Jana Vijimambo iliandika Mama Jessica Mushala ndiye katibu mkuu mpya wa CCM DMV habari hiyo ilikuwa makosa na usahihi ni Mama Jessica Mushala na mwenyekiti wa Vijana Ismail Mwilima ndio watakaokuwa wagombea wa nafasi ya katibu mkuu kweye uchaguzi utakaofanyika June 15, 2014 majina ya Jessica Mushala na Ismail Mwilima yalipitishwa kwenye mkutano wa Halmashauri ya tawi la CCM DMV uliofanyika jana Jumapili May 18, 2014. Katika picha ni mwenyekiti wa tawi ndugu George Sebo (kushoto) na katibu mwenezi na itikadi mama Salma Moshi (kulia) wakiwanyanyua mikono wagombea. Vijimambo inaomba radhi kwa usumbufu wote uliotokea.
↧