Quantcast
Channel: VIJIMAMBO
Viewing all 45982 articles
Browse latest View live

Free Concert UMOJA Church: ASANTE Choir


UKISHIKWA, SHIKAMANA

$
0
0
 Juu na chini ni picha siku ya Jumatano Februari 4, 2015 siku 10 kabla ya Valentine penzi motomoto kutoka kwa Mr. Matope kwa kipenzi mke wake Miss T baada ya kumzawadi gari aina ya Range Rover Sports na kusherehekea miaka 13 ya ndoa yao wakiwa wazazi wa watoto wao wawili.


WAZIRI MKUU AZUNGUMZA NA VIONGOZI WA DINI JIJINI DAR

$
0
0
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza katika kikao cha viongozi wa dini cha mashauriano kilichofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam jana.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza katika kikao cha mashauriano cha viongozi wa dini kilichofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifafa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari jana. Kulia ni ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam ,Alhad Salum Musa.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa viongozi wa dini wa mashauriano uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam jana.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimsikiliza Waziri wa Katiba na Sheria, Dr. Asha Rose Migiro katika mkutano wa mashauriano wa viongozi wa dini uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere mjini Dar es salaam jana. 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na baadhi ya viongozi wa dini baada ya kuzungumza katika mkutano wao wa mashauriano uliofanyika kwenye kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam jana.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa dini mara baada ya umalizika kwa kikao chao kilichofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifafa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari jana.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

RAIS - AKUTANA NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA IRAN

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akimlaki na kisha kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran, Mheshimiwa Javad Zarif na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es salaam, Jumatano, Februari 4, 2015. 
PICHA NA IKULU
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Tanzania imesema kuwa dhamira yake ya kufungua balozi katika baadhi ya nchi duniani iko pale pale na itatekeleza mpango wake huo kwa kadri hali ya fedha na uchumi inavyoruhusu.
Aidha, Tanzania imesema kuwa itaendelea kushirikiana na Iran katika kupambana na kukabiliana na ugaidi duniani kwa sababu nchi mbili hizo, kama ilivyo dunia nzima, zinahitaji dunia tulivu na inayosaka maendeleo ya watu bila usumbufu na matishio ya ugaidi.
Mambo hayo mawili yamejadiliwa leo, Jumatano, Februari 4, 2015 katika mazungumzo kati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran, Mheshimiwa Javad Zarif.
Mheshimiwa Zarif amewasili nchini leo akitokea Burundi katika ziara ambayo pia imemfikisha Kenya, Uganda na Rwanda akifuatana na maofisa wa Serikali na kundi kubwa la wafanyabiashara wa Iran.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam, Rais Kikwete amemwambia Mheshimiwa Zarif kuwa Tanzania bado inakusudia kufungua ubalozi mjini Teheran, mji mkuu wa Iran, kama ilivyoahidi na kuwa itafanya hivyo hali ya kifedha na kiuchumi itakaporuhusu. Rais ametoa maelezo hayo kufuatia ombi la Waziri Zarif kukumbushia umuhimu wa kuwepo kwa ubalozi wa Tanzania katika Iran.
“Tunakusudia kufungua balozi katika nchi marafiki ambako kwa sasa hakuna balozi ikiwamo Jamhuri ya Kiislam ya Iran. Katika Afrika, kwa mfano, tunapanga kufungua balozi katika Namibia, Angola, Algeria na Ghana. Hizi ni nchi rafiki ambazo baadhi yake zimekuwa na balozi katika Tanzania tokea uhuru wetu. Mbali na Iran katika Asia, tunaangalia nchi kama Uturuki, Qatar na Kuwait na nyingine marafiki,”Rais Kikwete amemwambia Mheshimiwa Zarif.
Kuhusu mapambano dhidi ya magaidi, Rais Kikwete amesema kuwa ni muhimu kwa Tanzania na Iran kuwa na msimamo ulio sawa wa jinsi ya kukabiliana na ugaidi.
“Wakati wote, sote tunakabiliwa na matishio ya ugaidi na hivyo tunalazimika wakati wote kuwa macho na uwezekano wa mashambulizi ya kigaidi. Sisi Tanzania bado tunakumbuka shambulio dhidi ya Ubalozi wa Marekani hapa nchini. Ulishambuliwa Ubalozi wa Marekani lakini watu wote waliopoteza maisha yao ni Watanzania.”
Rais Kikwete na Mheshimiwa Zarif pia wamejadili jinsi gani Tanzania na Iran zinavyoweza kuongeza ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji katika maeneo mbali mbali ya uchumi na Rais Kikwete amemweleza Waziri fursa zilizoko katika sekta za nishati na reli.
Waziri Zarif pia amemkumbusha Rais Kikwete mwaliko wa kumwomba Rais Kikwete kutembelea Iran kwa ziara ya Kiserikali.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

RAIS MUGABE APIGA MUELEKA

$
0
0
Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) na Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe (90) amenaswa na kamera akiwa ameanguka wakati akielekea kwenye gari, muda mfupi tu baada ya kusalimia wananchi waliofika kumlaki katika Uwanja wa Ndege akitokea Ethiopia kwenye mkutano wa AU.

Rais Mugabe amekuwa akisafiri kwenda katika nchi za Asia kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake na tiba, hasa ya macho. Anatarajiwa kusherehekea sikukuu ya kuzaliwa tarehe 21 Februari.
Picha wa hisani ya Wavuti

KAMA KWELI UNAMPENDA UNAKUBALIJE KUMUACHA KIRAHISI?

$
0
0
Ninachotaka kukizungumzia leo ni kuhusu watu kuachana katika mazingira ambayo wengi wasingetarajia. Zipo ndoa ambazo zimefungwa kwa mbwembwe sana lakini hazikudumu na ukiuliza utaambiwa chanzo ni mambo madogomadogo tena ya kuvumilika.

Yapo ambayo kiukweli hayavumiliki kabisa. Kuna sababu ambazo ukitajiwa kuwa ndizo zilizosababisha flani na flani kuachana, utasema hata ingekuwa wewe usingeweza kuvumilia lakini kuna nyingine ukitajiwa utashangaa na hutaweza kuamini.

Kwa nini nasema hivyo? Ni kwa sababu unayempenda huwezi kukubali kuachana naye kirahisi.
Yapo mambo ya kuumiza na kukera ambayo mtu anaweza kukufanyia lakini kutokana na unavyompenda unavumilia na kuyaacha yapite.

Hicho ndicho kinachotakiwa kufanyika. Tufahamu kwamba mapenzi ni kitu cha kuwa nacho makini sana. Yapo mengi yatatokea, yapo mengi utaambiwa kuhusu mpenzi wako lakini kikubwa ni wewe kupima kisha kutokuwa na papara ya kumuacha.

Iko hivi, ukisikia wawili waliotokea kupendana mpaka wakafikia hatua ya kuoana wameachana kwa sababu ya kufumaniana, hutashangaa sana.

Na hii ni kutokana na ukweli kwamba usaliti ni sababu ya msingi inayosababisha wengi kuachana.
Mimi naweza kuvumilia na kutomuacha mke wangu baada ya kumfumania lakini uamuzi huo unaweza kuwashangaza wengi ambao huenda ingewatokea wao wangechukua uamuzi wa kuwaacha wapenzi wao.

Lakini ifahamike kuwa watu tunatofautiana, huenda mimi nina moyo tofauti wa kuchukulia mambo makubwa kuwa madogo.

Sitakiwi kuonekana mjinga kwa kufanya uamuzi huo kwani huenda inatokana na namna nilivyopenda na ninavyoweza kuchukulia usaliti huo kama njia ya kuboresha uhusiano wangu.
Lakini pia wewe unaweza kumuacha mpenzi wako kwa kumfumania na wengi wakaona umefanya uamuzi sahihi kwa kuwa wanajua madhara ya kusalitiwa na namna inavyouma.

Kwa maana hiyo sasa, mpenzi wako akikusaliti na ukamuacha hilo haliwezi kuwa suala la kuwashangaza sana watu lakini kile ninachokizungumzia mimi ni watu kuachana kwa mambo ya kijinga.
Mtu anapelekewa maneno ya uongo kwamba mume wake kaonekana maeneo f’lani na mwanamke, mke badala ya kuchunguza anakuwa mkali.

Anaamsha timbwili na wakati mwingine kuomba hata talaka. Mtu wa sampuli hii utaamini kuwa sababu hiyo ndiyo iliyofanya aombe talaka kweli?

Achilia mbali hao, wapo ambao waliachana kwa sababu eti mwanaume anahisi anasalitiwa. Eti kwa sababu huwa anamuona mke wake anawasiliana sana na mtu flani basi anahisi anaibiwa na bila kuchunguza anakuwa mkali, kutokuelewana kunatokea na mwisho kuachana.
Jamani, hisia tu zikufanye uamue kumuacha mwenza wako uliyeapa kudumu naye? Una uhakika gani na kile unachokifikiria? Watu wakidhani umepata kimwana mwingine ndiyo maana unatafuta sababu ya kumuacha huyo uliye naye watakosea?

Ifike wakati tuheshimu mahusiano yetu. Kama kweli umeamua kuingia kwenye ndoa na mtu uliyetokea kumpenda basi kamwe usikubali kuachana naye kirahisi.
Yapo ambayo yakitokea na ukaamua kumuacha watu hawatakuona ni mtu wa ajabu kwa sababu kibinadamu kila mmoja ataona una hoja lakini hili la kuachana kirahisi linaashiria aidha hukuwa na mapenzi ya kweli au umemchoka tu.

Ninachotaka kusema hapa ni kwamba, wanaopendana kwa dhati watavumiliana sana na pale itakapotokea wameachana basi ujue Mungu ndiye ameona iwe hivyo.
Kama uko kwenye uhusiano jaribu sana kuulinda kwa gharama zozote. Ziba masikio yako ili wambeya wasikupenyezee maneno ya kukuharibia lakini pia mvumilie mwenza wako katika yale ambayo yanavumilika.

Kumuacha siyo suluhu. Unaweza kumuacha huyu ambaye umemfumania lakini huwezi kujua huyo mwingine utakayempata itakuwaje.

Wapo waliowahi kuwafumania wapenzi wao wakawasamehe na leo hii wanaishi maisha mazuri. Kwa nini? Kwa sababu waliamini usaliti unaweza kuboresha uhusiano wao na ikawa hivyo.

Mimi nikutie moyo wewe ambaye umekuwa ukiumizwa sana na mpenzi wako ambaye unampenda. Najua mara kadhaa unajiwa na mawazo ya kutaka kuachana naye lakini wakati mwingine jaribu kuwa mvumilivu, ukiona maji yamekufika shingoni na unakoelekea ni hatari zaidi, hapo sasa ukiamua kujitoa wala hutakuwa umekosea.

GPL

MAPOKEZI YA RAIS WA UJERUMANI ZANZIBAR

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na mgeni wake Rais wa Ujerumani Mhe,Joachim Gauck mara alipowasili katika Bandari ya Malindi Mjini Zanzibar leo akitokea Dar es Salaam akiwa katika ziara ya siku moja Nchini akifuatana ma Mkewe Daniela Schadt pamoja na viongozi mbali mbali wa Nchi hiyo
Rais wa Ujerumani Mhe,Joachim Gauck akisalimiana na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi (katikati) mara alipowasili katika Bandari ya Malindi Mjini Zanzibar leo akitokea Dar es Salam akiwa katika ziara ya siku moja Nchini akifuatana ma Mkewe Daniela Schadt pamoja na viongozi mbali mbali wa Nchi hiyo (kulia) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein 
Rais wa Ujerumani Mhe,Joachim Gauck akiwasili shada la mauwa na mtoto Salma Issa mara alipowasili katika Bandari ya Malindi Mjini Zanzibar leo akiwa katika ziara ya siku moja Nchini akifuatana ma Mkewe Daniela Schadt pamoja na viongozi mbali mbali wa Nchi hiyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Rais wa Ujerumani Mhe,Joachim Gauck wakipokea salamu ya heshma ya Gwaride la Jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ ikiwa ni mapokezi ya Rais huyo wa Ujerumani mara alipowasili katika Bandari ya Malindi Mjini Zanzibar leo akitokea Dar es Salaam akiwa katika ziara ya siku moja Nchini akifuatana ma Mkewe Daniela Schadt pamoja na viongozi mbali mbali wa Nchi hiyo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Mgeni wake Rais wa Ujerumani Mhe,Joachim Gauck (kushoto) mara baada ya mapokezi alipowasili katika Bandari ya Malindi Mjini Zanzibar akitokea Dar es Salaam akiwa katika ziara ya siku moja Nchini (kulia) Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi

Dk Shein Akiwa na Mgeni wake Rais wa Ujerumani Mhe Joachim Ikulu Zanzibar

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na mgeni wake Rais wa Ujerumani Mhe,Joachim Gauck katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar alipofika na ujumbe wake leo akiwa katika ziara ya siku moja nchini,[Picha na Ikulu.]

Simanzi shuleni

$
0
0
Wanafunzi wawili waangukiwa na ukuta, wafa, Watatu wajeruhiwa, wakimbizwa hospitalini.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Kihenya Kihenya.

Wanafunzi wawili wa darasa la nne katika shule ya msingi ya Unity, iliyopo Chamazi, eneo la Mbagala, Manispaa ya Temeke, wamefariki dunia baada ya kuangukiwa na ukuta wa darasa la shule hiyo uliogongwa na gari.

Kadhalika, wanafunzi watatu wamejeruhiwa baada ya kijana wa kazi wa mmiliki wa shule hiyo, ambaye siyo dereva kujaribu kuendesha gari na kuparamia darasa hilo na sehemu ya ukuta kuwaangukia wanafunzi waliokuwa darasani wakiendelea na masomo.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Kihenya Kihenya, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa lilitokea Februari 03, mwaka huu, majira ya saa 2:30 asubuhi, na wanafunzi wawili wamefariki na watatu kujeruhiwa na kwamba mtuhumiwa wa tukio hilo anashikiliwa na jeshi la Polisi.

“Wanafunzi watatu wametibiwa katika hospitali ya Mbagala na wameruhisiwa baada ya kupata nafuu,” alisema.

Hata hivyo, Kamanda huyo alipotakiwa kutaja majina ya wanafunzi hao na mtuhumiwa huyo, alisema yupo nje ya ofisi hawezi kukumbuka majina yote.

NIPASHE ilifika eneo la tukio na kukuta geti la kuingia kwenye shule hiyo iliyopo kwenye eneo moja na nyumba ya mmiliki ambaye jina halijafahamika, na kuona ukuta ukiwa umeanguka.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo, walisema chanzo cha ukuta huo kuanguka ni kijana mmoja wa familia hiyo anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 25 hadi 30, ambaye ni mmoja wa wanafamilia ya nyumba hiyo, aliyeendesha gari aina ya Rav 4 ambalo liliparamia ukuta huo.

Mashuhuda hao ambao hawakutaka kutaja majina yao walisema, tukio hilo lilitokea majira ya saa 2:30 asubuhi, wakati wanafunzi hao wakiwa darasani.

“Nikiwa bafuni naoga nilisikia kishindo kikubwa, nilitoka kwa kasi hadi eneo la shule na kukuta ukuta umeanguka umelalia watoto, tulianza kuwaokoa na tulifanikiwa kuwatoa watano kati yao wawili walikuwa wamelaliwa na matofali na wana hali mbaya,” alibainisha na kuongeza:

“Tulijiuliza nini kilitokea na baadaye tulimuona kijana aliyeendesha gari akiwa ndani ya gari, tulimtoa akiwa hajitambui na gari imeharibika vibaya, tulimpepea hadi akazinguka, tuliwajulisha polisi na baadaye kupelekwa kituo kikuu cha polisi cha Kizuiani,”.

Baba wa mtoto wa kiume Isiaka Mketo (12), aliyefariki katika tukio hilo, Twaha Mketo, akizungumza na NIPASHE wakati wa maziko ya mwanaye, alisema alirejea nyumbani majira ya saa mbili asubuhi na kujisikia mwili mzito na baadaye aliingilia ndani na kupumzika, lakini ndani ya muda mfupi alipigiwa simu na mkewe kuwa mtoto anaumwa sana yupo hospitalini.

“Nilikwenda hospitali ya Zakhem na kuwakuta walimu ambao waliniita pembeni na kunieleza kuwa watoto watano waliangukiwa na ukuta na mwanangu na mwingine wa kike wamefariki…niliumia sana, nililia sana, lakini ndiyo limeshatokea nimelipokea na jana nimemzika mwanangu,” alisema.

Alisema walimu walimueleza kuwa wanafunzi walikuwa darasani gari likagonga ukuta wa darasa lao na ukuta kuwaangukia na kwa bahati mbaya wawili walifariki.

Mwanafunzi wa kike aliyefariki katika tukio hilo, amejulikana kwa jina moja la Kulthum, wa eneo la Charambe, Magengeni.

Akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina, mmoja wa majeruhi akiwa na mzazi wake katika mazishi ya Isiaka, alisema alikisia kishindo kikubwa na ghafla matofali yakawafukia kwa muda na kwa kuwa alikuwa pembeni kidogo alijeruhiwa kichwani.

“Watu walikuja haraka kutusaidia, nilimuona Isiaka akiwa amelala aliitwa, lakini hakuitika…nafikiri alishakufa,” alisema huku akibubujikwa na machozi.

Mkuu wa shule hiyo, alipotafutwa kwa simu iliita bila kupokewa na baadaye ilizimwa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi haukujibiwa na NIPASHE ilifika shuleni na kukuta ulinzi umeimarishwa.
CHANZO: NIPASHE

Polisi auawa akiokoa mtoto asiuawe na baba yake mzazi

$
0
0
Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, David Misime.

Askari Polisi PC Joseph Swai, ameuawa wakati akimwokoa mtoto wa miezi minane, aliyekuwa akiteswa na baba yake mzazi katika mtaa wa Chang'ombe Juu mjini hapa.

Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, David Misime, alisema tukio hilo lilitokea jana saa 5:00 asubuhi na kumtaja mtoto aliyekuwa anateswa kuwa ni Valerian Mallya.

Alisema awali, polisi huyo alipigiwa simu na Mtendaji wa mtaa wa Chang'ombe Juu, akimjulisha kuwa amepokea taarifa kutoka kwa Oliva Baltazar (52), kuwa kijana wake, Tisi Mallya (29), anamtesa mtoto wake.

Alisema polisi huyo alikwenda eneo la tukio na alipofika aligonga mlango huku akijitambulisha kuwa ni askari, kisha akamuamuru atoke nje.

Hata hivyo, alisema Mallya alimnyanyua mtoto wake huyo kwa mkono mmoja miguu ikiwa juu na kichwa chini, akitishia kumuua kwa panga.

Kamanda Misime alisema askari huyo aliamua kumwokoa mtoto huyo kwa kumrukia mtuhumiwa lakini aliteleza na kuanguka chini na ndipo mtuhumiwa huyo alipopata mwanya wa kumkata kichwani na maeneo mengine ya mwili.

Alifafanua kuwa mama na mwanawe walifanikiwa kutoroka bila kupata madhara yoyote.

Kamanda Misime alisema baada ya mtuhumiwa kufanya unyama huo, alikimbia akiwa ameshika panga lililokuwa limetapakaa damu na polisi wanaendelea kumtafuta ili afikishwe mbele ya vyombo vya sheria kujibu mashitaka yanayomkabili.
CHANZO: NIPASHE

Tanzania mwenyeji wa mkutano wa kimataifa wa Wahasibu

$
0
0
Mhasibu Mkuu wa Serikali,Mwanaidi Mtanda akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam kuhusiana na mkutano wa 22 wa kimataifa wa Chama cha Wahasibu Wakuu wa Serikali wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAAG) utakaofanyika nchini kuanzia Machi 09, hadi 12 mwaka 2015.
Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya mkutano wa 22 wa kimataifa wa Chama cha Wahasibu Wakuu wa Serikali wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAAG) ambaye pia ni Makamu Mhasibu Mkuu wa Serikali Azizi Kifile akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam (hawapo pichani) kuhusu mkutano utakaofanyika nchini kuanzia Machi 09, hadi 12 mwaka 2015.


Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Tanzania itakuwa mwenyeji wa mkutano wa 22 wa kimataifa wa Chama cha Wahasibu Wakuu wa Serikali wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAAG) utakaofanyika nchini kuanzia Machi 09, hadi 12 mwaka 2015.

Kauli hiyo imetolewa na Mhasibu Mkuu wa Serikali,Mwanaidi Mtanda kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile jana jijini Dar es salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na mkutano huo utakaofanyika nchini.

Mhasibu Mkuu wa Serikali Mwanaidi alisema kuwa mgeni rasmi katika mkutano huo anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete.

Katika mkutano huo, mada mbalimbali zinatarajiwa kujadiliwa zikilenga kwa lengo la kukuza ushirikiano miongoni mwa nchi wanachama katika masuala ya hesabu za serikali na kutoa fursa ya kuwa na jukwaa kwa ajili ya washiriki ili kufanya tathmini kwa kujadiliana na kushirikishana uzoefu mbali mbali.

Aidha, mkutano huo unalenga kuhamasisha maendeleo ya watendaji wahasibu wa Serikali na kutoa mafunzo stahiki kupitia utekelezaji wa program shirikishi kwa kujifunza uzoefu wa masuala mbali mbali ndani ya nchi wanachama.

Mkutano wa wahasibu hao unatarajiwa kuwa na washiriki zaidi ya 1000 wakiwemo Wahasibu wakuu 14 kutoka nchi wanachama na wadau wengine.

Ujio wa wageni hao pamoja na ushiriki wao katika mkutano wa siku tano utakuwa wa tija na fursa muhimu katika utoaji wa huduma za jamii wakati wote watakapokuwa nchini.

Aidha, katika mahitaji yao ya malazi, chakula, usafiri na mahitaji mengine ya msingi, makadirio ni kwamba kila mgeni anaweza kutumia zaidi ya shilingi milioni moja, hivyo basi kwa hesabu za haraka haraka kutakuwa na matumizi ya shilingi za kitanzania zaidi ya bilioni tano katika muda wa siku tano tu.

“Wito wangu kwa watanzania, nawaomba wajitokeze kushiriki katika mkutano huu wa ESAAG wa 2015, hivyo natoa rai kwa wataalam, wahasibu na wadau wetu wote kwa ujumla wao ili tuweze kushirikiana kuufanikisha mkutano huu wa kimataifa unaofanyika nyumbani, Tanzania” alisema Mwanaidi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya mkutano huo ambaye pia ni Makamu Mhasibu Mkuu wa Serikali Azizi Kifile amesema kuwa nchi washiriki zinazounda umoja huo ni Botswana, Kenya, Lesotho, Malawi, Mauritius, Msumbiji, Namibia, Rwanda, Afrika Kusini, Swaziland, Uganda, Zambia, Zimbabwe na mwenyeji Tanzania.

Azizi aliwahakikishia washiriki wote kuwa maandalizi ya mkutano huo katika masuala ya usafiri, usalama na malazi yapo katika hatua nzuri na kamati yake imejipanga vema ili mkutano huo uwe wa mfano wa kuigwa kwa nchi zote wanachama watakapopata fursa ya kuandaa mkutano wa mwaka katika nchi zao.

ni wa serikali wa nchi za mashariki na kusini mwa Afrika,Kwa bahati nzuri chama hiki kikiwa na malengo yafuatayo

ESAAG ni chama cha wahasibu wakuu ambacho kilizaliwa miaka 20 iliypoita Arusha hapa nchini mwaka 1995 na mkutano wa mwaka huu wa 22 wa ESAAG unaongozwa na kauli mbiu “Uimarishaji na usimamizi wa fedha kwa ajili ya Maendeleo ya kijamii na Kiuchumi katika kanda’’.

CCM hatua moja kuelekea uchaguzi

$
0
0
Dodoma. Wakati Rais Jakaya Kikwete akitarajiwa kutua mjini hapa mwishoni mwa wiki hii kuendesha kikao cha Baraza la Mawaziri, huku Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), ikitarajiwa kukutana muda wowote kuanzia wiki ijayo kujadili pamoja na mambo mengine, mchakato wa Kura ya Maoni na Uchaguzi Mkuu.
Chanzo chetu cha habari kilisema jana kuwa Kikwete atakuwa mjini hapa wikiendi hii kuendesha kikao cha Baraza la Mawaziri.
Hata hivyo CCM imeanza hatua ya kwanza kuelekea Uchaguzi Mkuu wakati kikao cha NEC kikitarajiwa kufanyika mwezi huu kupanga tarehe na utaratibu mzima wa uchukuaji na urejeshaji fomu kwa wagombea wa chama katika ngazi za urais, ubunge na udiwani.
Tayari Rais Kikwete amepuliza kipenga cha mbio za urais kwa CCM katika sherehe za miaka 38 ya kuzaliwa kwake wakati wa maadhimisho yaliyofanyika mkoani Ruvuma, akiwataka wenye sifa wajitokeze kuchukua fomu huku akisema: “Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba, mwaka huu wa kupata rais wa awamu ya tano, utakuwa wa kihistoria.”
Waliotangaza, wanaotajwa
Hadi sasa makada wa CCM waliotangaza nia kuwania urais ni Naibu Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Mawasiliano, January Makamba; Mbunge wa Nzega, Dk Hamis Kigwangalla; Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu.
Pia wapo wanaotajwa kwamba huenda wakajitokeza mchakato huo utakapoanza rasmi ambao ni Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba; Mbunge wa Songea Mjini, Dk Emmanuel Nchimbi; Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja; Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe; Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta na mawaziri wakuu wa zamani, Edward Lowassa na Frederick Sumaye.
Wengine ni Spika wa Bunge, Anne Makinda; Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Asha - Rose Migiro; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandosya na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira.
Kura ya Maoni
Katika kikao cha NEC ambacho kitakutana muda wowote wiki ijayo inadaiwa kuwa suala la kura ya Maoni huenda likaibua mjadala mkubwa kutokana na kuibua mijadala mingi hasa kutokana na kile kilichoelezwa kuwa muda wa utekelezwaji wake hautoshi.
Viongozi wa vyama vya upinzani wameshatangaza kuwa hawatashiriki katika mchakato huo.

Jana, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi na Mbunge wa Kuteuliwa, James Mbatia aliwasilisha bungeni hoja za kutaka kuahirishwa kwa mchakato huo akisema uko nyuma ya wakati.
Mbatia alitoa hoja hiyo alipokuwa akiomba mwongozo wa Spika, mara baada ya kipindi cha maswali na majibu kumalizika: “Mwenyekiti nchi yetu hapa tulipo leo hii hakuna daftari la kudumu la wapiga kura. Julai 9, mwaka jana Tume ya Uchaguzi ya Taifa iliwakutanisha wadau na wakaambiwa daftari la kudumu la wapiga kura lililopo limechafuka, limechafuliwa ni chafu na halifai kutumika tena. Wakatwambia wameanzisha utaratibu wa kuandikisha upya wapigakura wote wa Tanzania na mfumo watakaotumia ni mfumo wa BVR. Walituhakikishia zoezi la kuandikisha wapigakura lingeanza Septemba 9 mwaka jana mwanzoni.”
Hata hivyo, alisema jambo hilo halikufanikiwa na badala yake Serikali ilisema lingefanyika Oktoba na Novemba. Desemba yalifanya majaribio katika majimbo matatu; Kawe, Kilombero na Katavi lakini yalikuwa na changamoto nyingi.
Akijibu mwongozo huo jana jioni, Mwenyekiti wa Bunge Mussa Azzan Zungu alisema Kamati ya Uongozi imeamua kwamba Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ifanye mkutano na wadau wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kujadili maandalizi ya Kura ya Maoni.
Alisema Kamati Bunge ya Katiba na Sheria imepewa jukumu la kufuatilia suala hilo ili kuhakikisha kwamba mkutano huo unafanyika na kuwasilisha taarifa kwenye kamati ya uongozi.
Wakati hayo yakitokea bungeni, taasisi za wanaharakati wa Zanzibar zilisema Kura ya Maoni ni batili kutokana na kukiuka sheria.
Mbali na masuala hayo, imelezwa kuwa kikao hicho kitapokea taarifa ya utekelezwaji wa maazimio ya Bunge kuhusu sakata la uchotwaji fedha katika Akaunti ya Tegeta Escrow.
Kikao hicho kinafanyika ikiwa ni takriban siku 20 baada ya kufanyika kwa kikao cha Kamati Kuu kilichokutana Zanzibar.
Alipoulizwa kuhusu taarifa hizo za kuwepo kwa kikao cha NEC, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema: “Hakuna kitu kama hicho… najua mnataka kuandika, lakini ninachotaka kusema, hakuna mkutano huo.
“Nitashangaa kesho nikiona mmeandika haya… lakini nimewazoea. Hata mkiandika CCM itashinda.”
MWANANCHI

MIRIAM KINUNDA NA UPISHI WAKE WA PILAU YA MBOGA

$
0
0

Modern Swahili Recipes For The West, cookbook is now Available at Amazon World-wide. Check Amazon in your country. Also in USA you can get at Walmart and Barnes and Noble Online or ask your nearest store. Now on sale at Amazon USA http://www.amazon.com/dp/0988735903/ Thank you Miriam Kinunda Author of Taste of Tanzania Cookbook

Mishumaa ya Kale LIVE .Ijumaa hii na kila Ijumaa

$
0
0
Mishumaa ya Kale ni kipindi ambacho kinakuletea muziki wa zamani na maelezo mbalimbali ju ya Muziki huo. Ungana na Dj Luke Joe na Mubelwa Bandio kila Ijumaa kuanzia saa 11 jioni mpaka saa moja kamili kwa saa za Marekani Mashariki (5:00pm - 7:00pm EST) kupitia Kwanza ProductionVijimambo Radio ama Border Radio

SAMATTA: sikubali, kwa kiwango changu Ulaya pananihusu

$
0
0
Mbwana Samatta 
By Gift Macha (email the author) 

Straika huyo amejipatia umaarufu mkubwa miaka ya hivi karibuni kutokana na umahiri wake uwanjani hasa katika kufunga mabao. Anayafanya haya akiwa na klabu yake ya TP Mazembe pamoja na timu ya Taifa Tanzania.
HAKUNA ubishi kwamba straika wa TP Mazembe na Taifa Stars, Mbwana Samatta, ndiye mwanasoka mahiri wa Tanzania katika zama hizi. Wapo wengi wanaotamba, lakini Samatta ni funga kazi kwa sasa.

Straika huyo amejipatia umaarufu mkubwa miaka ya hivi karibuni kutokana na umahiri wake uwanjani hasa katika kufunga mabao. Anayafanya haya akiwa na klabu yake ya TP Mazembe pamoja na timu ya Taifa Tanzania.

Samatta mzaliwa wa Mbagala Rangi Tatu, jijini Dar es Salaam, alisajiliwa na Mazembe mwaka 2011 akitokea Simba. Alisaini mkataba wa miaka mitano na sasa amebakiza mwaka mmoja tu.

Mwanaspoti, ambalo limeweka kambi kwa wiki nzima hapa Lubumbashi, limefanya mahojiano na Samatta na kuzungumzia masuala kadhaa kama ifuatavyo;

Dili la kwenda Urusi

Samatta alirejea hapa Lubumbashi Alhamisi ya wiki iliyopita akitokea Urusi ambako alikwenda kufanya majaribio ya soka la kulipwa katika klabu ya CSKA Moscow.

“Mwanzoni ilikuwa nisajiliwe moja kwa moja, lakini CSKA wakasema niende kwa ajili ya majaribio kwa wiki moja, nilishindwa kufanya katika siku mbili za mwanzoni kutokana na kuumia enka, lakini siku nyingine tano nilifanya,” anasema.

“Walivutiwa na mimi, hivyo kazi ikawa ni kuzungumza na klabu, nadhani Moise (Katumbi) kawatajia dau kubwa ndiyo maana imekuwa ngumu na mpaka sasa unaona kimya.

“Dirisha la usajili kule lilifungwa mwishoni mwa mwezi uliopita, hivyo inabidi nisubiri dirisha kubwa la usajili. Sina uhakika kama mabosi wa Mazembe wataniruhusu kuondoka kabla ya mkataba wangu kumalizika, lakini nitajitahidi kwa kadiri inavyowezekana kwa sababu nimebaini nina kiwango cha kutosha kucheza Ulaya.

“Tatizo kubwa timu nyingi za Ulaya zinafikiri wachezaji wa Afrika ni wa bei chee jambo ambalo bosi wetu hakubaliani nalo kabisa, anataka dau la maana.”

Maisha ya Lubumbashi

“Nimeshapazoea hapa, yaani ni kama nipo nyumbani vile. Nina marafiki wengi kwa sababu muda mwingi nipo huku,” anasema kwa tabasamu.

“Kwa sasa naishi kwangu, lakini mwanzoni nilipofika nilifikia kwenye nyumba za klabu, palikuwa kama kifungoni kwani muda mwingi nilikuwa mpweke, niliyakumbuka sana maisha ya Tanzania wakati ule.”

Programu yake ya mazoezi

Samatta anasema mbali na mambo mengine, anapenda mazoezi kupita kiasi na kila siku lazima afanye mara mbili, ikiwamo kwenda gym kujiweka fiti.

“Kila siku kabla ya mazoezi ya kawaida ya timu huwa nawahi nusu saa zaidi, natumia muda huo kufanya mazoezi binafsi kama kupiga mipira ya faulo na kujaribu kufunga kwa mbali,” anasema.

“Kama napiga faulo huwa natumia goli la mazoezi kama ukuta, huwa naliweka mbele ya goli halisi la uwanjani na najitahidi kuvusha mpira na kufunga, huwa sihitaji kipa kwa mazoezi haya, hayanisaidii sana lakini kuna nyakati huwa naona umuhimu wake.

“Tukiwa na mazoezi ya mara moja kwa siku, huwa natumia muda mwingine wa jioni kama kuanzia saa nane mchana kwenda gym, nafanya mazoezi ili kuwa fiti zaidi, nikifanya mazoezi kwa siku mara moja huwa naona hayatoshi, siku za mapumziko huwa nafanya mazoezi ya kukimbia barabarani, kuruka kamba na pushapu.”

Umaarufu wake

Samatta ni maarufu hapa Lubumbashi, ukiwa hapa hauhitaji kuambiwa na mtu utabaini tu. Mara baada ya mechi ya Mazembe, mashabiki wengi hutamani kupiga naye picha. Wengi hutamani kubeba begi na viatu vyake. Kwa kifupi ni kwamba Samatta anapendwa sana hapa.

“Ni vizuri pale unapokuwa na watu wengi wanaokukubali, hiyo inaonyesha namna kazi yako inavyowavutia, haikuwa kazi rahisi kupata watu wengi ambao wako upande wangu, nilipambana sana wakati nafika.” anaongeza kusema mtoto huyo wa mshambuliaji wa zamani wa Taifa Stars, Ally Samatta.

“Muda mwingine hii inakuwa ni changamoto, nikitaka hata kwenda dukani inakuwa shida, inabidi kwanza nitazame chini pana watu wangapi, ni furaha lakini siyo kila muda mtu unaweza kuwa kwenye furaha.”

Posho za maana

“Hapa tunapata posho nyingi na zinakuwa tofauti kutokana na aina ya mechi tunayocheza, inakuwa tofauti pia kulingana na mashindano na hatua tunayocheza,” anafafanua.

“Mfano mechi kubwa hapa ni sisi na AS Vita ya Kinshasa, ni mechi kama vita na huwa ina hamasa kubwa, posho ya mechi hiyo ni kubwa kuliko zile nyingine.

“Posho ya mechi za kimataifa ni kubwa pia, inapanda kulingana na namna tunavyozidi kusonga mbele, ni mara chache hapa wasitoe posho.”

Watanua na magari yao

Wachezaji wa TP Mazembe wanaonekana kuwa na maisha ya tofauti na yale ya wachezaji wa Tanzania kwani, wachezaji wengi wa timu hiyo hufika mazoezini na hata kwa baadhi ya mechi wakitokea makwao. Hutumia magari binafsi pia.

Kwenye mechi ya Jumamosi kati ya Mazembe na Don Bosco, asilimia 90 ya wachezaji wa Mazembe walikuja kwa magari yao, wachache walitumia basi dogo la klabu.


“Hapa tunaruhusiwa kutumia magari yetu, tunakuja nayo mazoezini na hata kwenye baadhi ya mechi, kama tumeweka kambi huwa tunatumia basi kubwa la klabu ama pale tunapocheza mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika,” anasema Samatta.

Fursa ya Watanzania ipo

“Nikitazama wachezaji wanaokuja kucheza hapa, hata wa kwetu Tanzania wanaweza, ni jambo la kuamua tu kwamba nakwenda kucheza Mazembe ama timu nyingine kubwa,” anasema.

“Kuna changamoto kadhaa, lakini vipaji ndivyo vitakavyowabeba, hakuna mtu anayeweza kufunika kipaji chako, mwanzo utakuwa mgumu lakini baada ya muda utafika mbali.”

Picha yake uwanjani

Unapoingia tu kwenye Uwanja wa Mazembe ukitokea katika vyumba vya kubadilishia nguo, kumechorwa picha za mastaa kadhaa waliotamba na wanaotamba na timu hiyo, picha ya Samatta pia ipo.

“Kuchorwa kwa picha yako pale si kazi rahisi na ndiyo sababu unaona siyo wote kwenye timu wamechorwa pale, inahitaji kufanya kazi ya ziada ili kuwavutia mabosi,” anasema kwa kujiamini.
“Nafurahi maana kumbukumbu yangu imebaki pale, hata nikiondoka Mtanzania mwingine akija kucheza hapa ataiona kumbukumbu yangu, ni jambo la kufurahia sana.
”SOURCE:MWANASPOTI

MWENYEKITI CUF ALIZIMIA MAHAKAMANI!

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Kata ya Sandare, Temeke jijini Dar, Abina Ally akiwa Mahakamani.

Denis Mtima/Amani
MAJANGA! Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Kata ya Sandare, Temeke jijini Dar, Abina Ally Abina amejikuta akipandwa na presha kisha kuzimia katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Tukio hilo ambalo lilikuwa gumzo lilijiri hivi karibuni mahakamani hapo ambapo Abina alikuwa miongoni mwa wafuasi 30 waliokamatwa kwa madai ya kufanya maandamano kutoka Temeke kwenda Zakhem na Mwenyekiti wa CUF Taifa, Prof. Ibrahim Haruna Lipumba.

MKASA MZIMA
Akisimulia mkasa mzima, mmoja wa wafuasi hao ambaye hakutaja jina alisema kuwa, tukio hilo la mwenyekiti wao kupatwa na presha na kuzimia lilitokana na kutomwamini mdhamini wake, Maulid Ngoyogo katika kutoa maelezo baada ya kuitwa na hakimu ili apatiwe dhamana.
Mwenyekiti huyo, Abina Ally akiamshwa kwa kumwagiwa maji.

HOFU YA KURUDISHWA RUMANDE
Katika msala huo, kila mtuhumiwa alipendekeza mdhamini wake ambapo walikuwa wakiitwa kwa zamu.
“Hali hii imetokana na kuhofia mdhamini wake kushindwa kujieleza kiufasaha huku akihofia kurudishwa rumande tena kwa kushindwa kutoa maelezo sahihi,” alisema mfuasi huyo.

AMWAGIWA MAJI, AZINDUKA
Hadi gazeti hili linaondoka kwenye viunga vya mahakama hiyo, jamaa huyo alimwagiwa maji na kuzinduka ambapo aliendelea na taratibu za dhamana huku akisubiri kesi hiyo ya maandamano bila kibali kuendelea kuunguruma.

Hata hivyo, hakuwa tayari kuzungumza na mwanahabari wetu juu ya tukio hilo.

EXCLUSIVE: TEVEZ AFUNGUKA ALIVYOTESWA, KUDHALILISHWA

$
0
0
Majeraha ya mgongoni aliyopata, Jumanne Hassan ‘Tevez’ wakati wa kuteswa.
Na Musa Mateja
EXCLUSIVE! Kile kisa cha mtalaka wa mwimba taarab mahiri Bongo, Aisha Ramadhani Nkongo ‘Isha Mashauzi’, Jumanne Hassan ‘Tevez’ kuteswa na kudhalilishwa nchini Afrika Kusini kisa kikidaiwa ni kudhulumu mzigo wa wafanyabiashara wenzake kimeingia awamu nyingine!
Kwa mara ya kwanza Gazeti Pendwa la Amani Tanzania limeweza kuzungumza na Tevez kwa dakika arobaini na tano kutokea nchini humo ambako anauguza majeraha.
KWANZA SIKU YA TUKIO
Kabla Tevez hajasimulia kilichompata na hali yake kwa sasa, ni muhimu kukumbuka kuwa, tukio hilo ambalo lilikuwa habari ya Jiji la Dar es Salaam, lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo picha zake zilizagaa zikimuonesha akiwa amefungwa kamba huku mwili wake ukiwa umetapakaa damu na majeraha kadhaa.

AMANI LAMSAKA
Kwa vile habari za tukio hilo ziliandikwa na baadhi ya vyombo vya habari bila kupata balansi (uwiano) na Tevez mwenyewe, Amani liliingia kazini kumsaka mhanga huyo usiku na mchana.

MSIKIE SASA
Akizungumza kwa hisia kali na gazeti hili juzi, Februari 3, mwaka huu kutoka Mji wa Durban, Afrika Kusini, Tevez alisema:
“Kusema ukweli tukio lililonikuta watu huko nyumbani (Bongo) wanalitafsiri tofauti sana. Nimesikia kwamba wanasema eti nilidhulumu mzigo wa mtu, ndiyo maana niliteswa! Si kweli.”
‘Tevez’ akiwa salama nyumbani kwake.

UKWELI NI UPI?
“Ishu iko hivi, mwenyeji wangu hapa Durban, anaitwa Ibra, ndiye ambaye alinipokea siku nilipotua hapa.
“Huyu bwana inaonekana ni tamaa. Aliniundia njama, aliita wenzake na kuniteka kisha kunitesa sana wakidhani nina pesa nyingi.
“Niliteswa sana kwa kweli. Kama mlivyoona picha. Nilidhalilishwa sana, lakini katika yote ukweli sijadhulumu mzigo wa mtu.”

ULICHOPOTEZA KATIKA UTESWAJI
“Katika mateso yangu, walifanikiwa kunipora Dola za Marekani elfu 14 (kama shilingi milioni 22) na Randi za Afrika Kusini elfu 3 (shilingi 480,000) zikiwemo simu zangu mbili aina ya Samsung na Nokia ambazo nilikuwa nazitumia sana kuwasiliana na watu wangu muhimu.”

HAIKUWA KAZI RAHISI
Tevez akazungumzia jinsi jamaa walivyomkamata: “Jamaa siku wananiteka usiku kiukweli nilipambana nao sana hadi wanafikia hatua ya kunizidi nguvu na kunifunga kamba. Nilikuwa nimewachapa kwelikweli ila kwa vile walikuwa wengi na walikuwa wakitumia silaha nilijikuta nikiishiwa nguvu baada ya kunipiga na kitu kizito kichwani nikapoteza fahamu, nilipojitambua ndiyo nikakuta wamenifunga kamba.”

KINACHOKUUMA NINI?
“Tukio linaloniuma zaidi ni yule jamaa ambaye anaonekana katika picha amekaa jirani na mimi, hana shati. Alinichoma pasi mgongoni, namchukia sana lakini nimemwachia Mungu.”
‘Tevez’ akiwa na mwanaye.

KUHUSU KUKATWA NYETI, KUFANYIWA KITU MBAYA
Tevez: “Nasikia watu huko Tanzania wanazusha eti nimekatwa nyeti, si kweli kabisa. Mimi nimepigwa na kuchomwa pasi wala hakuna kitu kama hicho zaidi ya kunichoma na pasi.
“Nimesikia wengine wanasema nimetobolewa macho, huo ni uzushi wa watu tu! Mimi niko safi na hali yangu ya kiafya inaendelea vizuri.”

SABA WAMEKAMATWA
Tevez tena: “Nashukuru sana serikali ya huku wameweza kunisaidia kwani mpaka sasa ninapoongea na wewe Musa Mateja hawa jamaa wamekamatwa saba.
“Jana (Jumatatu) walifikishwa mahakamani na kusomewa mashitaka ya kunishambulia na kupora fedha. Wanatarajiwa kurejea tena mahakamani baada ya siku 7, ingawa nimeambiwa kesho (jana Jumatano) wataletwa Polisi Central ya huku kwa ajili ya mimi kuwatambua zaidi.”

BONGO LINI TEVEZ?
“Bongo natarajia kurudi Alhamisi (leo) au Ijumaa (kesho) kama mambo yangu yatakuwa kwenye mstari ila pia sasa hivi natarajia kuwasiliana na balozi wetu ili nijue kama ana taarifa zangu na namna ambavyo ataweza kunisaidia kama kiongozi wangu.”

HALI YAKO KWA SASA
“Kusema ukweli naendelea vizuri ni majeraha tu ambayo hata hivyo yanakauka. Ila hili la pasi mgongoni ndiyo linasumbua kwa mbali, lakini naamini litakaa sawasawa.”

MCHUNGAJI GWAJIMA ADAI MTOTO ALIEJIFUNGUA FLORA MBASHA SIYO WAKE

$
0
0

Huyu ndiyo mtoto alie jifungua Flora Mbasha, mchungaji Gwajima aruka kimanga na kukana kuwa mtoto huyu siyo wake na kusema kuwa (It doesn't hold water) akiwa na maana haina mashiko. Mbasha nae alivyoulizwa juu ya mtoto huyu majibu yake aliyajibu kwa kutuma ujumbe wa wimbo huu wa injili hadi sasa watu wanashindwa kupata ukweli  wa nani baba wa mtoto huyu lakini mwenye majibu ya  maswali yote ni mwenyewe Flora Mbasha. Jitiririshe na wimbo wa Emmanuel Mbasha hapa chini kama majibu ya wale wote waliompigia simu na kuuliza kama mtoto huyu ni wake au yupo tayari kwenda kupima DNA.

MH LOWASA KAWA LULU BUNGENI...WABUNGE WAPANGA FOLENI KUMUONA

$
0
0
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, hali yenye msisimko na ya kuonyesha jinsi gani mbunge wa Monduli Ndugu Lowassa anakubalika, imefikia kipindi hapati nafasi ya kupumua kutokana..
na uwingi wa wabunge kupishana kumuona....
Sasa nafkiri imefikia wakati spearker wa bunge aangalie hili jambo, na ikiwezekana apige stop wabunge kwenda kumsalimia Lowassa, imesikika moja wa mbunge akisema hayo.....

Inakadiriwa kwa siku Lowassa anaonwa na zaidi ya wabunge 80 kitu ambacho kinafanya sehemu alipokaa panakuwa busy sana.... Huu ni muendelezo wa kuonyesha ni jinsi gani Lowassa ana mvuto na anavyokubalika katika jamii....

GHANA 3-0 EQUATORIAL GUINEA AFCON 2015 GHANA KUCHEZA NA IVORY COAST FINAL JUMAPILI.

$
0
0
 wachezaji wa Ghana  wakishangilia ushindi na kutinga fainali baada ya kuwakunja wenyewe Equatorial Guinea 3-0  kwaiyo sasa  Ghana kukutana na Ivory Coast tarehe 8 kwenye fainali. 
Baada ya kipenga cha mwisho wenyewe wa mashindano hayo ya AFCON walikuwa wamekubali kipigo cha magoli matatu ndipo washabiki walivyoanzisha timbwili hili uwanjani hapo.
Hali ilionekana siyo shwari toka kipindi cha kwanza pale Ghana walivyo pewa penati ya mapema hii hapa ilikuwa baada ya dk 45 za kwanza washabiki wenye mizimu ya kinyamulenge walianza kuwarushia makopo na chupa wacheza wa Ghana walivyokuwa wakielea kwenye vyumba vya mapumzikia.
Uwanjani hapo hali haikuwa shwari kwa muda wa dk 30 baada ya kipenga sha mwisho wa.
Polisi wakiwapandia washabiki jukwaani hili kuwaadabisha kutoka na vurugu hizo uwanjani hapo
Chupa za maji hiyo wakirushiwa wachezaji wa Equatorial Guinea kutoka kwa washabiki wenye jaziba baada ya timu yao kukubali kipindo.
Helicopter ikizunguka eneo la uwanja kujaribu kuzima vurugu hizo baada ya kipenga cha mwisho 
Viewing all 45982 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>