Quantcast
Channel: VIJIMAMBO
Viewing all 45982 articles
Browse latest View live

WIZARA YAWATAKA WAMILIKI WA VYOMBO VYA HABARI KUWAKATIA BIMA WAFANYAKAZI WAO

$
0
0
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia akijibu swali Bungeni mjini Dodoma.
Na Lorietha Laurence-Maelezo Dodoma.


Naibu Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia amewataka wamiliki wa vyombo vya habari kuwakatia wafanyakazi wao bima ili ziweze kuwasaidia wakati wanapopatwa na madhara wakiza kazini.


Akijibu swali la mbunge wa viti maalum Anna Mallac, kuhusu mpango wa Serikali kuwapatia ulinzi waandishi pale wanapokuwa wakifanya kazi katika matukio hatari, Naibu Waziri Nkamia alisema kuwa serikali inafahamu mazingira ya kazi ya wanahabari na inawajibika kikatiba katika kutoa ulinzi kwa raia wake wote wakiwemo wanahabari.


“Uandishi wa habari ni taaluma kama zilivyo taaluma nyingine muhimu katika jamii kama ilivyo taaluma ya sheria ualimu na udakatari na ni muhimu kufahamu na kuzingatia miiko ya taaluma pale wanapokuwa katika eneo la kazi”alisema Nkamia.


Aidha alibainisha kuwa jukumu la kwanza kwa waandishi wa habari ni kujilinda na kujihami wao wenyewe kwa kuwa wanayafahamu mazingira yao ya kazi na pia kuzingatia miiko ya taaluma yao kwa kuangalia wanayotakiwa kufanya na kutofanya katika eneo husika. Aliongeza kuwa wanahabari wanatakiwa wazingatie sheria bila shuruti kwa kuwa nao ni wananchi kama walivyo wananchi wengine na hakuna aliye juu ya sheria .


Hata hivyo Serikali imekuwa ikiwapatia waandishi wa habari vifaa maalum katika matukio mbalimbali ya kitaifa ikiwemo vitambulisho na mavazi maaalum ya kuwatambulisha wakiwa katika eneo la kazi ikiwa ni mojawapo ya njia ya kuwalinda na madhara yeyote.


Naibu Waziri Nkamia alieleza kuwa kwa sasa wizara yake imekuwa ikiandaa muswada wa sheria ya vyombo vya habari ambao utawasilishwa mbugeni wakati wowote kuanza sasa. 
SOURCE:JIACHIE

HABARI KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA LEO

$
0
0
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhandishi Athumani Mfutakamba akisoma taarifa ya kamati hiyo kwa niaba ya mwenyekiti wa kamati hiyo bungeni mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, Jasson Rweikiza akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge yaMasuala ya Ukimwi Lediana Mng'ong'o akiwasilisha taarifa ya kamati yake.
Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete akiuliza swali wakati wa kipindi cha maswali na majibu Bungeni mjini Dodoma.
Baadhi ya wageni waliofika kwenye Bunge la Jamhuri wakifuatilia Bunge.
Baadhi ya wabunge wakitoka nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba (wa pili kushoto) akibadilishana mawazo na baadhi ya wabunge nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma akiwemo Mbunge wa Morogoro Kusini Dkt. Lucy Nkya (kushoto) na kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, Jasson Rweikiza.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Mhe. Kapt (Mstaafu) George Mkuchika (wa pili kulia) akibadilishana mawazo na baadhi ya wabunge kwenye mlango wa Bunge mjini Dodoma.Picha zote na Hussein Makame-MAELEZO,Dodoma

SINGLE MPYA YA DIAMOND MARADHI YA MOYO JITIRIRISHR HAPA KIMYA MIMYA

ALIKIBA NA SINGLE YA WIFE WA DUNIA HII HAPA JITIRIRISHE KIROHO SAFI

Calling all Medical and Dental professionals and non-medical compassionate people!

$
0
0

Calling all Medical and Dental professionals and non-medical compassionate people!
Have you ever wondered what it would be like to practice medicine in a remote village in a third world country where you would rely on your skills, observation and your gut instinct?  Join us as we travel to Tanzania, Africa, to provide medical assistance in a humanitarian effort in May 18-28, 2015.   Teri Priebe and Becky Van Renan will escort this important mission.  The approximate all-inclusive land price is $2,500 per person. Teri can help you with your flight arrangements (estimated rate from Washington Dulles is $1,300).
This opportunity will provide a stimulating challenge with the chance to diagnose and treat people with just a hand full of test equipment and a few bags of medicine.  You may encounter some of the things that you have only read about in medical books.
There is a need for non-medical volunteers as well.  You could help distribute vitamins and toothbrushes, assist in testing and fitting eyeglasses, teach how to effectively brush teeth or wash hands, help with crowd control or serve as a runner for supplies.  The most important task is showing the people that you really care. 
If you join us on this humanitarian venture, you will spend 9 days in Tanzania;   4-5 days of mobile clinics and 4 days of enjoying the friendly people and beautiful countryside, including a 2-day safari to the world famous wildlife reserves!  We'll also enjoy a cultural visit to the fascinating Maasai.
The All-Inclusive Land price includes:
--8 nights' accommodations
--All meals (3 per day) & bottled water
--2 day safari including All Park and Conservation fees and Safari Vehicles
--Maasai Village visit
--All ground transportation while in Africa
--Tanzania Visa fee

For more information or to reserve your place in this humanitarian effort, contact:
Becky Van Renan             540-972-9264                     sokrmom21@gmail.com
Teri Priebe                         540-760-8178                     priebe.teri@gmail.com
Iddi Sandaly                      301-613-5165                     isandaly@watanzaniadmv.org



Travel arrangements made through King George Travel, 540-663-2718.



Filamu:Nunua au Angalia Vipindi Vya TMT Season 1.

UNAAMBIWA MGANGA ANASWA LIVE GUEST NA WAKE ZA WATU USIKU WA MANANE...ETI ANAWAPA DAWA YA MAPENZI.

$
0
0

Mganga wa jadi almaarufu sangoma aliyetajwa kwa jina la Wadebi akijutia baada ya kunaswa live. Tukio hilo la aina yake lilijiri maeneo hayo, usiku wa manane wa kuamkia Jumanne iliyopita, wakati waumini wa Dini ya Kiislamu waliofunga kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani wakila daku.

Kwa mujibu wa mashuhuda, jamaa huyo alidaiwa kuwa alikuwa akiwafanyia wake hao wa watu dawa ya mapenzi kwa kuwavua nguo zote kisha ‘kuwachezea’.
Ama kweli uswazi hakuishi vijimambo! Mganga wa jadi almaarufu sangoma aliyetajwa kwa jina la Wadebi Jinasa amepata aibu ya karne baada ya kunaswa ‘live’ na wake za watu kwenye gesti moja (jina linahifadhiwa) iliyopo Tandika jijini Dar es Salaam.
Sangoma amekuwa akiwavuta wanawake wengi kwa kuwatajia matatizo yao sawia bila kukosea. Ilidaiwa kuwa mbali na kuwachezea, amekuwa akiwafanyia mchezo usiofaa mmoja baada ya mwingine.Chanzo cha sakata hilo kilidai kuwa sangoma huyo amekuwa na tabia hiyo hasa akimuona mwanamke mwenye mvuto katika hali ambayo haikueleweka mara moja humuita majina yake matatu, yaani la kwake, baba hadi la babu yake, jambo linalosababisha anayeitwa kushtuka na kuhisi mtu huyo atakuwa anamfahamu kiundani. 

Ilidaiwa kuwa baada ya mwanamke huyo kusimama huanza kumwelezea matatizo yake na kumtajiwa hadi matatizo yanayowapata ndugu zake walio vijijini na sehemu nyingine za mbali. 

Kiliendelea kudai kwamba, sangoma huyo amekuwa akiwavuta wanawake wengi kwa kuwatajia matatizo yao sawia bila kukosea hivyo kuwachanganya na kumjengea imani kuwa ni ‘fundi’ wa masuala hayo.
Kufuatia vituko vyake, juzikati mume wa mwanamke mmoja (jina linahifadhiwa), Huruka Hassan alirejea nyumbani kwake na kukuta mkewe hayupo.Alidai alipofanya uchunguzi wa haraka, aligundua ameenda kwenye gesti hiyo kupata tiba.
Ilidaiwa kwamba, siku zote Huruka amekuwa akimuacha mkewe akapate tiba lakini siku ya tukio machale yalimcheza, alipofika kwenye gesti hiyo alijibanza ukumbini na kusikia sauti ya mkewe ikinong'ona chumbani na sauti ya 'besi' la sangoma huyo kwa mbaaali.
Ilisemekana kwamba uzalendo ulimshinda Huruka na kujikuta akivunja masharti ya kilinge cha sangoma huyo kwa kuchungulia kwenye tundu la kupitisha funguo."Haaamadi!" alisikika Huruka alimuona laivu mkewe akiwa mtupu akitaka kufanyiwa vitendo vichafu ambapo sangoma huyo alidaiwa kuwa alikuwa akjiandaa kumfanyia ‘amshaamsha’.
Ilidaiwa kuwa Huruka alishindwa kujizuia, akagonga mlango kwa hasira ambapo sangoma alivaa 'chapchap' na kufungua.Ilielezwa kwamba walipokutana uso kwa uso, Huruka alitunishiana misuli na sangoma huyo wakataka kuzichapa lakini jamaa akaona amchukue mkewe na kutimka naye. 

Baada ya mke wa Huruka kuokolewa kufanyiwa ukenge, mwanamke mwingine wa eneo hilo, Tabu Abdallah naye alidai kumnasa mkewe kwenye gesti hiyo akiwa amekalishwa kama alivyozaliwa, akitolewa vitu fulani tumboni na sangoma huyo. 

Akizungumza na Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publisher ambayo ilifika eneo hilo usiku baada ya kutonywa na chanzo chake, Tabu alisema alimnasa mkewe na sangoma huyo baada ya kutonywa juu ya mkewe kuingia gesti hiyo. 
Alisema sangoma huyo alimchukua mkewe kwa gia ya kumtibia kumbe alikuwa na lake jambo.

Baada ya kutokea kwa mtiti huo, Mjumbe wa Shina namba 29, Azimio-Tandika, Faraj Neto, wanawake waliodhalilishwa, waume zao, polisi na mmliki wa gesti hiyo, Ebenezer Ngowo, walimchomoa sangoma huyo kwenye gesti hiyo. 

Katika hali ya kushangaza mke wa Tabu alikuwa akimlaumu mumewe kwa kutaka kumpiga mganga wake ambaye alikuwa akitaka kummalizia matatizo huku wanawake wengine wakiwaomba radhi waume zao na kudai walirubuniwa. 
Akizungumizia mkasa huo mke wa Tabu alisema kuna siku alikutana na mganga huyo njiani ambapo alimwita majina yake matatu, aliposimama kumsikiliza ndiyo akaanza kumtajia matatizo yake, jina la mama yake mzazi na kumwambia mama huyo huko aliko ana tatizo sugu la miguu jambo ambalo ni kweli ndipo alianza kumuamini. 

MWISHO WA SAKATA 

Mwisho wa sakata hilo, mjumbe wa nyumba kumi alimtaka sangoma huyo kuondoka eneo hilo na mmiliki wa gesti hiyo alimtaka mganga huyo kuhama kwenye gesti yake kutokana na tabia yake ya kubadilisha wanawake. 

Kwa upande wao, polisi walimshikilia sangoma huyo kutokana na sababu za kiusalama kufuatia wenye wake na wananchi wenye hasira kutaka kumpiga mawe na kumuua. 

SAOURCE-GPL

UNAJUA ALICHOKISEMA ALI CHOKI NA ASHA BARAKA BAADA YA KUPATANA? UNGANA N...


INCOME TAX SERVICES

$
0
0

Seruwage Consulting and CPAs specializing in providing quality bookkeeping, accounting, tax and consulting services. We offer a comprehensive Bookkeeping, Accounting, Tax and Consulting Services with the inside knowledge only accountants can provide. Contact us at info@seruwagecpas.com or 301-613-5165.


If You Work, The Earned Income Tax Credit Can Work For You!

The Earned Income Tax Credit has helped workers with low and moderate incomes get a tax break each year. Four out of five eligible workers claim EITC, but the IRS wants everyone who is eligible to claim this credit. Here are some things you should know about this valuable credit:

• Review your eligibility.  If you worked and earned under $52,427, you may qualify for EITC. If your financial or family situation has changed, you should review the EITC eligibility rules. You might qualify for EITC this year even if you didn’t in the past. If you qualify for EITC you must file a federal income tax return and claim the credit to get it. This is true even if you are not otherwise required to file a tax return. Don’t guess about your EITC eligibility. 

• Know the rules.  You need to understand the rules before you claim the EITC, to be sure you qualify. It’s important that you get this right. Here are some factors you should consider:
o Your filing status can’t be Married Filing Separately.
o You must have a Social Security number that is valid for employment for yourself, your spouse if married, and any qualifying child listed on your tax return.
o You must have earned income. Earned income includes earnings from working for someone else or working for yourself.
o You may be married or single, with or without children to qualify. If you don’t have children, you must also meet age, residency and dependency rules. If you have a child who lived with you for more than six months of 2014, the child must meet age, residency, relationship and the joint return rules to qualify.
o If you are a member of the U.S. Armed Forces serving in a combat zone, special rules apply.

• Lower your tax or get a refund.  The EITC reduces your federal tax and could result in a refund. If you qualify, the credit could be worth up to $6,143. The average credit was $2,407 last year.

•  If you do your own taxes, the best way to file your return to claim EITC is to Efile. Software will figure your taxes and EITC for you. Combining e-file with direct deposit is the fastest and safest way to get your refund. 


If you have questions call me at 301-613-5165.
Iddi Sandaly, CPA

      KIJANA ANUSURIKA KUUAWA KISA WIZI MAMA AINGILIA KATI KUMUOKOA KIFO

      $
      0
      0


      Kijana mmoja mkazi wa Kigogo Sukita jijini Dar es Salam ameambulia kipigo kizito kutoka kwa wananchi wenye hasira kali na kufikia hatua ya kutaka kumchoma moto kutokana na kitendo cha kumuibia simu na shilingi elfu therasini mwanadada ambaye naye ni mkazi wa eneo hilo.

      Kutokana na kipondo cha aina yake alichokuwa akipewa na wananchi hao wenye hasira kali walionekana kumpania kutokana na vitendo vyake vya wizi wa mara kwa mara na kutokana na kipigi hicho kilichomfanya atapakae damu mwilimzima, mama yake mzazi aliamua kuingilia kati ili kumuokoa mwanaye ambapo naye alionja joto ya jiwe. 

      Kutokana na timbwili hilo la aina yake, mama huyo aliendelea kumshikilia mwanye huyo kana kwamba aliyekuwa tayari kwa lolote ilimradi amnusuru na kifo.

      "UZIMA ULIAZIMWA TUNZA NI HAZINA"

      $
      0
      0

      TIMU YA NesiWangu IKISHIRIKIANA NA AFRICAN AMERICAN HEALTH PROGRAM INAWAKARIBISHA NYOTE KATIKA UCHUNGUZI WA AFYA YA MOYO 

      Tarehe 7/2/2015 Saa 3:00 asubuhi hadi 7:00 mchana

      Silver Spring 1 Veterans Place( Civic Center) 

      Parking ni bure katika garage siku ya Jumamosi

      HII NDIYO TOFAUTI YA MAKABURI YA AFRICA NA ULAYA

      $
      0
      0


      Makaburi ya Africa yanakuwa na mlima kama hivi sehem ya makaburi huko Africa inaogopeka sana uwezi kupita usiku na ukipita utashikwa na woga hasa vijijini ni shida hata kujenga nyumba karibu na makaburi hakuna rangi utaacha kuona.
      Mjini makaburi hata hayana mlima kama ya Africa na unaweza kupita na ata kulala kama umezidiwa na usingizi bila kuogopa.

      SUGE KNIGHT AKIMBIZWA HOSPITALI BAADA YA KUSHIKWA NA MAUMIVU YA KIFUA AKIWA MAHAKAMANI WAGA HUO

      $
      0
      0
      Suge Knight akiwa ndani nguo za magereza akiwa mahamani kwa kesi ya mauaji ya kumua rafiki yake na kesi nyingine ya kugonga na kuua mtu mwingine kwa gari na kukimbia. Na ikumbukwe pia ni huyu huyu ndiyo kuhusichwa na kifo cha 2Pac mwaka 96 walivyokuwa pamoja kwenye kampuni ya Death Row Records.
       Suge Knight anashikiliwa kunzia ijumaa kwenye magereza ya Central huko Los Angeles, baada ya yeye mwenyewe kujisalimisha  West Hollywood Sheriff's Station na amekana mashitaka yanayomkabili.
      Suge Knight mwenye umri wa miaka 49 je atajinasua kwenye hili siku zote wanasema kuwa malipo ni hapa hapa duniani 2pac aliuwawa huku kukiwa na kiza kinene cha nani amemuua na huyo ndiyo alihusishwa sana wakati wa kifo cha 2pac kutokana na ukaribu ambao walikuwa nao.
      Hapa Suge Knight akiwa na marehemu 2Pac enzi hizo
      Suge Knight akiondoka mahakamani na baada ya hapa alipandishwa kwenye ambulance na kukimbizwa hospitali baada ya kushikwa na kifua ghafla akiwa kwenye chumba cha mahakama inasemekana ni panic attack. Akitoka hospitalini anarudishwa moja kwa moja jail kwani hakuna mdhamani kutokana na record yake mbaya na akikutwa na hatia juu ya kesi hii ni jail maisha.

      IBADA MAALUM YA MAZISHI YA BABA MPENDWA WA MAMERTHA NA HENRY KENTE

      $
      0
      0
      Mr. & Mrs. Deo Mosha wanawakaribisha kuungana nao kwenye Ibada maalum ya mazishi ya Baba Mpendwa wa Mamertha na Henry Kente aliyefariki Jumapili, Dar-es-Salaam, Tanzania. Ibada itakua kesho, Jumatano tar. 4/2/2014 kuanzia saa moja kamili jioni (7:00pm) nyumbani kwao. Address ni 
      4402 Hatties Progress Dr. Bowie, MD 20720. Kwa habari zaidi, wasiliana na 
      Deo Mosha-240 441 8433
      Vitalis Gunda 240 383 6950
      Mrs. Gloria Semiti 301 325 1843
      Tafadhali zingatia muda.
      Karibuni wote.

      Ferooz - Starehe jipakulie na hii na kumbuka ulikuwa wapi wewe


      TIC YAKUTANA NA UJUMBE WA WAFANYABIASHARA KUTOKA NCHINI UJERUMANI

      $
      0
      0
      Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC),Juliet Kairuki (wa pili kushoto) akizungumza katika mkutano maalum kati ya Uongozi wa TIC na ujumbe wa wafanyabiashara kutoka nchini Ujerumani,wenye lengo la kuhamasisha na kukuza Uwekezaji na biashara kati ya Tanzania na Ujerumani,uliofanyika jana jioni kwenye ukumbi wa Mikutano ya kituo hicho,jijini Dar es salaam.Ujumbe huo unaongozwa na Waziri wa Masuala ya Kiuchumi na Nishati wa nchini Ujerumani,Mh. Matthias Machnig (wa pili kulia).
      Mratibu wa Uwekezaji wa Kimataifa wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC),Zacharia Kingu akifafanua jambo wakati akiwasilisha taarifa ya uwekezaji katika maeneo mbali mbali nchini wakati wa mkutano maalum kati ya Uongozi wa TIC na ujumbe wa wafanyabiashara kutoka nchini Ujerumani,wenye lengo la kuhamasisha na kukuza Uwekezaji na biashara kati ya Tanzania na Ujerumani,uliofanyika jana jioni kwenye ukumbi wa Mikutano ya kituo hicho,jijini Dar es salaam.
      Ujumbe wa wafanyabiashara kutoka nchini Ujerumani pamoja uongozi wa TIC ukifatikia kwa makini taarifa ya uwekezaji iliyokuwa ikitolewa na Mratibu wa Uwekezaji wa Kimataifa wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC),Zacharia Kingu (kushoto).

      Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC),Juliet Kairuki (katikati) akitoa ufafanuzi wa maswala mbali mbali ya uwekezaji kwa ujumbe wa wafanyabiashara kutoka nchini Ujerumani waliotembelea kituo hicho jana jioni,jijini Dar es salaam.
      Kiongozi wa Msafara wa Wafanyabiara hao ambaye ni Waziri wa Masuala ya Kiuchumi na Nishati wa nchini Ujerumani,Mh. Matthias Machnig akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC),Juliet Kairuki. 
      Meneja wa Kitengo cha Uratibu Miradi ya Ubia (Sekta ya Umma na Binafsi) wa TIC,Said Amir akitoa ufafanuzi juu ya maswala ya ubia katika miradi,wakati wa mkutano maalum kati ya Uongozi wa TIC na ujumbe wa wafanyabiashara kutoka nchini Ujerumani,wenye lengo la kuhamasisha na kukuza Uwekezaji na biashara kati ya Tanzania na Ujerumani,uliofanyika jana jioni kwenye ukumbi wa Mikutano ya kituo hicho,jijini Dar es salaam.
      Kaimu Mkurugenzi wa Masuala ya Ushirika wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC),Revocatus Arbogust akichangia jambo katika mkutano huo.
      Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC),Juliet Kairuki (katikati) akifafanua jambo katika mkutano maalum kati ya Uongozi wa TIC na ujumbe wa wafanyabiashara kutoka nchini Ujerumani,wenye lengo la kuhamasisha na kukuza Uwekezaji na biashara kati ya Tanzania na Ujerumani,uliofanyika jana jioni kwenye ukumbi wa Mikutano ya kituo hicho,jijini Dar es salaam.
      Kiongozi wa Msafara wa Wafanyabiara hao ambaye ni Waziri wa Masuala ya Kiuchumi na Nishati wa nchini Ujerumani,Mh. Matthias Machnig akizungumza na mmoja wa wafanyabiashara aliofatana nao.
      Sehemu ya Wafanyabiashara hao wakifatilia kwa makini taarifa ya uwekezaji.
      Sehemu ya Ujumbe wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) ukifatilia kwa makini mkutano huo.
      Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC),Juliet Kairuki (wa pili kushoto) akiongea na ujumbe huo wakati akiwaonyesha moja ya Jengo lilalotumiwa Kituo hicho lililojengwa na Wajerumani.
       Picha zote na Othman Michuzi.

      First lady wa Rais wa Ujerumani, Bi Daniella Schadt atembelea Dawati la Jinsia na Watoto katika Kituo cha Polisi Temeke leo.

      $
      0
      0
      Mke wa Rais wa Ujerumani, Bi Daniella Schadt akisalimiana na maofisa wa Jeshi la Polisi wakati alipotembelea Dawati la Jinsia na Watoto katika Kituo cha Polisi Cha Temeke leo.
      Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto kutoka Jeshi la Polisi Tanzania, DCP Adolphina Chialo akitoa ripoti ya dawati la jinsia na watoto tokea kuanzishwa kwake wakati mke wa rais wa Ujerumani Bi Daniella Schadt alipotembelea dawati la jinsia na watoto katika Kituo cha Polisi cha Chang'ombe kilichopo Temeke.

      Baadhi ya wafanyakazi wa UNICEF, Viongozi wa Jeshi la Polisi pamoja na wadau wakisikiliza kwa makini ripoti fupi iliyokuwa ikitolewa na Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto kutoka Jeshi la Polisi Nchini, DCP Adolphina Chialo (hayupo pichani).
      Mke wa Rais wa Ujerumani, Bi Daniella Schadt akipelekwa katika ofisi ya Dawati la Jinsia na Watoto iliyopo katika kituo cha Polisi Chang'ombe Temeke wakati alipotembelea kituo hiko kuona jinsi Dawati hilo linavyofanya kazi.
      Mke wa Rais wa Ujerumani, Bi Daniella Schadt akibadilishana mawazo na ripota vijana wa UN kabla ya kufanya nao mahojiano mara baada ya kumaliza kuongea na viongozi wa dawati la jinsia na watoto katika Kituo cha Polisi Temeke.
       
      Ripota vijana wa UN wakifanya mahojiano na Mke wa Rais wa Ujerumani, Bi Daniella Schadt mara baada ya kumaliza kutembelea ofisi ya Dawati la Jinsia na Watoto katika Kituo cha Polisi Temeke.
      Akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa wa Jeshi la Polisi, ripota vijana wa UN.Picha na Josephat Lukaza - Lukaza Blog

      OLOLOSOKWAN WAPIGWA MSASA KUKITUMIA VYEMA KIJIJI CHA DIJITALI

      $
      0
      0

      Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Bw. Al Amin Yusuph akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues (aliyeipa mgongo kamera) wakati wa ukaguzi wa mwisho wa eneo la mradi wa kijiji cha digitali wa Samsung unaoendeshwa na UNESCO lilitolewa na serikali ya kijiji. Katikati ni Mwenyekiti wa kijiji cha Ololosokwan wilaya ya Ngorongoro, Kerry Dukunyi .(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)

      Na Mwandishi wetu, Ngorongoro

      SHIRIKA la Elimu ,sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa, UNESCO, limeanza maandalizi ya kuumilikisha mradi wa kijiji cha digitali cha Ololosokwan kwa wananchi wa kijiji hicho kwa kuendesha warsha ya siku mbili ya kutambua vipaumbele vya wananchi vitakavyoingizwa katika mradi huo.

      Vipaumbele hivyo ni katika elimu, afya na uchumi.

      Warsha hiyo ilishikirikisha wanakijiji wa Ololosokwan na vijiji vingine vinavyozunguka kijiji hicho,viongozi wa halmashauri, viongozi wa kimila, viongozi wa vijiji na wataalamu mbalimbali wa sekta ya afya, elimu na uchumi.

      Katika majadiliano yao wananchi walitambua changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo ambazo zina uhusiano wa moja kwa moja na mazingira na mfumo wa utamaduni walionao wakazi wa eneo hilo.

      Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akikagua eneo la mradi wa kijiji cha kidigitali Ololosokwani wilayani Ngorongro. Kushoto ni Mwenyekiti wa kijiji cha Ololosokwan, Kerry Dukunyi na Mratibu wa miradi wa Taasisi ya Irkiramat, Salanga Mako.

      Wakazi hao ambao ni wafugaji wenye kuheshimu mila na utamaduni wa kimasai na mfumo wa maisha wamesema kwamba lugha inayotumika katika kufundishia ni tatizo na ingawa wana shule mbili za msingi na sekondari lugha ya Kiswahili ni tatizo na wakifika sekondari lugha ya kiingereza nayo inakuwa tatizo.

      Aidha walisema kutokana na wazazi kutokuwa na elimu hawaoni sababu ya kuwafanya watoto wao wenye maarifa makubwa kwenda shule na badala yake hao wanaoelewa vitu hupelekwa kuchunga au wale wenye umri mdogo wa kike huolewa.

      Warsha hiyo pia ilibainisha tatizo la afya ya wanawake na watoto, ndoa za utotoni na magonjwa ya zinaa ya kuambukiza.

      Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akiteta jambo na ujumbe wake aliombatana nao kwenye kijiji cha Ololosokwan kwa ajili ya kuwapiga msasa wananchi wa kijiji hicho ikiwa ni maadalizi ya kupokea mradi wa kijiji cha kidigitali hivi karibuni.

      Kijiji hicho cha digitali ambacho ni nadharia ya Samsung katika kurejesha faida kwa umma kitakuwa na huduma mbalimbali ambazo zikiunganishwa na haja ya wananchi zitasaidia kubadili maisha ya wamasai na kuondokana na utegemezi wa mifugo pekee na kutambua thamani yao katika rasilimali zilizopo katika maeneo yao.

      Warsha hiyo ambayo imesimiwa na wataalamu kutoka UNESCO imelenga kuwafungua macho na kuwashirikisha wananchi kuhusu mradi huo mkubwa wa aina yake nchini na duniani.

      Kijiji cha dijitali nchini Tanzania ni cha nne cha kwanza kikiwa nchini Afrika Kusini, kingine Gabon na Ethiopia.

      Baadhi ya wanakijiji wa Ololosokwan na vijiji vingine vinavyozunguka kijiji hicho,viongozi wa halmashauri, viongozi wa kimila, viongozi wa vijiji na wataalamu mbalimbali wa sekta ya afya, elimu na uchumi wakimsikiliza Mkurugenzi mkazi wa UNESCO, Zulmira Rodrigues (hayupo pichani).

      Kijiji hicho ili kiwe endelevu wananchi wanaohusika wanatakiwa kuelewa mradi huo kuweka vipaumbele vyao na kuangalia jinsi ya kutumia mradi huo katika kukabili changamoto zinazowakabili kwa sasa.

      Katika majadiliano kwenye ngazi za elimu wananchi walielezea haja ya kushawishi wamasai kuanza kujifunza Kiswahili na Kiingereza ili kuweza kufuatilia kwa karibu masomo na pia kuwepo kwa sheria ndogo ili kuzuia utoro wa wanafunzi kwa ajili ya kwenda kuchunga mifugo na pia kuolewa mapema kwa mabinti.

      Mathias Herman, mratibu wa program za Afya , UNESCO, alisema kwamba pamoja na kwamba kijiji hicho kitakuwa na zahanati na huduma za mawasiliano ya tiba (telemedicine) hamasa kubwa inatakiwa kutolewa ili wananchi waweze kutumia huduma hizo kwani kwa sasa wamejikita zaidi huduma za waganga wa jadi.

      Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akiendesha mjadala kwa wanakijiji wa Ololosokwan na vijiji vingine vinavyozunguka kijiji hicho,viongozi wa halmashauri, viongozi wa kimila, viongozi wa vijiji na wataalamu mbalimbali wa sekta ya afya, elimu na uchumi ikiwa ni maandalizi ya kuupokea mradi wa kijiji cha kidigitali Ololosokwani wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.

      Alisema katika warsha kulielezwa kuwa kukosekana kwa madaktari katika zahanati zilizopo kijijini hapo kumefanya watu wengi kuendelea kuamini waganga wa jadi na kujifungulia huko hali ambayo imezaa kuwapo kwa idadi kubwa ya wanawake wanaokufa wakati wa uzazi na pia watoto wasiopata chanjo.

      “Wakifika hakuna madaktari hawawezi kuamini huduma hii wakati kuna waganga wa kienyeji na wakunga wa kienyeji” alisema Mathias na kuongeza kuwa katika warsha ilihimizwa kwamba watu watambue tatizo lililopo la kiafya linalosababishwa na mfumo wa mazingira na maisha ya wafugaji na kuhakikisha kwamba huduma zinazoletwa zinatumiwa vyema.

      Aidha alisema kuwapo kwa kiwango kikubwa cha maambukizi ya magonjwa ya zinaa, ndoa za utotoni na mimba katika umri mdogo ni sehemu ya matatizo ambayo yanaaminika kwamba yanaweza kutanzuliwa kwa kutolewa elimu na kushawishi wakubwa wa mila kutambua nafasi zao na elimu ya kisasa katika kushughulikia changamoto za kiafya.

      Afisa mipango ya Elimu wa Shirika la UNESCO, Bi. Jennifer Kotta (kulia) akiwa kwenye majadiliano na baadhi ya wanakijiji wa Ololosokwan kuhusiana na changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu na nini kifanyike kuboresha sekta ya elimu kwa ujumla katika kijiji hicho na kuishirikisha halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro katika maandalizi ya kupokea mradi wa kijiji cha kidigitali.

      “mila na heshima kwa wakubwa wa mila kumefanya wamasai kutegemea tiba za asili na mfumo wa asili wa kuendesha maisha bila kujua athari kwao ziwe hasi au chanya” alisema Mathias kauli iliyoungwa mkono na Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO, Zulmira Rodrigues ambaye alisema kunahitajika sana ushirikiano wa jamii, viongozi, wazazi kuhakikisha kwamba kijiji kinafanikiwa na kuwa cha kupigiwa mfano.

      Kijiji cha Ololosokwan kilichopo Loliondo, wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha kikiwa na watu 9000 kupitia mradi huo kitapewa pia mbinu za kuimarisha soko la utalii, kulitambua na kulitumia kwa manufaa yao na pia elimu ya ubunifu ambayo itawafanya wanawake wanaotengeneza urembo mbalimbali kuweza kumudu soko la utalii na la kawaida.

      Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Bw. Al Amin Yusuph akiendesha mjadala na baadhi ya wanakijiji wa Ololosokwan kuhusiana mradi wa kijiji cha kidigitali na kuuboresha ili kutatua matatizo ya wananchi pamoja na kuwapata taarifa za maendeleo kupitia redio jamii ya Loliondo FM inayofadhiliwa na UNESCO ikiwa ni katika maandalizi ya kuupokea mradi huo wa kijiji hicho unaotarajiwa kuwasili hivi karibuni kijijini hapo.

      Aidha mradi huo utafikisha umeme na elimu kwa njia ya Tehama huku, elimu hiyo ya Tehama ikikusudiwa kutumika kutoa elimu ya darasani kwa wanafunzi ambao wapo machungani.

      Mfumo wa wamasai ambao umejengwa katika utamaduni na kuthamini mifugo unatakiwa kubadilishwa kwa wazazi kupewa elimu ya kuwawezesha kutambua umuhimu wa elimu kwa watoto wao.


      Afisa Mradi wa Elimu ya Afya na VVU/UKIMWI kutoka UNESCO, Bw. Herman Mathias akiongoza mjadala wa nini kifanyike katika kuboresha sekta ya afya na changamoto zinazowakabili wanakijiji wa Ololosokwan kwa ajili ya maandalizi ya kuupokea mradi wa kijiji cha Kidigitali unaoendeshwa na UNESCO kwa kushirikiana na kampuni ya Ki-elektroniki ya Samsung unaotarajiwa kuwasili mapema mwezi februari kijijini hapo. Wa pili kushoto ni Mratibu wa Taifa wa tiba asilia na mbadala katika Idara ya Tiba Wizara ya Afya na ustawi wa jamii. Dkt Liggy Vumilia.

      Afisa mipango ya Elimu wa Shirika la UNESCO, Bi. Jennifer Kotta akiwasilisha kazi ya kikundi chake baada ya kujadiliana na wanakijiji wa Ololosokwan katika kuboresha sekta ya elimu ikiwa ni maandali ya kupokea mradi wa kijiji cha kidigitali kinachotarajiwa kuwasili hivi karibuni kijijini hapo.

      Mmoja wa washiriki wa kikundi kilichokuwa kikijadili masuala ya utamaduni na utalii akiandika changamato mbalimbali zinazowakabili wakinamama wakimasai wanaofanya biashara za urembo wa kimasai kwa watalii wanaotembelea hifadhi ya Ngorongoro.

      Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akishiriki kwenye mjadala na wanakijiji wa kijiji cha Ololosokwan katika maandalizi ya kupokea mradi wa kijiji cha kidigitali unaotarajiwa kuwasili mapema mwezi februari kijiji hapo.

      Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akisaini mkataba wa kukabidhiwa ardhi iliyotolewa na serikali ya kijiji kwa ajili ya mradi wa kijiji cha kidigitali huku tukio hilo likishishudiwa na uongozi wa juu wa serikali ya kijiji, wataalam kutoka UNESCO na halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro pamoja na wanakijiji.

      Valentine's day Photo Shoot SPECIAL !!

      MIAKA 38 YA CCM NA FALSAFA YA RAIS BORA LAZIMA ATOKE CCM

      $
      0
      0
      Rais wa awamu ya nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.

      CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) mwishoni mwa wiki iliyopita kimeadhimisha miaka 38 tangu kuzaliwa kwake katika kaya hii. Mazuri na mabaya yake sitayajadili leo bali nitaangalia jambo moja nalo ni IMANI.
      2015 ni mwaka wa uchaguzi. CCM kama chama tawala kinaingia kwenye kinyan’ganyiro hicho kikiamini falsafa ya ya kiongozi wake wa kwanza Mwalimu Julius Nyerere kuwa rais bora hawezi kutoka nje ya CCM.
      Kwa masikio yangu mimi Mkuu wa Kaya nilimsikia mwenyekiti wa chama hicho taifa, Jakaya Kikwete, akisherehesha imani hiyo alipokuwa anahutubia maelfu ya wafuasi wa CCM katika Uwanja wa Majimaji mjini Songea mkoani Ruvuma.

      Najiuliza; imani ya chama hicho tawala inaambatana na matendo? Maana ni wazi Nyerere aliposema rais bora atatoka CCM alimaanisha CCM bora siyo dhaifu.
      Msingi wa hiki ninachokisema unajengwa na kauli ya muasisi huyo pale aliposema: “Bila CCM imara nchi itayumba.” Hapa ndipo mahali pa kujadili.

      Je, wakati mwenyekiti wa sasa akisisitiza imani ya chama chake mbele ya wanachama anaamini kuwa CCM anayoingoza ni bora kama zama za Mwalimu na kwamba ina sifa za kutoa rais bora? 
      Namkumbusha; Kikwete aliposisitiza kuuenzi wosia wa Mwalimu anakumbuka kauli ya muasisi wake aliyosema; Watanzania wanataka mabadiliko na wasipoyapata ndani ya CCM watayatafuta nje?
      Kwa mawazo ya leo, hakuna asiyejua kuwa kioo cha CCM kimemeguka vipandevipande na taswira zinazoonekana ndani zinatofautiana. Chama kimegawanyika katika makundi.

      Leo hii mwenyekiti akisimama mbele ya kioo cha chama chake haonekani mwili mzima, amegawanyika kiasi cha kutoutambua utimilifu wake na ndiyo maana anasisitiza ongezeko la wagombea urais wenye sifa kwa kuwa waliojitokeza hawajaweza kuziba ufa wa kioo chake.

      Mwenyekiti angali anatishwa na kivuli cha makundi; Nyerere hakuwa mwoga, alikuwa jasiri, mwenye kusimamia anachokiamini. Waliofanya naye kazi wanashahidisha kuwa hakuongoza kwa matakwa ya chama bali ya wananchi.

      Msingi huu ndiyo ambao CCM inapaswa kuufuata katika kuelekea kuipatia kaya hii mkuu mpya mwenye sifa ya ubora. Vinginevyo imani waliyorithishwa kuwa rais bora atatoka CCM itakuwa haina maana.
      Mwananzengo wenzangu; wakati chama hicho kikiadhimisha miaka 38 ya uhai wake, falsafa tatu lazima tuzifikirie sana kwa mustakabali wa kaya hii, nazo ni RAIS BORA KUTOKA CCM, WATANZANIA WANATAKA MABADAILIKO NA BILA CCM IMARA NCHI ITAYUMBA.

      Kuelekea kwenye uchaguzi mkuu mwaka huu, lazima wananzengo tujihoji juu uimara wa chama tawala na kama kitaweza kumteua mgombea bora tunayemtaka. Maana tunaweza kuamini falsafa kuwa rais bora atatoka CCM lakini wakubwa wakajiteulia mgombea atakayelinda maslahi yao na sisi tukadanganywa kwa imani iliyokufa na kuzikwa kuwa rais bora lazima atoke CCM. Tusikubali!

      Jambo la pili ni uhitaji wa mabadiliko. Mgombea ajaye lazima awe na kigezo cha kuiletea kaya hii mabadiliko ambayo Wanazengo wanayataka. Tukiletewa mgombea ambaye hana sifa hii tutoke usingizini tuyatafute mabadiliko yetu nje ya CCM!

      Mwisho wake ni CCM dhaifu kuiyumbisha nchi. Kama nilivyosema, chama hiki kutokana na makundi ya urais yanayonyukana kuingia ikulu, yanaweza kukidhoofisha chama hicho. Hilo likitokea tusikubali kuyumbisha nchi nzima, badala yake tukiache chama kiyumbe chenyewe na ikiwezekana kianguke madarakani kabisa!
      Huu ndiyo msimamo wangu mimi Mkuu wa Kaya. Shime Wananzengo wenzangu, niungeni mkono katika mawazo haya!
      SOURCE:GPL
      Viewing all 45982 articles
      Browse latest View live


      <script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>