↧
MSIKILIZE MTOTO AKIELEZEA JINSI ALIVYOFUNDISHWA UCHAWI NA JINSI WALIVYOKUA WAKILA NYAMA ZA WATU
↧
MBUNGE RIDHIWANI KIKWETE AENDELEA KUFANYA MAMBO JIMBO LA CHALINZE, SAFARI HII NI ZAMU YA JESHI LA POLISI
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete kompyuta Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani Kamanda ACP Ulrich Onesphory Matei zilizokabidhiwa na mbunge huyo kwa ajili ya kuboresha shughuli za jeshi hilo jimbo la Chalinze katikati ni Mkuu wa kituo cha polisi Chalinze Afande J. S. Magomi.
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akikata utepe kufungua ili kuonyesha kompyuta hizo huku viongozi wa jeshi hilo mkoani Pwani na jimbo la Chalinze wakishiriki shghuli hiyo.
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akimuonyesha moja ya kompyuta Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani ACP Ulrich Onesphory Matei.
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akimsikiliza Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani ACP Ulrich Onesphory Matei wakati alipokuwa akitoa shukurani zake kwa niaba ya jeshi la polisi mkoani Pwani mara baada ya kukabidhiwa kompyuta hizo , katikati ni mkuu wa ituo cha polisi cha Chalinze Afande J.S Magomi.
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akizungumza na uongozi wa polisi Mkoa wa Pwani na Wilaya ya Kipolisi ya Chalinze pamoja na wananchi waliojitokeza katika hafla ya makabidhiano ya vifaa mbalimbali kwa jeshi hilo zikiwemo kompyuta, mifuko ya Saruji pamoja na fedha vilivyotolewa na mbunge huyo, Kwa ajili ya kutatua matatizo mbalimbali yanayolikabili jeshi la polisi katika utekelezaji wa majukumu yake ya ulizni na usalama wa raia na mali zao. Pamoja na kukabidhi kompyuta hizo zitakazosaidia katika utunzaji wa kumbukumbu pia mbunge huyo ametoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya polisi vya Mbwewe na Kiwangwa ambavyo thamani inafikia zaidi ya shilingi milioni 11, Kushoto kwake ni Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani ACP Ulrich Onesphory Matei, hafla ya makabidhiano hayo imefanyika jana kwenye kituo kikuu cha polisi Chalinze.
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akimsikiliza Mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Chalinze Mzee Bw. Kamis Kameza wakati alipokuwa akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa shule hiyo ambayo inajengwa na jeshi la kujenga taifa JKT kambi ya Ruvu.
Baadhi ya wanajeshi wa kambi ya JKT Ruvu wanaoshiriki katika ujenzi wa shule hiyo.
Moja ya madarasa ya shule hiyo ambayo yako katika hatua za mwisho za kukamilisha ujenzi wake.
Baadhi ya madarasa na maktaba ya shule hiyo yakiwa katika hatua mbalimbali za ujenzi wake.
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akisalimiana na wanafunzi wa darasa la saba wa shule ya msingi ya Chalinze Mzee wakati alipokagua ujenzi wa shule hiyo.
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akiendelea kufanya ukaguzi wa ujenzi shuleni hapo kushoto ni Diwania wa kata ya Bwilingu Chalinze Bw. Ahmed Nasser.
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikweteakikagua ujenzi wa Maktaba ya shule hiyo akiwa ameongozana na Diwani wa kata ya Bwilingu Ahmed Nasser mbele na Mwalimu mkuu wa shule hiyo Khamis Kameza.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria wakati wa hafla kukabidhi kompyuta kituo cha polisi Chalinze.
Diwani wa kata ya Bwilingu Chalinze Bw. Ahmed Nasser akizungumza wakati mbune wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete alipolokabidhi jeshi la polisi kompyuta kwa ajili ya kuboresha shughuli za jeshi hilo.
(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-CHALINZE)
↧
↧
FUTARI YA PAMOJA DMV- TAMCO
↧
KAMPUNI YA TAN COMMUNICATION MEDIA YAFUTURISHA JIJINI ARUSHA
Mkurugenzi wa Tan Communication Media inayo miliki kituo cha Radio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha Bw Robert Francis wakati akifuturisha,hafla iliyofanyika katika studio za redio hiyo zilizopo Njiro jijiniArusha iliyoudhuriwa na Viongozi wa dini na wadau wengine. Picha kwa hisani ya Jamii Blog

Sheikh Mkuu wa Bakwata mkoa wa Arusha,Shaaban Juma aliyekuwa mgeni rasmi katika halfa hiyo iliyoandaliwa na kampuni ya Tan Communication Media

Mbunge wa Arusha Godbless Lema wa pili kutoka kushoto naye alihudhuria halfa hiyo

Mkurugenzi wa Tan Communication Media inayo miliki kituo cha Radio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha Bw Robert Francis akiwa na mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema

David Lwekiza Rwenyagira ambaye pia ni mtangazaji wa kituo hicho ndiye aliyekuwa MC

Mchekeshaji kutoka nchini kenya Peter Sankale maarufu kama “Olexander Jospat”katika igizo la VIOJA MAHAKAMANI akitoa burudani baada ya Futari
Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Arusha, Isaack Joseph akikaribishwa na mkurugenzi wa kituo hicho Robert Francis
Mkurugenzi wa kituo cha Redio 5 Robert Francis akisalimiana na mke wa Mbunge wa Arusha

↧
ZANZIBAR BEACH SOCCER KUCHEZWA KENDWA ROCK'S HOTEL BEACH
Na Andrew Chale
TAASISI ya Mwangaza wa buradani Zanzibar (Zanzibar Light Entertainment ) ya mjini Unguja, Zanzibar, Imemtangaza rasmi Hotel ya Kendwa Rocks kuwa eneo litakapofanyika michuano m aalum ya soka la ufukweni lijulikanayo kama (Zanzibar Beach Soccer Championship Bonanza) linalotarajiwa kufanyika Agosti Mbili mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa yao hiyo kwa vyombo vya habari, iliyotolewa na Mwandaaji wa michezo hiyo, Muslim Nassor ‘Jazzphaa’ ilieleza kuwa, kamati ya mashindano hayo, ambayo kwa sasa hipo katika harakati mbalimbali zikiwemo za kusaka ufadhili kwa wadau, tayari baadhi ya wadau wameanza kuitikia wito huo huku Kendwa Rocks Hotel Beach, wakijitosa kudhamini ‘venue’.
“Kadri siku zinavyozidi kwenda ndipo maandalizi yanakuwa magumu zaidi. Tunafuraha kutoa taarifah kuwa ndipo tutakapofanyia mashindano haya ya Zanzibar Beach Soccer Bonanza 2014.” Alisema Muslim Nassor Jazziphaa.
Aidha, Muslim Nassor Jazziphaa aliweka bayaana kuwa, Director wa Kendwa rocks, Bwana Ally Kilupi tayari ametoa baraka zote za kufaanyika mchezo huo huku akifurahia mchezo kufanyika eneo hilo, huku akitoa rai kuwapo kwa amani na utulivu siku hiyo na siyo kuanza ugomvi na vitu ambavyo havina maana.
Kwa mujibu Bwana Ally Kilupi alieleza kuwa, kwa upande wao Kendwa Rocks wamejipanga kutoa huduma safi na ya aina yake zenye ubora wa kimataifa huku wakitarajia kuwa na wageni wasio pungua 300, siku hiyo.
Kwa upande wa Muslim Nassor Jazziphaa, alisema nifaraja kwao huku wakiendelea kujipanga zaidi katika kutekeleza yale waliyokubaliana na Kendwa Rocks. “Tunashukuru Kendwa Rocks Hotel Beach, kwa udhamini wao huu wa ‘venue’ na kama alivyotusisitizia juu ya masuala ya amani na usalama zaidi, hivyo tunamuakikishia hilo na kamati yetu imejiandaa vya kutosha” alisema Muslim Nassor Jazziphaa.
Aidha, uongozi na waandaji wa michezo hiyo Zanzibar Light, wametoa wito kwa wananchi kuwa kwa siku hiyo kudumisha Amani na utulivu ilikuona mchezo huo jinsi unavyochezwa kisheri a.
Muslim Nassor Jazzipha akitoa ratiba ya awali, alisema : Mechi ya kwanza itakuwa saa nne kamili asubuhi huu wakitarajia fainali ‘final’ itachezwa saa tisa na nusu na kumaliza saa kumi na baada ya hapo ni burudani na shangwe kwa wote.
“Baada ya kumalizika kwa shughuli za Beach Soccer, Kutafuatiwa na burudani itkayoangushwa na Dj Cartel ambae alikuwa ni Dj rasmi katika Tamasha la filamu za nchi za Jahazi ZIFF 2014.. atafanya mambo yake kwenye moja na mbili.” Alisema Muslim Nassor Jazziphaa
Pia aliomba wananchi kujitokeza kwa wingi ilikutoa support ya kutosha huku pia wakitarajia kuwa na wageni wengi siku hiyo huku wakiongozwa Rais mstaafu wa chama cha soka Zanzibar, ZFA, Ally Tamim Ferej, hivyo tucheze kwa pamoja, tucheze kwa ajili ya Afya na kudumisha urafiki. wote munakaribishwa na ni bure.
Na kuongeza kuwa, kwa kujali usalama wa watu na Family zao shughuli hiyo itaisha saa kumi na moja jioni na baadae usiku kutakuwa na Party itakayokuwa ikiendeshwa na uongozi wa Kendwa Rocks.
Kwa upande wa timu ambazo mpaka sasa zimeshapatikana kushiriki Beach Soccer ni pamoja na Shisha lounge , Makontena, ZIFF F, na Kendwa Rocks.
Kwa upande wa timu zilizo kwenye maongezi na uongozi wa waandaji ni pamoja na PBZ Bank, Vigo group of Company, Maru Maru hotel, Zan link na Six degree north.
Kauli mbiu ya mwaka wa huu ya Michuano hiyo ni “ZANZIBAR BEACH SOCCER CHAMPIONSHIP BONANZA 2014…PAMOJA SANA.!!
↧
↧
WATU WALIOKUFA KWENYE AJALI YA NDGE YA MALAYSIA NA NCHI WANAZOTOKA


↧
RAIS KIKWETE AFUNGUA OFISI ZA TAKUKURU MKOA WA RUVUMA
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua rasmi jengo la ofisi ya TAKUKURU mkoa wa Ruvuma jana mjini Songea.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na kaimu Mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU Bibi Mary Mosha wakifunua kitambaa katika jiwe la msingi wakati wa ufunguzi wa jingo la ofisi za TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma jana. Rais Kikwete yupo katika ziara ya kikazi ya wiki moja mkoani Ruvuma
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipanda mti wa kumbukumbu wakati wa ufunguzi rasmi wa ofisi za taasisi ya kuzuia rushwa TAKUKURU mkoa mjini Songea jana. Kushoto ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bibi Mary Mosha. Picha na Fredy Maro, IKULU
↧
Ukraine:Kudunguliwa kwa ndege ni uhalifu

Waziri mkuu wa Ukraine Arseniy Yatsenyuk
Waziri mkuu wa Ukraine Arseniy Yatsenyuk amesema kuwa kudunguliwa kwa ndege ya Malaysia ni uhalifu wa kimataifa unaopaswa kupelelezwa na mahakama ya jinai iliyoko The Hague.
Waziri huyo mkuu amesema kuwa mauwaji hayo yametekelezwa na Serikali ya Urusi, huku Rais wa Urusi, Vladimir Putin, akirushia lawama Ukraine.
Naye Waziri mkuu wa Australia Tony Abbott amesema kuwa ajali hiyo ya ndege ilionekana kuwa tendo la Ugaidi, kwani inaonekana ilishambuliwa na waasi wanaofadhiliwa na Urusi.
Waziri mkuu wa Uholanzi Mark Rutte amesema nchi yake inaomboleza vifo vya zaidi ya watu 150, raia wa taifa lake walioangamia katika ajali ya ndege ya Malaysia iliyodunguliwa Nchini Ukraine.
Lawama zimekuwa zikirushwa kati ya Ukraine na Urusi
Anasema kuwa kulikuwa na waholanzi 154 kwenye ndege hiyo.
Kati ya walioabiri ndege hiyo, kulikuwemo takriban watafiti 100 wa ugonjwa wa ukimwi, wafanyikazi katika idara ya afya na wanaharakati waliokuwa wanasafiri ughaibuni kuhudhuria mkutano wa kimataifa huko Melbourne.
Aliyekuwa rais wa Jamii ya Kimataifa inayoshughulikia maswala ya ugonjwa wa Ukimwi, Joep Lange anadhaniwa kuwa mmoja wa walioabiri ndege hiyo.
BBC
↧
Jeshi la ardhini la Israel laingia Gaza

Israel imeanzisha operesheni ya nchi kavu pamoja na mashambulizi ya anga na baharini dhidi ya vuguvugu la kupigania uhuruwa palestina Hamas katika ukanda wa Gaza.
Katika kipindi cha siku kumi zilizopita zaidi ya wapalestina mia mbili wameuwawa katika mashambulizi ya anga yaliyotekelezwa na Israel na Muisraeli mmoja aliuwawa katika mashambulizi ya mizinga ya roketi kutoka Gaza.
Oparesheni hiyo ya kupeleka majeshi ya ardhini imenza usiku, ni operation kubwa kufanywa katika kipindi cha miezi mitano.
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema lengo ni kuharibu kabisa miundo mbinu na silaha zinazotumiwa na vuguvugu la Hamas kuishambulia Israel.
Vifaru karibu kumi vimeshuhudiwa vikielekezwa Gaza huku mashambulio ya angani na majini yakiendelea, ripoti ambazo hazijathibitishwa zinasema huenda hata hospitali zimegwa na mizinga.
Watu zaidi ya 3 wamefariki katika duru hii ya mapigano mbali na wale zaidi ya 200 waliofariki awali.
Kundi la Hamas limesema watajibu oparesheni hiyo vilivyo lakini Israel inasema Hamas watapewa kipigo cha kudumu na kitakachowasambaratisha kabisa.
Israel imewaita maelfu ya wanajeshi wake wa akiba kuweka nguvu zaidi katika operation hiyo.
Jana jamii ya kimataifa ilikuwa na matumaini makubwa kwamba huenda kukawa na usitishwaji mapigano wa kudumu baada pande zote mbili kukubali mapendekezo ya kusitisha mapigano kwa mda wa saa 5 za kuruhusu huduma za kibinadamu.
BBC
↧
↧
Mwalimu aliyetuhumiwa kusababisha kifo cha mwanafunzi asimulia
Mwalimu Festo Twange, aliyeshambuliwa kwa mawe akituhumiwa kuua mwanafunzi kwa kumchapa viboko, amehadithia jinsi mkasa huo uliotaka kutoa uhai wake ulivyo mpata.
Akizungumza na NIPASHE mjini hapa jana, mwalimu huyo alisema siku ya tukio alitoka nyumbani kwake akiwa amechelewa kwa sababu alikuwa akimhudumia ndugu yake mgonjwa katika hospitali ya serikali ya Somanda mjini Bariadi.
Alisema alifika shuleni akiwa amechelewa na kusaini kitabu cha maudhurio na kisha kwenda moja kwa moja darasa la sita kufundisha somo la hisabati.
Alisema akiwa darasani ghafla alifuatwa na walimu wenzake na kuambiwa kuwa anatafutwa na Sungusungu kwa madai ya kumcharaza viboko mwanafunzi wake na kusababisha kifo chake alipofika nyumbani.
Huku akionyesha hali yake kuendelea vizuri hospitalini hapo, alisema baada ya kupata taarifa hiyo alikimbilia ofisi ya Mwalimu Mkuu kwa lengo la kujificha kunusuru adhabu za walinzi hao.
Alisema pamoja na mbinu hiyo bado hakufanikiwa kwani walimwona na kumfuata ofisi ya Mwalimu Mkuu na kuvunja mlango na kuanza kumshambulia kwa silaha za jadi, fimbo, marungu na mawe na kujikuta amepoteza fahamu.
“Baada ya kumaliza kufundisha nilishangaa walimu wakija wanakimbia na kuniambia natafutwa na Sungusungu kwa madai ya kumchapa mtoto na kumuua hali ambayo ilinifanya nijifiche katika ofisi ya mwalimu mkuu..lakini walivunja mlango na kuanza kunishambulia ambapo nilipoteza fahamu na kujitambua nikiwa hapa hospitalini” alisema Twange.
Alisema anachokumbuka ni kipigo kikali na mayowe na baadaye kujikuta akiwa yuko hospitalini huku kichwani akiwa amejeruhiwa vibaya.
Akisimulia zaidi mwalimu huyo alisema kuwa, siku hiyo mwanafunzi huyo Shilinde Ng’holo (12) ambaye sasa ni marehemu hakufika shuleni hapo na wenzake walipoulizwa na mwalimu akiwamo kaka wa binti huyo, alidai mdogo wake amemuacha nyumbani kwao akiwa amelala.
“Shilinde siku hiyo hakufika shuleni hata kwenye mahudhurio ya wanafunzi hakuwapo ambapo na nilipo wauliza wanafunzi wenzake na hata kaka yake alieleza amemuacha nyumbani amelala” alisema mwalimu huyo.
Jeshi la Polisi mkoani hapa linawashikilia watu saba kwa tuhuma ya kuhusika katika tukio la kumshambulia mwalimu huyo, wakiwamo makamanda wa Sungusungu ambao waliokwenda kumkamata mwalimu huyo.
Akizungumza na NIPASHE mjini hapa jana, mwalimu huyo alisema siku ya tukio alitoka nyumbani kwake akiwa amechelewa kwa sababu alikuwa akimhudumia ndugu yake mgonjwa katika hospitali ya serikali ya Somanda mjini Bariadi.
Alisema alifika shuleni akiwa amechelewa na kusaini kitabu cha maudhurio na kisha kwenda moja kwa moja darasa la sita kufundisha somo la hisabati.
Alisema akiwa darasani ghafla alifuatwa na walimu wenzake na kuambiwa kuwa anatafutwa na Sungusungu kwa madai ya kumcharaza viboko mwanafunzi wake na kusababisha kifo chake alipofika nyumbani.
Huku akionyesha hali yake kuendelea vizuri hospitalini hapo, alisema baada ya kupata taarifa hiyo alikimbilia ofisi ya Mwalimu Mkuu kwa lengo la kujificha kunusuru adhabu za walinzi hao.
Alisema pamoja na mbinu hiyo bado hakufanikiwa kwani walimwona na kumfuata ofisi ya Mwalimu Mkuu na kuvunja mlango na kuanza kumshambulia kwa silaha za jadi, fimbo, marungu na mawe na kujikuta amepoteza fahamu.
“Baada ya kumaliza kufundisha nilishangaa walimu wakija wanakimbia na kuniambia natafutwa na Sungusungu kwa madai ya kumchapa mtoto na kumuua hali ambayo ilinifanya nijifiche katika ofisi ya mwalimu mkuu..lakini walivunja mlango na kuanza kunishambulia ambapo nilipoteza fahamu na kujitambua nikiwa hapa hospitalini” alisema Twange.
Alisema anachokumbuka ni kipigo kikali na mayowe na baadaye kujikuta akiwa yuko hospitalini huku kichwani akiwa amejeruhiwa vibaya.
Akisimulia zaidi mwalimu huyo alisema kuwa, siku hiyo mwanafunzi huyo Shilinde Ng’holo (12) ambaye sasa ni marehemu hakufika shuleni hapo na wenzake walipoulizwa na mwalimu akiwamo kaka wa binti huyo, alidai mdogo wake amemuacha nyumbani kwao akiwa amelala.
“Shilinde siku hiyo hakufika shuleni hata kwenye mahudhurio ya wanafunzi hakuwapo ambapo na nilipo wauliza wanafunzi wenzake na hata kaka yake alieleza amemuacha nyumbani amelala” alisema mwalimu huyo.
Jeshi la Polisi mkoani hapa linawashikilia watu saba kwa tuhuma ya kuhusika katika tukio la kumshambulia mwalimu huyo, wakiwamo makamanda wa Sungusungu ambao waliokwenda kumkamata mwalimu huyo.
CHANZO: NIPASHE
↧
Mbowe akwama kufika mahakamani

Upande wa utetezi ukiongozwa na mawakili; Rajab Issa na Albert Msando, uliiambia Mahakama ya Wilaya hiyo kwamba, Mbowe alishindwa kufika mahakamani jana asubuhi baada ya gari lake kupata hitilafu na kisha kuachwa na ndege.
“Mheshimiwa hakimu, mteja wangu ameshindwa kufika mahakamani kwa sababu gari lake limepata hitilafu wakati akielekea uwanja wa ndege (Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere-JNIA).
Aliachwa na ndege iliyokuwa inakuja KIA. Kwa hiyo, naomba ichukuliwe kama udhuru na taarifa rasmi ya mahakama,” alisema Wakili Rajab.
Hata hivyo, wakili huyo alimweleza Hakimu Mfawidhi, Denis Mpelembwa, kwamba miongoni mwa mashahidi watakaotoa ushahidi wao mahakamani hapo ni Mbowe mwenyewe pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai, Clement Kwayu.
Baada ya taarifa hiyo, Hakimu Mpelembwa alisema mahakama imepokea rasmi ujumbe huo kama taarifa ya mahakama na kwamba, usikilizwaji wa utetezi wa shauri hilo utaanza Agosti 18, mwaka huu.
“Kwa kuwa mdhamini wa Mbowe yupo, dhamana ya mshitakiwa inaendelea kama kawaida lakini pia naamini upande wa utetezi umejipanga vizuri kuhusu mashahidi na vielelezo.Ushahidi wenyewe utatolewa kwa njia ya kiapo,” alisema Hakimu Mpelembwa.
Katika kesi hiyo ya jinai namba 73 ya mwaka 2011, Mbowe akiwa mmoja kati ya wagombea ubunge wa jimbo la Hai, anadaiwa kumshambulia Nassir Yamin katika Kijiji cha Nshara, Kata ya Machame Kaskazini, Wilaya ya Hai.
Katika uchaguzi huo, Mbowe aliibuka mshindi kwa kupata kura 28,585 akifuatiwa na Fuya Kimbita (CCM) kura 23,349, Hawa Kihogo (UDP) kura 258 na Petro Kisimbo (TLP) 135.
Hatua ya Mbowe kutakiwa kutaja orodha ya mashahidi wake mahakamani na kisha kuthibitisha kutohusika kwake katika tukio hilo, unatokana na uamuzi uliotolewa hivi karibuni na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya hiyo kwamba, mahakama imeona ana kesi ya kujibu katika shitaka la kumshambulia mwangalizi wa ndani katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.
CHANZO: NIPASHE
↧
Lowassa, Membe waitesa CCM

Dar es Salaam. Vigogo sita wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), akiwamo Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ambao walipewa onyo kali na kuwekwa chini ya uangalizi kwa miezi 12 wamezidi kukitesa chama hicho, na katika kuwadhibiti, kimetoa maagizo kwa Kamati ya Usalama na Maadili kufuatilia nyendo zao.
Uamuzi huo ulifikiwa juzi katika kikao cha kawaida cha Kamati Kuu ya CCM kilichofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, kuwa kamati hiyo ifanye mapitio ya mwenendo wa utekelezaji wa adhabu kwa vigogo hao waliotiwa hatiani kwa kufanya kampeni za urais kabla ya wakati.
Vigogo waliopewa adhabu hiyo ni Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe na Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye.
Wengine ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wassira, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba na aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja.
Vigogo hao ambao wamekuwa wakitajwa na wakati mwingine wenyewe kuzungumzia nia ya kushika nafasi hiyo, walipewa onyo kali ikiwamo kuwaweka chini ya uangalizi kwa miezi 12 tangu Februari mwaka huu ili kuhakikisha hawajihusishi na vitendo vyovyote vinavyokiuka maadili ya chama hicho.
Vigogo hao walipatikana na makosa ya kuvunja ibara ya 6 (2) (1-5) ya maadili ya viongozi wa chama hicho inayozuia kutoa michango, misaada, zawadi za aina yoyote, kukusanya michango na kufanya kampeni bila ya kupata kibali kutoka kamati ya siasa ya halmashauri ya eneo husika.
Jana, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema mwezi ujao kamati hiyo itafanya mapitio ya utekelezaji wa adhabu hiyo ili kubaini iwapo wanaitekeleza au la.
“Kama itabainika kuwa hawatekelezi ipasavyo masharti ya adhabu zao, itapendekezwa kwa Kamati Kuu ili waongezewe adhabu nyingine kufuatana na taratibu za chama,” alisema Nnauye.
Kwa mujibu wa Nnauye, Kamati Kuu imepokea taarifa za kuwapo kwa harakati za baadhi ya wanachama walioonyesha nia ya kuomba ridhaa ya chama hicho kugombea urais.
“Baada ya kutafakari kwa kina Kamati Kuu inawakumbusha kuwa ili wanachama hao wasipoteze sifa za kugombea, ni muhimu wakazingatia katiba, kanuni na taratibu za chama zinazosimamia masuala hayo,” alisema Nnauye.
Tangu wapewe adhabu hiyo, makada hao wamekuwa wakijitokeza hadharani kwa nadra, lakini Makamba na Wassira walikaririwa na vyombo vya habari wakitangaza nia ya kugombea urais.
Hata hivyo, CCM ilisema kuwa Makamba hakukiuka taratibu kwa kutangaza nia hiyo, ingawa Rais Jakaya Kikwete alisema mtoto huyo wa katibu mkuu wa zamani wa chama hicho anataka mambo makubwa na hakumtaarifu nia hiyo.
Yajadili Ukawa
Kuhusu mchakato wa kuandika Katiba Mpya, Nnauye alisema Kamati Kuu imefurahishwa na mazungumzo yanayosimamiwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi kati ya CCM na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kujaribu kuwashawishi wapinzani kurejea bungeni.
“Kamati imepongeza juhudi zinazofanywa na msajili na kwamba ni imani yake kuwa mazungumzo hayo yatazaa matunda ili wajumbe waliosusia Bunge Maalumu la Katiba waweze kurejea kuendelea na mijadala ya mchakato wa Katiba Mpya,” alisema Nnauye.
Wajumbe wa Bunge wanaounda Ukawa walisusia Bunge Aprili mwaka huu ni kutoka vyama vya upinzani vya Chadema, NCCR-Mageuzi, CUF na baadhi ya wajumbe wa kundi la 201 ili kushinikiza kujadiliwa kwa rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyopendekeza muundo wa serikali tatu badala ya ile ya serikali mbili inayodaiwa kupigiwa debe na CCM.
Wajumbe hao wanasisitiza hawawezi kurudi bungeni hadi watakapohakikishiwa kwamba kitakachokwenda kujadiliwa bungeni ni Rasimu ya Katiba na si vinginevyo.
Kutokana na hali hiyo, Jaji Mutungi ameanzisha mazungumzo na vyama hivyo ili kuwashawishi wajumbe kubadilisha uamuzi wao na hatimaye kurejea bungeni Agosti 5, mwaka huu.
↧
HAPPY BIRTHDAY
↧
↧
LEO IJUMAA NA JUMAMOSI SAFARI CLUB DJ SEIF KUWASHA MOTO KARIBUNI SANA
↧
NDEGE NYINGINE YATUA KATIKATI YA BARABARA NCHINI UGANDA

Philip Mukasa msemaji wa jeshi la polisi nchini Uganda amesema ndege hiyo iliyokua imebeba abiria wanane wakiwemo wafanyakazi wawili wa ndege hiyo, ilikuwa iliyokua ikielekea Sudani ya Kusini baada ya rubani kugundua hakuwa na mafuta ya kutosha aliamua kurudi uwanja wa kimataifa wa Entebbe ndipo ikabidi itue kwa dhalura katikati ya barabara kwenye mji wa Mityana uliopo kilomita 67 (maili 41) kutoka mji mkuu wa Kampala.
Hakuna mtu aliyejeruhiwa, rubani ametua ndege kwa dhalura katikati ya barabara na watu wote wametoka salama.
Haikujulikana ni kwa nini rubani hakuelekea Sudan ya Kusini na badala yake kaamua kutua katikati ya barabara baada ya ndege hiyo kuishiwa mafuta.
↧
HAPPY BIRTHDAY

Godfrey Oswald from Minnesota, USA
Timu ya Vijimambo inakutakia kheri ya siku ya kuzaliwa
↧
BBQ KWA WOTE- SUNDAY AUGUST 3- - TEAM IDDI
Team Iddi Sandaly. Inawakaribisha Watanzania Wote Kwenye Nyama Choma Siku Ya Jumapili August 3, 2014. From 4:00PM
Lengo Ni Kukukutana na Kusalimiana na Kuangalia Muelekeo wa DMV as One People .
DMV KWANZA
↧
↧
MANCHESTER UNITED YAWASILI NCHINI MAREKANI TAYARI KWA MECHI ZA KUJIANDAA CHINI YA KOCHA MPYA

Na hizi ndizo mechi ikatazocheza nchini Marekani
24 July: United v LA Galaxy - Chevrolet Cup
Rose Bowl Stadium, Pasadena
Kick-off: 04:06 BST (Local time: 23 July, 20:06 PT)
26 July: United v AS Roma - International Champions Cup
Sports Authority Field, Denver
Kick-off: 21:06 BST (Local time: 26 July, 14:06 MT)
30 July: United v Inter Milan - International Champions Cup
FedEx Field, Washington DC
Kick-off: 00:30 BST (Local time: 29 July, 19:30 ET)
2 August: United v Real Madrid - International Champions Cup
Michigan Stadium, Ann Arbor
Kick-off: 21:06 BST (Local time: 2 August, 16:06 ET)
↧
TAMASHA LA USIKU WA MATUMAINI 2014 ' NDONDI ZA MWAKA'
↧
WIMBO WANGU WA LEO
↧