Quantcast
Channel: VIJIMAMBO
Viewing all 45912 articles
Browse latest View live

TANGAZO KUTOKA UONGOZI WA TAWI LA CCM NEW YORK

$
0
0
Tangazo maalumu:
Mkutano mkuu wa CCM New York pamoja na vitongoji vyake  sasa utafanyika Jumamosi inayofuata October 11 kupisha sikukuu ya Eid. Mkutano huu utafanyika
 30 Over hill Road, Mt. Vernon, NY
 saa nane mchana. Kwa wale wote waliochukuwa forms za kugombea uongozi deadline ya kurudisha forms ni Jumamosi October 4. Shukran, CCM Uongozi, NY. Kwa maelezo zaidi wasiliana na 
Akida Seif kupitia 
namba.
917 557 3195.

MDEE NA WENZAKE WAPATA DHAMANA

$
0
0

Halima akionesha ishara ya Chadema
Halima Mdee na wenzake wakitoka mahakamani baada ya kuachiwa huru kwa dhamana leo.
Wafuasi wa Chadema wakijiandaa kuwapokea wanachama wao baada ya kuachiwa huru.…
Halima Mdee na wenzake wakitoka mahakamani baada ya kuachiwa huru kwa dhamana leo.
Wafuasi wa Chadema wakijiandaa kuwapokea wanachama wao baada ya kuachiwa huru.
Halima akiwa na wanachama wa Chadema baada ya kuachiwa huru.
Halima Mdee akisalimiana na wanachama wake baada ya kuachiwa huru.
Wakili wa kujitegemea wa Chadema, Peter Kibatara, akizungumza na wanahabari.
Wafuasi wa Chadema wakionyesha bango lenye ujumbe wa kumpongeza mbunge wao.

Mdee akiwa juu ya gari akitoka nje ya mahakama.
Gari la wanachama wa Chadema likitoka katika mahakama.

Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na wenzake 8 leo wamepata dhamana katika Mahakama ya Kisutu, Dar. Kesi yao kutajwa tena Oktoba 21, 2014.

Siku ya jana washtakiwa hao walipanda kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi Kaluyenda na kusomewa mashtaka mawili na Wakili wa Serikali Mkuu, Kangola aliwataja washtakiwa kuwa ni Mbunge wa Kawe, Mdee, Rose Moshi, Penina Peter, Anna Linjewile, Mwanne Kassim, Sophia Fanuel, Edward Julius, Martha Mtiko na Beatus Mmari.

Mdee na wenzake hao wanashitakiwa kwa makosa mawili la kwanza washtakiwa wote wanadaiwa Oktoba 4 mwaka huu, Mtaa wa Ufipa wilayani Kinondoni, walikaidi amri ya Ofisa wa Polisi SP Emmanuel Tillf iliyowataka watawanyike.

Shtaka la pili washtakiwa wote wanadaiwa Oktoba, mwaka huu, maeneo ya mtaa wa ufipa jijini Dar es Salaam wakiwa na lengo moja walikusanyika kinyume na sheria wakitaka kwenda ofisi ya rais.

(Habari/Picha na: Deogratius Mongela na Denis Mtima/GPL)

HAPPY BIRTHDAY

$
0
0
Wish you the Best Happy Birthday Honey from Dad, George and Justin

BENKI YA DUNIA NA IMF YAANZA MIKUTANO YA MWAKA MJINI WASHINGTON DC - MAREKANI

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu waserikali Dr. Servacius Likwelile akifurahia jambo na
Bw.Herve’ Joly ambaye ni Mkurugenzi msaidizi na Mkuu wa idara ya Afrika sehemu ya Mashariki. Mara baada tu yakuingia ukumbini.
Dr. Servacius Likwelile Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali akiwa pamoja na ujumbe kutoka Tanzania. Kutoka kushoto ni Kamishna wa Bajeti Bw. John Cheyo akifuatiwa na Bi.Mwanaidi Mtanda ambaye ni mhasibu mkuu wa Serikali na wa mwisho kutoka kulia ni Balozi Liberata Mulamula.
Bw.Herve’ Joly ambaye ni Mkurugenzi msaidizi na Mkuu wa idara ya Afrika sehemu ya Mashariki akishauriana na mwenzake baada ya kupokea hoja kutoka kwa Dr. Servacius Likwelile Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani –Washington Mhe.Liberata Mulamula pamoja na Serikali Dr. Servacius Likwelile Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha wakifurahia pongezi walizopewa na ujumbe wa IMF kuhusu muelekeo mzuri wa uchumi wa Tanzania.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile akielezea mikakati ya nchi ya Tanzania katika kuinua uchumi na kuongeza pato la Taifa kwenye Mkutano uliofanyika leo juu yuliohusu masuala na fedha na sera ya kiwango cha ubalilishaji fedha.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA FEDHA




TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
BENKI YA DUNIA NA IMF YAANZA  MIKUTANO YA MWAKA MJINI WASHINGTON DC - MAREKANI

Kila  mwaka Bodi ya Magavana ya Shirika la Fedha la Kimataifa na kundi la Benki ya Dunia hukutana kwa ajili ya kujadili  kazi za Taasisi zinazowahusu. Mikutano hii imeanza tarehe 06 Octoba na itafikia kilele chake hapo tarehe 13, mwezi Octoba, 2014.Mikutano hii hufanyika mjini Washington DC kwa miaka miwili mfululizo na kwa mwaka wa tatu hufanyika kwa nchi mwanachama. 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile ndiye kiongozi wa ujumbe kutoka Tanzania na yeye anawakilisha kama Gavana mbadala (Alternate Governor) pamoja na Gavana wa Benki Kuu  Prof. Benno Ndulu  ambaye pia ni Gavana katika mikutano hii.
Mikutano hii inatoa nafasi ya kuweza kujadiliana na Benki ya Dunia pamoja na Shirika la Fedha la Kimataifa kuhusiana na hali ya uchumi kwa maana ya sera za fedha na sera za mapato na matumizi. Nia yao kubwa ni kutaka kusikia mawazo yetu kuhusu jinsi ya kuboresha uchumi ili wawe katika nafasi nzuri ya kuangalia ni wapi wanaweza kutusaidia kuboresha na kuona kwamba nchi yetu inaendelea kufanya vizuri zaidi. Maeneo ambayo yameshajadiliwa ni pamoja sera kuhusu kiasi cha ubadilishaji fedha, mapato ya nchi kwa ujumla na mwendo wa matumizi ya fedha.
Hali ya  utendaji wa kiuchumi na hali ya matumizi na mapato ya fedha ya Tanzania imeonekana ni ya kuridhisha  japo pado kunachangamoto ya ajira.
Hali ya hewa mjini  hapa ni baridi kiasi na manyunyu ya hapa na pale   
                                                            

Imetolewa na:
Ingiahedi Mduma
Msemaji -Wizara ya Fedha
Washington D.C
7/10/2014

JK APOKEA KATIBA INAYOPENDEKEZWA MJINI DODOMA LEO

$
0
0
Mwenyekiti wa Bunge maalum la Katiba Mhe.Samuel Sitta akikabidhi katiba inayopendekezwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho kikwete na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt.Mohamed Ali Shein katika hafla iliyofanyika katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma Oktoba 08, 2014
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho kikwete na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt.Mohamed Ali Shein wakiwa wameinua juu Katiba inayopendekezwa katika hafla iliyofanyika katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma Oktoba 08, 2014 Kulia ni Mwenyekiti wa Bunge maalum la Katiba Mhe.Samuel Sitta akifuatiwa na Makamu wake Mhe samia Suluhu Hassan

UNHCR yakwamua maisha ya malaki ya wakimbizi Burundi

$
0
0
Mama Furaha akipika katika nyumba ya rafiki yyake Cady ambaye aliwakaribisha nyumbani mwake.© UNHCR/A.Nijimbere

Maisha baada ya kuishi ukimbizini huhitaji msaada mkubwa katika nyanja zote za uchumi, kijamii na hata kisaikolojia! Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR nchini Kenya limejikita kusaidia wakimbizi katika kustawisha maisha yao ambapo huanza kwa makazi.

Akizungumza wakati wa mahojiano na Joseph Msami wa idhaa hii mwakilishi mkazi wa UNCHCR nchini Burundi Abel Mbilinyi anasema hatua hiyo inakomboa maisha ya wakimbizi takribani laki tano huku pia akizungumzia nafasi ya wakimbizi katika uchaguzi mkuu ujao. Kwanza anaanza kufafanua namna UNHCR inavyopoka na kusidia wakimbizi

(SAUTI MAHOJIANO)

TAARIFA FUPI YA MAFANIKIO YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA SERIKALI MKOANI SINGIDA KIPINDI CHA 2005 - 2014

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Parseko Vicent Kone
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Parseko Vicent Kone.
Katibu Tawala Mkoa wa Singida Bw. Liana Hassan.
Katibu Tawala Mkoa wa Singida Bw. Liana Hassan.
Jengo la OPD katika Hospitali Mpya ya rufaa ya Mkoa wa Singida.
Jengo la OPD katika Hospitali Mpya ya rufaa ya Mkoa wa Singida.
Jengo la utambuzi wa Magonjwa katika Hospitali Mpya ya rufaa ya Mkoa wa Singida.
Jengo la utambuzi wa Magonjwa katika Hospitali Mpya ya rufaa ya Mkoa wa Singida.

CBA YATANUA KWENYE M-PAWA

$
0
0
DSC_0055
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara ya Afrika (CBA), Julius Mcharo akizungumza wakati kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja, ambapo alitumia fursa hiyo kuwashukuru wateja wao kwa kuichagua CBA pamoja na kuwapongeza wafanyakazi wa benki yake kwa kutoa huduma nzuri kwa wateja wao katika mkutano na wanahabari uliofanyika kwenye tawi la CBA Kariakoo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja anayeshughulikia wateja wa CBA Tanzania, Rehema Ngusaru na Afisa viwango na ubora wa huduma CBA Tanzania, Anicetius Buberwa (aliyesimama kushoto).(Picha na Zainul Mzige).
DSC_0001
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara ya Afrika (CBA), Julius Mcharo (aliyekaa kulia) akisikiliza maswali kutoka kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja wa benki ya CBA ambapo watatumia wiki hii kusikiliza nini wateja wao wanataka. Waliosimama kutoka kulia ni Meneja wa tawi la CBA Kariakoo, Vicky Munishi, Boniface Kiwia kutoka makao makuu ya CBA, Tanzania, Rehema Mashayo kutoka makao makuu wa benki ya CBA Tanzania. na kushoto ni Afisa viwango na ubora wa huduma CBA Tanzania, Anicetius Buberwa.
Na Mwandishi wetu
HUDUMA ya M-PAWA inayotolewa na Benki ya Biashara ya Afrika (CBA) imetoa mikopo ya shilingi milioni 200 katika kipindi cha miezi mitatu tangu ianzishwe.
Pamoja na fedha hizo huduma hiyo imewezesha kuwepo na amana za shilingi bilioni 6 kutoka kwa wateja laki 7 ambao wanapata huduma ya M-Pawa.
Taarifa hiyo ya mafanikio imetolewa na Kaimu Mtendaji Mkuu wa benki hiyo Julius Mcharo akizungumza kwenye uzinduzi wa wiki ya Huduma kwa Wateja iliyofanyika Kariakoo.
Mcharo alisema huduma hiyo inayotolewa kwa ushirikiano kati ya benki hiyo na Vodacom imepata muitikio kutokana na watanzania kuweza kufungua akaunti za huduma hiyo mahali popote pale walipo kwa kutumia mtandao.
Alisema huduma hiyo ambayo pia inawezesha kupatikana kwa mikopo na kupokea na kulipa huduma mbalimbali kwa m-pesa imerahisisha maisha ya wananchi wengi na kusema kwamba itaendelea kuboreshwa na kutanuliwa.
Akizungumzia wiki ya huduma kwa wateja alisema kwamba watendaji wote wa benki hiyo wanakwenda katika matawi yapatayo 11 nchini kote kutoa huduma kwa karibu zaidi na wateja wao kwa lengo la kufahamu changamoto zao.
Alisema changamoto hizo zitawawezesha kutambua mahitaji halisi ya wateja na kutengeneza bidhaa zinazolingana na mahitaji yao.
DSC_0080
Meneja anayeshughulikia wateja wa CBA Tanzania, Rehema Ngusaru akifafanua jambo kwenye mkutano na waandishi wa habari wakati wakitangaza rasmi kuzindua maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja watakayoitumia kusikiliza changamoto wanazokutana nazo wateja wao.
Alisema benki hiyo ambayo ina matawi matano Dar es salaam na mengine yakitawanyika katika miji ya Mtwara, Mbeya,Arusha, Tunduma imejitanua katika kutoa huduma kwa kutumia teknolojia hasa kwa kuwa na huduma za kibenki kwa njia ya mtandao.
Alisema kupitia njia ya mtandao wateja wao wanaweza kupata mikopo na hata kulipa huduma mbalimbali.
Aliwashukuru wateja na wafanyakazi kwa kuwezesha ndoto za wengi kutimia kwa kutumia huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo na kuwataka waendelee kutumia CBA katika kuchupa mbele kimaendeleo.
Baadhi ya wateja waliohojiwa katika uzinduzi huo walikiri kufurahishwa na huduma za benki hiyo hasa kutokana na kutokuwa na foleni na kujali wateja wao.
Charles Mlawa alisema kwamba wamefurahishwa sana na uwapo wa tawi la CBA Kariakoo kwani limefanya waweze kuwa na uhakika na utumaji wa fedha kwa wadau wao ili kupata bidhaa zinazotakiwa.
DSC_0091
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara ya Afrika (CBA), Julius Mcharo akitoa huduma kwa mkazi wa jijini Dar Bw. Ali Sareva aliyefika kwenye tawi la benki ya CBA lililopo Kariakoo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufungua akaunti ya kampuni yake wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja inayoadhimishwa ulimwengu mzima ambapo benki ya CBA wataadhimishi wiki hiyo kwa kusikiliza nini wateja wanachokitaka na kuwa nao karibu zaidi kuboresha huduma zao.
Mlawa alisisitiza kwamba tatizo la usafirishaji fedha nje lilikuwa kero kwao lakini tangu kufika kwa benki hiyo hali ni njema zaidi.Aidha alishukuru kwa huduma nzuri za ki
benki zinazotolewa.
Akizungumzia mikopo ya nyumba ambayo benki hiyo ilianza kutoa mwaka 2007 amesema program hiyo inaenda vyema na kwamba hadi sasa wametoa mikopo ya zaidi ya sh bil 25 huku muda wa kulipa ukiwa umeongezwa hadi miaka 20.
Alisema amefurahishwa sana kuwa moja ya mabenki matatu makubwa nchini ambayo yanatoa mikopo kwa ajili ya ujenzi wa makazi.
Meneja anayeshughulikia wateja wa CBA Tanzania, Rehema Ngusaru, amesema kwamba sasa hivi pia kuna mikopo ya kuboresha nyumba.
Aidha amesema kwamba wanahakika ya kuendelea kuwa na huduma nzuri kutokana na mikakati waliyojipangia na kuwakumbusha wafanyakazi namna bora ya kuhudumia wateja.
DSC_0097
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara ya Afrika (CBA) Tanzania, Julius Mcharo akimshukuru mkazi wa jijini Dar Bw. Ali Sareva kwa kuiamini na kuichagua benki ya CBA inayowajali wateja wake.
DSC_0108
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Commercial Bank of Africa (CBA) Tanzania, Julius Mcharo akimhudumia mmoja wateja wakubwa wa benki hiyo mfanyabiashara maarufu Kariakoo Bw. Charles Mlawa kwenye tawi la benki hiyo lililopo Mtaa wa Narung'ombe Kariakoo jijini Dar es Salaam katika kuadhomisha wiki ya huduma kwa wateja.
DSC_0121
Mkuu wa biashara na uendeshaji wa kampuni ya vifaa vya umeme ya Tropical ambaye pia ni mteja wa benki ya CBA tawi la Kariakoo, Bw. Charles Mlawa, akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema wamepata faida kubwa sana kwa benki ya CBA kuwepo Kariakoo akiwa yeye kama mteja wa siku nyingi wa benki hiyo ambapo pia ameipongeza benki hiyo kwa huduma bora na yenye uhakika ya gharama nafuu kabisa ambayo ni sawa na bure ya TT katika utumaji wa fedha. Katikati ni mteja mwingine wa benki ya CBA Tanzania, Bw. John Nenuta.
DSC_0134
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara ya Afrika (CBA) Tanzania, Julius Mcharo (waliosimama wanne kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na wateja wa benki ya CBA tawi la Kariakoo pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo kutoka makao makuu ya CBA Tanzania na wafanyakazi wa tawi la Kariakoo.
DSC_0137
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara ya Afrika (CBA) Tanzania, Julius Mcharo akiagana na mmoja wa wateja wa benki hiyo tawi la Kariakoo mara baada ya zoezi la picha ya pamoja.
DSC_0141
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara ya Afrika (CBA) Tanzania, Julius Mcharo katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wenzake.

MGONJWA WA EBOLA MAREKANI AFARIKI

$
0
0
Mtu wa kwanza kupatikana na ugonjwa wa Ebola nchini Marekani amefariki ,hayo ni kwa mujibu wa maafisa wa afya katika hospitali ya Texas.

Thomas Eric Duncan aliyeambukizwa ugonjwa wa Ebola huko nchini Liberia ,alikuwa amewekwa katika karantini katika hospitali moja ya mjini Dallas ili kupewa dawa za majaribio.

Awali ,Marekani ilitangaza masharti mapya ya usalama katika viingilio vyote vya taifa hilo ili kuwakagua wasafiri walio na dalili za ugonjwa huo.

Zaidi ya watu 3000 wamefariki na wengine 7500 kuambukizwa wengi wao kutoka Afrika Magharibi katika mlipuko mbaya wa ugonjwa wa Ebola.

Huku Dancun akiwa raia wa kwanza nchini Marekani kupatikana na ugonjwa huo,raia watatu wa Marekani pamoja na mpiga picha mmoja waliambukizwa virusi vya ugonjwa huo nchini Liberia.

Habari hizo zilijiri mda mchache tu baada ya waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani John Kerry kutoa wito kwa mataifa yote kuimarisha juhudi zao za kukabiliana na ugonjwa huo. BBC

REDD'S MISS TANZANIA 2014 KUFANYIKA MLIMANI CITY JUMAMOSI HII

$
0
0
Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency ambao ni waratibu wakuu wa Mashindano ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga (kulia) akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam leo, juu ya onyesho la Redd's Miss Tanzania 2014 linalotarajiwa kufanyika Oktoba 11, 2014 katika Ukumbi wa Mlimani City,Jijini Dar.Katikati ni Meneja wa Kinywaji cha Redd's ambao ni Wadhamini Wakuu wa Mashindano hayo, Victoria Kimaro na kushoto ni Meneja Maria Stopes Tanzania, Anna Shanalingigwa.
Meneja wa Kinywaji cha Redd's ambao ni Wadhamini Wakuu wa Mashindano ya Miss Tanzania, Victoria Kimaro (kushoto) akizungumzia zawadi watakayotoa kwa Washindi watakaopatikana kwenye Shindano hilo la Redd's Miss Tanzania 2014,ambapo mwaka huu mshindi wa kwanza katika kinyang'anyiro hicho atajinyakulia kitita cha sh. Mil. 18 taslimu huku washindi wengine wakiendelea kuondoka na zawadi mbali mbali.Katikati ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency ambao ni waratibu wakuu wa Mashindano ya Miss Tanzania,Hashim Lundenga na kulia ni Meneja wa Hoteli ya JB Belmont, Gillian Macheche pamoja na Afisa Habari wa Miss Tanzania ,Hidan Ricco.
Sehemu ya Wanahabari pamoja na Warembo watakaoshiriki kwenye kinyang'anyiro cha Redd's Miss Tanzania 2014 wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency ambao ni waratibu wakuu wa Mashindano ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga alipokuwa akizungumza.
Sehemu ya Warembo watakaoshiriki kwenye kinyang'anyiro cha Redd's Miss Tanzania 2014. 
Warembo watakaoshiriki kwenye kinyang'anyiro cha Redd's Miss Tanzania 2014 wakipata picha ya pamoja.
(Picha zote na Othman Michuzi)

KAMA KWELI UNAMPENDA MWENZIO USIJARIBU KUJARIBU NYUMBANI

HUYU NDIYO KAJALA MASANJA

$
0
0
Mwigizaji Kajala Masanja Wema alisahidia kumnusuru kutumikia kifungo jail lakini sasa uwezi kuamini wawili hawa hawapikiki chungu kimoja unaweza kujifunza nini kutoka kwao?. Au unafikiri ni nini kimesababisha haya yote kutokea?.

The Real Reason Why Gaddafi Was Killed

DK. SHEIN AZUNGUMZA NA UONGOZI WA ZANCHICK

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Kiongozi wa Kampuni ya ZANCHICK inayojishughulisha na biashara ya kuuza kuku (Perdue) kutoka Marekani Dk. David Elua akiwa na ujumbe wa kampuni hiyo ulipofika Ikulu Mjini Unguja jana kwa mazungumzo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akizungumza na Uongozi wa Kampuni ya ZANCHICK inayojishughulisha na biashara ya kuuza kuku (Perdue) kutoka Marekani unaoongozwa na Dk. David Elua katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja jana. [Picha na Ramadhan Othman Ikulu, Zanzibar.

Please vote for PETER MSECHU


UFUNGUZI WA MAADHIMISHO SIKU YA POSTA DUNIANI OKTOBA 9-2014

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Mkoma, akizungumza katika mkutano huo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Patrick Makungu akihutubia katika uzinduzi huo.
Meneja Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungy, akizungumza kwenye hafla hiyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Patrick Makungu (kushoto), akimkabidhi zawadi Mwalimu Lucy Mshomi wa Shule ya Wasichana ya Kifungiro kutokana na mchango mkubwa kwa wanafunzi wao. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Posta, Deus Mndeme.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Patrick Makungu (kushoto), akimkabidhi zawadi Mwalimu Josephine Mashare wa Shule ya Wasichana ya ST' Marys ya Mazinde Juu kutokana na mchango mkubwa kwa wanafunzi wao.Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Posta, Deus Mndeme.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Patrick Makungu (kushoto), akimkabidhi zawadi mwanafunzi mshindi wa kwanza kitaifa wa kuandika barua, Glory Mduma kutoka Shule ya Sekondari ya ST, Marys Mazinde Juu mkoani Tanga. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Posta, Deus Mndeme.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Patrick Makungu (kushoto), akimkabidhi zawadi Mshindi wa tatu wa shindano hilo, Khadija Rashid wa Shule ya Sekondari ya ST, Marys Mazinde Juu. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Posta, Deus Mndeme.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Patrick Makungu (kushoto), akimkabidhi zawadi mwanafunzi mshindi wa pili kitaifa wa kuandika barua , Ndehovye Nyindo wa Shule ya Wasichana ya Lufungiro iliyopo mkoani humo. 
Wanafunzi ambao ni washindi wa shindano la kuandika barua wakiwa katika picha ya pamoja na zawadi zao walizokabidhiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Patrick Makungu kwa niaba ya Waziri wa wizara hiyo, Profesa Makame Mbarawa katika hafla ya ufunguzi wa maadhimisho ya siku ya Posta Duniani 2014 yaliyofanyika Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni mshindi wa kwanza kitaifa wa shindano hilo, Glory Mduma kutoka Shule ya Sekondari ya ST, Marys Mazinde Juu mkoani Tanga, Mshindi wa pili, Ndehovye Nyindo wa Shule ya Lufingiro mkoani humo, na Mshindi wa tatu, Khadija Rashid wa Shule ya Sekondari ya ST, Marys Mazinde Juu.
Wanafunzi, Wazazi na wageni waalikwa wakiwa kwenye hafla hiyo.

Habari na Dotto Mwaibale
WANAFUNZI wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya St Mary's ya Mazinde Juu iliyopo mkoani Tanga wameibuka vinara wa shindano la uandishi wa barua lililoshirikisha wanafunzi wa shule mbalimbali nchini katika kuadhimisha siku ya posta duniani.
Shindano hilo la uandishi wa barua limeratibiwa na Shirika la Posta Tanzania kwa kushirikiana na umoja wa posta duniani.
Akizungumza Dar es saalam leo katika hafla ya uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya posta duniani, Mkurugenzi Mkuu wa Posta nchini, Deus Mdeme alitoa pongezi kwa washindi hao na walimu wao kwa kufanikiwa kuibuka videdea ambapo mshindi wa kwanza ataiwakilisha Tanzania katika mashindano ya barua ya kimataifa yatakayofanyika baadaye mwaka huu nchini Uswisi.

"Madhumuni ya shindano hili ni kuwajengea uwezo vijana ambao hawajazidi miaka 15'' alisema Mdeme.
Katika Shindano hilo la uandishi wa barua jumla ya washindi kumi walipatikana, huku St Mary Mazinde juu wakiibuka videdea kwa kutoa washindi wawili huku mshindi wa pili akitoka Shule ya Sekondari ya Lufingilo mkoani humo ambapo walikabidhiwa vyeti na zawadi mbalimbali.
Aidha katika kuadhimisha siku hiyo ya posta duniani, yenye kauli mbiu isemayo posta inachukua nafasi yake katika mageuzi ya sekta ya mawasiliano imeadhimishwa kwa kuelezea malengo na changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya Posta Tanzania.
Wakati huo huo Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Patrick Makungu kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo, Profesa Makame Mbarawa, alielezea mafanikio na changamoto mbalimbali zinazoikabili Sekta ya Posta Tanzania katika kufanikisha malengo yake.

Vilevile alitumia nafasi hiyo kuhamasisha wanafunzi wengi zaidi kushiriki katika shindano hilo linaloandaliwa na umoja wa posta duniani na kuwataka wadau wa posta nchini kushirikiana na shirika hilo ili likue na kutoa huduma kwa jamii baada ya kubadilisha ufumo wa utoaji huduza zake kwa kutumia zaida Tehama.

ANGALIA RECORDED LIVE MAHOJIANO KUTOKA WASHINGTON, DC NCHINI MAREKANI YA AUNTY EZEKIEL NA CASSIM MGANGA

Baregu afichua siri nzito Tume ya Katiba

$
0
0
Aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Mwesiga Baregu, ametoboa siri kuwa Mwenyekiti wa tume hiyo Jaji Joseph Warioba alikuwa na msimamo wa serikali mbili, kabla ya tume kuja na rasimu yenye muundo wa muungano wa serikali tatu uliotokana na maoni ya wananchi walio wengi.

Baregu alitoboa siri hiyo wakati akizungumza na NIPASHE katika mahojiano maalum yaliyofanyika nyumbani kwake mwanzoni mwa wiki hii. Alikuwa akijibu moja ya maswali aliyoulizwa kuhusiana na namna wao (tume) walivyoondosha tofauti za kimtazamo miongoni mwa wajumbe na kuandaa rasimu iliyokubaliwa na wajumbe wote; tofauti na wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambayo walitofautiana sana kuhusiana na suala la muundo wa muungano na mwishowe, wajumbe wengi wa upinzani wakasusia vikao kupitia mwavuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na kuwaachia wenzao wanaoundwa na wafuasi wengi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuendelea na kazi hiyo.

Wajumbe wanaounda Ukawa ambao wengi ni kutoka vyama vikuu vya upinzani nchini vya NCCR-Mageuzi, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Chama cha Wananchi (CUF) walisusia vikao vya Bunge la Katiba kutokana na madai yao kuwa rasimu iliyoandaliwa na tume iliyoongozwa na Warioba kwa kuzingatia maoni ya wananchi ilibadilishwa kwa maslahi ya CCM. Ukawa walikuwa wakitetea rasimu ya Warioba iliyopendekeza muundo wa muungano wa serikali tatu huku wajumbe wengi wa CCM wakisisitiza kuwa na muundo wa muungano wa serikali mbili lakini ulioboreshwa.

Akieleza zaidi, Baregu alisema kuwa kwa ujumla, tume ilijigawa kwenye kamati ndogo tatu wakati wa kuanza kujadili mapendekezo, ambazo ni kamati ya mihimili ya utawala (bunge, serikali na mahakama), kamati ya iliyokuwa ikishughulikia misingi na maadili ya taifa na kamati ya tatu ndiyo iliyokuwa ikishughulikia masuala ya muungano.

“Labda niwaeleze tu, hiyo kamati ya muungano tuliipa jina kama kundi la kifo... na ninalitaja kundi hili kwa masikitiko kwa sababu mmoja wetu, Dk. Mvungi alifariki kweli,” alisema.

Prof. Baregu alisema kundi la kifo lilikuwa la watu wenye misimamo kuanzia wa serikali moja, mbili, tatu na wengine waliokuwa na mawazo ya kuwa na muungano wa mkataba.

“Akina nanihii hawa... akina Warioba, akina Butiku, Jaji August... walianza na msimamo wa serikali mbili. Mimi siku nyingi ni mtu wa serikali moja. Wakawapo watu wa serikali tatu, including (akiwamo) Dk. Mvungi. Na kundi la nne la watu wenye msimamo wa serikali ya mkataba,” alisema.

Alisema pamoja na minyukano iliyojitokeza kutokana na misimamo hiyo binafsi ya wajumbe, bado waliweza kusimama imara na kuzishinda nafsi zao kutokana na mawazo ya wananchi waliyoyapata wakati wakikusanya maoni katika maeneo mbalimbali nchini, chini ya uongozi wa mwenyekiti wao (Warioba).

Alisema kuwa awali, mwenyekiti wao (Warioba) alitoa nafasi kwa kila mjumbe kwenye suala la muungano kuzungumza na kutoa mchango wake.

“Ninakumbuka kwenye issue hii ya muungano, kila mjumbe ilibidi azungumze. Na mwenyekiti ali-insist kwamba kila mmoja wetu ni lazima achangie, na tukalizungumza kwa karibu wiki nzima,” alisema.

Prof. Baregu alisema pamoja na kila mjumbe kuzungumza, pia waliangalia maoni waliyokusanya kutoka kwa wananchi na mwisho wa siku wakaja na maamuzi ya pamoja, ambayo yaliwafanya kuchukua msimamo wa pamoja pia.

Alisema hawakumuacha mjumbe yeyote nyuma akiwa bado hajaridhika kwa hoja na maoni waliyokusanya na kwamba, pale ilipotokea hivyo, walianza naye kwenye kikao kilichofuata hadi kuhakikisha kwamba mhusiaka ameridhika.

“Na ndiyo maana sasa hivi ukizungumza na wajumbe wote, sijasikia hata mmoja ambaye amebadilisha mawazo, ama... au amesema kwamba alirubuniwa kwenye tume au labda kwamba Jaji Warioba alifanya maamuzi ya ubabe,” alisema.

Alisema kutokana na namna walivyoendesha mambo yao kwa uwazi na kufikia maamuzi ambayo wote waliyaafiki kikamilifu kuwa yamezingatia kwa usahihi matakwa ya wananchi, ndiyo maana bado wana mshikamano mzuri hadi sasa na wameamua kwenda kuitetea rasimu ya tume kwa wananchi.

Amesisitiza kuwa wajumbe wa tume hiyo wamejipanga kuhakikisha wanawaelimisha wananchi kuhusu mapendekezo yaliyokuwa kwenye rasimu hiyo.

Alisema walipokuwa kwenye Tume walifanyakazi kwa bidii, weledi, nidhamu na kujenga maridhiano ndani ya jamii na ndani ya tume.

"Tuliwasikiliza wananchi wanataka nini na kuzingatia maoni ya Watanzania, na lengo la tume lilikuwa ni kupata katiba yenye maoni ya wananchi,” alisema.

KATIBA ILIYOPENDEKEZWA
Alisema sasa hivi, kwenye Katiba iliyopendekezwa, kuna mambo mengi ya msingi yamenyofolewa; kama mambo ya maadili, uwajibikaji, kumwajibisha mbunge, ukomo wa ubunge, madaraka ya rais na mawaziri kutokuwa wabunge; mambo ambayo yalipendekezwa na wananchi wengi.

Prof. Baregu alisema njia pekee ya kunusuru mchakato mzima wa katiba ni kukubali kwamba tumekwama na kukubali kusahihisha makosa badala ya kuburuza mchakato huo bila maridhiano.

Katiba iliyopendekezwa ilikabidhiwa juzi mjini Dodoma kwa marais, Jakaya Kikwete wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Dk. Ali Mohamed Shein wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

“Sisi ndani ya Tume tulijenga kwanza maridhiano ndiyo maana tuliweza kutoa rasimu ambayo sote tulikubaliana,” alisema
Prof. Baregu alisema: "Kwa hali hii, ilipaswa tuwe na ujasiri wa kupumua kwanza, tukaulizana na tukakubali kwamba tumekwama kwa malengo tuliyokuwa tumejiwekea... sasa hivi ni kama mtu umepotea njia lakini unasema twende tu."

Aliongeza kuwa: "Tulikuwa na lengo, tulikuwa na ramani kwa hiyo kama tungekuwa na ujasiri kama taifa tukasema ngoja tujiulize hapa tufanye nini ili tuweze kutoka hapa, mengi tungeweza kubadilisha." Alisema mchakato umekwama baada ya kutawaliwa na wanasiasa ambao hawawezi kupitisha mapendekezo ambayo yanapingana na maslahi yao.

"Ni vyema kama tungekubali kusema hapa tumekosea, tuunde upya Bunge la Katiba, na kukubali kwamba tumekosea sana... na siyo serikali tu, lakini sote kama taifa."

Alisema. "Nimekuwa nafikiri hivi... ni kama mama mwenye mimba anayepata abortion (mimba kuharibika). Anajisikiaje?” alisema Baregu.

Alisema kwa hali ilivyopelekwa, anahisi kuwa na hali kama hiyo ya mama aliyeharibikiwa na mimba yake, kwamba amekuwa kwenye timu iliyofuatilia watu karibu mwaka mmoja na nusu kutunga katiba, lakini inaishia kusakamwa.

Alisema tume imefanya kazi kwa uadilifu, weledi, tena usiku na mchana, siku saba kwa wiki, saa 24 kwa zaidi ya mwaka, lakini kazi waliyofanya kwa uadilifu na umakini mkubwa ni kama imekuwa bure tu.

UCHAMBUZI WA KINA
Baregu alisema kuwa baada ya uchambuzi wa kina na tafiti na taarifa za tume mbalimbali, wajumbe walibaini kwamba Muungano ni yatima na hauonekani kwa kuwa hakuna mamlaka inayosimamia maslahi ya Muungano.

Alisema ili kuondoa kero za Muungano, njia pekee ni kuweka mamlaka mahsusi ili kuuimarisha Muungano.

Alisema inashangaza kuona kwamba wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba (BMK), waliishia kuzungumzia gharama za serikali tatu badala ya kueleza ubaya au udhaifu wa serikali hizo na uzuri wa serikali mbili kwa kina.

"Mimi utabiri wangu, huko tunakokwenda, ama tutaendelea kutumia nguvu zaidi kuwaweka Zanzibar kwenye Muungano ama vinginevyo Muungano utavunjika."

Alisema wananchi wa pande zote za Muungano walitoa mapendekezo yao ambayo tume iliyachambua kwa kina na kutoa fursa kwa wajumbe wote kuchangia jambo hilo.

Akizungumzia tuhuma nyingi walizorushiwa na wajumbe wa bunge maalumu la katiba kuwa rasimu waliyotoa siyo maoni ya wananchi, bali maoni ya kina Warioba, alisema: “Kwa hili, mimi nasema wasitoe tuhuma za kitoto. Kama wana ushahidi, tuundiwe tume ya kimahakama ichunguze mwenendo wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kimaadili, kiweledi, kiuadilifu na kwa kila aina.”

Alisema kama tume hiyo itakuja na majibu kwamba tume ilifanya kazi yake chini ya kiwango, basi wao wawajibishwe na pia rasimu inaweza kubadilishwa.

Alisema siyo busara kuendelea kukosoa kazi ya tume na badala yake, kama ikionekana kwamba haikuwa na uaminifu wala uadilifu; ni vyema jambo hilo likachunguzwa ili kubaini kama ilifanya kazi kinyume cha sheria na pia kinyume cha hadidu za rejea.

Alikikosoa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa kuvuruga mchakato wa Katiba na kueleza kuwa Katiba ni suala la maridhiano zaidi na siyo wingi au uchache kwa kuwa hata wananchi walio wachache, wanapaswa kusikilizwa.

*Usikose kusoma mahojiano zaidi na Profesa Baregu Jumatatu.
CHANZO: NIPASHE

AMEKUSALITI, LAKINI BADO UNAMPENDA?-2

$
0
0
Ni wiki nyingine tena tunapokutana katika uwanja wetu huu mzuri wa kuzungumzia ishu za uhusiano wa kimapenzi. Wiki iliyopita niliiweka mada mezani juu ya nini cha kufanya inapotokea mwenzi wako amekusaliti ingawa ndani ya moyo wako bado unampenda sana.

Inaonekana mada imewagusa wengi kwani nimepokea maoni kwa wingi, kila mmoja akieleza kwa uzoefu wake namna ya kushughulikia tatizo hili. Nakushukuru wewe uliyeshiriki kuchangia mada kwa kutuma ujumbe mfupi na kutoa mawazo yako kuhusu mada hii inayowatesa wengi.
Mawazo yalikuwa ya pande mbili, wapo ambao wameendelea kushikilia msimamo kwamba hakuna msamaha kwa mtu anayesaliti kwenye mapenzi.

Hata hivyo, wengi wameshauri kwamba inawezekana kabisa kuendelea na uhusiano hata baada ya mwenzi wako kukusaliti, cha msingi ni kuusikiliza moyo wako na kumpima mwenzi wako kama amelijua kosa lake na analijutia.

Nauheshimu mchango wa kila mmoja alioutoa na nawapa pole wote ambao wamenisimulia jinsi walivyoumia ndani ya mioyo yao baada ya kugundua kuwa wanasalitiwa na watu wanaowapenda sana. Tuendelee na mada yetu kuanzia pale tulipoishia wiki iliyopita.

NINI CHA KUFANYA UNAPOSALITIWA?

1. JIPE MUDA WA KUTAFAKARI
Sote tunakubaliana kwamba hakuna kipindi kigumu kwenye mapenzi kama unapogundua kuwa mwenzi wako amekusaliti. Ni katika kipindi hiki mtu anaweza kujidhuru mwenyewe, kumdhuru mwenzi wake au mwizi wake.

Hata hivyo, wataalamu wa mapenzi wanaeleza kwamba hatua ya kwanza na ya haraka ambayo unatakiwa kuichukua baada ya kugundua kuwa mwenzi wako amekusaliti, ni kujipa muda wa kutafakari kwa kina kuhusu kilichotokea.

Tafuta sehemu tulivu, kaa ukiwa peke yako na tafakari kwa kina juu ya kilichotokea. Anza kwa kujichunguza mwenyewe kwani yawezekana umesababisha mwenzi wako akusaliti.
Maamuzi ya busara hayafanywi ukiwa na hasira, ukijipa muda wa kutafakari utagundua kilichosababisha akusaliti.

2. USIKILIZE MOYO WAKO
Jiulize ndani ya moyo wako kwamba licha ya yote yaliyotokea, bado unamhitaji mwenzi wako na upo tayari kumsamehe? Uzuri wa mapenzi, moyo ndiyo huzungumza ukweli, kama humhitaji tena, chukua uamuzi wa kuachana naye lakini kama bado unampenda, mpe nafasi ya pili.
Epuka kuchukua uamuzi kwa hasira kwa sababu unaweza kuamua kumuacha wakati moyo wako bado unamhitaji baadaye ukaja kujuta. Yafikirie mambo mazuri mliyowahi kuyafanya pamoja kisha yapime.

3. ZUNGUMZA NAYE
Ukishakuwa umezifanyia kazi hatua hizo mbili za hapo juu, tafuta muda wa kuzungumza na mpenzi wako na muulize kwa upole kwa nini amekusaliti. Mpe muda wa kujieleza na msikilize kwa umakini.
Ikiwa anaonesha kujutia makosa aliyoyafanya na akakuomba msamaha kutoka ndani ya moyo wake na kuahidi kutorudia tena, mpe nafasi ya pili. Ukiamua kumsamehe, kweli umsamehe na usibaki na kinyongo ndani ya moyo wako.

4. WASHIRIKISHE WATU UNAOWAAMINI
Yawezekana ukahisi umekosewa sana kuliko mtu mwingine yeyote lakini ukijaribu kuzungumza na watu unaowaamini, ushuhuda wao utakusaidia kuona kila kilichotokea kuwa ni cha kawaida.
Kama ndoa yenu ni changa, jaribu kuzungumza na watu walioishi kwenye ndoa kwa muda mrefu na utashangaa kugundua kuwa wengi walishawahi kusalitiwa lakini wakawasamehe wenzi wao na maisha yakaendelea.

Ni matumaini yangu kuwa mbinu hizo zitakusaidia kukabiliana na hali hiyo ngumu na utampenda tena pengine zaidi ya ulivyokuwa unampenda mwanzo.

GPL

Mauaji ya kutisha Kigoma, saba wateketezwa

$
0
0
Moja ya nyumba zilizoteketezwa katika Kijiji cha Murufiti ambapo watu saba waliuawa kwa kuchomwa moto. Picha na Diana Rubanguka.

Kigoma. Watu saba wameuawa kwa kuchomwa moto ndani ya nyumba katika tukio ambalo nyumba 18 ziliteketezwa na mbili kubomolewa na wananchi waliodai wanawaua wachawi katika Kijiji cha Murufiti, Kasulu, mkoani Kigoma.
Polisi wameeleza kuwa tayari watu 17 wamekamatwa kwa kuhusika kwenye tukio hilo.
Miongoni mwa waliouawa katika tukio hilo lililotokea Jumatatu iliyopita ni John Mavumba (68) na mkewe Elizabeth Kaje 55 ambao pamoja na wenzao walikuwa wakituhumiwa kuwa ni washirikina.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Josephat John ambaye ni mtoto wa Mavumba, alisema wazazi wake walichomwa moto na kundi la vijana waliokuwa wakiwatuhumu kuwa ni wachawi.
Alisema vijana walikuwa wamebeba mapanga, marungu na kupita katika nyumba mbalimbali wakifanya mauaji wakisema maneno kwa kurudiarudia kwamba watawamaliza wachawi kwa kuwaua, ndipo yeye na wenzake walikimbia usiku huo wakihofia kuuawa.
“Niliporudi alfajiri niliukuta mwili wa mama ukiwa umbali wa mita 10 kutoka ilipo nyumba yetu ukiwa umeungua na mwili wa baba ukiwa umeungua ndani ya nyumba,” alisema John.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Jafari Mohamed alisema mauaji hayo yalitokea Oktoba 6 kuanzia saa 4:00 usiku katika kijiji hicho.
John alisema baada ya tukio hilo wanaume wengi wameyakimbia makazi yao wakihofia kuuawa na kundi la vijana hao. “Kijiji kimebaki na wanawake tu, wanaume wamezikimbia nyumba zao wanahofia kuuawa,” alisema.
Mohamed alisema mauaji hayo yametokana na imani za kishirikina.
Aliwataja waliouawa kuwa ni John Muvumba (68), Elizabeth Kaje (55), Dyaba Kitwe (55), Vincent Ntiyaba (42), Herman Ndabiloye (78), Redempta Mdogo (60) na Ramadhan Kalaliza (70) wote wakazi wa kijiji hicho.
Alisema nyumba zilizochomwa moto ni 18, mbili zilibomolewa na kufanya jumla ya nyumba 20 zilizoharibika kabisa.
Wakazi wa kijiji hicho, Zablon Andrew na Eveline Enock walisema kwa nyakati tofauti kuwa chanzo cha mauaji hayo ni mganga wa jadi aliyefika kijijini hapo na kupiga ramli akiwataja watu waliouawa kuwa ni wachawi.
Andrew alisema baada ya mganga huyo kuwataja, vijana walikusanyana na kuanza kuwateketeza watu bila huruma.
“Kitendo hiki kimeturudisha nyuma kimaendeleo kwa sababu nyumba zetu zimechomwa moto na mazao yetu yameharibiwa,” alisema Andrew.
Hali ilivyo kijijini
Mmoja wa watu aliyechomewa nyumba, Evelyne Msilu alisema sasa kijiji hicho kina askari wengi wanaofanya doria.
“Hali inasikitisha, tumepoteza ndugu zetu waliouawa, wanaume wengi wamekikimbia kijiji kwa hofu ya kuuawa na vijana wengine wamekimbia wakiogopa kukamatwa,” alisema.
Kwa nini ipigwe ramli?
Akisimulia, Enock alisema kuna kijana mmoja katika kijiji hicho ambaye kazi yake ni kufyatua matofali aliwaomba vijana wanzake kuwa siku inayofuata wamsaidie kuyapanga katika tanuru.
Alisema jambo la ajabu ni kwamba walipoamka asubuhi walikuta matofali yamekwishapangwa na haikujulikana aliyefanya kazi hiyo.
Alisema kijana huyo na wenzake waliamini kwamba waliofanya kazi hiyo ni wachawi.
Akisimulia kisa kingine, Enock alisema siku chache zilizopita kuna msiba ulitokea kijijini hapo na baada ya mazishi, siku iliyofuata walikuta msalaba umeng’olewa na haujulikani ulipo, jambo ambalo pia lilihusishwa na ushirikina.
Ofisa mtendaji wa kijiji hicho, Ogen Gasper aliyeomba Serikali kujenga kituo cha polisi kijijini hapo, alisema baada ya kupata taarifa za tukio hilo alifanya jitihada kubwa kuwapata askari, lakini hawakufika kwa kilichodaiwa ni kukosa usafiri.
Gasper alisema hilo ni tukio la tatu kwa watu kuuawa kwa kutuhumiwa kuwa ni wachawi, la kwanza likiwa limetokea mwaka 1996.
Mwananchi
Viewing all 45912 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>