Quantcast
Channel: VIJIMAMBO
Viewing all 45984 articles
Browse latest View live

MJENGO WA BARAZA LA WAWAKILISHI LINALOSHAHABIANA NA MJENGO WA CAPITOL HILL NCHINI MAREKANI

$
0
0
Mjengo wa baraza la wawakilishi Zanzanibar
Mjengo wa Capitol Hill Washington, DC nchini Marekani

MKUTANO WA WANA-CCM JIMBO LA CALIFORNIA TAREHE 07-03-2015.

DIAMOND AMJIBU KWA VITENDO EX WA ZARI

$
0
0
Diamond akiwa kwenye baiskeli huku Zari akiwa kwenye BMW X6.

Baadhi ya post za King Lawrence Instagram akimkejeli Diamond.

STAA wa Bongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond’, ameamua kumjibu kwa vitendo anayedai kuwa aliwahi kuwa mpenzi wa mwandani wake wa sasa, Zarinah Hassani ‘Zari’, King Lawrence ambaye amekuwa akimtupia maneno ya kumtusi na kejeli mitandaoni.
Diamond akipozi na mpenzi wake Zari.

King Lawrence ambaye ni binamu wa aliyekuwa mume wa Zari aliyezaa naye watoto watatu Ivan amekuwa akimnanga Diamond mitandaoni hasa Instagram kama mtu aliyefulia na hana fedha ambapo siku za nyuma aliwahi kuandika post akisema kuwa yuko tayari kumpatia kiasi cha Usd 40,000 sawa na zaidi ya shilingi milioni 71 Diamond aachane na Zari.

Katika kuonyesha kuchoshwa na tabia hizo za King Lawrence, Diamond ameamua kutupia picha yake akiwa amepanda baiskeli huku mpenzi wake Zari akiwa katika mkoko mkali aina ya BMW X6 akimaanisha kumkebehi mtu huyo kuonyesha kuwa hana kitu ila anaomba penzi kwa mtoto mkali aliye kwenye BMW.

GPL

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU ZIARA YA RAIS WA UJERUMANI HAPA NCHINI

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
 
                                                 

Simu:255-22-2114615, 211906-12
Barua pepe: nje@nje.go.tz
Barua pepe: gcu@nje.go.tz

Nukushi: 255-22-2116600

              

 

                20 KIVUKONI FRONT,
                           P.O. BOX 9000,
                  11466 DAR ES SALAAM,  
                                    Tanzania.

 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Ujerumani, Mhe. Joachim Gauck anatarajiwa kuwasili nchini usiku wa tarehe 02 Februari, 2015 kwa ziara ya kitaifa ya siku tano kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.
Mhe. Rais Gauck atapokelewa rasmi na mwenyeji wake Mhe. Rais Kikwete Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 03 Februari, 2015 na atakagua Gwaride la Heshima na kupigiwa mizinga 21. Wananchi wanaombwa kuwa watulivu wakati mizinga hii ikipigwa kwani ni salama.
Baada ya mapokezi hayo, Mhe. Gauck atafanya mazungumzo ya faragha na Rais Kikwete yakifuatiwa na mazungumzo rasmi. Aidha Marais hao watakutana na Waandishi wa Habari.

Baadaye siku hiyo ya Februari 03, Mhe. Rais Gauck atakutana na Wafanyabiashara, atatembelea Kanisa la Kilutheri la Azania Front, atakutana na Wawakilishi wa Taasisi za Kiraia na kushiriki Dhifa ya Kitaifa itakayoandaliwa na mwenyeji wake Mhe. Rais Kikwete, Ikulu.
Mhe. Rais Gauck ambaye ameongozana na Mke wake Bibi Schadt, Viongozi Waandamizi kutoka Serikali ya Ujerumani na Ujumbe wa Wafanyabiashara tisa, ataondoka Dar es Salaam kuelekea Zanzibar tarehe 04 Februari, 2015 ambapo atafanya mazungumzo rasmi na Mhe. Dkt. Ali Mohammed Shein, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kabla ya kushiriki kwenye Mkutano wa Kamati ya Pamoja ya Viongozi wa Dini kuhusu Amani. Rais Gauck pia atakutana na Vijana kutoka Ujerumani wanaojitolea katika Programu ya Weltwarts Visiwani humo.
Jioni ya Februari 04, Mhe. Gauck ataondoka Zanzibar kuelekea Mkoani Arusha. Akiwa Mkoani humo siku ya tarehe 05 Februari, 2015 atatembelea Taasisi mbalimbali za kimataifa ikiwemo Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), na kuhutubia Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA). Mhe. Gauck na ujumbe wake watatembelea pia Hifadhi ya Wanyama ya Serengeti ambapo atazindua Kituo kipya cha kudhibiti Ujangili.
Mhe. Rais Gauck anatarajiwa kumaliza ziara yake hapa nchini tarehe 06 Februari, 2015 na kuondokea  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kurejea Ujerumani.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

01 Februari, 2015

BARABARA YA IGAWA – UBARUKU KUJENGWA KWA LAMI.

$
0
0

Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli (pichani) amesema serikali itajenga barabara ya Igawa hadi Ubaruku KM 18 kwa kiwango cha lami ili kuinua fursa za uchumi za wilaya ya Mbarali na kuwezesha magari makubwa kupita kwa urahisi kufuata mazao katika eneo hilo.
Waziri Dkt. Magufuli amesema hayo katika ziara yake inayoendelea mkoani Mbeya ambapo leo ameweka jiwe la msingi  ujenzi wa barabara ya igawa-ubaruku  yenye urefu wa KM 18 na kusisitiza barabara hiyo ni muhimu kwa uchumi wa mkoa wa Mbeya na taifa kwa ujumla.
“Nitahakikisha barabara hii inajengwa kwa kiwango cha lami na kukamilika mapema ili kuunga mkono juhudi za wananchi wa Mbarali wanaotekeleza sera ya kilimo kwanza kwa kuzalisha mpunga na mahindi kwa wingi”, amesisitiza waziri Magufuli.
Amewataka wananchi waliojenga katika hifadhi ya barabara kupisha eneo la barabara ili kuwezesha kazi ya ujenzi huo kufanyika kwa haraka na kumalizika kwa wakati.
Amemwagiza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini TANROADS Eng. Patrick Mfugale kufanya usanifu ili kuwezesha madaraja kumudu kupitisha magari yenye uzito wa tani 40 yatakayochukua mazao katika maeneo ya Rujewa na Ubaruku.
Eng. Mfugale amesema barabara ya Igawa-Ubaruku kwa sasa ni barabara ya mkoa na ujenzi wake utazingatia vigezo vya barabara za mikoa ili kukidhi mahitaji ya uzito wa magari yatakayopita katika barabara hiyo.

Kuhusu barabara ya Igawa –Madibira yenye urefu wa KM 153 ambayo upembuzi yakinifu na usanifu wake umekamilika waziri Magufuli amesema Serikali inatafuta fedha ili kuijenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami na hivyo kuifungua kiuchumi wilaya ya Mbarali.
Amesisitiza umuhimu wa umoja,mshikamano na uaminifu kwa wananchi wa Mbarali na kuwataka vijana watakaopata kazi wakati wa ujenzi wa barabara hiyo kuwa waaminifu.
Naye mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro amemshukuru Waziri wa Ujenzi kwa kuamua kujenga kwa lami barabara za Mpemba hadi Isongole wilayani Ileje ,Igawa hadi Ubaruku wilayani Mbarali na Kikyusa hadi Matema wilayani Kyela na kusisitiza barabara hizo zitakapokamilika zitaimarisha usafiri na kuibua fursa za ajira na uchumi kwa wakazi wengi wa mkoa wa Mbeya.
                                    
Mwisho

Imetayarishwa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Wizara ya Ujenzi.

TANGAZO KWA WATU WALIOSAFIRISHA MIZIGO TANZANIA TOKA USA KWA CONTAINER AMBAYO HAIJAFIKA

Makamo mwenyekiti wa UTU kuwasili Tanzania

$
0
0
Makamo mwenyekiti wa Umoja wa Watanzania Ujerumani UTU e.V Mheshimiwa Peter Kazaura kuwasili nchini Tanzania Kesho 02.02.2015 kwa ajili ya kufanya mazungumzo na kiongozi wa juu wa Taifa. akiwa Tanzania atafanya mazungumzo na uongozi wa mashirika yafuatayo TIC, Basata, Wizara ya Ardhi, NSSF, NHC, Tanzania Diaspora Initiative na Wizara ya Utamaduni Michezo na Vijana.
Mazungumzo hayo yatalenga upatikanaji wa Fursa zilizopo Tanzania kwa Diaspora. akiendelea kueleza msemaji wa Umoja huo Watanzania wanaoishi ujerumani wangependa pia kuhusishwa kikamilifu katika shughuli za maendeleo nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na Afya, Elimu.
naye Mwenyekiti wa Umoja huo Mhe. Mfundo Peter Mfundo alithibitisha kuwepo kwa safari ya Makamo Mwenyekiti Mhe Peter Kazaura na alisema UTU e.V umechukua uamuzi huo baada ya Watanzania nchini Ujerumani kukosa nafasi ya kuongea na Rais wa Tanzania wakati wa ziara ya Rais nchini Ujerumani.Pia watanzania wanaoishi ujerumani wanaulalamikia ubalozi kuwa viongozi wa umoja wao walinyimwa nafasi ya kuonana na kumsalimia Mhe.Rais Dkt.Jakaya Kikwete.

MSIBA DMV NA TANZANIA

$
0
0
Familia ya Mr. & Mrs. Deo Mosha (Mamertha na Deo) na Henry Kente, wanasikitika kutangaza kifo cha Baba mzazi wa Henry na Mamertha, Mr. Wilbard W. Kente, uliotokea leo, Jumapili tarehe 1 February 2015 huko nyumbani Dar-es-Salaam, Tanzania. Msiba upo nyumbani kwa Mr. & Mrs. Mosha, address
4402 Hatties Progress Dr.
Bowie, MD 20720
Kama ilivyo mila na desturi yetu karibuni tujumuike kutoa mkono wa pole na kuwafariji wafiwa.
Kwa wale walioko mbali ambao wangependa kutoa rambi rambi , wanaweza kutumia account ifuatayo
Henry Kente
Bank of America
Routing # 052001633
Account # 446030721450

Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na
Deo Mosha: 240-441-8433
Vitalis Gunda: 240-383-6950
Tumaini Katule: 301-433-3400
Mrs. Gloria Semiti: 301-325-1843

Mungu ampumzishe vyema Baba kwenye makao yake ya milele. Amen.

Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli Azindua barabara ya Igawa-Rujewa KM 9.8 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami.

$
0
0
 Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiweka jiwe la msingi kuashiria ufunguzi wa barabara ya Igawa-Rujewa KM 9.8 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro pamoja na viongozi wengine wa Wilaya ya Mbarali.
 Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akikata utepe kuashiria ufunguzi wa barabara hiyo. Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro pamoja na viongozi wengine.
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa barabara nchini TANROADS Eng. Patrick Mfugale akisoma taarifa ya mradi wa barabara ya Igawa-Ubaruku inayojengwa kwa kiwango cha lami.
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akiwahutubia wakazi wa Ubaruku na Rujewa Wilayani Mbarali.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiwahutubia wakazi wa Rujewa na Ubaruku wilayani Mbarali kuhusu ujenzi wa barabara ya Igawa-Ubaruku km 18.
 Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akifurahia ngoma pamoja na kikundi cha ngoma za asili cha Rujewa mara baada ya kuwahutubia wakazi wa Rujewa na Ubaruku wilayani Mbarali.
 Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiagana na wakazi wa Rujewa na Ubaruku mara baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara.

 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro katikati akizungumza na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli kuhusu ujenzi wa barabara ya Rujewa-Ubaruku inayotarajiwa kujengwa kwa kiwango cha lami. Barabara hiyo inatarajiwa kuwarahisishia wakazi wa maeneo hayo ambao wengi wao ni wakulima wa mpunga na mahindi.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akizungumza na wakazi wa Ubaruku wilayani Mbarali waliokuwa wanaomba wajengewe barabara ya Rujewa-Ubaruku kwa kiwango cha lami. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Ujenzi.

MAZISHI YA BABA WA P-SQUARE KAMA SHEREHE

$
0
0
STORI:LAGOS,NIGERIA/Ijumaa Wikienda
Acha kabisa! Mazishi ya baba wa mastaa wa muziki wa Nigeria, mapacha Peter na Paul Okoye wanaounda ‘Kruu’ ya P-Square, Moses Okoye aliyefariki dunia Novemba 24, 2014 yamekuwa kama sherehe, Ijumaa Wikienda limedodosa kilichojiri.
Mwili wa baba wa P-Square, marehemu Moses Okoye ukisindikizwa kwenye gari kwa tarumbeta.

Ishu hiyo ilijiri nyumbani kwa mastaa hao eneo la Ifitedunu, Jimbo la Anambra nchini humo Ijumaa iliyopita ikiwa ni siku 65 tangu mzee huyo alipofariki dunia baada ya kufanyiwa oparesheni ya goti alipodondoka kwenye ngazi nyumbani kwake maeneo hayo.
Wakina P-square wakiwa na wake zao katika msiba huo.

Tofauti na ilivyozoeleka kwamba kwenye msiba watu huwa wanalia na kuomboleza, mazishi hayo yaliyohudhuriwa na mastaa kibao nchini humo yalikuwa tofauti kwani watu walikuwa na nyuso za tabasamu huku wakiserebuka na matarumbeta juu.


Ulinzi mkali ukiimarishwa katika msiba huo.

Mbali na kuonekana kuwa kama sherehe, pia mazishi hayo yaliripotiwa kuwa ya gharama zaidi kuanzia jeneza lililobeba mwili wa baba yao, gari ‘spesho’ lililokuwa na jina la Dady badala ya namba za usajili na wahudhuriaji waliopiga sare nyeupe huku wakijifotoa picha wakicheka na kutupia kwenye mitandao ya kijamii.
Mwili wa baba wa P-Square ukiwa kwenye jeneza.

Pia kivutio kikubwa kilikuwa ni wake wa mastaa hao ambao walipewa ulinzi mkali uliowekwa katika mazishi hayo yaliyohudhuriwa kwa mualiko maalum.
Baba wa P-Square (aliyenyosha mikono) enzi za uhai wake.

Cha kushangaza, wakati mwili wa baba yao ukiwa mochwari, jamaa hao walidaiwa kuendelea na ratiba za kimuziki huku wakifanya shoo kama kawa jambo ambalo kwa Bongo haliwezekani.
Kwa sasa mastaa hao hawana mzazi hata mmoja baada ya mama yao naye kufariki dunia mwaka 2012

Rais Kikwete aanza kukabidhi madaraka nje

$
0
0
Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete akizungumza na mwenzake Rais wa Misri, Jenerali Abdel Fatteh El Sisi siku za hivi karibuni. Picha na Maktaba

Dar es Salaam. Rais Jakaya Kikwete amekabidhi madaraka ya Uratibu wa Kamati ya Wakuu wa Nchi na Serikali za Afrika ya Mazingira (CAHOSCC) kwa Rais wa Misri, Jenerali Abdel Fatteh El Sisi.
Rais Kikwete alibeba jukumu la uratibu wa CAHOSCC miaka miwili iliyopita baada ya kifo cha aliyekuwa mratibu wa kamati hiyo, Waziri Mkuu wa Ethiopia, Meles Zenawi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu, Rais Kikwete alikabidhi jukumu hilo Januari 31 na kuwatahadharisha viongozi wa Afrika juu ya athari za mabadiliko ya tabia ya nchi kwenye sekta ya kilimo barani Afrika.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa Kikwete aliwapongeza viongozi wengine wa Afrika wakati wa mkutano wa 24 wa Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa, kwa kupata mafanikio wakati wa uongozi wake.
Kikwete alibainisha changamoto mbalimbali zinazolikabili bara la Afrika kwenye mabadiliko ya tabia ya nchi na kutaka ushirikiano kati ya nchi zilizoendelea ambao ndiyo wachafuzi wakubwa wa mazingira na nchi zinazoendelea kutoka Afrika.
Rais alizitaka nchi za Afrika ambazo zinaathirika zaidi na athari za mabadiliko ya tabia nchi, kuongeza kasi katika kuzibana nchi tajiri ili zikubali kuchangia kwa kiasi kikubwa rasilimali za kubabiliana na athari hizo kwa sababu zinachangia asilimia 97 ya uchafuzi wa mazingira.
“Wao wanachangia asilimia 97 kuchafua mazingira na kusababisha mabadiliko ya tabia nchi, sisi tunachangia asilimia tatu. Hivyo, tunawataka wabebe mzigo mkubwa zaidi katika kurekebisha hali hiyo kuliko sisi kwa misingi ile ya wajibu wa pamoja lakini ulio tofauti,” alisema Rais Kikwete.
Aliongeza kuwa wakati wa  uongozi wake,Bara la Afrika limeongeza uhusiano na washirika mbali mbali duniani katika kusimamia umuhimu wa kukabiliana kwa pamoja na athari za mabadiliko ya tabia nchi na hasa kati ya Afrika na Bara la Ulaya.
Rais Kikwete alisema mikutano ya maandalizi iliyofanyika Malabo, Equatorial Guinea, Dar Es Salaam na katika Umoja wa Mataifa mjini New York wakati wa Uratibu wake, ilisaidia kuweka msimamo wa pamoja wa Bara la Afrika na kuliwezesha Bara hilo kuzungumza kwa sauti moja wakati wa Mkutano wa Lima.
MWANANCHI

Lipumba kumwona JK kuhusu ubabe wa polisi

$
0
0
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akionyesha jeraha la Naibu mkurugenzi wa mawasiliano wa chama hicho, Abdul Kambaya wakati wa mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana. Kambaya alijeruhiwa na polisi wakati wa maandamano Jumanne iliyopita. Picha na Salim Shao

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amesema anatarajia kwenda Ikulu kumwona Rais Jakaya Kikwete ili kumweleza mambo mbalimbali ikiwamo ubabe na upendeleo unaofanywa na polisi.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Profesa Lipumba alisema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimekuwa kikifanya mikutano bila ya kubughudhiwa na polisi tofauti na inavyofanyiwa CUF.
“Kinana anafanya mikutano kila siku lakini hatujawahi kuona akibughudhiwa na polisi lakini chama chetu kimekuwa kikiambulia mabomu ya machozi, vipigo na kuzuia mikutano yetu, Rais inabidi aingilie kati hasa katika kipindi hiki tunachoelekea katika uchaguzi mkuu,” alisema.
Profesa Lipumba alisema huko ni kuleta mgawanyiko unaoweza kusababisha machafuko kama hatua madhubuti hazitachukuliwa.
Jumanne iliyopita, Jeshi la Polisi lilizuia maandamano na mkutano wa chama hicho uliokuwa ufanyike kuadhimisha miaka 14 ya mauaji ya wenzao yaliyotokea Zanzibar Februari 26 na 27, 2001.
Katika tukio hilo, Profesa Lipumba na wafuasi 32 walikamatwa na baadaye kufunguliwa mashtaka mahakamani ya kula njama, kufanya maandamano na kukusanyika bila kibali. Vitendo hivyo vya polisi vilisababisha Bunge la Jamhuri ya Muungano kusitisha shughuli zake na kujadili tukio hilo bila kujali kwamba lilikuwa linaingilia mhimili mwingine wa nchi.
Jana, Profesa Lipumba alisema: “Nataka kuonana na Rais Kikwete ana kwa ana, siwezi kumwandikia barua kwa sababu nafahamu hana muda wa kusoma, hivi sasa nafanya kila juhudi ili kumwona.”
Profesa Lipumba alisema Januari 22, mwaka huu chama chake kilipeleka barua ya kufanya maandamano na mkutano kwenye Uwanja wa Zakhem, Mbagala wilayani Temeke na kiliwatangazia wananchi kwamba maandamano na mkutano huo vingefanyia Januari 27 kuanzia saa 8.00 mchana na maandamano yangeanzia Temeke Mwisho hadi katika uwanja huo.
Alisema Januari 26, saa 12.00 jioni ikiwa imebaki siku moja, ndipo Jeshi la Polisi likatoa amri ya kupinga kufanyika kwa maandamano hayo na mkutano.
“Tulishawatangazia wananchi kuhusu maandamano hayo na mkutano, usiku huo tungewajulisha vipi kufuta mkutano huo, kwa nini hawakutujulisha mapema? Matatizo kama hayo yanasababishwa na Jeshi la Polisi,” alisema Profesa Lipumba.
Alisema wakati wakisaini makubaliano ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa kati ya CCM na CUF Zanzibar, alipopewa nafasi ya kuzungumza alisema: “Tusameheane kwa mauaji yaliyotokea Zanzibar lakini tusiyasahau kwa sababu tukifanya hivyo yanaweza kujirudia.”
Alisema ndiyo maana kila mwaka, wamekuwa wakifanya kumbukumbu za mauaji hayo ili yasirudie tena.
Akizungumzia waliojeruhiwa na polisi, mwenyekiti huyo alisema maofisa wake wawili walijeruhiwa kwa vyuma na kuwasababishia maumivu makali.
Hata hivyo, Profesa Lipumba aliwataka wananchi kutolipiza kisasi licha ya wengi wao kusikitishwa na vitendo hivyo.
MWANANCHI

TASWIRA YA BUNGE LEO DODOMA

$
0
0
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba akijibu maswali wakati wa kipindi cha Maswali na Majibu Bungeni leo.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Anne Kilango Malecela akijibu maswali ya wabunge.
Baadhi ya Mawaziri wakiwa kwenye ukumbi wa Bunge
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara akiteta jambo na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Juma Nkamia Bungeni mjini Dodoma.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Diana Chilolo akiuliza swali la nyongeza kwa Waziri wa Katiba na Sheria kuhusu Mahakama ya Wilaya ya Iramba mkoni Singida.
Mbunge wa Mwibara (CCM), Kangi Lugola akichangia taarifa za kamati zilizowasilishwa leo Bungeni mjini Dodoma.
Baadhi ya wageni ambao ni wanafunzi wa Shule ya Awali ya Mchepuo wa Kiingerea ya Labi ya mkoni Dodoma wakiwa na walezi wao, wakifuatilia Bunge
Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima akizungumza na Mbunge wa Singida Mjini, Mohamed Dewji baada ya Bunge kuahirishwa leo asubihi. Father Kidevu

UNAMPENDA, UNATAKA NDOA LAKINI HUJUI PA KUANZIA?-2

$
0
0
Asalaam aleikum msomaji wa safu hii nzuri, ni matumaini yangu kwamba uko poa, nakukaribisha tena kwenye uwanja huu mzuri tujadili kuhusu mambo mbalimbali yahusuyo mapenzi.
Wiki iliyopita tulianza kujadili mbinu zinazoweza kumvuta mwanamke au mwanaume unayempenda na hatimaye mkafikia hatua ya kuishi pamoja mkiwa kama mume na mke.

Nakushukuru wewe uliyetuma ujumbe nakueleza jinsi ulivyoguswa na mada hiyo au kutoa ushauri. Leo tunaendelea na sehemu ya pili na ya mwisho ya mada yetu. Narudia tena kukupa angalizo kwamba ninachokielekeza hapa ni kwa mtu ambaye kweli ana nia ya dhati ya kuingia kwenye ndoa.
Hatufundishani mbinu hizi ili kesho na keshokutwa uwe bingwa wa michepuko kwa sababu umeshajua mbinu zinazoweza kukufanya ukampata yule umpendaye kwa urahisi.

Niliishia kukuelezea nini unacho-takiwa kufanya baada ya kufanikiwa kujenga mawasiliano ya kawaida na yule umpendaye na hatimaye kumfikishia ujumbe uliopo ndani ya moyo wako. Tunaendelea kuanzia pale tulipoishia:

Endelea kuwasiliana naye kwa mambo ya kawaida huku ukimpima kama yale uliyomwambia kuhusu unavyojisikia ndani ya moyo wako anayachukuliaje. Kama naye amekupenda, utaanza kuona mabadiliko kuanzia meseji atakazokuwa anakutumia, namna anavyopokea simu yako na uchangamfu atakaokuwa anakuonesha.

Kama bado haoneshi dalili zozote za kuelewa hisia zako juu yake, basi jua hajavutiwa na wewe na ukiendelea kuzungumzia mambo ya mapenzi, huenda ukaanza kumboa. Naomba niweke wazi jambo moja; kuna baadhi ya watu ambao huwa ving’ang’anizi kiasi cha kugeuka na kuwa kero.
Kama naye ana dalili za kuvutiwa na wewe kimapenzi, endeleza mawasiliano naye, omba kukutana naye sehemu tulivu kama ufukweni au popote ambapo mtakuwa wawili na hapo utakuwa na nafasi nzuri ya kueleza kwa kina juu ya hisia zako.

Endapo atakubali kukutana na wewe, basi hiyo ni hatua nzuri sana kuonesha kwamba unaelekea kufanikiwa. Jambo la msingi ni kuanza kujiandaa kwa ajili ya kukutana naye kwa sababu mwonekano wako wa kwanza mbele ya macho yake ndiyo utakaompa sababu ya kukuchagua au kukukataa.
Kwanza anza kwa kufanya kitu ambacho huwa kinakufurahisha na kukuweka kwenye mudi nzuri kama kuimba, kucheza muziki, kufanya mazoezi au chochote unachokipenda sana.

Baada ya hapo, hakikisha nguo zako ni safi, jipulizie manukato mazuri, piga mswaki, jitengeneze nywele zako vizuri na hakikisha kila kitu mwilini mwako ni kisafi. Pangilia mazungumzo kati yako na umpendaye kabla hata hamjakutana, hii itakuongezea kujiamini.

Hakikisha sehemu mnayoenda kukutania kwa mara ya kwanza unaifahamu vizuri na imetulia vya kutosha. Baada ya hapo, muandalie zawadi ndogo mfano chokleti, mkufu au ua zuri. Usihangaike kutafuta zawadi kubwa kwa sababu siyo muhimu mnapokutana kwa mara ya kwanza.

Muda utakapowadia, wahi kufika eneo mlilopanga kabla ya mwenzako, hii itamfanya akuheshimu zaidi kwa sababu atajua hubahatishi mambo. Msalimie kwa uchangamfu kisha mkaribishe sehemu ya kukaa. Jitahidi kupunguza maneno mengi badala yake zungumza kwa staha na muda mwingi msikilize yeye. Muulize kinywaji au chakula anachokipenda kisha muagizie.

Kama wewe ni mwanaume, mkishamaliza kunywa au kula, lipa bili hata kama yeye anao uwezo wa kulipa. Ukweli ambao wengi hawaujui, wanawake wanapenda zaidi kuhudumiwa hata kama wana utajiri mkubwa kiasi gani.

Mkishamaliza, uwanja ni wako sasa wa kueleza hisia za ndani ya moyo wako. Zungumza kwa busara na kwa utulivu, huna haja ya kupaniki kwa sababu mpaka amekubali kukutana na wewe, tayari una asilimia kubwa ya kumpata hivyo punguza woga. Jitahidi kumtazama kwenye macho yake unapozungumza naye, hii itakuongezea ujasiri.

Naam! Baada ya hapo naamini utakuwa umeutua mzigo mzito uliokuwa nao, usimlazimishe kukupa majibu hapohapo endapo ataomba umpe muda. Baada ya hapo, tayari utakuwa umefanikiwa kumvuta kwako kwa asilimia tisini, ongeza ukaribu zaidi na utaona matokeo yake kwa sababu hataweza kukataa ombi lako na mwisho mtatimiza lengo lenu la kufunga ndoa na kuishi pamoja siku za mbele.

GPL

FRANCIS CHEKA JELA MIAKA MITATU

$
0
0
cheka
BONDIA maarufu nchini wa ngumi za kulipwa, Francis Cheka amehukumiwa kifungo cha miaka 3 jela na kutakiwa kulipa fidia ya Sh. millioni 1 kwa kosa la kumpiga na kumjeruhi meneja wa baa yake (Cheka) iitwayo Vijana Social iliyopo Morogoro Mjini.

Akimsomea mashitaka, Hakimu wa Mahakama ya Mkoa wa Morogoro, Said Msuya alisema Cheka alikutwa na hatia ya kumpiga aliyekuwa meneja wa baa yake aitwaye Bahati Kabanda 'Masika'.

Alisema kuwa Cheka alitenda kosa hilo Julai 2, mwaka jana ambapo meneja huyo alikwenda kwenye baa hiyo kudai fedha zake alizokuwa hajalipwa na bondia huyo wakati akifanya kazi ya umeneja katika baa yake hiyo.


Hakimu Msuya alisema kuwa Cheka alikataa kumlipa na kumshushia kipigo kilichosababisha kulazwa hospitalini.

Baada ya hukumu hiyo huku Cheka akipandishwa kwenye difenda tayari kupelekwa gerezani akionekana kutokuwa na wasiwasi wowote, mashabiki wake walimvaa meneja huyo wakitaka kumshushia kipigo hivyo kuibua taharuki mahakamani hapo.

Hata hivyo, baadhi ya mashabiki hao walikuwa wakisema wapo tayari kujichanga ili kukata rufaa wakiamini kuwa bondia huyo ameonewa. GPL

Mbali na hukumu hiyo mahakamani hapo, kulikuwa na kesi nyingine mbili zilizokusanya umati, moja ikiwa ni ya Sheikh Ponda juu ya uchochezi na ile ya mtoto wa boksi inayowakabili baba na mama Nasra.

USAFIRSHAJII MIZIGO DAR NA ZANZIBAR

$
0
0
TUMA BIASHARA ZAKO KWA NJIA YA BAHARI AMBAYO NI NAFUU KWA UZITO WOWOTE ULE, CONTAINER LETU LINAONDOKA MWISHO MWA FEBRUARY.KWA TAARIFA ZAIDI WASILIANA NASI  KWA CONTACT 

LOOK OF THE DAY

$
0
0

Staa wa muziki na filamu Bongo, Baby Joseph Madaha

JK apuliza kipyenga urais 2015

$
0
0
 Asema kama wanaojitokeza hawafai, washawishiwe wengine, Asisitiza kura ya maoni katiba pendekezwa ni Aprili.
Wakati Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikitarajia kutangaza ratiba yake ya mchakato wa uteuzi wa wagombea wake katika uchaguzi mkuu wa Oktoba, mwaka huu, Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete, jana alipuliza kipyenga cha mbio za urais.

Alisema kwamba kama wanachama walioanza kujitokeza kuwania uteuzi wa urais hawana sifa, wananchi na wanachama wasisite kushawishi watu wengine wenye sifa wajitokeze kuchukua fomu.

Rais Kikwete alitoa rai hiyo jana wakati akihutubia mamia ya wananchi kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM yaliyofanyika kitaifa mjini Songea katika uwanja wa Majimaji.

“Uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba, mwaka huu wa kupata rais wa awamu ya tano, utakuwa wa kihistoria, nataka rais atoke CCM na maelezo ni rahisi tu; Mwalimu Nyerere alishawahi kusema rais anaweza kutoka chama chochote cha siasa, lakini rais bora lazima atoke CCM, na huu ni wosia mzuri na muhimu sana,” alisema.

Hadi sasa makada wa CCM waliotangaza nia kuwania urais kupitia chama hicho ni Naibu Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Mawasiliano, January Makamba; Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba; Mbunge wa Nzega, Dk. Hamis Kigwangalla; Waziri Mkuu wa sasa, Mizengo Pinda na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu.

Wanaotajwa kuwania ni Mbunge wa Songea Mjini, Dk. Emmanuel Nchimbi; Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja; Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe; Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta na mawaziri wakuu wastaafu, Edward Lowassa na Frederick Sumaye.

Wengine ni Spika wa Bunge, Anne Makinda; Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Asha-Rose Migiro; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Prof. Mark Mwandosya na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira.

Rais Kikwete alisema viongozi na wanachama wa CCM ni lazima wawe mstari wa mbele kupata mgombea aliye bora ambaye siku atakapotangazwa wananchi hawatakuwa na wasiwasi naye.

“Siyo wakiulizwa waanze kusema hapa hapana, tutakuwa tumepuuza wosia wa muasisi wa Taifa, Mwalimu Nyerere,” alisema.

“Nyerere alisema bila CCM imara nchi itayumba, viongozi tusikubali tuwe wa kwanza kukiuka wosia huu, laana yake itakuwa kubwa kwa Taifa na nchi itayumba, watu wazuri CCM wapo na kama walioanza kujitokeza sasa hawafai, tuwashawishi wajitokeze wengine wakachukue fomu, hata sisi tulishawishiwa japo hatukuwa na mpango wa kuwania urais,” alisema.

Alisema kujitokeza au kumshawishi mtu agombee uongozi siyo dhambi na kwamba chama hicho kisifanye ajizi katika jambo hilo la kupata viongozi bora kwa sababu lina maslahi ya chama na nchi kwa ujumla.

Rais Kikwete alisema suala la kushinda dola ndiyo madhumuni makuu na msingi wa chama hasa ikizingatiwa kuwa CCM siyo chama cha kucheza mpira au cha burudani na kwamba zipo kanuni na vigezo vya kupata viongozi walio bora ambao wanachunjwa katika ngazi zote za vikao vya chama.

“Hapataharibika jambo, CCM itawapatia wagombea bora ambao wananchi watawakubali, cha msingi wagombea wasingatie masharti ya kikatiba ya chama, kanuni na maadili ya kuteuliwa, asiyezingatia hayo asije akakilaumu Chama bali ajilaumu mwenyewe kwa kutozingatia kanuni zilizowekwa,” alisema.

Rais Kikwete alisema tangu Tanzania ilipoingia katika mfumo wa vyama vingi vya siasa mwaka 1992 CCM imeendelea kuimarika, kudumisha amani na mshikamano , Watanzania na wananchi wameendelea kukiamini Chama hicho.

Alisema ushindi ambao CCM imeupata katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika mwishoni mwaka jana ni dalili nzuri kwa vyama vya wapinzani, akisema hawana chao katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Hata hivyo, alisema wanachama wa CCM wasibweteke na ushindi uliopatikana katika uchaguzi huo kwa sababu uchaguzi mkuu ujao unaweza kuwa na changamoto nyingi ambazo ni lazima zihitajike nguvu ili kukiwezesha Chama kupata ushindi wa kishindo.

Alisema viongozi na wanachama wa CCM ni lazima watambue kuwa nguvu ya Chama inaanza kwenye chama, hivyo lazima kuwe na ari na nguvu mpya ya viongozi na wanachama wa CCM kwani bila umoja ushindi hauwezekani.

Rais Kikwete alisema wakati uchaguzi mkuu ukiwa umekaribia, wapo baadhi ya viongozi ambao hawajafanya chochote katika maeneo yao na kwamba wanamsikitisha sana kwa kuwa watasababisha chama kupata upinzani mkali.

ATAHADHARISHA FEDHA CHAFU
Alisema yapo mambo kadhaa ambayo Chama kilikubaliana ambayo ni pamoja na kila ngazi ya chama wilaya na mkoa kuhakikisha inakuwa na mfuko wa uchaguzi ambao mwaka huu ndiyo unatakiwa kufanya kazi.

“Nawatadharisha msichukue fedha za moto mtaungua vidole, msichukue kila fedha nyingine zina matatizo, tunapoanza safari ya miaka 39 tunapashwa kuondoa utegemezi wa fedha, misaada, ruzuku na misaada ya wafanyabiashara kwa sababu si mambo endelevu,” alisema.

Rais Kikwete alisema huu ni mwaka wa kuhakikisha kunakuwa na nyenzo za kazi ambazo ni jumuiya za CCM ili kukiwezesha chama kuungwa mkono na jamii pana ya Watanzania.

Rais Kikwete aliongeza kwa ukifanya maandalizi mazuri sasa wakati wa uchaguzi hutahangaika, utakuwa unavaa suti tu kwani kila kitu kitakuwa mteleremko, usipofanya maandalizi utafanya henya henya, lazima jasho likuvuje.

Alisema wanachama na viongozi wa CCM wanatakiwa kufanya kazi kwa nguvu zaidi kasi na ari zaidi kama kauli mbiu ya chama inavyoeleza kwa kutambua ahadi ambazo zilitolewa wakati wa uchaguzi mkuu uliopita na kuzifuatilia kama zimetelekezwa.

“Zipo ahadi za rais, chama mkoa, wilaya ambazo nyingine tulibanwa tukaziahidi,” alisema.

Alisema mwaka 2015 ni wa kuongeza ukumbwa wa jeshi ambalo ni wanachama, hivyo jitihada zifanyike kuongeza idadi ya wanachama na kwamba Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, ameagiza kuongeza kadi mpya milioni mbili.

Alisema jambo lingine ni kwa viongozi wa chama hicho kuwatembelea wananchi na kuzungumza nao, lakini makatibu wa CCM wamekuwa hawafanyi hivyo.

Rais Kikwete alisema amekuwa akiwatuma watu kufuatilia maagizo yake na kumweleza kuwa wamekuwa hawatekelezi ipasavyo na kuonya kuwa viongozi na wanachama wa CCM lazima watambue kuwa CCM haiwezi kupata ushindi kwa watu wasiowatembelea kusikiliza kero zao.

Alimpongeza Kinana kwa kazi kubwa anayofanya ya kukiimarisha chama tofauti na viongozi wa chama hicho wa ngazi ya wilaya na mikoa.

“Tumewapa magari tena ya mkonga mtembelee wananchi, lakini hawawaoni, wenzetu wa upizani wanafanya vyema katika hili, bila kuwatembelea wananchi hatuwezi kuwa na uhakika wa kushinda,” alisema.

Rais Kikwete alisema viongozi waache kung’ang’ania kukaa ofisini, badala yake watoke kuzungumza na wananchi na kuwashawishi waichague CCM.

KURA YA MAONI
Rais Kikwete alisema maandalizi kwa ajili ya kura ya maoni kuamua Katiba Inayopendelezwa yanaendelea na kinachofanyika sasa ni uandikishaji wapiga kura pamoja na uchapishaji na usambazaji wa katiba hiyo.

“Watani wetu watatoa elimu hasi na sisi tutoe elimu chanya ili ipite,” alisema.

Alisema Katiba Inayopendekezwa imebeba maslahi ya nchi na misingi yote imezingatiwa, lakini wapinzani wanaikataa kwa sababu tu muundo wa serikali tatu haupo.

Alisema kitendo cha vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kutangaza kususia kura za maoni kinasikitisha na hakimshangazi kwa kuwa tangu mchakato wa katiba mpya umeanza wamekuwa wakizua kila jambo jipya.

Aliwaambia Watanzania kuwa haoni sababu ya kuikataa Katiba Inayopendekezwa la sivyo Katiba ya sasa ya mwaka 1977 itakuwa inaendelea kwa vile hakuna nyingine hadi miaka ijayo hadi rais ajaye au baada ya huyo.

Alisema anaweza kuja mwingine na kusema hakuna haja ya kuandikwa katiba mpya.
CHANZO: NIPASHE

MTOTO WA WHITNEY HOUSTON, BOBBI KRISTINA ALAZWA HALI YAKE NI TETE

$
0
0
Bobbi Kristina mtoto wa Whitney Houston aliyezaa na Bobby Brown (picha juu) amekutwa ameanguka kifudifudi bafuni na kukimbizwa hospitali siku ya Jumamosi Januari 31.

Bobbi Kristina alikutwa kwenye bafu huku uso wake ukiwa ameinamia chini huku akishindwa kupumua na kukimbizwa hospitali ambapo madaktari wamejaribu kumrudisha katika hali yake ya kawaida ambayo sasa inaonekana ubongo wake unafanyakazi kwa asilimia ya chini kitu ambacho madaktari wamesema sio dalili nzuri kwa mgonjwa wa namna hiyo na kuwaambia familia ya Bobbi Kristina kuendelea kusali na kumwombea Bobbi Kristina apate nafuu haraka.

Baba ya Bobbi Kristina Bobby Brown mwanamuziki aliyetamba enzi hizo akiwa na kundi la New Edition na baadae kujiengua na kuwa peke yake sasa hivi yupo pembeni mwa kitanda cha mwanae akiwa ameacha shughuli zote na kuendelea kumuuguza kwa karibu zaidi mtoto wake.

Whitney Houston kabla ya kifo chake nae alikutwa bafuni akiwa hoi hajiwezi ikiwa amezidiwa na madawa ya kulevya aliyokua amebiya kitu ambacho kilidhaniwa ndicho alichokua amekifanya mtoto wake huyo mara tu alipokuwa amekutwa nae bafuni akiwa amezidiwa huku uso wake ukiwa umeinamia chini huku akishindwa kupumua.

Aliyemgundua ni Nick Gordon ambae ni mchumba wa Bobbi Kristina akiwa na marafiki zake na kutoa taarifa polisi ambao walifika kwenye tukio na baadae waliikagua nyumba ya Bobbi Kristina wakitafuta kama kulikuwa na madawa ya kulevya na kukuta hakuna madawa yaliyopatikana.

Habari zilizotufikia hivi punde zinasema leo Jumatatu madaktari waliendelea na vipimo vya ubongo na madaktari kupata matumaini japo kidogo ubongo umeonyesha dadlili nzuri kidogo jambo ambalo limefufua matuamaini ya madaktari japo wameomba familia na watu wakaribu wazidi kumwombea Bobbi Kristina aendelee kupata nafuu.

ALOCHOANDIKA JOHN TERRY KWENYE INSTAGRAM BAADA YA MTANANGE WAO NA MAN CITY

$
0
0
#JohnTerry instagrams after the match...

A good point after yesterday's game which leaves us top and 5 points clear of Manchester City.
Lamps is a proper Chelsea LEGEND and I'm so pleased he got a great send off after the game because I know how much Chelsea means to him. Lamps won everything with us and in my opinion the best and most consistent player ever.
Love Ya mate
#respect
Viewing all 45984 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>