Hiki ndiyo kikosi cha kwanza cha ( NYATI ) kitakacho iangamiza DC jumamosi hii ya Memorial weekend. DC wanajigamba na kusema kufungwa na New York ni sawa na dagaa kummeza paka, Na New York wana sema kufungwa na DC ni sawa na sungura kumkaba kobe. Habari ndiyo hii mwisho wa yote ni tarehe 24, timu ya New York itaingia DC usiku wa Ijumaa na kuweka kambi ya masaa 20 kabla ya kushuka uwanjani.
New York
(NYATI)
kutoka jiji la wasilo lala katika picha ya pamoja
Solo Mollel aka Arachuga boy akiwa na sura makini ya kazi tayari kwa kutia njaa kwenye lango la wapinzani.
Na mwandishi wetu New York.
Timu ya mpira wa miguu ya New York jana Jumapili May 18, 2014 ilimaliza mechi yake ya mwisho ya majaribio baada ya kuifunga timu ya kombaini ya Mexico kwa bao 1-0 mechi iliyochezewa katika viwanja vilivyopo Manhattan,
Katika mchezo huo uliokuwa wakujipima nguvu na kujiweka sawa na mpambano wao na DMV utakaochezewa kwenye viwanja wa Walker Mills Park, Capitol Heights, Maryland siku ya Jumamosi May 24, 2014 kwa mechi inayotarajiwa kuanza saa 10:30 jioni (4:30 pm).
Katika mechi hiyo na kombaini ya Mexico, timu ya New York ilionyesha mchezo safi na wakuvutia tofauti na ilivyocheza mechi yake na
timu ya Watanzania kutoka Boston, Massachusetts na kuibanjua magoli kibao.Kocha wa timu ya New York Salim Akida amesema kikosi chake kipo imara na tayari kwa mpambano na timu ya DMV ambayo kwake yeye hatishiki nayo na anaamini vijana wake wataibuka na ushindi mnono siku hiyo ya Jumamosi May 24, 2014 mpambano unaosubiliwa kwa hamu na mashabiki wa soka wa DMV na vitongoji vyake.
Timu hii ya New York Ijumaa jioni ya May 23, 2014 imekaribishwa na Balozi wa kudumu wa Tanzania umoja wa Mataifa New York, Mhe. Tuvako Manongi kwa chakula cha jioni nyumbani kwake na atawakabidhi bendera kama alama ya ushindi. Balozi Tuvako Manongi alipoongea na Vijimambo alisema lengo la kufanya hivyo ni kuwatia nguvu vijana wake na yeye ni shabiki namba moja wa timu hiyo ya New York na angependa kuwahusia mawili matatu yahusuyo soka na baada ya hapo atawakabidhi bendera.
Timu ya New York inatarajiwa kuwasili DC siku ya Jumamosi asubuhi ya siku hiyo ya mpambano na DMV. Mechi hii ni sehemu ya shamrashamra ya sherehe za Memorial Weekend ambazo mwaka huu kwa mara ya kwanza zinafanyika DMV na sherehe hizo zitaanzia siku ya Ijumaa usiku Safari Club kwa usiku wa vijana wa zamani na siku ya Jumamosi kufuatiwa na mpambano wa New York na DMV na baadae siku hiyo usiku kufanyika usiku wa kimataifa hapo hapo Safari Club na Jumapili ndiyo kutakuwa na nyama choma Meadowbrook park na baadae usiku Safari Club kwa hitimisho la usiku kwa muziki wa Reggae.
Captain wa timu akitoa maelezo kabla ya mechi ya kujipima nguvu kuanza
Arachuga boy akitia njaa kwenye lango la wapinzani kwa bao lake moja la mguu wa nuksi wa kushoto DC kazi wanayo.
Rich (Kamachumu) boy leo alikuwa na kazi ya kupata massage tu hili siku na DC awe tayari kusafisha pale nyuma mashmbulizi yote kutoka kwa forward ya DC.
Wachezaji wakipasha kabla ya mchezo hapa ni Kisaka kulia tajiri asiekuwa na kitambi na kuchoto ni Jecha a.k.a Jaje wa kibanda uvivu.
Mundhil the Golden boy akionyesha kiwango
Ally mzee wa Kiks kushoto akistretch na kulia ni Mundhil the Golden boy akipacha |
Solo Arachuga boy na Ny Ebra. |