Quantcast
Channel: VIJIMAMBO
Viewing all 45945 articles
Browse latest View live

HAPPY BIRTHDAY

$
0
0
Ramaman Marijani from Dar es Salaam, Tanzania
Timu ya Vijimambo inakutakia kheri ya siku ya kuzaliwa

KOCHA MPYA WA MANCHESTER UNITED ATUA

$
0
0
kocha mpya wa Manchester United Louis van Gaal tayari aishatua Manchester na ameishaanza kuinoa timu yake mpya na kesho Ijumaa July 18, 2014 Man U itaondoka Uingereza kuelekea Marekani itakaposhiriki mechi za kiangazi za kujiandaa na ligi ya Uingereza. Mechi yao ya kwanza watacheza na LA Galaxy July 23, 2014 na kucheza mechi yao ya pili na Inter Milan July 29, 2014 kwenye uwanja wa Fedex uliopo Landover, Matyland.

Kocha mpya Louis van Gaal akiwa na executive vice-chairman Ed Woodward

WIMBO WANGU WA LEO

HAPPY BIRTHDAY

$
0
0
Happy bday to this handsome fella,my love&amy bestfriend I thank Allah for giving u another year I love u so much and I'm wishing u many many more years to come and can't wait to grow old together. We love u so much. Ur kids made sure u cut the cake today they couldn't wait lol we enjoyed every second. Message from your wife Asha Shauri wa Hoston. TX.

MBUNNGE JOSHUA NASARE ASHIRIKI MDAHALO WA VIONGOZI WADOGO BARANI AFRIKA NCHINI MAREKANI

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassari akizungumza wakati wa mdahalo wa viongozi wadogo wanaoshiriki programu ya rais Obama kwa viongozi wadogo wanaoonyesha dira .Mdahalo huo umefanyika katika chuo kikuu cha Arkansas ambacho Rais Mstaafu wa Marekani Bill Clinton na mkewe Hillary walianzia kazi ya kufundisha Sheria.
Baadhi ya washiriki katika mdahalo huo ambamo miongoni mwa waalikwa walikuwa ni watanzania waishio Arkansas.
Mkurugenzi wa program ya Rais Obama ya "Young African Leaders initiative "(YALI) Dr, Leyah akizungumza katika mdahalo huo uliobeba kichwa cha "BRINGNG THE GAP BETWEEN THE DIASPORA AND OUR HOME COUNTRIES".
Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari akizungumza muda mfupi baada ya kutembelea makao makuu ya shirika la Heifer International ambalo limetoa ahadi ya kuendelea kusaidia jamii hususani katika elimu na mitaji huku likitoa mradi wa Ng'ombe wa maziwa kutoka kwa jimbo la Arumeru Masharik
Mbunge jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nssari akila pozi la picha na mratibu wa kijiji cha Heifer ,Bi Hellen Brown .
Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari pia alipata nafasi ya kushiriki mahojiano juu "vijana na mustakabali wa Afrika"katika kituo cha Luninga cha Umma kinachojulikana kama Fayetteville Public Access Television.shoto ni mwandishi wa kituo hicho Dan,Prof Mitiku toka chuo kikuu cha Makelle nchini Ethiopia,wote hawa wanashiriki program ya Rais Obama ya viongozi wadogo wa kiafrika katika chuo kikuu cha Arkansas nchini Marekani.
Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassari akiwa na mshiriki mwenzake katika programu ya rais Obama ya viongozi wadogo wa kiafrika inayofanyika katika chuo kikuu cha Arkansas nchini Marekani ,Bi Clara toka nchini Nigeria ambaye pia ni balozi wa UN Charter nchini Nigeria. Picha na Jichie












CCM KUONGEZA ADHABU KWA WATAKAOKIUKA MASHARTI YA ADHABU ZAO

$
0
0


Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Sekretarieti ,Makao Makuu ya CCM,Ofisi Ndogo Lumumba.


Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye amezungumza na waandishi wa habari leo katika Ofisi ndogo za CCM Lumumba na kuwaeleza yale yaliojiri kwenye kikao cha kawaida cha siku moja mjini Dar es Salaam.

Jana tarehe 16/07/2014 Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM ilifanya kikao cha kawaida cha siku moja mjini Dar es salaam. Kikao hicho kiliongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Dr. Jakaya Mrisho Kikwete.

Pamoja na mambo mengine kikao hicho kilipokea taarifa ya mazungumzo yanayoendelea kati ya CCM kwa upande mmoja na CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi kwa upande wa pili.

Mazungumzo hayo yanayosimamiwa na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi yana lengo la kuangalia kwa kina ni kwa nini baadhi ya wajumbe wachache wa Bunge Maalum la Katiba walisusia na kutoka nje katika awamu ya kwanza ya Bunge hilo, na kuangalia namna watakavyorudi ili kukamilisha mchakato wa mabadiliko ya Katiba nchini.


Kwa ujumla Kamati Kuu ya CCM imeridhishwa na mwenendo wa mazungumzo hayo na kupongeza juhudi hizo zilizofanywa na Msajili wa Vyama vya Siasa na Vyama husika. Kamati Kuu inapenda kueleza imani yake kuwa mazungumzo hayo yatazaa matunda kwa wajumbe wachache waliosusia Bunge Maalum la Katiba, kurejea Bungeni na kumalizia sehemu ya mchakato uliobakia. Kamati Kuu inayatakia kila la kheri mazungumzo hayo.

Kamati Kuu pia ilipokea taarifa za harakati za baadhi ya wanachama wa CCM walioonesha nia ya kuomba ridhaa ya CCM kugombea Urais. Baada ya kutafakari kwa kina, Kamati Kuu inapenda kuwakumbusha wote kuwa ili wasipoteze sifa za kugombea, ni muhimu wakazingatia Katiba, Kanuni na taratibu za Chama zinazosimamia masuala hayo.

Kuhusu wale waliopewa adhabu na Kamati Kuu kutokana na kukiuka baadhi ya taratibu za Chama kwa suala hili, Kamati ya Usalama na Maadili ya Chama itafanya mapitio ya mwenendo wao wa utekelezaji wa adhabu hiyo mwezi wa nane (Agosti 2014), na kama itabainika kuwa hawatekelezi ipasavyo masharti ya adhabu zao, itapendekeza kwa Kamati Kuu kuongezwa kwa adhabu kulingana na ukubwa wa uvunjaji wa masharti ya adhabu husika.

Ni muhimu wanachama wote wakakumbuka kuwa Chama ni pamoja na Katiba, Kanuni na taratibu zake, hivyo kutoziheshimu na kuzifuata ni kukivuruga, jambo ambalo halivumiliki.
Nia ya CCM kusimamia haya ni kuhakikisha Chama kinakuwa na umoja na mshikamano ambao ni muhimu sana, hasa tunapoelekea kukamilisha kazi ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2010/2015 na Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.

Aidha, Kamati Kuu imewatakia kheri na fanaka Watanzania wote wakati huu wanapomalizia mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Nape akijibu baadhi ya maswali yanayohusu bunge la Katiba na Ukawa alisema kwanza hoja ya UKAWA ilikuwa ndogo sana haikuchukua hata dakika 3,pia alisema Katiba ya Wananchi ya kweli itakwenda kupigwa kura na wananchi na njia sahihi ya kupigiwa kura na wananchi lazima Bunge la Katiba liishe,kulifanya Bunge la Katiba lisiishe maana yake unazuia Katiba isifike kwa wananchi na itaeleweka unakimbia aibu ya kushindwa.

T444Z offers a holistic approach to improve a person's hair

$
0
0
We all know what hair offers to people - confidence and self-esteem. It is true for both women and men. T444Z offers a holistic approach to improve a person's hair.

If you are not using it yet, What are you waiting for?? Give us a call/whatsapp us @ 1-617-504-3727 Or via our TOLL FREE # 1-855-687-7336 then dial 101# and you will be connected to us it's that simple.

Visit: www.t444zhairfood.com

HAPPY BIRTHDAY

$
0
0
Hussein Lujuo Mohammed from Dar es Salaam, Tanzania
Timu ya vijimambo inakutakia kheri ya siku ya kuzaliwa

KWA WAJASILIAMALI WANAOPENDA KUCHUKUA MEZA KWENYE SHEREHE YA VIJIMAMBO

$
0
0
Kamati ya maandalizi ya sherehe ya Vijimambo itakayofanyika Sept 13, 2014 inapenda kuwataarifu na kuwakaribisha kushiriki kwenye sherehe ya miaka 4 ya Vijimambo wajasiliamali wote wanaopendelea kuchukua meza kwa ajili ya kuonyesha shughuli wanazofanya.

Tafadhali wasiliana na wanakamati namba za simu Baraka Dudi 301 792 8562, Asha Nyang,anyi 301 793 2833, Julius Katanga 202 400 4218, Idd Sandaly 301 613 5165, Mayor Mlima 301 806 8467 na Tumaini Kaisi 301 433 3411.

Ushirikiano wako ndio mafanikio ya sherehe hii.

Asante.

KAMATI YA MAANDALIZI

Dua Said akamatwa tuhuma wizi wa maji

$
0
0
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla (kulia), akimhoji mchezaji wa zamani wa Simba, Dua Said ambaye alikuwa miongoni mwa watu watano waliokamatwa kwa tuhuma za kujiunganishia maji isivyo halali kutoka kwenye mabomba ya Mamlaka ya Maji Safi na Taka (Dawasa), kwenye nyumba zao zilizopo Bonde la Mto Msimbazi, Kigogo, Dar es Salaam. Makalla alikuwa kwenye ziara ya kukagua miradi ya maji Dar es Salaam. (picha na Kamanda wa Matukio)

Mchezaji wa zamani wa timu ya Simba na Taifa Stars, Dua Said, anashikiliwa na jeshi la Polisi mkoa wa Kinondoni kwa tuhuma za kuiibia maji kampuni ya Maji Safi (Dawasco).

Mchezaji huyo alikamatwa jana wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala, aliyeongozana na wabunge wa Chadema, John Mnyika, Halima Mdee na Suzan Lymo katika operesheni ya dharura ya kuwasaka wezi wa maji katika wilaya ya Kinondoni.

Hata hivyo, mbunge wa Kinondoni, Idd Azan ambaye eneo lake ndilo walilokamatwa watuhumiwa hao, hakuwapo katika ziara hiyo.

Mbali na Dua Said, pia nyumba ya mchezaji wa zamani Nico Bambaga, ambaye kwa sasa ni marehemu ilikutwa imeunganishwa katika mtandao huo wa wizi wa maji sambamba na nyumba zingine tatu.

Akizungumza baada ya kukamatwa, Dua alisema nyumba iliyokutwa imeunganishwa na mfumo huo wa maji katika eneo la Kigogo ni mali yake na kwamba kwa sasa hakai hapo baada ya kuhamia Kinyerezi.

Alisema kuwa kabla ya kuondoka Kigogo alikuwa ni miongoni mwa wajumbe wa kamati ya maji waliokuwa wakipambana na mfumo wa wizi wa maji na kwamba yeye hauzi maji bali anapeleka kwenye nyumba yake nyingine.

"Niliomba kuunganishiwa maji kihalali na sikuyapata mpaka ninaondoka Kigogo ndiyo maana jana nilipoambiwa nije kuna tatizo sikusita kuja," alisema Dua.

Akizungumza baada ya kuwakamata watuhumiwa hao, Makala alidai kuwa Dua alikuwa akivuna maji kiasi cha lita 90,000.

"Moja ya vitu vinavyochangia tatizo la maji ni hili la wizi wa maji, watu hawa kwa ujanja wao wameikosesha serikali mapato pamoja na kuwafanya wananchi wengi wakose maji, lazima wachukuliwe hatua stahiki," alisema.

Jiji la Dar es Salaam na maeneo mengine mengi ya Tanzania yamekuwa katika tatizo sugu la huduma ya maji kwani huduma inayotolewa hailingani na mahitaji.
CHANZO: NIPASHE

RAIS KIKWETE APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO ZA BALOZI WA NEW ZEALAND HAPA NCHINI

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Mhe. Richard Stuart Mann, Balozi wa New Zealand hapa nchini mwenye makazi yake Afrika Kusini. Hafla hiyo fupi ilifanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 15 Julai, 2014.
Balozi Mann akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) mara baada ya Balozi huyo kuwasilisha Hati zake za Utambulisho kwa Mhe. Rais Kikwete, wakwanza kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Kazi maalum Mhe. Prof. Mark J. Mwandosya (Mb.)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Mhe. Richard Stuart Mann
Balozi Richard Stuart Mann akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili Ikulu.
Balozi Mann akisikiliza Wimbo wa Taifa lake ukipigwa kwa heshima yake mara baada ya kuwasili Ikulu. Kulia ni Mkurugenzi na Mkuu wa Itifaki, Balozi Mohammed Juma Maharage na wakwanza kushoto ni Mnikulu, Bw. Shaaban Gurumo.Picha na Reginald Philip.

Mwanamke auawa kwa kucharangwa mapanga

$
0
0
Mwanamke aliyejulikana kwa jina la Milembe Masanja (50), ambaye ni mkazi wa Kitongoji cha Muhida, Kijiji na Kata ya Busangi, Wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga, ameuawa kikatili kwa kukatwa na mapanga kichwani na mikononi na watu wawili, wanaodaiwa kukodiwa kufanya mauaji hayo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Justus Kamugisha, alisema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana kuwa tukio hilo lilitokea Julai 14, mwaka huu, saa 2.00 usiku.

Aliwataja waliofanya mauaji hayo kuwa ni Chuchu Lugodisha na mwenzake, Ngeja Kugodisha, ambao wote ni wakazi wa Kijiji cha Izumba, Kata ya Luguya, mkoani Tabora.

Alisema watu hao walikodiwa na Madaha Luhemeja ili kufanya mauaji hayo.Ilielezwa kuwa familia ya marehemu ilikuwa na ugomvi wa mipaka ya mashamba na familia ya Luhemeja.


Hata hivyo, Kamanda Kamugisha alisema watuhumiwa wote watatu walikimbia baada ya mauaji hayo na Jeshi la Polisi linaendelea na msako mkali kuwakamata.

Alisema kufuatia mauaji hayo polisi mkoa wa Shinyanga inawashikilia watu watatu kwa mahojiano.

Watu hao ni Pili Paulo(37), Juma Paulo (19) na Daudi Ngassa (57), ambao ni wote wakazi wa Busangi, Wilaya ya Kahama.

Kamanda Kamugisha aliwataka wananchi kutoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwa watu wanaofanya vitendo vya mauaji kwa kukata mapanga baada ya kukodiwa.
 
CHANZO: NIPASHE

Labor Day Weekend - Soka Festival

$
0
0

New England Umoja Foundation, Inc.
Proud to Welcome You on …
12th Annual Soka Festival
Bringing together families and friends for a fun filled day of activities, sporty, tradition, and so much more including an exciting range of talented vendors showcasing Tanzanian made products and LIVE music & performances.
WHEN: Labor Day Weekend: Sunday August 31st, 2014
TIME: 9AM – 9PM
WHERE: Camp Kee-Wanee
Greenfield, MASS

FREE Parking, Food & BBQ
For More Information visit:
www.NewEnglandUmoja.net
FACEBOOK  : TWITTER @NewEnglandUmoja | #NewEnglandUmoja


KARIBUNI WOTE !!!

JHIKOMAN ADATISHA KATIKA INTERNATIONAL AFRICAN FESTIVAL TUBINGEN,UJERUMANI

$
0
0
KUTOKA BAGAMOYO HADI UGHAIBUNI UJERUMANI ! JHIKOMAN MOTO MKALI !
Tubingen,Ujerumani,
Mwanamuziki maarufu wa reggae barani Afrika Jhiko Manyika aka Jhikoma kutoka Bagamoyo,Tanzania,alifanikiwa kuwadatisha akili washabiki wa muziki nchini ujerumani siku ya alhamisi 17 julai 2014 katika maonyesho makubwa ya kimataifa 5th International African festival Tubingen 2014,yanayofanyika katika viwanja vya Festplatz,mjini
Tubingen,Ujerumani. Mwanamuziki huyo nguli wa reggae amepewa heshima zote za kimataifa kwa uwakilishaji wake kama balozi wa reggae wa Afrika.ratiba ya maonyesho hayo inaonyesha kuwa Jhikoman atapanda tena jukwaani siku ya jumapili 20.Julai 2014 jioni kwa ajili ya maombi maarumu ya washabiki waliotaka kumuona tena mflame huyo wa reggae.
Pia taarifa zimetosha kuwa jumamosi 19 julai 2014 saa 2.00 usiku FFU-Ughaibuni aka Ngoma Africa band watatumbuiza katika maonyesho hayo.
www.jhikoman.com

WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA RAIS-MAZINGIRA AFANYA ZIARA KIWANDA CHA NIDA.

$
0
0
 Picha ikionyesha jinsi maj i yenye kemikali  yanavyotiririshwa toka katika kiwanda cha kutengeneza nguo cha NIDA kilichopo barabara ya Mandela.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira Injinia Dkt Binilith Mahenge akiangalia uharibifu wa mazingira  uliosababishwa na maji yenye kemikali yanayotiririshwa na kiwanda cha NIDA. Anayemfuatia ni Mkurugenzi Mtendaji wa NEMC Bonaventura Baya, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Eng. Angelina Madete.
 Jengo la kiwanda cha NIDA likionekana kwa nje
 
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira Injinia Dkt Binilith Mahenge akiongea na Menejimenti ya kiwanda cha kutengeneza nguo cha NIDA Textiles kuhu kiwanda hicho kinavyoharibu mazingira kwa kutiririsha maji yenye kemikali katika mto kibangu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira Injinia Dkt Binilith Mahenge, akiongea na Vyombo vya habari kuhusu ziara yake aliyoifanya katika kiwanda cha NIDA textiles jijini Dar es Salaam

Rai imetolewa kwa wawekezaji wote Nchini kuhakikisha wanajali na kutunza Mazingira.Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt Binilith Mahenge wakati  alipofanya ziara ya kutembelea kiwanda cha kutengeneza nguo cha NIDA kilichopo barabara ya Mandela katika kata ya Kigogo jijini Dar es Saalam.
Kiwanda hicho ambacho kinalalamikiwa na wananchi kuwa kinatiririsha maji machafu yenye kemikali katika mto kibangu uliopo pembeni ya kiwanda hiko ambako wananchi wanalima mbogamboga kando yamto huo na wanatumia kula pia  wanauza ili kujipatia kipato pasipo kujali athari zilizopo kwenye maji hayo yenye kemikali.

Akiongea na Menejimenti ya kiwanda hiko Dkt. Mahenge baada ya kutemebelea mto huo na kujionea maji yalivyoathiriwa na kemikali zitokazo kiwandani, aliitaka Menejimenti ya kiwanda hiko kuacha mara moja kutiririsha maji yenye kemikali katika mto kibangu na hivyo basi kuchukua hatua za kitaalamu ili kuondoa kemikali zilizopo kwenye maji hayo.
Akiongea kwa niaba ya Menejimenti ya Kiwanda Afisa Utawala Mohammed Olewo aliahidi kwamba watafanyia kazi maagizo ya Waziri kwa ufasaha na wanaahidi watarekebisha makosa yote yaliyotokea pia watadumisha na kutunza  mazingira.
Ziara hiyo ni moja ya ziara za Waziri anazofanya kutembelea  maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya kukagua utunzaji wa mazingira.   

TAMKO LA KIKUNDI KAZI CHA SERIKALI ZA MITAA CHA POLICY FORUM KUHUSU UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2014

$
0
0
policy forum

Sisi wajumbe wa Kikundi Kazi cha Serikali za Mitaa cha Policy Forum, tunaowakilisha zaidi ya Asasi  70 za Kiraia tuliounganisha nguvu zetu  ili kuchangia katika kuifanya michakato ya sera ngazi ya serikali za mitaa kuwa yenye uwazi zaidi, ya kidemokrasia, iliyo shirikishi na yenye uwajibikaji, tunapenda kutoa  mchango wetu katika mchakato huu  muhimu wa uchaguzi wa serikali za mitaa wa 2014.  
Tunatambua umuhimu wa serikali za mitaa, ambazo zinalenga kupeleka madaraka kwa jamii au kusogeza madaraka ya kufanya maamuzi kwa wananchi ili kuboresha na kuimarisha utoaji wa huduma kulingana na matakwa ya wananchi.  Tunatambua pia, kwamba mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa unategemea mchakato wa katiba mpya ambao umepoteza ratiba yake ya awali ambapo katiba mpya ingezinduliwa tarehe 26 Aprili 2014 na kwa sasa umefika njiapanda na hivyo haijulikani wapi tunaelekea katika uandikaji wa katiba mpya.

Kutokana na ukweli kwamba uchaguzi wa serikali za mitaa ulitakiwa kufanyika kati ya Septemba na Oktoba 2014 na kutokana na matamko mbalimbali yaliyokwishatolewa na viongozi pamoja na wachambuzi wa masuala ya kisiasa pamoja na wadau mbalimbali na sisi kama wadau katika uongozi wa serikali za mitaa tunajiuliza maswali mengi juu ya hatima ya uchaguzi wa serikali za mitaa kwa mwaka huu.


Tungependa kujua kama wadau wakuu ni lini Uchaguzi wa Serikali za mitaa utafanyika? Kama tunavyofahamu kipindi kama hiki utaratibu umekuwa kwamba kanuni za uchaguzi huwa zinakuwa zimeshaandaliwa na kutolewa ambazo kazi yake kubwa ni kutoa mwongozo na taratibu wa jinsi serikali za mitaa zitakavyoendeshwa hivyo tungependa kujua kama kanuni za uchaguzi zimeshaandaliwa? Na kama zimeshaandaliwa zimeandaliwa na chombo gani? Na ushiriki wa wadau ulikuwaje?
Sisi tunataka kusema kuwa tumeona mkutano wa vyama vya siasa na TAMISEMI uliofanyika Morogoro hivi karibuni ambao tumesoma kupitia vyombo vya habari ulikuwa wa kuandaa kanuni za uchaguzi wa serikali na hapa tunataka kusema kuwa kama wadau toka mashirika yasiyo ya kiserikali hatujashiriki wala kushirikishwa katika mchakato wa kuandaa kanuni.
Sisi kama kikundi kazi cha mtandao ambao unajihusisha na masuala ya serikali za mitaa nchini Tanzania tunaungana na Rais Daktari Jakaya Mrisho Khalfan Kikwete kuwa Tanzania kama nchi kwa sasa iko kwenye mtikisiko mkubwa kuhusiana na mchakato wa kuandika katiba mpya hivyo haiwezi kuhimili pamoja na mchakato wa katiba na chaguzi mbili kuu, hivyo basi tunapendekeza uchaguzi wa serikali za mitaa ufanyike pamoja na Uchaguzi Mkuu Oktoba 2015 kama ilivyo kwa Kenya na Zimbabwe.

Kwa  kutambua kuwa TAMISEMI sio chombo mahususi cha kuendesha chaguzi hapa nchini,  pia tunapendekeza uchaguzi wa serikali za mitaa  usimamiwe na kuendeshwa na Tume Huru ya Uchaguzi na kwa sasa tupate nafasi ya kubadilisha sheria za uchaguzi na kufanya maandalizi mengine ili tuwe na chaguzi huru na zenye ufanisi mkubwa.

Taarifa kwa waandishi:
Kwa habari zaidi tafadhali wasiliana na wafuatao:
·         Mwenyekiti Kikundi Kazi cha Serikali za Mitaa : Hebron Mwakagenda:  theleadership2000@yahoo.com,0713612681

·         Alex Ruchyahinduru   +255 757716333, policy2@policyforum.or.tz

PRESS RELEASE

$
0
0
Rt. Hon. Dato' Sri Mohammad NajibTun Abdul Razak

PRESS RELEASE

H.E. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania has sent a condolence message to Rt. Hon. Dato' Sri Mohammad NajibTun Abdul Razak, Prime Minister of Malaysia following the loss of lives due to the crash of a Malaysian airliner on Thursday 17th July 2014. The message reads as follows:

“Rt. Hon Dato' Sri Mohammad Najib Tun Abdul Razak,
The Prime Minister of Malaysia,
Kuala Lumpur.
Malaysia

I have learnt with great shock and sorrow the sad news of the loss of so many lives due to the crash of a Malaysian airliner on its way from Amsterdam to Kuala Lumpur that occurred on Ukrainian territory on Thursday 17th July 2014.

The crash is an immense tragedy not only for the loved ones of those who perished but also for all the people of Malaysia and their friends. As a country, our thoughts and prayers are with the people of Malaysia in this time of grief.

On behalf of the Government and the people of the United Republic of Tanzania, and indeed on my own behalf, I offer you our sincere condolences, support and solidarity.

Please accept, Your Excellency the assurances of my highest consideration”.

Issued by: The Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation, Dar es Salaam

18th July, 2014

Invitation to Diaspora Trade & Investment Activities - August

$
0
0
My Fellow Tanzanians, 
 
Greetings from EADBC!
 
As many of you know, President Obama will be hosting the first US-Africa Leaders Summit in Washington, D.C. from August 4-6, 2014. At EADBC, we are looking forward to welcoming leaders from across the African continent to the Nation’s Capital to further strengthen ties with our dynamic countries.
 
In the backdrop of this historic occasion, together with our affiliates, EADBC has an interesting program of Diaspora-facing events in Washington, DC metro region. It is such a pleasure to welcome you to join me and the entire EADBC team, the African Diaspora community and the African leaders on this journey to explore trade and investment opportunities that we can explore NOW. 
 
Below is a synopses of the events. Please click on the links below to learn more and register.
 
African Diaspora Investment Symposium
Monday, 4 August 2014 at 08:00AM – 5:00 PM
 
Ronald Reagan Building- Pavilion RoomLed by Developing Markets Associates, Homestrings, the Small Enterprise Assistance Fund and the International diaspora Engagement Alliance in partnership with EADBC
 
Themes:
Morning event (general admission): The focus of this event will be on sharing insights from current Diaspora initiatives and investment platforms and will be open to the general public.
Afternoon event (Accredited Investors Only): This session will explore private investment transactions in which attendees can invest in directly using the Homestrings platform

Doing Business in East Africa Forum:
Tuesday, August 5th, 2014
 
9:00 AM – 5:00 PMDoing Business in East Africa Forum
Led by EADBC and Prince George’s County Africa Trade Office
Theme: Developing Partnerships in Trade, Investment and Economic Growth

Public Works Study Tour:
Wednesday, August 6th, 2014
 
9:00 AM – 1:00 PMDC Water and Sewer Authority – Tour of the Wastewater Treatment Facility and Renewable Energy Plant
Led by Ernest Jolly, Energy Manager, DC Water
Theme: Turning Sewage into Electricity and Fertilizer while Creating Jobs
2:00 PM – 4 PMDC Water and Sewer Authority – Tour of the City’s Water Treatment and Distribution Operations. 
Led by Thea Browne-Dennis – Chemical Engineer, DC Water
Theme: Planning and Delivery of Water Services in a Growing City
 
Prince George’s County 2nd Annual Gateway to Africa Gala
Friday, August 8, 2014.
Theme: Promoting International Trade
Led by Prince George’s County Economic Development Corporation – Africa Trade Office
 
To keep you better informed of EADBC activities around the summit, we invite you to visit http://eadiaspora.org/events. It will continue to be updated as we move closer to August. If you know any events that you would like to publicize on the website, please let me know.
 
We look forward to seeing you in Washington, DC.


Kindest Regards, 


Benedict Kazora, MSEE, MBA
President,  Eastern Africa Diaspora Business Council (EADBC)President,  Tanzania Community Dallas, TX
Email:         president@eadiaspora.org
Email:         bkazora@alumni.purdue.edu
Facebook:   https://www.facebook.com/EasternAfricaDiasporaBusinessCouncil
Website:     www.eadiaspora.org
"Engaging the Diaspora for Eastern Africa Global Competitiveness"

WIMBO WANGU WA LEO

Introducing Toto Shine Magazine

$
0
0
I’m so excited that one of the projects that is so dear to my heart (to empower women and children) for the last 3 years I have been working very hard on it, is soon to become a reality…

The Toto Shine Magazine is now looking for drawings, poems or short stories from children ages 6 -14.

This magazine is for the whole East Africa region and beyond, so we want as many kids from Tanzania as possible to participate.  

I do remember when I was a little kid Mama na Mwana show read something I sent to them on the radio that was one of my best days. Also I answered some questions and they mailed me a congratulatory letter for being one of the winners. That little piece of paper I received was one of my inspirations growing up and I kept it for so many years.....

Motivate your kids to participate.  Thanks to my very good friends who believe me on this project so far we pay US $20  if we use each drawing, story or poem on our magazine. 

It is not just funny to earn money while still a kid but its also empowers. That little achievement your child, niece or nephew will receive can be a solid foundation of his/her ambition and determination to do much more in life. 

The phone app is coming soon to easily update your kid’s work direct from your phone or tablet.  

Tell you kids, nieces and nephews and everyone you know. From abstract art and traditional drawing to sketching, painting, or doodling or perhaps it’s something that symbolizes the culture or maybe it’s a moment in her/his life that stands out. It could be a character he/she has created, or a drawing of a favorite pet. We are looking for it all. 

For poems we prefer non-rhyming poetry (free verse poems) though if your kid prefers rhyming poetry don’t hesitate to send it to us. 

For short stories 1500 words or fewer works best for our readers’ ages. 

For a chance your kid to be accepted make sure you or a teacher carefully read his/her writing or look at his/her artwork before submitting, and then consider any suggestions to make it better. Often, there are events in stories that don’t make sense, and having someone read it and make suggestions always helps! 

You or your child/niece/nephew must be 6-14 years old to participate.

Follow us at @totoshinemag and facebook ID Toto Shine for more updates 
The website www.totoshine.com is soon coming 

Also for those who would like to support our effort you can download our media kit athttp://www.kwanzapress.com/Toto%20Shine%20media%20kit.pdf

Best Regards,
Pauline

Viewing all 45945 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>