↧
Free Mammogram screening to our DMV community
↧
GERMANY WON THE 2014 WORLD CUP

They hired him to work on the team chemistry to prepare those nine players for the World Cup. Now Spain and Germany had the same results. Nine players from Spain played for Barcelona and nine players from Germany played for Bayern Munich and the won the World Cup. This guy pep Guardiola is the one who helped those two countries to win the World Cup. So guys be smart when you watch soccer and when coaches are being transferred around. And when Germany playe Brazil in the semi finals they used exactly Barcelonas attacking system.
The Brazilian coach prepared them to think Germany was going to play long balls. Before he adjusted it was too late Anyway he didn't recognize the system they braught him in to help them out. Most of the kids are in the academy but registration but most of the time they send them back to play in street soccer. Right now soccer is played by low income people because they recognize that street level soccer players are the ones that have the ability to bring Germany to victory.
Klinsmann started bringing good players who are from low income that's play in street soccer some in Germany and some in u.s. This time Brazil got punished because they used too many players from academy's who have no creativity. Meanwhile Germany stopped doing that and started getting players from the streets. America's economy is in trouble because they send a bunch of their products to be made in china. Brazil is in trouble now because the send their players to be manufactured somewhere else. Barcelona does the same thing. They register their players in the academy but send them back to play in the streets.
↧
↧
CHELSEA YAMSAJILI FILIPE LUIS

Timu ya Chelse ya Uingereza hatimae imekamilisha usajili wa mchezaji beki Filipe Luis kutoka Atletico Madrid, Mbrazil huyo miaka 28 anajiunga na wachezaji wenzake wengine waliosajiliwa na Chelsea msimu huu kufanya kufikia idadi ya wachezaji 3 wengine waliojiunga na Chelsea ni Cesc Fabregas na Diego Costa.
↧
Dk Slaa: Tulishinda urais 2010

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe (Kulia) akiteta jambo na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willbrod Slaa wakati wa kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika jana Dar es Salaam. Picha na Venance Nestory
Dar es Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kuwa kinaamini kilishinda uchaguzi wa rais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 chini ya mfumo wa vyama vingi.
Katibu Mkuu wa Chadema Dk Willbrod Slaa, ambaye pia alikuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho kwenye uchaguzi huo, alibainisha hayo hivi karibuni wakati wa mahojiano maalumu na waandishi wa gazeti hili.
Dk Slaa alisema kuwa ana uhakika kuwa chama chake kilipata kura nyingi zaidi za urais, tofauti na mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Mrisho Kikwete aliyetangazwa mshindi.
“…Baada ya uchaguzi wa mwaka 2010, tulikataa kumtambua Rais Kikwete, ingawa wakati ule hatukujua kwa uhakika kama tulishinda. Kadiri nilivyozunguka, ndiyo kadiri tulivyoanza kuamini kwamba tulishinda,” alisema Dk Slaa.
Alisema kuwa takwimu walizonazo zinaiaminisha Chadema kwamba ilishinda Uchaguzi Mkuu wa urais mwaka 2010.
“Sababu, unafika kwenye jimbo wanakusomea kura ulizopata katika uchaguzi ule wakizilinganisha na alizozipata Kikwete na Profesa Ibrahim Lipumba… wanasema Dokta hapa ulimshinda… kwa kura 20,000, pale ulimshinda kwa kura 15,000 pale ulimshinda kwa kura…,” alifafanua na kusisitiza:
“Sasa ndiyo, tuna uhakika kama tulishinda na ndiyo maana Kikwete hajawahi kwenda kwa wananchi kushukuru kwa kumchagua, tofauti na tabia yake. Anachofanya sasa ni kwenda kuzindua miradi.”
Hata hivyo, Dk Slaa alisema hawakuweza kuendelea na madai yoyote kwa sababu kwa mujibu wa Sheria na Katiba ya nchi, mshindi wa urais akishatangazwa hairuhusiwi kupinga kwa namna yoyote hata mahakamani, akieleza kuwa hiyo pia ndiyo sababu ya kuhitaji Katiba Mpya.
Tume ya uchaguzi na CCM
Alipoulizwa kuhusu tuhuma hizo, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), Jaji Mstaafu Damian Lubuva alisema anasubiri kwanza kusoma kwenye vyombo vya habari alichokisena Dk Slaa ndiyo ataweza kuzungumzia suala hilo.
“Kwa kuwa wewe ndiyo umeniambia Dk Slaa amesema hivyo, ngoja nione kwanza halafu tume itatoa maelezo,” alisema Jaji Lubuva.
Alipopigiwa simu Makamu Mwenyekiti wa CCM- Bara, Philip Mangula ili atoe ufafanuzi kuhusu suala hilo, alimsikiliza mwandishi wetu, kisha akasema yupo katika kikao na kukata simu.
Wizi wa kura
Alipoulizwa kama wanaelewa kura zinavyoibwa kutokana na malalamiko ya mara kwa mara ya Chadema na vyama vingine vya upinzani, Dk Slaa alisema:
“Watu wengi wanafikiri huo ni wimbo tu wa kila siku, sasa kama tunaibiwa tunyamaze? Tuseme uongo kama hatukuibiwa kura…? Hakuna uwanja sawa katika uchaguzi.
“Uchaguzi kimsingi ni uwanja wa mpira. Umeshaona kama katika uwanja wa mpira upande mmoja kuna kichuguu na kinaachwa pale? Kinaondolewa. Kilichokosekana nchi hii ni dhamira ya kuondoa vichuguu katikati ya kiwanja cha mpira; usipoondoa hivyo vichuguu hutapata uchaguzi wa haki hata siku moja.”
“Kumbuka Arumeru tulitangaza, tukasema tumegundua vituo hewa 55 vyenye jumla ya wapigakura 20,000, tulitangaza. Bahati nzuri pale tuliweza kusimamia na mnakumbuka pale tulivyotukanana na ofisa wa polisi ambaye leo ni DCI, unaweza kumpigia simu Mwigulu Nchemba akueleze jinsi tulivyotunishiana misuli… tukafanikiwa pale kuokoa kura 20,000,”alisema.
Aliongeza: “Kalenga tulipiga kelele mwanzoni kabisa kuhusu kuwapo majina mapya kwenye Daftari la Kudumu la Wapigakura, kama daftari liliboreshwa… yaliingiaje kwenye daftari hili la 2010. Ndiyo maana hatuna imani na Tume ya Uchaguzi….”
Alibainisha: “Mimi nina uzoefu wa kesi za uchaguzi katika ushindi wangu mara tatu Jimbo la Karatu hakuna hata mara moja ambayo sijapelekwa mahakamani.
“Mara ya mwisho niliponea chupuchupu, ndiyo akili ikafunguka. Hukumu ilitolewa niwafungulie CCM kesi ya kughushi. “Kwa sababu mahakama ilikuta kura zaidi ya 5,000 kupitia fomu namba 21b (result form) siyo sandukuni ndipo walipoibia, lakini kwenye matangazo ya awali nilishinda kwa kura 1,060, wamekwenda mahakamani wakasema wamenishinda kwa kura 177.
“Kwa miezi mitatu niliangalia bila kugundua, nikipiga hesabu naona ni kweli, kumbe walitengeneza vituo hewa na katika vituo vya kujumlisha kura na kuvipa namba kama iliyopo kwenye fomu halali za matokeo na kujaza kura za wizi. Waliipa CCM kura 300, Dk Slaa kura 20, za kwao zilipanda zangu zilishuka, makahama imesema kazi hiyo haikufanywa kijijini bali na wataalamu, ndiyo maana tunataka Tume Huru ya Uchaguzi ili kuwa na uwanja sawa katika uchaguzi.”
Wingi wa wanachama CCM/Chadema
Kuhusu wingi wa wanachama wa Chadema na CCM, Dk Slaa alisema: “Kwa taarifa yako nina taarifa ya mkaguzi aliyewauliza CCM orodha ya wanachama wake ikashindwa kutoa. Kama hawana orodha ya wanachama, hiyo milioni sita wanaitoa wapi? Uongo, ‘nawachalenji’ watoe hadharani….”
“Ushahidi wa pili, kujua kama una wanachama ni uhai wa wanachama. Taarifa ya CCM ya 2010 inaonyesha kwamba walikuwa wanapata kutoka kwa wanachama wao Sh9 bilioni za kadi kama ada, zimeshuka hadi Sh2 bilioni, utahesabu ni wangapi hao. Wasitudanganye…, tuna vyanzo vingi vya kupata taarifa.
Mimi sitakupa leo nina wanachama wangapi kwa sababu tunafunga kompyuta kwenye kila kanda, jimbo na kata, tumeanzisha ‘data base’ baada ya kukamilika nitakwambia tuna wanachama wangapi,” alisema na kuongeza:
“Uongo wa CCM usikudanganye kwamba nguvu yao ni wanachama, kama nguvu yao ni wanachama, uchaguzi haupigiwi kura na wanachama, kura zinapigwa na wapigakura, wananchi wanaotaka huduma kwa sababu wanalipa kodi.
Wanapiga kura ili wapate kiongozi ili asimamia kodi zao, waondokane na maisha magumu, wapate huduma za afya na elimu bora...”
Mwananchi
↧
Chadema yapasuka Kigoma

Bendera za Chadema
Kigoma. Viongozi watatu wa Chadema mkoani Kigoma, wametangaza kujitoa katika chama hicho kwa madai hakina demokrasia.
Viongozi waliojitoa ni Kasisiko Ramadhani ambaye alikuwa Mwenyekiti Mkoa, Msafiri Wamalwa Katibu Mkoa na Malunga Simba, Katibu Bawacha.
Mwenyekiti wa chama hicho Kasisiko Ramadhani ambaye pia ni Makamu mwenyekiti wa baraza la wazee taifa alisema, uamuzi huo ameutoa kutokana na migogoro ambayo imekuwa ikijitokeza hasa kwa kutotenda haki kwa wanachama wake.
Kasisiko alisema awali chama hicho kilikuwa kinaheshimu demokrasia, lakini sasa kinatumia ubabe na kutoa uamuzi usio wa busara.
Alisema, chama hicho kimeanza kukiuka katiba kwa kuwa hakuna mahali palipoandikwa masharti ya mwanachama kugombea nafasi yoyoye na kwamba mwanachama Zitto Kabwe alitolewa katika Chama hicho kwa kutaka kugombea nafasi ya Mwenyekiti Taifa.
Kwa upande wake katibu wa chama hicho Mkoa Msafiri wa Malwa, alisema sababu kubwa ya kujitoa katika chama hicho ni kukuza demokrasia ya nchi kutokana na kuwa lengo kubwa la kuanzishwa kwa vyama vingi ni pamoja na kukuza demokrasia.
Naye Malunga Simba ambaye ni katibu Bawacha Mkoa alisema amehama chama hicho kwa moyo mmoja kutokana na chama hicho kuwa na masilahi ya watu wa chache ikiwa ni pamoja na kutotenda haki kwa wanachama wake.
Mwanachi
↧
↧
HAPPY BIRTHDAY TO YOU JIMMY

Jimmy Mkude from Washington State, USA
Birthdays come and go. But our love and respect for each other will always be rock solid. None of the forces of universe can change it. We will always be there for each other this day and everyday to come. I am truly blessed to have a person like you in my life. Happy Birthday to my love.
↧
CHADEMA JIMBO LA KIGOMA KASKAZINI: TAMKO KUHUSU KUONDOKA KWA WALIOKUWA VIONGOZI

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Jimbo la Kigoma Kaskazini tunapenda kutoa taarifa kwa umma kutokana na sintofahamu inayotaka kulazimishwa mbele ya jamii kuhusu uimara wa chama chetu mkoani Kigoma.
Tangu jana na leo kumeenea taarifa zinazowahusu watu watatu, Jaffari Kasisiko, Msafiri Wamarwa na Mama Malunga Masoud, ambao vyombo mbalimbali vya habari vimeandika kuwa wamehama chama chetu cha CHADEMA na kukimbilia wanakojua wao (maana CCM inafanya kazi zake katika sura mbalimbali).
Katika hatua ya awali, sisi CHADEMA Jimbo la Kigoma Kaskazini tungependa kusema machache juu suala hilo la watu hao kuhama;
1. Kwanza watu hao mbali ya kwamba walikuwa ni viongozi wa chama ngazi ya mkoa, kwa uhakika kabisa walikuwa ni kikwazo kama si kizuizi cha muda mrefu sana kwa chama chetu kustawi na kuwa imara zaidi katika mkoa mzima wa Kigoma ili kiweze kukimbizana na wenzetu wa maeneo mengine nchi nzima. Badala yake walikikumbatia na kukiatamia chama. Wakati maeneo mengine wenzetu wakiongeza wabunge majimboni, Kigoma chini ya uongozi wao ikauza majimbo.
2. Tunaweza kusema kuwa viongozi hawa pamoja na wengine wachache ambao tunajua wako mbioni kuondoka kati ya leo na kesho, walikuwa ni sawa na KOTI LILILOTUBANA. Kwa muda wao wote wa uongozi hawakuwahi kufanya kazi yoyote ya kioganazesheni na kukieneza chama mkoa mzima. Wao walikuwa watu wa mikutano ya hapa na pale Kigoma mjini pekee au pale ambapo kunakuwa na uongozi wa kitaifa au wabunge.
3. Kwa muda mrefu saa wamekuwa viongozi ‘waliotubana’ kwa sababu walifanya kazi kwa kuangalia zaidi maslahi yao. Sasa kuondoka kwao, ni nafuu kwa chama. Pia ni fursa iliyokuja kwa wakati mwafaka kwa wanachama makamanda waaminifu na watiifu waliofungiwa milango kwa muda mrefu, kusonga mbele kukijenga chama chetu kwa imani kubwa ya kuendelea kubeba matumaini ya Watanzania wanyonge.
4. Upo ushahidi wa wazi katika hili. Kwa muda mrefu sasa viongozi hao na wengine wenzao waliopangwa kuondoka kwa awamu nyingine, wamekuwa wakilalamikiwa kufanya kazi ya chama kingine cha siasa kwa maslahi na maelekezo ya CCM.
5. Katika madai yao ya kuhama chama watu hao wamesema wamefikia hatua hiyo eti kutokana na chama chetu kuwa cha kibabe eti kwa sababu tu Zitto Kabwe alivuliwa nafasi Naibu Katibu Mkuu ndani ya chama!
6. Madai hayo yanashangaza kwa sababu mbali ya chama kuwa na sababu nzito za kumvua Zitto (na wenzake akina Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba) cheo hicho kutokana na tuhuma za utovu wa nidhamu, pia tunaamini hakuna mwanaCHADEMA amejiunga na chama hiki kwa ajili ya cheo. Ndani ya chama chetu tunaamini katika kugawana majukumu si vyeo.
7. Katika hali ya kushangaza zaidi wanasema eti Zitto amezuiwa kugombea uenyekiti. Sasa tunajiuliza hiyo nia ya kugombea ambayo hatujawahi kuisikia ikitangazwa kwa kufuata katiba, kanuni, maadili, miongozo na itifaki za chama, waliambizana wao wenyewe na mtu wao? Lakini kwa wanachama wa CHADEMA Mkoa wa Kigoma tunaelewa Jafari Kasisiko analipa fadhila za misaada binafsi ikiwemo kupelekwa nje ya nchi.
8. Ninaomba kutoa wito kwa viongozi wenzangu wa wilaya na majimbo ya Kasulu Mashariki, Muhambwe, Buyungu, Kasulu Magharibi, Manyovu, Kigoma Kaskazini, Kigoma Kusini na Kigoma Mjini, tukutane kwa ajili ya kikao cha Baraza la Mashauriano la Mkoa ili sasa tuchukue hatua zingine za muhimu na haraka za kuhakikisha tunasafisha chama chetu kwa kuwaondoa vibaraka na wasaliti wote waliosalia.
9. Pia tunaomba katika hali ya dharura Chama Makao Makuu pia kiingilie kwa kutumia kifungu cha Katiba 6.1.3, ili kupata chombo cha kuendelea kuwaunganisha wanachama wakati mkoa ukijiandaa kuchukua hatua hiyo kupitia Baraza la Mashauriano.
10. Sisi wa CHADEMA Kigoma Kaskazini tunawataka wale wengine waliosalia katika mkakati huo wa kuhamisha watu wachache lakini kwa makundi ili eti kujenga taswira ya CHADEMA kubomoka, wakiwemo viongozi kadhaa wa Kanda wasisubiri. Chama chetu kitajengwa na watu wenye imani watakaoweka maslahi na matakwa ya wananchi mbele kwa kuzingatia misingi yetu kama inavyoelezwa katika Katiba ya Chama, kanuni, maadili na miongozo.
Kwa niaba ya Wanachadema imara na makamanda watiifu na waaminifu kwa mabadiliko yanayobeba matumaini na haki za Watanzania wanyonge, naomba kutoa taarifa hii.
Ally Kisala
Mwenyekiti wa CHADEMA Jimbo la Kigoma Kaskazini
Mjumbe wa Baraza la Mashauriano la Mkoa wa Kigoma
↧
Ufaulu kidato cha sita watia shaka wadau wa elimu

Wanafunzi wa Kidato cha Sita wa Shule ya Sekondari ya wavulana mchepuo wa Sayansi ya Iyunga ya Jijini Mbeya, wakiwa wamesomangana katika chumba kimoja wakati wa masomo yao jana asubuhi. Mkuu wa Shule hiyo France Mng'ong'o, alisema kuwa kidato kimoja kina wanafunzi zaidi ya 100 na kutokana na upungufu wa walimu wanalazimika kusongamana ndani ya chumba kimoja kwa lengo la kumsikiliza mwalimu wa somo husika. Picha na Godfrey Kahango
Dar es Salaam. Wadau wa elimu nchini wameonyesha kushtushwa na matokeo ya mtihani wa kidato cha sita kuonyesha kuwa asilimia 95.98 ya watahiniwa wamefaulu mtihani huo bila kuwapo na mikakati inayoonekana ya kuboresha kiwango cha ufaulu.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, wadau hao walisema pamoja na matokeo hayo kuonyesha ongezeko la ufaulu, wana wasiwasi iwapo matokeo yaliyoandikwa kwenye karatasi yanaakisi ufahamu wa wanafunzi.
Waziri Kivuli wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Susan Lyimo (Chadema) alisema hakuna mkakati wowote uliochukuliwa na Serikali kuhakikisha ufaulu unaongezeka, hivyo ni jambo la kushangaza kuona matokeo yanaonyesha wanafunzi wamefanya vizuri kiasi hicho.
“Hapo kinachooneka goli limepanuliwa ili magoli yaingie zaidi kwani kati ya mwaka jana na mwaka huu kitu gani kimefanyika. Ukaguzi wa walimu na wanafunzi haufanyiki, ufaulu unaongezekaje?” alihoji Susan.
Aliongeza kuwa kinachofanyika hivi sasa ni kutaka kuwaridhisha wazazi ambao walikata tamaa kutokana na matokeo mabaya ya wanafunzi wao kwa miaka miwili iliyopita.
“Walimu wanajua kuwa hata wasipofundisha wanafunzi kuna mtu huko juu atawafaulisha tu,” alisema.
Mkurugenzi wa shirika la Uwezo linalojihusisha na masuala ya elimu, Ziada Mgalla alisema wanafunzi waliofaulu wanapaswa kupongezwa iwapo asilimia 95.98 ya ufaulu inawakilisha ufahamu wao.
Alisema historia inaonyesha kuwa wapo baadhi ya wanafunzi ambao walifaulu kwa kiwango kikubwa lakini hawakuwa na uwezo wa kufafanua kile walichokiandika kwenye mitihani jambo linalotia shaka kuwa huenda matokeo ‘yalichezewa’.
“Matokeo hayo hayatakuwa na maana kama wanafunzi waliofaulu hawawezi kuwa na ufahamu unaolingana na matokeo yao. Pia wastani unaozungumzwa lazima mwanafunzi awe amepata kuanzia alama 60 kuendelea kama amepata chini ya hapo hakuna sababu ya kushangilia,” alisema Ziada.
Akizungumzia sababu za shule za umma kufanya vibaya, mkurugenzi huyo alisema kuwa Serikali ijiulize kwa nini walimu wanaofundisha shule hizo wanafunzi wao hufeli, lakini wakienda kufundisha shule za binafsi, wanafunzi wao hufaulu.
“Suala siyo tu kuwa na walimu, wawasikilize wanapolalamika vinginevyo itafika wakati mwanafunzi wa sayansi ataonekana amefaulu lakini akifika kwenye upasuaji akashindwa kufanya kazi taifa likatia aibu,” alisema.
Meneja Utafiti na Uchambuzi wa Sera wa HakiElimu, Boniventura Godfrey alisema wakati watu wanashangilia matokeo hayo yaliyotajwa kuwa ni mazuri yakilinganishwa na miaka iliyotangulia, wadau wa elimu wanapaswa kujiuliza kwa nini shule za umma zilizokuwa zikiongoza miaka ya nyuma zinazidi kufanya vibaya.
Alisema Serikali inatakiwa kuchukua hatua za haraka kukabiliana na tatizo hilo kwa kuwa hata mazingira ya shule hizo kwa sasa yameharibika ikilinganishwa na ilivyokuwa siku za nyuma ingawa zina idadi kubwa ya walimu.
Godfrey alisema matokeo hayo hayana uhusiano wowote na mpango wa Serikali wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) kwa kuwa haiwezekani ndani ya mwaka mmoja kukawa na mafanikio ya kiwango hicho.
“Sijui matokeo haya ni mazuri kwa namna gani kwa sababu wala BRN (Matokeo Makubwa Sasa) haiwezi kuwa na mafanikio ya haraka namna hii.
Ninadhani suala la kuangalia hapa ni kwa nini shule za umma zimefelisha huku za binafsi zikiendelea kuongoza,” alisema.
MWANANCHI
↧
VIJIMAMBO WATOTO- UBONGO KIDS
↧
↧
HAPPY BIRTHDAY
↧
MSIBA DMV NA TANZANIA
ALBERT MATESO (KOCHA) AMEFIWA NA BABA YAKE MZAZI TANZANIA SIKU YA IJUMAA JULY 18, 2014
YEYE ALBERT ATAONDOKA LEO JUMAMOSI JULY 19, 2014 JIONI KUELEKEA TANZANIA KWENYE MAZIKO YA MPENDWA BABA YAKE, MKEWE ATAKUWEPO.
UKIPATA UJUMBE HUU MTAARIFU NA MWENZIO TAARIFA ZAIDI ZITAFUATA KWA SASA UNAWEZA KUMPIGIA SIMU MFIWA ALBERT MATESO (KOCHA) NAMBA YAKE NI 301 437 9367 NA KUMPA POLE KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU CHA KUONDOKEWA NA BABA YAKE MZAZI
YEYE ALBERT ATAONDOKA LEO JUMAMOSI JULY 19, 2014 JIONI KUELEKEA TANZANIA KWENYE MAZIKO YA MPENDWA BABA YAKE, MKEWE ATAKUWEPO.
UKIPATA UJUMBE HUU MTAARIFU NA MWENZIO TAARIFA ZAIDI ZITAFUATA KWA SASA UNAWEZA KUMPIGIA SIMU MFIWA ALBERT MATESO (KOCHA) NAMBA YAKE NI 301 437 9367 NA KUMPA POLE KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU CHA KUONDOKEWA NA BABA YAKE MZAZI
↧
PICNIC
THE WAY OF THE CROSS GOSPEL MINISTRIES

*****PICNIC - PICNIC - PICNIC******
Kanisa la the Way of the Cross Gospel Ministries linapenda kuwatangazia waumini na watu wote hapa DMV kuwa limeandaa picnic kwa watu wote. Picnic hiyo itafanyika POINT STATE PARK kwenye Delta ya mto Potomac, kandokando ya Bahari ya Atlantic na karibu na Bay Bridge (maili 35 kutoka Washington DC)
ANWANI
1100 EAST COLLEGE PARKWAY
ANNAPOLIS, MD 21409
Njoo usikilize neno la Mungu kwa lugha ya Kiswahili na ushuhudie UBATIZO WA MAJI MENGI kwa baadhi ya waumini wake, upunge upepo wa bahari, uvue samaki na uweze kuogelea na pia ukutane na ndugu na jamaa zako kwenye upepo mwanana wa bahari. “Njoo na Kiti chako, Zulia pamoja na Mwamvuli”
SIKU NA TAREHE
TAREHE : JULY 26, 2014, SIKU YA JUMAMOSI
SAA: 11:00AM – 6:00pm, church Van itaondoka Hyattsville, MD saa 10:30AM
Usafiri upo kwa watakaopiga simu mapema. Waleteni watoto waje waogelee.
Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana na:
MCHUNGAJI: 240-476-6718
MZEE WA KANISA: 443-636-1781
MZEE WA KANISA:- 240-645-2131
KATIBU: 240-217-6335
KARIBUNI SANA
↧
RAIS KIKWETE ZIARANI NYASA, RUVUMA
(Picha na Freddy Maro).
↧
↧
SPIKA ANNE MAKINDA AWASILI ARUSHA, AKAGUA UKUMBI UTAOTUMIKA KATIKA MKUTANO WA 45 WA MABUNGE WA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA MADOLA


↧
BARAZA LA HABARI WAMUAGA BALOZI WA NORWAY



↧
TUJUMUIKE PAMOJA KWENYE IBADA YA SHUKURANI YA MSIBA YA MDOGO WA MCHUNGAJI M.D. MATURLU
↧
MH.BALOZI MULAMULA AZUNGUMZA NA WAGOMBEA WA DMV PAMOJA NA KAMATI YA UCHAGUZI




Bi.Nyami akipata futari.
↧
↧
T444Z HAIR JOURNEY START YOURS TODAY
This is real beautiful people T444Z is the answer to all your hair problems!!
It's a product for Real Problems, Real People & Real Solutions..
We do ship all over the USA
Call/whatsapp us @ 1-617-504-3727
If you are in Tanzania call/whatsapp the distributor @ the following #'s
TIGO Piga # 0655844497 na VODA Piga # 0758844490
Or Like there FB pg @
↧
VOTING FOR MISS AFRICA USA 2014 HAS OFFICIALLY BEGUN, PLEASE VOTE FOR JOY KALEMERA
Miss Tanzania USA Pageant Joy Kalemera
Kind regards,
Joy Kalemera
Link to vote http://missafricausa.org/?portfolio=miss-tanzania-2014-joy-kalemera
↧
Wazazi wa wasichana waliotekwa wakataa kukutana na Rais Jonathan

Serikali ya Nigeria inasema familia za zaidi ya wasichana wa shule 200 waliotekwa nyara wanakataa kukutana na Rais Goodluck Jonathan kutokana na ombi la kundi la wanaharakati la Bring Back Our Girls. Tukio hilo linawaweka wasichana waliotekwa nyara kuwaingiza katika siasa za kitaifa ambapo zimepamba moto kabla ya uchaguzi mkuu mwaka ujao.
Jumatatu Rais Goodluck alimuahidi mwanaharakati Malala Yousafzai wa Pakistan anayehamasisha elimu kwa msichana kwamba atakutana na familia za wasichana walioshikiliwa mateka na wanamgambo wa kundi la Boko Haram kwa miezi mitatu iliyopita.
Mkutano ulipangwa kufanyika jumanne mjini Abuja lakini familia zimeakhirisha.
Doyin Okupe, msaidizi wa masuala ya umma kwa Rais anasema familia zimekataa kuhudhuria mkutano katika dakika za mwisho na kulilaumu Bring Back Our Girl, kundi moja la wanaharakati ambalo linafanya maandamano takribani kila siku kudai kuokolewa kwa wasichana hao.
Hata hivyo bwana Okupe analishutumu kundi la Bring Back Our Girls kwa kushirikiana na wanasiasa wa upinzani wanaotaka kuchukua nafasi ya bwana Jonathan katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.
Serikali inashutumu kampeni za Bring Back Our Girls kwa mchezo mchafu na wenye kuchukiza na kurudia ahadi ya serikali ya kuwatafuta wasichana na kutokomeza uasi wa kundi la Boko Haram.
VOA
↧