.jpg)
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Gabriel Fuime.
Mkurungenzi wa Mashitaka (DPP), amemfutia mashitaka ya kuua bila ya kukusudia aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Gabriel Fuime (61) na kisha kumuunganisha na wenzake 11 na kuwasomea upya mashtaka 27 ya mauaji ya kukusudia kufuatia kuporomoka jengo la ghorofa 16 katika mtaa wa Indira Gandh, jijini Dar es Salaam.
Mbali na Fuime washtakiwa wengine ni, Diwani wa Kata ya Goba, Ibrahim Mohamed maarufu kama Kisoki, Raza Ladha, Goodluck Mbanga, Willbroad Mugyabuso, Mohamed Abdulkarim, Charles Ogare, Zonazea Oushoudada, Vedasto Ruhale, Michael Hema, Albert Mnuo na Joseph Ringo.
Washtakiwa hao walisomewa hati mpya ya mashitaka jana mbele ya Hakimu Mkazi Devota Kisoka, baada ya kuondolewa hati ya zamani ya mauaji ya bila kukusudiwa na kuunganishwa Fuime na idadi yao sasa kufikia 12. Upande wa Jamhuri uliongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Benard Kongola akisaidiana na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tumaini Kweka na Wakili wa Serikali Joseph Maugo.
Kongola alidai kuwa, kwa mujibu wa kifungu kidogo cha 294 (1), upande wa Jamhuri unaomba ridhaa ya mahakama ya kumuongeza mshtakiwa Fuime katika hati mpya ya mshitaka.
Hakimu Kisoka alisema mahakama haina pingamizi na maombi ya Jamhuri ya kubadilisha hati ya mashitaka dhidi ya washtakiwa.
Kwa mujibu wa Mwenendo wa Sheria ya Makosa ya Jinai (CPA), mashitaka yanayowakabili washtakiwa hao hawatakiwi kujibu chochote hadi pale upelelezi wa kesi hiyo utakapokamilika na kesi kuhamishiwa Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam kwa ajili ya kusikilizwa.
Hakimu Kisoka alisema kesi hiyo itatajwa tena Machi 26, mwaka huu na washtakiwa dhamana yao imefutwa na kupelekwa mahabusu.

CHANZO: NIPASHE