo hapa nchini” alibainisha na kuongeza Jabiri.

Pembezoni mwa mazungumzo na ujumbe huo pia, Mkurugenzi Mkuu Jabiri aliwaeleza wajumbe hao kwamba Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha sekta ya mawasiliano barani Afrika inaimarika na ndiyo sababu imekuwa ikishirikiana na Shirika la Posta Afrika (PAPU) kuhakikisha ujenzi wa Ofisi ya PAPU makao makuu ambayo ujenzi wake unaendelea jijini Arusha unakamilika kwa wakati ambapo matarajio ni kukamilisha ujenzi wa jingo la kisasa jijini Arusha itakapowadia 2022.

Nae Mkurugenzi wa Masuala ya Kisekta wa TCRA Dkt. Emmanuel Manasseh ambae sekta ya Posta inasimamiwa na kurugenzi anayoingoza alibainisha kwamba hakuna namna uchumi wa kisasa utajengwa bila kuhusisha posta kwani sekta hiyo ni muhimu katika masuala ya usafirishaji na ufikishaji wa taarifa mbalimbali zinazowezesha kujenga uchumi wa kisasa (Uchumi wa kidijitali).

“Tunapoenda kwenye uchumi wa kidijitali posta ni sekta muhimu sana ambayo hatuwezi kukwepa kuitumia kwani itatuwezesha kufikia azma ya kujenga uchumi wa kidijitali.” Alisisitiza Dkt Manasseh.

Mara baada ya kuhitimisha ziara hiyo ujumbe huo ulibainisha kufurahishwa na maarifa waliyopata baada ya kutembelea TCRA ili kujifunza na kuahidi kwamba watatendea kazi yale waliyojifunza katika kukuza sekta ya Posta nchini Burundi.

VICHWA VITATU VYA TRENI YA RELI YA KATI VYAWASILI

$
0
0
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, akifafanua jambo kwa Uongozi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), pamoja na wadau wake katika hafla ya mapokezi ya vichwa vitatu vya treni ya reli ya kati (MGR), katika Bandari ya Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, akizungumza na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Bi. Angelina Ngalula, katika halfa ya mapokezo ya vichwa vitatu vya treni ya reli ya kati (MGR), jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, akifurahi jambo pamoja na wadau wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), mara baada ya kuhutubia katika halfa ya mapokezo ya vichwa vitatu vya treni ya reli ya kati (MGR), jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli la Tanzania (TRC), Bw. Masanja Kadogosa, akitoa taarifa kwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, upokeaji wa vichwa vitatu vya treni ya reli ya kati (MGR) vilivyonunuliwa na Shirika hilo na kampuni ya SMH RAIL kutoka nchini Malaysia mara baada ya kuwasili katika Bandari ya Dar es Salaam
Moja ya kichwa cha treni ya reli ya kati kati ya vitatu kikishushwa katika Bandari ya Dar es Salaam mara baada ya kuwasili jijini hapo na kupokelewa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa (hayupo pichani). Vichwa hivyo vitatu vinavyomilikiwa na Shirika la Reli Tanzania (TRC), vimegharimu kiasi cha shilingi Bilioni 22.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Nchini (TPA), Bw. Erick Hamis akitoa neno mbele ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (wa pili kushoto), katika hafla ya upokeaji wa vichwa vitatu vya treni ya reli ya kati (MGR) vilivyowasili katika Bandari ya Dar es Salaam.


Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (mwenye shati la bluu), akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), mara baada ya kupokea vichwa vitatu vya treni ya reli ya kati (MGR), katika Bandari ya Dar es Salaam.

PICHA NA WUU



Serikali kupitia Shirika la Reli Tanzania (TRC), limepokea vichwa vitatu vya treni ya reli ya kati (MGR), vilivyonunuliwa na Serikali kupitia mradi wa uboreshaji wa reli hiyo kwa gharama ya shilingi Bilioni 22.

Ununuzi wa vichwa hivyo ni moja ya mkakati ya Serikali katika uboreshaji wa miundombinu ya Reli hapa nchini (Tanzania Intermodal and Rail Development – TIRP), unaotekelezwa kwa kutumia fedha za mkopo wa Benki ya Dunia.

Vichwa hivyo vilivyopokelewa katika Bandari ya Dar es Salaam na kushuhudiwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, vina lengo la kuongeza tija ya uzalishaji wa Shirika hilo katika usafirishaji wa mizigo kutoka bandarini ya Dar es Salaam hadi Bandari Kavu ya Isaka.

Waziri Prof. Mbarawa, amelitaka Shirika hilo kufanya biashara na kutumia watalaam wenye sifa na uwezo wa kuviendesha vichwa hivyo ili kuweza kusafirisha tani 7,000 mpaka 10,000 za mizigo kwa mwezi na hivyo kuongeza ufanisi wa ubebaji mizigo mara mbili zaidi ya vichwa vilivyopo sasa.

“Nitashangaa sana vichwa hivi wapewe watu ambao hawana sifa na uwezo wa kuviendesha kibiashara kwani kufanya hivyo mtakuwa mmeikosea sana Serikali”, amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.

Aidha Prof. Mbarawa, amefafanua kuwa kupitia vichwa hivyo gharama za uendeshaji zitapungua lakini pia itapunguza muda wa mizigo kukaa bandarini bila ya kusafirishwa hali inayopelekea msongamano bandarini.

Ameongeza kuwa kuimarika kwa huduma za bandari hapa nchini kumepelekea kuongezeka kwa mizigo inayopita Bandari ya Dar es Salaam hivyo mahitaji ya behewa na vichwa vya treni kwa ajili ya kuhudumia wateja wa nje na ndani ya nchi kwasasa umeongezeka.

Amesema vichwa hivyo vina uwezo wa Horse Power 3,000 kwa kila kimoja kwa ajili ya kuvuta behewa 20 ambazo ni sawa na tani 1,200 kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro tofauti na awali ambapo vilikuwa vikifungwa vichwa viwili.

Prof. Mbarawa amefafanua kuwa usafirishaji wa mizigo kwa njia ya reli utapunguza uharibifu wa barabara zetu hapa nchini kwa kiasi kikubwa.

Awali akitoa taarifa ya vichwa hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la TRC Bw. Masanja Kadogosa, ameeleza kuwa mkataba wa ununuzi wa vichwa vitatu ulisainiwa tarehe 4 Machi 2019 katika shirika hilo na kampuni ya SMH RAIL kutoka nchini Malaysia kwa mkataba wa siku 360.

Bw. Kadogosa amefafanua kuwa kichwa kimoja cha reli hiyo ya kati kitaongezewa mzigo hadi kufikia tani 2,000 ambazo ni sawa na behewa 33 ambapo mzigo huo ukisafirishwa kwa njia ya barabara ni sawa na malori 66 yenye uwezo wa kubeba tani 30 kila moja.

Ameongeza kuwa vichwa hivyo vipya vimefungwa mifumo ya kisasa ambayo itasaidia kuongeza ufanisi na uimarishaji wa usalama wa safari za treni.

“Treni hii imefungwa kifaa cha kutoa taarifa kwa waongoza treni kwa njia ya mtandao ili kuweza kufatilia mwenendo wa safari kuanzia Dar es Salaam hadi mwisho wa safari lakini pia katika taarifa zitazopatikana ni pamoja na mwendokasi wa treni, aina treni, matumizi ya mafuta, mahali treni ilipo na hitilafu ya kichwa cha treni pindi inapopata shida ili kupata ufumbuzi wa haraka”, amefafanua Bw. Kadogosa.

Mradi wa ununuzi wa vichwa vitatu vya treni za reli ya kati kutalifanya Shirika la Reli Tanzania (TRC) kuwa na jumla ya vichwa vya treni 43 vya masafa marefu na vichwa vya sogeza 7 katika uendeshaji wake.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi

WAZIRI MKUU ATEMBELEA WAGONJWA HOSPITALI AGA KHAN

$
0
0
=
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza familia ya aliyekua Waziri wa Fedha na Utawala wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na aliyekua Waziri Mstaafu wa Wizara tofauti kwenye awamu ya kwanza na pili, Mzee Al noor Kassum, ambaye amelazwa katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es salaam
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimjulia hali, Mke wa Waziri Mstaafu wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, Bora Isack (kulia), ambaye amelazwa katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es salaam, Novemba 18, 2021 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

SERIKALI KUENDELEA KUFUNGUA FURSA KWA WANAWAKE – NAIBU WAZIRI KATAMBI

$
0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Patrobas Katambi akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa WAENDELEZE iliyofanyika nyumbani kwa balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Novemba 17, 2021 Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya washiriki na wanufaika wa mradi wa WAENDELEZE wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Patrobas Katambi (hayupo pichani) wakati wa hafla hiyo.
Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Mhe. Wiebe de Boer akieleza jambo wakati wa hafla hiyo iliyofanyika Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Lindam Bi. Zuhura Muro akifafanua kuhusu mradi wa WAENDELEZE wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi huo iliyofanyika nyumbani kwa balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Novemba 17, 2021 Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Patrobas Katambi (kushoto) akizungumza na Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Mhe. Wiebe de Boer alipokabidhiwa zawadi ya begi lenye nembo ya mradi wa WAENDELEZE ikiashiria mchango wake katika kufanikisha mradi huo. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Lindam Bi. Zuhura Muro.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Patrobas Katambi (wa pili kutoka kushoto) akijadiliana na Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Mhe. Wiebe de Boer (kushoto) na wanufaika wa mradi wa WAENDELEZE wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi huo iliyofanyika Novemba 17, 2021 Jijini Dar es Salaam.

PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU

Na: Mwandishi Wetu – DAR ES SALAAM

SERIKALI imeazimia kuendelea kufungua fursa zaidi kwa wanawake nchini katika kufanya biashara, kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji ikiwa ni pamoja na kuwapatia mafunzo ya kukuza biashara na mitaji, kufungua masoko na kuwatambua vitendea kazi muhumu kwa ajili ya kufanyia biashara zao.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Patrobas Katambi wakati akizindua mradi wa WAENDELEZE unaoratibiwa na Serikali kwa kushirikiana na Ubalozi wa Uholanzi nchini Tanzania.

Alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan imeendelea kutoa fursa kwa wanawake kujiendeleza kibiashara ili kuinua uwezo wao na kuwawezesha katika kuchangia maendeleo ya Taifa.

“Mradi huu wa Waendeleze ni moja ya jitihada za Serikali inayoongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa ushirikiano mzuri na wadau wa maendeleo ambao unalenga kumuinua mwanamke anayefanya biashara aweze kufikia hatua za juu zaidi,” alisema Naibu Waziri Katambi

Aliongeza kuwa katika kufanikisha mradi huo wa WAENDELEZE, Ubalozi wa Uholanzi nchini umewezesha mafunzo kwa wafanyabiashara wanawake kwa kushirikiana na Taasisi ya Uongozi ambapo wanawake kutoka kanda ya ziwa, kanda ya nyanda za juu kusini, kanda ya kati, kanda ya magharibi na kanda ya mashariki wamenufaika.

“Tumeshuhudia hapa wafanyabiashara wanawake wanaojishughulisha na shughuli mbalimbali za uzalishaji mali ikiwemo kilimo, ufugaji, usindikaji na kadhalika namna mafunzo hayo yalivyowasaidia kufungua fursa nyingi ikiwa ni pamoja na kukuza mtandao wa biashara zao na masoko,” alisema

Aidha, Naibu Waziri Katambi aliwasihi wanawake walionufaika na mafunzo hayo kutoa elimu na kuwa mfano wa kuigwa katika maeneo wanayofanya biashara ili kuwapa hamasa wengine.

Sambamba na hayo alitumia fursa hiyo kuwahimiza Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu kuchangamikia fursa ya mikopo ya asilimia 10 (4% Vijana, 4% Wanawake na 2% Wenye Ulemavu) kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri ili kuanzisha na kuendeleza shughuli au miradi itakayowaingizia kipato na kutimiza ndoto zao.

Kwa upande wake, Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Mhe. Wiebe de Boer alisema kuwa serikali ya ufalme wa Uholanzi itaendelea kushirikina na Serikali katika kuboresha na kuendeleza wafanyabiasha wanawake nchini kupitia mradi huo wa WAENDELEZE.

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Lindam Bi. Zuhura Muro, alisema kuwa mradi huo umewawezesha wafanyabiashara wanawake kupata hamasa ya kuchangia pato la Taifa na pia kupitia shughuli zao za kiuchumi wameweza kutoa fursa za ajira kwa wengine.

Pamoja hayo, Mkuu wa Kitengo cha Kilimo Biashara kutoka Benki ya NMB, Bw. Issack Masusu alieleza kuwa benki hiyo ya NMB imepunguza riba katika eneo la sekta ya kilimo na kilimo biashara ambapo riba hiyo imeshuka kutoka asilimia 18 hadi 10.

“Benki ya NMB imetenga kiasi cha Tsh. Bilioni 100 kwa ajili ya kuwezesha mikopo kwa wafanyabiashara ambapo kiasi cha laki 2 hadi bilioni 10 zimekuwa zikitolewa kwa mkopaji mmoja, hivyo ni vyema wanufaika wa mradi huu wakakimbilia fursa hiyo ambayo itakuwa chachu katika ukuaji wa biashara zao,” alisema Masusu

UCHIMBAJI SALAMA WA MADINI UWE AJENDA KATIKA SHUGHULI ZA UCHIMBAJI MADINI-WAZIRI BITEKO

$
0
0
Na Mwandishi wetu,Mwanza,

“Uhai wa mtu mmoja ni muhimu kuliko uwepo wa mgodi, uhai wa mtu unathamani kubwa kuliko mgodi wenyewe, uchimbaji salama inapaswa kuwa ajenda katika shughuli zote za uchimbaji madini nchini,”.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Madini, Doto Biteko alipotembelea mgodi wa Mhalo uliopo wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza mara baada ya kupata taarifa ya ajali iliyowapata wachimbaji 9 ambapo nane miongoni mwao waliokolewa na mmoja bado hajapatikana.

Akizungumza katika tukio hilo Waziri Biteko ametoa pole kwa waathirika wote waliokuwa kwenye ajali hiyo na kuwataka waokoaji kuendelea na jitihada za kumtafuta Immanuel Isaac mwenye umri wa miaka 26 ambaye mpaka sasa hajapatikana.

Aidha, Waziri Biteko amewataka wachimbaji wote nchini kuhakikisha wanachimba kwa utaratibu na kwa kufuata maelekezo ya wataalamu wa migodi wanaoshughulika na masuala ya ukaguzi na usalama katika maeneo ya migodi.

“Naomba nichukue fursa hii kuwaelekeza wachimbaji wote nchini kuhakikisha mnazingatia usalama mahala pa kazi ili kuepusha matukio ya ajali kama hili lililotokea katika mgodi huu wa Nyamikoma uliopo hapa kijijini Mhalo,” amesema Waziri Biteko.

Katika hatua nyingine, Waziri Biteko amewataka wachimbaji wa madini katika eneo lenye mlipuko wa madini lililogunduliwa na wachimbaji wadogo mnamo tarehe 6 Novemba, 2021 kuhakikisha wanachimba kwa kufuta taratibu na kuzingatia usalama katika shughuli zao.

Pia, Waziri Biteko ameitaka Tume ya Madini pamoja na Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Ernest Maganga kuhakikisha wanatoa leseni ndani ya wiki mbili katika mgodi huo wa Kiwili uliopo katika kijiji cha Mhalo wilayani Kwimba.

“Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan anatamani wachimbaji wote wa madini nchini watajirike, ongezeni juhudi na maarifa katika utendaji kazi wenu na msiruhusu majungu kati yenu, pendaneni na msiruhusu mtu aje awagombanishe,” amesema Waziri Biteko.

Akijibu ombi la Mbunge wa Jimbo la Kwimba Shanif Mansoor, Waziri Biteko amesema Wizara yake itaangalia uwezekano wa kufungua Kituo cha ununuzi wa madini katika eneo hilo na kumpeleka Afisa Madini atakaye simamia eneo hilo ili Halmashauri ya wilaya ya Kwimba iweze kunufaika na uwepo wa madini katika eneo lao ambapo kwa sasa madini yanasafirshwa kupelekwa Soko la Mkoa wa Mwanza.

Pamoja na mambo mengine, Waziri Biteko amewasisiza wachimbaji wote katika kijiji cha Mhalo kuhakikisha wanajitokeza kuhesabiwa katika Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika mwaka 2022 iliserikali ijue idadi ya wachimbaji wa madini nchini na kuwataka wachimbaji wote nchini kuhakikisha wanachanjwa ili kuepuka ugonjwa wa uviko-19.

Kwa upande wake Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Ernest Maganga amesema baada ya tukio la kuanguka kwa nguzo iliyokuwa inashikilia ukuta chini ya shimo katika mgodi wa Nyamikoma, Ofisi ya Madini ya Mkoa wa Mwanza walifika eneo la tukio na kufanya ukaguzi ambapo watu 9 walikuwa wanaendele na shughuli za uzalishaji ambapo watu 8 walifanikiwa kutoka na mtu mmoja hakuonekana ambapo mpaka sasa juhudi za kumtafuta zinaendelea.

Pia, Maganga amesema Novemba 6, 2021 wachimbaji wadogo wa madini waligundua uwepo wa madini katika eneo la Kiwili katika kijiji cha Mhalo ambapo Ofisi ya Madini ya Mkoa wa Mwanza ilifika katika eneo hilo na kuwatambua waliogundua na kuwashauri juu ya uchimbaji salama.

NAIBU WAZIRI MOLLEL AFANYA ZIARA MKOANI KAGERA

$
0
0
Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel ameanza ziara ya kikazi katika Mkoa wa Kagera na kupokelewa na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa huo Meja Jenerali Charles Mbuge.

Akiwa mkoani Kagera Dkt. Mollel leo atashiriki katika uzinduzi wa Mpango wa Kikanda wa Mapambano dhdi ya Ugonjwa wa Malaria katika Nchi za Maziwa Makuu unaohusisha nchi za Tanzania, Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Demokrosia ya Congo, Uganda, Kenya pamoja na Sudani ya Kusini.

Uzinduzi huo kwa nchi ya Tanzania na Rwanda unatarajiwa kufanyika Wilayani Ngara katika Mpaka wa Rusumo unaotenganisha Tanzania na Rwanda.

Katika mazungumzo yao, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Charles Mbuge amesema kuwa Mkoa huo uko juu katika maambukizi ya ugonjwa wa malaria kwa 15.4% huku kiwango maambukizi ya ugonjwa huo kitaifa ni 7.4% na kusema kuwa Ugonjwa Malaria bado ni tishio katika Mkoa huo.

Aidha Meja Jenerali C. Mbuge amesema kuwa Mkoa huo umepokea fedha kiasi cha Tsh Bilioni 20 kutoka katika Mpango wa Taifa wa Maendeleo na mapambano dhidi ya UVIKO-19 fedha ambazo zitaelekezwa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo na kumshurku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya maendeleo ya Mkoa huo na Taifa kwa ujumla.

Kuhusu hali ya utoaji wa Chanjo ya UVIKO-19, Meja Jenerali C. Mbuge amesema kuwa Mkoa huo awali ulipokea dozi 45,000 ambazo zote zilikwisha na kuongezewa tena dozi zaidi ya 61,000.

Dkt. Mollel amewataka wataalam wa afya pamoja na Taasisi za Afya mkoani Kagera kutoa ushirikiano kwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa pamoja na watendaji wengine wa Serikali.

Amewataka watumishi wote kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi na kutoa huduma bora kwa wananchi pamoja na kuendelea kutoa elimu ya UVIKO-19 na kuhamasisha wananchi kupata chanjo.

Kuhusu miradi inayoendelea na ile itakayotekelezwa kupitia fedha zilizotelewa kupitia Mpango wa Maendeleo ya Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO-19 Dkt. Mollel amewataka watendaji kusimamia vyema miradi hiyo na kuitekeleza ndani ya wakati huku akiwaonya wote ambao watahusika katika rushwa na hujuma za miradi hiyo kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

BALOZI MBENNAH ATETA NA MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MAURITIUS

$
0
0
Makamu Rais wa Jamhuri ya Mauritius Mhe. Eddy Boissezon, GOSK akiteta na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Mauritius mwenye makazi yake Harare, Zimbabwe, Prof. Emmanuel Mbennah
Makamu Rais wa Jamhuri ya Mauritius Mhe. Eddy Boissezon, GOSK akisalimiana na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Mauritius mwenye makazi yake Harare, Zimbabwe, Prof. Emmanuel Mbennah

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Mauritius mwenye makazi yake Harare, Zimbabwe, Prof. Emmanuel Mbennah amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu Rais wa Jamhuri ya Mauritius Mhe. Eddy Boissezon, GOSK.

Katika mazungumzo hayo Viongozi hao walionesha utashi kuona kwamba ushirikiano baina ya Nchi hizi unazidi kuimarika katika nyanja za uchumi, biashara utalii na uwekezaji.

Makamu wa Rais pia aliipongeza Tanzania kwa Mtanzania Abdulrazak Gurnah kushinda Tuzo ya Amani ya Fasihi.
Viewing all 45982 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>