Quantcast
Channel: VIJIMAMBO
Viewing all 45912 articles
Browse latest View live

2014 Alabama Mana Conference


RAIS DK. SHEIN AMFUTA KAZI MWANASHERIA MKUU SMZ NA KUMTEUA MWANASHERIA MPYA

$
0
0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein amemteua Mh. Said Hassan Said kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa leo na Katibu wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee, Dkt Shein amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu 55(1) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.

Mheshimiwa Said Hassan anachukua nafasi ya aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mh. Othman Masoud Othman ambaye Uteuzi wake umefutwa kwa mujibu wa Vifungu vya 53, 54 (1) na 55 (3) vya Katiba ya Zanzibar ya 1984 na Kifungu 12(3) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Namba 2 ya 2011.
Kabla ya Uteuzi huo Mheshimiwa Said Hassan Said alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Uteuzi huo umeanza tarehe 07, October, 2014

MBUNGE WA KAWE CHADEMA ALALA SEGEREA BAADA YA KUSHINDWA MASHARTI YA DHAMANA

$
0
0
Mbunge wa Kawe na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Halima Mdee na wenzake tisa wamepelekwa katika Gereza la Segerea jijini Dar baada ya kushindwa kutimiza baadhi ya masharti ya dhamana yao.
Mdee na wenzake nane mapema leo walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar na kukana tuhuma zinazowakabili.
Mdee na wenzake hao wanashitakiwa kwa makosa mawili kototii amri za maofisa wa polisi na kufanya maandamano kinyume na sheria Jumamosi iliyopita ya Oktoba 4, mwaka huu.
Watapandishwa tena kizimbani hapo kesho saa 4 asubuhi.

MENINAH NA DIAMOND TUMEONA MOSHI TUNGOJEE MOTO

$
0
0
Meninah
habari mpya zinasema kuwa vikao vya harusi ya Diamond na Meninah ambaye ni mwanamuziki wa Bongo fleva vimeanza kimya kimya nyumbani kwa mama Diamond huku mmoja wa wahudhuriaji wakiwa ni mama Diamond mwenyewe na Queen Darling ambaye ni dada wa Diamond.
Kwa mujibu wa Baabkubwa magazine paparazzi wake alienda nyumbani kwa Diamond hivi juzi kati kufanya nae mahojiano hata hivyo hakumkuta Diamond lakini alimkuta mmoja wa watu wake wa karibu ambaye yupo pia upande wa Wema Sepetu. 
Chanzo hicho kilimwaga news kuwa hakuna cha ndoa ya Diamond na Wema bali ndoa inayopangwa kwasasa ni ya Diamond na Meninah na vikao vimeanza kwa mama Diamond. Chanzo hicho kilisema kuwa Diamond na Meninah walikutana takribani miezi mitano iliyopita wakati wa maandalizi ya tuzo za Kili Awards 2014 ambapo wote walitumbuiza. Baada ya hapo wakaingia mapenzini kimya kimya mpaka wiki za hivi karibuni gazeti moja lilipovujisha habari hizo za mahaba ya Diamond na Meninah na media nyinmgine kuziandika kwa kasi.
Meninah
Kwa mujibu wa chanzo hicho ni kuwa Wema ametoswa sababu ya kuendekeza pombe inayompelekea kuwa mvivu na kutotaka kufanya kazi badala yake ni starehe tupu, kwa maana kuwa hata nyumbani kwa mama Diamond haendi mara kwa mara kumsalimia inaweza hata kupita miezi 3 hajaenda ila Meninah anaenda na akifika kule humsaidia mama Diamond kazi, kupika na kupakua. Chanzo hicho kimesema kuwa hata Wema anajua kuwa Diamond na Meninah wana ishara zote za kuwa wapenzi lakini hana cha kufanya, huku Meninah yeye akiwa tayari amejitoa muhanga kwa Diamond lakini anawaogopa Team Wema kumshambulia hasa kwa mvua za matusi kama ilivyo kawaida yao lakini mama Diamond anampoza kuwa asiwe na shaka yeye kamkubali Diamond hawezi kukataa kumuoa hilo amuachie yeye mama Diamond.

Vikao hivyo licha ya kuhudhuriwa na mama Diamond na Queen Darleen, chanzo hicho kimesema pia kuwa kuna ndugu wengine wa Diamond na mama Diamond wanahudhuria ila yeye hawajui sababu hana ukaribu nao. 
Wema na Diamond

KAMA UREMBO NIKUOLEWA BASI HAWA WASHINDWE WENYEWE KUPATA WAUME KWANI NI WAREMBO HASWA.

$
0
0

Hamisa Mobeto
Meninah Abdulkareem

Hamisa Mobeto
Lulu Michael
Pitia  picha za warembo hawa watatu na utakubari kuwa wanaurembo na kama wanatulia na kuolewa basi mume hawezi kuchelewa kurudi nyumbani.


Meninah Abdulkareem
Add caption
Lulu Michael
Hamisa Mobeto
Lulu Michael
Meninah la Diva

KWA NINI WAGANGA WANAWEZA KUWASAIDIA WATU KUWA MATAJIRI WAKATI WAO NI MASIKINI?

$
0
0
Kuna watu ambao wanapata mafanikio makubwa kwa kutumia uchawi. Ila mafanikio yale hayaletwi na uchawi bali imani ya mtu husika. 

Tutajadili kwa nini waganga wanaweza kuwapatia watu wengine dawa au mbinu za kuwa matajiri wakati wao ni masikini. Na pia tutaangalia jinsi ambavyo unaweza kutumia mbinu hizi wanazotumia waganga bila ya wewe kuwa mchawi na ukafikia mafanikio makubwa.
Kila mmoja wetu anaelewa kwamba kuna watu wanakwenda kwa waganga na wanasaidiwa kupata utajiri. Japokuwa utajiri huu haudumu, lakini angalau wanaupata kwa kiwango fulani. 

Wakati waganga hawa wanawasaidia watu kuweza kujenga magorofa, wao bado wanakaa kwenye vibanda vya nyasi. 

Sasa kwa nini wao wasingetumia uchawi wao na kuwa matajiri zaidi ya hao wateja wao? Ina maana wao hawapendi utajiri huo? 

Mbinu za waganga kuwasaidia watu kupata utajiri. 
Watu wanaokwenda kwa waganga ili kupata utajiri au mafanikio yoyote hupewa masharti ambayo ni magumu kwa kiasi fulani. 

Na watu hawa huambiwa wakivunja masharti hayo tu utajiri wao unaisha mara moja. Ni masharti haya ambayo humjengea mtu nidhamu kubwa sana na kumfanya aweze kufanya kazi kwa juhudi kubwa kuliko wengine ambao wanafanya anachofanya. 

Kwa mfano mganga anamwambia mtu kila siku aamke asubuhi na mapema sana na apasue nazi barabarani ndio aende kwenye biashara zake. 

Kupasua nazi hakuna uhusiano wowote na mafanikio yake ila kuamka asubuhi na mapema kila siku ina msaada mkubwa kwenye mafanikio yake. 

Hivyo mtu huyu atafuata masharti haya kila siku na hata kama kuna siku hajisikii itambidi afanye tu kwa sababu ameshaaminishwa akiacha atafilisika. 

Sasa wewe ambaye huna sharti la aina hii siku ukiwa hujisikii vizuri unalala, siku nyingine unachelewa na hivyo kushindwa kufikia mafanikio makubwa. 

Masharti mengine kama kutokufanya starehe, kutokunywa pombe, kuvaa nguo moja na mengine mengi yanapelekea mtu kupunguza matumizi na kupata muda mwingi wa kufikiria kazi au biashara yake. 

Masharti mengine yanayotolewa na waganga ni kumfanya mtu aweze kuondoka kwenye woga wake(comfort zone). Kila mmoja wetu kuna vitu fulani anaogopa kufanya, lakini vitu hivi ndio vinaweza kumletea mafanikio. 

Ili kukuondolea woga huu mganga anamfanya mtu afanye jambo kubwa sana ambalo litamuondolea woga kabisa. 

Kwa mfano mtu anaambiwa aue, kwa kuona kwamba ameweza kuua mtu, inamfanya mtu asizuiwe na kitu chochote. 

Kikubwa ambacho mganga anamsaidia mtu ni kumjengea utaratibu ambao lazima kila siku ataufuata na pia kumjengea nidhamu binafsi na hivyo kuweza kufanya jambo hata kama hajisikii kufanya. Na hili ndio hitaji kubwa la kuweza kufikia mafanikio. 

Kwa nini waganga hawawezi kutumia mbinu hii wenyewe.? 
Kwa sababu wanajua inavyofanya kazi na pia hawana mtu wa kuwajengea imani hiyo kubwa kwao wenyewe. 

Kwa nini watu baadaye hufilisika? 
Wengi hufilisika baadae kwa sababu wanapopata mafanikio wanasahau kutumia yale masharti waliyopewa na pia imani yao inakuwa imewekwa kwenye vitu fulani(mfano hirizi) badala ya kuwa kwao wenyewe. 

Ufanyeje ili uweze kutumia mbinu hii kufikia mafanikio. 
Cha kwanza kabisa lazima ujijengee nidhamu binafsi. Jiwekee masharti yako ambayo utayafuata kila siku na hakikisha unayafuata. 

Kwa mfano weka utaratibu kwamba kila siku utakuwa unaamka saa kumi asubuhi, kuipanga siku yako na kisha kujisomea kidogo. 

Baada ya hapo unawahi kwenye eneo lako la kazi au biashara na kuanza kazi zako mapema. Pia unaweza kujiwekea utaratibu kwamba kila mteja au mtu yeyote unayekutana naye kwenye siku husika atajisikia vizuri kukutana na wewe. 

Fuata masharti haya kila siku na utaona mabadiliko makubwa kwenye maisha yako na shughuli zako. 

Kwa hiyo mpaka sasa una mbinu mbili za uhakika za kufikia mafanikio; 
1. Una uwezo mkubwa uko ndani yako, ila unatakiwa kuwa na imani kubwa sana kwamba unaweza kupata kile unachotaka. 

2. Lazima uwe na nidhamu binafsi, uwe na masharti(rituals) na uwe na utaratibu wa kufanya kila siku (routine). Vitu hivi jiwekee mwenyewe na vifuate kila siku kwenye maisha yako. 

Ukiweza kufanya mambo hayo mawili ni lazima utafikia mafanikio makubwa. 

Nakutakia kila la kheri katika kufikia mafanikio. Kumbuka unaweza kufanikiwa kwa kiwango kikubwa sana bila ya kutumia uchawi au kwenda kwa mganga.Uchawi kamili upo kwenye kichwa chako. Anza kuutumia sasa.

MTOTO WA MILLIONI 50 MWANAAFA BAADA YA KUNYAKUA MILIONI 50 AUAMUA KUHAMIA DAR

$
0
0

Mwanaafa anasema kuwa kampuni ya Proin Promotions imemjengea mazingira mazuri ya kuishi kama nyota hivyo hata kama anapasi mtihani wake atahamia hapa kwani kazi ya kurekodi filamu ambayo ndio kazi anayoamini si rahisi kuifanya Mtwara, filamu ya TMT movie imeanza kurekodiwa na kinara ni Mwanaafa.
Mshindi wa shindano la kusaka vipaji la lillojulikana kwa jina la Tanzania Movie Talent (TMT) Mwanaafa Mwinzago, msanii huyo ambaye kwa sasa anaishi jijini Dar es Salaam baada ya kujinyakulia milioni 50, anasema kuwa anafanya mipango ya kusoma Dar es Salaam na si Mtwara tena. 
“Nilirudi Mtwara kwa ajili ya kufanya mtihani wangu wa darasa la saba, na nimerudi Dar tena kwa ajili ya kurekodi filamu ya TMT Movie, siwezi tena kurudi Mtwara nitasoma hapahapa tu,”anasema Mwanaafa.

UZINDUZI WA SHINA JIPYA LA CCM NDANI YA JIJI LA VIONGOZI WICHITA, KANSAS

$
0
0
Mratibu wa Matawi ya CCM Marekani Loveness Mamuya aliwaomba wanaCCM Wichita wawe mfano bora Kwa kujitokeza kwenye jumuiya ya TaWichita kwani Jumuiya ni kwanza na kuwaomba waweze kupendana na kushirikiana kwanza kama watanzania. Tumefungua matawi tukiwa na niya ya kukutanisha watanzania ili waweze kuchangia maendeleo ya Nchi yetu. Chama Cha Mapinduzi kinatambuwa jamii ya watanzania na ushirikano wao. Pia aliwaomba watu wajiunge na jumuiya kwanza na kushirikiana kwa karibu na vilevile kukemea kujiunga na CCM bila ya kujiunga na jumuiya zetu kwani Watanzania lazima tuheshimiane katika makundi ya siasa bila kujali umetoka chama kipi bali zaidi tubishane kwa hoja
Mwenyekiti wa Shina la Wichita Patrick Mbezi
Katibu wa Shina Ndugu Cyprian Mayemba Akisema Machache Kwenye Ufunguzi
Kutoka Kushota - Katibu wa Shina la Oklahoma Edgar Chiwanga, Mwinyekiti wa Shina la Patrick Mbezi na Ndugu Moses Hosea
Mwenyekiti wa Shina la Oklahoma Emmanuel Kamala akipata Ukodak na MwanaCCM wa Wichita Anna Mambali
Mwenyekiti wa Shina la Oklahoma Emmanuel Kamala, Felix Mgimwa na Mratibu wa Matawi CCM Loveness Mamuya


Mwenyekiti wa Shina la Oklahoma Emmanuel Kamala akipata Ukodak na MwanaCCM wa Wichita Moses Hosea 
Mwenyekiti wa Shina la Oklahoma Emmanuel Kamala akipata Ukodak na MwanaCCM wa Wichita 
Mwenyekiti wa Shina la Oklahoma Emmanuel Kamala akipata Ukodak na MwanaCCM wa Wichita
Mwenyekiti wa Shina la Oklahoma Emmanuel Kamala akipata Ukodak na MwanaCCM wa Wichita Bwimbo Kajanja aka Mambo ENT.
Mwenyekiti wa Shina la Oklahoma Emmanuel Kamala akipata Ukodak na Raisi wa Jumuiya ya Watanzania Wichita Zai Mipawa












Homeless Kenyan man in US appeals for help to return

$
0
0
A man who has lived in North America for 46 years now says he has had enough and would like to come back to Kenya to be with his family.

Timothy Majanja, 67, left Kenya for Canada in 1968 and now lives in squalor in the United States after losing his job 21 years ago.

Speaking to the Nation in Atlanta on Thursday, Mr Majanja said he moved to the state of Georgia in the United States in 1993.

“I have been leading a miserable life here and it is high time I left this country,” he said in an interview on Memorial Drive in Atlanta, Georgia.

Mr Majanja, however, said he is stuck because he lost all his documents and cannot travel.

He appealed to the Kenyan Government, through the Ministry of Foreign Affairs, to help him out.

POLITICAL OFFICE

In 1973, he said, he was recruited by the Canadian government into the prestigious Royal Canadian Mounted Police, where he served before venturing into politics.

He run for political office as a city representative in Calgary, Alberta, before unsuccessfully contesting a vacant mayoral seat.

Mr Majanja, however, declined to disclose when or why he left the Canadian police service.

“That matter is confidential,” he said.

After relocating to Atlanta, he worked for a transport company before losing his job.

“I lost my driver’s license and all the other documents which I had kept in a safe deposit at a local bank,” he said.

Mr Majanja said he has sought help several times from the US and Canadian governments without success.

“I have no single document and can’t travel anywhere,” he said, adding, “I appeal to the Kenyan embassy to give me some travel documents so I can visit my relatives back home.”

MARRIED TO CANADIAN

During the interview with the Nation, he showed photos of his sojourn in Canada in which he looked young and energetic.

“I married a Canadian lady and we had a son, but now I can’t even travel there to visit them,” he said.

“I thought I was strong enough, but now I need help,” added Majanja, who looked weak and a pale shadow of his former self.

Though hardly reported due to the stigma associated with homelessness, drug addiction or mental illness, cases of destitute Kenyans living in the United States have risen in recent years.

In 2012, the body of a homeless Kenyan was discovered in a lake near Boston, Massachusetts.

Early this year, police in Atlanta found a homeless and mentally unstable Kenyan man in a forest in Decatur, Georgia.

The authorities handed the man over to the pastor of a Kenyan community church who asked the congregation to raise money for his upkeep and eventual repatriation to Kenya.

In May, he was reunited with his family in Kenya.

By BMJ Murithii

LOOK OF THE DAY

WIMBO WANGU WA LEO

MENINAH AMWANIKA DIAMOND TENA!! AFUNGUKA MENGI KUHUSU MAHUSIANO YAO,AELEZA JINSI WEMA ALIVYO MPA PRESHA

$
0
0
Kwa mara ya kwanza tangu wadaiwe kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Meninah a.k.a Meninah la diva na Nguli wa Bongo Fleva nchini Nasib Abdul 'Diamond' hatimaye ukweli umepatika baaada ya kuzinasa meseji za meninah alizofunguka kususu mahusiano yake na Diamond.
Meseji hizo zimenaswa kutoka kwenye simu ya Meninah ambaye alikuwa akichati naye kuhusu mwenendo mzima wa Mahusiano yake na Diamond kupitia "Chating" hizo Meninah amekiri kwamba Diamond alimtaka kimapenzi na alifikia hatua ya kujitambulisha nyumbani kwao kwa nia ya kumuoa lakini alimtolea nje kwa sababu tayari alikuwa na mchumba mwingine na alishavishwa pete.
Aidha, Meninah aliendelea kubainisha kwamba Diamond alianza kulifukuzi penzi lake toka 'Long time' toka alivyokuwa na mpenzi wake Nasri, Diamond aliendelea kupiga Nyayo Nyumbani kwao kila siku
"Alikuwa akinisumbua toka niko na mpenzi wangu Nasri mpaka nimeachana naye mpaka leo ananitaka"Alifunguka Meninah katika moja ya meseji hizo
aliendelea kufunguka na kusema kuwa Diamond alionyesha hisia zake kwa kupeleka taarifa kwenye moja ya magazeti ya udaku kwa minajili ya kumlegeza ili akubali kuwa mpenzi wake.
"Sasa yeye(Diamond) akadhani kwamba anitoe kwenye magazeti labda mimi nitaogopa then nitajikuta niko nae, mimi Diamond simtaki.....akaa...kwanza wa nini!"
Hata hivyo Meninah aliitaja sababu nyingine ya kumpiga chini Diamond akisema kwanza tayari yuko na Wema na mimi Wema nam-respect halafu nimevishwa pete na mchumba wangu nimsaliti yanini ninayempenda.....
akangeza na utani"Domo lake lile nitalipeleka wapi he is not even cute.......we can't match."Habari ndiyo iyo!!!"

HAPPY BIRTHDAY

$
0
0
Asya Mwilima wa New York City.
May your day be as joy-filled and wonderful as it can possibly be. Vijimambo team wish you happy birthday.

TANZANIA UHURU NIGHT WASHINGTON DC DEC 6 ..#ELEGANT SETTINGS

$
0
0

FEATURING LIVE PERFORMANCES FROM THE BIGGEST ARTISTS FROM EAST AFRICA, HOSTED BY ..............
#TegaSikio..


TANGAZO LA CHANJO YA MAFUA MAKALI KUTOKA KAMATIYA AFYA DMV

$
0
0

KAMATI YA AFYA  DMV
INATUKUMBUSHIA KUCHUKUWA  TAHADHARI KWA MAFUA MAKALI KWA KUPATA CHANJO YA MAFUA  SASA
Mafua/influenza (Flu) ni ugojwa wa kuambukiza (contagious disease) ambao husambaa hapa marekani wakati wa masika kati ya mwezi wa 5 na mwezi wa 10 .Mafua haya husababishwa na virusi vilivyo katikavya kundi la Influenza
1. Influenza A (H1N1),
2. Influenza A (H3N2)
3. Influenza B.
Maambukizi ya   Ifluenza A & B hupatikana pale unapokuwa karibu na mtu mwenye flu kupitia kukohoa, chafya au kugusana kwa karibu.Yashauriwa kuosha mikono mara kwa mara ili kupunguza maambukizi .Chanjo ya mafua (Flue shot) ni  mchanganyiko wa aina tatu za chanjo(Trivalent vaccine) ambazo hukinga watu dhidi ya virusi vya influenza .
DALILI ZA FLU
  • Homa 100F
  • Mafua,chafya,kukwaruza kwa koo
  • Maumivu ya kichwa,mwili,viungo
  • Uchovu wa mwili
  • Kichefuchefu,kutapika hata kuharisha
FAIDA YA CHANJO
a) Kukinga mwili na ugonjwa wa mafua makali / influenza (“Flu”)
b) Kupunguza Makali au kukinga kuambukiza mafua kwa watu wengine
NANI ALIYE HATARINI ?
  • Watoto (chini ya umri wa miaka mitano)
  • Wazee (miaka 65 na Zaidi)
  • Wagonjwa wenye kinga hafifu za mwili
  • Wanawake Wajawazito
  • Wafanyikazi wa vitengo vya afya
  • Watu wenye kusumbuliwa na magonjwa ya kisukari, asthma, shinikizo la damu, na sarakani.
CHANJO YA MAFUA BURE AU KWA BEI NAFUU HUPATIKANA HAPA.
Weka appointment kupitia: montgomerycomd.gov. Search flu shot location, select: flu clinic appointments 2014.
  • October 20, 2014 from 4 to 8 pm _Montgomery college: Rockville Campus, 9630 Gudesky Dr, Rockville MD 20850.  Giving shots for individuals 6 months of age or older by appointment only. FREE

  • October 31, 2014 from 9 am to 12 noon. Kennedy High school, Richard Montgomery high school and Seneca Valley high school for flu mist clinic by appointment only. Schedule appointments on at: Montgomerycomd.gov. Search flu shot location, select: flu clinic appointments 2014. FREE

  • November 3 and 17, 2014 from 1 pm to 4 pm. Silver Spring health center. 8630 Fenton st. Silver Spring, MD 20910: Schedule appointments on at: montgomerycomd.gov. Search flu shot location, select: flu clinic appointments 2014.FREE
  • November 17, 2014 from 8:30 am to 11:30 am – Germantown Health center.12900 Middlebrook Rd, Germantown MD 20874.
  • Muslim community clinic (MCC). Clinic ipo New Hampshire ave towards north kwenye majengo ya msikiti.
NOTE: Sehemu ambazo huduma sio bure unaombwa uje na health insurance kadi yako na wale wasio na Health Insurance kutakuwa na chaji ya $20 kulingana na MD kipimo cha umaskini ( MD state poverty sliding scale).
                            ILI TUSONGE MBELE, AFYA KWA WANADMV KWANZA !

Ref./Thanks
http://www.cdc.gov/flu/about/disease/symptoms
images


SHUKRANI ZA DHATI KWA WENYEJI WA NORTH CAROLINA, DICOTA, NA WAGENI WOTE WALIOHUDHURIA

$
0
0

JUMUIYA YA WATANZANIA DMV INAPENDA KUTOA SHUKURANI ZA DHATI KWA UONGOZI WA WENYEJI WA NORTH CAROLINA,  DICOTA, WAGENI RASMI NA  WOTE WALISHIRIKI KULETA MAFANIKIO MAKUBWA KATIKA MKUTANO WA DICOTA 2014.

TUNASHUKURU KWA UPENDO WENU WA DHATI, HUDUMA YA HALI YA JUU NA ELIMU KUBWA TULIYOIPATA.
TUMENUFAIKA NA KUJIFUNZA MENGI NA KUTUPATIA CHANGAMOTO YA KUSONGA MBELE
PAMOJA TUNAWEZA NA TUTAFIKA
ASANTENI SANA
UONGOZI WA JUMUIYA DMV  

TANGAZO LA KISOMO.

$
0
0


Familia ya Bi Hamida Majili, inapenda kuwakaribisha kwenye shughuli ya kisomo 

(Hitima) cha marehemu Zubeda Majili ambaye ni mamake mzazi, Bi Hamida 

Majili. Marehemu alifariki tarehe 31.08.2014 na kuzikwa huko nyumbani kwao 

Handeni, Mkoa wa Tanga.

Shughuli hii ya Kisomo, itafanyika siku ya Ijumamosi tarehe 11.10.2014 kuanzia 

saa 10.00 jioni hadi saa 2.00 usiku. 
Anwani 
14212 Long Green Drive
Silver Spring, MD 20906

Kama ilivyo ada, tunawaomba Watanzania na wanajumuia wote wa hapa DMV 

tujumuike kwa pamoja katika kumuombea marehemu kwa mwenyezimungu na 

kuwaombea wote waliokwishatangulia mbele ya haki. 

Kwa taarifa zaidi, wasiliana na wafuatao hapa chini:

1. Hamida Majili- 301-221-6630

2. Fatima Melbourne-202-329-7320

3. Hassan Mweyungu-718-810-3397

4. Mayor Mlima- 301-806-8467

5. Hilder Kivembele-301-467-5290

6. Lilian Mabundo-301-213-7329

 WOTE MNAKARIBISHWA!

HASSAN MAAJAR TRUST FUNDRAISING EVENT

$
0
0

he Hassan Maajar Trust will be having their Annual Fundraising Event on Friday 31st October 2014 at the VIP Diamond Jubilee Hall.



As an ardent supporter of the Hassan Maajar Trust we once again count on you to post our attached poster on your well read blog.


We appreciate your support for the ' A Desk for Every Child Campaign'.

Kind regards,
Diana

KAJALA WEMA WATOANA JASHO POLISI

$
0
0

Mwigizaji Kajala Masanja ‘Kay’.

Stori: Waandishi Wetu
Kufuatia matusi ya mama wa staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu, Miriam Sepetu kwenda kwa mwigizaji Kajala Masanja ‘Kay’, mastaa hao wamejikuta wakitoana jasho kwenye Kituo cha Polisi cha Kijitonyama almaarufu Mabatini jijini Dar mwishoni mwa wiki iliyopita.
DURU ZA ‘KIUBUYU’
Duru za ‘kiubuyu’ zilidai kwamba Kajala, baada ya kuchoshwa na matusi hayo ambayo yalianzia kwenye sherehe ya kuzaliwa kwa Wema, alijikuta akiishiwa na uzalendo kisha kuingia mzigoni ili kukomesha matusi hayo kwenye mitandao ya kijamii.

MATRIDA MBARONI
Ilidaiwa kwamba, Kajala akiwa na timu yake (Team Kajala) alifanikiwa kumtia mbaroni dada mmoja aliyetajwa kwa jina la Matrida akidaiwa kwamba ni mfuasi wa Wema (Team Wema).
Ilisemekana kwamba Matrida anayetumia jina la ‘Mat Kiboko Yao’ kwenye ukurasa wake wa Instagram ndiye ambaye amekuwa akiongoza jahazi la kumtusi Kay.

Ilizidi kunyunyizwa kwamba sakata hilo la kuanikwa Instagram lilianza siku mbili baada ya ile pati ya kuzaliwa ya Wema ambapo Mat Kiboko Yao alimtukana Kajala matusi ya nguoni (hayaandikiki gazetini) kupitia ukurasa wake kwenye mtandao huo.

KAJALA ACHOKA, AKIMBILIA POLISI
Ilidaiwa kwamba Kajala alipoona amechoka kutukanwa, alitafuta wataalam ili kujua namna ya kumkamata na alipomjua ndipo akakimbilia Kituo cha Polisi cha Mabatini kwenda kutoa taarifa.
RB

Staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu.

Gazeti hili lilifanikiwa kunasa namba ya jalada la kesi hiyo iliyosomeka KJN/RB/8854/2014-MATUMIZI YA MATUSI MTANDAONI.

Ilisemekana polisi walitumia mbinu zao na kufanikiwa kumkamata Mat Kiboko Yao na kumweka nyuma ya nondo za mahabusu kituoni hapo ndipo sarakasi za pande mbili zikaanza.

KWANZA
Mara tu baada ya Mat Kiboko Yao kukamatwa mishale ya saa 2:00 usiku, taarifa zilisambaa kama moto wa kifuu ndipo Team Wema ikaingia mzigoni kutaka kumtoa mwanadada huyo lakini wakagonga mwamba.

WEMA, PETIT MAN WATINGA MABATINI 
Ilidaiwa kwamba, baada ya Mat Kiboko Yao kutiwa mbaroni, Wema na jeshi lake akiwemo Petit Man walitinga Mabatini kwa ajili ya kumtoa mwanadada huyo lakini aligonga mwamba na kumuacha akilala kituoni hapo.

“Yaani ulikuwa ni usiku wa kutoana jasho na kupimana ubavu kwamba nani ni nani. Ilikuwa akitoka Kajala kuhakikisha kwamba mtuhumiwa wake aachiwi, Wema naye anatinga kituoni kwa mbwembwe kutaka Mat Kiboko Yao aachiwe kwa gharama yoyote.

“Hapo ndiyo ngoma ilikuwa nzito, kila mmoja alikuwa anamuonyesha mwenzake kuwa ni zaidi na ni maji marefu hadi kulipokucha muvi likaendelea,” alisema shuhuda aliyefuatilia sakata hilo kinagaubaga.

Mama wa staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu, Miriam Sepetu.

WAANDISHI WAPEWA UBUYU, WATINGA MABATINI 
Kulipokucha, waandishi wetu walipewa ubuyu huo ndipo wakatinga Mabatini kisha wakatega ‘rada’ zao na kuweka doria.

Wanahabari wetu, wakiwa kituoni hapo walimshuhudia Kajala akilinda kituoni hapo asitokee mtu yeyote akamtoa Mat Kiboko Yao.
Hata hivyo, alipoulizwa Kay kulikoni kuwa eneo hilo alisema alikuwa ameitwa kwa ajili ya kusuluhishwa badala ya kupoteza muda kwa jambo kama hilo.

KAJALA NA KUNDI LAKE
Awali Kay alionekana akiingia kituoni hapo na kundi lake la watu watatu akiwemo mwanaume mmoja ambapo yeye aliingia mpaka kwenye chumba cha mkuu wa kituo.

Kajala akiwa kwa mkuu wa kituo, haikujulikana kilichokuwa kikiendelea ndani kwani kulikuwa na kikao cha muda mrefu ambapo ghafla Kajala na mtuhumiwa wake waliyeyuka.

WEMA AINGIA MITINI
Wakati hayo yakiendelea kituoni hapo, si Wema wala jeshi lake waliofika kwa ajili ya kumtetea Mat Kiboko Yao ambaye ndiye kiongozi wa Timu Wema kwa kutukana.

Hata hivyo, baadaye alionekana mmoja wa marafiki wa karibu ambaye ni ndugu wa Mat Kiboko Yao aliyekuwa akihaha kumtoa mwenzake.

TUJIKUMBUSHE
Hivi karibuni Mama Wema alimtolea uvivu Kajala na kumtusi ndipo akafufua upya kile kidonda cha Sh. milioni 13 ambazo Wema alimlipia Kay asiende jela na kinachoonekana, bado fedha hizo ni tatizo kubwa.

Imeandaliwa na Hamida Hassan, Imelda Mtema, Mayasa Mariwata na Shani Ramadhani.
Credit:GPL

KINANA ATOA WITO KWA VIONGOZI KUFANYA MIKUTANO NA WANANCHI NA KURHUSU MASWALI YANAYOHUSU MAENDELEO YAO

$
0
0

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wakazi wa Kilolo Mnadani waliojitokeza kumlaki katika ziara yake wilayani Kilolo.

MBUNGE wa jimbo la Kilolo mkoani Iringa Profesa Peter Msolla akiwasalimia wananchi wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kufyatua matofali ya kikundi cha vijana cha Muungano ambacho kina jumla ya vijana arobaini waliopata mafunzo ya kufyatua matofali na ujenzi.

  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongea na wajumbe wa halmashauri kuu ya wilaya ya Kilolo katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Kilolo.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kijiji cha Utengule kata ya Ihimbo ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa uchaguzi wa Serikali za mitaa mwezi Desemba CCM itashinda kwa kishindo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi  wa kijiji cha utengule kata ya Ihimbo wilaya ya Kilolo mkoani Iringa ambapo aliwaambia viongozi wa Kata na Vijiji pamoja na ngazi ya wilaya wafanye mikutano na wananchi wao na waruhusu maswali ilikujua changamoto zinazowakabili wananchi .
 Mwenyekiti wa Kijiji cha Utengule Ndugu Pancras Mkakatu ambaye ni mwanachama wa Chadema akiongea na wananchi mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambapo  alimpongeza sana Katibu Mkuu wa CCm kwa kazi nzuri anayofanya na kueleza kuwa yeye ni CCM ila alitoka tu kwa sababu ya migongano na viongozi wengine wa CCM .
 Zahanati ya Kijiji cha Utengule ambayo imekamilika ilabado haijapata madaktari
 Mwenyekiti wa Kamati ya ujenzi wa shule ya sekondari ya Uwindi Ndugu Charles Kigwile akiuliza swali linalohusu ujenzi wa madarasa ya shule hiyo ambao umesimama.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhiwa mkuki kama ishallah ya kuwa Mtemi wa Wahehe.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwashukuru wananchi wa kijiji cha Utengule kwa kumpa heshima ya kuwa Mtemi kwenye kijiji chao
 Katibu Mkuu wa CCM akiwa kwenye picha ya pamoja na Watemi wenzake wa kijiji cha Utengule.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwaaga wananchi waliofurika kwa wingi kwenye mkutano wake.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipeana mikono ya kwa heri na wananchi wa kijiji cha Utengule.
Mwalimu Josephine Konga wa Shule ya msingi akimuonyesha  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana uchache wa vyumba vya madarasa katika shule hiyo kiasi kupata shida sana katika kufundisha.
Viewing all 45912 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>