Quantcast
Channel: VIJIMAMBO
Viewing all 45982 articles
Browse latest View live

ANGALIA TOFAUTI YA MAREKANI NA TANZANIA MTU AKIWA AMESHAHUKUMIWA KWENDA MAGEREZA

$
0
0
Hapa Cheka ameshahukumiwa kwenda magereza miaka 3 anaongea na simu na anasindikizwa kama anaenda chooni vile na simu anatumia kuaga ndugu na marafiki bongo raha saana.
Hapa ni Marekani mtuhumiwa ufungwa pingu hadi miguuni akisikiliza kesi yake au akisha hukumiwa upelekwa akiwa hivi kwenye gari la magereza au hata mahabusu.
 Tafauti kati ya bongo na Marekani ndiyo hii polisi wanavyo watreat watuhumiwa wakiwa mahakamani na baada ya kuhukumiwa.
Hapa mtuhumiwa akiwa mahakamani pingu mikononi.
Hapa mtuhumiwa amesha hukumiwa nchi Tanzania akisindikizwa na polisi kupanda gari la kumpeleka magereza kutumia kifungo.
hapa Marekani mtuhumiwa amesha hukumiwa
Cheka akichukuliwa na mahabusu wengine kwenye karandinga kwenda kuswekwa lupango.
Hii hapa ni basi linalotumika kubebea watuhumiwa nchini Marekani.

HIRIZI YAKUTWA KWA WEMA

$
0
0
Wananchi wakishuhudia hirizi getini kwa Miss Tanzania 2006 asiyechuja, Wema Abraham Sepetu ‘Madam’.
Stori: Issa Mnally na Richard Bukos/Risasi Mchanganyiko

IMANI za kishirikina? Mshangao wa aina yake umetokea nyumbani kwa Miss Tanzania 2006 asiyechuja, Wema Abraham Sepetu ‘Madam’ baada ya kutupiwa hirizi getini kwake, Risasi Mchanganyiko lina stori kamili.
Tukio hilo lililokusanya watu wapenda ‘ubuyu’ lilijiri alfajiri ya Jumamosi iliyopita, nyumbani kwa mlimbwende huyo, Kijitonyama-Bwawani jijini Dar baada ya mapaparazi wetu kutonywa juu ya uwepo wa tukio hilo.
TUJIUNGE NA CHANZO
“Njooni hapa kwa Wema tumekuta mfuko mweusi wa nailoni, ndani yake una hirizi, nazi zimeandikwa maandishi ya Kiarabu huku zikiwa zimevunjwavunjwa na pia kuna picha ya Diamond ndani yake,” kilisema chanzo hicho.

MAPAPARAZI WATIA TIMU
Mapaparazi wetu ambao walikuwa kwenye mizunguko yao kikazi, walitumia usafiri wa pikipiki kwenda nyumbani hapo ambapo ndani ya dakika ‘sifuri’ walikuwa wameshafika na kukuta vitu hivyo vikiwa vimezunguka na mashuhuda.
Wananchi wakizitazama kwa karibu zaidi hirizi hizo.

KILA MTU ASEMA LAKE
Wakati mapaparazi wetu walipokuwa wakidadisi juu nani aliyetupa kifurushi hicho na sababu za kufanya hivyo, mashuhuda hao kila mmoja alieleza lake.
“Sisi hatujui aliyetupa inaonekana atakuwa alikuja usiku sana lakini inaonesha mtupaji atakuwa anataka Wema na Diamond warudiane na ndiyo maana ameambatanisha na picha ya Diamond,” alisikika shuhuda mmoja huku mwingine akidakia:
“Aliyetupa hapa atakuwa ameweka zindiko ili Diamond asirudiane tena na Wema. Atakuwa anataka Diamond aendelee na Zari.”

Katika hali ya kushangaza, mlinzi wa kampuni moja inayolinda nyumbani kwa mlimbwende huyo, aliupiga teke na kuusambaratisha mfuko uliokuwa umehifadhi vitu hivyo pamoja na hirizi.

MAPAPARAZI WAMGONGEA WEMA
Ili kutaka kujua Wema amelichukuliaje tukio hilo, mapaparazi wetu waligonga geti la Wema ambapo alitoka binti mmoja ambaye hakutaka kujitambulisha jina lake na kuzungumza pasipo kufungua geti akiwa anachungulia kupitia uwazi mdogo uliopo getini hapo.
Hizi ndizo hirizi zilizokutwa getini kwa Wema zikiwa na picha ya 'Diamond'.


“He mimi sifungui, Madam (Wema) hayupo kwanza naogopa hivyo vitu si vya kawaida, mimi nakwenda zangu ndani,” alisema binti huyo na kutoweka.

APIGIWA SIMU
Mapaparazi wetu walimvutia waya Madam ambapo kilongalonga chake kiliita bila ya kupokelewa, kesho yake (Jumamosi) mapaparazi walitia timu tena nyumbani hapo na kuambiwa Madam hayupo huku simu yake ikiwa haipatikani.

WAHARIRI MZIGONI
Juzi, Jumatatu wakati gazeti hili lilipokuwa linakwenda mitamboni, wahariri wa gazeti hili walifunga safari hadi nyumbani kwa Wema na kugonga getini kwake ambapo alitoka mtu wa karibu na Wema, Petit Man. Mazungumzo yakawa hivi:
Petit: Yeah karibuni.
Staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu.


Wahariri: Tumekuja kumuona Madam, tumemkuta?
Petit: Mna miadi naye?
Wahariri: Hatuna ila we mwambie wahariri wa Global Publishers wanakuita.
Petit: Ok subirini.
(Baada ya sekunde 30)

WEMA, PETIT WATOKA NA GARI
Wakati wahariri wakiendelea kusubiri, Wema na Petit walitoka getini wakiwa na gari aina ya Murano (lile la alilopewa Diamond) ndipo wakashusha kioo ili waweze kuzungumza nao.
Mhariri: Mambo? Vipi mzima?
Wema: Mzima niambie.

Mhariri: Dakika mbili kidogo basi tuongee.
Wema: Nina haraka lakini.
Mhariri: Hata dakika moja. Ni hivi, kuna picha tumeletewa na mapaparazi wetu zinaonesha juzi hapa nyumbani kwako kuna mfuko ulitupwa hapa ukiwa na hirizi na mazagazaga yanayosadikiwa kuwa ni ya kishirikina.
Mkali wa Bongo Fleva, 'Diamond Platnumz'.
Wema: (Kwa mshtuko) Haaaah! Hapa...kwa...ngu.
Mhariri: Hapa kwako ndiyo tena ndani yake kuna picha ya Diamond.
Wema: Kwa kweli mimi...sijui...hata sielewi kama kuna kitu kama hicho kimetokea nyumbani kwangu.
MABAKI YAONEKANA
Wakati wahariri wakiendelea na mazungumzo na Wema, waliona mabaki ya vipande vya nazi pembeni ya geti hilo na kumuonesha Wema ambaye alizidi kutaharuki.
“Haaah! Kweli jamani vipande vya nazi...sawa lakini mimi imani yangu haiamini hivi vitu,” alisema Wema.
Baada ya mazungumzo hayo, wahariri walimuaga Wema huku akiwa katika hali ya sintofahamu!
SOURCE:GPL

KUZUKA KWA UGOJWA WA SURUA ( MEASLES) NCHINI MAREKANI

$
0
0
Habari za afya zinazozidi kuenea nchini Marekani ni kuzuka kwa  ugojwa wa surua toka mwezi Dec. 2014 jijini California. Habari kamili toka shirika la kudhibiti magojwa yenye  maambukiza nchini Marekani "CDC" inaeleza kuwa,  tukio la kwanza la  ugojwa huo linasadikika kuanzia Disneyland Resort Park, iliyopo Orange County jijini California. Mbali na tukio hilo, idadi kamili ya waathirika kuanzia January Mosi hadi January 30,2015 yapata 102 katika majimbo 14 yaliyosambaa ugojwa huo.

RAMANI HII INAASHIRIA MAJIMBO YALIYO NA MATUKIO YA SURUA 2015





KWA UFAHAMU ZAIDI KUHUSU UGOJWA WA SURUA BOFYA ;

Mafiamatembezi: SURUA NI NINI?:     Surua ni mojawapo ya magonjwa ya kuambukiza ambao una kiwango cha juu cha maambukizi pindi mtu apatapo vimelea vya ugonjwa huu. Pamoj...


Shukrani
http://mafia-matembezi.blogspot.com/
http://emergency.cdc.gov/han/han00376.asp

Story
NesiWangublogspot.com

NDEGE YA TAIWAN YAANGUKIA MTONI NA KUUA WATU 12

$
0
0
Ndege hiyo ikigonga daraja kabla ya kuangukia kwenye kwenye mto
Waokoaji wakinasua watu waliokuwa ndani ya ndege hiyo.

Taswira kutoka eneo la ajali hiyo.


Ndege inayoimilikiwa na Shirika la Ndege la Taiwan, la TransAsia imepata ajali na kuangukia kwenye mto katika mji mkuu, Taipei na kuua watu 12.

Vyombo vya habari vya Taiwan vimesema watu zaidi ya 50 walikuwa ndani ya ndege hiyo, wakati ajali ilipotokea na idadi kubwa ya watu wameripotiwa kujeruhiwa.

Shirika la Habari la Taiwan limeonesha picha ya ndege hiyo ikiwa imezama kwa kiasi kikubwa katika mto Keelung.

Chanzo cha ajali bado hakijajulikana.

Watu kadhaa wameokolewa na kupelekwa hospitali na wengine 10 bado wamenasa katika ndege hiyo.

Ndege hiyo ilikuwa ikiruka kutoka uwanja wa ndege wa Songdshan Taipei kuelekea uwanja wa ndege wa Kinmen nje ya Taiwan.

RAIS WA UJERUMANI ATEMBELEA KANISA KUU LA KILUTHERI LA AZANIA FRONT JIJINI DAR

$
0
0
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa (kulia), akimkaribisha Rais wa Ujerumani, Joachim Gauck alipofika kutembela kanisa hilo Dar es Salaam jana jioni.
Rais wa Ujerumani, Joachim Gauck akisalimiana na Mama Anna Mkapa baada ya kuwasili kanisani hapo.
Rais wa Ujerumani, Joachim Gauck (katikati), akisaini baada ya kufika kanisani hapo.
Wanakwaya wakitumbuiza.
Askofu Malasusa na Rais wa Ujerumani, Gauck wakiteta jambo.
Muonekano wa Kanisa la Azania Front.
Rais Gauck akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa kanisa hilo pamoja na waumini. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)

LOOK OF THE DAY

$
0
0
Staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’

COVENANT BANK, AAR WAZINDUA BIMA YA MATIBABU YA TSH. 1000 KWA SIKU

$
0
0
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Covenant Bank, Balozi Salome Sijaona (Katikati) akikata utepe kufungua kadi za Bima ya Matibabu kwa wateja wa kwanza wa Akaunti Mpya ya Bima ya Matibabu ambayo inawawezesha wateja wa Benki hiyo kupata Bima ya Matibahu kwa Shilingi 1000 kwa siku kwa familia nzima na kuweza kutibiwa hospitali Binafsi na za Serikali. Wanaoshirikiana nae ni Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja (Kulia) na Meneja Uendeshaji wa AAR. Majula Manyama.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Covenant Bank, Balozi Salome Sijaona (Katikati) akikagua kadi za Bima ya Matibabu punde baada ya kukabidhiwa kutoka AAR, Kadi hizo zinawawezesha wateja wa Benki hiyo kupata Bima ya Matibahu kwa Shilingi 1000 kwa siku na kuweza kutibiwa hospitali Binafsi na za serikali pamoja na kununua dawa, Wanaoshuhudia (Kulia) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja na Meneja Uendeshaji wa AAR. Majula Manyama.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Covenant Bank, Balozi Salome Sijaona (Katikati) akikabidhi kadi ya Bima ya Matibabu kwa Zaituni Zoro, ambae ni miongoni mwa wateja wa kwanza wa Huduma mpya ya Bima ya Matibabu ambayo zinawawezesha wateja wa Benki hiyo kupata Bima ya Matibahu kwa Shilingi 1000 kwa siku na kuweza kutibiwa hospitali Binafsi na za serikali pamoja na kununua dawa. Wanaoshuhudia (Kulia) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja na Meneja Uendeshaji wa AAR. Majula Manyama.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Covenant Bank, Balozi Salome Sijaona (Katikati) akikabidhi kadi ya Bima ya Matibabu kwa Mary Temu, ambae ni miongoni mwa wateja wa kwanza wa Huduma mpya ya Bima ya Matibabu ambayo zinawawezesha wateja wa Benki hiyo kupata Bima ya Matibahu kwa Shilingi 1000 kwa siku na kuweza kutibiwa hospitali Binafsi na za serikali pamoja na kununua dawa. Wanaoshuhudia (Kulia) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja na Meneja Uendeshaji wa AAR. Majula Manyama.
Baadhi ya Wajasiriamali waliojitokeza katika uzinduzi wa Akaunti ya Bima ya Matibabu.
Wateja waliokabidhiwa kadi zao wakiwa katika picha ya pamoja.

HASSAN ISIHAKA NA RAMADHAN SINGANO KUFANYA MAJARIBIO REAL MADRID

$
0
0
kikosi cha wekundu wa Msimbazi

Endapo watafanikiwa kucheza timu ya vijana ya klabu tajiri duniani, Real Madrid ya Uhispania, basi itakuwa ni habari njema kwa soka la Tanzania, ambayo wachezaji wake kadhaa wamekuwa wakifeli majaribio ya kucheza soka la kulipwa ughaibuni, hasa nchi za Ulaya katika miaka ya nyuma.

Kufuatia tetesi za kutakiwa kwenda kufanya majaribio Real Madrid, mashabiki wa soka wa klabu ya Simba ya Dar es Salaam wamewaombea wachezaji wao kila la kheri katika majaribio yao ili waweze kusakata kabumbu Ulaya.

Haruna Hamisi, mmoja wa mashabiki na mwanachama wa Simba amesema beki wa kati wa klabu hiyo, Hassan Isihaka na straika Ramadhan Singano anayejulikana kama "Messi" kwa jina la uwanjani wana uwezo wa kucheza soka la kulipwa.

‘Vipaji tunavyo, ila vinakosa nafasi na kuharibiwa na mfumo wetu mbaya wa kutolea wachezaji wakiwa bado wadogo”, alisema Hamisi.

Emmanuel Temaeli, shabiki mwingine amesema endapo watafanikiwa, basi itakuwa faida si tu kwa Simba, bali taifa zima.

“Tukiwa na wachezaji wengi wanaocheza soka nje, tutakuwa na timu ya taifa imara kwa ajili ya michuano mbalimbali kama vile ya Mataifa ya Afrika na michuano ya kufuzu kucheza kombe la dunia”, alisema Temaeli.

Taarifa zinasema kuwa klabu ya Real Madrid ya Hispania, ambayo maofisa wake wamekuja nchini kuingia ubia na shirika la hifadhi ya jamii (NSSF) kujenga kijiji cha michezo kwa ajili ya kulea wachezaji vijana kitakachosimamiwa na klabu hiyo ya Cristiano Ronaldo, wameomba CD (video) ili wawafanyie tathmini kupitia mechi walizocheza hivi karibuni.

Mabosi hao wamevutiwa na wachezaji hao vijana baada ya kuwaona katika mechi ya ligi kuu wakati Simba ilipocheza na klabu tajiri ya Azam na kutoka sare ya 1-1 majuma mawili yaliyopita.

Wachezaji kadha wa Tanzania wamefanikiwa kufanya majaribio kucheza nje bila mafanikio akiwemo mshambuliaji machachari, Mrisho Ngasa (anayecheza Yanga hivi sasa) aliyekwenda kufanya majaribio klabu ya West Ham ya Uingereza mwaka 2009 ikiwa chini ya kocha Gianfranco Zola.

Hivi karibuni, CSKA ya Urusi imemchukua mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na mchezaji wa klabu tajiri barani Afrika ya TP Mazembe ya Congo (DRC), Mbwana Samatta kwa ajili ya majaribio na tetesi zinasema mabosi wa timu wamevutiwa naye licha ya kuendelea kumjaribu

BBC

JK azungumzia kupigwa kwa Lipumba

$
0
0
Rais Jakaya Kikwete amewakingia kifua polisi waliotembeza kichapo kwa wafuasi wa Chama Cha Wananchi (Cuf), na kudai kuwa maandamano na mikutano yote ni lazima iwe na kibali cha polisi.

Rais Kikwete aliyasema hayo jana Ikulu jijini Dar es Salaam, baada ya kuwaeleza waandishi wa habari walichozungumza faragha na mgeni wake, Rais wa Ujerumani, Joachim Gauck, na baadaye kuja mbele ya waandishi wa habari na kujibu maswali mbalimbali.

Akijibu swali la waandishi wa habari wa Ujerumani, aliyetaka kujua hali ya usalama na haki za binadamu nchini ikoje hasa ikizingatiwa Januari 27, mwaka huu, kulikuwa purukushani kati ya polisi na wafuasi wa Cuf, na kutumia nguvu kubwa katika kuwadhibiti.

Akijibu swali hilo, Rais Kikwete alisema zipo sheria, kanuni na taratibu zinazoongoza watu wanapotaka kuandamana au kufanya mikutano ya hadhara na kwamba ni lazima zifuatwe kwa kupata kibali cha Polisi.

“Huwezi kuamka asubuhi na kuanza kuandamana au kufanya mkutano wa hadhara ni lazima sheria na taratibu zilizopo zifuatwe…vyama vya upinzani vimekuwa vikifanya mikutano na maandamano bila kubugudhiwa iwapo wamefuata sheria zilizopo,” alisema na kuongeza:

“Usipokuwa na kibali Polisi hawawezi kukuruhusu uandamane au ufanye mkutano.”

Kauli ya Kikwete imekuja siku mbili tangu Mwenyekiti wa Cuf, Prof. Ibrahim Lipumba (pichani), kuwaeleza waandishi wa habari kuwa ameanza taratibu za kuonana na kiongozi huyo ili kujadiliana namna ya kuweka utaratibu wa kutenda haki kwa vyama vya siasa dhidi ya Jeshi la Polisi kuelekea uchaguzi mkuu, Oktoba, mwaka huu.

NIPASHE iliwasiliana na Prof. Lipumba kujua hatua aliyofikia katika kutafuta nafasi ya kuonana na Rais, ambaye alisema amepeleka taarifa kwa njia ya mtandao (Info line), na anasubiri jibu na kwamba amehofia kupeleka taarifa kwa barua kwa kuwa kuna uwezekano wa barua kufunguliwa kabla ya kumfikia.

Hata hivyo, baada ya msimamo huo wa Rais Kikwete, Prof. Lipumba alisema watawasilisha kilio cha vitendo vya uonevu vinavyofanywa na Polisi kwa Rais Gauck.

Aidha, Rais Kikwete alizungumzia pia uhuru wa vyombo vya habari akieleza kuwa serikali inaheshimu uhuru wa vyombo vya habari na ni nchi yenye vyombo vingi ikiwamo magazeti, runinga na radio zinazomilikiwa na watu binafsi na kukiwa na vichache vinavyomilikiwa na serikali.
CHANZO: NIPASHE

MKITOKA UGOMVINI, KUWA MWANGALIFU KUSAMEHE

$
0
0
KUNA mambo mengi yanatokea katika hii dunia, ambayo wakati mwingine yanatulazimisha kuzungumza na watu wetu ili kuwapa kile kidogo tunachokijua, tukiamini mchango wa mawazo yetu unaweza angalau kuongeza wigo wa ufahamu juu ya kitu kinachosababishwa na mapenzi.

Kupitia vyombo vya habari, yakiwemo magazeti redio na televisheni, tutakuwa tunaona na kusikia kuhusu wapendwa wetu wanavyopoteza maisha kutokana na mapenzi. Juzi, nilikuwa napitia habari moja hivi kutoka Tarime kule Mara, ikaniuma sana. Mdada mmoja alipigwa na mumewe na kupewa majeraha makubwa sana, eti tu kwa sababu alichelewa kupata ujauzito.

Lakini kama kuna tukio liliniharibia siku katika mwezi huu wa kwanza wa mwaka, basi ni ile ishu ya jamaa aliyemchinja mkewe pale hotelini Manzese jijini Dar es Salaam. Ninajaribu kulizungumzia suala hili ili likusaidie katika maisha yako ya kimapenzi kwa sababu ninaliona ni tukio linalojirudia kati ya wapenzi wa kada mbalimbali.

Jamaa alikuwa hana maelewano mazuri na mke wake, wakiishi kwa migogoro isiyokwisha, kiasi kwamba mwanamke akaamua kuondoka nyumbani kwao na kwenda kwa kaka yake, angalau akapumzike kwa muda. Ni vigumu kidogo kujua chanzo cha ugomvi wao, lakini tunaelezwa kuwa baada ya mama kuondoka, baba alimfuata na kumtaka wasahau tofauti zao, warejee katika uhusiano wao kama zamani.

Kinachoonekana ni kwamba mume hakuwa na dhamira ya kusamehe, kwani baada ya mwenzake kumwelewa vizuri, akakubali kuandamana hotelini ambako walikubaliana wakakae na kuzungumza yao. Matokeo yake, akatumia kisu alichokuwa nacho na kumuua mwenzake kikatili.

Orodha ya watu wanaopoteza maisha kwa sababu ya wivu wa mapenzi ni ndefu sana na kila wahusika, wana simulizi tofauti na mwingine ingawa zote ni za aina moja. Nataka nizungumzie hili la kugombana, mkafikia sehemu ya kununiana, kuhama nyumba au chumba na baadaye kurejeana.

Kwanza kabisa ieleweke kuwa ugomvi baina ya wanandoa au walio katika uhusiano ni jambo la kawaida kabisa. Sitaki kujiongopea au kukupa nafasi ya kuwaongopea wengine kuwa hili ni jambo jipya. Kila siku, sehemu fulani kuna wanandoa wanazozana, wanapigana, wanatengana na kadhalika. Tatizo linalotutofautisha kati yetu sisi na wao ni namna tunavyoumaliza ugomvi wetu.

Kuna watu hawamalizi wiki bila kuzozana ndani ya nyumba yao, lakini wakiwa nje, hakuna mtu anayefahamu kilichotokea. Unaweza kuwa shahidi kuwa umeshawahi kusikia mara nyingi juu ya ugomvi wa watu ambao siku zote uliamini wanapendana sana.

Ugomvi unaomalizika kwa mmoja kuondoka ndani ya nyumba, ni wazi kwamba umefikia kiwango ambacho hakivumiliki. Mtu anaona ni bora aondoke kidogo ili kupoza hasira iliyopo, kutuliza hali ya hewa au kutoa nafasi kwa watu zaidi kushiriki katika kutafuta suluhisho la ugomvi huo.

Sasa katika ugomvi kama huo, mambo mengi yanakuwa yamefanyika baina ya wanandoa. Kitendo cha kuondoka nyumbani kinaleta tafsiri tofauti kwa anayebaki, wengi wanafikiri kuhusu kutolewa kwa siri zao nje. Huamini kwamba huko walikoenda, wanazungumza kuhusu udhaifu wao, kitu ambacho wengi hawapendi.
Ninachotaka kusisitiza ni kwamba sisi tunajua tunapogombana, nani anakuwa amekosea na nini suluhisho lake. Tunajua kwa namna gani mwenza wetu ameumia au amekwazwa.

Jambo la muhimu
tusimuamini mara moja, mtu ambaye siku chache nyuma, alitishia kutoa uhai wetu anapokuja kuomba tumalize tofauti zetu kirahisi.

GPL

MATAYARISHO YA UJIO WA RAIS WA SHIRIKISHO LA UJERUMANI ZANZIBAR

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akitembelea Bandari ya Malindi kuangalia matayarisho ya ujio wa Rais wa shirikisho la Ujerumani Bwana Joachik Gauck.

Kushoto ya Balozi Seif ni Mshauri wa Rais anaesimamia Uchumi, Uwekezaji na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Moh’d Ramia na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar Nd. Abdulla Juma Abdulla.
Balozi Seif akiwa na Viongozi wa Kamati ya kuratibu Mapokezi ya Rais wa Ujerumani wakirudi kukagua eneo la kushukia boti ziendazo kwa kasi katika Bandari ya Malindi.

Kushoto yake ni Mshauri wa Rais Balozi Moh’d Ramia, Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje Zanzibar Balozi Silima Kombo Haji pamoja na Mkurugenzi Bandari Nd. Abdulla Juma.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwa pamoja na Balozi Mdogo wa Heshima wa Shirikisho la Ujerumani hapa Zanzibar Balozi Has –Dieter Allgaier wakielekea kukagua chum,baa cha watu Mashuhuri { VIP } kiliopo Bandari ya Malindi ambacho kimewekwa hakiba kwa ujio wa Rais wa Shirikisho la Ujerumani Bwana Joachim Gauck.
Mshauri wa Rais anayesimamia Uchumi,Uwekezaji na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Moh’ d Ramia akimuelezea Balozi Seif hatua zilizochukuliwa katika matayarisho ya ujio wa Rais wa Ujerumani.

Kati kati yao ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Moh’d Aboud Moh’d na kulia ya Balozi Ramia ni Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje Zanzibar Balozi Silima Kombo Haji.

Picha na – OMPR – ZNZ.

Rugemalira wa IPTL sasa ‘mikononi’ mwa Takukuru

$
0
0
Dar es Salaam. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imesema imemhoji na inaendelea kumchunguza mmiliki mwenza wa zamani wa Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power Tanzania Ltd (IPTL), James Rugemalira.
Akizungumza na gazeti hili jana, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk Edward Hoseah alisema vigogo wote waliohusika na sakata la uchotwaji wa fedha katika Akaunti ya Tegeta Escrow, ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) wanachunguzwa akiwamo Rugemalira.
“Tunawachunguza wote, hatuwezi kufanya kazi harakaharaka kama zimamoto, tunakwenda hatua kwa hatua, uchunguzi ukikamilika wote watakaopatikana na hatia watapelekwa mahakamani,” alisema Dk Hoseah.
Rugemalira akiwa mbia wa IPTL chini ya Kampuni ya VIP Engineering and Management (VIPEM), ndiye kiini cha vigogo wengi wa Serikali kupewa mgawo wa fedha kupitia Benki ya Mkombozi.
Akizungumzia suala hilo, Msemaji wa Takukuru, Doreen Kapwani alisema Rugemalira anachunguzwa na kueleza kuwa taratibu zote za uchunguzi ikiwamo mahojiano zimeshaanza kufanyika... “Tumeshamuhoji na tunaendelea kumchunguza, hilo linaeleweka.”
Walioburuzwa kortini na Takukuru
Mpaka sasa Takukuru imeshapeleka watuhumiwa kadhaa mahakamani wakiwamo maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).
Miongoni mwao ni Meneja Misamaha ya Kodi TRA, Kyabukoba Leonard Mutabingwa, Mwanasheria Mwandamizi wa Tanesco, Steven Roman Urassa na Mkurugenzi wa Fedha BoT, Julius Rutta Angello ambao wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka ya kuomba na kupokea rushwa ya mamilioni ya fedha kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow.
Wengine waliofikishwa mahakamani hapo ni Mhandisi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (Rea), Theophillo Bwakea anayedaiwa kupokea Sh161,700,00. Mwingine ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Rugonzibwa Mujunangoma ambaye anadaiwa kuwekewa kiasi cha Sh323 milioni.
Waliosombwa na escrow bungeni
Viongozi wengine Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge, aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Mbunge wa Sengerema (CCM), William Ngeleja aliyekuwa akiongoza Kamati ya Sheria na Utawala na Mbunge wa Chunya (CCM), Victor Mwambalaswa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini walijiuzulu nafasi zao hizo kutokana na kashfa hiyo.
Chenge anadaiwa kupokea Sh 1.6 bilioni na Ngeleja Sh40 milioni na Mwambalaswa alikuwa katika Bodi ya Tanesco ambayo Bunge liliazimia ivunjwe.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, aliwajibishwa na Rais Jakaya Kikwete Desemba mwaka jana katika mkutano wake na wazee wa Dar es Salaam. Profesa Tibaijuka anadaiwa kupokea mgawo wa Sh1.6 bilioni.
Awali, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema alijiuzulu wadhifa wake baada ya Bunge kushinikiza awajibishwe kwa mujibu wa sheria kwa kuipotosha Serikali kuhusu suala hilo.
Mbali na viongozi hao, Serikali pia imemsimamisha kazi Katibu Mkuu wa Nishati na Madini, Eliakim Maswi kupisha uchunguzi dhidi yake katika kashfa hiyo.
Januari, 23, aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospter Muhongo alijiuzulu wadhifa wake huku akisisitiza kuwa ni msafi na hawezi kuuza utu wake kwa kupokea rushwa ili kuwakandamiza Watanzania.
Kuhusu kufilisiwa mali wale waliohusika katika sakata hilo, Dk Hosea alisema hiyo ni kazi ya Mahakama kwani Takukuru kazi yake ni kuchunguza na kuwafikisha watuhumiwa sehemu husika.
Wanaodaiwa kupata mgawo wa escrow
Ripoti ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali iliyowasilishwa bungeni ilitoa orodha ya watu waliopokea mgawo wa fedha za akaunti hiyo kuwa ni pamoja na aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona (Sh40.4 milioni), aliyekuwa mjumbe wa Bodi ya Tanesco, Dk Enos Bukuku (Sh161.7 milioni).
Wengine ni Majaji wa Mahakama Kuu, Profesa Eudes Ruhangisa (Sh404.25 milioni) na Jaji Aloysius K. Mujulizi (Sh40.4 milioni) pamoja na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usajili wa Vizazi na Vifo (Rita), Philip Saliboko (Sh40.4 milioni).
Pia, wamo aliyekuwa Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Emmanuel Ole Naiko (Sh40.4 milioni), Ofisa wa TRA, Lucy Appollo (Sh80.8 milioni), Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba, Methodius Kilaini (Sh80.9 milioni), Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Eusebius Nzigirwa (Sh40.4 milioni) na Padri Alphonce Twimannye Simon (Sh40.4 milioni).

Ripoti ya PAC kuhusu kashfa ya Tegeta Escrow inatokana na uchunguzi maalumu wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kuhusu fedha hizo zilizochotwa ndani ya BoT, zilipokuwa zinatunzwa zikiwa gharama za uwekezaji (capacity charge) kwa IPTL baada ya kutokea mgogoro wa kibiashara baina yake na Tanesco.
Tanesco ililalamika kuwa ilikuwa inailipa zaidi IPTL kinyume na gharama za uwekezaji, hivyo kuamuliwa na Mahakama kuwa fedha ilizokuwa inatakiwa kulipa ziwekwe katika escrow hadi upatikane ufumbuzi wa mgogoro huo.
Hata hivyo, kesi hiyo ilipohukumiwa Februari 12 mwaka jana, ikibainisha kweli Tanesco ilikuwa inailipa zaidi IPTL, tayari fedha zilizokuwa katika akaunti hiyo zilishachotwa na IPTL kwa ruksa ya baadhi ya viongozi wa Serikali.
MWANANCHI

ZAHIR ALLY ZORRO FT MWANA FA

MSAADA KWENYE TUTA

$
0
0
 
msaada, kuna jamaa wapo Atlanta wanaandaa cultural events in Atlanta and somewhere in Florida.  Wangependa kuwa na Tanzanian group as part of their event.   Kuna yeyote ambaye anajua any Tanzania cultural group iliyopo Atlanta na vitongoji vyake au Florida?
Naomba mnijulishe, tafadhali. 618 378 6076

Mazungumzo na Mhe. Balozi Mustafa Nyang'anyi (Pt 1)

$
0
0
Karibu sana na asante kwa kujiunga nasi katika kipindi hili cha HUYU NA YULE
Tumepata fursa ya kuongea na Mhe. Balozi Mustafa Nyang'anyi ambaye ametueleza mengi juu ya safari yake kimaisha
Katika sehemu hii ya kwanza, Mhe. Balozi Nyang'anyi anaelezea
1: Historia yake.
 2: Aliposoma na alivyosoma.
 3: Namna alivyofika / kupata kazi Shirika la Utangazaji Tanganyika (TBC)
 4: Alivyoingia kwenye masuala ya diplomasia na kisha.....alivyoiona nafasi ya ubunge kwa mara ya kwanza 1970. Hii ni safari ndeefu ambayo kwa hakika utapenda kuisikia.
 KARIBU

TEMBAPHOTO OFFICIAL PHOTOGRAPHER SIKU YA SHEREHE ZA CCM NEW YORK OMMY "DIMPOZ" NDIYO HABARI YA MJINI

$
0
0
 Ukumbi wa sherehe za CCM New York  tarehe 21 mwezi wa 2, Tembaphoto ndani ya mjengo kukuletea ukodak wa kiwango.

Ukiwa na shughuli yeyote inayohusu ukodak basi ni tembaphoto ndiyo suluhisho ya yote. Tembelea web site ya tembaphoto kujionea ubora wa picha.
http://tembaphoto.com/


MULTICHOICE YAZINDUA KING’AMUZI KIPYA CHA DStv HD

$
0
0
Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi (Katikati) akifafanua jambo kwenye mkutano na wanahabari (hawapo pichani), wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa king'amuziki kipya cha DStv HD leo jijini Dar. Kulia ni kwake ni Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo na kushoto ni Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu.(Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog)

Na Andrew Chale

KAMPUNI ya MultiChoice Tanzania wasambazaji wa ving’amuzi vya DStv, leo imezindua king’amuzi kipya cha DStv HD ambacho kitaanza kutumika kwa mara ya kwanza hapa Nchini.

Akizungumza na wandishi wa habari mapema leo jijini Dar es Salaam, Meneja Uendeshaji wa MultiChoice Tanzania, Ronald Shelukindo, akielezea umuhimu wa huduma hizo alisema king’amuzi hicho kina ubora wa hali ya juu ikiwemo kuonyesha picha zenye ubora mzuri zaidi.

Pia alieleza kuwa, DStv HD mteja atapata kuona picha zenye mvuto zaidi pamoja na kiwango cha juu cha sauti Dolby Digital 5.1.

“Wateja wa DStv watafurahia ving’amuzi hivi kwa ubora wa hali ya juu hivyo ni wakati wa kuchangamkia ofa kwani ndio mara ya kwanza kuingia kwa Tanzania” alisema Ronald Shelukindo.
Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo akielezea ubora wa king'amuzi hicho cha DStv HD wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari leo jijini Dar.

Ronald Shelukindo akielezea kwa kina, alisema DStv HD, mteja anaweza kufurahia vipindi mbalimbali ikiwemo mifumo na mipangilio ya kila vipindi kwa kupendekeza atazame kipi gani, muda gani na wakati gani?.

King’amuzi cha “DStv HD, mteja anaweza kujipangia atazame kipindi gani ama kwa wakati autakao yeye, ambapo anachoweza ni kuseti hicho kipindi akipendacho na kisha anaweza kukiangalia kwa wakati wake, hata kama muda umepita kwa wakati huo kinarushwa kwenye chaneli husika” alifafanua Ronald Shelukindo.

Kwa upande wake, Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania, Furaha Samalu aliwahimiza watanzania kuchangamkia vinga’muzi hivyo vya DStv HD, ambavyo kwa sasa vipo karibu maduka yote ya Mawakala wa DStv, kwa bei rahisi kabisa vikiwa vinapatikana kwa sh 99,000/ kwa mteja mpya huku kwa wateja walio na ving’amuzi vya zamani vya DStv watakaotaka kubadilishiwa, watalipia sh 39,000/ tu.
Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo akionesha king'amuzi kipya cha DStv HD kwa waandishi wa habari (hawapo pichani).

“Ofa hii ni kwa ajili ya kipindi hiki cha fainali za AFCON, hadi hapo michuano hii itakapofikia tamati ambapo bei itabadilika kutoka hizi za sasa, hivyo ni wakati wa kuchangamkia ofa hii ya kipekee na kwa mara ya kwanza, kupata kitu cha ubora wa hali ya juu na kwa bei rahisi.” Alisema Furaha Samalu.

Kwa upande wake, Afisa Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi alieleza kuwa, siku zote MultiChoice itaendelea kuwa mstari wa mbele kwa kutoa huduma zilizo bora na za kisasa katika ulimwengu huu wa digitali ambapo bidhaa hizo za DStv zimeendelea kuwa bora kila siku.

“Huduma za DStv siku zote zimekuwa bora ikiwemo kutoa huduma zisizoleta usumbufu. Ving’amuzi vyetu daima vinaonyesha ubora wa hali ya juu na hutoweza kusumbuliwa na ukatikaji wa picha ama mikwaruzo... Hivyo ni wakati sasa wa kuchangamkia ofa hizi.” Alibainisha Barbara Kambogi.
Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu akifafanua bei za king'amuzi hicho kipya ambapo kwa wateja wapya watajipatia kwa ofa ya Tsh. 99,000/ kuanzia leo hadi siku Jumapili kilele cha fainali za michuano ya AFCON huku ambao ni wateja tayari wanabadilishiwa kwa gharama ya Tshs. 39,000/ ambayo pia ni ofa. Ving'amuzi hivyo vipya vya DStv HD vinapatikana kupitia mawakala wote wa DStv Tanzania nzima.

Katika hatua nyingine, DStv wamezindua huduma mpya kwa wateja wao waliounganishwa na ving’amuzi hivyo vya DStv kuweza kuendelea kufurahia huduma hiyo kupitia simu zao za viganjani zenye uwezo wa ‘Android’, Kompyuta mpakato (Laptop), Tablet, na vifaa vingine vyenye uwezo wa kupokea usajili wa ‘App’.

Akielezea, juu ya huduma hiyo, Ronald Shelukindo, alibainisha kuwa, kinachotakiwa ni kwa mteja wa DStv, kwenda kwenye simu yake au Laptop, ama Tablet na kisha kujisajili kupitia ‘App’ kwa kujisajili kwa kuandika ‘DStv Now’.

Aidha, Ronald Shelukindo alisisitiza kuwa, huduma hiyo ya DStv Now ni kwa wateja waliouganishwa na ving’amuzi hivyo tu ambapo wataifurahia huduma hiyo kwa kuendelea kuangalia chaneli zaidi ya 12 za DStv, ikiwemo ya Super Sport 3, za filamu, na nyinginezo mbalimbali.

Pia kwa maelezo zaidi wateja wanaweza kutembelea tovuti ya DStv.com
Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo akionesha huduma mpya ya DStv Now ambayo mteja ataweza kuangalia vipindi vya DStv kupitia simu yake ya kiganjani, kompyuta mpakato (Laptop) pamoja na Tablet. Huduma hii ni kwa wateja ambao wameunganishwa na ving'amuzi vya DStv kupitia akaunti zao.
Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi (katikati), Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo (kulia) na Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu (kushoto) wakiangalia promo ya namna ya kujiunga na huduma ya DStv Now "application" inayopatikana katika simu zote za Android pamoja na kompyuta mpakato (Laptop) unajiunga kwa kutembelea www.dstv.com
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakifuatilia uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar leo.
Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo (katikati) na Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu (kulia) na Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi (kushoto) wakipozi na king'amuzi kipya cha DStv HD.

RAIS KIKWETE AONGOZA SHEREHE ZA SIKU YA SHERIA NCHINI LEO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia katika sherehe za Siku ya Sheria
nchini katika viwanja wa Mahakama barabara ya Chimala jijini Dar es
salaam leo February 4, 2015


PICHA NA IKULU

SUPER STAR "OMMY DIMPOZ " LIVE IN NEW YORK CITY SATURDAY FEB 21 (RED CARPET AFFAIR )

$
0
0
PERFORMING HITS LIKE -NAI NAI / BAADAE /ME &YOU /TUPOGO /NDAGUSHIMA/ 
KIGOMA/ RADIO/ MISS KOI KOI/ CHUKUA TIME /NUMBER ONE AND MORE
                                     * KIINGILIO  $ 40 ADVANCE   |  MLANGONI $ 50 *
                                                                   ( INCLUSIVE OF )
                           *RED CARPET ENTRANCE  PHOTO SHOOT (FROM 5PM-6PM*
                                                              *3 -COURSE DINNER *
                                                                    *SOFT DRINKS *
                                                *ELEGANT SETTINGS AND SERVICES*
                                             * POZ KWA POZ LIVE ENTERTAINMENT*
                                    *CASH BAR - BEER $3   | LIQUOR $5   | WINE  $5  *
                       *TICKETS & MORE INFO CALL- 347-663-0781  |  917-698-6943 *

     ************************************************************************
 ============================================================

Binti Kiziwi wapo wengi lakini wamepotelea wapi basi jikumbushe na hii

Viewing all 45982 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>